Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

SAFARI LAGER NYAMA CHOMA KURINDIMA JIJINI MWANZA JUMAPILI HII

$
0
0
SAFARI LAGER NYAMA CHOMA MWANZA FINALS
Sunday, 17 March 2013 – Kiwanja Cha Furahisha
  • Kwa mara nyingine tena, Safari Lager inakukaribisha kushuhudia mchuano wa mwisho kuona ni Baripi inayochoma nyama Bomba zaidijijini Mwanza!.
  • Ni Jumapili hii tarehe17 March, katika Kiwanja Cha Furahisha jijini Mwanza kuanzia saa 4.00asbh.
  • Njoo ushuhudie bar zilizoingia fainali Mwanza zikichuana kukupa Nyama Choma Bomba zaidi;
    • Victoria Prince Bar Kirumba.
    • Shokeni Bar Mkuyuni.
    • AR Pub Kilimahewa.
    • Lunara Bar Nyakato.
    • Shooters Bar Kirumba.
Washindi watajipatia zawadi zaidi ya shilingi milioni nne!.
  • Njoo uburudike kwa aina tofauti za nyama choma, kuanzia mapande hadi mishkaki, nyama za Kuku, Ngombe na Mbuzi!!.Chachandu, Kachumbari, pilipili, ndimu nk.. vitakuwepo.
  • Kutakuwa na zawadi kibao kutoka Safari Lager, burudani za wasanii mbalimbali, na kufunga kazi jukwaani watakuwepo The Africana Music Band!!..
  • Tamasha la Safari Lager Nyama Choma jumapili hii pale kiwanja cha Furahisha jijini Mwanza ni BURE, hakuna Kiingilio!.
  • Bila Safari Lager, Nyama Choma Haijakamilika!!..

Viongozi Wakuu wa Barclays Afrika wakutana na Waandishi wa Habari jijini Dar leo

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Barclays wa Huduma za Rejareja za Biashara ya Kibenki,Craig Bond akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wao wa kuelezea mipango yao endelevu ya biashara za kibenki Barani Africa,uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Wengine pichani ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa,Kennedy Bungane (wa pili kushoto),Mkurugenzi Mkuu wa Barclays Tanzania,Kihara Maina (wa pili kulia) na mwisho ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Barclays Africa,Willie Lategan
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa,Kennedy Bungane (wa pili kushoto) akisisitiza jambo mbele ya waandisi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wao wa kuelezea mipango yao endelevu ya biashara za kibenki Barani Africa,uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Barclays Tanzania,Kihara Maina (katikati) akizungumza kwenye Mkutano huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Bima wa Barclays Africa,Willie Lategan na Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Africa,Kennedy Bungane.

moshi mweusi wafuka vatican; papa bado hajapatikana

$
0
0

Moshi mweusi umefuka leo katika Chapel ya Sistine huko Vatican, kuashiria kwamba Papa mpya bado hajachaguliwa katika siku ya kwanza ya upigaji kura za siri.
Papa Benedict XVI aliustua ulimwengu kwa kuwa Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani wa kwanza kujiuzuru katika miaka 600,  na hali hii ya leo inaonesha Makardinali 115 wanaochagua wanataka kuhakikisha mrithi wa Joseph Ratzinger (jina la Papa aliyepita) ni mtu sahihi.
Habari toka Vatican zinasema kwa kawaida Makardinali hao watapiga kura mara nne kwa kila siku hadi atapopatikana mteule wao. Wanatarajiwa kurejea tena kupiga kura kesho katika uchaguzi huo ambao hauna kikomo cha siku za kufikia uamuzi.
Katika uchaguzi uliopita mwaka 2005, uchaguzi ulichukua siku mbili, lakini kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopot, mnamo mwaka 1268 iliwachukua miezi 33 kumpata Papa Gregory wa Tano.

DKT. BILAL AKUTANA NA MKURUGENZI WA 'CITIBANK'S'

$
0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Citibank's, Patrick Dewide, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 12, 2013 kwa mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Citibank's, Patrick Dewide na Mkurugenzi Mtendaji wa Citibank Tanzania, Joseph Carasso (kushoto) wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.

BALOZI WA UMOJA WA ULAYA (EU) NCHINI AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, DK EMMANUEL NCHIMBI OFISINI KWAKE, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza jambo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi (katikati) kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya EU na wizara hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi (katikati). Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima. Balozi huyo alipofanya ziara ya kikazi wizarani hapo, jijini Dar es Salaam.

kamata kamata ya wezi wa umeme yaendelea, safari hii mjini Dodoma

$
0
0
Kikosi cha ukaguzi cha makao makuu ya Tanesco kimeendelea na kamata kamata za wezi wa umeme na leo mashine ya kukoboa na kusaga ya Kikuyu Community Development ya mjini Dodoma imebambwa ikitumia nishati hiyo kwa wizi. Hawa wamekutwa wakitumia umeme usiopitia kwenye mita. Mmiliki wa mashine hakuweza kupatikana amedai yupo Dar es Salaam. Anasakwa.
 Mashine ya kukoboa na kusaga ya Kikuyu Community Development ya Dodoma mjini iliyokamatwa kwa wizi wa umeme 
 Mita iliyoongezewa waya mdogo rangi nyekundu upande wa kulia wa mita
Jengo la mashine ya kukoboa na kusaga ya Kikuyu Community Development, iliyokamatwa kwa wizi wa umeme

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
The Temptations wanakukumbusha 'Treat Her Like A Lady'

GOLDIE MEMORIES - 14TH MARCH 2013

$
0
0

It’s a month today 14th MARCH 2013 when you mysteriously disappeared from us, To date you left us puzzled not knowing what to say or think, With all your greatness and accomplishments in life, GOLDIE we Believe God Loves you more than us as he took you away on the 14th FEBRUARY 2013 “THE MEMORY DAY OF ST. VALENTINO” the date stands for “LOVE”, GOLDIE will be missed more for her giving personality, charisma, caring for others, love and most of all her BIG HEART!!. GOLDIE gave it all every day to each and every one of us and our lives have forever been hollowed without her...Thanks to all of you for reaching out to us in this time of our immeasurable loss. 
 REST IN PEACE GOLDIE.
 B.D.D quotes on behalf of MMG. 


MJADALA WA ELIMU WA TANZANIA WAENDELEA UGHAIBUNI - SEHEMU YA TATU

$
0
0

Sehemu ya Tatu ya WanaDMV wafanya mjadala wa kushuka kwa kiwango cha Elimu na matokeoa mabaya ya kidato cha Nne wakianza kuelezea Elimu zamani ilivyokuwa na nini kimesababbisha kuporomoka kwa Elimu Je nani alaumiwe na nini kifanyike kuokoa janga hili WASIKILIZE

TAARIFA YA KIFO

$
0
0
FAMILIA YA MAREHEMU MZEE DAVID ELIYA MGWASSA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MPENDWA MAMA YAO, MAMA SUZAN MGWASSA, KILICHOTOKEA TAREHE 13/03/2013 KATIKA HOSPITALI YA AGAKHAN DAR ES SALAAM.

MSIBA UPO NYUMBANI KWAKE MAREHEMU KIJITONYAMA NYUMA YA KAMPUNI MPYA YA VING'AMUZI YA DIGITEK, AMA USONI PA KIJITONYAMA MAGHOROFANI.

SISI TULIMPENDA, BWANA ALIMPENDA ZAIDI NA KUMTWAA. MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. 

- AMINA

BALOZI WA INDIA NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, DK EMMANUEL NCHIMBI OFISINI KWAKE, JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza jambo na Balozi wa India nchini, Debnath Shaw. Balozi na waziri huyo walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya ubalozi huo na wizara.
Balozi wa India nchini, Debnath Shaw (kulia) akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi wakati balozi huyo alipofanya ziara ya kikazi wizarani hapo, jijini Dar es Salaam.

KATIBU MKUU WA CCM NA UJUMBE WAKE WATEMBELEA KIWANDA CHA VIATU CHA TIANJIAN, CHINA

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na ujumbe wake, wakionyweshwa maumbo ya namna kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, wakipata maelezo kwa video, kuhusu kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akitazama kiatu, wakati yeye na msafara wake walipotembelea kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China. Wengine kutoka kwa Kinana ni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Mohamed Yusuf.

The BeatDown this FRIDAY @Synergy Lounge This Friday

1 Week Left. Executive Friday: Creating Effective Business Systems

TAPSEA 2013 AT AICC ARUSHA


Huyu ndio Papa Francis I,kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani

$
0
0
Papa Francis I

Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa Argentina (pichani) ndie amechaguliwa kuwa Papa mpya wa Kanisa Katoliki Duniani kote.

Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa Papa.

Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I.

Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa. Hii ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao.

Kadinali Bergoglio anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Papa Benedict XVI, ambaye alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.

Makadinali 115 walikuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku. Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya.

Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha nani angelichaguliwa.
Moshi mweupe

Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikwa wamekusanyika katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne.

Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa .
Papa Francis I ni nani?

Alizaliwa Mjini Buenos Aires huko Argentina mwaka1936.

Papa Francis 1 ni mtu wa kwanza katika kipindi cha miaka elfu moja (1,000) kwa mtu kutoka nje ya bara la Ulaya kutawazwa kuwa papa wa Kanisa Katoliki.

Papa Francis 1 ni mwana wa Mtaliano aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la gari Moshi kabla ya kuhamia nchini Argentina miaka ya zamani.

Kama kadinali wa Jimbo la Buenos Aires ,Kadinali Bergoglio amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Argentina. Hata hivyo Kadinali Bergoglio anapendwa sana na wafuasi wa kanisa hilo huko Argentina na hasa watu maskini.

adinali Jorge Bergoglio, mwenye umri wa mwaka 76, kwa karibu miaka yake yote kama Kasisi amehudumu nyumbani kwao Argentina. Kadinali huyo wa Jimbo la Buenos Aires inasemekana aliibuka nambari mbili wakati Papa Benedict alipochaguliwa mwaka 2005


 Papa Francis akijitokeza kwa mara ya kwanza

Anaaminika kuwa na ujuzi mkubwa ambao wengi wanasema utamsaidia sana katika uongozi wake.

Katika maisha yake ya huduma kwa Kanisa Katoliki huko Amerika Kusini ambapo Kanisa Katoliki lina waumini wengi zaidi duniani, Kadinali Bergoglio ameibuka kuwa mtu anayependa sana udhabiti wa kisiasa katika nchi zilizo katika bara la Amerika Kusini.

Bergoglio anasifiwa kwa kuleta mageuzi makubwa katika Kanisa la Argentina huku katika eneo hilo la Amerika Kusini Kanisa bado linashikilia itikadi za kale.

Chanzo:BBC Swahili.

kampuni ya bia ya serengeti yazindua kampeni yake mpya jijini dar leo.

$
0
0
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Bwa.Ephrahim Mafuru akizungumza jambo mbele ya Wanahabari waliofika kushuhudia uzinduzi wa kampeni mpya ya bia ya Serengeti Premium Lager itakayoitwa "TUPO PAMOJA-KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO,ambayo inatarajiwa kufanyika nchi nzima katika maeneo mbalimbali.
Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Bwa.Allan Chonjo akitoa ufafanuzi wa namna kampeni hiyo  "TUPO PAMOJA-KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO",itakavyofanyika, mbele ya Wanahabari waliofika kushuhudia uzinduzi wa kampeni hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika nchi nzima katika maeneo mbalimbali.
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,pichani kulia Bwa.Ephrahim Mafuru,pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Allan Chonjo wakiandaa kufanya uzinduzi wa kampeni yao mpya ya kinywa cha Serengeti Premium Lager.Pichani kati anaeshuhudia ni Meneja wa Mahusiano ya ndani ya kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Iman Lwinga.
 Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,pichani kulia Bwa.Ephrahim Mafuru akitoa ufafanuzi mbele ya Wanahabari waliofika kushuhudia kampeni hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika nchi nzima katika maeneo mbalimbali.
 Moja ya ratiba za shangwe hizo zitakapokuwa.
 Baadhi ya Wanahabari wakishuhudia uzinduzi wa kampeni mpya ya kinywaji cha Serengeti Premium Lager  "TUPO PAMOJA-KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO",iliyofanyika mapema leo asubuhi.
Meneja wa Mahusiano ya ndani ya kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Iman Lwinga akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo mbele ya Wanahabari,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya JB Belmonte,Jijini Dar wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kinywaji chake cha Serengeti Premium Lager.Anaaefuatia ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Bwa.Ephrahim Mafuru,Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Allan Chonjo pamoja na Meneja Masoko Mosses Kebba 

Wilaya ya Kilwa yapokea walimu wapya kukabiliana na changamoto la Elimu

$
0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Addo Mapunda akisisitiza jambo wakati hafla fupi ya kuwakaribisha walimu wapya watakaofundisha katika shule zilizopo kwenye Halmashauri hiyo ya Kilwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Mh. Abdallah Ulega akitoa nasaha zake kwa walimu waliofika Wilayani hapo.
Walimu wapya wa shule za msingi na Sekondari ambao wameripoti na kupokelewa Wilayani Kilwa. 

Na Abdulaziz Video,Lindi.

HALMASHAURI ya wilaya ya Kilwa imekabidhi meza nne za maabara inayotembea kwa ajili ya mafunzo ya vitendo katika masomo ya Baiolojia, Kemia , Kilimo na Fizikia kwa shule nne za sekondari ikiwa ni sehemu ya hatua za kukabili changamoto za matokeo mabaya ya shule za sekondari za wilaya hiyo Hususan katika masomo ya sayansi.

Meza hizo zenye thamani ya shilingi Milioni 24 ikiwa ni awamu ya kwanza ili ya kuziwezesha shule za zote za sekondari kuwa na Maabara zinazohamishika.

Tukio hilo lilioenda sambamba na kupokea walimu wapya wa shule za msingi na Sekondari waliopangwa katika Halmashauri hiyo.

Akiongea katika katika hafla hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Abdallah Ulega sambamba na kuwashukuru walimu hao kwa kufika wilayani humo Pia alitoa wito kwa Jamii kujenga Nyumba Bora hususan Vijijini ili kusaidia watumishi wanaopangwa huko kwa huduma za jamii zikiwemo Elimu na Afya.

kutokana na mazingira ya kusomea kutokuwa yenye mvuto ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa zana muhimu na maabara, na kwamba hatua ya kusambazwa kwa teknolojia hiyo rahisi licha ya kuwawezesha wanafunzi sasa kujifunza katika hali iliyobora zaidi kwa vitendo,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Bw Addo Mapunda aliwasihi walimu hao kufanya kazi kwa kuwa Wilaya hiyo inaupungufu mkubwa wa walimu hususan vijijini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw Ally Mohamed Mtopa alitoa ahadi ya kununua kitanda na godoro kwa walimu watakaopangwa katika KATA yake lakini pia aliwageukia walimu hao kuhusiana na suala la migomo ya walimu ambapo aliwasihi kutojiingiza katika masuala hayo badala yake aliwaomba walimu hao kufikisha malalamiko yao kwa Madiwani ambao ndio wenye maamuzi ya Halmashauri hiyo.

Wilaya ya kilwa ilipangiwa jumla ya walimu 104 wa msingi na 78 wa Sekondari,Kati ya hao 7 hawajaripoti kwa shule za msingi huku sekondari walimu 23 hawajaripoti licha ya tarehe zilizowekwa na wizara kumalizika

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari kutoka kwa Mh. Membe

VIONGOZI WA SEKTA YA ULINZI NCHINI WATUA OFISINI KWA WAZIRI NCHIMBI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimfafanulia jambo Mwenyekiti wa Chama cha Sekta ya Ulinzi nchini (TSIA), Athuman Maige (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Isaya Maiseli. Viongozi hao walikutana na waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya chama hicho na wizara.
Mwenyekiti wa Chama cha Sekta ya Ulinzi nchini (TSIA), Athuman Maige (katikati) akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya chama chake na wizara hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Isaya Maiseli.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images