Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 673 | 674 | (Page 675) | 676 | 677 | .... | 3278 | newer

  0 0  0 0

  Miss World 2014,Rolene Strauss akiwamwenye furaha kubwa mara baada ya kutwaa taji hilo jioni hii katika ukumbi wa mikutano na maonesho wa ExCel London Exhibition and Convention Centre huko nchini Uingereza.
   Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Miss World, Julia Evelyn Morley akimtangaza Miss World 2014 ambaye mwaka huu anatokea nchini Afrika Kusini,Rolene Strauss.
  Miss World 2014,Rolene Strauss akipungia mara baada ya kutwaa taji hilo. Kulia ni Mshindi wa pili, Nia Sanchez (USA) na kushoto ni mshindi wa tatu,Edina Kulcsár (HUNGARY)
  Mambo ya Miss World 2014.
  Miss World 2013 Megan Young akimvisha Miss South Africa Rolene STRAUSS shashi la ushindi wa mwaka 2014 katika ukumbi wa mikutano na maonesho wa ExCel London Exhibition and Convention Centre. Jumla ya washiriki 125 walipanda jukwaani na kushindania taji hilo, akiwemo mrembo Happiness Watimanywa wa Tanzania. 
  Warembo walioshiriki Fainali za 64 za shindano la urembo la Miss World lililofanyika usiku huu jijini London.

  0 0
 • 12/14/14--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Technotronic - Pump Up The Jam

  0 0
 • 12/14/14--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Haddaway - What Is Love

  0 0
 • 12/14/14--22:30: Article 24


 • 0 0

  Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Rukia Mtingwa (kushoto) akitoa elimu kuhusu ujasiriamali na baadhi ya vijana kutoka vyuoni walio katika kambi maalumu iliyoandaliwa na kampuni ya Maa Media kwa udhamini wa NBC mjini Bagamoyo, Pwani hivi karibuni. NBC ilitoa kiasi cha zaidi ya shs milioni 100 ambapo mbali na ujasiriamali vijana hao walifundishwa pia madhara na jinsi ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya.
  Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter (kulia), akisalimiana na Meneja Miradi wa Kampuni ya Maa Media, Albany James wakati yeye na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa (kulia) walipotembelea kambi ya vijana iliyoandaliwa na Maa Media ili kuwafundisha masuala ya ujasiriamali, madhara na jinsi ya kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya. NBC ilitoa kiasi cha zaidi ya shs milioni 100 kwa ajili ya kambi hiyo iliyofanyika mjini Bagamoyo. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Lekoko Furaha.


  0 0  0 0  0 0

  Viongozi wa NATATA, toka kushoto ni Katibu Mkuu Halima Guga,Mwenyekiti Given Massawe na mratibu wa Elimu Abdulkarim Baksh.
    Mwenyekiti wa NATASA ,Given Massawe akipozi kwa picha na wadau wa NATASA, toka kushoto  ni Henry Mzava,Evance,Letitia Smith ambae yeye anatoka Namibia, Henry,Hamza Riyani, Charles na Mercy.
   M/kiti wa NATASA Given Massawe akikata keki ya ya kuzindua umoja huo pamoja kuazimisha miaka 53 ya Uhuru wa Tz huku katibu wake Halima Guga akishuhudia.
   Wakina dada wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa Nanchang ambao ni wanachama wa NATASA wakipozi kwa picha wakiwa na bendera zao za Tanzania siku ya uzinduzi huo.
   .Wakina dada wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa Nanchang ambao ni wanachama wa NATASA wakipozi kwa picha wakiwa na bendera zao za Tanzania siku ya uzinduzi huo.
   wadau wa NATASA wakiwa ndani ya ukumbi  wa Hotel ya XIN DIAN TI wakibadilisha mawazo mawili matatu na kukumbushana story mbali mbali za nyumbani Tanzania.
   Mzee wa Shekeli Geofrey Njalangi  na kitamba chake cheupe mkononi mbele kabisa akisataka rhumba siku ya uzinduzi huo wa NATASA pamoja na Charles kulia na Elvis kushoto kwake  ndani ya ukumbi wa  XIN DIAN TI HOTEL kwenye mjii wa Nanchang nchini CHINA.
    
  Mo van der Mhando,Nanchang, China.

  Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma kwenye mjii wa  Nanchang nchini China wameanzisha umoja wao na  Jumamosi iliyopita wameuzindua rasmi umoja huo wenye lengo la kuwasaidia kwa mambo mbali mbali wakiwa kwenye nchi ya kigeni.
  Jumla ya wanafunzi 54 wa Kitanzania wapo kwenye mjii huo wakiwa wanasoma kwenye vyuo mbali mbali na walikuwa hawana kitu chochote kinachowaweka karibu kama Watanzania na ndio maana wakaanzisha umoja huo.
  Umoja huo unaojulikana kwa jina la Nanchang, Tanzanian Students Association (NATASA) ulizinduliwa rasmi na mwenyekiti wake Given Massawe ambae alisema kuanzishwa kwa umoja huo lilikuwa ni wazo la muda mrefu na hatimae hivi sasa ndoto imetimia.Massawe alifafanua kuwa kwenye mingine ya nchini China ambako kuna wanafunzi wa Kitanzania nao wanajumuia zao ambazo zinawasaidia hivyo kwa wanafunzi wa Nanchang kuwa na umoja huo ni sehemu ya fungua milango kwao.
  Mwenyekiti huyo amesema hivi sasa wapo kwenye harakati za kutengeneza katiba yao ambayo ndio itakuwa dira ya uongozi wao na pia kuzinduliwa kwa chama hicho ni msaada tosha kwa wanafunzi hao wa Kitanzania kuanzia kwenye masomo hadi maisha ya kila siku.
  Uzinduzi wa umoja huo ulienda sambamba za sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania bara na hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wanafunzi wa Nanchang kusherekea siku yao ya Uhuru wakiwa pamoja.

  0 0

  Marehemu Shem Ibrahim Karenga enzi za uhai wake.

  Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini ,Shem Ibrahim Kalenga amefariki Dunia mapema leo katika hospitali ya Amana,Ilala Jijini Dar.Habari zilizotufikia zinaeleza kuwa mkongwe huyo amefariki hospitali ya Amana na kuwa msiba utakuwa nyumbani kwake Buguruni.Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho makaburi ya kisutu baada ya sala ya Alasiri

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI -AMINA

  =======  ======  ======= ========

  SHEM IBRAHIM KARENGA ni mmoja kati ya wanamuziki wachache wenye uwezo wa kucharaza gita huku akiimba kwa wakati mmoja. Shem alitamba sana miaka ya 1970  akiwa na bendi ya Tabora Jazz wana Segere Matata.

  Alizaliwa mwaka 1950 eneo la Bangwe mkoani Kigoma na kupata elimu yake katika shule ya msingi Kihezya kati ya mwaka 1957 na 1964.

  Alianza kujifunza muziki akiwa mwanafunzi katika shule ya wamissionari na huko ndiko fani hiyo ilianza kuchipua hatimaye mwaka huo huo wa 1964  akajiunga na bendi ya Lake Tanganyika Jazz iliyokuwa na maskani yake mjini Kigoma. Alipoingia Lake Tanganyika Jazz alijifunza Ala za muziki za drums, Kinanda na gita la rhythm, Solo. Besi gita pamoja akiimba.

  Alidumu  katika bendi hiyo kwa kipindi cha miaka minane na mwaka 1972 Shem Kalenga aliitwa katika bendi ya Tabora Jazz ambako aliingia kwa kishindo na nyimbo zake alizozitunga akiwa na Lake Jazz na kuanza kuzipiga katika bendi yake mpya.

  Nyimbo hizo zilikuwa Dada Asha na Remmy ambazo zilimpa umaarufu na kujulikana kwa haraka na kuwa simulizi katika kila pembe za mji  huo wa Tabora.

  Shem alipata ushindani mkubwa baada ya kuwakuta wakali wengine wa kupiga gita akina Kassimu Kaluwona, Athuman Tembo pamoja na Salumu Luzila na  Issa Ramadhan ‘Baba Isaya’ lakini alijitutumua  na kuwa mmoja kati ya wapiga solo gita  bora la katika bendi hiyo.

  Mwaka wa 1983 Shem Kalenga aliicha bendi hiyo kwa sababu zake mwenyewe na kuachana na mambo ya muziki kwa muda.Lakini baada ya kuondoka yeye bendi hiyo haikudumu tena na ikapotea katika ramani ya muziki.

  Aliondoka Tabora  mwaka 1990  baada ya kuitwa na mfanyabiashara wa jijini Dar  es Salaam Baraka Msilwa ambaye alimuomba ajiunge katika bendi yake ya M.K. Beat iliyokuwa ikipiga katika mtindo wa ‘Tunkunyema’ Bendi hiyo ilikuwa ndugu na ile ya M.K. Group.

  Ndani ya M.K.Beat Shem Kalenga  aliwakuta vijana machachari akina Maliki Star, Bwani  Fanfan, Sisco Lunanga na Fungo Shomari. Kwa mshikamano waliokuwa nao  waliweza kuiinua Bendi hiyo vilivyo na kuwa tishio kwa bendi zingine za jijini Dar es Salaam.

  Bendi hiyo ilisambaratika mwaka 1995 na mwaka uliofuatia alianzisha bendi yake ya Tabora Jazz Star ambayo ina wanamuziki sita na huburudisha katika kumbi mbalimbali za jijini Dar  es Salaam hadi sasa. 

  Anasema miaka ya hivi karibuni biashara huria ziliporuhusiwa, Studio nyingi binafsi zilifunguliwa lakini hazina manufaa kwao kufuatia kiwango cha pesa zinazotozwa na Studio hizo  kuwa kubwa mno kiasi cha wao kushindwa kumudu kulipia.

  Kalenga anatoa wito kwa Serikali aidha kwa  wafadhili kuwaona kwa jicho la huruma wanamuziki hao wazamani kuwawezasha  kwa vile bado wanao uwezo mkubwa wa kupiga muziki na kutoa elimu kwa jamii pamoja burudani kwa wapenzi kama zamani.

  Anajutia umaskini na ufinyu wa fikra uliowakumba wanamuziki wa dansi wa zamani umewafanya kushindwa kujitutumua na kwamba wanchosubiri ni kudra za mwenye mungu, serikali, wafadhili au yeyote atakayeguswa  kutaka kuwakwamua  wakongwe hao kwa kuwapatia vyombo vya muziki.

  Shem Kalenga anakumbuka miaka ya nyuma jinsi Serikali ilivyokuwa ikiwasaidia kurekodi nyimbo zao bure katika Studio za Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), ambapo  gharama yao ilikuwa ni nauli ya kwenda Dar na kurejea  Tabora.

  Anaendelea kuifagilia Studio RTD  enzi hizo ilivyokuwa ikichuja nyimbo zao  tofauti na sasa ambapo  Studio nyingi zinarekodi pasipo kuzichuja matokeo yake baadhi ya nyimbo zinazosikika katika vituo vya redio hazina maadili mema kwa jamii.


  Mzee mzima Kalenga ambaye sifa zake zimezagaa kila kona Afrika ya Mashariki na Kati anawaasa vijana wa muziki wa kizazi kipya kujifunza kupiga Ala za muziki badala ya kutembea na CD mkononi. 

  0 0

   Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kitongoji cha Msikitini kwenye Kijiji cha Mbwewe wilaya ya Bagamoyo Said Mlinde kulia akiongea na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alipotembela kituo hicho kushuhudia zoezi la upigaji kura.
  msimamizi msaidizi wa kituo cha kupigia kura Kitongoji cha Mkwajuni kwenye Kijiji cha Miono wilaya ya Bagamoyo Faustina Oforo  akisubiria wapiga kura wa uchaguzi wa vitongoji, vijiji na mitaa uchaguzi uliofanyika juzi.

  Na John Gagarini, Bagamoyo.
  HUKU uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji ukiwa umefanyika juzi na matokeo yakiendelea kutoka wananchi 514 wa Kijiji cha Mwetemo Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo wameshindwa kupiga kura kutokana na uhaba wa karatasi za kupigia kura.

  Uchaguzi huo ulishindwa kufanyika kutokana na karatasi za kupigia kura kuwa chache hivyo watu wengine kushindwa kupiga kura ambapo watafanya uchaguzi huo Desemba 19.

  Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kitongoji hicho kuangalia zoezi hilo la upigaji kura wa kuchagua viongozi akiwemo mwenyekiti na wajumbe watano msimamizi msaidizi wa uchaguzi Thomas Madega alisema kuwa wamekubaliana uchaguzi huo kufanyika siku hiyo.

  “Karatasi za kupigia kura kwanza zilichelewa kwani zilifika kituoni saa 10 kasoro jioni na pia zilikuwa chache hivyo watu wachache walipiga kura na wengine walishindwa kupiga kabisa,” alisema Madega.

  Madega alisema kuwa walikaa na viongozi wa vyama vyote na kukubaliana kusogezwa mbele zoezi la upigaji kura. “Tumekubaliana na vyama vyote kusogeza uchaguzi huo hadi Ijumaa na wamekubali tumewaambia wawatangazie wafuasi wao juu ya hili,” alisema Madega.

  Juu ya kuahirisha kwa muda mrefu tofauti na maeneo mengine ambayo yalikuwa na matatizo na uchaguzi kufanyika jana alisema kuwa wametoa muda mrefu ili waandaliwe vifaa vya upigaji kura kwa uhakika.

  Kwa upande wake mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete alisema kuwa muda huo ni mrefu sana kwani maeneo mengine yalifanya uchaguzi kesho yake. “Nadhani suala la siku ya kupiga kura lirudishwe nyuma kwani Ijumaa ni mbali sana hivyo kuna haja ya wahusika kuliangalia hilo ili wasipishane na wengine,” alisema Ridhiwani.

  Ridhiwani alishauri zoezi la namna ya kupiga kura washirikishwe zaidi wananchi kwani wale wanaowachagua ni viongozi wao hivyo wao ndiyo wenye nafasi kubwa ya kushauri na si viongozi wa vyama vya siasa.

  Baadhi ya vijiji na vitongoji ambavyo vilifanya uchaguzi wao jana Jumatatu badala ya Jumapili ni Kijiji cha Changarikwa, Vitongoji vya Kwamkula, Mkambala A na B, Kwaluguru A na B, Pugwe, Migola na Kwadivumo kwenye kata ya Mbwewe.

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Ibrahim Matovu alipoulizwa juu ya baadhi ya maeneo kushindwa kupiga kura alisema kuwa bado hajapata takwimu sahihi ndiyo anafuatilia kujua changamoto hizo.

  Uchuguzi mdogo uliofanywa na mwandishi wa habari hizi ulibaini zoezi la upigaji kura ulikumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa vifaa vya upigaji kura kama vile upungufu wa karatasi, picha za wagombea kuwekwa kwenye nembo ya chama kisichohusika na kukosekana kwa  fomu za wagombea wa nafasi ya ujumbe.

  0 0

   Kulia ni Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga Erick Chinimbaga na wa kwanza kushoto ni Afisa Fedha kutoka PSPF Makao Makuu Samweli Haule wakiwakabidhi zawadi za Krismasi watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo cha Buhangija kilichopo Shinyanga  zawadi za Sikukuu ya Krismasi hapa watoto wenzao wakipokea zawadi hizo kwa niaba.  

  Akikabidhi Msaada huo Afisa Fedha wa PSPF kutoka Makao Makuu alisema kwamba Mfuko wa Pensheni wa PSPF unalo lengo la kuwasaidia watoto wenye Uhitaji Maalum ili nao waweze kujisikia wapo katika jamii kama watoto wengine na kwamba kuwa hapo sio ndio kwamba wametengwa, alisisitiza kuwa Hata watakapo kuwa wakubwa wengine wataikuta PSPF na watakuwa wanachama na wengine watakuja kufanya kazi kabisa katika mfuko huo.
   Mlezi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha  Buloma Foundation kilichopo Picha ya Ndege Kibaha Bi Simphania Aidan wa kwanza kushoto akipokea Zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa niaba ya Msimamizi na Mwenye kituo hicho Bi.Fransisca Kyando Kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF , wa katikati ni Meneja wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka na wa kwanza kulia ni Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani.  

  Akikabidhi Msaada huo Meneja wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka alisema kuwa PSPF inatoa zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa watoto yatima ili nao washerekee vizuri na wasijisikie vibaya , aliongeza kuwa pamoja na PSPF kuwa na wanachama watu wazima lakini pia inafanya hivyo kwa watoto ili waanze kuijua PSPF wakiwa wadogo na wakiwa watu wazima waje kuikumbuka na kujiunga na Mfuko huo Bora wa Pensheni na hata kuja kufanya kazi katika Mfuko huo.

  Nae Afisa Mahusiano wa PSPF kutoka Makao Makuu Coleta Mnyamani  Aliongeza neno kuwa Watoto yatima ni kama watoto wengine ambao wanahitaji kupata huduma na malezi Bora kama watoto wengine wenye wazazi au wanaolelewa bila shida yotote, alimalizia kwa kusema kuwa PSPF ipo pamoja na watoto hao wenye uhitaji na itaendelea kuwasaidia .


   Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga wa pili kushoto  Erick Chinimbaga akimkabidhi zawadi Mmoja wa walezi wa watoto hao bwana Revocatus Robert   wa kwanza Kulia zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa Wasichana waliotoka katika Mazingira magumu wanaolelewa na Kituo cha Agape Mkoani shinyanga, wasichana hao walipata zawadi za Mafuta, Mbuzi, Mchele, Sabuni,Sukari pamoja na vitu.

  0 0

  Lorietha Laurence -Maelezo.

  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo  ametoa wito kwa kampuni za Filamu nchini kuwasilisha filamu zao ili ziweze kuhakikiwa na kulipiwa  kwa kupata kibali cha kuingia sokoni  kama sheria ya filamu ya mwaka 1976 kifungu namba 4 inavyoeleza.

  Akizungumza  katika ofisi za Bodi leo jijini Dar es Salaam, Fisoo ameipongeza  kampuni ya Al-Riyamy Production  ambayo imeweza kutimiza wajibu wake na kulipia filamu 134 ambazo zimepata kibali cha kupatiwa stamp za  TRA na hivyo kuwa tayari kuingia sokoni. Aliongeza kuwa kuna baadhi za  kampuni za filamu nchini zimekiuka utaratibu na kushindwa kuwasilisha filamu zao kwa Bodi ikiwemo filamu zile zilizoigizwa  miaka ya zamani ambazo zimekuwa zikionyeshwa bila kibali.

   “Nimefurahishwa sana  kwa namna ambavyo kampuni ya Al-Riyamy  Production kwa kufuata sheria na kanuni za filamu nchini, hivyo natoa wito kwa kampuni nyingine pia kuweza kufanya  hivyo ili kukuza uchumi wetu na wao waweze kufanya biashara bila usumbufu” alisema Fisoo.

  Naye mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala, amewaomba wasanii wenzake wenye kampuni za filamu waweze kufuata taratibu na sheria za bodi ya filamu ili kukuza soka la filamu na kuinua uchumi wa nchi yetu.

  “Nawasiii wasanii wenzangu na wamiliki wa kampuni za filamu nchini waweze kufuata sheria na kanuni za filamu ili tuweze kwenda vizuri kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika ulimwengu huu wa filamu” alisema Mzee Jangala. 

  Baadhi ya kampuni ambazo zimeweza kuwasilisha kazi zao katika Bodi ya filamu ,ni pamoja na kampuni ya  Wananchi wote wamewasilisha filamu 119, Game First Quality filamu 35, steps Entertainment filamu 739, na Al-Riyamy Production  filamu 134.
   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo  akiamwandikia kibali cha filamu mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kulia) baada ya kufanya malipo ya filamu zao zote zikiwemo za zamani na mpya,leo jijini Dar es Salaam.
   Mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kulia) akimuonyesha stakabadhi ya malipo Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo baada ya kufanya malipo ya kupata kibali kwa ajili ya filamu za kampuni hiyo,leo jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo  akimkabidhi kibali cha filamu mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kulia) baada ya kufanya malipo ya filamu zao zote zikiwemo za zamani na mpya,leo jijini Dar es Salaam.
   Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Clarence Chelesi(kulia) akimpa mkono wa pongezi mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kushoto) baada ya kupata kibali cha filamu,leo jijini Dar es Salaam.
  Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Simon Peter (kulia)  akimpa mkono wa pongezi mwakilishi wa kampuni ya Al- Riyamy Production Bakari Kassim almaarufu Mzee Jangala,(kushoto) baada ya kupata kibali cha filamu wanaotazama ni Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Clarence Chelesi(katikati) na   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu , Joyce Fisoo (kushoto) ,leo jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo).

  0 0
 • 12/15/14--04:33: Hii ni hatari
 • Dereva wa boda boda (haonekani pichani) akiwa amembeba abiria wake na mizigo yake kama ionekanavyo pichani,hali inayopelekea kuhatarisha usalama wa maisha yao.Picha hii ilinaswa na Camera ya Globu ya Jamii katika barabara ya Msata-Bagamoyo mapema jana jioni. 

  0 0

   Wachezaji wa timu ya Chuo cha Sayansi za Jamii, wakijifua kwa mazoezi kabla ya mchezo wao dhidi ya timu ya Chuo cha Uhandisi na Teknolojia katika fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosaa taa.

    Wachezaji wa timu za Chuo cha Sayansi za Jamii (jezi nyeusi) na Chuo cha Uhandisi na Teknolojia, wakigombea mpira wakati wa mchezo wa fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosa taa. 
    Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Betram Mapunda akikagua wachezaji wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia, kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufuatia giza kuingia na uwanja kukosa taa.Kushoto ni Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga.
  Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Betram Mapunda akikagua wachezaji wa Chuo cha Sayansi za Jamii, kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali ya mashindano ya vitivo mbalimbali vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyodhaminiwa na Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Uni 255, yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu jijini Dar es Salaam juzi. Timu hizo zilitoka sare ya magoli 1-1 katika mpambano huo, uliomalizika kabla ya muda kufutia giza kuingia na uwanja kukosa taa.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi  wa Mpya wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa Zanzibar Dr. Andemichael Ghirmay Redae alipofika kutambulishwa na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Nchini Tanzania Rofaro Chatora (katikati) halfa hiyo ilifanyika leo  Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ikulu.]
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza  Mwakilishi  wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Nchini Tanzania Rofaro Chatora (katikati) wakati alipofika kumtambulisha Mwakilishi  wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa Zanzibar Dr. Andemichael Ghirmay Redae (kushoto)   Ikulu Mjini Zanzibar leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Mwakilishi  wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa Zanzibar Dr. Andemichael Ghirmay Redae baada ya mazungumzo yao leo alipofika kutambulishwa kwa Rais naMwakilishi  wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Nchini Tanzania Rofaro Chatora (katikati)  Ikulu Mjini Unguja.

  0 0

    Mkurugennzi msaidizi katika Idara ya Kamati kutoka Ofisi ya Bunge Ndg. Angumbwike Ng'wavi akitoa Mada kuhusu umuhimu kuwa na taarifa za  pamoja za kibunge kwa ajili ya wadau mbalimbali wa Bunge  na namna ya utekelezaji wake wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo wadau wa Bunge kutoka Serikarini na taasisi binafisi. Semina hiyo imeandaliwa na Bunge kupitia mradi wake wa kuwajengea Wabunge na Watumishi uwezo unaofadhiliwa na UNDP.
    Maafisa wa Serikali pamoja na Wadau mbalimbali wa Bunge wakifuatilia mada hiyo kwa makini.

   Afisa Habari wa Bunge Ndg. Owen Mwandumbya akitoa Mada kuhusu umuhimu wa Bunge kuwa na Mpango Mkakati wa Mawasiliano  wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo wadau wanaofanya kazi na Bunge kutoka Serikarini na Taasisi binafisi. Semina hiyo imeandaliwa na Bunge kupitia mradi wake wa kuwajengea Wabunge na Watumishi uwezo unaofadhiliwa na UNDP iliandaliwa kwa lengo la kuanisha changamoto zitazolikabili Bunge kushirikiana na wadau wake.
   Maafisa wa Serikali pamoja na Wadau mbalimbali wa Bunge wakifuatilia mada hiyo kwa makini.


  0 0

  Na John Gagarini, Kibaha
  TIMU ya soka ya wanawake ya mkoa wa Pwani imeingia kambini kwenye shule ya sekondari ya Baden Powell iliyopo wilayani Bagamoyo kujiandaa na mchezo wake na timu ya mkoa wa Morogoro utakaochezwa Desemba 28 mwaka huu.
  Mchezo huo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi wilayani Kibaha wa kuwania kombe la Taifa kwa wanawake.
  Akizungumza leo mjini Kibaha, katibu wa chama cha soka la Wanawake (TWFA) mkoa wa Pwani Florence Ambonisye alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vizuri.
  Ambonisye alisema kuwa timu hiyo inanolewa na mchezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake Hilda Masanche iliingia kambini wiki iliyopita.
  “Timu inatarajiwa kurejea Desemba 26 wilayani Kibaha ambapo itaingia kambini kwenye kambi ya Ruvu JKT Mlandizi siku mbili kabla ya mchezo huo,” alisema Ambonisye.
  Aidha alisema kuwa timu hiyo itaongezewa wachezaji wanne mara itakaporudi Kibaha ili kuipa nguvu timu hiyo inayoundwa na wachezaji wengi vijana ambao ni wanafunzi shule za sekondari.
  “Changamoto kubwa inayoikabili timu hiyo ni ukosefu wa vifaa kwani wachezaji wanatumia vifaa vyao binafsi walivyoendanavyo kambini,” alisema Ambonisye.
  Alibainisha kuwa wanatarajia kushinda mchezo huo kwani timu yao imejiandaa vyema na mchezo huo licha ya kuwa wapinzani wao nao wako vizuri na wana uhakika wa kuingia 16 bora.

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Chama cha mapinduzi kimeibuka kidedea katika uchaguzi wa uwenyekiti wa mitaa katika mitaa yote iliopo ndani ya mkoa wa Arusha baada ya kuvishinda vyama vingine vya upinzani .

  Akitangaza  matokeo ya uwenyeviti wa mitaa Mkurugenzi wa jiji la Arusha Iddi Juma alisema kuwa mpaka sasa uchaguzi wa uwenyekiti umekamilika katika mitaa yote na vituo vyote isipokuwa kituo kimoja ambacho uchaguzi wake utarudiwa siku ya kesho.

  Alisema kuwa   katika uchaguzi huu jumla ya wananchi  1,13909 walijiandikisha kupiga kura na jumla ya vyama sita vilisimamisha wagombea katika kila mtaa ambapo alitaja vyama ambavyo vilisimamisha wagombea kuwa ni pamoja na ACT,chama cha mapinduzi CCM,NCCR mageuzi ,CUF pamoja na TLP   .

  Akitaja matokeo ya uwenyekiti wa mitaa alisema kuwa ccm imeweza kuongoza kwa kupata mitaa mingi zaidi ambapo alisema kuwa CCM imeweza kupata kura 78 ambapo kati ya kura hizo kura sita ni za kupita bila kupigwa, ikifuatiwa na chadema ambao wana kura 75 ,ACT ikiwa aijapata kura ,NCCR ikiwa aijapata kura ,CUF ikiwa aijapata kura pamoja na TLP

  Aidha alibainisha kuwa jumla ya vituo 154 vilikuwa wepo kwa ajili ya kupigia kura na vyote vimekamilisha uchaguzi isipokuwa kimoja ambapo kilifutiwa matokeo hayo na kulazimika kurudiwa ambapo alisema kuwa katika kituo hicho uchaguzi utarudiwa hapo kesho .

  mpaka sasa uchaguzi wa uwenyekiti umemalizika ila tumelazimika kurudia uchaguzi katika vituo vitatu ambapo katika vituo hicho kituo kimoja ambacho ni cha Oysterbay uchaguzi utarudiwa kwa watu wote na maanisha uchaguzi wa kuanzia kwa mwenyekiti wa mtaa ,wajumbe  watano pamoja na wajumbe watatu wa viti maalumu huku katika kituo cha AICC -Sekei uchaguzi utarudiwa kwa wajumbe watatu wa viti maalumu ambapo hii inatokana na kura za kufungana kwani wote walipata 31 kwa 31  na katika kituo cha Oldpolisi line ambapo napo uchaguzi utarudiwa kwa watu wawili ambao nao pia  ni wajummbe wa viti waamaalu  walifungana kwa kura 64 kwa 64.

  Juma alisema katika uchaguzi wakesho ambao  wanarudia wamejipanga vizuri kusimamia kwani nguvu zote wanazielekeza katika vituo hivyo ambapo alibainisha kuwa katika kila kituo kutakuwa na wasimamizi nane pamoja na ulinzi wa kutosha  .

  Aidha alitumia fursa hii kuwashukuru wananchi wate na viongozi kwa kufanya uchaguzi wa amani na kistarabu  pamoja na kuvumiliana huku akiongeza kuwaanamatumaini utulivu huu na uvumilivu walionyesha utaendelea hata katika vituo hivi ambavyo vinarudiwa.

  0 0

    Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akisalimiana na baadhi aya madiwani wa Loliondo juzi alipokwenda kujadiliana nao kuhusu mgogoro wa ardhi katika maeneo hayo. 
  Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ngorongoro, Raphael ong'oi akizungumza wakati ea kikao na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kujaduli mgogoro wa ardhi Loliondo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiw ana mkuu wa wilaya ya Loliondo EliasLala lawai alipowasili katika ueanja wa ndege wa Waso, Loliondo kwa ajili ya mazungumzo na madiwani kuhusu mgogoro wa aerdhi uliodumu kwa miongo .
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na madiwani wa Ngorongoro juzi wakati alipokutana nao ili kujadili jinsi ya kumaiza mgogoro wa ardhi Loliondo.

older | 1 | .... | 673 | 674 | (Page 675) | 676 | 677 | .... | 3278 | newer