Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

KIOTA KIPYA CHA MARAHA CHA UEFA GOO NIGHT CLUB KUZINDULIWA MKESHA WA KRISMAS

$
0
0
3Kiwanja kipya cha maraha Uefa Goo Night Club kinatarajiwa kuzinduliwa mkesha wa sikukuu ya Krismas jijini Dar es salaam Kiwanja hiki ni cha Kisasa kiko maeneo ya Ukonga Mombasa Barabara ya kuelekea Moshi Baa Karibu na njia panda ya Mahitamita 200 kutoka barabara kuu iendayo Pugu, siku ya mkesha wa Krismas burudani kibao zimeandaliwa na na kiko katika hatua za mwisho mwisho kukamilisha kila kitu ili kuwapa burudani wateja wake ikiwa ni pamoja na Ligi mbalimbali za ulaya, muziki wa kisasa kama vile Bongofleva na muziki wa zamani na vyakula mbalimbali vitapatikana
12Hizi ni baadhi ya picha zinazoonyesha jengo kwa nje na maendeleo ya kukamilisha ujenzi kwa ndani kwenye klabu hiyo ambao umefikia asilimia 99 kabla ya kufunguliwa mkesha wa Krismas.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda awasili Qatar kwa ziara ya kikazi

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Watanzania watanufaika na kipato na maarifa ya teknolojia ya kisasa kutokana na ajira ambazo watapata katika nchi ya Qatar baada ya mkataba kusainiwa hivi karibuni. 
 Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Desemba 20, 2014) jijini Doha, Qatar wakati akizumgumza na waandishi wa habari ili kuwapa taarifa fupi juu ya mambo yaliyojiri kwenye mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Abdulla Nasser Al Thani. 
 Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika ofisini kwa Sheikh Abdulla, Waziri Mkuu Pinda amesema wamekubaliana kutoa ajira kwa Watanzania kwa sababu nchi hii inahitaji wafanyakazi wengi kwenye sekta mbalimbali na raia wake ni wachache. 
 “Hivi sasa wapo Watanzania wanaofanya kazi hapa lakini ni wachache mno. Mazungumzo yalishaanza siku za nyuma. Tukisaini mkataba katika muda mfupi ujao, tutajua ni idadi gani wanahitajika na wanaweza kuja kila baada ya muda gani,” alifafanua Waziri Mkuu. 
 “Hapa Qatar kuna uwekezaji mkubwa umefanyika, kwa hiyo wanahitaji watu wa kufanya kazi... kwenye mahoteli, viwandani, na kikubwa hapa ninachokiona watu wetu watapata kipato lakini pia watapata ujuzi kwa maana ya maarifa yanayoendana teknolojia ya kisasa,” aliongeza. Akeleza mambo mengine ambayo wamekubalina kushirkiana kama nchi rafiki, Waziri Mkuu alisema kuna mambo makuu manne likiwemo hilo la ajira. 
“La kwanza ni Kilimo. Hapa Qatar ni jangwa kila mahali. Wamekubali kuja kuwekeza kwenye kilimo, ufugaji na uvuvi kwa sababu sisi tuko karibu nao zaidi kuliko Marekani au Brazil.
“Wanaweza kupata mchele, matunda, nyama kwa maana ya machinjio na viwanda vya kusindika nyama lakini pia katika uvuvi wa samaki. Tunayo bahari ila mitaji yetu ni midogo. Kwa hiyo wamekubali kuangalia eneo hilo pia,” alisema. 
 Alisema eneo la pili ni la gesi na mafuta. “Wamekubali kutusaidia utaalmu ili tushirikiane nao katika namna kutumia gesi kwenye ngazi ya chini hasa viwanda kwa sababu wenzetu wana uzoefu wa muda mrefu. Hata kwenye mafuta wameonyesha kuwa wako tayari,” alisema. 
Eneoa la tatu alilitaja kuwa ni kutoa fursa ya ajira kwa Watanzania na la nne ni TEHAMA. 
“Hawa wenzetu wamechanganya TEHAMA na sayansi na sasa wana Jiji la Sayansi na Teknolojia. Chini ya makubaliano tutakayofikia, watu wetu watakuja kujifunza masuala ya gesi na mafuta.” Alisema wamekubaliana na Sheikh Abdulla al Thani kuunda timu ya pamoja baina ya nchi zao ili ifanye kazi ya kuainisha ni maeneo gani wanataka waanze nayo kwanza kulingana na mahitaji. “Nimemuahidi nikifika nyumbani nitaandika barua ili mchakato wa kuunda timu uanze rasmi,” alisema. 
 Mchana huu, Waziri Mkuu Pinda atakuwa na mazungumzo ya Kiserikali na Mawaziri wa Kazi na Ustawi wa Jamii; Uchukuzi; Miundombinu na Uwekezaji wa Qatar. Naibu Mawaziri atakaokutana nao ni wa Uchumi na wa Nishati. 
 Jioni Waziri Mkuu amepangiwa kukutana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Qatar (Qatar Business Community), wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Qatar (Chamber of Commerce of the State of Qatar) na pia atakutana na Watanzania waishio Qatar. 
Kesho (jumatatu, Desemba 22, 2014) atatembelea Mamlaka ya Bandari ya Qatar na makao makuu ya kampuni ya uchimbaji gesi ya Qatar. 
 Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kimani; Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Maalim; Naibu Waziri wa Nishati, Bw. Charles Kitwanga; Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Godfrey Zambi. 
 Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, wabunge wawili Bi. Amina Makilagi na Bw. Aeshy Hilali, Dk. Gideon Kaunda wa TPSF na Bw. Shigela Malocha kutoka TPDC.
 IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU,
 DAR ES SALAAM. 
JUMAPILI, DESEMBA 21, 2014
 Waziri Mkuu Mhe.  Mizengo Pinda akiwa na Mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Abdullah Nasser Al Thani baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu wa Qatar  iliyopo Doha kwa mazungumzo ya kiserikali akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo leo. 
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda  akiongozwa na Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh  Abdullah Nasser Al Thani  kwenda  kwenye chumba  cha mikutano  baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu huyo  iliyopo Doha  kwa mazungumzo ya kiserikali akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo leo
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na Waziri Mkuu wa Qatar,  Sheikh Abdullah  Nasser Al Thani kwenye Ofisi ya  Waziri Mkuu huyo iliyopo Doha leo
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Titus Kamani (kulia) akizugumza na Waziri wa Mazingira wa Qatar, Ahmed bin Amir Al Humaidi , kwenye Hoteli ya Sheraton iliyopo Doha nchini Qatar leo Desemba 21, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Dkt. Bilal kuzindua majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria Tanzania kesho Jumatatu

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (The Law School of Tanzania) itakayofanyika kesho Jumatatu, tarehe 22 Disemba, 2014 jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa toka Wizara ya Sheria na Katiba, hafla hiyo itafanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi – saa 6:00 mchana katika eneo lililopo nyuma ya Jengo la Mawasiliano (Mawasiliano Towers), barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam yalipojengwa majengo hayo. Aidha, majengo haya yapo karibu kabisa na kituo kipya cha daladala cha Ubungo. 

Majengo yatakayozinduliwa ni Mahakama ya Mafunzo (Teaching Court); Vyumba vya Madarasa (Lecture Theatres); Maktaba (Library); Jengo la Utawala (Administration Block); Mgahawa (Cafeteria); na Nyumba za Watumishi (Staff Quarters).
 Pamoja na Makamu wa Rais, viongozi wengine watakaohudhuria ni Mawaziri, Majaji, Makatibu Wakuu, Mawakili, Wabunge, Wahadhiri na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria. 
Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania ilianzishwa na Sheria ya Bunge (Sura 425) mwaka 2007 kufuatia jitihada na mapendekezo ya muda ya muda mrefu ya Tume na Kamati mbalimbali zilizofanya utafiti katika sekta ya sheria nchini na kuona umuhimu wa kuwa na chuo cha kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria ili kuongeza ujuzi na stadi baada ya kupata mafunzo ya nadharia katika vyuo vikuu.

 Ujenzi huo wa majengo ya kudumu ya Taasisi umeigharibu Serikali zaidi ya Tshs 16.1 bilioni na ulianza mwezi Oktoba, 2010 na kukamilika mwezi Juni, 2013. Ujenzi ulifanywa na Kampuni ya BECG (Beijing Engineering Construction Group) kutoka China na ulisimamiwa na kampuni ya Co-Architecture yenye makao makuu yake hapa nchini. Kampuni hizi ndizo zilizoshinda zabuni za kazi zao.

Wanahabari kutoka vyombo vyote mnakaribishwa katika hafla hiyo.

sherehe ya kuwakaribisha wanafuzi wapya Watanzania huko Wuhan, China

$
0
0
 Baadhi ya wanafunzi wapya waliohudhuria sherehe hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja. 
 Baadhi ya wadau wa China University of Geosciences (DIDA). Kutoaka kushoto ni Bwana Saiboko, Yazidi, Masanja na Baraka.
 Baadhi ya wadau wakiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyekiti wa WUTASA bwana Thomas Mtaki (wa tatu kutoka kushoto).
 Katibu wa WUTASA bwana Mkoko akijaziwa mapochopocho.

 Baadhi ya wadau waliohudhuria.
 Mambo ya mduara.


Martin Skrtel awatoa nishai arsenal dakika za lala salama leo

$
0
0
Na Sultani Kipingo 
Goli la kusawazisha lililofungwa kwa kichwa na Martin Skrtel (pichani) dakika saba ndani ya muda wa nyongeza leo umewapa Liverpool ushindi waliostahili dhidi ya Arsenal katika uwanja wao wa nyumbani wa Anfield. 

Refa Michael Oliver aliongeza dakika tisa kufuatia mpira kusimama kwa muda mrefu baada ya Skrtel kuumizwa na kupatiwa huduma ya kwanza baada ya kugongana kwa bahati mbaya na Olivier Giroud wa Arsenal. 

Giroud alionekana tayari kaipaisha Arsenal kuelekea kwenye kulipiza kisasi cha kupigwa bao 5-1 hapo hapo Anfield msimu uliopita baada ya kufunga bao la kuongoza, baada ya Mathieu Debuchy kusawazisha sekunde chache kufuatia bao la Liverpool la kuongoza lililofungwa na Philippe Coutinho dakika moja kabla ya mapumziko. 
Lakini Skrtel, akiwa amefungwa bandeji kubwa kichwani huku Liverpool wakiwa watu 10 kufuatia mchezaji wa akiba Fabio Borini kutolewa nje kwa mchezo mbaya, alipaa hewani na kuweka kimiani mpira wa kona uliopigwa na Adam Lallan dakika ya 97 na kumpita kipa Wojciech Szczesny mbele ya mashabiki maarufu wa Bwawa la Maini - The Kop.


Chuo Kikuu cha Nelson Mandela jijini Arusha chaingia mkataba na kampuni ya Huawei Tanzania

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya HUAWEI Tanzania, Peter Jiang(Kushoto) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Arusha, Profesa Lughano Kusiluka, wakisaini mkataba wa Shilingi Milioni 51 kama msaada wa kuchangia utafiti wa matatizo mbalimbali ya jamii nchini zilizotolewa na Kampuni hiyo mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya HUAWEI Tanzania, Peter Jiang(Kushoto) akimkabidhi mkataba, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Arusha, Profesa Lughano Kusiluka mara baada ya kusainishana wa Shilingi Milioni 51 kama msaada wa kuchangia utafiti wa matatizo mbalimbali ya jamii nchini zilizotolewa na Kampuni ya HUAWEI mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya HUAWEI Tanzania, Peter Jiang (Kushoto) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Arusha, Profesa Lughano Kusiluka, wakiteta jambo mara baada ya kusainishana mkataba wa Shilingi Milioni 51 kama msaada wa kuchangia utafiti wa matatizo mbalimbali ya jamii nchini zilizotolewa na Kampuni ya HUAWEI Nchini mwishoni mwa wiki.

CHUO Kikuu Cha Nelson Mandela Sayansi na Teknolojia (NM-AIST) kimesaini makubaliano ya kiasi dola za kimarekani 30,000 sawa na kiasi cha shilingi hamsini na moja milioni kutoka kampuni ya Huawei Tanzania ikiwa ni katika malengo mahususi ya kuwasaidia wanafunzi wa shahada ya uzamili katika kufanya tafiti kwenye Nyanja za teknolojia na habari (TEKNOHAMA).

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo jijini Arusha mwishoni mwa wiki, Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Lughano Kusiluka amesema kuwa huu ni mwaka wa pili wa makubaliano na Huawei ya kukisaidia chuo kiasi cha dola 30,000 kila mwaka kwa muda wa miaka mitatu katika mikakati ya kuwainua wanafunzi wa Teknohama kwenye tafiti.

Profesa Kusiluka aliongezea kuwa msaada huo siyo tu utakisaidia chuo na wanafunzi kuweza kuisadia nchi yetu ya Tanzania katika kupiga hatua za kiuchumi na maendeleo kupitia sekta ya mawasiliano na habari.

“Kama mliovyomsikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akihutubia wahitimu, amesisitiza kuwa tafiti za kisayansi ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa taifa lolote lile Duniani, hivyo msaada huu kutoka Huawei utaleta chachu kubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi,” alisema Aliongezea: “Kwa niaba ya Uongozi wa Chuo, tunaishukuru sana kampuni ya Huawei Tanzania kwa mchango wake ambao kwa kiasi kikubwa umefanikisha sana matokeo ya wahitimu hawa tulio nao leo.

Huawei wamejitolea kuchangia utafiti kwa miaka mitatu na huu ni mwaka wa pili, tunawaomba waendelee kuwa nasi hata baada ya mwaka wa tatu wa makubaliano”

Akizungumza kwa niaba ya wanavyuo wenzake waliofaidika, Michael Mollel alisema: “Binafsi natoa shukrani zangu za dhati kwa Huawei Tanzania kwa mchango huu, mimi nilifanya utafiti wangu katika jiji la Dar es Salaam, ilinichukua miezi mitatu kukamilika, na kwa gharama zilivyo katika jiji hilo, nimgekuwa katika hali ngumu sana na hata kushindwa kumaliza utafiti kama siyo kwa msaada kutoka Huawei” Mollel aliongezea kuwa mafanikio yake hadi kufikia kutunukiwa shahada ya uzamili yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na msaada huo wa Huawei waliotoa katika chuo cha NM-AIST.

Kampuni ya Huawei Tanzania mwishoni mwa wiki ilishuhudia mafanikio makubwa ya mpango wake wa kuchangia utafiti kwa wanachuo wa shahada ya uzamili katika Taasisi ya Sayansi na Technolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) ya Jijini Arusha.

NM-AIST imefanya mahafali yake ya pili ambapo wahitimu wa shahada ya Uzamili walikuwa 93 na uzamivu walikuwa 13, ambayo ni asilimia 95 na karibu asilimia 50 ya jumla ya wadahiliwa wa makundi haya.

Wahitimu wa shahada ya uzamili wa kike ni asilimia 33 na wa shahada ya uzamivu ni asilimia 25. Mahafali hayo yalihudhuliwa na Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dr Mohamed Gharib Bilal pamoja na waziri wa Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa.

HERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA KUTOKA FLAVIANA MATATA FOUNDATION

Rais Kikwete azindua mradi wa ujenzi Nyumba za maafisa wa jeshi

$
0
0
Amiri Jehi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.Hussein Ally Mwinyi(kushoto) Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Adolf Mwamunyange wakiweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa nyumba za maafisa wa jeshi huko Monduli mkoani Arusha jana.Katika mradi huo jumla ya nyumba elfu kumi zinatarajiwa kujenga katika kambi mbalimbali za jeshi nchini
Picha na Freddy Maro


ngoma azipendazo ankal - special request from Eliud Pemba

$
0
0
Kolumba ft Wetare - Mimi Na Wewe

KITUO CHA RADIO 5 WAFANYA KAMPENI YA USHINDI KWA WATOTO YATIMA

$
0
0
Kampuni Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  imeeanda tamasha kwa watoto yatima wanaoishi katika vituo lenye jina "Kampeni ya USHINDI"linalowashirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Arusha

Mkurugenzi wa kituo hicho  Robert Francis anachukua jukumu la kuwasihi jamii kwa ujumla kuwa na tabia ya kuwakumbuka mayatima hasa kipindi hichi cha sikukuu ili nao wasijione kutengwa

Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo alisema kuwa kila mtoto anastahili kuwa na furaha na baadhi yao ni wale wenye uwezo mdogo ni vyema kuwakumbuka na tusiwatenge na tukifanya hivi watajiskia vizuri

Meneja masoko wa Redio 5 Sarah Keiya ametoa shukrani kwa wadau wote walioshirikiana na kituo hicho kwa kuwezesha kampeni hiyo kufanikiwa,wadau wakubwa walioshiriki ni Redio 5,Pepsi,Fifis bakery,Arusha meat,Skytel,Monaban,Vibration duo,Brundful company,World garden.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog).
SAM_0388Wafanyakazi wa kituo cha redio 5 Arusha wakikabidhi misaada mbalimbali katika kampeni ya "USHINDI"inayoendeshwa na kituo hicho,misaada hiyo ilitolewa na wahisani mbalimbali kwaajili ya watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima Mkoani Arusha,katika Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo kushoto ni Sarah Keiya wakiwakabidhi watoto wa kituo cha kiwohede ndoo ya mafuta ya kupikia kwaajili ya sikukuya Krismass na mwaka mpya jijini hapa jana katika hotel ya world Garden
SAM_0393Wafanyakazi wa kituo cha redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha kiwohede na huruma katika hotel ya world Garden iliyopo moshono jijini Arusha katika tam
SAM_0390Mkuu wa vipindi wa kituo hicho Mathew Philip akikabidhi moja ya msaada kwa shcha watoto huruma.

Article 24

MKUU WA WILAYA YA KIGOMA AKANUSHA VIONGOZI WA HALMASHAURI YA KIGOMA KULA PESA YA TASAF

$
0
0
Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma 
 MKUU Wa Wilaya ya Kigoma Mhe  Ramadhani Maneno amewataka wananchi wa Wilaya ya Kigoma kuacha kuwashutumu viongozi wa wilaya na Halmashauri kuwa wamekula pesa za TASAF shilingi milioni 183,539 zilizotolewa na serekali kwaajili ya kusaidia kaya maskini Wilayani humo. 
Mhe  Maneno amewaambia wanahabari ofisini kwake leo kuwa pesa iliyotolewa na TASAF kwa ajili ya kusaidia kaya maskini na zinazoishi katika mazingira magumu katika Wilaya ya Kigoma zilikuwa pesa za mitaa 39. 
"Mpaka sasa katika mitaa hiyo 39 wamefanikiwa kulipa mitaa 36 na bado mitaa 3 ambayo ilikuwa na dosari katika taarifa zake za uhakiki ndo maana zoezi la kulipa mitaa hiyo ilisimama kwanza na pesa zao zipo salama katika akaunti ya Halmashauri.
"Mpaka sasa kuna fikra tofauti kwa baadhi ya wananchi kuwa kuna baadhi ya viongozi wa serekali wa Wilaya ya Kigoma wamekula fedha hizo za mitaa hiyo mitatu.
 ''Kwa kweli mimi ninachosema hizo pesa milioni 183,539 hakuna mtu yeyote aliyekula zipo katika mikono salama kwenye akaunti ya Halmashauri na taratibu zitakapo kamilika zitalipwa kwenye hiyo mitaa mitatu ambayo bado haijalipwa''alisema 
Mkuu huyo wa wilaya  alisema kuwa watumishi wa umma wote waliojiandikisha katika zoezi hilo na kusababisha mkanganyiko katika zoezi hilo watachukuliwa hatua za kinidhamu za kisheria za utumishi wa umma 
 Naye Mkurugenzi wa uratibu wa TASAF kutoka makao makuu Bw. Alphone Kyariga alisema kuwa TASAF awamu ya tatu imetoa msaada wa fedha kwa kaya maskini Wilaya ya Kigoma jumla ya shilingi milioni 249,822,000 kwa mitaa 39 ambayo inakadiliwa kuwa na kaya maskini 18,738. Alisema kuwa pesa zinazosemwa kuwa zimeliwa na viongozi milioni 183,539 zilikuwa ni pesa zilizotakiwa kulipwa katika mitaa mitatu nayo ni Burega,Sokoine na Lake Tanganyika lakini ilishindikana kuzilipa kwasababu ya mapungufu yaliyojitokeza katika mitaa hiyo. 
Bw.  Kyariga alisema kuwa zoezi la uhakiki wa kaya maskini katika mitaa hiyo ambayo haijalipwa zoezi la uhakiki na uandikishwaji litafnyika upya na wale wanaostahili kulipwa fedha hizo watalipwa kwani fedha zipo.
 ''Walio kuwa wakipita na kuandikisha kaya maskini ndiyo ili ziweze kusaidiwa na fedha za TASAF ndiyo walioleta mkanganyiko huu na kusababisha mitaa hiyo mitatu kushindwa kulipwa kwa wakati na kuonekana dosari mbalimbali ikiwemo kuandikisha watu wasio maskini kama vile watumishi, kaya moja kuandikishwa zaidi ya mara moja''alisema Mkurugenzi huyo.
  Alisema lengo la TASAF kutoa msaada huo ni kuwasaidia watu wenye kipato cha chini kabisa lakini kuna baadhi ya wananchi wenye uwezo wa kujikimu na maisha wanatumia fursa hiyo kujipenyeza ili na wao wapate msaada na kufanya viongozi kushindwa kukamilisha zoezi hilo ipasavyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake (ambao hawapo pichani) kuhusu taarifa zilizoeenea kuwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma wamekula hela za TASAF awamu ya tatu shilingi milioni 183,539,kushoto kwake ni Mkurugenzi wa utaribu kutoka makao makuu ya TASAF Alphonce Kyaliga 

Airtel yawapatia kundi la walemavu mtaji na mafunzo ya biashara

$
0
0
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akikata utepe kama ishara ya kukabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu wenye ulemavu, wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), kwa ajili kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamari, katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi Buguruni Viziwi jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya na (kulia) ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Abubakar Rakesh na mnufaika wa kibanda hicho, Hebron Mwansele (kwenye baiskeli).
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akihutubia wakati wa hafla hiyo.
Sehemu wa wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye Ulemavu (HREDP), wakiwa katika hafla hiyo.

MIHIMILI MITATU ISIPOELEWANA NCHI HAIWEZI KUTAWALIKA - UTOUH

$
0
0
Na Bakari Issa,Dar es Salaam

ALIYEKUWA Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG),Ludovick Utouh amesema mihimili mitatu iwekewe mipaka na kuangalia isiingiliane katika utendaji wake wa kazi kuruhusu kwake kuingiliana ni kufanya serikali isitawalike.

Hayo amesema leo jijini Dar es Salaam katika kupokea tuzo ya uadilifu kutoka kwa Kampuni ya Dream  Success Enterprises kutokana na kutambua umuhimu wa utendaji wake wa kazi.

Alisema kuwa mihimili mitatu isipojua mipaka yake itawaweka wananchi washindwe kujua uwepo wa mihimili hiyo na kufanya nchi ishindwe kutawalika kutokaka na mihimili hiyo kuwa na mianya ya kutoafikiana katika utendaji..

Utouh alisema kuna vitu hataweza kusahau katika ofisi ya CAG moja ni fedha zilizochotwa katika akaunti za nje (EPA) pamoja na ripoti ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, David Jairo ambapo wabunge walishindwa kujua uhalali wa fedha zilizochangishwa  na Jairo na hakuna sheria yeyote iliyovunjwa.

“Tuzo hii nimepata lakini nimepita  katika kipindi ambacho jina la ufasadi limeweza kuzaliwa kutokana  na uchotaji wa fedha za EPA na kufanikisha zingine kuweza kurudi, nchi zingine huwa zinashindwa kabisa kurudisha fedha za namna hiyo”alisema Utouh.

Waziri Fenella afunga fainali Copa Coca Cola 2014

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara(MB) akikagua timu za Vijana waliochini ya miaka 15 kutoka Kinondoni na Dodoma ambazo zilishiriki hatua ya fainali katika mashindano ya Copa Coca Cola mwishoni mwa wikiendi katika uwanja wa Krume jijini Dar es Salaam. Ambapa katika fainali hizo kwa upande wanaume toimu kutoka Dodoma iliibuka bingwa wa mashindano hayo kwa kuichapa Kinondoni jumla ya magoli 4 -0, wakati kwa upande wa wanawake Kinondoni ilinyakua ubingwa kuifunga Ilala kwa mikwaju ya penati 2 – 1 baada ya dakika tisni kumaliza kwa sare ya mbili mbili.
Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wanawake kutoka Kinondoni akifunga penati wakati wa fainali za Copa Coca Cola 2014 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mapema wikiendi hii, Kinondoni ilinyakua ubingwa kwa kuifunga Ilala mikwaju ya penati 2 – 1 baada ya dakika tisni kumaliza kwa sare ya mbili mbili.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) (wa tatu kutoka kushoto) akifurahia mara baada ya kukabidhi zawadi ya mchezaji bora wa kike katika mashindano ya Copa Coca Cola kwa Golikipa wa timu ya Kinondoni Zubeda Mohamed (15). Wakwanza kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Coca Cola Bw. Godfrey Njowoka, Rais wa TFF Jamal Malinzi na nyuma ya waziri anayecheka ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo.
Wachezaji wa timu ya Dodoma wakifurahia baada ya kukabidhiwa zawadi zao za ubingwa wa michuano ya Copa Coca Cola baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano hayo kwa mwaka 2014 kwa mashindano hayo kwa kuichapa Kinondoni jumla ya magoli 4 -0, wakati kwa upande wa wanawake Kinondoni ilinyakua ubingwa kuifunga Ilala kwa mikwaju ya penati 2 – 1 baada ya dakika tisni kumaliza kwa sare ya mbili mbili. Picha na Frank Shija, WHVUM.

ADHA YA USAFIRI JIJINI DAR

$
0
0
 Abiria katika moja ya Daladala linalofanya safari zake kati ya Mbezi - Posta wakigombea kuingia kwenye gari hilo kupitia mlango wa Dereva,baada ya Kondakta wa Basi hilo kutofungua mlango kutokana na uwingi wa abiria hao.tukio hili limetokea jioni hii katika kituo cha Daladala cha Posta Mpya,jijini Dar es Salaam.
 Mara Dereva akashukia mlango wa abiria na kuja kuwazuia abiria kupanda basi hilo kupitia mlango wake,hapo napo ilikuwa mbinde ile mbaya.
 Mara akafanikiwa kuwadhibiti na kuwataka abiria wote kwenda kwenye mlango husika.

Mhe .Ummy Mwalimu Aendesha Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Wasichana wa Wilaya ya Muheza - Tanga

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Mhe Ummy Mwalimu kupitia Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake wa Mkoa wa Tanga (TAWODE) ameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wasichana wa Wilaya ya Muheza, Mkoani Tanga wenye umri kati ya miaka 10 - 24. Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wasichana hao kujitambua na kujithamini katika masuala ya afya ya uzazi ili kujikinga na mimba na ndoa za utotoni na maambukizi ya VVU/UKIMWI.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Mhe Ummy Mwalimu akifungua mafunzo kwa wasichana wa Wilaya ya Muheza juu ya kujitambua na kujithamini katika masuala ya Afya ya uzazi. Mafunzo hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Muheza.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Mhe Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kujitambua na kujithamini Wilayani Muheza mwishoni mwa wiki.
Wasichana wa Wilaya ya Muheza wakifanya majadiliano na mawasilisho katika vikundi juu ya changamoto wanazokumbana nazo katika kipindi cha ujana.

Magolikipa wawapa kichapo cha Mbwa mwizi Waandishi!

$
0
0
TIMU ya magolikipa inayoongozwa na mlinda mlango  Ivo Mapunda wa Simba, Shaaban Kado wa Coastal Union na Salehe Malande wa Ndanda juzi waliiongoza timu yao ya Chama Cha Magolikipa Tanzania (TAGA FC) kuiadhibu ile ya waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa FC) magoli 3-0 kwenye mchezo maalum wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika kwenye uwanja wa Karume kabla ya kuahamishiwa uwanja wa bora kutokana na ?Mizengwe? ya dakika za mwisho  ya wamiliki wa uwanja huo.

Timu zote zilianza mchezo huo kwa kasi na kukosa nafasi kadhaa za wazi. TAGA ndio ilikuwa ya kwanza kulifikia lango la Taswa FC ambayo ilizindua jezi zake kwa mara ya kwanza zilizotolewa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), hata hivyo shuti la mshambuliaji, Ivo Mapunda likatoka nje.

Makipa walikuwa katika nafasi nzuri ya kufunga tena katika dakika ya sita ya mchezo, hata hivyo penati ya Shaaban Kado ikipanguliwa na kipa wa Taswa, Ahmed Famau.

Taswa FC iliibuka katika dakika ya nane ya mchezo na Zahoro Mlanzi alikosa bao la wazi akiwa na kipa wa TAGA FC, Fatuma Omari ambaye pia alifanya kazi ya ziada kuokoa mipira miwili ya kona iliyopigwa na Majuto Omary ambayo ilielekea golini. 

Licha ya kutofanya mazoezi kila siku kulinganisha na timu ya makipa, wachezaji wa Taswa, Ali Mkongwe, Martin, Majuto, Ibrahim Masoud,  Zahoro Mlanzi, Shafii Dauda, Wilbert Molandi, Sweetbert Lukonge, Muhidini Sufiani, Salum Jaba, Juma Ramadhani na Julius Kihampa walionyesha uwezo mkubwa katika mchezo huo .
Mapunda aliipatia TAGA goli la kuongoza dakika ya 14 kufuatia krosi safi ya Saleh Malande aliecheza vizuri na Juma Kaseja na Ali Mustapha (Barthez)

Bao la pili la makipa lilifungwa na Shaaban Kado baada ya kazi nzuri ya Deogratius Munishi 'Dida' na Malande kuhitimisha ushindi wa TAGA dakika ya 86.

Rais wa makipa hao, Alex Ndembeka alisema kuwa wamefarijika sana mchezo huo ambao umetumika rasmi kuzindua chama chao ambacho lengo lake kubwa ni kuendeleza fani hiyo kwa kuvumbua vipaji na kuondoa fikra za kuwa ?magolikipa? hawapendani.

"Tunawapongeza waandishi kwa kukubali wito wetu na kufanikisha kuzindua chama hiki, nadhani umeona jinsi ilivyo kwa makipa wetu kucheza pamoja, kufurahi na kuondoa mtazamo hasi wa kuwa makipa hawapendani", alisema Ndembeka.

DKT. SHEIN KUWA MGENI RASMI MASHINDANO YA KITAIFA YA RIADHA ZANZIBAR

$
0
0
Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika mashindano ya Kitaifa ya Riadha ya wilaya ambayo yanatarajiwa kufanyika katika kiwanja cha Amaani Disemba 26-27 mwaka huu.

Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Rais Shein kwa lengo la kukuza sekta ya michezo nchini yametayarishwa na Baraza la michezo la Taifa Zanzibar (BMTZ) kwa kushirikiana na chama cha Riadha (ZAAA) Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa baraza la michezo Bi Sharifa Khamis katika ukumbi wa wizara ya habari , utamaduni, utalii na michezo huko kikwajuni wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema mashindano hayo yatakayozishirikisha Wilaya zote 10 za Unguja na Pemba yatajumuisha wanariadha 250 ambapo michezo yote ya riadha ikiwemo kukimbia masafa ya mita 100 , 200, 400, na 1500 kwa wanawake na wanaume itafanyika. Aidha ameongeza kuwa jumla ya vikundi 12 kutoka Kenya , Uganda na Tanzania Bara vimealikwa kushiriki Mashindano hayo.

Amefahamisha kuwa sambamba na Riadha pia kutakuwa na michezo ya kurusha mkuki , tufe, ,na kisahani. Amebainisha kuwa Washiriki wa mashindano hayo watapatiwa huduma zote za michezo bure ikiwemo malazi , mavazi ya michezo , chakula, usafiri na zawadi zote za washindi za vikombe , medali na fedha taslim.

“Lengo kuu la mashindano hayo ni kuinua mchezo wa riadha Zanzibar kuanzia vijijini , maskulini na maeneo mengine mbali mbali kwa nia ya kutafuta vipaji vya wanariadha kutoka katika sehemu hizo ili kuviendeleza vipaji hivyo “ alisema Bi Sharifa.

Amesema dhamira ya Rais wa Zanzibar ni kuona Zanzibar inarejesha hadhi yake ya asili ya ubingwa katika michezo tofauti ambayo amesema sifa hiyo imepotea kwa kipindi kirefu ikilinganishwa katika miaka 70.

Mashindano hayo nisehemu ya utekelezaji wa sera tya michezo Zanzibar , ambayo inasisitiza kuwa vyama vyote vya michezo Zanzibar vifanye jitihada za makusudi za kuinua michezo ili nchi iweze kupiga hatua kubwa katika michezo.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Bi Sharifa Khamis akizungumza na Wanahabari kuhusu Mashindano ya kitaifa ya Riadha yatakayofanyika Disemba 26-27 mwaka huu katika Ukumbi wa wizara ya habari Kikwajuni mjini Zanzibar. Rais Shein anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi wa Mashindano hayo. Picha na Makame Mshenga.

zinauzwa hapa

Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images