Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 672 | 673 | (Page 674) | 675 | 676 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Wanafunzi wa Shemssah Junior Nursery School iliyopo Karakata Uwanja wa Ndege Jijini Dar es Salaam wakiwa katika ziara ya kimasomo ufukwe wa Bahari, Funy City Kigamboni pamoja na mahafali yao ikiwa kusheherekea kumaliza elimu ya awali. Shule hii ipo chini ya Mwalimu Aisha Juma Kibukillah
  Mmoja wa  Wanafunzi wa Shemssah Junior Nursery School akipokea cheti toma kwa mgeni rasmi
  Baadhi ya Wanafunzi wa Shemssah Junior Nursery School wakiwa Fun City, Kigamboni
  Wanafunzi wa Shemssah Junior Nursery School wakipumzika
  Wanafunzi wa Shemssah Junior Nursery School wakicheza Fun City

  0 0

   
   Dj KT kutoka Tanzania akiwa anaangusha bonge la moja Burudani .....
   
   Hakuna kulala full ku party ...
   DJ Pinye Mkali kutoka nchini Kenya .. akiangusha Burudani ... Hii ilikuwa hatare sana Mashabiki walifurahia Burudani hii ya nguvu.
   Twende Dj Pinye....
   Dj Crusia Toni kutoka Nchini Kenya akiendelea na Burudani ya Nguvu ... Party inaendela.... Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bibi Fionuala  Gilsenan akiongoza ujumbe wa Wabunge wa Ireland walipofika Ikulu Mjini Unguja 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza  na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bibi Fionuala  Gilsenan (wa pili kulia) akiwa na  ujumbe wa Wabunge wa Irelenad walipofika Ikulu Mjini Unguja leo kwa mazungumzo. [Picha na Ikuluanzibar

  0 0


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Waziri wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dr. Finella Mukangara (katikati) Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Abdilah Jihadi Hassan (kulia) wakiwa na Mwandishi wa Habari Salim Said Salim na Mama Fatma Karume wakiwa katika Hafla ya utoaji wa tunzo kwa wanamichezo bora kwa mwaka 2013/2014 katika ukumbi wa  Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi tunzo ya Heshma     Mama Fatma Karume mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Karume tunzo hiyo imetelolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)  kwa kutambua mchango mkubwa wa Mzee Karume kwenye michezo, ikiwa ni pamoja na kujenga majengo ya klabu za Yanga na Simba na mambo mengine mengi. Hafla hii ilifanyika  katika  ukumbi wa  Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
   Mama Fatma Karume mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Marehemu Mzee Abeid Karume  akiwa ameishikilia  tunzo ya Heshma baada ya kukabidhiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika hafla maalum ya utoaji wa tunzo hiyo  katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake fupi kwa wanamichezo mbali mbali katika hafla ya utoaji wa tunzo kwa wanamichezo bora  2013/2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam jana ambapo tunzo ya heshma ilitolewa kwa Mama Fatma Karume mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar  Marehemu Mzee Abeid Karume 
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipomkabidhi Tunzo Mwanamichezo bora wa jumla wa Mwaka Sheridah Boniface wakati utoaji wa tunzo zilizoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Taswa katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam (kushoto)Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari za Michezo TASWA Bw.Juma Pinto
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bara Dr. Finella Mukangara ,Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Abdilah Jihadi Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo waliopta tunzo zilizotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo katika ukumbi Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu


  0 0

   Katibu Mtendaji Baraza la Biashara Zanzibar Bw. Ali Haji Vuai wa kwanza (kulia) akizungumza na wandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa nane wa Baraza hilo, utakaofanyika Disemba 16 Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
   Wandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza Katibu Mtendaji Baraza la Biashara Zanzibar Bw. Ali Haji Vuai ofisini kwake Kinazini Mjini Zanzibar.
  Mwandishi wa Habari wa Radio Coconat Fm Tabia Makame akiuliza swali kuhusu Mkutano wa nane wa Baraza hilo katika Mkutano wa wandishi wa Habari uliofanyika Ofisi ya Baraza la Biashara Zanzibar Kinazini Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalum Prof Mark Mwandosya akisisitiza jambo kwenye mkutano wa mkuu wa 47 wa chama cha madaktari unaofanyika kwa siku 2 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Dodoma.
  Madaktari ambao ni wajumbe wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) wakifuatilia jambo katika ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma walipokuwa kwenye mkutano wao wa 47
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalum Prof Mark Mwandosya na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Kebwe Stevin Kebwe wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa chama cha madaktari waliokuwa kwenye mkutano wao mkuu.
  Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakiwa nje ya ukumbi wa Pius Msekwa kwa ajili ya mapumziko kabla ya kuendelea na mkutano. Picha na Pamoja Pure Blog

  0 0

   Mkazi wa karikoo Mashariki  Kata ya Kariakoo Bw. Fumbuka Ditopile akipiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Lumumba ,kwa ajili ya kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa Mitaa akiwemo  Mwenyekiti  na Wajumbe leo jijini Dar es Salaam.

   Mkazi wa karikoo Mashariki  Kata ya Kariakoo akipiga kura katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Lumumba 
   Msimamizi wa upigaji kura, Mwalimu Lucy Buzuka akitoa maelekezo kwa wapiga kura wa Kariakoo Mashariki, Kata ya Kariakoo jinsi ya kupiga kura katika zoezi la kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa ambapo siku ya leo jijini Dar es Salaam.
  Msimamizi wa upigaji kura, Mwalimu Lucy Buzuka akitoa maelekezo kwa wapiga kura wa Kariakoo Mashariki, Kata ya Kariakoo jinsi ya kupiga kura katika zoezi la kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa ambapo siku ya leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo.

  0 0

   Wanafunzi wa shule ya msingi Igomaa wilaya ya Mufindi wakipata maelekezo ya namna ya kuanzisha vitalu cha bustani ya miti kutoka mtaalam.

  Ofisa Maendeleo ya jamii msaidizi Bi. Martha Sanga akigawa vifaa ya bustani kwa mwalimu wa shule ya sekondari sadani.

  Ofisa Maendeleo ya jamii msaidizi Bi. Martha Sanga akiongea na wanafunzi

  Na Friday Simbaya, Mufindi

  Shirika la Hifadhi ya Mazingira Duniani (WWF) kupitia Programu ya Maji Ruaha (RWP), mkoani Iringa limekabidhi vifaa kwa ajili ya kuanzisha vitalu vya bustani za miti katika shule mbalimbali za Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.
  Ofisa Maendeleo ya Jamii msaidizi wa shirika hilo, Martha Sanga alisema vifaa vilivyotolewa ni pamoja na tolori,water can,leki, viliba, majembe, chepe na mbegu aina saba za miti, ambavyo vilikabidhiwa kwa kamati za mazingira za shule.
  Shule zilizopewa nyenzo hizo ni pamoja na Shule ya Sekondari Sadani, Shule ya Msingi ya Igomaa na Shule ya Sekondari Isalavanu.
  Alisema kuwa zaidi ya shilingi milioni tatu (3m/-) zilitumika kwa ajili ya vifaa pamoja na malipo ya wawezeshaji, mafuta ya gari na mengineyo.
  Alisema kuwa wameamua kutoa vifaa hivyo kwa shule ilikupandiza mbegu ya uhifadhi kwa watoto wa shule na hatimaye kupeleka elimu ya kutunza mazingira kwenye familia zao. na imeshindwa kutunza miti ya matunda katika mashamba darasa hayo zilizotolewa na shirika hilo.
  “Tuliwahi kuipa jamii mbegu za miti ya matunda iliweze kuanzisha bustani za matunda wakashindwa kuitunza na kwa safari hii tumeamua kuwapa wanafunzi vifaa vya bustani kupitia kamati zao za mazingira kwa sababu ni rahisi kutunza mazingira,” alisema Sanga.
  Naye mtaalamu kutoka idara ya ardhi na maliasili kitengo cha misitu, Khalid Kayowa wa halmashauri ya wilaya Mufindi alitoa mafunzo kwa kamati za mazingira hizo ya namna ya kutumia vifaa pamoja na namna ya kutungeza vitalu vya miche.
  Alivitaja vitu vinavyohitajika kuanzisha eneo la kuwatika mbegu za miti kuwa ni udongo,mchanga, mbolea ya mbonji pamoja na viliba na madawa kwa ajili ya kuulia wadudu na lazima na kivuli cha kutosha pamoja kuwe na uzio.
  Alisema kuwa kamati za mazingira hizo hazinabudi ya kufuata ushauri wa kitaalamu ya namna ya kuanzisha bustani kwa ajili ya kuzalishia miche ya miti itakayopandwa katika maeneo mbalimbali shule.
  Shirika la WWF limejikita katika kuhamasisha shughuli za utunzaji wa mazingira, rasilimali za maji, pamoja na maendeleo ya jamii, ikiwemo kilimo, ambapo limekuwa likishiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu na vifaa kwa wanajamii.

  “Mto Ruaha Mkuu ndiyo chanzo kikuu cha maji katika bwawa la Mtera ambako kuna mitambo ya kuzalisha umeme na lengo kubwa ni kuhakikisha mto huo unatililisha maji kwa mwaka mzima” alisema ofisa maendeleo ya jamii msaidizi.

  WWF huendesha Programu ya Maji (RWP) katika wilaya nane ambazo ni Iringa Vijijini, Kilolo, Mufindi, Njombe, Mbarali, Mbeya Vijijini, Chunya na Makete.

  Hivi karibuni Shirika la Hifadhi ya Mazingira Duniani (WWF) kupitia Programu ya Maji Ruaha (RWP), mkoani Iringa lilikabidhi vifaa vya upaliliaji wa zao la mpunga kwa wakulima wa Kata ya Mlenge, Tarafa ya Pawaga wilayani Iringa.

  Vifaa vilivyotolewa vitakavyosaidia kupalilia pamoja na kuwanufaisha wakulima wa mpunga wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mlenge, kutoka vijiji vya Kinyika, Isele, Kisanga na Magombwe.

  0 0


  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa na baadhi ya Wahitimu wa Kituo cha Chekechea cha Florence cha Kigogo Dar es salaam.
  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala  akizungumza katika Mahafari ya Kituo cha Chekechea cha Florence yaliyofanyika Kigogo Dar es salaam. Watoto mia moja wamehitimu katika Kituo hicho na wote wamejifunza na kuelewa  kusoma na kuandika.
  Balozi Kamala amewashukuru Bwana na Bibi Mbezi kwa kuanzisha kituo hicho. Aidha, Balozi Dr. Kamala ameanzisha mfuko wa zawadi wa Dr. Kamala "Dr. Kamala Award Fund" utakaokuwa unatoa zawadi kila mwaka kwa mtoto atakayeonesha kipaji cha uongozi. Baada ya Balozi Kamala kutoa laki moja za kuanzisha mfuko huo wazazi walimuunga mkono kwa kuchangia laki moja.
  Balozi Kamala amehaidi kuchangia milioni moja mfuko huo na riba itakayopatikana kila mwaka itatumika kutoa zawadi kwa mtoto atakayeonesha kipaji cha uongozi. Vile vile Balozi Kamala alichangia shilingi laki mbili na nusu kituo hicho na amehaidi kukitafutia wafadhili wa kukisaidia.

  0 0

  Balozi Ndayiziga katika mojawapo ya warsha ya EAC hivi karibuni. Kulia ni mtaalamu wa habari na mratibu wa mafunzo ya wandishi wa habari EAC, Bw. Sukhdev Chhatbar.
  Mkufunzi Balozi  Jeremy Ndayiziga (kushoto enzi za uhai wake) akimkabidhi cheti Mroki Mroki, kutoka Father Kidevu Blog ambaye pia ni Mpigapicha wa Masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,  kwa kushiriki kikamilifu mafunzo hayo ya masuala ya Mtengamano wa EAC. Anaeshuhudia Katikati ni Elizabeth Wanyoike wa GIZ ambao walifadhili mafunzo hayo na Jumuia ya Afrika Mashariki.
  **********
   Na Mtua Salira, EANA
  Mshauri Mtaalamu wa muda mrefu wa Masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Jeremy Ndayiziga (54) amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa kisukari mjini Bujumbura,Burundi.
  Balozi huyo raia wa Burundi kwa mujibu wa marafiki wa karibu na ndugu zake alifariki Jumatano wiki iliyopita na anatarajiwa kuzikwa nchini Burundi Jumanne ijayo, Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA) limeripoti.
  Kutokana na hali yake ya afya kuendelea kudorora, Balozi Ndayiziga alilazimika kukatwa mguu wake wa kulia  katika Hopsitali ya Nairobi kutokana kuzidiwa na ugonjwa wa kisukari na hivyo kubaki hospitalini kwa miezi ipatayo minne. Afya yake ilionekana kuimarika kidogo na alikuwa anakaribia kupona.
  Mara ya mwisho alionekana makao makuu ya EAC mjini Arusha, Tanzania katikati ya Novemba mwaka huu katika mkutano wa Maofisa Mawasiliano wa EAC.
  Jina la Balozi Ndayiziga ni maarufu kwa watendaji wa EAC kutokana na umahiri wake wa uchapaji kazi,uongozi wa busara na kuwa muumini wa itikadi ya Shirikisho la EAC. Ndiye aliyeiongoza nchi yake katika harakati za kujiunga na EAC 2007.

  ‘’Marehemu Balozi Ndayiziga alikuwa mtu maarufu, mchapakazi mwenzangu na kwa kweli, zaidi ya yote alikuwa rafiki yangu wa karibu sana,’’ alisema Jean Rigi,Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki  nchini Burundi na kuongeza kuwa wengi watamkosa na ni pigo kubwa kwa wote wanaopigania kujenga Afrika Mashariki na raia wake.

  Mkongwe wa masuala ya habari nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu kufuatia taarifa ya kifo hicho alisema: ‘’Nimepata mshtuko mkubwa! Nilijua kwamba alikuwa anaugua lakini nilifikiri kwamba ni jambo la kawaida tu linaloweza kudhibitiwa.
  Nimesikitishwa sana kwa sababu alikuwa ni mtu makini na mwalimu mwenye uelewa wa hali ya juu na alikuwa mwakilishi mzuri wa masuala ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Nilifanya naye kazi kwa karibu sana kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano.’’
  Naye mmoja kati wafanyakazi aliokuwa anafanya nao kazi kwa karibu ni Sukhdev  Chhatbar, Mtaalamu wa Masuala ya Habari, ambaye alielezea kusitishwa na kifo Balozi Ndayiziga.‘’Tulikuwa tunawasiliana vyema katika uekelezaji wa miradi mbalimbali.Alikuwa mtu maarufu, mwenye msimamo thabiti,mwenye busara na alikuwa tayari kufanya lolote kuimarisha mchakato wa mtangamano wa kikanda,’’ alisema Chhatbar, mwandishi wa habari maarufu aliyekuwa anasafiri na kusimamia miradi ya pamoja ya EAC na marehemu Balozi huyo katika nchi wananchama wa jumuiya.
  Marehemu ameacha mjane na watoto wanne.

  0 0  0 0

  Bi. Twitikege Mlagha Mafumu enzi za uhai wake

   Baadhi ya waombolezaji wakitoa pole kwa ndugu na jamaa katika msiba wa  marehemu Bi. Twitikege Mlagha Mafumu, ambaye ni mama mzazi wa wanahabari Kulwa, Dotto na Nico Mwaibale Mbagala Kuu, jijini Dar es Salaam.
    Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msiba wa Bi. Twitikege Mlagha Mafumu unaofanyika jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye msiba wa Bi. Twitikege Mlagha Mafumu unaofanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ulinzi ya Security Group (T) Ltd (SGA), Eric Sambu akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo muda mfupi kabla ya kuanza kuufanyia usafi ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuadhimisha miaka 30 ya utendaji kazi wa kampuni hiyo nchini.
  Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya ulinzi ya Security Group (T) Ltd (SGA), wakifanya usafi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Mbezi Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kudhimisha miaka 30 ya kampuni hiyo tangu kuanza kufanya kazi zake hapa nchini.
  Meneja Mawasiliano wa kampuni ya ulinzi ya Securty Group (T) Ltd (SGA), Sofia (kushoto) akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa zoezi la kufanya usafi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ikiwa ni kuadhimisha miaka 30 ya utendaji kazi wa kampuni hiyo hapa nchini.
  Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Security Group (T) Ltd (SGA) akifurahia katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha zoezi la ufanyaji usafi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuadhimisha miaka 30 ya utendaji kazi wa kampuni hiyo nchini.
  Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Security Group (T) Ltd (SGA) wakionesha sehemu ya taka ngumu walizookota katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam wakati walipoufanyia usafi ufukwe huo kuadhimisha miaka 30 ya utendaji kazi wa kampuni hiyo hapa nchini.

  0 0

  Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.
  Hali ya kushtusha imetokea katika uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Migombani  baada ya Afisa Mtendaji  kufika  na kutangaza kimyakimya Kuwa UChaguzi huo umesitishwa
  Mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kusikia ndipo walipoanza sasa kutafuta mchawi na kumtia nguvuni afisa mtendaji huyo wa mtaa kwa kutaka kujua sababu za msingi zinazopelekea yeye kuja kutangaza kusitisha uchaguzi huo.
  Afisa mtendaji huyo baada ya kuulizwa sababu za msingi alijitetea kuwa ameagizwa na Mkurungenzi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Ilala.
  Baada ya Kutoa sababu hiyo ndipo wakazi wa mtaa wa migombani walipoona kuna dalili za kuchakachuliwa kwa kura zao ndipo walipomuweka mtu kati na kumtaka Afisa mtendaji huyo kutangaza kwa maandishi kuwa uchaguzi unaendelea. 
  Pia wahakikisha anaandika barua hiyo ya kuendelea na uchaguzi, ambapo wakazi wa mtaa wa Migombani walikwenda nae katika ofisi ya kata kwa ajili ya kugonga muhuri kuthibitisha Uchaguzi huo kuendelea. Hayo yalipofanyika  uchaguzi ukaendelea na hadi muda huu zoezi la kuhesabu kura linaendelea bila kelele wala mikwaruzo.
  Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea (katikati mwenye shati la draft) akiwa kawekwa mtu-kati mara baada ya kuja na kutaka kusitisha uchaguzi bila sababu ya msingi. Waliomzunguka ni wakazi wa mtaa wa segerea wakimuhoji afisa mtendaji huyo sababu ya kutaka kusitisha uchaguzi huo wakati hakukuwa na vurugu wala kero ya aina yoyote iliyojitokeza katika kituo cha kupigia kura cha Migombani.
   Wakazi wa Mtaa wa migombani wakumzuia afisa mtendaji kuondoka hadi pale atakapotangaza tena kuwa uchaguzi unaendelea.
  Hii ndio barua aliyokuwa akiandika afisa mtendaji wa kata ya segerea inavyosomeka ambapo baadae alienda nayo ofisi kwa kuongozana na wakazi wa migombani kwaajili ya kugonga muhuri wa kata kuthibitisha kuwa uchaguzi unaendelea
  Afisa Mtendaji wa Kata ya Segerea, Akiandika barua ya kutamka kuwa uchaguzi unaendelea mara baada ya wakazi wa mtaa wa migombani kutaka afisa huyo kueleza sababu za msingi za kutaka kujaribu kusitisha uchaguzi huo.Pembeni ni wakazi wa Mtaa wa Migombani wakishuhudia kuwa afisa mtendaji huyo anaandika ipasavyo hiyo barua.

  Afisa mtendaji wa Kata ya Segerea (Mwenye shati la drafti) akiongea na wakazi wa mtaa wa migombani mara baada ya vurugu kutaka kutokea mara baada ya afisa mtendaji wa kata ya segerea kujaribu kusitisha uchaguzi bila sababu za msingi. Picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0


  Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Migombani Kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Bw. Japhet Kembo akifurahia huku akipongezwa na wanachama na wapenzi wa Chadema mara baada ya kuibuka mshindi wa Kiti cha Mwenyekiti kwa Kupata Kura 510 huku CCM wakiwa wamepata kura 215 na NCCR kupata kura 205

   Mawakala wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Migombani wakihesabu kura ambapo sanduku hilo ndio lilikuwa sanduku la mwisho kuhesabiwa katika Kituo cha Kupigia kura cha Migombani ambao wakazi wa Mtaa wa Migombani walikuwa wakisubiria matokeo

  Baadhi ya wapita njia nao ilibidi wasimame maana uchaguzi huu ulivuta hisia za watu wengi kutokana na hali iliyoonyeshwa na wakazi wa mtaa huo kukaa mpaka dakika za mwisho

   Msimamizi wa Uchaguzi katika Kituo cha Kupigia Kura cha Migombani akitangaza Mshindi wa Uchaguzi huo uliomalizika kwa Mgombea wa Chadema akiwa ameibuka Mshindi kwa Kupata Kura 510 huku wapinzani wake wakiwa na Kura 215 za CCM na Kura 205 za NCCR

   Wakazi wakishangilia kwa Ushindi. 
  Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

  0 0

  Sehemu ya Wafanyakazi wa kampuni ya mafuta ya Engen Tanzania wakijadiliana jambo kabla ya kuanza mtanange wao katika Bonanza la kusherehekea kumaliza mwaka 2014,lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Sunrise,Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa kampuni ya mafuta ya engen wakiendelea kuonesha vipaji vyao vingine kwenye sherehe ya kumaliza mwaka.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  KAMPUNI ya Scania nchini Tanzania imekutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wafanya biashara wa mabasi ya abiria pamoja na wafanya biashaya ya kutengeneza mabodi ya mabasi ya abiri kutoka makampuni mbalimbali wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Chesisi za Scania yaliyoandaliwa na Kampuni ya Scania yaliyojulikana kama “ Scania Bus Expo” yaliyo fanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari Meneja mauzo wa Kampuni ya Scania Tanzania, Godwin Rwegasira alisema leo ni siku ya kuwakumbusha wafanya biashara wa mabasi ya abiria na watengeneza mabodi kuwa watumie Chesisi za Scania kwa wale ambao hawajawahi na wale ambao wanatumia waendelee kutumia kwani ni bora,imara na zinadumu kwa muda mrefu na zaidi ya yote spea zake zinapatika mahali pote kwenye vituo vya Scania.

  Alisema Rwegasira, Scania ni vumilivu sana inaweza kuhimili miundombini ya namna yeyote hususani barabara zetu za Afrika mashariki za vumbi, hivyo tutumie chesisi za Scania mkombozi kwa biashara yako ya mabasi ya abiria.

  Nae Afisa mauzo kutoka Kampuni za kutengeneza mabodi ya mabasi ya Master kwa niaba ya watengeneza mabodi kutoka makampuni mbalimbali alisema Chesisi za Scania ni bora, zina zinahimili shida, ni imara na spea zake zinapatikana hivyo kwa niaba ya watengeneza mabodi alitoa wito kwa wafanyabiashara kutumia Chesisi za Scania katika biashara zao za mabasi ya abairia.

  Makampuni mabalimbali ndani nan je ya nchi yalialikwa katika maonyesho hayo ambayo ni Master Fabricator kutoka Kenya, Dar Coch kutoka Tanzania, Choda kutoka Kenya, LSHS kutoka Tanzania, Quality Garage kutoka Tanzania, Stanbic Bank na Scania Finance pamoja na wafanyabishara wa mabasi ya abiria.
  Meneja Mauzo na masoko wa kampuni ya kutengeneza mabodi ya mabasi ya abiria ya Choda kutoka Kenya, Pius Wambua(kulia) akiwaonyesha wageni waalikwa baadhi mabasi waliyowahi kutengenezwa na kampuni hiyo katika picha wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Scania yaliyojulikana kama “Scania Bus Expo” yenye malengo ya kuhamasisha wafanyabiashara wa mabasi ya abiria kutumia Chesisi za Scaina.Maonyesho yalifanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha mabasi yaendao mikoani cha Ubungo Dar es Salaam.
  Meneja mauzo wa Kampuni ya Scania Tanzania, Godwin Rwegasira(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Chesisi za Scania yaliyojulikana kwa “Scania Bus Expo” yenye malengo la kuwahamasisha wafanya biashara wa mabasi ya abaria kutumia chesisi za Scania kutokana na ubora wake.Maonyesho hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni watengeneza mabodi wa mabasi ya Abiria, Pius Wambua meneja mauzo na masoko kutoka kampuni ya Choda Kenya(kushoto) na Peter Gitau Afisa mauzo ktoka kampuni ya Masters kutoka Kenya.
  Afisa masoko wa kampuni ya kutengeneza mabodi ya mabasi ya, Master kutoka Kenya, Peter Gitau(kushoto) akiwaonyesha wageni waalikwa baadhi mabasi waliyowahi kutengenezwa na kampuni hiyo katika picha wakati wa maonyesho ya Kimataifa ya Scania yaliyojulikana kwa “Scania Bus Expo” yenye malengo ya kuhamasisha wafanyabiashara wa mabasi ya abiria kutumia Chesisi za Scaina.Maonyesho yalifanyika mwishoni mwa wiki katika kituo cha mabasi yaendao mikoani cha Ubungo Dar es Salaam.

  0 0

  Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Asumpta Malya, akionyesha tuzo ambayo PPF ilipata kwenye shindano la Afrika linaloandaliwa na taasisi ya ISSA, kuhusu utoajin bora wa huduma wa mifuko ya hifadhi ya jamii barani Afrika, hususan kwenye fao la elimu. Alikuwa akiwaonyesha wahariri wa vyombo vya habari kwenye semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani Jumamlosi Desemba 13, 2014 baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa utoaji huduma bora kwa wanachama wake.Alikuwa akiwaonyesha wahariri wa vyombo vya habari kwenye semina ya siku moja ya Wahariri wa vyombo vya habari iliyofanyika mjini Bagamoyo , mkoa wa Pwani, Jumamosi Desemba 13, 2014.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyofanyika Jumamosi Desemba 13, 2014, huko Bagamoyo mmkoani Pwani.


  0 0

  Kaka Issa Michuzi,

  Pole na mihangaiko yako ya kila siku. Kwa kweli kwa upande wangu mambo si mazuri. nasumbuliwa na tatizo la upungufu wa nguvu zetu kwa hiyo ni karaha saana. Sina raha kwa kukosa chakula ya usiku.
  Nimeona kwenye blog yako hili tangazo hapa kwenye hii linki:


  Ningependa kupata mrejesho toka kwa huyu ndugu lakini naona hajibu tena meseji. Basi nakuomba uliweke hili tangazo kwenye blog yako ili mwenye suluhu aweze kutuelekeza wapi pa kuipata. naomba msaada kaka najua wajua karaha aipatayo mwanamume pale mambo yanapogoma.

  Naomba uweke email yangu tujndalwa@yahoo.com ili nisijulikane.

  Natanguliza shukrani kaka.

  0 0


older | 1 | .... | 672 | 673 | (Page 674) | 675 | 676 | .... | 3278 | newer