Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 682 | 683 | (Page 684) | 685 | 686 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (kushoto) na Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma wakifurahia burudani ya ngoma za asili, wakati wakiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais Zuma alipokuwa akiondoka baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja nchini.
  Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakikagua gwaride la heshima, wakati Rais huyo wa Afrika ya kusini, akiondoka nchini baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati akiondoka nchini baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja. Picha na OMR.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Nishati Duniani Bwana Selim Kuneralp (kushoto) na Mhandisi John F. Kitonga wa kitengo cha Maendeleo ya Nishati Wizara ya Nishati na Madini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bwana Kuneralp amefika ofisi za Ubalozi wa Tanzania Ubeligiji kubadilishana mawazo na Balozi Kamala kuhusu kazi za Baraza la Nishati Duniani na jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika na shughuli za Baraza hilo.

  0 0

  MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Kambangwa,Denis Casmiry mwenye umri wa miaka 16 (pichani) amekutwa kwenye ufukwe wa Salander Bridge akiwa amefariki dunia

  Akizungumza na Ripota wetu huku akionekana kuwa na masikitiko makubwa,Baba Mzazi wa Mtoto huyo aliejitambulisha kwa jina la Casmiry,amesema kuwa walipata taarifa ya mtoto wao kupotea toka Jumamosi Desemba 20,2014 ambapo inadaiwa kuwa aliondoka nyumbani kwao akiwa na marafiki zake kwenda kwenye Mazoezi ya viungo kwenye ufukwe huo wa Coco Beach.

  "Aliondoka hapa nyumbani asubuhi na mapema kwenda kwenye mazoezi akiwa na wenzake,na walipomaliza kufanya mazoezi yao hayo,waliamua kuogelea kidogo ikiwa ni kawaida yao kila wanapomaliza mazoezi wanafanya hivyo,mara baada ya kumaliza kuogolea wenzake walitoka kwenye maji na hapo ndipo walipobaini kuwa mwenzao hawakuwa nae" alisema Bw. Casmiry.

  Aliendelea kusema kuwa "Baada ya kufanya juhudi za kumtafuta mwenzao bila mafanikio,vijana hao walirudi nyumbani na kutupatia taarifa na sisi bila kuchelewa tulitoa taarifa kituo cha Polisi na kutoa na askari wachache mpaka eneo la tukio na pia hatukuweza kumuona mpaka leo hii tunaukuta mwili wake Ufukweni,inauma sana kwa kweli".

  Mwili ya kijana huyo umekutwa kwenye ufukwe ya Salander Bridge,Jijini Dar es Salaam leo.
  Askari Polisi waliokuwepo kwenye eneo la tukio wakijadiliana jambo wakati wakijiandaa kwenda kuuhifadhi mwili wa kijana huyo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili,jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Bashir Yakub
  Ni ukweli usiofichika kuwa  biashara  na ujasirimali  kwa pamoja vimekua  kwa kiwango kikubwa. Hili linatokana na sababu nyingi ikiwemo ya kukua kwa biashara za kimataifa, maendeleo ya mawasiliano, marekebisho ya baadhi ya sera za nchi na sababu nyinginezo. Hali  hii imeleta ugumu kwa wanaofanya biashara nje ya kampuni. 

  Si rahisi kufanikiwa katika biashara bila kuifanya biashara yako katika mtindo wa kampuni. 

  Hata iwe ndogo ya kuuza mayai au kufuga kuku mafanikio zaidi ni pale biashara hiyo utakapoifanya kampuni. Ni kutokana na umuhimu ikanilazimu niwajuze hasa vijana  kuhusu kampuni tukijielekeza zaidi katika aina na uundwaji wake kutokana na Sheria ya Makampuni  ya mwaka 2002.


  0 0

  1. Pombe za Chimpumu, Dengerua, Kabungusi, Kangara, Komoni, Mbege na Chibuku.

  Hupoteza uwezo wa kufikili wa mtumiaji Huongeza ufanisi wa viungo vya mwili vilivyo katikati ya miguu ya mtumiaji chini ya kiuno kwa mbele, hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kujiusisha na ngono zisizo salama na kubaka. Zaidi ya 60% ya kesi zote za kubaka zilizotokana na ulevi zimehusishwa na utumiaji wa pombe hizi!Hukakamaza misuli ya midomo na kuongeza ufanisi wa koromeo (voicebox),hivyo si ajabu kuwakuta watumiaji wa pombe hizi wakipayuka ovyo na kwa sauti za juu kuliko kawaida.

  2. Pombe za Pingu na Gongo

  Hupunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kufikiri wa mtumiaji Huongeza joto la mwili la mtumiaji kwa kuongeza spidi ya metabolism (metabolic activities), hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kuvua nguo hadharani, ili kupunguza joto la mwili! Kwa upande wa pombe ya pingu, hii huongeza spidi ya myeyusho wa chakula(Digestion) na ikitokea mtumiaji hajala kwa muda mrefu huishia kutapika mpaka nyongo. Baada ya kuongeza spidi ya myeyusho wa chakula pombe hii hulegeza vifuniko vya mwili (sphincter muscles) hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kuachia kokoo madimba iliyo rojorojo(uharo wa nguvu na wenye harufu kali). Kwa watumiaji wa lile gongo litengenezwalo kwa kinyesi cha binadamu (kigamboni ni eneo maarufu kwa biashara hii), wengi wao huishia Intensive Care Units (ICU), na baada ya hapo hupelekwa Psychiatric Units (wodi za vichaa), kwani zaidi ya 63% ya watumiaji wa pombe hii huishia kuwa vichaa kamili!

  3. Pombe ya Mnazi

  Kiasi cha ulevi (alcoholic contents) kilichomo katika pombe hii,hushambulia sehemu ya ubongo wa kati (cerebellum), ihusikayo na kutunza utashi, hivyo si ajabu kwa mtumiaji wa pombe hii kuishia kuvurumusha matusi ovyo na kuyumba barabara nzima!Iwapo mtumiaji wa pombe hii hatakuwa mwangalifu na hivyo kunywa mdudu fulani aitwaye kigoto anayekuwa katika pombe hii, basi mtumiaji huyo atakuwa mlevi mbwa wa mnazi maishani mwake!Watu hushauriwa kuviepuka vyoo vilivyotumiwa na walevi wa pombe hii kwani harufu wanayoiacha huko chooni inahusishwa na kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya pua na ubongo (nose and cerebral cancer)

  4. Pombe ya Ulanzi

  Pombe hii hushambulia viunganishi vya mwili (Body Joints), kwa hiyo asilimia kubwa ya watumiaji wa pombe hii huishia kulala mabarabarani,vyooni na sehemu nyingine zisizo za kawaida kwa kushindwa kutembea!

  5. Pombe za Bia, Konyagi. Wiski na Wine mbalimbali

  Pombe hizi huongeza hali ya kujiamini kwa watumiaji na pia kuwakumbusha kuwa hapo zamani za kale, waliwahi kupitia shule,hivyo si ajabu kuwakuta watumiaji wa pombe hizi wakizoza kimombo na kujihusisha na mijadala isiyo na kichwa wala miguu punde baada ya kulewa!Pombe hizi hushambulia sehemu zilizo katikati ya miguu chini ya kitovu kwa mbele ya mtumiaji na kuzifanya sehemu hizo kuwa imara na zenye nguvu(strong and active) na hivyo kuongeza uwezekano wa kujihusihsa na ngono zisizotarajiwa na zisizo salama!
  SASA KAZI KWAKO KUPAMBANUA!!!

  HUU NI UTAFITI ULIOFANYWA NA MDAU WA GLOBU YA JAMII KUTOKA SUMBAWANGA

  0 0

  Na Editha Karlo Globu ya Jamii,Kigoma

  JUMLA ya maiti 14 zimezikwa baada ya makubaliano baina ya serekali ya Tanzania na serekali ya Demokrasia ya Congo(DRC)ambapo katika mazishi hayo serekali ya Congo iliwakilishwa na Balozi wa Congo kutoka ubalozi mdogo wa DRC Mkoani Kigoma.

  Akizungumza muda mfupi baada ya mazishi ya raia hao Balozi mdogo wa DRC nchini kutoka Ubaozi mdogo Mkoani hapa,Mh. Riki Moleme alisema.

  Mh. Maleme alisema kuwa amefarijika sana kwa namna serekali ya Tanzania ilivyochukulia kwa umuhimu mkubwa swala la maafa hayo ya Raia wa Congo na namna ilivyojitoa kushughulikia mazishi ya miili hiyo

  Naye Mhifadhi wa mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mahale,Herman Batiho alisema alianza kuona miili ya watu majira ya jioni ya Desemba 20 Mwaka huu na ndipo walipoamua kutoa taarifa katika mamlaka mbalimbali ambapo waliwasiliana na uongozi wa kijiji cha kalilani ambapo uongozi wa kijiji kwa kushirikiana na wanachi walianza kazi ya uopoji wa miili.

  Mwenyekiti wa kijiji cha Kalilani,Songoro Saidi alisema kuwa waliona moja ya mili wa maiti hizo asubuhi ya Desemba 21 ukiwa umeibuka juu,pia walipata kuwepo kwa miili mingine ikiibuka na kuelea ndani ya Hifadhi ya Mahale na ndipo waliposhirikiana kuipoa miili hiyo na hadi kufanikisha mchakato wa mazishi.

  Desemba 12 mwaka huu ya watu 128 walifariki dunia na wengine 250 waliokolewa kufuatia meli waliyokuwa wakisafiria kutoka Mobaa kuelekea Kalemii kuzama katika mwambao mwa ziwa Tanganyika katika Mkoa wa Kalemii nchini DRC,
  Askari wa jeshi la ulinzi wa Tanzania(JWTZ)wakiwaongoza viongozi wa serekali ya Tanzania na Congo na viongozi wa kijiji cha Kalikani pamoja na wananchi katika mazishi ya raia 14 wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo(DRC) waliofariki katika ajali ya meli Desemba 12 mwaka huu katika Mkoa wa Kalemi na miili yao kuibuka katika Hifadhi ya Mhale.Picha na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma

  0 0

  Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akikaribishwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Qatar, Bw. Yusuf Ahmad Al Hammadi wakati alipotembelea eneo inapojengwa bandari hiyo kubwa na yakisasa akiwa katika ziara ya kikazi nPhini humo Desemba 22, 2014. (picha na fisi ya Waziri Mkuu)

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  ya Gesi ya Qatar (Qatargas Operating Company Limited), Bw. Khalid Al Thani wakati alipotembelea ofisi kuu ya kampuni hiyo mjini Doha kujifunza uwekezaji wenye maslahi mapana ya taifa katika sekta ya gesi akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Desemba  22, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribishwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Mradi wa ujenzi wa bandari mpya ya Qatar, Bw. Yusuf Ahmad Al Hammadi wakati alipotembelea eneo inapojengwa bandari hiyo kubwa na yakisasa akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Desemba 22, 2014. 
  --------------------------------------------------
  WATANZANIA wanaoishi nchini Qatar wameiomba Serikali iangalie uwezekano wa kufungua ofisi ya ubalozi  nchini humo ili iwe rahisi kwao kufikisha matatizo yao na pia wawe na uhakika wa masuala yao kushughulikiwa kikamilifu.

  Wametoa ombi hilo kwa nyakati tofauti jana usiku (Jumapili, Desemba 20, 2014) wakati wakitoa hoja na amatizo yao mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye yuko nchini Qatar kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.

  Akizungumza kwa niaba ya Watanzania waishio Qatar katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Sheraton jijini Doha, Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania wanaoishi Qatar, Bw. Said Ahmed Said alisema ubalozi wanaoutegemea kwa sasa hivi uko Saudi Arabia ambako ni mbali na kwamba inakuwa vigumu kuwasilisha shida zote zinazowakabili Watanzania.

  “Kwa mfano kuna suala la fursa za watoto wetu kusomeshwa elimu ya juu na kulipiwa na Serikali ya hapa. Inakuwa vigumu kupata hiyo fursa kwa sababu hakuna mtu wa kutusemea,” alisema Bw. Said na kushangiliwa na wenzake.

  “Watoto wetu waliozaliwa hapa wakimaliza sekondari hawawezi kwenda Chuo Kikuu chochote kwa sababu mfumo wa hapa hauwaruhusu. Hata wale tuliowaacha nyumbani huwezi kuwaleta wakasomea hapa kwa sababu ya huo mfumo. Lakini wenzetu kutoka nchi nyingine wanapata hizo fursa kwa sababu wana quota yao. Tunaamini tukiwa na ubalozi hapa nchini, tutaweza kupata fursa kama wenzetu,” alisema.

  Watanzania wengine waliochangia hoja ya kuwa na ofisi ni Bw. Abdallah Sima Abdalla (kutoka Zanziabar), Bw. Hersi Mohammed Adam (kutoka Singida) na Bw. Iddi Ali Ameir ambaye pia anatoka Zanzibar.

  Hata hivyo, Bw. Hersi Mohammed Adam ambaye amefanya kazi kwenye kamouni ya Al Mazrui Oil Industries kwa miaka tisa, alisema kuna haja ya kuwaleta Watanzania wengi  wajifunze kazi ndogondogo zinazohusu uchimbaji mafuta kwani wana fursa ya kufundishwa wakiwa kazini. “Kuna kazi ambazo hazihitaji vyeti vya juu sana kama kusafisha mabomba ya gesi lakini pia ni za muhimu na zitawasaidia wengi kupata ajira wakati kazi kama hizo zikianza nchini Tanzania,” alisema.

  Akizungumzia suala la kuwa na ubalozi, Waziri Mkuu alisema wazo lao ni la msingi ikizingatiwa kwamba kuna Watanzania zaidi ya 300 wanaoishi Qatar. “Hili suala ni la Serikali na mimi naona jibu la msingi ni kuwa na ofisi ya ubalozi hapa Doha kwa sababu mko wengi na tuna mahusiano ya karibu sana na wenzetu,” alisema na kuahidi kulifuatilia kwa sababu amekwishajadiliana na  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Mahadhi Maalim ambaye yuko kwenye msafara wa Waziri Mkuu.
  Akizungumzia suala la ajira, Waziri Mkuu aliwahakikishia Watanzania hao kwamba Serikali ya Qatar imesharidhia mkataba wa kuruhusu raia wa Tanzania waje kufanya kazi Qatar. “Sisi tulianzisha huu mkataba na wenzetu hawa wameuridhia mwezi uliopita... naamini utatusaidia sana kwenye suala la ajira za watu wetu lakini itabidi tuangalie ninyi ambao mlikuwepo zamani kabla mkataba haujasainiwa tunawafaya nini,” alisema.

  Wakati huo huo, Waziri Mkuu Pinda alitoa nakala zipatazo 30 za Katiba Inayopendekezwa kwa Watanzania waishio Qatar na kuwataka waisome na kutoa mapendekezo yao hasa katika eneo la uraia pacha. “Hakikisheni mnaisoma na kujadili kwa kina eneo hili na kisha mtupe majibu yenu kwa sababu suala hilo liliibua mjadala mkubwa ndani ya Bunge Maalum la Katiba wakati likijadiliwa,” alisema.

  Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kimani; Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Mahadhi Maalim; Naibu Waziri wa Nishati, Bw. Charles Kitwanga; Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Godfrey Zambi.

  Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, wabunge wawili Bi. Amina Makilagi na Bw. Aeshy Hilali, Dk. Gideon Kaunda wa TPSF na Bw. Shigela Malocha kutoka TPDC.

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini Jumatatu  ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya Jumatatu, Desemba 22, 2014, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Jacob Zuma.

  Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, yalichukua kiasi cha saa moja na dakika 45 na yalihusu uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini.

  Rais Zuma ambaye aliwasili nchini usiku wa jana, Jumapili, Desemba 21, 2014, ameondoka nchini mara baada ya kumalizika mazungumzo hayo.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu.

  Dar es Salaam.


  22 Desemba, 2014


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, walipoingia katika chumba maalum cha mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo wakati wa uzinduzi wa Majengo ya Taasisi hiyo ya  Mafunzo ya Sheia
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuweka Jiwe la Msingi katika Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo hayo

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la viwanja vya Majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania, baada ya kuzindua rasmi majengo hayo yaliyopo eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akiendesha kikao cha 43 cha chombo hicho cha utendaji cha Jumuiya ya Madola Jijini London Uingereza.

  0 0

  Na Sultani Kipingo 
  Baada ya siku kadhaa za kupekua kila mahali kwenye vitabu vya historia, nimekuta hakuna ajuaye has asili ya saluti. Ila nimekuta maelezo kwamba katika historia ya askari, mkono wa kuume (ama mkomo wa silaha) ulikuwa ukiinuliwa kama ishara ya salamu za kirafiki. 
  Wanahistoria wanasema huenda hiyo ilikuwa ni ishara ya kuonesha kwamba hauko tayari kutumia silaha na kushambulia. Ila toka enzi hizo, ni askari asiye na cheo ama mwenye cheo kidogo ndiye alikuwa analazimika kutoa ishara hiyo mwanzo.
   Hadithi ingine ya kihistoria inatanabahisha kwamba saluti hii ya askari ya leo imetoka enzi za Wafalme nchi za magharibi, ambapo askari aliinua mkono wa kuume na kugusa mfuniko katika kofia yake ya delaya kwa mbele ili afande apate kumjua wanapokaribiana. Hata hivyo, kitendo cha saluti ya askari imekuwa ya aina tofauti kwa karne na karne. 
  Kuna wakati inasemekana ilikuwa ikipigwa kwa mikono yote miwili! Wakati mwingine saluti ilipigwa kwa mkono kuishia kifuani huku viwiko vikiangalia chini. Hili linasemekana lilizuka katika meli za vita ambapo askari wa chini aghalabu huwa na mikono michafu kwa kazi za kusafisha meli, hivyo ilikuwa kama unamkosea adabu afande kumuonesha mkono uliojaa girisi. 
  Pia kwenye maabrasha mengine ya kihistoria kumeonekana saluti za mkono wa kushoto. Pia kuna maelezo ya kihistoria yanayosema kwamba ilikuwa ni kitendo cha lazima kwa askari wa cheo cha chini kuonesha heshima mbele ya afande wake kwa kuvua kofia, ambapo kiasi hili linaonekana lina ukweli fulani ndani yake. 
  Hata hivyo saluti hii haikukaa sana kwani makofia mengine ya askari yalikuwa kazi kuyavua chap chap. Hivyo kwenye karne ya 18 na 19, askari wakaachana na hiyo saluti ya kuvua kofia, na badala yake kukaja kugusa kofia hiyo kwa mbele. Baada ya hapo, staili zikabadilika badilika hadi hii saluti ya kisasa ikawa imeshika hatamu. 
  Askari wa Ujerumani chini ya Adolf Hitler walikuwa na saluti ya aina yake toka achukue madaraka mwaka 1933, ile ya kunyoosha mkono mbele na iliitwa  "Hilter Salute" ambapo si askari tu hata raia walitakiwa kuipiga huku wakimaka "Heil Hitler!" Ila ikaja  kupigwa marufuku baaada ya Hitler kuangushwa mwaka 1945 katika vita kuu ya pili ya dunia.
  Katika miaka ya 1745 (takriban karne mbili na nusu zilizopita) inasemekana katika kitabu cha kanuni za jeshi la uingereza kinasema: "Askari wanaamriwa kutovua kofia zao wanapopishana na afande, ama kusemeshwa naye, ila wanatakiwa kugusa paji la uso kwa vidole vya mkono wa kuume na kuinama wakati wa kupishana na afande" 
   Kwa vyovyote vile, kitendo cha mwenye cheo cha chini kumpigia saluti afande ni cha kuonesha heshima, na pia kutambua umuhimu, wajibu na ufahari wa kazi za uaskari.

  0 0
 • 12/22/14--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • Mr Blue - Pesa

  0 0

  Bw. Johnson Lukaza
  Bw. Mwesigwa Lukaza 

  Na Happiness Katabazi (UB)
  HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imemwachilia huru Mwenyekiti  wa Makampuni ya Proin, Bw. Johnson Lukaza na mdogo wake Mwesiga Lukaza waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Sh.Bilioni Sita Katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu (EPA), baada ya kumuona hana hatia Katika Kesi iliyokuwa ikimkabili.

  Hukumu hiyo Imetolewa Jaji wa Mahakama Kuu Edson Mkasimongwa aliyekuwa alisaidia na Hakimu Mkazi Pamela Mazengo.

  Bw. Lukaza ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) alikuwa akitetewa na Wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana na Wakili Alex Mshumbusi.

  Akisoma hukumu hiyo Jaji Mkasimogwa alisema Kesi hiyo ya Mwaka 2008 , Mahakama imesikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kupitia vielelezo mbalimbali, na Mahakama yake imefikia uamuzi wa kuwaachiria huru washitakiwa wote wawili kwa sababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi thabiti ambao ungeishawishi Mahakama hiyo iwakute na hatia washitakiwa Hao.

  0 0

  PARTY starts Wednesday the 24th Dec; X-MAS EVE ndani ya isumba lounge (jollies club). 
  PARTY continues on Thursday the 25th Dec; X-MAS DAY. 
  Friday boxing day, Saturday, Wednesday the 31st Dec 2014  NEW YEAR'S EVE and... 
  Thursday the 1st January 2015: NEW YEAR'S DAY!! Ladies and gentlemen it's party time with 
  DJ JOHN DILLINGA & DJ FAST EDDIE. 
  Karibu sana

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik na kulia ni katibu wa Baraza la wazee wa Dar es Salaam Mzee Mtulia.
  Baadhi ya wazee na wananchi wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akilihutubia taifa kupitia wazee wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
  Picha na Freddy Maro. Picha zaidi BOFYA HAPA

  Bofya Link hiyo kumsikiliza 

  0 0

  Benki ya NMB leo imefungua tawi jipya maeneo ya Gongo la mboto- Dar es Salaam tawi linalokadiriwa kuhudumia zaidi ya wateja 300 kwa siku. Tawi hili lipo karibu na kituo cha dala dala cha Mzambarauni mkabala na kituo cha mafuta Oil com.

  Tawi hili linatoa huduma kwa wakazi wa Chanika,Pugu,Majohe,Kitunda,Mongo la ndege na maeneo yote ya karibu.Vile vile huduma zote za kibenki zinapatikana katika tawi hili zikiwamo ufunguzi wa akaunti mbali mbali,Huduma za mikopo pamoja na huduma za kuweka na kutoa fedha.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe. Raymond Mushi, akikata utepe kuashiria  uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Gongo la Mboto .  Kushoto  ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar e salaam – Bw. Salie Mlay  na  kulia ni  meneja wa NMB Tawi la Airport Bi.Hellen Mapunda.
  Mhe.Raymond Mushi akiongea na sehemu ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Tawi.
  Mhe. Raymond Mushi akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa NMB mara baada ya uzinduzi rasmi wa tawi la Gongo la Mboto.

  0 0

  Wafanyakazi wa Rwandair wakipozi katika picha ya pamoja na zawadi zao, kushoto ni Lucy Ismail RwandAir country manager, Gladys Buhama na Hamida Hamza Reservation staff na kulia ni Eugene Mugisha Airport Station Manager
  RwandAir Tanzania Country Manager, Lucy Ismail akifungua sherehe kwa kukaribisha wageni waalikwa na kutambulisha baadhi ya staff,kulia ni Roshni,Lucy, Mayyada,Gladys na mwisho kushoto ni Naina.


  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde akijaribu baiskeli ya mazoezi aliyokabiodhiwa kama zawadi katika hafla ya kuwapongeza watumishi wa Wizara waliostaafu iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki na kulia ni Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi.
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akimkabidhi zawadi Mtunza Kumbukumbu Mstaafu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Clara Mlamlyingu katika hafla ya kuwapongeza watumishi wa Wizara waliostaafu iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Bi. Mlamlyingu ni Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi na kulia ni Jaji Dkt. Gerrald Ndika, Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania.
  Watumishi Wastaafu wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa na vyeti vyao katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa Wizara wakiongozwa na Naibu Waziri Mhe. Angellah Kairuki na Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi. Hafla ya kuwapongeza ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.


  0 0


older | 1 | .... | 682 | 683 | (Page 684) | 685 | 686 | .... | 3286 | newer