Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 680 | 681 | (Page 682) | 683 | 684 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Na Sultani Kipingo

  Inasemekana kila jina lina asili yake na maana pia. Hata hilo jina lako ulipewa kwa sababu, na lina asili yake. Kama si la kutoka katika Biblia ama Quran, basi ni la kimila lenye kumaanisha jambo, kama vile siku, tukio, mahali ama hata shida au raha aliyopata mama wakati wa uzazi wako.

  Jiji la Dar es salaam  zamani liliitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyelipa jiji hili jina "Dar es Salaam" linalotokana na lugha ya Kiarabu  (Dār as-Salām) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili yanayofanana katika Kiarabu yaani "dar" (=nyumba) na "bandar" (=bandari).

  Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo pana ya mto Kurasini. Kuanzia 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala. Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu 1904 ziliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara kuwa koloni ya Tanganyika chini ya Uingereza.

  Bado kuna mabishano ya ni nini hasa asili ya jina Africa. Wengine wanadai linatokana na neno la Kigiriki la APHRIKE, lililomaanisha kusikokuwa na baridi, ama la Kilatini APRICA, lenye kumaanisha nchi yenye jua daima.


   Wengine wanasema neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Waroma wa Kale. Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali eneo katika jimbo la Carthage ama Tunisia ya leo tu. Asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile.

  Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini ya Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).

  Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara. Jina la "Afrika" limekuwa kawaida kuanzia karne ya 16 BK.

  Misri ya wakati huo ilikuwa inachukuliwa kama sehemu ya bara la Asia,na alikuwa Mwanajiografia aitwaye Ptolemy (85-165A AD) ambaye aliigawa Afrika na Asia na Ulaya kwa kuchora ramani inayoonesha Suez na Bahari Nyekundu kuwa ndio mpaka baina ya Asia na Afrika.





  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (aliyevaa miwani) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi  wa timu za mpira wa miguu za vijana wa Tanzania  Ubeligiji baada ya kuwakabidhi jezi za mpira wa miguu. Balozi Kamala amewashukuru vijana hao kutangaza Tanzania vizuri na kudumisha umoja na ushirikiano miongoni mwao.

  0 0


  0 0


  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa walipohudhuria sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli mkoani Arusha leo.  
   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa akiongea na  maofisa waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwemo na Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange (kushoto) kwenye sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli, mkoani Arusha leo
   Mkuu wa Majeshi Jenerali  Davis Mwamunyange akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa alipowasili kwenye sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa cheo cha Luteni Usu, iliyofanyika katika chuo cha jeshi hilo Monduli. Picha na Aboubakar Liongo.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambae ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)  akitoa  hutuba yake katika mahfali ya 10 ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Chuo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja,
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambae ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) akimkabidhi zawadi Hamad Abdalla Nassor akiwa ni miongoni mwa wanafunzi bora waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao wakati wa mahfali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Chuo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambae ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) akimkabidhi zawadi Najat Zahoro Said akiwa ni miongoni mwa wanafunzi bora waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao wakati wa mahfali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Chuo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
    Mwanaidi Ali Faki na Ngano Suleiman Faki mbele ni wanafunzi waliohitimu mafunzo ya fani ya Kiswahili na Elimu wakiwa katika mahfali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Tifa cha Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika leo katika viwanja vya kampasiya Chuo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akiwa mgeni rasmiRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambae ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)
  Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya Sayansi na Elimu katika chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakiwa katikamahfali ya 10 yaliyofayika chuoni hapo Kampasi ya Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Ungaja  akiwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambae ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar(SUZA). Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na John Gagarini, Chalinze 
  MBUNGE wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete Ijumaa alifanyiwa sherehe za kijadi za kabila la Kikwere kijijini kwao Msoga, kwa mujibu wa mila za hapo.
  Sherehe hizo,  ambazo ziliendana na kukabidhiwa vitu mbalimbali vya kijadi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, ni jadi ya Wakwere ambapo mtu baada ya kupata uongozi hutambikiwa na kukaribishwa rasmi kwenye kundi la wazee wa kijiji. 
  Baadhi ya vitu alivyoakabidhiwa na mzee wa kabila hilo Zaidi Rufunga ni pamoja na kitanda cha kamba, msuli, kigoda na kinu pamoja na vitu mbalimbali. Sherehe hizo za kijadi ziliamabatana na ngoma ya Kikwere na ulaji wa chakula kiitwacho Bambiko ambacho hutumiwa na kabila hilo.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete kushoto akipata maelekezo kabla ya kuanza kula chakula cha kabila la Kikwere kiitwacho Bambiko wakati wa sherehe za kijadi za  kumkaribisha katika kundi la wazee kwenye kijiji cha Msoga zilizofanyika juzi.
  Mzee Zaidi Rufunga kulia akimkabidhi vyungu mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete wakati wa sherehe za jadi za kumkaribisha nyumbani zilizofanyika juzi kijiji cha Msoga. 
  Kulia mzee Zaidi Rufunga akimuelekeza jambo kabla ya kula chakula cha jadi cha kabila la Wakwere kiitwacho Bambiko wakati wa sherehe za jadi za kumkaribisha nyumbani Ridhiwani Kikwete zilizofanyika juzi kijijini hapo.
  Baadhi ya akina mama waliohudhuria sherehe za jadi za kumkaribisha mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani KIkwete zilizofanyika Ijumaa kijijini Msoga.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kushoto na katikati diwani wa kata ya Msoga Mohamed Mzimba na baadhi ya wageni wakila chakula cha jadi kiitwacho Bambiko mara baada ya sherehe za jadi za kumkaribisha nyumbani kwenye Kijiji cha Msoga 

  0 0

   Ankal ana T-Shirt kibao anataka kugawa katika msimu huu wa sikukuu. Ila anaomba kwanza umwekeze taswira hii imechukuliwaje, na kwa ataeweza hata kutaja kamera ilotumika atapewa T-Shirt mbili....


  0 0

   Hapa ni mwisho wa lami katika barabara kuu ya kutoka Kondoa  mkoani Dodoma kuelekea Babati mkoani Manyara. Tayari ujenzi wa barabara ya lami kutoka Kondoa hadi hapa mwisho wa lami umeshaanza.


  0 0
 • 12/20/14--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Ebenezer- Angela Chibalonza

  0 0

   Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza Luteni Usu Edwin Engelbert Kessy wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni maafisa wa jeshi baada kuibuka mwanafunzi bora wakati wa mafunzo ya maafisa wa jeshi yaliyofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mjini Arusha
   Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza Luteni Usu Edwin Engelbert Kessy wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni maafisa wa jeshi baada kuibuka mwanafunzi bora wakati wa mafunzo ya maafisa wa jeshi yaliyofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mjini Arusha
  Rais Kikwete akitunuku Kamisheni maafisa wa jeshi katika chuo cha Jeshi huko Monduli Mkoani Arusha leo.Jumla ya maafisa 171 walitunukiwa kamisheni wakati wa hafla hiyo. Picha na Freddy Maro.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  (Jeshi la Magereza)
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, anawatangazia wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Jeshi la Magereza baada ya kufaulu mitihani ya usaili iliyofanyika kati ya tarehe 10 Desemba, 2014 hadi 17 Desemba, 2014 katika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam pamoja na wale wa Kidato cha Nne na Sita waliosailiwa kutoka Kambi mbalimbali za JKT.
  Wahusika wote wanatakiwa kuripoti Ofisi za Magereza za Mikoa husika ifikapo tarehe 30 Desemba, 2014 tayari kwa safari ya kwenda Chuo cha Mafunzo ya Awali kilichopo Kiwira Tukuyu Mkoani Mbeya. Mafunzo yatafunguliwa rasmi tarehe 8 Januari, 2015 hivyo mwisho wa kuripoti Chuoni ni tarehe 7 Januari, 2015. Yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa tarehe ya mwisho iliyotamkwa kwenye tangazo hili hatapokelewa na atarudishwa kwa gharama zake.

  Wahusika wanatakiwa 
  kuzingatia mambo yafuatayo:-

  i. Vyeti halisi vya masomo na kuzaliwa, vikiwa na nakala 5 za kila cheti,
  ii. Picha za rangi(pass-port size) 5 za hivi karibuni,
  iii. Fedha taslim Tzs.90,000/=,
  iv. Kalamu za wino, kalamu za risasi na madaftari ya kutosha,
  v. Chandarua cheupe cha duara ft 31/2, shuka nyeupe mbili, mto wenye foronya nyeupe zisizo na maua/maandishi,
  vi. Cheti cha Afya kutoka Hospitali ya Serikali, 
  vii. Nguo za kiraia za kutosha, sweta, raba (brown au nyeusi) na soksi, 
  viii. Kwa wale wenye kadi za bima za afya waje nazo, na
  ix. Kila mwanafunzi atajitegemea kwa nauli ya kwenda.

  Tangazo hili linapatikana kwenye Mbao za Matangazo zilizopo Bwalo Kuu la Magereza, tovuti ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.go.tz sanjari na blog ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.blogspot.com


  Imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza.

  J.C. Minja
  KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
  Bofya hapo chini kuona majina ya waliochaguliwa kwa mchanganuo ufuatao:-

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  MPAMBANO wa ngumi wa kufungua mwaka unatarajiwa kupigwa Ifakara mkoa wa Morogoro  kuhamasisha na kukuza mchezo wa masumbwi nchini. promota wa mpambano huo Hiari Bohari amesema kuwa kwa sasa anataka aendeleze mchezo wa masumbwi Ifakara kwa kuwa watu wapo na mchezo unapendwa.

  Alisema siku hiyo ya January 2. 2015 itakuwa ni siku ya kufungua mwaka kwa mpambano wa masumbwi kati ya Abdallah Kilima na Abdul Amwenye huku Saleh Makuka akipambanma na Said Chamaki

  Aliongezea pia  kutakuwa na mapambano mawili kwa ajili ya kuhamasisha wanawake waje washiriki katika michezi ya ngumi ambapo siku hiyo Aika Georger atapambana na Najma Ally.

  Bohari ameomba  wadau mbalimbali kutoa sapoti na kumuunga mkono katika harakati za kuinua mchezo wa masumbwi ili uweze kusonga mbele.

  0 0

  Kaka michuzi habari za jumapili. Pole na hongera kwa kazi nzuri unayofanya. kaka mimi ninaomba unisaidie kuweka hili jambo hadharani. Kuna mtu mwenye email adress yakimusi200@outlook.com. huyu mtu amekuwa akituma email kwa watu hasa walioko kwenye ndoa . anachofanya yeye anahack email za watu anaowataka na kuanza kuwatumia email kuwaambia kuwa wenza wao wanacheat. 
  Nashindwa kuelewa yeye lengo lake linakuwaga ni nini. nikupe kisa kimoja. mimi na mdogo wangu na mkewe tuna kampuni yetu na tunafanya kazi pamoja.mwezi wa nane akamtumia mdogo wangu meseji kuwa mkewe anamcheat anatembea na boss wake huko anakofanya kazi while kazi tunafanya wote pamoja. 
  But the way anavyomwongelea huyo wifi yangu ni kwamba inaonekana anamjua maana wifi yangu ni mjamzito akamwambia hiyo mimba itakuwa sio ya kwako maana kuna boss anatembea naye hapo anakofanya kazi. sasa tukashangaa kazi tunafanya wote information anazotoa mbona sio za kweli? mdogo wangu akaignore but akawa bado anaendelea kumtumie hizo emails.
  Last week akamtumia mume wa rafiki yangu email akamwambia mkewe anamcheat  eti  so awe mwangalifu sana. akamwambia anampenda ndio maana ameamua kumtumia huo ujumbe.

  Sasa kaka michuzi huyu mtu anakuwa ana lengo gani na watu na familia zao?au starehe yake inakuwa akiona ndoa imevunjika ? na hata ikivunjika yeye anafaidika nini? naamini huwa anawatumia watu wengi sana naomba uiweke hii hadharani ili watu wawe na tahadhari na huyu mtu  na kama hajaoa au kuolewa aingie kwenye ndoa apate experience ndio ajue cha kufanya ni nini sio anatumia watu email za kijinga namna hiyo.
  Ni matumaini yangu kaka uatiweka hii haraka.

  0 0

  Afisa Uhusiano mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (Kushoto), akipena mikono na Ummy Shaaban,  mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Buyuni II,  iliyoko Chanika, wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam,wakati akikabidhi msada wa madawati kwa ajili ya shule hiyo mwishoni mwa wiki. (Katikati ni mwalimu mkuu wa shule hiyo,  Rogather Palla. 
  Afisa Uhusiano mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Njaidi, (Kushoto), akitoa elimu kupitia vipeperushi kwa baadhi ya walimu wa shule hiyo.
   Wanafunzi wakibeba dawati kupeleka darasani.
   Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameketi kwenye madawati hayo.
   Afisa Uhusiano mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, akiwaelimisha wanafunzi hawa wa shule hiyo, kuhusu huduma mbalimbali  zitolwewazo na Mfuko huo  Wanafunzi wakishangili msada huo wa madawati
   Baadhi ya Wanafunzi wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa madawati hayo. 

  0 0

  Mshindi wa kwanza wa shindano la AppStar tabaka la wabunifu waliobobea Roman Mbwasi akielezea jambo wakati wa shughuli ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao iliyofanyika makao makuu ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki hii. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Abigail Ambweni, akimsikiliza kwa makini pamoja na mshindi wa kwanza katika tabaka la wabunifu chipukizi, George Machibya (kulia) Shindano hilo linaendeshwa na kampuni hiyo.
  Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Abigail Ambweni (kushoto) akimkabidhi zawadi ya pesa taslimu Tsh. milioni 2/- mshindi wa kwanza wa shindano la AppStar tabaka la wabunifu waliobobea ambao programu zao tayari zinatumiwa na watu zaidi ya 50,000 Roman Mbwasi (wa pili toka kushoto). Shindano hilo linaendeshwa na kampuni hiyo.
  Washindi wa shindano la AppStar wakionyesha zawadi zao za pesa taslimu walizokabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Abigail Ambweni (wa tatu toka kushoto) Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo mwishoni mwa wiki. Shindano hilo linaendeshwa na kampuni hiyo.


  0 0


  Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai,Mh. Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walipomtembelea ofisini kwake kumuaga leo.

  0 0


  KOCHA wa Yanga Hans Van Puljim (pichani chini kulia) amedai kusikikitshwa na mlinda mlango Juma Kaseja (juu kushoto) kuingia kwenye bifu na uongozi wa klabu hiyo wakati alimtegemea kuongoza wachezaji wenzake siku za nyuma akiinoa timu hiyo.



  Puljim ambaye alichukua nafasi ya Ernie Brandts mwaka jana kabla ya  kutimuliwa mara baada ya mechi ya Mtani Jembe mwaka jana ambapo Yanga ilinyukwa mabao 3-1 alimtumia Kaseja kuwa nahodha katika kikosi chake lakini leo amesema anasikia uchungu kumkosa mlinda mlango huyo.



  "Nimefika hapa, hayupo Juma, hayupo Didier Kavumbagu, hayupo Hamisi Kiiza, kibinadamu kama watu ulizoea kufanya nao kazi ukasikia uongozi umewasaspendi, sitaki kujua sababu, wala sitaki kuingia masuala yao, lakini roho inaniuma, ni kama mwanafamilia akifariki, mtalia sana, roho zitauma, mtasikitika lakini mwisho wa siku maisha ni lazima yaendelee, "alisema Puljim ambaye unaweza kumwita "Kocha wa Mtani Jembe" kwani amechukua nafasi ya Mbrazil Marcio Maximo ambaye pia  amefungashiwa virago baada ya Yanga kuchukua kichapo cha mabao 2-0 katika mechi ya Mtani Jembe iliyofanyika Desemba 13 kwenye uwanja wa Taifa.
  Kavumbagu
  Puljim alisema "Nawaheshimu wachezaji waliopo, nimeshaongea nao jana (Jumamosi) ikiwa ni mazoezi yangu ya  kwanza kufanya nao. Kikubwa nimewambia wasahau yaliyopita, wasisikitike kuondoka kwa wenzao wasisikitike kuondoka kwa kocha. Yaliyopita yamepita sasa tuanze maisha mapya, tukiwa na lengo moja la kuifanya Yanga iwe juu.

  "Kikubwa nilichowataka ni kujitambua, Yanga ni klabu kubwa. Kama mchezaji anapata nafasi basi lazima ajue jukumu lake. Mkakati wangu ni kuhakikisha Yanga inacheza soka la kuvutia na mpangilio mzuri. Najua wote ni binadamu na kuna makosa ya kibinadamu hutokea lakini ninawataka kila mmoja acheze kiushindani na morali ya hali ya juu.

  "Kazi yangu kama kocha ni kuwajengea wachezaji morali, naipenda timu yangu, tunatakiwa tushirikiane viongozi watimize wajibu wao, mimi kama kocha nitimieze wajibu wangu, na wachezaji pia watimize wajibu wao wacheze kwa kutumia akili na soka la kuvutia.
  Kiiza
  Hata hivyo, Pluljim aligoma kuweka wazi fomesheni atakayotumia kuhakikisha Yanga inachukua taji la Ligi Kuu msimu huu kwa kile alichodai kuwa fomesheni sio inayofanya kushinda mchezo.
  "Ushirikiano na kujituma ndio kunakowezesha kushinda mchezo, sina hofu na wachezaji, nina hofu na mbinu zangu nitakazowapa kama watazielewa na kuzitekeleza, kuna wachezaji wapya ambao siwafahamu miezi minne ya michache kusema naweza kuiweka Yanga kwenye kiwango cha juu, litawezekana kukiwa na ushirikiano wa kutosha."alisema
  Puljim amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuionoa timu hiyo hata hivyo amedai kuwa Yanga ni nyumbani itakapotokea ametimuliwa kabla ya muda wake kumalizika basi ataheshimu maamuzi ya uongozi ingawa hategemei hilo kutokea, kwa kuwa yeye ni mwanachama wa Yanga na amerudi nyumbani.

  0 0

  Mkandarasi wa soko kuu la Mwanjelwa linaloendelea kujengwa jijini mbeya ndugu,Balwinder Singh kutoka katika kampuni ya (NECCO) amezungumza na Ripota wetu juu ya maendeleo ya soko hilo kubwa lenye zaidi ya maduka 400 ya biashara ndogondogo,Benki mbili na kituo kikubwa cha polisi ambapo amesema soko hilo anatarajia kulikabidhii mwakani (2015) mwezi wa tano.

  Akiendelea kuzumza,Mkandarasi huyo amesema kuwa hali ya Ujenzi inaendelea vyema na wapo kwenye hatua za mwisho,hivyo hadi mwezi Mei mwakani soko litakuwa limekamirika kabisa na kulikabidhi.
  Mkandarasi wa Ujenzi wa Soko kuu la Mwanjelwa jijini Mbeya,Balwinder Singh akiandika baadhi ya maelezo ya vipimo muhimu vya Ujenzi kama alivyokutwa na Kameramani wetu.
   muonekano wa mbele wa soko la Mwanjelwa. 
   muonekano wa nyuma wa soko hilo. 


  0 0





  MWENYEKITI wa kamati ya usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope amewataka Simba ukawa kufuta kesi iliyopo mahakamani ili wawarejeshee uwanachama wao. 
  Pope alisema leo  kuwa hawana ugomvi na Ukawa, na kwamba uongozi uliopo madarakani upo tayari kuwarudisha Ukawa na kuwa kitu kimoja kwa maslahi ya kuijenga Simba. 
  "Ukawa ni matawi mawili ya Mpira Pesa na Mpira maendeleo, nimeshakutana na mpira pesa nikazungumza nao, nimewashauri wawasiliane na wenzao wakafute kesi ili tuungane na tuwe kitu kimoja kama zamani, kwa maslahi ya maendeleo ya Simba. 
  “Wanachama hawa walifutwa kwa kufuata taratibu za kikatiba,tutawarudisha kwa kufuata sheria."alisema Pope Wanachama hao walikuwa wakihusishwa kuhujumu matokeo ya sare sita mfululizo za Simba kwenye mechi sita za kwanza za ligi kuu ya Bara, lakini Pope alisema "Matokeo mabaya ya Simba hayakuhusiana na Ukawa.
  "Simba ilifanya vibaya kwa sababu za kiufundi. Tumeona mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi za mwanzo. Tumeyafanyia kazi kwa kusajili wachezaji wapya ambao tunaamini watatusaidia na kuziba mapungufu yaliyojitokeza. 
  “Wanachama na wapenzi wa Simba waachane na dhana potovu kuwa kundi hili ni wasaliti, ndio waliosababisha kufanya vibaya.” Kundi la 'Ukawa' liliundwa na wanachama 71 waliofutiwa uwanachama baada ya kufungua kesi mahakamani wakipinga mchakato wa uchaguzi kwa kile walichodai umekiuka katiba kwa kumuondoa kwenye kinyang'anyiro aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais Michael Wambura. 
  Baada ya mwenyekiti wa sasa Evans Aveva kuingia madarakani, akawafutia uwanachama Michael Richard Wambura pamoja na wanachama 71 katika mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika mapema mwezi Novemba ulioudhuriwa na wanachama 860 wa Simba  kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukiuka katiba kwa kupeleka masuala ya soka mahakamani. 
  Kabla ya kufikia uamuzi wa kufanya mkutano, Simba kupitia kwa Rais wake, Evans Aveva ilitoa nafasi kwa wao kumuona na kuwasilisha utetezi wao. Hata hivyo, hakuna hata mwanachama mmoja aliyejitokeza kwa ajili ya kulizungumzia suala hilo.

older | 1 | .... | 680 | 681 | (Page 682) | 683 | 684 | .... | 3284 | newer