Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

kutoka maktaba: Underline a.k.a Sunderland SC enzi hizo....

$
0
0
Naam Underline hao! ( a.k.a Sunderland Sports Club.) Kisukari  ,Durban, Kimimbi, Emmanuel 'Full-up'Arthur Mambeta,Gilbert Mahinya, Ali Kajo, Kibunzi VC10/auYussuf Salum Maleta. Waliochuchumaa Hatibu ,Kilomoni,Choteka,Mbaraka Salum Magembe, Liston na Haji Lesso.  

Wahitimu IJA-Lushoto waaswa kulinda maslahi ya umma

$
0
0
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akihutubua katika mahafali ya 14 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama - Lushoto wilayani Lushoto hivi karibuni.

Wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto (IJA) wameaswa kutumia elimu waliyopata kwa kuwatumikia wananchi kwa uaminifu ili kulinda heshima ya chuo hicho.

Akizungumza hivi karibuni katika mahafali ya 14 ya chuo hicho yaliyofanyika wilayani Lushoto mkoani Tanga, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mheshiwa Angellah Kairuki aliwakumbusha wahitimu hao kuwa waaminifu na kulinda maslahi ya umma popote watakapobahatika kufanya kazi.

“Nitumie fursa hii kuwaasa sana wahitimu kwamba, popote mtakapobahatika kupata kufanya kazi, fanyeni kazi kwa umahiri mkubwa na kwa uaminifu, kwa wakati na kulinda maslahi ya umma wa Tanzania na hivyo kubeba taswira nzuri ya Chuo ipasavyo,” alisema Naibu Waziri Kairuki katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chuo hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Jaji Mstaafu John Mrosso.


Wateja wa TTCL Kununua Salio Kupitia ‘Mobile Banking’

$
0
0
KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) sasa imerahisisha upatikanaji wa vocha zake baada ya kuingia makubaliano kuishirikiano na benki 13 nchini zinazotoa huduma zake pia kwa kupitia simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo sasa mteja wa TTCL ataweza kuongeza salio kupitia simu yake ya mkononi (TTCL top-up).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere alisema huduma hiyo ya kununua salio kwa njia ya simu kupitia mabenki 13 imeanza kufanya kazi hivi sasa hivyo mteja wa TTCL anaweza kununua salio lake popote alipo kwa kutumia simu yake.

Alisema TTCL imeingia makubaliano ya kiushirikiano katika uuzaji wa muda wa maongezi kwa benki za Standard Chartered, Akiba Commercial (ACB), Tanzania Postal Bank (TPB), Exim Bank, Dar Es Salaam Community Bank (DCB), Mkombozi Bank, KCB Bank pamoja na Bank of Africa ambazo wateja wa beki hizo wanaweza kununua salio kupitia simu zao popote walipo kwenye akaunti zao.

“…Jumla ya benki 13 zimeingia ubia wa kibiashara na TTCL kwa ajili ya kuuza vocha za TTCL kupitia benki zao…hapo juu nimetaja majina ya benki zote ambazo zinatumika kwa ajili ya kufanya miamala mbalimbali ikiwemo TTCL TOP-UP,” alisema Bw. Bizere.

Akifafanua zaidi juu ya huduma hiyo Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla alisema huduma ya TTCL TOP-UP na Mobile banking ni njia ambayo TTCL imeanzisha kwa wateja wake kwa ajili ya kuongeza salio la muda wa maongezi kwa simu za mezani, mkononi na kununua vifurushi vya intaneti hivyo mteja ataweza kununua salio lake muda wowote na popote.

“…Mteja atakayenufaika na huduma hii ni yule mwenye akaunti ya benki, na amejisajili katika huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi yaani 'mobile banking'. Hata hivyo alisema ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma kwa wateja wa wao vocha za TTCL pia zinapatikana katika vituo vya Maxmalipo na Selcom ‘wireless Point’ na kwenye Ofisi za TTCL, pamoja na vituo vya huduma kwa wateja ambako viko katika kila mkoa na wilaya.
Meneja Mipango na Mauzo wa TTCL, Benjamin Bizere (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa huduma ya kuongeza salio kwa kupitia simu za mkononi (Mobile Banking) ambapo sasa mteja wa TTCL ataweza kuongeza salio kupitia simu yake ya mkononi (TTCL top-up). Wengine pichani ni Mkuu wa Mauzo wa TTCL, William Chamla (katikati) na Ofisa Habari wa TTCL, Edwin Mashasi

Tanzania yasaini mkataba wa Sh. bilioni 15.5 kutoka benki ya ADB kuboresha kituo cha utafiti MUHAS.

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile (kushoto) akisaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero akisaini mkataba huo kwa niaba ya Rais wa benki hiyo Dkt. Donald Kaberuka.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando (kushoto) akitoa neno la shukurani baada ya kusainiwa  Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero na katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile.

 Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam wakati wa kusaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
(Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO).

Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
12/12/2014.
Serikali ya Tanzania imetiliana saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 9.4 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 15.5 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Mkataba huo wa makubaliano umesainiwa leo jijini Dara es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero kwa niaba ya Rais wa benki hiyo Dkt. Donald Kaberuka.

Dkt. Likwelile alisema kuwa kituo hicho kitasaidia kupunguza tatizo la wataalam wa afya nchini na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na hivyo kupunguza idadi kubwa ya  wagonjwa wanaotibiwa nje ya nchi.

Kwa upande wake Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero ameipongeza Tanzania kuwa nchi ya kwanza kusaini mkataba huo kati ya nchi nne za jumuiya ya EAC zinazokusudiwa kujenga kituo kama hicho.

Bi Tonia alisema kuwa benki ya ADB imejiwekea lengo kuboresha rasilimali watu katika fani ya afya ambapo mradi wa ujenzi wa kituo kinachojengwa MUHAS upo katika mkakati wa benki hiyo ambao uulianza 2011 hadi 2015, mpango mkakati wa benki wa 2013 hadi 2017 na mfumo mpya wa elimu katka nchi za Afrika.

Mfumo huo unalenga kutatua tatizo la utaalaam katika soko la ajira kwa kupitia vituo bora vya kanda vya afya ili kuendana na dira ya maendeleo ya Taifa na mkakati wa kupunguza umasikini ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mbando ameushukuru uongozi wa benki ya ADB kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuahidi fedha hizo zitatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.

Hadi kukamilika kwa kituo hicho cha afya kinachojengwa katika chuo cha MUHAS kitagharimiwa na benki ya ADB kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

Tanzania and U.S. unite to combat poaching and wildlife trafficking in the Ruaha landscape

$
0
0
U.S. Ambassador Mark Childress (left) and Minister of Natural Resources and Tourism Lazaro Nyalandu (second from left) receive a demonstration of the Spacial Monitoring and Reporting Tool (SMART) at the launch of the USAID supported SHARPP Program in the Ruaha National Park on Wednesday, December 10, 2014. SMART is a new and improved tool for measuring, evaluating, and improving the effectiveness of wildlife law enforcement patrols and site-based conservation activities.

WAZAZI WA MISS TANZANIA 2O13 WAELEKEA LONDON KUMPA SAPOTI MTOTO WAO

$
0
0

shangingi lapigwa kiberiti baada ya kugonga na kuuwa madereva watatu wa bodaboda jijini Dar es salaam leo

$
0
0
Gari aina ya Toyota VX likiwaka moto baada ya kuchomwa na wananchi mchana leo huko Bunju B jijini Dar kwa kusababisha ajali na kuuwa madereva watatu wa bodaboda. 
Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya gari aina ya Toyota VX imeua madereva watatu wa bodaboda mchana leo. Picha na GPL

Balozi marmo awasilisha hati za utambulisho wa rais wa austria

$
0
0
  Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Balozi Philip Sang'ka Marmo  akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Austria Mhe. Heinz Fischer katika Ikulu ya Vienna, Austria. Balozi Marmo anawakilisha pia Austria akiwa Ujerumani.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Balozi Philip Sang'ka Marmo  akiongea na wenyeji wake baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho katika Ikulu ya Vienna, Austria.

Mabalozi mbalimbali wakisaini kitabu cha maombolezo ofisi za ubalozi wa Palestina kufuatia kifo cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais nchini Palestina, Ziad Abu Ein

$
0
0
 Balozi wa Sudan nchini, Dr Yassir Mohamed Ali akijiandaa kusaini kitabu cha maombolezo ofisi za ubalozi wa Palestina Tanzania eneo la upanga Dar es Salaam leo, kufuatia kifo cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais nchini Palestina, Ziad Abu Ein, aliyefariki Jumatano wiki hii
Balozi wa Iran nchini, Mehd Aghajafari akisaini kitabu cha maombolezo ofisi za ubalozi wa Palestina Tanzania eneo la upanga Dar es Salaam leo, kufuatia kifo cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais nchini Palestina, Ziad Abu Ein, aliyefariki Jumatano wiki hii
 Balozi wa Syria nchini Abdulmonen Annan akisaini kitabu cha maombolezo ofisi za ubalozi wa Palestina Tanzania eneo la upanga Dar es Salaam leo, kufuatia kifo cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais nchini Palestina, Ziad Abu Ein, aliyefariki Jumatano wiki hii
Balozi wa Yemen nchini, Abdullah Almir akisaini kitabu cha maombolezo ofisi za ubalozi wa Palestina Tanzania eneo la upanga Dar es Salaam leo, kufuatia kifo cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais nchini Palestina, Ziad Abu Ein, aliyefariki Jumatano wiki hii.

msako wa KARAFUU CHAFU kisiwani PEMBA wapamba moto

$
0
0
 Afisa mdhamini shirika la biashara la taifa Zanzibar ZSTC Pemba Abdalla Ali Ussi (kulia), akiwa na mkulima wa zao la karafuu Khatib Suleiman Amour, ambae anadaiwa kuchanganya karafuu na makonyo na kugundulika na watendaji wa ZSTC wa Finya, wilaya ya Micheweni
 
 Mpimaji wa karafuu wa kituo cha mauzo ya zao hilo, Wete Pemba,  Kitwana Salim Kitwana, akipima karafuu hizo kituoni hapo. 
 Wananchi waliokodi shamba la mikarafuu la serikali eneo la Makuwe wilaya ya Micheweni Pemba, ambao kwa sasa wamekosa majamvi maalumu ya kuanikia na kusababisha kuanika kwenye maturubali ya plasitiki, ambayo husababisha kupoteza ubora wake
 
Ofisa Mdhamini wa ZSTC Pemba Abdalla Ali Ussi akikagua karafuu za wananchi waliokodi shamba la mikarafuu la serikali, ambapo wananchi hao kwa sasa wanahitaji kupatiwa majmvi ya kuanika ili kuepusha karafuu zao kuharibika. Picha zote na Haji Nassor, Pemba

VYOMBO YA HABARI VINA UWEZO WA KUZUIA AU KUWA CHANZO CHA MACHAFUKO.

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, New York 
 Imeelezwa kuwa waandishi wa habari pamoja na vyombo wanavyofanyia kazi wana nafasi kubwa ya ama kuchochea uibukaji wa machafuko katika nchi zao au kuyazuia kwa kutumia kalamu zao. 
Hayo yameelezwa siku ya Alhamis hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfumo mpya wa uchambuzi unaolenga kutathmini viashiria hatarishi vya uhalifu, mauaji ya kimbari ,uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita 
Hafla ya uzinduzi wa mfumo huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mauaji ya kimbari na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu wajibu wa kuwalinda raia (R2P) iliandaliwa kwa ushirikiano wa Wakilishi za Kudumu za Tanzania na Italia katika Umoja wa Mataifa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji wa mauaji ya Kimbari na ulinzi wa Raia. Uzinduzi uliohudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson.
 Mfumo huo( framework of Analysis for Atrocity Crimes, a tool for prevention) pamoja na mambo mengine licha ya kutoa ufafanuzi, tafsri na maelezo ya kina kuhusu viashiria na mazingira ambayo yanaweza kupelekea au kusababisha mauaji ya halaiki au kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa makosa ya kivita unapanua wigo wa kuvishirikisha vyombo vya habari na asasi za kiraia kama wadau muhimu wa si tu kufanya tathmini ya awari ya viashiria hivyo lakini ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za mapema za kuuzia kuibuka kwa matatizo hayo katika jamii. Vyombo vya habari na Asasi za kiraia vinaelezwa kama wadau muhimu licha ya ukweli kwamba wajibu wa kwanza wa kuzuia machafuko ya aina yoyote ile pamoja na kutoa ulinzi wa raia ni wa serikali kuu. 
 Na kwa sababu hiyo imeshauriwa kuwa waandishi wa habari wanapashwa kwanza kutambua vyema viashiria hatarishi dhidi ya Amani na usalama na kuwa nyenzo muhimu ya kuzuia kuibuka kwa uhalifu huo badala ya kuwa sehemu ya uhalifu huo. 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson amesema , mwaka 2014 umeshuhudia umwagaji mkubwa wa damu kuliko miaka mingine yoyote. 
Amesema hali hiyo inatoka na ama kwa Jumuiya ya Kimataifa kutotambua mapema na katika hatua za awali za dalili ya kutokea uhalifu na uhalifu dhidi ya binadamu au ni kwa jumuiya ya kimataifa kutofautiana kimtazamo na kimaslahi kuhusu njia muafaka za kuzuia uhalifu huo. 
Akasema uzinduzi wa mfumo huo unatoa fursa kwa serikali na wadau wengine ya kutambua mapema viashiria vya uwepo wa mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binafamu na uhalifu wa kivita. Lakini kubwa na la msingi anasema ni kuzuia uhalifu huo kabla haujatokea. 
Amesisisitiza kuwa uhalifu dhidi ya binadamu hauibuki mara moja, bali ni jambo linalokuwa limepangwa na kuandaliwa kwa muda mrefu ukiwashirikisha wadau mbalimbali. 
Amesema hali ilivyo hivi sasa ni kwamba jumuiya ya kimataifa imejikuta ikijikita zaidi katik a kushughulikia matatizo ambayo tayari yameshajitokeza badala ya kuyazuia katika hatua za awali hali inayosabibisha kutumia gharama kubwa zaidi. 
Kwa upande wake Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi, pamoja na kuelezea umuhimu na manufaa ya mfumo huo wa tathmini ya viashiria vya uwepo wa mazingira hatarishi. Amesema Tanzania inaunga mkono ushirikishwaji wa wadau mbalimbali kama sehemu muhimu katika eneo zima la Amani, usalama na ulinzi wa raia.
 Hata hivyo ametahadharisha kuwa pamoja na kutambua mchango wa wadau wengine, ni vema basi pawepo na utaratibu wa uwajibikaji wa wadau hao ikiwa ni pamoja usimamizi lengo likiwa ni uwajibikani kama baadhi ya wadau hao wanakuwa chanzo au chachu cha machafuko hayo.
 Aidha Balozi Mwinyi amesema Tanzania ni rafiki wa mchakato huo wa wajibu wa kuwalida raia (R2P). Lakini ni ukweli usionpingika kuwa dhana hiyo ya wajibu wa kuwalinda raia bado imegubikwa na utatamwingi na kwamba kwa nchi nyingi hususani za afrika bado dhana hiyo haijakubalika au haijapokelewa vema. 
Amesema sababu ya kutopokelewa vema kwa dhana hiyo na waafrika kunatokana na ukweli kuwa dhana hiyo inalenga zaidi katika kuingilia masualaya ndani ya nchi husika na pia ni dhana inayolenga katika kuleta mabadiliko ya kiuongozi katika nchi husika ( regime change). Na kwa sababu hiyo, Mwakilishi huyo wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa amesisitiza haja na umuhimu wa kuwapo na usimamizi na utambuzi maalumu kuhusu dhana hiyo ya wajibu wa kulinda raia bila ya kuingilia uhuru wa nchi husika. 
Katika uzinduzi huo, baadhi ya wachangiaji wa mfumo huo wa thathmini pamoja na dhana ya R2P akiwamo Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anayehusika na masuala ya uzuiaji wa mauaji ya kimbari, Bw. Adama Dieng wameielezea Tanzania kama nchi ambayo ni kielelezo halisi cha Amani, usalama na utulivu ikilinganishwa na mataifa mengine Barani Afrika. 
Akizungumzia wajibu wa vyombo vya habari katika kuzuia machafuko ambayo yanaweza kupelekea kutoka kwa matukio ya uhalifu na makosa ya jinai dhidi ya binadamu. Bi, Agnes kut Callamard kutoka Chuo Kikuu cha Columbia. Amesisitiza haja na umuhimu kwa waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi zao huku akitilia mkazo utendaji kazi huru wa vyombo hivyo ikiwa ni pamoja na haki ya kupata habari na kusambaza habari. 
Amesisitiza kuwa uzoefu umeonyesa kuwa sehemu nyingi ambapo kumetokea machafuko, vyombo vya habari vimebainika kuchangia kwa asilimia kubwa uwepo wa hali hiyo. Naye B.i Peggy Hicks kutoka Human Rights Watch akizungumzia kuhusu nafasi ya asasi zisizo za kiserikali pamoja na mambo mengine amesema kuwa Tanzania ina mfumo mzuri unaoziwezesha asasi zisizo za kiserikali kutekeleza majukumu yao pasipo kuingiliwa sana na serikali kuu. Na kusisitiza asasi hizo za tanzania hazihitaji kujifunza kutoka nje juu ya utekelezaji wa majukumu yao. 
Aidha katika uzinduzi huo Tanzania imeelezwa pia kuwa Taifa ambalo kumekuwapo na ustawi, maridhiano na kuvumiliana kwa hali ya juu baina ya madhehebu mbalimba ya dini. `
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson akizungumza  wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa thathmini na utambuzi wa viashiria vinavyoweza kama visipodhibitiwa mapema kuleta uhalifu, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita. uzinduzi huo umefanyika  siku ya  Alhamisi hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
  Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa  Balozi Ramadhan Mwinyi  akizungumza wakati wa hafla hiyo ambayo iliandaliwa kwa pamoja na  Wakilishi za Kudumu za Tanzania na Italia katika Umoja wa Mataifa pamoja na  Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuzuia mauaji ya Kimbari na Wajibu wa Kulinda Raia
Sehemu ya Washiriki wa  uzinduzi huo ambapo  mkazo mkubwa ulikuwa ni ushiriki wa wadau wengine kama vile vyombo vya habari na asasi zisizo za kiserikali na wajibu wao katika utambuzi wa  viashiria vya uvunjifu wa amani na hatua mbalimbali ambazo vyombo hiyo vinaweza kusaidia kuzuia  uvunjifu huo

TPDC yachangia ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari za Mtwara vijijini.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Ndg, Wilman Ndile akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Kaimu Meneja Mawasiliano wa TPDC, Bi. Venosa Ngowi wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya. TPDC imechangia ujenzi wa maabara kwa shule za sekondari za Mtwara vijijini. 

MAMA SALMA KIKWETE AFANYA KAMPENI KATIKA KATA ZA CHIKONJI NA MINGOYO HUKO LINDI MJINI

$
0
0

 Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi wa Kata ya Chikonji wakati alipofika kwenye Makao Makuu ya Kata hiyo kwa ajili ya mkutano wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini tarehe 14.12.2014.
 Mamia ya wananchi waliofurika katika mkutano wa kampeni ulifanyika katika Kata ya Chikonji iliyoko katika Wilaya ya Lindi Mjini na kuhutubiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mama Salma Kikwete tarehe 12.12.2014.
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijiandaa kupokea kadi kutoka kwa Ndugu Abdallah Mohammed Kilimbalimba aliyekuwa mwanachama wa Chama Cha Wananchi (CUF) ambaye aliamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi wakati wa mkutano wa kampeni huko Chikonji katika Wilaya ya Lindi Mjini
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa Kata ya Chikonji kwenye mkutano wa kampeni ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini tarehe 14.12.2014.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

ankal akutana na magwiji wa teknohama wa Maktech ambao ingawa hawavumi lakini wamo....

$
0
0
Leo Ankal amepata bahati ya kukutana na Maktech, kampuni inayojishughulisha na kutatua changamoto na kuweka mambo sawa katika uhandisi wa  TEKNOHAMA Tanzania. Pichani na Ankal akiwa na baadhi tu ya wadau wa Maktech ambao walimkaribisha kwa chakula cha mchana Ijumaa na kubadilishana naye mawazo.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DR. ALI MOHAMMED SHEIN MGENI RASMI TUZO ZA TASWA USIKU HUU

$
0
0

0001

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Ali Mohammed Shein akikabidhi tuzo ya heshima ya mwanamichezo bora wa mwaka kwa Mama Fatma Karume Mjane wa Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliyotolewa na Chama cha Waandishi wa habari za Michezo TASWA kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Usiku huu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo TASWA Bw. Juma Pinto.)
003
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Ali Mohammed Shein akisoma hotuba yake mara baada ya kukabidhi tuzo hiyo kwa Mama Fatma Karume Mjane wa Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam usiku huu.
0002
Mama Fatma Karume  akitoa nasaha zake kwa wanamichezo usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo TASWA Bw. Juma Pinto na Maulid  Baraka wa Kitenge Mtangazaji wa Redio ya EFM ambaye alikuwa MC wa hafla hiyo.

Maandalizi ya USIKU WA LUIZA MBUTU utaofanyika desemba 20, 2014 mango garden yapamba moto, komandoo hamza kalala ndani

$
0
0
Luiza Nyoni-Mbutu akipozi  na mumewe Farijala Mbutu ambaye ni mtoto wa mwanamuziki wa zamani wa Orchestra Makassy Marehemu Mzee Simaro Aimala Mbutu. Farijala  pia ni mwanamuziki hodari akiwa na Kilimanjaro Connection ambayo inapiga muziki ndani na nje ya nchi.
KIONGOZI wa bendi  mpya  ya Utalii Jazz Band ambaye pia mwanamuziki Mkongwe wa muziki wa dansi nchini ‘Komandoo Hamza kalala ama unaweza kumwita Mzee wa Madongo’ amethibitisha kushiriki katika onesho maalum  la miaka 16  ya mwanamuziki Luizer Mbutu kuwa Twanga Pepeta.
Mkurugenzi wa Kampuni ya  The African  Stars Entertainment (ASET)  Asha Baraka amesema kwamba  Komandoo tayari amethibitisha kushiriki na hivyo usiku huo utakaofanyika  Desemba 20 ndani ya ukumbi wa Mango Garden utakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakongwe.
Pia alimtaja Stara Thomas ‘Stara T’ , Siza Mazongera 'Mamaa wa Segere’, pia wanafanya mazungumzo na wasanii mbalimbali ambao waliwahi kufanya kazi na Mbutu tangu bendi  hiyo ilipoanzishwa  kama vile Bob Gaddy, Banza Stone, Adolph Mbinga  na wengineo.
 Asha Baraka amesema kuwa wameandaa onyesho hilo ambalo litakua maalum kwa Kiongozi wa bendi hiyo ambaye anaetimiza miaka 16 ndani ya bendi bila kuhama tangu ilipoanzishwa.
“Uongozi wa ASET umeamua kuandaa usiku maalum wa kumuenzi Luiza kutokana na kua na msimamamo wa kukaa katika bendi kwa muda wote huo bila kuhama hilo ni jambo la kujivunia” alisema Asha.
Aliongeza kwa kusema kuwa onyesho hilo litakwenda kwa jina la Luiza Mbutu na Twanga Pepeta ambalo pia kutakuwa na shamrashamra zake ambazo zitatajwa siku itakapowadia” alisema Asha.

Pia aliongeza kwa kusema kuwa wao kama ASET wanatambua mchango wa Luiza ndani ya bendi hiyo hivyo kutakuwa na tukio laaina yake ambalo mashabiki na wadau wa bendi hiyo pamoja na wapenzi wa Luiza wajitokeze kwa wingi siku hiyo kushuhudia litakalojiri sambamba na kupata burudani kutoka kwa bendi ya Twanga Pepeta.Kiingilio kitakuwa sh. 10,000.

mambo ya gado

$
0
0
iBrain - You don't need to use your brain anymore!

British charity, UK Police Aid Conveys, gifts Tanzania vital fire fighting and police equipment

$
0
0

British High Commissioner, Dianna Melrose, handed over a variety of fire fighting and police equipment on 11th December on behalf of the UK charity ‘UK Police Aid Conveys’, to Minister Mathias Chikawe, Ministry of Home Affairs and Minister Dr Seif Rashid, Ministry of Health and Social Welfare.
Speaking at the event, Ms Melrose said:
“The donation of these materials demonstrates the collaborative nature of the United Kingdom’s partnership with Tanzania. Today we are handing over a large quantity of different items – from fire fighting and medical items, to police uniforms and protective clothing, and furniture. These goods have been provided by numerous different donors in the UK – by the National Crime Agency, a number of UK Police Forces, the Fire Service, the Ambulance Service, and by hospitals across the United Kingdom. They will benefit Tanzania’s Fire and Police Services and medical centres across the country”.
The goods were organised by UK charity National Police Aid Convoys. The UK Police Aid Convoys is a volunteer charity based in the UK that collects, sorts and then dispatches this sort of development aid to communities all over the world.
Wanda Adams, the secretary of the UK Police Aid Convoys charity said:
“I am delighted to see everything delivered safely in Tanzania and look forward to news of its reception and utilisation.  We would like to express our thanks to the National Crime Agency in the UK and to Songas Ltd in Dar es Salaam for supporting the costs of importing the containers to Tanzania  Thanks also to the  National Police Aid Convoys in the UK for selecting Tanzania and Zanzibar to be the benefactors of this equipment.”
Speaking on behalf of Songas Ltd Nicodemus Chipakapaka said:
“Songas is proud to play a part in supporting this strong collaborative partnership between the United Kingdom and United Republic of Tanzania. These contributions will be of immediate benefit to the Police, Fire and Medical services and hence to people of Tanzania”.
A further 42 foot container of emergency services equipment is in the process of being prepared for handover to authorities in Zanzibar shortly.
The donation represents a small part of the wider programme of partnership working that is achieved on a daily basis between the UK and Tanzanian institutions, but is demonstrative of the collaborative approach that we believe provides the most benefit to both nations’.
 HC Dianna Melrose from The British High Commission-Dar, Minister Mathias Chikawe from Ministry of Home Affairs and Representatives from Police Force
 HC Dianna Melrose shake hands with Minister Mathias Chikawe after handling over of equipments

HC Dianna Melrose, The British High Commission Dar hand-over equipment to Police Force

WENYEVITI WA TAIFA WA VYAMA VYA NCCR -MAGEUZI ,JAMES MBATIA NA AGUSTINE MREMA WA TLP WAWANADI WAGOMBEA WAO JIMBONI VUNJO.

$
0
0
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi akiendelea na mikutano ya kampeni katika kijiji cha Kisangesangeni kata ya Kahe akiwanadi wagombea wa nafasi za Uenyekiti.
Msafara wa Pikipiki ukiongoza kuelekea kijiji cha Ngaseni kwa ajili ya mikutano ya kampeni ya chama cha NCCR-Mageuzi.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MANISPAA YA KINONDONI YAZINDUA HUDUMA YA BURE YA INTERNETI KWENYE KITUO KIPYA CHA DALADALA CHA SINZA

$
0
0

Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, imedhihirisha jitihada zake za kwenda na wakati katika huduma zake, baada ya kuamua kutoa huduma ya bure ya mtandao wa intrenet wa WiFi kwenye Kituo kipya cha Mabasi cha Sinza, jijini Dar es Salaam.

Akizindua huduma hiyo, jana, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda alisema, mtandao wa WiFi umeunganishwa kwenye kituo hicho kupitia mkongo wa mawasiliano kupitia Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Mwenda alisema, mtandao huo utakuwepo usiku na mchana na kila mwenye kompyuta au simu zenye uwezo wa kunasa Wi-Fi ataona katika simu au kompyuta yake akitaarifiwa kuwepo mtandao wa bure wa KMC_FREE WiFi.

Alisema, mdau atakachofanya ni kujinga bure na kuendelea kupata taarifa mbalimbali zikiwemo za tovuti ya serikali na ya Manispaa hiyo ya Kinondoni na nyingine zote atakazotaka.

Mwenda alisema, baada ya kuweka mtandao kwenye Kituo hicho, mwakani Manispaa hiyo itaweka mtandao huo wa WiFi kwenye Kata zote 34 za Manispaa hiyo.

Alisema, mradi huo wa WiFi umegharimu sh. milioni 21, na Manispaa hiyo itakuwa ikiendelea kulipia huduma hiyo sh. milioni 2 kila mwezi ambazo itakuwa inalipa kwa mkupuo kwa mwaka. 


Kuzinduliwa kwa huduma hiyo, kumeifanya Manispaa ya Kinondoni kuwa ya kwanza nchini kote, na pengine hata Afrika Mashiriki, kutoa huduma hiyo bure tena bila kutumia namba ya siri.

Mwandishi wa habari hii alishuhudia huduma ya aina hii kwa mara ya kwanza alipotembelea nchini China, ambapo WiFi inapatikana bure kwenye simu hata ukiwa barabarani.

 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yussuf Mwenda akibofya kompyuta kuzindua huduma ya WiFi ya bure kwenye Kituo cha Mabasi cha Sinza, wilayani humo, Ijumaa, Desemba 12, 2014
 Mwenda akizungumza baada ya kuzindua huduma hiyo
 Mwenda akikata utepe kwenye chumba ilimo mitambo ya kuendesha mtandao huo wa huduma ya WiFi kwenye Ofisi za Kituo hicho cha mabasi
 Baadhi ya wafanyakazi katika ofisi hiyo yenye kugawa WiFi
 Kweli: "WiFi ya Manispaa ya Kinondoni inapatikana bure! vijana wakisema baada ya kuipata WiFi iliyozinduliwa kwenye Kituo hicho cha Mabasi 
 Vibao vinavyoonyesha Mabasi yaendeko  kutoka kwenye Kituo hicho
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images