Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110079 articles
Browse latest View live

JOHN STEPHEN AKHWARI :NGULI MCHEZO WA RIADHA ALIYEWEKA HISTORI YA KIMATAIFA

$
0
0
JOHN Stephen Akhwari ni miongoni mwa wanariadha wenye historia kubwa

hapa nchini kutokana na umahiri wake katika mchezo huo.

Akhwari anakumbukwa sana katika Michezo ya Olimpiki kutokana na kauli
yake ya kizalendo aliyoitoa wakati aliposhiriki mbio za marathoni
katika Michezo ya Olimpiki iliyofanyika huko Mexico mwaka 1968


JOHN Stephen Akhwari akiwa na baadhi ya medalii zake alizozipata katika mashindono ya riadha



Airtel yatangaza kumi bora wa wiki wa shindano la Airtel Trace Music Stars

$
0
0
Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando (kulia)  na Meneja masoko wa Airtel Tanzania, Bi. Aneth Muga (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Airtel Trace Music Stars leo mara baada ya washiriki hao kuongea na waandishi wa habari kwaajili ya kuomba wananchi kuwapigia kura.
Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipotangaza washiriki waliongia nafasi ya kumi bora katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars kwa wiki hii. Kulia ni Aneth Muga Meneja Masoko wa Airtel Tanzania anaesimamia mashindano hayo ya Airte Trace Music Stars. Hafla ya kutangaza washiriki hao wa 10 bora aimefanyika makao makuu ya Airtel jijini dar es salaam leo.
Meneja Masoko wa Airtel Tanzania,Bi. Aneth Muga akielezea jinsi ya kupiga KURA kwa washiriki waliofanikiwa kuingia 10 bora ya mashindano ya Airte Trace Music Stars. Kulia ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando katika hafla ya kuwatangaza washiriki hao iliyofanyika ofisi za Airtel makao makuu morocco Dar es salaam leo.

Makampuni saba yajisajili Tuzo za Bodi Bora Sekta ya Benki na Bima

$
0
0
MAKAMPUNI saba yamethibitisha ushiriki wao katika tuzo za bodi yenye uongozi bora katika sekta ya kibenki na bima zijulikanazo kama Best Board Leadership Awards (BBLA), zilizopangwa kufanyika Januari 30, mwakani katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mratibu wa tuzo hizo, Bi. Neema Gerald, imezitaja benki zilizothibitisha kushiriki katika tuzo hizo kuwa ni pamoja na Benki ya Posta (TPB), Benki ya Exim na Benki ya CRDB.

Aliyataja makampuni ya bima yaliyothibitisha kushiriki katika tuzo hizo kuwa ni Heritage Insurance, Alliance Insurance Corporation, Alliance Life Assurance na Strategis Insurance (T) Limited.

Tuzo hizo zimelenga kutambua uongozi bora wa Bodi za Wakurugenzi katika Sekta ya Kibenki na Bima.

Bi. Neema aliendelea kuzisihi kampuni zaidi zilizopo katika sekta ya kibenki na bima kujitokeza kwa wingi ili kujisajili katika tuzo hizo zilizoandaliwa chini ya mwamvuli wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA) na Chama cha Makampuni ya Bima Tanzania (ATI).

“Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa makampuni yaliyoonyesha mwamko wa kushiriki kwenye tuzo hizi katika hatua hizi za mwanzo za maandalizi,” alisema na kuongeza:

 “Tuzo hizi zitatoa fursa ya ufahamu wa jinsi gani bodi bora inaweza kusaidia taasisi kupata mafanikio na kufikia utendaji bora hususani katika eneo walilobobea kiutalaam. Hivyo ningependa kuziasa kampuni zaidi kujitokeza na kushiriki,” alisema Bi. Neema.

Alibainisha kuwa zoezi hilo, tathmini na upangaji wa mwisho wa matokeo utafanywa na jopo la majaji waliobobea na wenye rekodi bora za kiutendaji.

Tathmini hiyo italenga zaidi katika ufanisi wa Bodi ya Wakurugenzi katika suala la utawala wa taasisi, usimamizi wa fedha na uwezo wa kuiongoza dira ya taasisi kwa ujumla wake. Maeneo mengine ni umakini wa bodi katika uwazi, uwajibikaji, utendaji, na ufuataji wa hatua madhubuti na  utendaji wake.

Alitaja maeneo mengine ambayo bodi itafanyiwa tathmini kuwa ni utoaji wa mitazamo yakinifu ya bodi katika kusisitiza umuhimu wa utendaji wa mtaji watu katika ngazi ya bodi na kuweka mbele vigezo vitakavyowezesha utendaji bora zaidi wa bodi, "alisema.

Bi. Neema aliwataja wadhamini wa tukio hilo la kipekee kuwa ni pamoja na Capital Plus Internaional Limited, Real PR Solutions Limited, Afrimax Strategic Partnerships Limited, Serena Hotel na IPP Media.

"Tumeona umuhimu wa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na wakurugenzi wa bodi katika taasisi zao.Tunaamini kuwa katika kila mafanikio ya taasisi ya kifedha, nyuma yake kuna bodi ya wakurugenzi imara na makini. Sasa, sifa hizo ambazo wajumbe wa bodi wengi wanakua nazo zinapaswa kutambuliwa na kuthaminiwa, "alisema.

Bi. Neema alisema kuwa ni utamaduni uliozoeleka kwa Maafisa Watendaji Wakuu na Wakurugenzi Wakuu pekee kuthaminiwa na kutambuliwa na waajiriwa au jamii nzima kwa ujumla.

"Ni wakati muafaka sasa kwa bodi zenye utendaji bora kutambuliwa na kuzawadiwa kikamilifu kwa jitihada zao," alisema.
Bi. Neema aliongeza kuwa tuzo hizo zimeanzishwa kwa wakati muafaka nchini kipindi ambapo sekta za Bima na kibenki zinapitia mabadiliko makubwa huku makampuni mengi zaidi ya bima yakijitokeza na masoko zaidi kuongezeka ili kufikia wateja wengi katika nyanja zote za maisha.
"Kwa mabadiliko haya yanayotokea wakati huu, hasa katika sekta ya fedha ambapo idadi kubwa ya makampuni ya bima na benki yamekuwa yakifungua biashara Tanzania, wateja wanahitaji kuwa na uhakika kuwa malipo yao ya bima yako salama na wanaweza kupatiwa kwa wakati wowote", alisema.

NEW VIDEO: BRACKET - ALIVE Ft. DIAMOND & TIWA SAVAGE

$
0
0
Giving thanks to the Almighty God is good thing to do as the year comes to a close and Afro-pop duo; Bracket have done it well and with a massive collaboration. Their new video; Alive features East-African star Diamond Platinumz and the sensational Tiwa Savage as they reflect on the moments when one half of the group; Vast was diagnosed and treated for cancer. Bracket is thankful to the Lord for being alive.

MSD YAKUBALI AGIZO LA SERIKALI KUWEKA ALAMA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA

$
0
0
NA CHALILA KIBUDA GLOBU YA JAMII,DAR

KAIMU Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD),Cosmas Mwaifwani amesema bohari ya dawa imepokea agizo la serikali kuweka alama katika dawa  za umma pamoja na vifaa tiba ili kuweza kudhibiti upotevu wa dawa pamoja na vifaa tiba.

Mwaifwani aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati  bohari hiyo katika kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Alisema katika mkakati mwingine ni kuanzisha maduka ya jumla ya dawa na vifaa tiba ikiwa ni lengo ya kuweza kusambaza  dawa katika ngazi zote kuliko ile ya dawa kufika katika ngazi za wilaya.


“Ifikapo Januari 30  mwakani ,MSD itatekeleza mabadiliko yenye lengo la kuhakikisha dhima ya kuwezesha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora na bei nafuu ambayo kila mtanzania anaweza kumudu hiyo na utekelezaji huo ni vitendo na sio kusema bila kufanya utetekelezaji”alisema Mwaifwani.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD),Cosmas Mwaifwani akizungumza na waandishi wa habari( hawapo pichani) kuhusu mradi wa uzalishaji dawa na Vifaa tiba kwa Ubia wa sekta Binafsi katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakichukua habari ya kaimu Mkurugenzi wa MSD. 

Katibu mkuu mpya wa Yanga atangaza mikakati yake ya kuhakikisha Klabu inajiendesha kiuchumi

$
0
0
Katibu mpya wa Yanga Dk. Jonas Tiboroha, ametangaza mikakati yake ya kuhakikisha Yanga inajiendesha kiuchumi ikiwa ni pamoja na kupitia upya mikataba yote ya wadhamini.

Akizungumza Makao Makuu ya Klabu hiyo leo, Tiboraha alisema kuwa Yanga ni klabu kubwa hiyo ni wakati wa kujiendesha yenyewe badala ya kutegemea mtu binafsi na kwamba haiwezi kuwa na mikataba ambayo haikithi maslahi ya klabu hiyo.

"Yanga ni bidhaa inayojiunza yenyewe uwezi kuingia mkataba wake sawa na Stand United, haiwezekani ikapata mgao sawa kama wanafunzi wa shule ya msingi unawapanga mstari unawambia haya kila mtu unamgawia pipi moja moja na wanaridhika, haiwezekani ni lazima Yanga iwe tofauti.

"Klabu kama Liverpol, inawashabiki wengi hata kama haipo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi linapokuja suala la mgao wa fedha inapata fungu kubwa kwa vile tayar inajiuza, sasa Yanga ingie mikataba sawa na kina Stand United dunia nzima itatushangaa."alisema.

MPINGA AWASHUKIA MAWAKALA WA MABASI NA MADEREVA NCHINI

$
0
0
KIKOSI cha Usalama Barabarani  nchini  kwa kushirikiana na Chama cha Kutetea  Abiria Tanzania (CHAKUA) limesema wataendelea kudhibiti upandishaji wa holela wa nauli  za mikoani kuelekea katika sikukuu za kufunga mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Mohamed  Mpinga amesema watachukua hatua kali kwa mawakala wataopandisha nauli za mikoani.

Mpinga alisema kikosi cha usalama barabarani kimejipanga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora usafiri kwa bei zilizopangwa pamoja na kutoa onyo kwa madereva wanaoendesha mabasi na magari kufuata sheria za usalama barabarani.

“Hatutavumilia mawakala na madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani yote haya ni kutaka wananchi wetu wasinyanyasike katika kipindi cha sikukuu siku zijazo sheria zimewekwa na lazima watu wazifuate”alisema ,Mpinga.

Aidha alisema wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano pale watapoona wanaopandisha nauli ili kuweza sheria ichukue mkondo wake kukaa kimya kwa wananchi kunafanya jeshi kushindwa kuwabana watu wanaofanya hivyo.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed R. Mpinga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu abiria kutoa taarifa kwenye mamlaka husika ili watetewa na fedha  zao ziweze kurudishwa hata kama ni Tsh. 100/=.

vurugu zazuka kariakoo leo,wengi wapoteza fahamu

$
0
0
Msamaria mwema akimbeba Mamalishe alifahamika kawa jina la Khadija Rashidi aliezirai baada ya milipuko ya mabomu katika ghasia za wamachinga na Askari Polisi leo mchana katika eneo la kariakoo. Mama lishe huyo alikuwa katika shughuli zake za kutayarisha chakula ghafla wamachinga waliokuwa wanakimbia kutaka kujificha katika sehemu za wafanyabiashara hao. 
baadhi ya wasamaria wakimsaidia Mama lishe aliefahamika kwa jina Mwanahamisi ambaye alizimia baada ya mabomu kurindima katika vurugu kati ya wamachinga na Askari Polisi cha FFU leo mchana.
Mashuhuda.
Askari Polisi wakiwapakia kwenye gari baadhi ya Wamachinga waliosababisha tafrani katika eneo la Kariakoo,Jijini Dar es salaam mchana wa leo. 

NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA ZIARA KATIKA WITUO VYA AFYA MKOA WA KASKAZINI ''A'' UNGUJA

$
0
0
Mkuu wa kituo cha Afya cha Mkokotoni Mcha Haji Makame akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (alievaa miwani) alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya afya vya Wilaya Kaskazini A. Wa kwanza (kushoto) mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Andymicheel Ghirmany akifuatiwa na mwakilishi wa UNICEF Zanzibar Bibi Fransisca.
Mkuu wa kituo cha Afya Mkokotoni akiwaonyesha wawakilishi wa UNICEF Bibi Fransisca na mwenzake wa WHO Ghirmany jiko la kuchoma takataka za Hospitali hiyo.

Black &White Bash 55th Birthday party ya Asia Idarous Khamsin Desemba 24

$
0
0
Na Andrew Chale
WABUNIFU wa Mavazi wachanga na chipukizi wamemwandalia Sherehe za kuzaliwa ya Mama wa Mitindo, Asia Idarous Khamsin, zitakazofanyika usiku wa Desemba 24, ndani ya ukumbi wa M.O.G Bar (Nyumbani Lounge) huku ikisindikizwa na Spice Modern Taarab pamoja na Mini fashion show.

Katika usiku huo maalum, kiingilio ni sh 5,000, huku vazi maalum likiwa Black & White, ambapo pia wadau watakaojumuika na Mama wa Mitindo, watapata burudani kali ya muziki kutoka kundi hilo la Spice Modern taarab, Dj Mapuu pamoja na shoo ya ubunifu wa mavazi (Min fashion show) itakayopambwa na wabunifu wanaochipukia.

Usiku huo wa Black &White Bash 55th Asia Idarous Khamsin, pia itakuwa na Red Carpet na wadau watapiga picha na mastaa mbalimbali sambamba na pongezi za kunyakua tuzo ya ‘Life Time Achievement Swahili Fashion Week 2014’.

Kampuni ya TTCL yatoa msaada Hospitali ya Ocean Road

$
0
0
Mkuu wa Huduma kwa wateja wa kampuni ya TTCL, Laibu Leonard (wa kwanza kulia) akimkabidhi baadhi ya misaada Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ocean Road, Marry Haule (nguo ya bluu) waliyoitoa kwa wagonjwa. Wengine ni maofisa wa TTCL. Mkuu wa Huduma kwa wateja wa kampuni ya TTCL, Laibu Leonard (wa kwanza kulia) akimkabidhi baadhi ya misaada Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ocean Road, Marry Haule (nguo ya bluu) waliyoitoa kwa wagonjwa. Wengine ni maofisa wa TTCL.Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wakishusha bidhaa mbalimbali ambazo wamezitoa kama msaada kwa wagonjwa wa kansa Hospitalini hapo. Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TTCL wakishusha bidhaa mbalimbali ambazo wamezitoa kama msaada kwa wagonjwa wa kansa Hospitalini hapo.Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ocean Road, Marry Haule (nguo ya bluu) akishukuru TTCL mara baada ya kukabidhiwa msaada huo. Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Ocean Road, Marry Haule (nguo ya bluu) akishukuru TTCL mara baada ya kukabidhiwa msaada huo.

TUNDA MAN - MAPENZI YALE YALE (Official Video)

KAEGESHA

MH. ZAINABU KAWAWA AMUENZI HAYATI MZEE KAWAWA KWA VITENDO

$
0
0
Na Mdau Sixmund J.B
Mh Zainabu Kawawa ameamua kuendelea kumuenzi kwa vitendo aliekuwa mmoja wa wahasisi wa Taifa letu Marehemu Baba yake Mzee Rashidi Mfaume Kawawa, kwa kuikarabati shule ya msingi aliyo soma Mzee Kawawa. 

Akiwa wilayani Liwale alipokulia na kusomea Marehemu Mzee Kawawa, Mh Zainabu aliwatembela wazee mbali mbali waliokuwa marafiki wa Mzee Kwawa ili kuwawajulia hali na kusikia mitazamo yao ya Liwale ya sasa nakipindi walipo kuwa na Marehemu Mzee Kawawa. 

Wakitoa mitazamo yao Mzee Saidi Mussa Suramoyo na Mzee Mohamedi Hasani Kichukwi walisema kuwa Mzee Kawawa aliwajali sana watu Waliwale kwani alihakikisha kila mkazi wa wilaya hiyo analima ili apatemazao yakutosha na si kuishi kwa kutegemea wengine, pia alisema Mzee Kawawa aliweza kufanya wanaliwale kuwa kitu kimoja na hakuwagawa tofauti na ilivyo sasa baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwagawa wananchi kitu kinacho sababisha mifarakani.

“Sikuizi wanaliwale tunaishi kama hatujuani, watu wanaishi kimakundi makundi tu, tena wale waliokuwa karibu na wakubwa ndio wanafaidi nakuonekana wamaana sana kuliko sisi wazee ambao inaonekana hatuna msaada kwa hao wakubwa, namkumbuka sana rafiki yangu Rashidi Kawawa alitupenda sanaa lakini sasa weacha tu.” Alisema Mzee Saidi Mussa Suramoyo.

Nae Mzee Mohamedi Hasani Kichukwi akiongea kwa tabu kutokana na uzee aliokuwanao alimshukuru sana Mh Zainabu kwa kufuata nyayo za Baba yake kwa kuwaonesha upendo wa kuwatembelea na hata kuikarabati shule ya Msingi aliyo soma Muhasisi wa Taifa letu Mzee Rashidi Mfaume Kawawa, kwani ilikuwa katika hali mbaya kimajengo.

Akiongea na Muandishi wa habari hizi, Mh Zainabu aliwashukuru wanaliwale kwa kuishi vyema na Baba yake Mzee Kawawa na kuendelea kumkumbuka kwa mema yote aliyo wafanyia, pia anatoa wito kwa watanzania wote kumuenzi Mzee Kawawa kwa undeleza yale yote mazuri aliyo tuachia hasa la viongozi kuwajali wananchi wanao watumikia.

Mh Zainabu aliwaahidi wazee hao wa Liwale kuendelea kushirikiana nao ili kuyaendeleza yale yote aliyo yafanya mzee Kawawa enzi za uhai wake akiwa kama Mbunge wa wilaya hiyo.
Pichani ni rafiki yake kipenzi cha Hayati Mzee Rashidi Kawawa Mzee Mohamedi Hasani Kichukwi wa kijiji cha Mpengele akifafanua jambo alipo tembelewa na Mh Zainabu Kawawa ambae ni mototo wa Mzee Kawawa.
Pichani Mwenye furahaa ni Mh Zainabu Kawawa akiwa mbele ya madarasa aliyosomea Baba yake Mzee Rashidi Mfaume Kawawa, kwa sasa shule hii inaitwa Shule ya Msingi Kawawa.
Mzee Saidi M. Suramoyo akielezea namna walivyo ishi na rafiki yake Hayati Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Nyumba hii ndiyo nyumba ya kwanza ya Muhasisi wa Taifa hili Mzee Rashidi Mfaume Kawawa iliyopo kijiji cha Mpirani Wilaya ya Liwale hata hivyo Mzee Kawawa alimzawadia nyumba hii rafikiyake huyu.

TASWIRA MBALIMBALI JIJINI DAR


ngoma azipendazo ankal

$
0
0
MANDOJO & DOMOKAYA - NIKUPE NINI

MASHAUZI CLASSIC YAPANIA KUITEKA MOROGORO X-MAS

$
0
0
Kundi zima la Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi, litafanya utambulisho wa wimbo wao mpya “Sura Surambi” kwa wakazi wa Morogogo Disemba 25 kwenye maadhimisho ya siku ya Christmas. 

 Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhani maarufu kama Isha Mashauzi (pichani juu), ameuambia mtandao huu kuwa onyesho hilo litafanyika ndani ya ukumbi wa Savoy Hotel na watasindikizwa na mfalme wa kigodoro Msaga sumu. 

 Isha amesema “Sura Surambi” ni ngoma yao mpya kabisa iliyoachiwa mwishoni mwa mwezi uliopita na Morogoro unakuwa ndio mji wa kwanza baada ya Dar es Salaam, kuonjeshwa ladha ya wimbo huo ambao unafanya vizuri sana kwenye vituo vya radio.

 “Huu ni utunzi na uimbaji wangu mimi mwenyewe, sina mengi ya kuongea zaidi ya kuwaahidi wakazi wa Morogoro burudani iliyokwenda shule,” alisema Isha. 

 Sura Surambi ni maandalizi ya albam mpya ijayo ya Mashauzi Classic ambapo tayari nyimbo mbili zimesharekodiwa, hii ikiwa ni pamoja na “Ubaya Haulipizwi” ulioimbwa na Asia Mzinga, binti wa waimbaji wakongwe wa taarab Abbas Mzinga na Bi Mwanamtama Amir.

OLOLOSOKWAN WAJIWEKA TAYARI KUTIMIZA NDOTO YA KIJIJI CHA DIJITALI

$
0
0
DSC_0010
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues aliposimama kwenye Kijiji cha Ngeresero kwa ajili ya kuwaungisha wanawake wa kimasai wanaofanya biashara ya kuuza bidhaa mbalimbali za shanga kwa watalii wanaosimama kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kupata mahitaji mbalimbali, wakati akielekea kijiji cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na shirika lake la UNESCO.

Na Mwandishi wetu, Arusha
NDOTO ya kuwa na kijiji cha dijitali nchini Tanzania itaanza kutimia Januari mwakani wakati vifaa vinavyotakiwa kukamilisha mradi huo vitakapowasili kutoka kampuni ya Samsung Electronics.

Kwa mujibu wa watekelezaji wa mradi huo mkubwa unaotarajiwa kutumia dola za Marekani milioni 1, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) vifaa hivyo vinatarajiwa kuingia Bandari ya Dar es Salaam Januari tano mwakani.

Mkataba wa kuanzishwa kwa kijiji cha dijitali eneo la Ololosokwan tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro ulitiwa saini kati ya Unesco na Samsung electronics Novemba 6 mwaka huu.

Akizungumza na halmashauri ya kijiji cha Ololosokwan , Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues amewataka wanakijiji kujiandaa kwa mabadiliko makubwa ya kijiji chao kinapoingia katika dunia ya dijitali.
DSC_0111
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiwaonyesha jambo wakina mama wa kimasai jinsi gani teknolojia inayvowaleta watu kwa ukaribu zaidi kupitia "Tablet" ambapo katika kijiji hicho cha digitali cha Samsung wakazi wa eneo hilo watakua wakipewa mafunzo kutumia kifaa hicho cha "Tablet".

Wateja wa Airtel Money kutuma pesa bure kwa msimu huu wa siku kuu

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa mara nyingi tena imewazawadia wateja wake wakatia wa msimu huu wa sikukuu na  OFA maalum itakayowawezesha  kutuma pesa bila kikomo BURE kupitia Huduma ya Airtel Money.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Mawasiliano Bi Beatrice Singano Mallya alisema” Tumeona ni vyema kuwazawadia wateja wetu nchin nzima na kuwawezesha  kutuma pesa BURE wakati wa msimu huu wa sikukuu kwani tunatambua wateja wetu na watanzania wanafanya miamala ya pesa kwa wingi wakati wa kipindi hiki cha msimu wa Sikukuu za Xmass na Mwaka mpya na kusherehekea nao. kuanzia sasa wateja wetu wataweza kutuma pesa kwa ndugu jamaa na familia popote nchini Airtel –Airtel BURE kabisa.

Hii ni nafasi pekee kwa wateja wetu na tunaamini kabisa kwamba ofa hii itawapatia wateja wetu thamani ya pesa zao na kuwawezesha kupata pesa ya akiba kwa matumizi mengine katika msimu huu wa sikukuu”.

Pamoja na ofa hii pia ya Airtel Money pia tumeweza pia kuwazawadia wateja wetu Katika msimu huu wa sikukuu na Ofa kabambe ya simu za kisasa kwaajili ya wapendwa wao zinazopatikana katika maduka yetu zikiambatana na vifurushi , Ofa kabambe nchini .

 na uzinduzi wa Ofa hii ya Airtel Money leo ni mwendelezo wa shamrashamra za kusherehekia msimu wa sikukuu na wateja wetu.

“Sambamba  na hilo huduma yetu ya Airtel Timiza bado inaendelea, wateja wanaweza kukopa pesa na kukidhi mahitaji .Mikopo hii ni salama, haina akiba na ina riba nafuu na inapatikana katika kiganja chako cha mkono kupitia simu yako ya  mkononi. Hivyo tumewawezesha wateja wetu si kutuma pesa bure tu bali kupata pesa wakati wowote wanapohitaji.

ili kufurahia ofa hii ya Airtel Money mteja anatakiwa kupiga *150*60# na moja kwa moja utakuwa umeunganishwa na orodha ya huduma za Airtel Money na utume pesa sehemu yoyote  BURE”. Ofa hii itadumu kwa muda wa mwenzi mmoja.

DK. SHEIN ATOA VIFAA VYA MCHEZO WA RIADHA LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiwapa mawaidha yake mafupi viongozi wa mchezo wa Riadha walipofika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo katika hafla ya kuwakabidhi vifaa alivyoviandaa kwa Mchezo huo katika Wilaya kumi za Unguja na Pemba katika mpango wake wa kuimarisha na kuupa nguvu mchezo huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi vifaa vya Riadha Katibu wa mchezo huo Wilaya ya Magharibi Unguja Othman Ali wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali vya Riadha katika Wilaya ya kumi za Unguja na Pemba leo Ikulu Mjini Unguja.

Viewing all 110079 articles
Browse latest View live




Latest Images