Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 66 | 67 | (Page 68) | 69 | 70 | .... | 3286 | newer

  0 0


   Mshambuliani wa pembeni wa timu ya netiboli ya Free Media Queens, Clezencia Tryphone akimiliki mpira wakati wa michuano ya NSSF Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Free Media ilishinda 23-20. (Picha na Habari Mseto Blog)
  Kikosi cha Free Media Queens.
   Mshambuliani wa pembeni wa Free Media Queens, Clezencia Tryphone akimiliki mpira wakati wa michuano ya NSSF  Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Free Media ilishinda 23-20.
   Wachezaji wa timu ya Free Media Queens wakiwa mapumziko.
   Matokeo ya mchezo kati ya Free Media Queens na Uhuru Queens.
   Mfungaji wa timu ya TBC Queens akijiandaa kuifungia timu yake katika michuano ya NSSF Media Cup ilipopambana na Sahara Media ambapo katika mchezo huo TBC iliibuka na ushindi wa mabao 56-1
    Mfungaji wa timu ya TBC Queens akiwatoka wachezaji wa Sahara Media katika michuano ya NSSF Media Cup ilipopambana na Sahara Media ambapo katika mchezo huo TBC iliibuka na ushindi wa mabao 56-1

  0 0

   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akitoa Maelekezo kuhusu Uchafuzi wa Mazingira kwenye kiwanda cha Mwatex kinachotiririsha Maji kwenye  Makaazi ya  Wananchi Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza Kulia Mkurugenzi Rasilimali Watu Bw Evodius Gordian.

  Naibu Wazir Ofisi ya Makamu waRais Charles Kitwanga akitoa Maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Bi Amina Juma wakati alipotembelea kiwanda cha Mwatex Wilayani Ilemela ambacho  kinatiririsha Maji kwenye Makazi ya Wananchi katikati Mkurugenzi wa kiwanda Bw Amin Ladhan wapili Mkurugenzi Rasilimali Watu Bw Evodius Gordian
   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Charles Kitwanga akiangalia Mfumo wa Maji taka kwenye Kiwanda cha Samaki cha Tanperch Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza Kulia Jeneral Meneja Bw Ashak Vannadil
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akipata maelezo Juu ya Uzalishaji wa Chuma kwa Meneja wa Kiwanda cha Chuma cha Nyakato Steel Bw Ramarao Uppala wakatiNaibu Wazir alipofanya Ziara ya Kuangalia Uchafuzi wa Mazingira Mkoani Mwanza. 
  Picha na Ali Meja

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiangalia maonesho ya kazi za vikundi vya wajasiriamali wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja,alipokuwa katika ziara ya kuangalia maendeleo ya miradi mbali mbali leo. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0
 • 03/12/13--10:41: Article 21


 • 0 0
 • 03/12/13--10:43: THE BEAT Friday 15.3.13


 • 0 0

  htt
  HI NI SEHEMU MOJAWAPO YA FILAMU HIYO AMBAPO MADAKTARI WA KIHINDI WAMESHIRIKISHWA

  0 0

  Mtoto Simon Mlope mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa eneo la mahenge katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma alilazimika kukatisha masomo yake ya shule ya msingi akiwa darasa kwanza kutokana na mtoto huyo kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo .

   Awali tulitoa habari za mtoto huyu akiomba msaada lakini hadi sasa bado hajapata msaada wowote ule wa kuweza kuokoa maisha yake. Nahivi sasa hali ya mtoto huyu inazidi kuwa mbaya kiafya .

  Mtoto Simon Mlope alikubwa na ugonjwa huo wa moyo tangu mwaka 2001 mara baada ya kuzaliwa na kugundulika kuwa moyo wake una tundu hali ambayo inamsababishia mtoto huyo kuvuta pumzi kwa shida.

   Mama wa mtoto Simon Mlope anayeitwa AMINA ALLY anawaomba watanzania kumsaidia mtoto wake fedha za matibabu Baada ya kuambiwa na madaktari kuwa Simon anatakiwa kwenda nchini india kutibiwa,baada ya kupata rufaa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili mwaka 2006 huku familia yake ikiwa haina uwezo kabisa.

  Majirani wa familia ya Simon nao wanasema kuwa mtoto huyo anahitaji msaada wa haraka kwa kuwa hali yake sio nzuri na kuwaomba watanzania wamsaidie.

  Kinachosikitisha zaidi baba wa mtoto huyo anayejulikana kwa jina la MLOPE ameondoka nyumbani hapo tangu mwaka 2011 na hajulikani aliko kwa sasa, ingawa mwanzoni alisema yuko nchini Msumbiji.

  Kwa anayeguswa na tatizo hili na anataka kumsaidia SIMONI MLOPE atumie simu namba 

   0752732290
  Mtoto Simon Mlope anavyoonekana hivi sasa kutokana na maradhi ya moyo yanayomsumbua.
  Mtoto Simon Mlope akiwa na Mama yake Mzazi atambulikae kwa jina la Amina Ally.

  0 0
 • 03/12/13--13:00: Article 17


 • 0 0

  Pictureheikh 

  Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akizindua kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi katika hafla iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam. (picha: Magreth Kinabo - MAELEZO)
   Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amewataka viongozi nchini kuienzi na kuithamini lugha ya Kiswahili ili kuendelea kujenga taifa lenye umoja na mshikamano.

  Kauli hiyo imetolewa  na Mzee Kingunge Ngombare Mwiru ambaye alikuwa  mgeni ramsi katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee,  jijini Dar es Salaam.

  Kitabu hicho kimeandikwa na Mathias Eugen na uzinduzi wake uliandaliwa na familia ya Kaluta wakishirikiana na baadhi ya wataalamu wa lugha hiyo kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA). Kitabu hicho kimekusanya kazi mbalimbali zilizofanywa na Hayati Kaluta wakati wa uhai wake.

  Mzee Kingunge anawaasa Watanzania kuwa wazalendo na kutumia lugha ya hiyo kwa ufasaha tofauti na ilivyo sasa katika shughuli mbalimbali, mfano Bungeni.

  “Lugha ni chombo cha msingi kwa binadamu pia inatofautisha kati ya binadamu na viumbe vingine ambapo kupitia lugha ndipo tunapokuza uwezo wa kufikiri kwani huwezi kukuza uwezo wa kufikiri biala ya kuwa na lugha ya kueleweka,”alisema Kingunge na kuongeza: “Hatima ya Taifa inategemea lugha ya Kiswahili. Viongozi wanawajibu mkubwa katika kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inakuwa kwani wao ndio wanaweza kukipandisha au kuiua lugha ya Kiswahili kwakuwa jamii inawategemea kwa kiasi kikubwa,” alisema Mzee Kingunge.

  Hata hivyo, aliunga mkono  lugha hiyo kuwa rasmi kufundishia, lakini ametoa changamoto kuwa yatupasa kuwa makini katika kuitumia hususani katika ngazi elimu ya msingi, sekondari hadi vyuo vikuu. Mzee Kingunge alitolea mfano wa wajukuu zake kuwa masomo mengine kama vile hesabati wanapata  alama 90 hadi 95, lakini lugha hiyo wanapata alama ya 60 mpaka 70. Hivyo inaelekea ufundishaji wake ni tatizo.

  “Kama kufundisha lugha ya Kiswahili katika elimu ya sekondari ni tatizo na Kiingereza ni tatizo . Kiswahili kipi kifundishwe katika elimua ya Chuo Kikuu,”alisema, huku akitolea mfano kuwa kumekuwa na matumizi ya maneno ambayo si sahihi kama vile neno masaa badala ya saa.

  Kwa upande wake mwanazuoni na mdau wa lugha hiyo  Profesa Mugyabuso Mulokozi na Profesa Joshua Madumula wameiomba serikali kuwa na utaratibu wa kuenzi   fasihi za Watanzania.

  Watu wengine mashuhuri waliohudhuria katika uzinduzi huo ni pamoja na Balozi Job Lusinde, Suleiman Hega na Hashim Mbita.


  0 0


  Helen Joseph (pichani), bondia mwanadada ambaye anaishi katika jiji la Accra, nchini Ghana akipigana ngumi yuko mboni kupanda kilele cha mafanikio katika maisha yake ya ngumi. Ni wakati ambao Helen Joseph anayetoka katika nchi ya Nigeria aliokuwa anaungojea katika maisha yake ya ngumi.
   Mwaka jana alikutana na bondia Dahianna Santana katika jiji la San Domingo, nchini Dominican Republic kugombea ubingwa wa dunia wa IBF katika uzito wa Unyonya (Fearherweight). Taabu na kashikashi zote alizozipata wakati wa patashika ile ya mwaka jana zimekuwa fundisho tosha kwa Helen wakati anapojiandaa kukutana na Marianna Gulyas kutoka nchini Hungary kugombea ubingwa wa IBF wa mabara katika uzito wa unyoya.
   Mpambano huo, unaoandaliwa na kampuni maarufu ya kukuza ngumi ya GoldenMike Boxing Promotion Syndicate ya nchini Ghana unategemea kuwa wa patashika kweli kutokana na mabondia wote wawili kuwa na ujuzi tele ulingoni. Wawili hawa watakutana tareeh 30 March katika uwanja wa michezo wa Accra na mpambanohuu utarushwa moja kwa moja na luninga ya Super Sports. 
  Ni mapromota wachache na mameneja wachache  ambao wanaweza kuwekeza kiasi kikubwa hivyo cha pesa katika mchezo wa ngumi namna ambapo kampuni ya GoldenMike Boxing Promotions Syndicate ya nchini Ghana imewekeza katika kuinua kipaji cha mwana dada Helen Joseph.
   Kwa upande wake Helen ambaye ni nadhifu, mtanashati na mwenye nidhamu ya hali ya juu, mchezo wa ngumi ndio unaomlisha katika maisha yake na atatumia uwezo wake wote kuhakikisha kuwa taji hli kubwa la ngumi linabaki barani Afrika na kulitumia kama ngazi ya kukutana tena na Dahianna Santana katika ubingwa wa dunia!  
  ISSUED BY:
  INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
  DAR-ES-SALAAM, TANZANIA


  0 0


  0 0

  Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jana (Tar 12/03/2013) kwa kauli moja ilipitisha bajeti ya Tshs. 156,439,616,904 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ofisi za Manispaa hiyo, Dar es Salaam.

  Kati ya fedha hizo Tshs. 49,206,498,064 ni mapato ya ndani ya Manispaa, ambapo zaidi ya 50% ya bajeti imelenga kuhudumia miradi ya maendeleo zikiwemo barabara, maji, shule, hospitali, mikopo ya vijana na wanawake na masoko.

  Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda alisema Manispaa yake imejipanga kuhakikisha inasimamia miradi hiyo ili ilete mabadiliko ya kuchumi katika Manispaa hiyo.

  “Tumejizatiti kuisimamia vizuri miradi hii ili ilete tofauti katika Manispaa yetu ya Kinondoni.” Alisema.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza wakati wa kikao cha Bajeti cha Manispaa hiyo kilichofanyika jana (Machi 12) katika ofisi za Manispaa hiyo, Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu wake, Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Natty.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty akizungumza wakati wa Kikao cha Bajeti cha Manispaa hiyo kilichofanyika katika ofisi za Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana (Machi 12). Katikati ni Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda na Naibu wake, Songoro Mnyonge.
  Sehemu ya Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni wakifuatilia kwa makini wakati wa Kikao cha Bajeti cha Manispaa hiyo kilichofanyika katika ofisi za Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana (Machi 12).

  0 0
 • 03/12/13--19:47: IN LOVING MEMORY
 • OUR BELOVED YONILLA MAKOTA SAMAKA

  It is one year today since you departed from our midst to be with the Lord on March 13, 2012. The heartbreak and pain that we felt has not and will never cease.

  However, God continues to be our refuge and inspiration. Your precious memories remain fresh in our hearts and minds. The love you placed within our hearts no millionaire could buy.

  You are fondly remembered by your loving husband, Joseph F. Samaka, daughters Josephine, Julieth, Clara and Claudia, sons Francis and Anthony, grandsons Jonathan and Jayden, grand-daughter Abbriana, son-in-law Emmanuel, relatives, neighbours and friends. We will always remember you.

  There will be a memorial mass at the Msimbazi Catholic Church on Saturday, March 16, 2013 at 6:45 am in remembrance of the late YONILLA MAKOTA SAMAKA. All are welcome.

  MAY THE ALMIGHTY GOD REST HER SOUL IN ETERNAL PEACE, AMEN.

  0 0
 • 03/12/13--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Hii ngoma inaitwa Breakin' (There's No Stopping Us)lakini kina David V na mdau Mesiaki walikuwa wanaimba "Maiko Jekson njooo, sitaki kama hutaki nenda...." Ah! Raha tupu...

  0 0


  Punde waumini takribani bilioni 2 wa Kanisa Katoliki ulimwenguni watapata kiongozi  mpya.

  A). Je ni nani wanamchagua?

  Kuanzia jumanne jioni  tarehe 12/03/2013, idadi ya Makardinali 115 wa kanisa Katoliki kutoka sehemu mbalimbali duniani wameingia katika “conclave” ndani ya kanisa dogo maarufu kwa jina la Sistine tayari kwa shughuli hiyo nyeti kabisa ambayo itawachukua siku kadhaa. Awali ilitarajiwa Makardinali 117 kati ya 153 wenye sifa za kumchagua kiongozi huyo wa juu wa kanisa hilo wangefika makao makuu Vatikani kwa shughuli hiyo. Lakini kutokana na sababu za kiafya, Kardinali emeritus  Julius Ruyadhi DARMAATMADJA ,sj kutoka Jarkata, Indonesia hakuweza kufika kwa sababu za kiafya, na Kardinali Keith O’Brien, ex- Cardinal toka Ediburgh, Scotland hakufika kwa sababu zake binafsi.

  Hivyo watakaojisogeza katika “boksi” kumchagua kiongozi huyo ni 115 wenye umri chini ya miaka 80.

  B). Mgawanyo unaenda hivi:

  Bara la Ulaya linawakilishwa na makardinali 60; wakitokea : Italia pekee ni : 28. Ujerumani: 6.Uispania: 5. Polandi: 4. Ufaransa: 4. Austria: 1. Ubelgiji: 1. Uswisi: 1. Ureno: 2. Uhaolanzi: 1. Ireland: 1. Jamuhuri ya Czech: 1. Bosnia-Herzegovina: 1. Hungary: 1. Lithuania: 1. Kroatia:1. na Slovenia ni 1.

  Bara la Amerika ya Kusini, maarufu pia kama Latino Amerika ni Makardinali 19; Wakitokea : Brazil: 5. Mexico: 3. Argentina: 2. Kolombia: 1. Chile: 1. Venezuela: 1. Jamuhuri ya Dominikan : 1. Cuba: 1. Honduras: 1. Peru: 1. Bolivia: 1. na Ecuador ni 1.

  Bara la Amerika Kaskazini hasa Marekani ni Makardinali 14 ; wakitokea:  Marekani ni: 11. na Kanada:  ni 3.

  Bara la Afrika litawakilishwa na Makardinali 11: wakitokea Nigeria: 2. Tanzania: 1. (Polycarp PENGO, Askofu mkuu wa jimbo kuu la Dar-es-Salaam, Tanzania). Afrika ya Kusini : 1. Ghana: 1. Sudan: 1. Kenya: 1. Senegal: 1. Misri: 1. Guinea: 1. Na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ni : 1

  Na bara la Asia litawakilishwa na makardinali 10: wakitokea India: 4. Ufilipino: 1. Vietnam: 1. Indonesia: 1. Lebanon: 1. China: 1. na Sri Lanka: 1.

  Kati ya Makardinali 117wenye kupiga kura, 67 waliteuliwa na Papa Benedikti wa XVI. Wanaobakia 50 waliteuliwa na Papa John Paul II. --Kati ya hao walio hai ni 6 na ndiyo pekee  walikuwepo wakati wa Mtaguso wa pili yaani tunaweza kuwaita  (Council Fathers at the Second Vatican Council) nao ni Makardinali Angelini, Arinze, Canestri, Delly, Fernandes de Araújo, na Lourdusamy). Na waliosalia wana zaidi ya miaka 80 na hivyo hawataingia katika hiyo “Conclave”. -- Kati ya makardinali walio hai leo, 99 walishiriki katika uchaguzi wa mwaka 2005. Kati yao  49 tyari wana zaidi ya miaka 80 hivyo hawataweza kumchagua Papa mpya. (Baba mtakatifu Benedikti wa XVI naye alikuwa kati ya walioshiriki uchaguzi wa 2005.)

  C). WANAOPIGIWA CHAPUO.

  Ikumbukwe kuwa viongozi hao walikutana Vatican ambako ni makao makuu ya Kanisa hilo na kuzungumzia maswala mbalimbali yanaloligusa kanisa na waumini wake. Kwa nyakati mbalimbali Makardinali hao walielezea maswala mbalimbali yanayoligusa Kanisa hilo kutoka katika maeneo yao.

  Katika hali la “kuwachora” au kuwasanifu” jamaa kutoka kusini mwa jangwa la  sahara, ambapo waandishi na watu mbalimbali wamekuwa wakiwadadisi kama kiongozi huyo atatokea bara hilo watajisikiaje. Sikatai kuwahoji mawazo na fikra pia maoni yao ni vizuri. Lakini katika hali ya ukweli  walikuwa wakiwa“chora” tu maana kwa sasa mtazamo na wakati wa kupata kiongozi toka ukanda huo unaonekana wazi kuwa bado wakati wake haujaiva. Pengine inawezekana maana ni kazi ya Roho Mtakatifu.

  Wadadisi, watetesi  wa mambo na vyanzo mbali mbali vinatabiria na kubashiri kuwa huenda majina haya yakatoka ndani ya “Conclave” hiyo kama Baba Mtakatifu, kiongozi wa kanisa hilo. Hii ni kwa mpangilio wa chagizo hizo.

  1). K. ANGELO SCOLA, (71) Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Milan, Italia.

  2). K. ODILO PEDRO SCHERER, (63) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Sao Paulo, Sao Paulo, Brazil.

  3). K. MARC OUELLET, (68) kiongozi mkuu mstaafu wa Maaskofu katika Roma, maarufu kama“Prefect Emeritus of the Congregation for Bishops” ni Askofu mkuu wa jimbo la Quebec, Canada-Francophonie.

  4).LUIS ANTONIO TAGLE, (55) Askofu mkuu wa jimbo la Manila, Ufilipino. Ndiye kijana wa pili kwa umri mdogo. Wadadisi wa mambo wanatabiri pia anaweza kuwepo kwenye uchaguzi ujao kama kandidate wa uongozi huo. 5). K. FRANCISCO ROBLES ORTEGA, (64) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Guadalajara, Jalisco, Mexico. 6). K. CHRISTOPH SCHÖNBORN, (68) Askofu mkuu wa jimbo la kuu la Vienna, Austria. 7). K. JORGE MARIO BERGOGLIO, (76) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Buenos Aires, Argentina. 8). K. SEAN PATRICK O’MALLEY, (68) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Boston, Massachusetts, USA. 9). K. PETER ERDO, (60) Askofu mkuu wa jimbo kuu l’Esztergom-Budapest, Hungary. 10). K. ALBERT MALCOM RANJITH PATABENDIGE DON, (64) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Colombo, Sri Lanka. 11). K. TIMOTHY MICHAEL DOLAN, (63) Askofu mkuu wa jimbo kuu la New York, New York, USA. 12). K. TELESPHORE PLACIDIUS TOPPO, (73) Askofu mkuu wa jimbo kuu la Ranchi, India. 13). K.  JOAO BRAZ de AVIZ,  (65) Askofu mkuu wa zamani wa jimbo kuu la Brasilia, Brazil. Sasa anafanya kazi Vatican, Rome. 14). K. FERNANDO FILONI, (66), Italia,  Kiongozi wa ofisi ya  uinjilishaji makao makuu Vatican.15). K. Leonardo SANDRI, (69) Argentina, Anafanya kazi makao makuu Vatican.


  D). WAKATI KANISA LIKIKUWA ZAIDI NCHA YA KUSINI, UONGOZI UNABAKI KWA KIASI KIKUBWA HAPA ULAYA.

  Zaidi ya karne moja iliyopita ukuaji wa kanisa, idadi ya waumini inaongezeka nje ya bara Ulaya na sasa kuna wastani wa zaidi ya waumini milioni 200 wa kanisa Katoliki wapo katika bara la Latini-Amerika ukilinganisha na Ulaya. Ukiangalia kwa makini Makardinali toka bara la Ulaya wanakaribia nusu ya wapiga kura wote. Ikumbukwe kuwa ili kumpata baba mtakatifu, inatakiwa achaguliwe na zaidi ya kura 77 ; kati ya 115.


  Tunaona bara la Amerika ya Kusini ndilo bara lenye wakatoliki wengi kuliko mabara mengine. Afrika inaonyesha kuendelea kukua kwa kasi kwa kuwa na idadi ya waumini wa kanisa hilo. Bara Asia linaonyesha kuendelea kuongeza idadi ya waumini wakanisa hilo kwa siku za usoni. Kwa Afrika, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndiyo inaonyesha kuwa na idadi kubwa ya Wakatoliki ikifuatiwa na Nigeria ya tatu ikiwa ni TANZANIA ikifuatiwa na Uganda kwakaribu kabisa. Halafu Angola inafuatia huku Kenya ikifuatia.

     
  Imeandaliwa na Frédéric Meela, Paris 
  kwa msaada wa vyanzo mbalimbali.


  0 0

   Mhe. Jaji Engera Mmari Kileo, akizungumzia  uzoefu wa  Majaji Wanawake wa Tanzania katika kukabiliana na  tatizo la  matumizi mabaya  ya mamlaka kudhalilisha kijinsia na kushawishi rushwa ya mapenzi  ( sextortion) wakati Chama cha Majaji   Wanawake- Tawi la Tanzania  kilipoanda mkutano wa pembezoni ( side-event) sambamba na   mkutano unaoendelea wa 57 wa Kamisheni ya  Umoja wa Mataifa kuhusu Hadhi ya  Wanawake ( CSW). aliyekaa kati kati ya  Jaji Kileo, na  Naibu Mwakilishi wa Kudumu  Balozi Ramadhan Mwinyi ni,  Bw. John Hendra aliyewahi kuwa Mratibu wa UNDP nchini Tanzania,  Bw. Hendra ndiye aliyekuwa mwendashaji wa mkutano huo, bado anakumbuka vizuri kiswahili, kwa sasa ni Katibu Mkuu Msaidizi na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa   Sera na Mipango katika Taasisi ya UN- Women
    Bi. Anne T. Goldstein, Esg; Kutoka Chama cha Kimataifa cha Majaji  Wanawake akizungumza wakati wa mkutano huo,  Chama cha Kimataifa cha Majaji wanawake, kinafanya kazi kwa karibu na Chama cha Majaji  Wanawake- Tawi la Tanzania, na ndiyo chimbuko la  neno Sextortion. katika mchango wake licha ya kueleza kwa mapana  udhalilishaji wa kijinsia na rushwa ya   mapenzi, alihimiza sana  umuhimu wa wazazi kuzungumza  na watoto wao wote wa kike na wakiume kuhusu madhara ya ukatili huo na namna ya kukabiliana nao.

   wajumbe wanaoshiriki mkutano wa 57 wa CSW wakijumuika na washiriki wengine kujifunza nini Chama cha Majaji kinafanya katika ajenda zima ya kupiga vita udhalilishaji wa wanawake na watoto wa kike
   Mshiriki  ambaye alijitambulisha kwamba ni askari Polisi kutoka nchini Zambia akiuliza swali 
  wajumbe kutoka Tanzania wanaoshiriki mkutano wa 57 wa CSW wakijumuika na washiriki wengine kujifunza nini Chama cha Majaji kinafanya katika ajenda zima ya kupiga vita udhalilishaji wa wanawake na watoto wa kike.


  Na Mwandishi Maalum

  Mwenyekiti wa  Chama cha Majaji Wanawake  Tawi la Tanzania,  Mhe. Jaji Engera Mmari Kileo ameeleza kwamba  jamii ikishirikiana inaweza  kwa kauli moja  kupiga vita udhalilishaji  wa kijinsia na rushwa ya  mapenzi.

  Jaji Kileo ametoa kauli  hiyo siku ya jumanne, wakati  chama hicho cha majaji kilipoanda mkutano  wa  pembezoni ( Side event) sambamba na  Mkutano wa 57  wa Kamisheni  ya Umoja wa Mataifa  kuhusu   hadhi ya mwanamke ( CSW) unaoendelea  hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,

  Chama hicho cha Majaji, kiliandaa mkutano huo  ikiwa ni mara ya kwanza kuendesha mkutano  wa aina hiyo  ndani ya viunga vya Umoja wa Mataifa, kwa lengo la kuelimisha, kufahamishana, kupashana na kubadilishana mawazo  na wajumbe wengine, kuhusu matumizi  mabaya ya mamlaka  kwa lengo la  kudhalilisha   kijinsia  na kushawishi  rushwa ya mapenzi ( Sextortion).

   Bw.  John Hendra  ambaye aliwahi kufanya kazi nchini Tanzania kama Mratibu wa UNDP ndiye aliyekuwa mwendeshaji wa mkutano huo  uliovutia wajumbe wengi waliokuwa na hamu ya  kujielimisha kuhusu sextortion.  Hendra kwa sasa ni Katibu Mkuu  Msaidizi na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Será na Mipango katika Taasisi ya UN-WOMEN

   “ Unyanyasaji wa kijinsia na rushwa ya  mapenzi ni mambo yanayotokea  katika jamii yetu,  yanatokea  vyuoni,  mashuleni, majumbani, maofisini na hata mitaani. vitendo hivi siyo tu kwamba ni kosa la jinai , bali  pia ni ukiukwaji wa haki za binadamu” akasema  Mhe. Jaji Engera Kileo ambaye alikuwa mmoja wa wasemaji wakuu katika mkutano huo.

  Na kwa  sababu hiyo  na   kwa kulitambua tatizo hilo,  akasema,Tanzania kupitia Chama cha Majaji Wanawake, imekuwa ikitekeleza  mikakati mbalimbali ikiwamo ya  kuwaelimisha wanawake na watoto wa kike katika  taasisi za elimu ya juu, mashuleni  na katika maeneo mengine kuutambua na kutoufumbia macho ukatili huo.

  Aidha amefafanua kwamba, udhalilishaji wa kijinsia na rushwa ya ngono, si tatizo linalowakumba wanawake na watoto wakike pekee , bali  hata watoto wa kiume wamekuwa wahanga wa janga hilo.

  Mhe. Jaji Kileo amesema  hivi sasa kumekuwa na mwamko mkubwa wa kulitambua tatizo hilo, ingawa amekiri kwamba    bado    safari  ni ndefu na changamoto nyingi.

  Akazitaja  baadhi changamoto hizo ni  ufinyu wa raslimali ili kuwafikia walengwa wengi zaidi, kutokuwapo kwa utashi wa wahanga kujitokeza na kutafuta haki yao,  uwezeshaji  wa wakufunzi pamoja na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake na watoto wa kike.

  Katika utoaji elimu hiyo wa suala zima la sextortion,  Mzungumzaji mwingine alikuwa ni  Bi. Anne Goldstein, Esq ambaye ni  Mkurugenzi wa  Elimu ya Haki za Binadamu,  katika Chama cha Kimataifa cha Majaji wanawake.

  Akitoa  ufafanuzi kuhusu  udhalilishaji wa kijinsia na rushwa ya mapenzi,  Anne,alisema tatizo hilo haliko katika nchi zinazoendelea peke yake bali lipo duniani kote.

  Akasema ni tatizo  kubwa, sugu na lenye sura nyingi na  kwamba kulikabili kunataka nguvu za pamoja na ushiriki wa wadau wengi.

  Lakini akasema ni tatizo linaloweza kutafutiwa ufumbuzi ikiwa tu wadau wote wataonyesha utashi wa kufanya hivyo.

  Akahimiza sana suala la wazazi kukaa na watoto wao  wa kike na   kiume na kuelezana kinabaubaga kuhusu madhara ya udhalilishaji wa kijinsia na rushwa ya ngono ikiwa  ni pamoja na kuwajengea mazingira ya kuwa huru  kueleza pale wanapohisi kutaka kufanyiwa ukatili huo.

  Akasema chama cha Kimataifa cha Majaji Wanawake,  kimekuwa kikifanya kazi kwa karibu sana na Chama cha Majaji Wanawake – Tawi la Tanzania, na kwamba wanajivunia uhusiano na ushirikiano huo na  kitaendelea kufanya kazi kwa karibu   na Majaji watanzania.

  Naye   Katibu Mkuu  Msaidizi, Bw. John Hendra, yeyé  pamoja na kuwapongeza Chama cha Majaji  Wanawake kwa  kazi nzuri, kwa ujumla aliipongeza Serikali na watanzania wote, kwa kukubali na kutambua kwamba kuna tatizo hilo la udhalilishaji  wa kijinsia na rushwa  ya ngono na hivyo kuamua kulikabili.

  Akasema  UN- Women itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Tanzania katika maeneo mbalimbali.
  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akizungumza na Waziri wa Nchi wa Ireland anayeshughulikia masuala ya Biashara na Maendeleo, Mhe. Joe Costello alipofika Wizarani kwa mazungumzo na Mhe. Waziri Membe kuhusu kukuza  ushirikiano kati ya nchi hizi mbili na pia kuimarisha ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji.
  Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo na Mhe. Costello. Wengine katika picha ni Balozi Dora Msechu (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Naimi Aziz (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda.
  Mhe. Membe katika mazungumzo na Mhe. Costello. Wengine katika picha ni ujumbe uliofuatana na Waziri huyo wa Ireland akiwemo Balozi wa Ireland hapa nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan (wa kwanza kulia)


  Mhe. Costello akifafanua jambo kwa Mhe. Membe.
  Ujumbe wa Ireland wakati wa mazungumzo.
  Balozi Msechu (kushoto),  Balozi Naimi (katikati) pamoja na Bi. Zainabu Angovi (kulia) wakisikiliza mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Costello (hawapo pichani).
  Mhe. Membe akijadili jambo na Mhe.  Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland hapa nchini huku Mhe. Costello akisikiliza.
  Mhe. Membe akiagana na Mhe. Costello mara baada ya mazungumzo yao.

  0 0

   Mchezaji wa timu ya TSN, Sodi Ahmed (kulia) akimramba chenga Abdallah Fundi, wa timu ya Free Media, wakati wa mchezo wa michuano ya Kombe la NSSF 2013, uliochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu ya TSN imeibuka na ushindi wa mabao 5-0, mabao hayo yakiwekwa kimiani na wachezaji, Rashid Kagusa, aliyesalimia nyavu mara tatu, Evance Samwel, aliyefunga bao 1 na Said Kabasha, aliyetupia bao 1.
   Beki wa TSN, Sufianimafoto (kushoto) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Free Medi, saleh Ally, wakati wa mchezo huo.
   Mshambuliaji wa Free Media, Saleh Ally (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa TSN, wakati wa mchezo huo.
  Kwa picha zaidi bofya hapa

  0 0

  Na Anna Nkinda – aliyekuwa Magu

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekipongeza kituo cha utamaduni cha Bujora kwa kutunza na kuhifadhi utamaduni wa mtanzania unaolitambulisha kabila la wasukuma jambo litakalosaidia kizazi kijacho kuweza kujifunza utamaduni huo.

  Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alitoa pongezi hizo hivi karibuni alipokitembelea kituo hicho kilichopo wilayani Magu katika mkoa wa Mwanza.

  Alisema kuwa kituo hicho kimeonyesha mfano wa kuigwa kwani amejionea na kujifunza mambo mbalimbali ambayo hakuwa anayafahamu hapo awali kuhusiana na kabila hilo jambo la muhimu wahakikishe kuwa wanaendelea kutunza utamaduni wao.

  “Kazi mnayoifanya ni nzuri na inatakiwa kuigwa na watu wengine, hakika kwa kufanya hivi mtarithisha utamaduni wenu kutoka kizazi kimoja hadi kingine, watoto wenu wanatakiwa kujua mila zao kwani mtu asiye na utamaduni ni mtumwa”, alisema Mama Kikwete .

  Akisoma taarifa ya kituo hicho Padre Fabian Mhoja ambaye ni Mkurugezi alisema kuwa kituo kilianza mwaka 1954 kikiwa na lengo la kuhifadhi na kuendeleza tunu bora ya maisha ya watu ili waweze kumfahamu Mungu na kuishi kadiri ya mpango wake kwa kutumia utamaduni.

  Alisema kuwa wanajihusisha na shughuli za kutunza na kuendeleza urithi wa utamaduni wa mtanzania kwani kupitia kituo hicho wameweza kutangaza utalii na utamaduni ndani na nje ya nchi kupitia ngoma , nyimbo na michezo mbalimbali.

  Kituo hicho kimekuwa kikiandaa tamasha la Bulabo ambapo Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amekuwa akichangia ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka na kukusanya watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

  0 0


older | 1 | .... | 66 | 67 | (Page 68) | 69 | 70 | .... | 3286 | newer