Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 688 | 689 | (Page 690) | 691 | 692 | .... | 3272 | newer

  0 0

  BENKI ya Posta Tanzania (TPB), Tawi la Tunduma imetoa mafunzo kwa wajasiriamali wa Tunduma, wilayani Momba. Semina hiyo iliyohudhuriwa na wajasiriamali wapatao 100, ililenga kuwaelimisha wafanyabiashara hao kuhusu matumiza mazuri ya huduma za kibenki, hususan mikopo inayotolewa na benki hiyo.

   Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiudy Saideya, aliipongeza Benki ya Posta kwa kutoa mafunzo ambayo alisema yanawasaidia wafanyabiashara wa Tunduma kukuza uelewa wa matumizi sahihi ya huduma zinazotolewa na taasisi za fedha. 

   Aliwashauri wafanyabiashara wachukue mikopo ili kukuza mitaji yao na kuongeza uzalishaji, lakini bila kuwa na elimu sahihi juu ya matumizi ya mikopo hiyo faida yake inaweza isipatikane. "Nawashauri wafanyabiashara mnaohudhuria semina hii kutimia fursa hii kujadiliana na benki ya Posta ili mfikie muafaka katika huduma mnazozitaka," alisema Mkuu wa Wilaya hiyo. 

   Aidha aliwaasa wafanyabiashara kujiepusha na biashara haramu zitokanazo na bidhaa haramu zilizozagaa mpakani mwa wilaya yao, kwani kufanya hivyo bishara zao zinaweza kutaifishwa na hivyo kupoteza mitaji yao bila kujua. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya Posta, Henry Bwogi iliwasisitiza wafanyabiashara hao kutembelea tawi la benki hiyo lililopo Tunduma ili kujipatia huduma zote za kibenki hususan mikopo itakayowawezesha kukuza mitaji yao. 

  Pamoja na hayo aliongeza kuwa benki ya TPB inatoa mikopo ya aina nyingi, kuanzia ile ya vikundi hadi ya wafanyabiashara wakubwa, huku riba zinazotozwa na benki hiyo ni nafuu sana.
  Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiudy Saideya akizungumza katika mafunzo kwa wajasiliamali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), Tawi la Tunduma.Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiudy Saideya akizungumza katika mafunzo kwa wajasiliamali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), Tawi la Tunduma.Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo Tunduma.Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasilia mali yaliyotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB) ikiwa ni jitihada za benki hiyo kutoa elimu ya namna ya kutumia mikopo na kuelezea fursa zilizopo katika Benki hiyo Tunduma.Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasiliamali wakipiga picha za kumbukumbu mara baada ya semina hiyo.Baadhi ya washiriki katika mafunzo kwa wajasiliamali wakipiga picha za kumbukumbu mara baada ya semina hiyo.

  0 0

  Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Tambwe akiipatia timu yake bao la kusawazisha katika mtanange wa muendelezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam leo.Mechi hiyo imemalizika kwa timu zote kufungana bao 2-2.Magoli ya Azam yametiwa kimiani na Didier Kavumbagu (dakika ya 5) na John Bocco (dakika ya 65) wakati magoli ya Yanga yakifungwa na Hamis Tambwe (dakika ya 7) huku goli la pili likufungwa na Simon Msuva (dakika ya 51).Picha zote na Othman Michuzi.
  Mfungaji wa goli la kwanza kwa timu ya Yanga,Hamis Tambwe na Mfungaji wa Bao la pili,Simon Msuva wakishangia ushindi wao dhidi ya timu ya Azam katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam leo.
  Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi na Washabiki wao.
  Wachezaji wa timu ya Azam FC wakishangilia goli yao la kwanza dhidi ya Yanga.


  0 0


  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Mlele Mkoani Katavi kwenye shule ya Sekondari ya Mamba Desemba 28, 2014.
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimia na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Mlele mkoani Katavi wakati alipowasili kwenye shule ya Sekondari ya Mamba kufungua Mkutano wa Baraza hilo Desemba 28, 2014.


  0 0

  Warembo walioshika nafasi za kwanza za Miss Temeke walipofanya hafla ya kumpongeza Joketi Mwegelo kwa mafanikio ya kupata mkataba mnono wa dola milion 5 hivi karibuni. Hafla ya kumpongeza ilifanyika juzi kwenye hoteli ya Kempiski Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam.
  Kutoka kushoto; Miss Temeke 2004, Cecylia Assey, Happyness Magese ' Millen' (2001), Joketi Mwegelo ( 2006) na Miss Temeke 2014, Sitti Mtemvu. Nyuma Mshindi wa tatu 2013, Edda Sylvester, mshindi wa pili 2013, Narietha Boniface na mshindi wa pili 2011, Cynthia Kimasha.

  0 0

  Sheikh Ali Mzee Comorian (pichani) amefariki dunia muda mchache uliopita nyumbani kwake mtaa wa Kariakoo jijini Dar es salaam. Shughuli za maziko zinafanyika hapo hapo nyumbani kwake.
  Habari ziwafikie ndugu, jamaa, marafiki na majirani popote pale walipo.
    Maziko yatafanyika kesho Jumatatu saa nne asubuhi. Atasaliwa Msikiti wa Makonde na atazikwa katika Viunga vya Wangazija mtaa wa Bibi Titi Mohamed, Dar es salaam.

   Mwenyezi Mungu ampe Kauli Thabit 
   Imetolewa na:
  Abdulrahman S. I.  Mbamba

  0 0
 • 12/28/14--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • 0 0

  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Mh. Prof. Mark Mwandosya akiwa kwenye picha ya pamoja na wajukuu zake wakati wa kusherehekea kutimiza miaka 65 ya kuzaliwa kwake,aliyoiadhimisha jana huko kijijini kwake Lufilyo, Busokelo, Wilayani Rungwe.
  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Mh. Prof. Mark Mwandosya akikata keki sambamba na wajukuu zake wakati wa kusherehekea kutimiza miaka 65 ya kuzaliwa kwake,aliyoiadhimisha jana huko kijijini kwake Lufilyo, Busokelo, Wilayani Rungwe.
  Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Mh. Prof. Mark Mwandosya na Mkewe Mama Lucy Mwandosya (wa pili kushoto nyuma) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajukuu zao wakati wa kusherehekea kutimiza miaka 65 ya kuzaliwa kwa Mh. Mwandosya,aliyoiadhimisha jana huko kijijini kwake Lufilyo, Busokelo, Wilayani Rungwe.

  0 0

  Na  Bashir  Yakub
  Katika adhima ya  ya mwendelezo wa makala za namna ya kuendesha kampuni leo tena tuangalie  kuhusu hisa na hasa namna ya kuhamisha hisa. 

  HISA NININI.
  Kwa maana ambayo inaweza kueleweka kwa wepesi zaidi  ni kusema kuwa hisa  ni aina ya maslahi ya mtu ya katika kampuni.Natumia neno aina kwakuwa maslahi katika kampuni ni mengi si hisa tu isipokuwa hisa ni mojawapo ya maslahi. Hivyo kile ambacho mtu anamiliki katika kampuni  ndio hisa zake. Hisa hutofautiana kutokana na uwezo wa mtu kwa maana wapo wenye hisa ndogo wapo wenye kubwa na kati. 

  KUUZA  NA  KUNUNUA  HISA.
  Hisa ni mali inayohamishika. Ni mali sawa na mali nyingine zozote zinazohamishika. Kama ambavyo mali nyingine zinaweza kununuliwa au kuuzwa, kutolewa zawadi na kurithiwa ndivyo pia hata hisa zinavyoweza kuwa.Hii yote huitwa kuhama kwa hisa. Kuhama kwa hisa kwa lugha ya kitaalam  ambayo ndio hutumika katika katiba za makampuni ni ( Transfer of shares). Mara nyingi suala la  kuuziana hisa linawahusu wanahisa wenyewe na hivyo  wanahisa wanapokuwa wameuziana hisa au wamepeana zawadi   ni lazima nyaraka inayoonesha muamala huo wa mauziano au zawadi ambayo ina muhuli wa wakili  iwasilishwe kwenye uongozi wa kampuni kwa ajili ya kusajiliwa.  Kama hakuna nyaraka yoyote iliyowasilishwa mbele ya kampuni  kuthibitisha uhamisho  ni kosa kampuni kusajili uhamisho au mauziano hayo. 


  0 0


  theNkoromo Blog, Singida
  Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.

  Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu wanayotaka Watanzania.

  Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.

  Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.

  "Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa moto", alisema Nyalandu

  Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM", alisema.

  Mkutano huo wa jimbo ambao ulipambwa na shamrashamra mbalimbali zikiwemo za wasanii wakiwemo kina Rose Mhando, ulifurika maelfu ya wananchi waliohamasika kumsikiliza Nyalandu.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo.


  0 0

  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa CCM wa Tawi la Kilimahewa lililoko katika Kata ya Mwenge Ndugu Mohammed Madodo mara baada ya kuwasili katika Tawi hilo kwa ajili ya mkutano na viongozi wa Tawi tarehe 28,12.2014.
  Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akihutubia wajumbe wa Halmashauri ya Tawi la Kilimahewa huko Lindi Mjini wakati wa ziara yake ya kuyatembelea matawi ya CCM wilayani humo tarehe 28.12.2014.
  ‘Kitu hicho!……Chukua’ Ndivyo alivyosikika akisema Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM Mama Salma Kikwete wakati alipokuwa akiongea na viongozi wa CCM wa Tawi la Kilimahewa .


  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band a.k.a FFU-Ughaibuni a.k.a "watoto wa mbwa" au viumbe wa ajabu "Anunaki anunnaki aliens" yenye makao yake nchini Ujerumani, inatoa Salam za heri ya mwaka mpya 2015 kwa wadau wote popote pale mlipo,mwaka mpya 2015 uwe wa mafanikio ,Amani na Upendo kwa wote. 
  HAPPY NEW YEAR 2015 ! HAPPY NEW YEAR 2015 ! 
  msikose burudani kamili bofya 
  moja ya show za Ngoma Africa band nchini Ujerumani.

  0 0

  NesiWangu Show ni kipindi kinachokusudia kuongeza mwako katika uwanja wa Afya, upatikanaji wa huduma zake na elimu-afya kwa jamii.
  Katika kipindi hiki, tunazungumza na Mkurugenzi wa Jenga Tanzania Foundation, Nassor Basalama anayezungumzia kuhusu kipimo cha Malaria ambacho Jenga Tanzania Foundation inapanga kukisambaza bure kwa watu wa kipato cha chini nchini Tanzania.
  Karibu uungane nasi

  0 0

  Meneja wa ATM na Kadi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Wambura John (kushoto) akiweka pesa kwa kutumia ATM katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya kuweka pesa (deposit) kwa kutumia mashine za ATM ya benki ya NBC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni mteja wa benki hiyo, Francis Xavier na kulia ni Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter
  Mteja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Francis Xavier (kushoto) akiweka pesa (deposit) katika mashine ya ATM ya benki hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja wa ATM na Kadi wa NBC, Wambura John (katikati) na Meneja Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter.

  BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma mpya ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM jijini Dar es Salaam katika juhudi za benki hiyo kuboresha huduma za kifedha nchini.

  Kuanzishwa kwa huduma hiyo kunathibitisha malengo ya benki hiyo ya kutoa huduma sahihi na ya wakati kwa wateja wake nchini nzima na huduma hii ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM itakuwa ikipatikana masaa 24 kila siku.


  0 0

  Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akimpongeza Mhe. Mansour Yussuf Himid baada ya kuamua kujiunga na chama hicho na kumkabidhi rasmi kadi ya CUF katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.
  Mwanachama mpya wa CUF Mansour Yussuf Himid akizungumza na wanachama wenzake , baada ya kujiunga na chama hicho katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.
  Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.


  0 0
  0 0

  Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Notker Kilewa (kulia) akielimisha abiria wa basi liendalo Morogoro wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika leo Mkoani Pwani kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima madereva kiwango cha pombe mwilini. Akisikiliza kwa makini ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto).
  Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Notker Kilewa (kushoto) akielimisha abiria wa basi liendalo Morogoro wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika leo Mkoani Pwani kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia).


  0 0
 • 12/29/14--06:02: YALE YALEEEE......

 • 0 0

  Walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF wameanza utekelezaji wa miradi ya ajira za muda na kisha kulipwa ujira katika miradi wanayoibua kwenye maeneo yao .
  Walengwa wa vijiji kadhaa vilivyoko kwenye Mpango huo kikiwemo kile cha Mzuri na Kijini vilivyoko katika eneo la Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wameanza kutengeneza barabara yenye urefu wa zaidi ya kilometa moja na vitalu vya miche ya miti ya asili na matunda katika eneo lao na kisha kulipwa fedha chini ya utaratibu ulioandaliwa na TASAF ambao ni moja ya mkakati  wa kuwaongezea kipato walengwa na kupambana na umaskini.


  Akizungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo Sheha wa eneo hilo Bwana Mwita Masemo Makungu amebainisha kuwa mpango huo umeitikiwa vizuri na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika eneo hilo na kuwa jitihada hizo za TASAF zimeamsha ari ya wananchi kujiletea maendeleo kwenye maeneo yao na kupunguza kero ya barabara iliyokuwa inawakabili.


  Hata hivyo Bwana Makungu amesema pamoja na ushiriki wa wananchi kwenye kazi hiyo kupitia mpango wa ajira za muda bado wananchi hao wanakabiliwa na tatizo la vifaa na utaalamu hususani katika ujenzi wa barabara ambao unahitaji vifaa vizito ambavyo havipo kwenye maeneo yao na hivyo kuomba serikali kuona namna ya kukamilisha kazi hiyo.


  Zifuatazo ni baadhi ya picha za walengwa wa PSSN katika wilaya ya Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wakishiriki katika kazi kupitia ajira za muda PWP.
  Kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini -Makunduchi mkoa wa kusini Unguja ambayo ni moja ya mkakati wa TASAF wa kuwaongezea kipato walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia ajira ya muda PWP.

  Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na TASAF katika kijiji cha Kijini Makunduchi mkoa wa kusini Unguja wakishiriki katika kazi za ujenzi wa barabara kupitia mpango wa ajira za muda PWP.

  Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini katika eneo la Kijini Makunduchi mkoa wa kusini Unguja wakiwa katika harakati za ujenzi wa barabara kupitia mpango wa ajira za muda PWP kupitia TASAF.

  Barabara inayojengwa kupitia mpango wa ajira ya muda PWP ambapo walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini kupitia TASAF wakiwa katika eneo la mradi wa barabara yenye urefu wa kilometa Moja .

  Wakazi wa kijiji cha Mzuri -Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja wakiwa katika mradi wa kitalu cha miti moja ya mradi ulioibuliwa na walengwa wenyewe kupitia PWP unaoendeshwa na TASAF ambapo walengwa hulipwa fedha kwa kazi hiyo.

  0 0

  Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba fupi kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Jinsia kwa Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza, leo Desemba 29, 2014 katika Ukumbi wa Rombo Green View Hotel. Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili ambapo yatafungwa rasmi kesho Desemba 30, 2014(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunura(wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Augustino Mboje(kulia) ni Mkuu wa Mafunzo ya Kijeshi wa Magereza, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Mbarak Semwenza.
  Baadhi ya Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza wanaoshiriki Mafunzo ya Jinsia katika Ukumbi wa Rombo Green View Hotel wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi. Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili ambapo yatafungwa rasmi kesho Desemba 30, 2014.
  Mshiriki wa Mafunzo ya Jinsia kutoka Makao Makuu ya Magereza, Mkaguzi wa Magereza, Amina Lidenge akijitambulisha kabla ya Ufunguzi rasmi wa Mafunzo ya Jinsia.
  Mtoa Mada wa Kwanza kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Magreth Mussai akiwasilisha Mada yake kuhusiana na dhana ya Jinsia kama anavyoonekana katika picha.
  Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa, Askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza(waliosimama) mara baada ya Ufunguzi rasmi wa Mafunzo ya Jinsia leo Desemba 29, 2014 katika Ukumbi wa Rombo Green View Hotel, (kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Kato Rugainunura, (wa pili kushoto) ni Mtoa Mada wa Kwanza kutoka Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Magreth Mussai(wa pili kulia) ni Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwila, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Loyce Luhembe, (kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Augustino Mboje(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akisalimiana na Katibu mkuu wa Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea kwa ajili ya kumjulia hali, nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana. Mh Lowassa alikuwa Zanzibar kwa mapumziko ya kusherekea skukuu ya Krismasi.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akiwa katika mazungumzo na Katibu mkuu wa Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana. Mh. Lowassa alikuwa Zanzibar kwa mapumziko ya kusherekea sikukuu ya Krismasi. Kushoto ni Mke wa Sukwa, Fatma Mussa.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Katibu wa Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana.

older | 1 | .... | 688 | 689 | (Page 690) | 691 | 692 | .... | 3272 | newer