Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 666 | 667 | (Page 668) | 669 | 670 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Mshambuliaji Danny Mrwanda amemwaga wino wa kuitumikia klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam kwa mkataba wa mwaka mmoja usiku huu.

  Yanga imewafanyia umafia watani zao wa jadi Simba,ambayo ilionyesha nia kubwa ya kumuhitaji Mrwanda ikiwa ni kwa hudi na uvumba na tayari
  ilishatangaza nia yake hiyo ya kutaka kumsajili.

  Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kinasema kuwa,Yanga imeamua kumsajili Mrwanda kuchukua nafasi ya Said Bahanuzi aliyetolewa kwa mkopo kwenda Polisi Morogoro wakati Jerry Tegete akiwa ni majeruhi,na mshambuliaji pekee wa ndani wanayemtegemea ni Hussein Javu.

  0 0

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Novemba, 2014 umepungua hadi kufikia asilimia 5.8 kutoka 5.9 iliyokuwepo mwezi Oktoba ,2014 kutokana na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa na huduma katika maeneo mbalimbali nchini.

  Akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa  waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa  Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa kupungu kwa mfumuko wa Bei nchini kumesababishwa na kupungua kwa bei za bidhaa za vyakula na zile zisizo za vyakula. 

  Amezitaja bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kuwa ni pamoja na Unga wa mahindi , unga wa ngano, tambi na vyakula vya lishe kwa watoto.


  Bidhaa nyingine ni mavazi ya wanaume zikiwemo suti, suruali, sare za shule na viatu vya wanaume huku bidhaa za gesi, mafuta ya taa, mkaa, mazulia, vyandarua pamoja na simu na saa za mkononi zikichangia kwa asilimia 17.2.

  Kuhusu Fahirisi za bei kwa maana ya kiwango cha badiliko la kasi ya bei  za makundi ya bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na Kaya binafsi kwa kuzingatia kipimo cha mwezi amesema kuwa zimeongezeka hadi kufikia 150.54 mwezi Novemba kutoka 149.70 za mwezi Oktoba, 2014.

  Amefafanua kuwa kuongezeka kwa Fahirisi hizo kumechangiwa na ongezeko la bei ya bidhaa za vyakula hususan mchele, vitafunwa vinavyotokana na unga wa ngano,samaki, matunda,mbogamboka,viazi mviringo, mihogo na viazi vitamu.

  Akizungumzia uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Novemba , 2014 amesema kuwa umefikia shilingi 66 na senti 43. 

  “Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma kwa mlaji umepungua ,hii inamaanisha  mtu anahitaji kuongeza ziada  ya shilingi 33 ili aweze kununua bidhaa na huduma zilezile anazozihitaji”

  Kwa upande wa mfumuko wa Bei wa mwezi Novemba 2014 katika nchi za Afrika Mashariki amesema  kuwa una mwelekeo unaofanana , Kenya ukipungua  kwa asilimia 6.04 kutoka asilimia 6.43 za mwezi Oktoba, Uganda  mfumuko wa bei ukiongezeka hadi asilimia 2.1 kutoka asilimia 1.8 za mwezi Oktoba.
  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Novemba, 2014 leo jijini Dar es salaam.

  0 0
 • 12/08/14--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • Kesh  ft. Davido, Olamide - Shoki

  0 0

   Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiinua juu bango linalonadi UHURU KAMILI miaka 53 iliyopita. Leo ni sikukuu ya kukumbuka siku hii adhimu
  Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwasili uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kujiunga na wananchi kusherehekea sikukuu ya Uhuru miaka 53 iliyopita.

  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi  Ngoma Africa Band almaarufu FFU-Ughaibuni yenye makao nchini Ujerumani,inawatakia kila la heri katika kusherehekea miaka 53 ya Uhuru . Salam hizi za heri ya 9 Disemba ziwafikie watanzania wote walio nyumbani na nje ya nchi.Ngoma Africa band chini ya uongozi wake Kamanda ras Makunja unaweza kuwasikiliza pia katika kambi yao ya FFU-ughaibuni bofya http://www.ngoma-africa.com   pia at https://itunes.apple.com/album/id947329929 au 

  0 0

  SAM_0616
  Wachezaji wa Tanzania na Kenya wakiwa katika mashindano ya wabunge wa jumuiya ya Afrika mashariki leo,  katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha, mechi hiyo ilivuta hisia za wakazi wa jiji hilo waliomiminika kuja kushuhudia wabunge hao wakimenyana uwanjani, baada ya dakika ya tano bunge la kenya walijipatia bao la kwanza, bao lililofungwa na Mh.Steven Nyatta na hatimaye Tanzania kusawazisha dakika ya 24 kwa njia ya penalt baada ya Mh.Mbunge Joshua Nassari kudondoshwa eneo la hatari kwa kugongwa na mlinda mlango wa kenya Kega Kanin.
  SAM_0003
  Mlinda mlango wa Timu ya kenya Kega Kanin akijaribu kuzuia goli lililopatikana kwa njia ya penalt katika dakika ya 24 .
  SAM_0018
  Naibu Waziri   wa  Fedha   Adam  Malima akichechemea uwanjani baada ya kuanguka na kupewa huduma ya kwanza.
  SAM_0012
  Wachezaji wa timu ya Tanzania wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza
  SAM_0013
  Wachezaji wa timu ya Kenya wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza.

  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi Ngoma Africa Band almaarufu FFU-Ughaibuni yenye makao nchini Ujerumani,inawatakia kila la heri katika kusherehekea miaka 53 ya Uhuru . Salam hizi za heri ya 9 Disemba ziwafikie watanzania wote walio nyumbani na nje ya nchi.Ngoma Africa band chini ya uongozi wake Kamanda ras Makunja unaweza kuwasikiliza pia katika kambi yao ya FFU-ughaibuni bofya http://www.ngoma-africa.com pia at https://itunes.apple.com/album/id947329929 au http://play.spotify.com/album/4kG86JgvuyWQtgCPCPmCkY

  0 0
 • 12/08/14--23:51: DMV All Stars - Najivunia
 • Disemba 9, 2014 ni siku ya uhuru wa Tanganyika. Wakati taifa la Tanzania linaadhiminisha miaka 53 ya uhuru, tunapenda kuwasilisha rasmi wimbo “Najivunia”. Wimbo “Najivunia” umetungwa na kurekodiwa Maryland, USA na kundi la wasanii wa Kitanzania waishia Marekani kwa ushirikiano na DMK Global Promotions kuadhimisha miaka 53 ya uhuru wa Tanzania.
  Wasanii wenyewe ni:

  DMV All Stars:

  Mr.Tz aka SanTized
  Prince Herry
  Dominic
  E-Breezy (Ibra. Max)
  AJ Ubao

  0 0

  Mdau Edward Mwambopo na mai waifu wake Anitha Makundi wote wakazi wa jijini Mbeya wakiingia ukumbini kwa madaha wakati wa sherere yao ya kupongezwa na ndugu,jamaa na marafiki mara baada ya kumeremeta kwao.Sherehe hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mkapa,Soko Matola jijini Mbeya.
  Mdau Edward Mwambopo akitoa neno kwa wageni waalikwa.
  Mdau Edward Mwambopo na mai waifu wake Anitha Makundi wakiwa na nyuso za furana na upendo tele katika Sherehe yao ya kupongezwa,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mkapa uliopo Soko Matola,Jijini Mbeya.


  0 0

  Vijana wa Kikundi cha “Hisia Theatre Group” wakionesha ujuzi wao wa sarakasi wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini leo Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
  Mwamuzi wa michezo ya sanaa za maonesho na Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam Delphine Njewele (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwanasheria wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA) Hamisi Tika kwenye banda la PPAA wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe leo jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.


  0 0


  Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya CRDB, Philip Alfred akihutubia wakati wa Mahafali ya 5 ya Chuo Kikuu cha St. John's  Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu)

  Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma, Dickson Chilongani (kushoto), akikabidhiwa na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya CRDB, Philip Alfred, mfano wa hundi na bahasha mara baada ya hotuba. Hundi hiyo ina thamani ya hundi ya sh. milioni 10 ukiwa ni msaada wa benki hiyo kwa Chuo Kikuu cha St. John's wakati wa Mahafali ya 5 ya chuo hicho Mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara,Ndg. Phillip Mangula (wa pili kulia) na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa (CCM),Mh. Pius Msekwa (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgombea wa Nafasi ya uenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Osterbay,Ndg. Zefrin Kimolo Lubuva (wa pili kushoto) mara baada ya uzinduzi wa kampeni za kuwawanadi Wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya CCM katika Mtaa wa Osterbay,zilizofanyika juzi jioni katika Viwanja vya Farasi.
  Mgombea wa Nafasi ya uenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Osterbay,Ndg. Zefrin Kimolo Lubuva (wa pili kulia) akisalimiana na Mh. Anne Abdallah ambaye ni Mbunge na Kiongozi Mwandamizi wa CCM wakati wa uzinduzi wa kampeni za kuwawanadi Wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya CCM katika Mtaa wa Osterbay,zilizofanyika juzi jioni katika Viwanja vya Farasi.
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara,Ndg. Phillip Mangula akimnadi Mgombea wa Nafasi ya uenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Osterbay,Ndg. Zefrin Kimolo Lubuva wakati wa uzinduzi wa kampeni za kuwawanadi Wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya CCM katika Mtaa wa Osterbay,zilizofanyika juzi jioni katika Viwanja vya Farasi.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu, amesema habari zinazodai kuwa Serikali inataka kuwaondoa wakazi wa zaidi ya 40,000 katika eneo la Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha  hazina ukweli wowote.

  Novemba mwaka huu, gazeti The Guardian la nchini Uingereza, liliandika habari kuwa serikali ina mpango wa kuwafukuza Wamasai wanaoishi eneo hilo.

  Gazeti hilo lilidai kuwa, lengo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu.

  Akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai wilayani Ngorongoro mwishoni mwa wiki, Nyalandu alisema habari hizo hazina ukweli wowote isipokuwa zina lengo la kuchafua taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa.

  Aliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi bila hofu, kwa sababu serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye makazi yao.

  “Nami niwahakikishie wanajamii wa Loliondo, Ngorongoro na wanajamii wote wa kimasai ambao wametishiwa nyau, kuwa serikali ya Tanzania haina mpango wowote wa kumfuata na kumfukuza mtu yoyote,” alisema.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akijaribu kurusha mkuki alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akitoka nje ya nyumba ya kimasai alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.


  0 0

  Mganga mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Mtumwa Mwako akizungumza wakati wa ufunguzi wa kambi ya watoto (Ariel camp) wanaopata huduma katika vituo mbalimbali vya afya vinavyosaidiwa na shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI linalofanya kazi katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu.
  Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na watoto, walezi na wafanayakazi wa AGPAHI.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo wa kwanza (kulia) akikata utepe kuzinduzua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu Korogwe mjini, katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.Hafla hiyo imefanyika hivi karibuni.
  Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(kulia)akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo(kushoto)kuhusiana na kifaa cha Router chenye uwezo wa kuunganisha zaidi ya watu nane kutumia huduma ya intaneti wakati wa uzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo mtaa wa manundu wilaya ya Korogwe mjini.Katikati ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu na anaeshuhudia kulia ni Abubakary Lubuva.


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Sikonge Bi.Hanifa Selengu akimkabidhi kadi ya kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii  CHF mmoja kati ya wakulima wa tumbaku katika kijiji cha Kisanga wilayani humo wakati wa kampeni ya Uzinduzi wa mfuko huo. 
  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kisanga waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hiyo ya uhamasishaji kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF wilayani Sikonge.


  0 0

  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade, kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo, Prof Mick Moore, wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha
   Wataalamu wa kimataifa  wa masuala ya kodi  wakiendesha mjadala katika mkutano wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya kodi,mkutano uliofanyika jana  jijini Arusha ,Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Uganda (URA), Milly Nalukwago (kushoto), Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade (katikati) na  Mtaalam wa Kodi wa Uingereza, Rhiannon Mc Cluskey.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Viongozi wa Kitaifa wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.


  0 0

   Kushoto Waziri mh. Fatma  Fereji kutoka Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Kulia Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais mazingira mh.dkt Binilith Mahenge wakifuatilia hotuba ya katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Bw Ban ki Moon hayupo pichani katika ufunguzi wa mkutano wa 20 wa nchi wanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi ulihusisha viongozi wa juu marais na mawaziri..(High level segment) mjini Lima, Peru.
   Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. dkt Gharib Bilal..akisoma Hotuba kumuwakilisha mh Rais Jakaya mrisho KIkwete,ambae ni Rais wa Mazingira Africa (CAHOSSC) katika ufunguzi wa mkutano wa mawaziri na marais (High level segment) uliofunguliwa leo mjini LIma, Peru 
   Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Bw. Ban Ki Moon akisoma hotuma ya ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa mazingira na marais katika mkutano wa high level segment mjini Lima, Peru. Picha na Evelyn Mkokoi


older | 1 | .... | 666 | 667 | (Page 668) | 669 | 670 | .... | 3286 | newer