Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

SOMO LA Cyber Security na Tanzania Yetu KUTOKA KWA MDAU Ben Mabeba, Jr


MAMIA WASHIRIKI MAZISHI YA MKE WA JAJI ANTHONY BAHATI

$
0
0
Mwalimu Laurentia Bahati enzi za uhai wake.
Jaji mstaafu Mhe. Anthony  Bahati akiweka shada la maua katika kaburi la mke wake, Laurentia Bahati wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni.
Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania Mhe.  Augustino Ramadhani akiweka shada la maua.

kakakuona aonekana kigamboni leo, wananchi watabiri ni ishara ya mvua nyingi msimu huu

$
0
0
 Wananchi wakiwa wamemzunguka Kakakuona aliyeonekana asubuhi majira ya saa moja maeneo ya Kigamboni Kisiwani Mtaa wa Chaboko ambapo kwa mujibu wa ripota na mpiga picha wetu Salma Bob Kassim, mnyama huyo aliwekewa Unga, ndizi, maji pamoja na pesa. 
Lakini akaishia kunywa maji tu kabla ya kukimbilia vichakani. Wananchi kwa mamia waliofurika kumuona Kakakuona huyo walisikika wakisema kuwa huenda huo ni utabiri kwamba huenda mvua zikawa nyingi msimu huu. 
Polisi walifika eneo la tukio na baada ya kuona hakuna uvunjifu wa amani wakatoa taarifa kwa maafisa wa Maliasili ambao walifika na kumtia mnyama huyo kwenye kiroba na kuondoka naye
 Kakakuona akijikunja baada ya umati wa watu kuzidi kuwa mkubwa 
Baadaye, huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha, Kakakuona huyo alielekea vichakani huku umati ukiendelea kumshangaa. Baadaye watumishi wa Maliasiali walifika na kumtia kwenye kiroba na kuondoka naye.
Picha na Salma Bob Kassim

SAA 24 ZA BURUDANI DAR LIVE, NJOO TUFUNGE NA KUFUNGUA MWAKA 2015

AJALI YA LORI NYORORO IRINGA, LAFUNGA BARABARA KWA SAA KADHAA

$
0
0
Edwin Moshi wa Eddy Blog
Watumiaji wa barabara ya Iringa Njombe wamekwama toka jana majira ya saa 10 jioni kufuatia ajali ya lori lililobeba shaba lenye namba za usajili T 261 BCM linalovuta tela lenye namba za usajili T 595 BAS kupata ajali na kufunga barabara na kusababisha magari kushindwa kupita. 
 Mtandao huu umeshuhudia msururu mkubwa wa magari yanayokwenda mikoa ya njombe Ruvuma Mbeya na nchi jirani, pamoja na yanayotoka kwenye mikoa hiyo kwenda Iringa Dodoma, Dare es Salaam na mikoa mingine yakiwa yamekwama kwenye msururu huo. Ajali hiyo imetokea eneo la Nyororo mkoani Iringa. 
Baadhi ya abiria na madereva wa malori waliokuwa eneo la tukio wamelalamikia ufinyu vya kulitoa lori hilo kuwa ni hafifu hali iliyopelekea wakae hapo muda mrefu(karibia siku moja). 
 Hali hiyo iliondolewa majira ya saa tatu asubuhi baada ya lori hilo kufanikiwa kuondolewa barabarani na kusogezwa pembeni ndipo magari hayo yakaendelea na safari.  

Sehemu ya msururu wa magari yaliyokwama baada ya ajali hiyo kuziba barabara ya Iringa-Njombe
Msururu wa magari yaliyokwama baada ya ajali hiyo kuziba barabara ya Iringa-Njombe
Sehemu ya Lori lililopata ajali
Wafanyakazi wa Lori hilo wakitafakari nini cha kufanya

Sherehe za kubarikiwa kwa Mchungaji Dickson Kiwori zafana huko Masama, Moshi

$
0
0
 Mchungaji Dickson Kiwori akifurahia na mkewe baada ya kubarikiwa rasmi  kuwa mchungaji katika Ibada iliyofanyika Jumamosi katika Kanisa LA KKKT usharika wa Sonu Masama katika Ibadan iliyoongozwa na Askofu Dkt.Martin Shao
 Mke Wa Mchungaji mpya Dickson Kiwori Hilder Akimlisha mumewe kipande cha ndafu wakati Wa Sherehe  ya kumpongeza iliyofanyika Huko Usharika Wa Sufi Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro
Mchungaji mpya Dickson Kiwori  akipongezwa wakati Wa Sherehe  ya kumpongeza iliyofanyika Huko Usharika Wa Sufi Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro
 Ndafu wa sherehe
Mchungaji mpya Dickson Kiwori  akishukuru wakati Wa Sherehe  ya kumpongeza iliyofanyika Huko Usharika Wa Sufi Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro

introducing "Masela wangu" by Zaiid & P the MC Ft. Mejah Power

Requiem Mass for Tony Barretto to be held on Wednesday

$
0
0
 A Requiem Mass for Tony Barretto's one year death anniversary will be held on Wednesday 31st December at 17:30hrs at the Don Bosco Youth Centre, Upanga, in Dar es salaam. All are welcome to celebrate his life.
Brother Tony: You are   greatly missed and dearly remembered.  
May you rest in peace, Amen. 



Mamia wamzika Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian leo kwenye Makaburi ya Wangazija, jijini Dar es salaam

$
0
0
Na Chalila Kibuda, 
Globu ya Jamii, Dar es salaam
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan mwinyi leo ameongoza mamia ya waombolezaji kwenye  mazishi ya Sheikh Ali Mzee Comorian yaliyofanyika leo katika makaburi ya Wangazija yaliyopo katika barabara ya Bibi Titi Mohamed jijini Dar es Salaam. 
Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo  Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe Adam Malima, Mufti Mkuu Sheikh Simba Shaban Bin Simba, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na viongozi wengine.
Mazishi ya Sheikh Comorian yamefanyika  huku mvua kubwa ikinyesha kwa takriban masaa mawili mfululizo. 
Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongea katika msikiti wa Makonge ilikofanyika swala ya mazishi  alisema kifo cha sheikh huyo ni mipango ya Mungu na kwamba  kila mtu safari yake ipo. 
Alisema kifo cha sheikh kinatakiwa kuenziwa kwa mema aliyoyafanya katika uhai wake katika kupigania na kuendeleza Uislamu. 
 Rais Mstaafu wa awamu ya pilimAlhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto),Waziri Mkuu Mstaafu,Dkt. Salim Ahmed Salim (wa nne kulia), Mufti  Mkuu wa Tanzania Sheikh Simba Shaaban Simba (wa pili kushoto) na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mussa Salum (wa tatu kulia) wakijumuika pamoja na waombolezaji wengine kwenye  mazishi ya Sheikh Ali Mzee Comorian, katika makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam mapema leo. 
Picha na Othman Michuzi/Emmanuel Massaka.
Sehemu ya Umati wa Waombelezaji ukiwa umebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian ukiwasili kwenye Makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed,jijini Dar es salaam huku mvua kubwa ikinyesha mapema leo.
Waombolezaji wakiendelea na shughuli ya Mazishi ya Marehemu Sheikh Ali Mzee Comorian kwenye Makaburi ya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed, jijini Dar es salaam licha ya mvua kubwa kunyesha mapema leo.

ngoma azipendazo ankal

Music Planet ilivyobamba jijini Dar

$
0
0
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya,Mad Ice akiangusha bonge moja la show sambamba na bendi yake katika Music Planet iliyofanyika Samaki Samaki mpya ya Masaki,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyoisha.
Dj Cartel the undisputed champion 4 rounds wins all by K.O akifanya yake ndani ya Music Planet iliyofanyika Samaki Samaki mpya ya Masaki,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyoisha.
Masai wakiimba nyimbo zao juu ya mangoma makali kutoka kwa DJ Gabi ikiwa ni mambo ya Music Planet iliyofanyika Samaki Samaki mpya ya Masaki,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyoisha.

SALAM ZA MDAU MUBELWA BANDIO: Mwaka unakatika....Tumesonga mbele ama tumerudi nyuma???

$
0
0
 Amani, Heshima na Upendo kwa wana-blog wote.
Kwanza namshukuru MUNGU kwa baraka ya uhai ambayo mimi nawe tunayo mpaka sasa. Pili nikupe pole kwa harakati za maisha ambazo sote twazipitia kufanikisha yale mema tupendayo.
Ni harakati kubwa sana hasa katika kusonga na maisha yetu ya kila siku na pia kuendeleza gurudumu hili la blogs
Nimekuwa nikituma makala, vipindi na kazi zangu kwenu nanyi mmekuwa wakarimu sana kuzipokea. Ushirikiano ambao umenifanya nizidi kujivunia kuwa mmoja wa bloga
Lakini pia, najivunia sana kuwasiliana na kila mmoja wetu hivi sasa ili kuanzisha mjadala wa changamoto zilizo mbele yetu kama JAMII YA WANA-BLOG wenye lengo la kuigusa jamii.
Ningependa tuanze kwa kujiuliza, Je! Tunasonga mbele ama nyuma katika harakati zetu.
Nashukuru kwa blogs na tovuti mpya ambazo zinachipuka na kuendeleza nia njema ya kuigusa jamii. Kaka Luta Kamala aliwahi kuandika akijuliza KWANINI TUNA-BLOG? (Bofya hapa) na hata Kaka Chambi Chachage aliuliza kama uwepo wa blogu zetu unakuza ama kufifisha tasnia nzima ya uandishi (Ipitie hapa)
Jibu halisi tunalo mioyoni mwetu kulingana na dhamira tulizonazo.
Lakini kwa ujumla, haijalishi ni sababu gani ilikufanya u-blog, mwisho wa safari sote tunajikuta na zao moja ama "mlaji" mmoja ambaye ni JAMII.
Bloga awekaye picha anataka kuionesha jamii alichokiona.
Bloga ahabarishaye anataka kuihabarisha jamii. Yule aandikaye Utambuzi anataka jamii ijitambue. Anayeweka kumbukumbu ni sababu anataka jamii ije isome baadaye. Atangazaye biashara anataka jamii ijue palipo na huduma ama biashara husika. Afunzaye mapishi, mitandao, mavazi, mitindo nk, woote wanalenga katika kuielimisha jamii.
Kwa maana nyingine sote twaiandikia JAMII.
Na hili ni lengo jema.
Lakini swali linarejea kuwa......
Mwaka huu ambao unaomalizika wiki hii unaonekana kuwa hatua gani kwetu?
Logo hapo juu inaonyesha hatua iliyopigwa katika siku za mwisho za mwaka. Kuanzishwa kwa mtandao wa bloga ambao (ukitumiwa vema) utakuwa chachu ya mabadiliko ya nchi hasa kwa mwaka huu wa uchaguzi.
Ninalowaza ni hili.....
Vipi tunaweza kuweka nguvu na jitihada zetu pamoja kuweza kuitumikia vema na kwa ufasaha jamii yetu???
Mafanikio ya bloga mmoja mmoja yanaweza kudhihirisha kuwa TUNAWEZA, lakini tunalostahili kufanya sasa, ni kushirikiana na kuwa makini katika kila jema tutendalo.

Tunapoumaliza mwaka 2014, tuangalie nyuma na kujiuliza, mwaka unakatika....Tumesonga mbele ama tumerudi nyuma??


Na jibu la swali hili, liwe CHANGAMOTO YETU sote

Baraka kwenu nyote

Heri ya Mwaka Mpya 2015

PSPF KUWAKUTANISHA WACHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA NA SIMBA

$
0
0
MFUKO wa Pensheni wa PSPF umedhamini mchezo wa kirafki utakaowakutanisha wachezaji waliowahi kuwika katika timu kongwe nchini Simba na Yanga.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika tarehe 1 Januari 2015 katika uwanja wa chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam, kiingilio kitakuwa bure ikiwa ni zawadi ya mwaka mpya kutoka PSPF.

Katika mchezo huo baadhi ya wachezaji wa Simba wanaotarajiwa kushuka uwanjani ni Thomas Kipese, George Lucas, Bita John, George Masatu, Mustafa Hoza, Emmanuel Gabriel, Idd seleman. Timu ya Simba inafanya mazoezi katika uwanja wa Leaders uliopo Kinondoni, ipo chini kocha mchezaji Kasongo Athuman.

Wanaotarajiwa kushuka uwanjani kwa upande wa Yanga ni Peter Manyika, Mwanamtwa Kihwelo, Edibily Lunyamila, Mohamed Husein, Chibe Chibindu, Aboukar Salum, Bakari malima. Yanga wanafanya mazoezi katika uwanja wa kauda ulipo katika makao makuu ya klabu hiyo kariakoo Jijini Dar es Salaam, wakiongozwa na kocha Peter Tino.

Lengo la mchezo huo ni kutoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na maeneo ya karibu hususani katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka. PSPF itatumia fursa hiyo kutangaza huduma zake mpya ambazo Mkopo wa Elimu na Mkopo wa Kuanza Maisha.
Tunatoa mwito kwa wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwaona wakongwe waliowahi kutikisha nchi katika anga ya soko nchini.

THE MBONI SHOW KUANZA KUUNGURUMA JANUARY 2 NDANI YA TBC

$
0
0
Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba (wa pili ktoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana katika  ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kuanza kwa msimu wa tatu wa kipindi chake 'The Mboni Show' kinachotarajia kuanza Jan 2, 2015. Kushoto ni kiti MC Zimpompa na kuanzia kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba.
Kutoka Kulia Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema akizungumza wakati wa uzinduzi kipindi cha Mboni Show uliofanyika katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba pamoja na Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba.

Na Mwandishi Wetu.
Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba ameamua kuhamishia kipindi cha Mboni show katika kituo cha utangazaji cha Taifa (TBC) kutoka EATV ili kuvutia watazamaji wengi na wapya kwa wazee pamoja na vijana.
Kipindi cha Mboni Show kitaanza kurushwa TBC kuanzia January 2 mwaka 2015 siku ya
Ijumaa saa 3 Usiku-4 Usiku na marudio Jumanne saa 9:00 mchana-10:00mchana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mboni Masimba ametoa shukrani kwa EATV kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote alichokuwa nao,na kusema kuwa amehamishia kipindi cha Mboni Show katika kituo cha TBC ili kuvutia watazamaji wengi na hakuna atakaye tumia jina la Mboni Show na hakuna kitakachomkwamisha kwa vile ana hati miliki.
“Nimehamia TBC kwa kuwa nahitaji watazamaji wengi ,wote wazee na vijana na hakuna atakaye tumia jina langu la Mboni Show kwa kuwa nina hati miliki ya jina hili”, alisema Mboni.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw.Fadhili Chilumba amesema wamefurahi kuwepo kwa Mboni Show katika kituo cha Taifa(TBC) na kutoa wito kwa mashabiki kuweza kuwadhamini watu kama wakina Mboni na wanamkaribisha sana.
Nao wadhamini wa Mboni Show,Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema wamesema wanamwezesha Mboni kuwepo hewani ili kuhamasisha,kuelimisha pamoja na kuburudisha umma wa Watanzania.

DIAMOND WASHINGTON DC DEC 6 2014 SHOW TRAILER..FULL DOCUMENTARY STILL LOADING...


Matukio ya kutishia amani ya nchi na usalama wa raia yatapungua kama mabalozi wa nyumba kumi watafanya kazi zao kwa uaminifu - Vuai Ally Vuai

$
0
0
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi

Matukio ya kutishia amani ya nchi na usalama wa raia yatapungua kama mabalozi wa nyumba kumi watafanya kazi zao kwa uaminifu kwani wao ni viongozi wa kwanza walio karibu na wananchi hivyo basi wanatakiwa kuwafahamu wakazi wa maeneo yao.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Vuai Ally Vuai wakati akifungua semina ya siku moja ya  uwezeshaji wa chama hicho kwa  mabalozi (viongozi wa mashina) wa wilaya ya Lindi mjini.

Vuai alisema Balozi ni kiongozi wa kwanza anayetakiwa kujua idadi ya wakazi wake, kazi wanazozifanya na majina yao kitendo ambacho kitasaidia kuimarisha usalama wa eneo husika lakini miaka ya hivi karibuni wameacha kufanya kazi hiyo kwa uadilifu na kuviachia vyombo vya dola pekee.

“Jukumu la kulinda amani ya nchi na usalama wa taifa letu ni la kila mtu, lakini hivi sasa kazi hiyo vimeachiwa vyombo vya dola pekee, mabalozi fanyeni kazi ya kuwatambua wakazi wa maeneo mnayoishi hii itasaidia kumtambua mualifu pale atakapofika katika eneo lenu”, alisema Vuai.

mwanafunzi wa MUCE alamba Mil. 3 za BayPort

$
0
0
Ruth Bura, Mratibu wa Bima ya Elimu Bayport Tanzania kulia akimkabidhi hundi bwana Kennedy Kaupenda kwa ajili ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu baada ya kufariki mzazi wake. 
Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura kulia, akizungumza jambo katika makabidhiano ya hundi kwa bwana  Kennedy Kaupenda kushoto kwake, Makao Makuu ya Bayport, mapema wiki hii. 

TAASISI ya kifedha ya inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Tanzania, imempatia Sh Milioni tatu (3,000,000) mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa (MUCE), Kennedy Kaupenda, kufuatia huduma mpya ya Bima ya Elimu inayoendeshwa na taasisi hiyo nchini.

Huduma hiyo mpya ya Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania ilianza mapema mwaka huu kwa ajili ya kuwapatia fursa wanafunzi kuendelea na masomo baada ya mzazi aliyejiunga na huduma hiyo kufariki Dunia.

bofya hapa kusoma zaidi



Waziri Mwandosya akagua Miradi ya Umwagiliaji ,Busokelo, Rungwe

$
0
0
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya (wa pili kulia) akipata maelezo ya Mradi wa Umwagiliaji wa Mbaka.Utakapo kamilika Mradi utakuwa na uwezo wa kumwagilia hekta 600 kwenye vijiji vya Mbambo,Kambasegele,Katela,na Kapula-Mpunguti.Wananchi 1300 watanufaika na Skimu hii.wengine pichani kutoka kulia ni Gideon Mapunda,Afisa Kilimo,Ndugu Said Mzeru,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busokelo na Mhe. Alfred Mwakasapi,Diwani wa Kata ya Kambasegela;wakiwa kwenye banio la chanzo cha mradi kwenye Mto Mambwe.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya (wa pili kushoto) akipata maelezo ya utekeelezaji wa miradi ya umwagiliaji Busokelo kutoka kwa Afisa Umwagiliaji wa Halmashauri,Ssid Majula,wa nne kushoto.

UNATAKA AU UMEFUNGUA KAMPUNI, JE WAJUA NAMNA YA KUNUNUA, KUUZA HISA

$
0
0

Na  Bashir  Yakub

Katika adhima ya  ya mwendelezo wa makala za namna ya kuendesha kampuni leo tena tuangalie  kuhusu hisa na hasa namna ya kuhamisha hisa.

HISA NININI.

Kwa maana ambayo inaweza kueleweka kwa wepesi zaidi  ni kusema kuwa hisa  ni aina ya maslahi ya mtu ya katika kampuni.Natumia neno aina kwakuwa maslahi katika kampuni ni mengi si hisa tu isipokuwa hisa ni mojawapo ya maslahi. Hivyo kile ambacho mtu anamiliki katika kampuni  ndio hisa zake. Hisa hutofautiana kutokana na uwezo wa mtu kwa maana wapo wenye hisa ndogo wapo wenye kubwa na kati.

KUUZA  NA  KUNUNUA  HISA.

Hisa ni mali inayohamishika. Ni mali sawa na mali nyingine zozote zinazohamishika. Kama ambavyo malinyingine zinaweza kununuliwa au kuuzwa, kutolewa zawadi na kurithiwa ndivyo pia hata hisa zinavyoweza kuwa.Hii yote huitwa kuhama kwa hisa. Kuhama kwa hisa kwa lugha ya kitaalam  ambayo ndio hutumika katika katiba za makampuni ni ( Transfer of shares). 
Mara nyingi suala la  kuuziana hisa linawahusu wanahisa wenyewe na hivyo  wanahisa wanapokuwa wameuziana hisa au wamepeana zawadi   ni lazima nyaraka inayoonesha muamala huo wa mauziano au zawadi ambayo ina muhuli wa wakili  iwasilishwe kwenye uongozi wa kampuni kwa ajili ya kusajiliwa.  Kama hakuna nyaraka yoyote iliyowasilishwa mbele ya kampuni  kuthibitisha uhamisho  ni kosa kampuni kusajili uhamisho au mauziano hayo.

SHIMUTA, NSSF WAMJAZA MANOTI MJANE WA GURUMO

$
0
0
Hatimaye mjane wa marehemu Muhidini Gurumo, Pili Kitwana amepokea Sh2 milioni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF kwa ajili ya ununuzi wa Bajaji.

NSSF ilitoa fedha hizo ikiwa ni juhudi za Shirikisho la Muziki nchini (SHIMUTA), ambapo walimuahidi kumpatia mjane huyo kiasi cha fedha ambacho kitamuwezesha kununua bajaji imsaidie kuendesha maisha yake.

"Mwaka huu mwezi wa tano tulimuahidia mama Gurumo tutamsaidia kusaka fedha kwa wadau mbali mbali tuweze kufanikisha azma yetu ya kununua Bajaji, tuliomba NSSF na leo wamempatia mjane wa Gurumo Sh2 milioni."alisema Addo November Rais wa SHIMUTA na kuongeza

"Shirikisho tulishampa Sh1.2 na leo anapatiwa Sh2 milioni lengo letu lilikuwa bajaji lakini anakabidhiwa fedha rasmi yeye ni mtu mzima ataamua mwenyewe fedha hizo kama atazitumia kwa matumizi yake au kwa biashara ni umauzi wake, lakini sisi kama shirikisho bado tunaendelea na juhusi zetu za kuhakikisha tunamsaidia kwa njia moja au nyingine."alisisitiza.

Naye Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa (NSSF), Juma Kintu alisema "tunathamini michango ya wasanii, tunajua bajaji itamsaidia kuingiza mapatoa, hakuna asiyefahamu mchango wa Gurumo kwenye tasnia ya muziki, NSSF tutaendelea kusaidia wasanii wetu pale inapohitajika.

Mwanamuziki mkongwe Kassim Mapili akizungumzia hilo huku akijipigia chapuo asaidiwe dawa za ugonjwa wake wa moyo alisema "Gurumo hakuwa mvivu wa kazi toka enzi za Nuta, Juwata hadi Msondo, alitutoka tarehe kama ya leo, NSSF nisaidieni na mimi nipate hela za kununua dawa nasumbuliwa na ugonjwa wa moyo, nililazwa Muhimbili kwa wiki mbili mpaka sasa natumia dawa.

Hata hivyo, ofisa mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu alisema ombi hilo wamelipokea na kuitaka SHIMUTA kuandika barua rasmi ili waweze kumsaidia mkongwe huyo wa muziki.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu (wa pili kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil 2 kwa mjane wa marehemu Muhidini Gurumo, Pili Kitwana.katikati ni Shirikisho la Muziki nchini (SHIMUTA),Addo November.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images