Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 687 | 688 | (Page 689) | 690 | 691 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Download Single Mpya "Bou Nako-Ni Shida" HAPA https://mkito.com/song/ni-shida/9462
  Powered by @mkitodotcom @vmgafrica www.vmgafrica.com

  0 0
  0 0


  0 0


  0 0


  0 0
 • 12/26/14--19:00: ngoma azipendazo ankal

 •  Professor Jay ft Juma Nature - Ndio mzee

  0 0


  Na Mwandishi Wetu

  Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, Desemba 28, 2014 (kesho J’pili) atafanya mkutano mkubwa kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na wananchi wa Singida Vijijini na Watanzania wote kwa kutimiza miaka 15 ya ubunge.


  Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Mbunge huyo, Elia Diga, imesema kuwa mkutano huo ambao utaambatana na burudani mbalimbali, utafanyika katika Kata ya Ilongero na utahudhuriwa na viongozi wa Chama na serikali, viongozi wa dini zote na wananchi zaidi ya 20,000 kutoka kata zote zinazounda jimbo hilo na zile za jirani.  Katika mkutano huo, Nyalandu atahutubia wananchi pamoja na kueleza mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi chote cha miaka 15.  Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana mpaka sasa, Nyalandu pia ataeleza wananchi mwelekeo mpya wa jimbo hilo na mahali anapopenda lifike.  Viongozi wote wa CCM Wilaya ya Singida wakiongozwa na mwenyekiti wake, watahudhuria mkutano huo na kutoa hotuba fupi kwa wananchi.  Wasanii nyota wanaotamba nchini wakiongozwa na kundi la Makomandoo, Rose Muhando, Christina Shusho, H-Baba, Mchekeshaji Steve Nyerere na Bendi ya New Life Bandi watakuwepo kukonga nyoyo.  Pia kutakuwepo na vikundi  mbalimbali vya ngoma za asili vikiwemo Njagmba, Ilongero Group na vingine vingi vitakuwepo kutoa burudani.

  0 0

   
   NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuongoza Tamasha Maalumu la 'Upendo wa Mama' linalotarajiwa kufanyika katika Kanisa la Rutheran Mabibo Extenal jijini Dar es Salaam na kushirikisha waimbaji wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania. 

  Akizungumzia tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam, Rais wa taasisi ya Upendo kwa Mama Foundation yenye makao makuu yake mkoani Arusha, Injinia Carlos Mkundi alisema Naibu Waziri Nchemba ndiye mgeni rasmi wa Tamasha hilo maalumu ambalo pamoja na mambo mengine linafanyika kutambua mchango mkubwa wa mama kuanzia katika ngazi ya familia na jamii nzima. Injinia Mkundi alisema tamasha hilo litakalofanyika Januari Mosi, 2015 chini ya uratibu wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, litashirikisha waimbaji wa injili akiwemo Faraja Ntaboba kutoka Congo, Stella Joel, Ado Novemba, Jane Misso, Edson Mwasabwite wote kutoka jijini Dar es Salaam. 

  Na Rose Molel, Helen Kigazi wote kutoka mkoani Arusha. Injinia Carlos Mkundi na mwimbaji wa muziki wa injili ambaye naye atatumbuiza katika tamasha hilo, aliwataja waimbaji wengine ambao watashiriki katika tamasha ni pamoja na Mbunge, Matha Mlatta, Kwaya ya Mamajusi kutoka Moshi, mwimbaji Tumaini Njole, Messi Chengula na waimbaji wengine wengi. 

  "...Washiriki kila mmoja anaweza kuja na mamayake anayempenda pamoja na zawadi yake maalum, ambayo atamkabidhi wakati itakapotangazwa...kutakuwa na waimbaji wa muziki wa injili kutoka nje na ndani ya nchi ili kuleta mvuto zaidi tunawaomba wananchi wajitokeze zaidi kuja kutambua mchango wa mama na kuonesha upendo kwa mama zao," alisema Injinia Mkundi. 

  Akifafanua zaidi alisema Tamasha la Upendo kwa Mama litakuwa la bure na litaanza majira ya saa saba mchana siku hiyo na kuendelea hadi jioni litakapofungwa. Alisema siku hiyo washiriki wanaombwa kuja na zawadi maalumu ambayo kila mmoja atamkabidhi mamayake anayempenda katika familia zao. Rais wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, Injinia Caros aliongeza kuwa lengo lingine ni pamoja na kuwatia moyo akinamama na kuwaonesha upendo juu ya kazi kubwa wanayoifanya katika familia zao na jamii kwa ujumla.

   Alisema baada ya uzinduzi wa tamasha hilo kanisani hapo yataandaliwa matamasha mengine makubwa na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa pamoja na mengine katika mikoa mbalimbali. Aidha aliongeza tamasha kama hilo pia lilifanyika mkoani Arusha Novemba 16, 2014 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeib na kuwashirikisha akinamama zaidi ya 40,000.  

  0 0

  MISS Tanzania namba mbili 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za kibongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’,  leo ametoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Kulea Yatima cha Extrem kilichopo  Tandare kwa Bi Mtumwa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

  Mrembo huyo ambaye pia ni mkurugenzi  wa kampuni ya  Kidoti inayojihusisha na masuala ya urembo, alitoa msaada huo kama zawadi yake ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya kwa watoto hao kama sehemu ya kuwafariji ili nao kujiona wako sawa na wengineo wanaioshi nawazazi wao.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Jokate alisema kuwa ameguswa na kituo hicho ambacho huwa hakikumbukwi na wahisani kutokana na mazingira ya eneo hilo.

  “Nimefika hapa kutoa msaada kama sehemu ya kuonyesha ninavyoguswa na jamii ya watoto kama hawa, lakini pia nikiwa na lengo la kuwafariji ili nao kujiona ni sehemu ya jamii ya Watanzania,” alisema.

  Kidoti alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watu wenye uwezo, kampuni na taasisi mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii kwani nao wana haki ya kuishi na kufurahia maisha kama wengine.

  Msaada aliokabidhi kwa ushirikiano na kampuni ya Raibow Shell, ni mchele, unga wa sembe, sabuni, jozi za viatu vyenye nembo za Kidoti.

  Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, mlezi wa watoto hao, Mwamvua Jumanne, alitoa pongezi kwa Kidoti na kuwasihi wengine kuiga mfano wa mrembo huyo kusaidia makundi maalum.

  Akielezea changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mwamvua alisema ni kukosa uwezo wa kifedha kuwalipia ada watoto wanaosoma elimu ya msingi na sekondari, gharama za matibabu pamoja na kukosa watu wa kuwatembelea ili kuwafariji.
  Miss Tanzania namba mbili 2006, Mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegelo, akicheza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mtumwa Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. 
  Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegelo, akimpa zawadi ya ndala mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mtumwa Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti.
  Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegelo, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mtumwa Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na Jumanne Juma.

  0 0

  Naibu Waziri wa maji Amos Makala wapili toka kulia akimkabidhi mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mwezi Novemba Rashid Mandawa wa Kagera Sugar(wapili toka kushoto) hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 1/=na kombe kabla ya mechi kuanza kati ya Simba na Kagera Sugar ambapo simba ililala kwa bao 1-0. Wengine kulia ni Makamu Mwenyekiti wa bodi ya ligi Said Mohamed. Kushoto Ofisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.

  Wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wamekabidhi zawadi ya Sh. Milioni moja na kombe kwa mchezaji bora wa mwezi (Novemba) Rashid Mandawa wa Kagera Sugar.

  Zawadi hiyo ilikabidhiwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi ya raundi ya nane ya VPL ambayo Kagera Sugar waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Ijumaa.

  Akizungumza mara tu baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, mshambuliaji huyo wa Kagera Sugar aliwashukuru makocha, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kwa kumuunga mkono kwani alipata ushindani mkali kutoka kwa Fulgence Maganga wa Mgambo Shooting pamoja na Nahodha wa Simba,Mganda Joseph Owino waliofanya vizuri pia mwezi Novemba,Alisema Mandawa.

  "Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kutwaa tuzo hii, ninawashukuru pia watendaji wote wa Kagera Sugar na mashabiki wetu kwa kuniunga mkono. Huu ni mwanzo mzuri kwangu msimu huu. Nitajitahidi nifanye vizuri zaidi, ikiwezekana kutwaa tuzo ya mfungaji bora.

  "Mpaka sasa nina magoli manne ingawa watu wengi wanajua kwamba nina mabao matatu. Nilifunga dhidi ya JKT Ruvu, Polisi Morogoro, Coastal Union na Mtibwa Sugar. Ninawaahidi mashabiki wetu kwamba sitawaangusha," alisema Mandawa.

  Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema kampuni hiyo inajisikia fahari kwa wachezaji bora kupatikana kwani ni moja ya mafanikio ya jitihada zao na kampuni hiyo ipo tayari kuboresha maisha ya wachezaji wanaoshiriki ligi kuu ya Vodacom na maisha yao kuwa murua.Vodacom Tanzania itaendelea kuboresha ligi kuu kila mwaka na tutakuwa tunaleta ubunifu kila mwaka na tutaendelea kutoa zawadi hiyo kwa mchezaji anayefanya vizuri kila mwezi ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuongeza ushindani katika ligi hiyo alisema Nkurlu.

  Mandawa anakuwa mchezaji wa tatu kupewa tuzo hiyo tangu kuanzishwe utaratibu  huu katika msimu huu. Kiungo Antony Matogolo wa Mbeya,. ambaye amepelekwa kwa mkopo Panone FC ya Kilimanjaro, alikuwa mchezaji wa kwanza kupewa tuzo hiyo kama mchezaji bora wa Mwezi Septemba kabla ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy' kuibuka mchezaji bora wa Oktoba.

  Kikosi cha Kagera Sugar kilikosa huduma ya Mandawa katika mchezo uliopita dhidi ya Simba kwa sababu iliyoelezwa na Kocha Mkuu wa wakata miwa hao wa Kagera, Maganda Jackson Mayanja kuwa alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya kifundo cha mguu (enka) wa kushoto.

  Wachezaji wengine wenye mabao manne sawa na Mandawa kabla ya mechi za VPL mwishoni mwa wiki ni Mrundi Didier Kavumbagu wa Azam FC, Mkenya Rama Salim wa Coastal Union, Ame Ally Amour wa Mtibwa Sugar na Dan Mrwanda (Polisi Morogoro/Yanga).

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa zamani,Mh. Ali Ameir Mohamed wakati alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Kichaviani, Jimbo la Donge, Zanzibar.Mh. Lowassa yuko visiwani Zanzibar kwa mapumziko ya Krismasi.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akielezwa jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani wa zamani,Mh. Ali Ameir Mohamed wakati alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Kichaviani, Jimbo la Donge, Zanzibar.Mh. Lowassa yuko visiwani humo kwa ajili ya mapumziko ya Krismasi.

  0 0
 • 12/27/14--04:48: YALE YALEEEE.....


 • 0 0

   Maandalizi ya kutandika Mkeka wa nguvu katika Barabara ya kutotea Tanesco Mikocheni A mpaka Msasani  kama inavyoonekana pichani.hii ni sehemu ya maendeleo yanayofanywa na Serikali yetu sikivu.
   Siku si nyingi mambo yatakuwa mswano na watu watakuwa wanaleza tu jamvini.
  Mmoja wa wataalam wa ujenzi wa barabara hiyo akiangalia kama mambo yako vyema.

  0 0

  Pichani ni maandalizi ya ujenzi wa mradi wa New Kawe City unaoendelea kwa kasi hivi sasa katika eneo la Tanganyika packers,Kinondoni jijini Dar.Mradi huo unasimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).Camera ya Globu ya Jamii ilikatiza maeneo hayo jioni ya leo na kujionea maandalizi makubwa ya ujenzi huo ambao wakazi wake watapata makazi bora na ya kudumu kwa bei nafuu.

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bwa.Nehemia Mchechu aliwahi kuzungumza kwenye moja ya jukwaa la uwekezaji wa sekta ya nyumba lililofanyika jijini Dar,na kueleza kuwa shirika hilo limedhamiria kuyabadilisha maeneo mengi ya jiji la Dar na mikoa mingine kuwa ya kisasa zaidi.


  0 0

  Na Andrew Chale 
  USIKU wa ‘Old Is Gold’ na Spice Modern Taarab, unatarajiwa kurindima  usiku wa Desemba 28, Mwaka huu ndani ya   ukumbi wa Safari Carnival uliopo Mikocheni B, jijini Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, mwandaaji na mdhamini wa onyesho hilo,  mashabiki  wa Old Is Gold watapata burudani ya aina yake katika kiota hicho cha burudani kila jumapili kukumbushana enzi.

  “Kwa kiingilio cha sh 5,000 tu, wadau watafurahia shoo kabambe kutoka kwa Spice Modern Taarab ndani ukumbi wa Safari Carnival. Huku wadau wakijumuika pamoja na kubadilishna mawazo” alisema Asia Idarous.

  Asia Idarous alilielezea kundi hilo ni la magwiji wa muziki huo wa mwambao ikiwemo kupiga nyimbo za taarab za zamani na zile za sasa.

  Onyesho  ni la kila siku za Jumapili kwenye ukumbi huo huku likidhaminiwa na Fabak Fashions (Mikocheni), Safari Carnival,  wadau wengine wakiwa ni pamoja na Clouds tv, Michuzi Media Group  na wengine wengi.
  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Mtoto Sofia Kombo Makame aliyekimbia umbali wa kilomita nyingi kutokana na umri wake katika mashindano ya Riadha zawadi hiyo alipewa wakati wa ufungaji wa Mashindano ya Riadha katika Wilaya kumi za Unguja na Pemba katika uwanja wa Amaani Studium leo Mjini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikabidhi Kombe la Ushindi wa Jumla kwa Kassim Hussein Saleh na fedha tasilimu Shilingi Millioni Moja akiwakilisha wilaya ya Mjini iliyopata medali 17 za zahabu,13 fedha na 5 za Shaba katika ufungaji wa Mashindano ya Riadha katika Wilaya kumi za Unguja na Pemba aliyoyafunga leo katika uwanja wa Amaani Studium (kushoto) Kaimu Waziri wa Habari,Utalii,Utamadunu na Michezo pia Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdilahi Jihadi Hassan.


  0 0

  MISS Tanzania namba mbili 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za kibongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, jana ilitoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Kulea Yatima cha Extreme kilichopo Tandare kwa Bi Mtumwa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam. 
  Mrembo huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti inayojihusisha na masuala ya urembo, alitoa msaada huo kama zawadi yake ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya kwa watoto hao kama sehemu ya kuwafariji ili nao kujiona wako sawa na wengineo wanaioshi nawazazi wao. Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Jokate alisema kuwa ameguswa na kituo hicho ambacho huwa hakikumbukwi na wahisani kutokana na mazingira ya eneo hilo. 
   “Nimefika hapa kutoa msaada kama sehemu ya kuonyesha ninavyoguswa na jamii ya watoto kama hawa, lakini pia nikiwa na lengo la kuwafariji ili nao kujiona ni sehemu ya jamii ya Watanzania,” alisema. 
   Kidoti alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watu wenye uwezo, kampuni na taasisi mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii kwani nao wana haki ya kuishi na kufurahia maisha kama wengine. 
   Misaada aliyokabidhi kwa ushirikiano na kampuni ya Rainbow Shell, ni mchele, unga wa sembe, sabuni, jozi za viatu vyenye nembo za Kidoti. 
   Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, mlezi wa watoto hao, Mwamvua Jumanne, alitoa pongezi kwa Kidoti na kuwasihi wengine kuiga mfano wa mrembo huyo kusaidia makundi maalum. Akielezea changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mwamvua alisema ni kukosa uwezo wa kifedha kuwalipia ada watoto wanaosoma elimu ya msingi na sekondari, gharama za matibabu pamoja na kukosa watu wa kuwatembelea ili kuwafariji.
  Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akicheza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. 
  Jokate Mwegello, akicheza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne
  Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akimpa zawadi ya ndala mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti.  Picha na Jumanne Juma
  Miss Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate Mwegello, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mwamvua Jumanne, alipotembelea kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti.  Picha na Jumanne Juma

  0 0

  File photo of National Service recruits
  at camp - not related to the article 
  My parents had migrated from British India to Tanganyika Territory in 1947. I was born in Dar-es-salaam. Then it was a cultural norm among the Indian society to educate their girls till primary education for 8 years only. As I was very much interested in studying further, I was allowed to go to Indian girls’ secondary school for additional four years to achieve Cambridge School certificate.
  Tanganyika became independent from British rule on 9 December 1961. By 1964, main land Tanganyika united with the People's Republic of Zanzibar to form the United Republic of Tanzania. As in 1962, less than 2% of 11-16 year old children were in secondary education and about 85% of population was illiterate. To overcome the problem, free primary education was offered to all children. Talented students were selected for high schools and at universities free of charge.
   In 1964, an act of compulsory National Service was introduced for all, boys or girls, who had graduated free of charge from high schools and University. According to the act, one should do two years national training service which included both military as well as nation building activities. Out of these two years, six months should be spent on the military camps and during the rest of 18 months one should practise the normal profession with reduction of the salary by 40%.

  The aim of staying in a camp for six months was to provide standard military training as well as training on human rights, civics, and the history of the union of Tanganyika and Zanzibar, and also aimed to impart students with a sense of unity and patriotism.
  Many of my class mates went to India or UK for further education with the aim of settling overseas due to the political instability. My father could not afford to send me abroad. I was one of the two Indian girls who were selected from our school to go for high school education (A-level) in 1965.It was a dilemma whether I should accept the offer of going to A-level or not, because if I accept, I had to go for six months of national service after I finished my studies. My parents were not keen on this idea as this was a new concept for them. 
  They were fearful for my safety and what the society would say for sending a young girl away to unknown challenges. Obviously my parents were protective, worried and anxious, as I had never lived away from them. But I managed to convince them after weighing the pros and cons. They were very proud of my academic achievement so far and wanted me to fulfill my dream. We decided to tackle the problem when it came.  0 0

  Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi

  Wakazi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kushikamana kwa  pamoja, kufanya kazi kwa bidii  na kuzitumia rasilimali zilizopo ili kujiletea maendeleo.

  Rai hiyo imetolewa jana Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mitwero Stendi Kata ya Rasibura wilayani humo.

  Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema mkoa wa Lindi  umejaliwa kuwa na rasilimali nyingi  ikiwa ni pamoja na zao la korosho, ardhi yenye rutuba, bahari  na  gesi lakini bado kuna changamoto zinazowakabili wananchi na hivyo kukwamisha maendeleo yao.

  Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na elimu kwani baadhi ya wanafunzi wafikapo darasa la tano wanaacha  shule kwa ajili ya utoro, mimba za utotoni na vijana kutokufanya kazi kwa bidii.


  0 0
 • 12/28/14--03:01: TAARIFA YA MSIBA
 • MZEE RAYMOND KULLAYA

  BI FORTUNATA RAYMOND (MENEJA NHIF MKOA WA LINDI) ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BABA YAO MPENDWA MZEE RAYMOND KULLAYA KILICHOTOKEA TAREHE 21/12/2014 HOSPITALI YA DR. MVUNGI KINONDONI DAR ES SALAAM.

  MAZISHI YATAFANYIKA TAREHE 30/12/2014 KIJIJI CHA CHEKERENI-MOSHI.

  IBADA YA KUMUOMBEA MAREHEMU NA SHUGHULI ZA KUAGA KABLA YA SAFARI YA KUELEKEA MOSHI KWA MAZISHI ITAFANYIKA KATIKA KANISA KATOLIKI HANANASIFU KINONDONI SAA 6:00 TAREHE 29/12/2014.

  HABARI ZIWAFIKIE NDUGU JAMAA NA MARAFIKI POPOTE WALIPO

  ***BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIHIMIDIWE***

older | 1 | .... | 687 | 688 | (Page 689) | 690 | 691 | .... | 3278 | newer