Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

kishapigwa mweleka.....


hivi mchepuko huu unaruhusiwa??

$
0
0
Hapa ni eneo la Tabata Relini jijini Dar,ambapo hilo daladala liliamua kuchepuka baada ya kuona msongamano katika njia husika.hivi inaruhusiwa kweli kufanya hivi??
alianzia huku mchepuko wake.

WAGANDA WAMPONZA PHIRI, GORAN KUTUA LEO!!

$
0
0
Wachezaji wa Simba raia wa Kiganda ndio wamemponza kocha Mzambia Patrick Phiri kufungashiwa virago ndani ya klabu hiyo ya Msimbazi huku Mserbia Goran Kopunovic akitarajiwa kutua rasmi kesho Jumatano.

Habari za uhakika kutoka Simba zinasema kuwa uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti wake Evans Aveva uliketi juzi usiku majira ya saa mbili na kikao kumalizika saa saba usiku kwa maazimio ya kumfukuza Phiri na jana jioni alikabidhiwa rasmi barua yake ya kuachishwa kazi na nafasi yake kuchukuliwa na Serbia, Goran Kopunovic.

Chanzo hicho kinasema kuwa matokeo mabovu dhidi ya Kagera ndio yamemponza Phiri kutimuliwa hasa baada ya kukaidi agizo la viongozi la kumtaka kocha huyo asiwapange wachezaji wote waganda.

"Kocha aliambiwa panga wachezaji alioenda nao Zanzibar na kufanya nao mazoezi kuanzia siku ya kwanza, akambiwa hata 'sub' (mabadiliko) wasiwepo lakini yeye alipomuona Okwi akaanza kushangilia mechi ya Kagera kapanga wachezaji aliotaka yeye matokeo yake timu ikafungwa.

Wachezaji waganda waliomponza Phiri ni Joseph Owino, Emmanuel Okwi, Dan Sserunkuma, Juuko Murshid na Simon Sserunkuma.

Akizungumzia suala hilo Phiri alisema "Nipo tayari kupokea lawama zozote nilishasema toka mwanzo, wao wameamua hivyo mimi sina jinsi ingwa mpaka muda huu (saa saba mchana jana) Aveva (Mwenyekiti wa Simba) hajaniambia chochote.

"Ila najua kila kinachoendelea, najua wameshatoa uamuzi ya kunifukuza nasubiri Aveva aniambie rasmi, najua walikuwa na kikao, kuna mtu mmoja alinipigia na kunieleza kila kitu kilichokuwa kinaendelea kwenye kikao chao na uamuzi waliyochukua, nipo tayari nasubiri tu uongozi uniambie rasmi." alisema na kudai kuwa iwapo uongozi hautampa barua ya kuvunja mkataba wake ataendelea na mazoezi leo kwenye uwanja wa TCC na mchana ataelekea Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Hata hivyo mmoja wa viongozi wa Simba alisisitiza tayari wameshaafikia kuvunja mkataba na Phiri na kumlipa mshahara wake wa miezi miwili kama fidia ambayo ni dola 10,000. Phiri amekuwa akilipwa dola 5,000 kwa mwezi.

Kiongozi huyo pia alidai kuwa timu hiyo itaenda Zanzibar ikiwa chini ya kocha msaidizi Selemani Matola.

Katika hatua nyingine ya mastaa watatu wa klabu hiyo wametimua nchini Uganda kutaka fedha zao na si mali kauli. Habari za kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo ya Msimbazi zinasema kuwa Waganda hao wamekwea pipa jana asubuhi wakishinikiza uongozi wa Simba uwape fedha zao.

"Owino ana mgogoro na viongozi kwa vile aligoma kusaini mkataba akishinikiza arekebishiwe maslahi yake uongozi haukufanya hivyo Owino akagoma kusaini, viongozi ndio wamemuwekea bifu hawataki apangwe kwenye mechi, "Juuko Murshid na Simon Sserunkuma wao wanadai fedha zao za usajili na mpaka sasa uongozi unawazungusha.

Blog ya Jamii iliwatafuta viongozi wa Simba kwa nyakati tofauti akiwemo mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria Hans Pope lakini simu yake ilikuwa ikiita kwa muda mrefu bila kupokelewa hali kadhalika kwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Evans Aveva na katibu mkuu Steven Ally.

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZOEZI KITAIFA KUFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Chama cha Mchezo wa Mazoezi ZABESA Amer Mohd Makame akielezea madhumuni ya kufanyika kwa Tamasha la kwanza la siku ya mazoezi 01/01/2015 katika ukumbi wa Wizara ya habari Utamaduni Utalii na Michezo alipokutana na Waandishi wa Habari Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Mazoezi ZABESA Mohd Zidi akifafanua jambo katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maadhimisho ya siku ya Mazoezi Kitaifa 01/01/2015 yatakayo fanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar,ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein,na Ujumbe wa Mwaka huu ni Fanya Mazoezi Imarisha Afya yako Epuka Maradhi yasioambukiza. PICHA NA YUSSUF SIMAI-HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

AirAsia QZ8501: Forty bodies found in missing plane search

$
0
0
At least 40 bodies have been recovered from the sea in the search for missing AirAsia Flight QZ8501, the Indonesian navy says.

The bodies were spotted along with debris floating in the Java Sea off the Indonesian part of Borneo, in one of the search zones for the plane.

There has been no official confirmation that the remains come from the plane.

The Airbus A320-200, carrying 162 people from Surabaya in Indonesia to Singapore, disappeared on Sunday.

The search operation is now in its third day, with the area widened to cover 13 zones over land and sea.

In a separate development, there were reports of a second incident involving an AirAsia plane at Kalibo in the central Philippines. The reports said the plane overshot the runway.

OLD IS GOLD TAARAB KUFANYIKA MKESHA WA MWAKA MPYA NDANI YA SAFARI CARNIVAL

$
0
0
Na Andrew Chale

SAFARI Carnival kwa kushirikiana na Asia Idarous Khamsin (Fabak fashions) usiku wa 31/12/2014, Wameandaa shoo maalum ya Mkesha wa mwaka mpya 'Old Is Gold taarab', Ndani ya ukumbi wa Safari Carnival, Kawe jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin alieleza shoo hiyo maalum wadau

mbalimbali watakutana kuupokea mwaka kwa pamoja huku wakipata burudani ya muziki wa taarab wa zamani 'Old is Gold' pamoja na 'Surprise' kibao.

"Kwa kiingilio cha sh 5,000, tu, Fabaki fashions na Safari Carnival, tumeandaa usiku huu maalum wa Mkesha wa mwaka mpya.

Utakaoambatana na burudani ya taarab za zamani na za sasa pamoja na Surprise mbalimbali" alisema Asia Idarous.

Aidha,  Asia Idarous alisema usiku

huo, pia umedhaminiwa na Michuzi Media Group, Clouds fm,Gone Media, Maji Poa na wengineo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA MABALOZI WA URUSI, CANADA NA ALGERIA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Mhe. Djelloul Tabel, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Zoka, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga akienda kuanza kazi rasmi nchini Canada.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Alexander Rannkikh, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.

AZAM, MTIBWA, SIMBA, YANGA KUCHEZA MAPINDUZI


Miss Tanzania 2014 asaidia kituo cha New Life Orphans Home,Boko jijini Dar

$
0
0
Miss Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akimkabidhi zawadi ya mwaka mpya Msimamizi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life kilichopo Boko, Mwanaisha Magambo kwa ajili ya watoto 102 waliopo kituoni hapo, tukio hilo lilifanyika juzi.
Miss Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akiwa na Miss Kinondoni Maria Shila wakiwa wamembeba mtoto aliekuwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life cha Boko, mtoto huyo alifikishwa hapo akiwa na siku nne tu tangia kuzaliwa kwake.
Sehemu ya Watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life kilichopo Boko,wakimsikiliza Miss Tanzania Lilian Kamazima.

CelebrateTwaweza 8Jan2015

Afro Urban Night in Berkshire,New-Years Eve Red Carpet Party

$
0
0
The Biggest Afro Urban Night in Berkshire,New-Years Eve Red Carpet Party in Style..!on Wed 31st Dec jumpoff 2015 No work on Thursday@ Riley's Sports Bar rg1 8nq featuring The Finest Deejays on Rotation Dj Deejay Collo /Dj Richie Dee /Dj Say Camara / D.j. Gich time 10pm till 4am Damage £10 all Night.!! Attractions on the night: -FREE SHOTS AT THE ENTRANCE BEFORE MIDNIGHT & BOTTLE OF WINE for best dressed Lady + Gent..For Birthdays & VIP Bookings HOT LINE: 07853482158 / 07446135676 / 07450289941BONGODEEJAYS EVENT ORGANISER / CLUB PROMOTER / TALENT /ARTIST MANAGAMENT 
For Entertainment News & Free Dj mixes for download logon www.bongodeejays.com
 For Booking Contact  Bongo Deejays
Bongo Deejays Quality through Experience


TAARIFA YA UFAFANUZI WIZARA YA NISHATI NA MADINI

$
0
0
Katika gazeti la NIPASHE la Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014 ziliandikwa habari kuhusu Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) chini ya kichwa cha habari “Wanaomtetea Muhongo Wajibu haya”. 
Hoja zilizotolewa katika gazeti hilo zililenga kupotosha ukweli. 
Wizara inapenda kutoa maelezo kuhusu hoja zilizotolewa kama ifuatavyo: BOFYA HAPA

ngoma azipendazo ankal - Special request by Wabogojo

WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF WACHIMBA MTARO WA MAJI

$
0
0
WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF WACHIMBA MTARO WA MAJI  KUPITIA UTARATIBU WA AJIRA YA MUDA KATIKA SHEHIA YA MPAPA,MKOA WA KUSINI UNGUJA.

Maelfu ya wakazi wa shehia ya Mpapa wilaya ya Kusini Unguja wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa maji unaotekelezwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaoratibiwa  na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa utaratibu wa ajira ya muda PWP.

Wakizungumza katika eneo la mradi baadhi ya walengwa hao wameonyesha utayari wao katika kuchimba mtaro huo huku wakiipongeza  serikali kupitia TASAF kwa kubuni utaratibu huo ambao wamesema licha ya kuwaongezea fedha lakini pia utapunguza kero ya upatikanaji wa maji katika eneo lao .

Chini ya utaratibu wa ajira za muda ,walengwa kutoka kaya maskini huibua miradi katika eneo lao na kuitekeleza na kisha kulipwa ujira ikiwa ni mkakati wa TASAF wa kuziongezea kaya maskini kipato kwa kukidhi mahitaji muhimu hususani katika Nyanja za elimu,afya,lishe na uchumi, ambapo kwa mujibu wa utaratibu asilimia  75 ya fedha ni malipo kwa walengwa wakati asilimia 25 ni kwa ajili ununuzi wa vifaa .

Mpango wa ajira za muda utatekelezwa nchini kote wakati wa kipindi cha hari au kipindi kigumu kama wakati wa ukame au mafuriko kupitia Mpango wa Kunusuru  kaya maskini,PSSN ambao umebuniwa na  serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na unatarajiwa kuhudumia kaya maskini zipatazo laki tisa na ishirini elfu nchini kote kazi ianayotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Marchi 2015.

ifuatazo ni picha za baadhi ya wananchi wa shehia ya Mpapa mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi ya kuchimba mtaro wa maji kupitia utaratibu wa ajira za muda.
 Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika shehia ya Mpapa mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi ya uchimbaji wa mtaro wa maji kupitia Mpango wa ajira za muda ambao huwawezesha walengwa kulipwa fedha .
 Mtaro wa maji uliochimbwa na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika shehia ya Mpapa wilaya ya Kusini Unguja inayotekelezwa chini ya mpango wa ajira za muda kupitia TASAF.

Mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini wa TASAF katika shehia ya Mpapa wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja akishiriki kazi ya kuchimba mtaro wa maji.

Serikali yatakiwa kusitisha uporomokaji wa bei za Filamu Nchini - Wadau

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel aliyesimama akifungua Mkutano Baadhi ya wasambazaji wa Filamu nchini (hawapo pichani)kuhusu kuporomoka kwa bei ya filamu, wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini. Bi. Joyce Fissoo.Mkutano huo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam

Na Genofeva Matemu – Maelezo

Serikali imewapongeza wasambazaji na wadau wa filamu nchini kwa mchango wao mkubwa katika kuelimisha, kuhabarisha na kufundisha maadili ya mtanzania huku wakichangia katika pato la taifa na kukuza uchumi wa nchi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokua akifungua mkutano wa serikali na wasambazaji wa filamu nchini jana jijini Dar es Salaam kujadili uporomokaji wa bidhaa za filamu nchini.

“Tunathamini sana kazi mnayoifanya, Serikali inawajali na ipo tayari kushirikiana nanyi kwa kazi nzuri mnayoifanya hivyo ni vema kufanya mkutano huu kuwa wa kisanyansi kwa kuangalia gharama mnazotumia kuandaa bidhaa za filamu ili kuweza kukua kibiashara na kukuza uchumi wa nchi” amesema Pro. Gabriel.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo amesema kuwa Bodi haitaruhusu bidhaa zilizo chini ya kiwango kupelekwa kwa watanzania kwa daraja la bei ya chini pamoja na soko huria kwani hakuna uhuria usio na mipaka.

Bibi Fisoo amesema kuwa wananchi siyo dust bin wanapaswa kupelekewa kazi bora na zenye hadhi kwani Bodi inahitaji kujiridhisha kuhusu viwango vya filamu hizo na kuheshimu fedha za watanzania kwa kuwauzia kazi bora zinazoendana na thamani ya fedha zao.

Aidha Mwenyekiti wa wasambazaji wa bidhaa za filamu nchini Bw. Emmanuel Miamba amewataka wadau na wasambazaji wa filamu nchini kuwa wakweli, wazalendo, pasipo kuogopa kitu chochote na kuangalia maslai ya wasambazaji wote na kama wataona uwekezaji katika kazi za filamu haulipi basi wawekeze katika masuala mengine na sio kushusha bei kuua tasnia ya filamu nchini.

Naye Bw. Chacha Matula kutoka Jembe entertainment amewaomba wasambazaji kuwa na umoja na mshikamano utakaowawezesha kushirikiana kwa pamoja na serikali kusitisha uporomokaji wa bei za filamu na kuwadhibiti watu wanaotaka kuua kampuni za wasambazaji wadogo nchini.

MTUNZI MKONGWE WA VITABU ZANZIBAR AZINDUA VITABU VITATU VYA HADITHI ZA KALE

$
0
0
Mtunzi mkongwe wa vitabu Zanzibar Bi. Fatma Moh’d Salim (Jinja) akionyesha vitabu vya hadithi za kale alivyovitunga, katika sherehe za uzinduzi wa vitabu hivyo zilizofanyika nyumbani kwake Chukwani Zanzibar.
Mwandishi wa Habari wa Redio Annur Fm Kasim Khamis akimuuliza suali Bi. Fatma Jinja kuhusiana na utunzi wa vitabu vyake alivyo vizindua.
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa vitabu hivyo wakimskiliza Bi. Fatma Jinja (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo juu ya utunzi wa vitabu hivyo .
Waandishi wa Habari wakifanya mahojiano na mtunzi wa vitabu Bi. Fatma Jinja huko nyumbani kwake Chukwani Zanzibar baada ya uzinduzi wa vitabu vyake. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM

Tupende na tuuenzi utamaduni na asili yetu watanzania

TCAA WATOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI KWA KITUO CHA KULEA YATIMA CHA HNEW HOPE FAMILY KILICHOPO MWASONGA KIGAMBONI JIJINI DAR

$
0
0
Afisa habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Ali Changwila akimkabidhi Peter Benard gunia la mchele kwaniaba ya wenzake wakati walipokwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo mafuta ya kupikia na madaftari kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kuleta yatima cha New Hope Family chenye watoto 36. Kilichopo mwasonga kigamboni jijini kata ya kisarawe 2 ,Temeke jijini Dar es Salaam.
Mshauri wa Kituo cha kule watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu cha New Hope family Maiko Lugendo ,( kulia) akimuonyesha Afisa habari wa Mamka ya usafiri wa anga Tanzania (TCAA) Ali Changwila wakati walipokwenda kutoa msaada wa vitumbalimbali vikiwemo vyakula kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya kwenye kituo hicho kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe 2 Kigamboni jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Hellen Erasto. 

IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' NA COSMAS CHEKA KUZICHAPA FEBRUARI 28,2015

$
0
0
Mratibu wa mpambano wa ubingwa wa U.B.O Africa,Antony Rutta (katikati) akiwainua mikono juu mabondia Cosmas Cheka (kushoto) na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaopigwa  februari 28,2015  katika ukumbi wa frends corner manzese jijini Dar es salaam.
Mabondia Cosmas Cheka (kushoto) akitunishiana misuli na Ibrhahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O Africa utakaofanyika februari 28,2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam. picha na SUPER D BOXING NEWS
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images