Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 671 | 672 | (Page 673) | 674 | 675 | .... | 3272 | newer

  0 0  0 0


  Ndugu zangu,

  Kutokana na sababu za kiufundi zikiwamo za marekebisho muhimu, blogu yako ya kijamii, Mjengwablog.com haiko hewani kuanzia jana jioni. 

  Wataalam wanalishughuIikia swala hilo  na Mjengwablog itarudi tena hewani kabla ya saa sita mchana kwa saa za Afrika Mashariki. 

  Hata hivyo, KwanzaJamii Radio iko hewani kama kawaida, sikiliza live...http://www.ustream.tv/channel/kwanzajamii-radio

  Poleni kwa usumbufu.

  Maggid Mjengwa,
  Mwenyekiti Mtendaji
  IkoloMedia
  Iringa.

  0 0

  MFUKO wa Pensheni wa LAPF umeunga jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na maabara kwa kutoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya sh.milioni 3.5 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari ya Mihande iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
   
  Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Mlandizi wilayani humo jana, Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki wa mfuko huo, Isaya Mwakifulefule alisema mfuko huo umejiwekea utaratibu wa kusaidia kutoa misaada mbalimbali katika  shughuli za maendeleo ya kijamii.
   
  “Mfuko wetu kila kanda nchini wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo na katika hilo mnaweza kuwa mashuhuda kwani siku za hivi karibuni mmeweza kuona tulivyotoa msaada kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (albino)” alisema Mwakifulefule.
   
  Alisema ujenzi maabara katika shule hapa nchini ni muhimu sana katika wakati huu wa ulimwengu wa sayansi na teknolojia ambapo wanahitaji wanayansi wengi kwa utaalamu wa aina mbalimbali hasa katika masuala ya utafiti.
   
  Alitaja vifaa vilivyotolewa na mfuko huo kuwa ni mabati na rangi kwa ajili ya kukamilishia ujenzi wa maabara hizo na alitoa mwito kwa wadau wa maendeleo na mifuko mingine kujitokeza kusaidia eneo hilo kwani kuna mahitaji makubwa ya maabara nchini.
   
  Akipokea msaada huo kwa niana ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu wa wilaya hiyo, Doris Semkiwa alisema msaada huo utapunguza changamoto ya ujenzi wa maabara kwenye shule hiyo.
   
  Alisema ujenzi wa maabara katika wilaya hiyo umekamilika kwa asilimia 67 na kuwa ujenzi huo unaendelea kwa kasi ambapo wanatarajia kukamilisha kazi hiyo mapema iwezekanavyo.
   
  Alisema kwa wilaya nzima yenye shule za sekondari 8 mahitaji ni kuwa na maabara 24 na tayari wamejenga 14 na kuwa fedha zinazotumika kwa ujenzi huo zinatoka katika mapato ya ndani ya Halmshauri, wadau mbalimbali na nguvu za wananchi.
   
  Aliongeza kuwa ujenzi huo utagharimu zaidi ya sh, milioni 400 na kuwa changamoto kubwa ni mapato ya ndani kuwa kiduchu na kuwa kama wangekuwa na fedha za kutosha wangeweza kumaliza kwa wakati ujenzi huo.
   
  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha aliwashuku LAPF kwa msaada huo pamoja na Halmsahauri kwa fedha za luzuku inazozitoa kila mwezi kusaidia mambo mbalimbali katika shule hiyo na zingine sanjari na ujenzi wa maabara hizo.

  “Naishukuru Halmshauri kwa fedha hizo ambazo imekuwa ikitupa kila mwezi kusaidia katika maeneo mbalimbali” alisema Masha. 
  Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto),  akimkabidhi, Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa (kulia), bati na rangi zenye thamani ya sh.milioni 3.5 zilizotolewa na mfuko huo jana, kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari ya Mihande ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na maabara. Anayeshuhudia makabidhiano hayo katikati ni Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha.
  Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto),  akipeana mkono na Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha wakati akikabidhi msaada huo. Kulia ni   Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa. 
  Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akipeana mkono na Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha.   
  Hapa ni kubadilishana mawazo baada ya makabidhiano hayo.

  0 0

   Na Mwandishi Maalum, New York 
  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema, mafanikio ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) yatategemea uimarishishwaji wa ushirikiano kati ya Makahama hiyo na Afrika. 
  Na kwa sababu hiyo, Tanzania imeshauri kuwa Rais Mpya wa Mkutano wa Nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai hana budi kuhakikisha kuwa moja ya vipaumbele vyake vijielekeze katika kuimarisha uhusiano wa Makahama hiyo na Afrika. 
   Ushauri huo umetolewa na Balozi Irene Kasyanju, Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati akizungumza katika mkutano wa kumi na tatu wa Nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai. 
   Amesema Tanzania ina imani kubwa na Rais mpya wa Mkutano wa Nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, Bw. Sidiki Kaba, kutoka Senegal, kuwa afanye kila awezalo katika kuimarisha uhusiano huo ambao kwa sasa umezorota. 
   Vile vile Balozi Kasyanju amesema Rais huyo anashika uongozi katika kipindi ambacho, Mahakama inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwenendo mzima wa mahakama na hasa uhusiano wake na Afrika. 
   Amebainisha kuwa, changamoto hiyo ya mahusiano na nyinginezo zinahitaji majadiliano ya uwazi yatakayowashirikisha wadau wote, na kwamba Tanzania inaamini kuwa anao uwezo huo. Akizungumzia zaidi kuhusu ushirikiano kati ya Mahakama na Afrika, Tanzania imeeleza kuwa namna ICC ilivyoshughulia shauri la Kenya hakutafanya mambo yawe shwari, kutokana na ukweli kuwa ICC ilishindwa kulifanyia kazi ombi la awali lililowasilishwa na Afrika mbele ya chombo hicho la kutaka kuahirishwa kwa shauri hilo kumechangia katika kuongeza malumbano kati ya ICC na Afrika. 
  Kwa mantiki hiyo Tanzania imesema uamuzi wa hivi karibuni wa kumwondolea mashtaka Rais Uhuru Kenyata unapaswa kutoa fursa kwa mahakama hiyo kujitazama upya. Vile vile Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetumia fursa hiyo kumpongeza Rais Kenyatta kwa kuonyesha ushirikiano na ICC. 
  Katika hatua nyingine Tanzania pia imeishauri ICC kuangalia namna itakavyoweza kufanya kazi kwa karibu na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa hasa katika kushughulikia makosa ya jinai yanayofanywa na Nchi ambazo si wanachama wa Mkataba wa Mahakama hiyo ili kuondoa dhana ya undumilakuwili katika utendaji wa ICC. 
   Tanzania imeujulisha mkutano huu kwamba ipo katika hatua yake ya awali ya kuziingiza sheria zitokanazo na Mkataba wa ICC katika mfumo wa Kisheria wa Nchi. Balozi Kasyanju anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo wa wiki mbili unaohusisha pia uchaguzi wa majaji sita wa mahakama hiyo.
   Balozi Irene Kasyanju,  Mkurugenzi wa Idara ya  Masuala ya  Sheria, Wizara ya  Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Kimataifa, akizungumza wakati wa   Mkutano wa  Kumi na Tatu wa  Nchi  Wanachama wa Mkataba wa  Mahakama ya  Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC). Mkutano huo wa wiki mbili  unafanyika hapa Makao  Makuu ya Umoja wa Mataifa.

  Sehemu ya  wajumbe wa nchi wanachama wa Mkataba wa  Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai wakimsikiliza  Mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huo, Balozi Irene Kasyanju ambaye katika hotuba yake pamoja na mambo mengine ameishauri Mahakama hiyo kuimarisha  uhusiano wake na Afrika..

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bibi Fionuala Gilsenan akiongoza ujumbe wa Wabunge wa Ireland walipofika Ikulu Mjini Unguja leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bibi Fionuala Gilsenan (wa pili kulia) akiwa na ujumbe wa Wabunge wa Irelenad walipofika Ikulu Mjini Unguja leo kwa mazungumzo , [Picha na Ikulu.]

  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katka picha ya pamoja na wanachama wa Umoja wa wake wa viongozi ( New Millenium Women Group) katika chakula cha jioni kilichoambatana na burdani mbalimbali kwenye ukumbi wa Kardinal Rugambwa, Oysterbay jijini  Dar es salaam, Desemba 12, 2014.  Chakula hicho  kiliandaliwa ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maboresho ya kituo cha  kulea watoto yatima cha Buhangija mkoani Shinyanga.
   Baadhi ya  washiriki wa maonyesho ya mavazi yaliyoandaliwa na  Umoja wa wake wa viongozi ( New Millenium Women Group) katika chakula cha jioni kilichoambatana na burdani mbalimbali kwenye ukumbi wa Kardinal Rugambwa, Oysterbay jijini  Dar es salaam, Desemba 12, 2014 wakijitambulisha baada ya onyesho hilo.  Chakula hicho  kiliandaliwa ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maboresho ya kituo cha  kulea watoto yatima cha Buhangija mkoani Shinyanga
   Baadhi ya  washiriki wa maonyesho ya mavazi yaliyoandaliwa na  Umoja wa wake wa viongozi ( New Millenium Women Group) katika chakula cha jioni kilichoambatana na burdani mbalimbali kwenye ukumbi wa Kardinal Rugambwa, Oysterbay jijini  Dar es salaam, Desemba 12, 2014 wakijitambulisha baada ya onyesho hilo.  Chakula hicho  kiliandaliwa ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maboresho ya kituo cha  kulea watoto yatima cha Buhangija mkoani Shinyanga
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katka picha ya pamoja na washiriki wa maonyesho ya mavazi yaliyoandaliwa na  Umoja wa wake wa viongozi ( New Millenium Women Group) katika chakula cha jioni kilichoambatana na burdani mbalimbali kwenye ukumbi wa Kardinal Rugambwa, Oysterbay jijini  Dar es salaam, Desemba 12, 2014.  Chakula hicho  kiliandaliwa ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maboresho ya kituo cha  kulea watoto yatima cha Buhangija mkoani Shinyanga

  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, Bw. Ludovick Utouh (kulia), na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad (kushoto), katika hafla ya kumpongeza na kumuaga Bw. Utouh iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam,11 Desemba, 2014.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, juzi tarehe 11 Desemba 2014, alimuaga rasmi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu Bw. Ludovick Utouh, katika hafla maalum iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
  Hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na baadhi ya Watendaji Wakuu na Waandamizi kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali ilikuwa mahsusi pia kumkaribisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu mpya wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Juma Assad.
  Katika hotuba yake ya kumpongeza Bw. Utouh, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue, alielezea historia ya Utumishi uliotukuka ya Bw. Utouh ambayo imeleta sifa kubwa Ofisi hiyo ndani na nje ya nchi na katika medani za kimataifa. Kwa ujumla, hotuba ya Katibu Mkuu Kiongozi ilijikita kuelezea mchango binafsi wa Bwana Utouh kwa taifa ndani ya miaka zaidi ya arobaini (40) ya Utumishi wake Serikalini.
  Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi alielezea mafanikio ya Serikali kwenye eneo la utawala bora, uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za fedha za umma ambayo yamechangiwa na Bw. Utouh. Balozi Sefue aliwasihi watumishi wa umma kuiga weledi, uaminifu, msimamo, bidii na maarifa ambayo Bw. Utouh alivionyesha kwa vitendo katika utumishi wake.
  Katibu Mkuu Kiongozi alitumia fursa hiyo pia, kumtakia kila la kheri, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mpya, Profesa Juma Assad, katika kufanikisha majukumu aliyopewa.
  Bwana Utouh alistaafu rasmi nafasi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, tarehe 19 Septemba, 2014 baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa miaka saba na miezi kumi tangu alipoteuliwa na Rais, tarehe 19 Agosti, 2006

  0 0

  Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa ndani ya MV Liemba mara walipofika kujionea mandhari ya meli hiyo kongwe duniani.
  Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akisaini kitabu cha wageni ndani ya MV Liemba. Kulia ni Nahodha wa Meli hiyo, Kapteni Mathew Mwanjisi.


  0 0
 • 12/13/14--04:52: Call Out for Artists

 • ZIFF is East Africa’s largest film, music and arts festival, bringing together talent from all over the world for a Zanzibar Tamasha! ZIFF puts together the island’s best parties. Bringing live music, dance, DJs and performances on a number of platforms. A carnival fever hits Zanzibar for 10days! 
  We bring musicians together from all over Africa, and the world at large.

   
  Zanzibar International Film Festival is currently calling for Musicians and Performing Artists to send their request in order to be part of ZIFF 2015. Applying is free. Please submit you sample works by sending a YouTube link, Vimeo, Sound Cloud, pictures and Artist profile to mpa@ziff.or.tz.


  Deadline: 31st January, 2015 at 12Noon.


  0 0

  Diwani wa kata ya Mlangarini, Mhe Mathius Manga,  akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa CCM kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa  serikali za mitaa utakaofanyika jumapili Desemba 14 mwaka huu.

  Diwani Manga amewaasa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura wagombea wa CCM kwani wanasifa stahiki za kuwaongoza. 

  Aidha amesisitiza kulimnda amani kipindi cote cha uchaguzi na hata matokeo yatakapo tangazwa na kuepuka vitendo vya vurugu. 
   Wananchi wa kata ya Manyire wakimsikiliza diwani wa kata hiyo hayupo pichani wakati wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa serukali za mitaa. Picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Jumanne Sagini akiwaeleza waandishi wa Habari kuhusu utaratibu utakaotumika hapo kesho wakati wa upigaji kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa mbili asubuhi (2:00) hadi saa kumi alasiri (10:00) ambapo wananchi wote watakaokuwepo vituoni hadi kufikia muda huo wataruhusiwa kupiga kura hadi watakapokuwa wamemalizika.Kushoto ni Mratibu wa uchaguzi huo bw.Denis Bandisa

  FRANK MVUNGI-MAELEZO

  Serikali imewataka wananchi wote waliojiandikisha  kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa  kushiriki kwa wingi ili waweze kuwachagua viongozi wao katika maeneo yao.

  Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Jumanne Sagini wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam .

  Akifafanua Sagini amesema wapiga kura wazingatie kuwa kila mpiga kura anatakiwa kupiga kura moja tu na apige kwenye kitongoji au mtaa anaoishi  na si vinginevyo.

  Pia Sagini alitoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa, Asasi zisizo za Kiserikali kuwahamasisha wapiga kura kujitokeza kwa wingi hapo kesho kuchagua viongozi wao.

  Akiwatahadharisha wananchi kuhusu kupiga kura Zaidi ya mara moja au kutaka kupiga kura wakati  si mkazi wa eneo hilo  Sagini alisema  hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaojaribu kukiuka sheria, Kanuni na taratibu za uchaguzi huo.

  Katika uchaguzi huo sagini alibainisha kuwa utaratibu utakaotumika ni kupiga kura,kuhesabu na kutangaza matokeo ambapo taratibu zote zimefafanuliwa katika Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za mwaka 2014 na katika mwongozo wa uchaguzi huo.

  Wapiga kura wote wametakiwa kufika katika maeneo ya kupigia kura wakiwa na kitambulisho cha mpiga kura cha Uchaguzi Mkuu, Kitambulisho cha kazi,Hati ya kusafiria,Kadi ya benki,Kadi ya Bima ya Afya,Kitambulisho cha shule au chuo,Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha uraia kwa ajili ya kuwatambulisha.


  Uchaguzi wa Serikali za mitaa katika ngazi za vijiji,Mitaa na vitongoji utafanyika siku ya jumapili ya tarehe 14 Desemba,2014 ambapo katika uchaguzi huo watachaguliwa wenyeviti wa vijiji na wajumbe wa Halmashauri za Vijiji,Wenyeviti wa Mitaa na wajumbe wa Kamati za mitaa na wajumbe wa kamati za Mitaa na wenyeviti wa vitongoji.


  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani  Mh.Mathias Chikawe (kushoto)  akishuhudia  dereva wa pikipiki  akivalishwa  pete zenye ujumbe wa “Wait to Send” wakati  wa  uzinduzi wa kampeni ya usalama barabarani uliofanyika eneo la Mwenge makutano ya barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi jijini  Dar es Salaam, uzinduzi huo uliambatana na  upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva na ugawaji wa pete maalumu za kuwakumbusha madereva kuacha kutumia simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed Mpinga
   Waziri wa Mambo ya Ndani  Mh.Mathias Chikawe (kushoto)  akishuhudia  dereva wa pikipiki  akivalishwa  pete zenye ujumbe wa “Wait to Send” wakati  wa  uzinduzi wa kampeni ya usalama barabarani uliofanyika eneo la Mwenge makutano ya barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi jijini  Dar es Salaam, uzinduzi huo uliambatana na  upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva na ugawaji wa pete maalumu za kuwakumbusha madereva kuacha kutumia simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed Mpinga
  Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohammed Mpinga akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usalama barabarani iliyozindiliwa  na Waziri wa Mambo ya Ndani  Mh.Mathias Chikawe katika eneo la Mwenge makutano ya barabara ya Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi jijini  Dar es Salaam leo, uzinduzi huo uliambatana na  upimaji wa kiwango cha pombe mwilini kwa madereva na ugawaji wa pete maalumu za kuwakumbusha madereva kuacha kutumia simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.

  0 0

  Ndugu zangu,
  Ni saa kadhaa zilizopita. Tunawashukuru wote mliotutumia jumbe na kutupigia simu kuulizia kulikoni. Mmeonyesha kujali. 


  Tunaamini, kuna wengi pia ambao hawakupata nafasi ya kuulizia tatizo, lakini, kuwa wapo pamoja nasi,tunawashukuru sana. 
  Unaweza sasa kutembelea
  http://mjengwablog.com

  0 0

  Kaimu Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki, Isaya Mwakifulefule (kushoto), akimkabidhi, Ofisa Elimu wa Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Kibaha, Doris Semkiwa (kulia), bati na rangi zenye thamani ya sh.milioni 3.5 zilizotolewa na mfuko huo jana, kusaidia ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari ya Mihande ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kuhakikisha kila shule ya sekondari nchini inakuwa na maabara. Anayeshuhudia makabidhiano hayo katikati ni Mkuu wa shule hiyo, Flora Masha.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Asteria Muhozya, Nzega 
  Mgodi wa Resolute uliopo Wilayani Nzega Mkoani Tabora jana tarehe 12 Desemba, 2014, ulikabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma katika hafla fupi iliyofanyika na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia madini Stephen Masele.
  Wengine walioshuhudia ni, Mkuu wa Wilaya ya Nzega aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Bituni Msangi, Viongozi Waandamizi wa Wilaya ya Nzega, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, Kamati ya Kitaifa ya uchimbaji, Uongozi wa Juu wa kampuni ya Resolute na wananchi.  Naibu Waziri Masele alieleza kuwa, tukio la kukabidhiwa eneo hilo la Mgodi kwa Chuo ni tukio ambalo limefungua ukurasa mwingine kutokana na kwamba Chuo cha Madini Dodoma kitaiwezesha Tanzania kuzalisha wataalamu zaidi waliobobea katika tasnia hiyo ambao mchango wao kwa taifa unahitajika katika kuendeleza sekta ya madini.
   “Tunataka wanafunzi wasome kwa vitendo, hii itawezesha kupata wataalamu waliobobea. Ni nafasi kwa wanafunzi na Chuo cha Madini kuitumia fursa hii vizuri. Najua kuna mawazo mchanganyiko ya kupoteza mapato kwa Halmashauri na mengine ya kupata Chuo lakini, kufunga mgodi ni sehemu ya Sheria ya madini”, aliongeza Masele.
   Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi, akizungumza katika halfa hiyo, alieleza kuwa, Mgodi wa Resolute una historia ya kuwa mgodi wa kwanza nchini kuzalisha madini ya dhahabu na kuogeza kuwa, ndani ya kipindi cha miaka 12 cha uhai wa mgodi huo umeweza kuchangia kiasi cha shilingi bilioni 290 za Kitanzania ikiwa ni kodi mbalimbali zilizotolewa na mgodi huo kama mrahaba. 
  Aliongeza kuwa, Halmashauri iliweza kupata kiasi cha shilingi bilioni 6 ikiwa ni kodi na kiasi cha Tsh bilioni 6 kilitumiwa na mgodi huo kuwezesha za kijamii ikiwemo ujenzi wa zahanati, shule, upatikanaji wa huduma safi ya maji katika eneo linalozunguka mgodi huo. 
  Pamoja na eneo la mgodi huo kukabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma, vilevile mgodi umekabidhi majengo, mitambo, maabara ambapo, kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo cha Madinini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile alieleza kuwa, eneo hilo litatumiwa na wanafunzi wa mwaka wa pili kwa ajili ya masomo ya vitendo. 
  Mgodi wa Resolute umefunga rasmi shughuli zake za uchimbaji madini ya dhahabu katika eneo hilo, ambapo ulianza kazi zake mwaka 1998. Kabla ya makabidhiano hayo, mgodi huo umefanya ukarabati, ujenzi wa madarasa, na uhifadhi wa mazingira.
   Sehemu  mgodi ambao shughuli za uchimbaji zilikuwa zikifanywa na mgodi wa Resolute ambao pia umekabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma. Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe ameeleza kuwa,mgodi huo utatoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuhusu shughuli za uchumbaji.
   Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Mhe Stephen Masele (aliyesimama katikati na pama) akishuhudia halfa fupi ya kusaini makabidhiano ya eneo la Mgodi wa Resolute kwa Chuo cha Madini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile, katikati ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Resolute Peter Beilby. Wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi (wa pili kuchoto aliyesimama),Mkurugenzi Kampuni ya Resolute Rose Aziz na baadhi ya waliohudhuria.

   Meneja Mazingira   baada Mgodi wa Resolute Jackie Sinclair (Kulia), akimkabidhi funguo mbalimbali za majengo ya eneo la mgodi wa Resolute Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini)  Stephen Masele (Kushoto) mara  makabidhiano ya eneo la mgodi.

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe funguo mbalimbali za majengo ya mgodi wa Resolute kwa ajili ya Chuo cha Madini Dodoma. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 12/13/14--06:45: APPRECIATION
 • In the sure and certain hope of the resurrection to eternal life, we give thanks for the life and example of SIMON SAMWEL SALAMBY KAHEMELE whose part of life with us on earth ended in a tragic road accident that occurred at Kimelembe, Ludewa on November 14, 2014.


  We, the family of Rev. Can. Humphrey and Mama Mary Kahemele of Njombe, would like to take this opportunity to say thank  you to all those who have been with us during this challenging time of passing of Simon. 

  We are not able to thank each one of you individually at this point hence we request that you all accept our sincere appreciation for all that you have been to us at this time. Your support and presence was not only a relief, but a source of strength for our family in this difficult time. Your participation and contributions to the services were a tremendous comfort.


  We will remain eternally grateful!


  Thank you!  May Simon rest in peace and rise in glory!


  0 0

   Parliament of Uganda are the champions of the Inter-Parliamentary football tournament once again! 
   Parliament of Uganda beat Parliament of Tanzania 2-1 in an entertaining final played at the Sheikh Abeid Amri stadium yesterday to take the trophy away for the fourth time in consecutive. 
   The victors started the game on a high pace testing the Tanzania defence several times. 
  Strikers Hon Odonga Otto and Hon Muhammad Nsereko made constant raids but the defence marshaled by Hon Adam Malima held on. 
   Tanzania’s goalkeeper, Hon Iddi Azzan made many stops in the first half. He was called to save a hard shot from Hon Otto in the 6th minute of the match. 
  However, three minutes later, Hon Nsereko beat the defence to slam the ball in the net to give his side the lead. 
   In the second half, Parliament of Tanzania came in a more forceful side and attempted many times to penetrate the rock-solid defence of Uganda. 
   Uganda however, made a counter attack and notched in the second goal through Hassan Tindyebwa following spadework by Hon Nsereko. 
   The introduction of Mark Tanza for Tanzania changed the tempo of the game with Yusuf Gogo, Yona Kirumbi and Hon Joshua Nassari combining well.
   It did not take long before Hon Nassari chipped in the ball to earn Tanzania the consolation goal. 
   Parliament of Kenya was crowned third after earning a 2-0 walk-over over EALA following the latter’s inability to field a team. 
   According to EALA officials, several key players of the team were nursing injuries. The rules currently allow only three staff members to be fielded. 
   The Clerk (in person) can also be fielded. 
   Earlier on, the EALA Organising Committee suspended the netball games owing to time constraints vis a vis the number of protests received from both the Parliament of Uganda and the Parliament of Tanzania over fielding of staff players, perceived to be active professional players. 
   Parliament of Uganda protested against the fielding of Ms. Imelda Hango on December 8, 2014. 
   According to the appeal, the player in question who is a staff member of the Parliament of Tanzania played in the 1st division netball league as a goal attacker of Police Dodoma. 
   The letter signed by Uganda’s team manager, Hon Kiiza Winnie, also states that she played in the 2013 FIBA Africa Basketball championship. On December 11, 2014, Parliament of Tanzania on its part through a letter signed by team captain, Hon Halima J Mdee, protested against Elizabeth Namuhenge saying she was a national player and had played for a club, NBC in Uganda. 
   The rules governing the Inter-Parliamentary Netball games bar from participation, any staff member who plays the game at an active/professional level. 
  Such privilege at the moment is the preserve of Parliamentarians only. During the awards, EALA’s Taslima Twaha was awarded the Most Valuable Player (MVP) while Hon Muhammad Nsereko earned the golden boot (top scorer) after scoring 4 goals. 
   Parliament of Burundi won the Fair Play/Most disciplined team of the tournament. Parliament of Tanzania won the women and men’s tug of war as well as the women’s athletics championship. Parliament of Kenya meanwhile bagged the Athletics’ men category.
  Hon Abdullah Saadala, Deputy Minister for EAC, Tanzania is introduced to Hon Ken Kiyingi Bbosa, of Parliament of Uganda by the captain, Hon Nsanja Patrick.  Uganda beat Tanzania 2-1 in an entertaining final 

  Part of the action in the game

  The Deputy Minister of EAC, Tanzania, Hon Dr. Abdullah Sadala presents the winners trophy to Uganda's Captain, Hon Nsanja Patrick  0 0

  Rais Mstaafu wa awamu ya pili nchini Tanzania,Alhaj Ali Hassan Mwinyi ametembelea miradi mbalimbali ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo aliweza kutembelea na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni, daraja ambalo linategemea kukamilika mwezi wa saba mwaka 2015 na vilevile amepata nafasi ya kutembelea Ujenzi wa nyumba za shirika la NSSF ambao unaendelea katika eneo la Mtoni Kijichi Kigamboni na baadhi ya nyumba hizo zimeishauzwa. Pia Rais Mstaafu aliweza kutembelea ujenzi wa mji mpya wa Dege uliopo eneo la Kigamboni jijini Dar.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Injinia Abubakar Rajabu akifafanua jambo baada ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kufanya ziara ya kutembelea ujenzi wa Daraja la Kigamboni,Nyumba za Mtoni Kijichi na Ujenzi wa mji mpya wa Dege.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dk. Ramadhan Dau (wa kwanza kulia) akimweleza jambo Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alipofanya ziara yake kuona ujenzi mkubwa unaodhaminiwa na NSSF.

  BOFYA HAPA PICHA ZAIDI 

  0 0

  Mechi ya Nani Mtani Jembe namba 2 inachezwa jioni hii ya leo Jumamosi Desemba 13,2014 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo inawakutanisha Watani wa Jadi timu za Yanga dhidi ya Simba SC zote za jijini Dar.
  Hadi hivi sasa tunaingia mitamboni Simba inaongoza mabao 2- 0 yaliyotiwa kimiani na Wachezaji Awadhi Juma (dk 30) aliewahi mpira wa faulo uliopigwa na Mshambuliaji Emmanuel Okwi baada ya Kipa wa Yanga,Munishi Dida kuutema,Goli la pili lilifungwa na Elius Maguli (dk 41).

  Kipindi cha pili cha Mchezo kimeanza na Timu ya Yanga walitawala mpira dakika zote za mwanzo wamepoteza nafasi nyingi za wazi, Na kwa upande wa Mashabiki wa Yanga hali ishakuwa tete na wengi wameanza kutolewa kwa machela wakiwa wamepoteza fahamu.

  Mpira umeisha na Simba wanatoka kifua mbele kwa bao 2 - 0 
  ----------------------------------------------------------
  Simba: Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid, Joseph Owino, Donald Musoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Henry Joseph, Amisi Tambwe, Said Hamis na Awadh Juma. 

  Yanga : Juma Kaseja - 29,Mbuyu Twite - 6 ,David Luhende - 3,Nadir Haroub "Cannavaro" - 23(C),Kelvin Yondani "Cotton" - 5, Athuman Idd " Chuji" - 24, Mrisho Ngassa - 17, Frank Domayo - 18, Didier Kavumbagu - 7, Hamis Kiiza - 20, Haruna Niyonzima - 8 
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano wa Vijana wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika kwenye ukumbi wa Eco Sanaa, Mikocheni Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umeandaliwa na Global Power Shift Tanzania Chapter (NPS) kwa kushirikiana na Tanzania Youth Cultural Exchange Network (TYCEN). Picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 671 | 672 | (Page 673) | 674 | 675 | .... | 3272 | newer