Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109975 articles
Browse latest View live

yale yaleeeeee: wizi katika mizigo ya abiria uwanja wa ndege huko majuu...


wakongwe wa atomic jazz band waburudisha katika mchaparo wa sherehe za miaka 53 ya uhuru ikulu, dar es salaam

Mhe. MARTHA MLATA AMWAGA SOLA SEKONDARI YA MKALAMA, SINGIDA

$
0
0

Na mwandishi wetu

KERO ya maji safi na salama katika Shule ya Sekondari ya Nduguti wilayani Mkalama, mkoani Singida, imeanza kupatiwa ufumbuzi baada ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa huo Mhe. Martha Mlata, kubeba jukumu la kusaidia.

Mhe Mlata, ambaye amekuwa akishiriki kwenye kusaidia huduma za kijamii kuhususan elimu na afya, ametosa sh. Milioni tatu katika kuhakikisha kero hiyo inapatiwa ufumbuzi.
Awali, wanafunzi walikuwa wakilazimika kukatisha masomo kwa saa 40 kwa mwezi ili kufuata maji umbali mrefu hivyo kukosa masomo.

Akizungumza kwenye mahafali ya Sita ya Shule hiyo ambapo mgeni rasmi alikuwa Martha, Mkuu wa Shule Frank Malile, alisema tatizo la maji limekuwa sugu shuleni hapo.

Hata hivyo, alipongeza msaada huo wa Martha akisema utasaidia kupunguza kero hiyo na kwamba, ni mwanga wa kuelekea kwenye mafanikio ya kero hiyo kubaki historia.

“Shule yetu inakabiliwa na tatizo sugu la maji ambalo hukwmisha shughuli ikiwemo chakula kwa wanafunzi. Maji hufuatwa umbali mrefu na baadhi ya visima yanapopatikana ni vya wazi hivyo kuhatarisha usalama wa wanafunzi wetu,” alisema.

Changamoto nyingine iliyowasilishwa mbele ya Martha ni uhaba wa nyumba za walimu, mabweni ya wanafunzi kutokuwa na madirisha, vitanda, vyoo na ukosefu wa jengo la utawala.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu, Martha alisema nyumba za walimu pamoja na umaliziaji wa majengo ya bweni la wanafunzi wa kike, nguvu za kila mzazi na mlezi zinahitajika.

Pia aliahidi kuwasiliana na uongozi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), ambayo imejikita zaidi kuhakikisha mabweni kwa ajili ya wanafunzi wakiwemo wa kike yanajengwa katika shule mbalimbali nchini.

Martha alisema TEA imeonyesha nia ya dhati ya kuanza kujenga mabweni 30 kwa ajili ya wanafunzi wa kike, ambao ni wahanga wa vitendo viovu katika jamii.

“Serikali imeamua kulivalia njuga suala hili kukomboa mtoto wa kike kutokana na vikwazo anavyopata katika elimu vikiwemo mila potofu kuwatumia watoto wa kike kama chombo duni kisicho na msaada.

Katika mahafali hayo, mbali na kukabidhi sh. Milioni tatu taslim mbunge huyo, miti 50 ya miembe kwa ajili ya kuimarisha mazingira, vifaa vya michezo kwa shule za wanawake na wanaume.

Pia, alikabidhi sola 19 ambazo zitasambazwa kwenye sekondari za kata kwa ajili ya kuwezesha wanafunzi kusoma nyakati za usiku.

TAMASHA LA WAFALME KUWEKA HISTORIA SIKUKUU YA XMAS DAR LIVE

KONGAMANO LA SIKU MBILI LA UKATILI WA JINSIA DHIDI YA WANAWAKE NA WALEMAVU LILILOANDALIWA NA SHIRIKA LA SEED TRUST LAFIKIA TAMATI MKOANI MOROGORO DESEMBA 9-2014

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Seed Trust, Margareth Mkanga (MB) akizungumza katika kongamano hilo. Kulia ni Mwenyekiti wa Shirika hilo, Stephen Mashishanga. Kongamano hilo la Majadiliano kuhusiana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na walemavu limeshirikisha wadau mbalimbali kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania na kuandaliwa na Shirika la Seed Trust la mjini Morogoro kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA).

ngoma azipendazo ankal

$
0
0

Atomic Jazz Band - Tanzania yetu ni nchi ya furaha

JUST IN: TAARIFA YA BODI YA WADHAMINI WA JOHA TRUST KWA WAZAZI NA UMMA KUHUSU MCHANGO WA SHS BILIONI 1.617 KUTOKA KWA BW. JAMES RUGEMALIRA

Twaweza Appoints Aidan Eyakuze as its new Executive Director

$
0
0
Twaweza East Africa today announced the appointment of Aidan Eyakuze as its new Executive Director. Eyakuze, who was selected after an extensive international search, will take up his new post on 1 March, 2015. He will replace Twaweza’s founder and current head, Rakesh Rajani.

Educated as an economist, Eyakuze has been a thought leader on issues of development in East Africa for the past 15 years.  He currently serves as Associate Regional Director of the Society for International Development (SID) and head of the SID Tanzania office. He is a scenario practitioner who has participated in national scenario-building projects in Kenya, Tanzania, South Africa, Nigeria and elsewhere. 

As Director of the SID’s Futures Programme since 2006, Eyakuze has led the publication of the State of East Africa Reports and facilitates futures thinking for private sector, civil society and public organisations. He is an Archbishop Desmond Tutu Leadership Fellow and is a member of the Aspen Global Leadership Network (AGLN). He serves on the Governing Board of the Millennium Challenge Account (Tanzania), ICEA Lion General Insurance Company (Tanzania) and NIC Bank Tanzania Limited. 


VODACOM CHALI KATIKA FAINALI YA LIGI ZA MAKAMPUNI

$
0
0
Mchezaji wa Timu ya Vodacom Tanzania, Osca Coby akiwatoka wachezaji wa Timu ya CRDB katika fainali ya ligi za makampuni iliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Laureate International School jijini Dar es Salaam,CRDB waliilaza Vodacom1-0.
Mchezaji wa Timu ya Vodacom, Carlos Sylvester (kushoto) akitafuta mbinu ya kumtoka mchezaji wa timu ya, BQ CONTRACTORS, Emil Michael katika fainali ya ligi ya makampuni iliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Laureate International School jijini Dar es Salaam,BQ CONTRACTORS ilishinda 3-1.
Ofisa rasilimali watu wa Vodacom Tanzania, Ndihagati Biduga akishangilia baada ya timu yake kupata goli la kufutia machozi wakati wa fainali za makampuni ambapo Vodacom ilishindwa na BQ CONTRACTORS 3-1, mchezo huo uliofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Laureate International School jijini Dar es Salaam.

Wadau wa Sekta ya Afya kutoka Tanzania Washiriki Maonyesho ya Sekta ya Afya jijini Istanbul -Uturuki. Dec 2014.

$
0
0
Washiriki Kumi na Wanne (14) kutoka Tanzania wajumuika na wenzao 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika katika Maonyesho ya Pili Sekta ya Afya chini Uturuki. Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka na kwa lengo la kuendeleza mahusiano na ushirikiano katika kuboresha Sekta ya Afya kwa nchi husika. Maonyesho ya Mwaka huu yalikuwa na washiriki kutoka nchi 60 duniani kote.  Kwa upande wa Afrika mkutano huu ulioratibiwa na kusimamiwa na kampuni ya kuendeleza mahusiano ya maendeleo na biashara kati ya Afrika na Uturuki iitwayo TurkaAfrica Ltd (www.turkafrica.co.tz).
  Waandaaji wa TurkAfrica wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao TUSMSIAD,na Washiriki kutoka Tanzania.
 Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Rashid Seif Suleiman akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Afya wa Uturuki Hon. Mehmet Müezzinoğlu. Kushoto ni Dr. Lulu Fundikira (kutoka Hopitali ya Taifa Muhimbili) akifuatiwa na Mshauri wa mambo ya Uchumi na Maendeleo wa Serikali ya Uturuki ambaye pia ni Raisi wa Taasisi ya Uchumi na Biashara ya Uturuki (TUMSIAD) – Dr. Hassan Sert. Kulia ni Jumanne Simba.
 Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Rashid Seif Suleiman akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa sekta ya Afya wa Serikali ya Uturuki mara baada ya mazungumzo ya njia mbalimbali za kuboresha sekta ya Afya na mahusiano kati ya Serikali ya Uturuki na Tanzania.
 Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Rashid Seif Suleiman akifanya mazungumzo na Waziri wa Afya wa Uturuki Hon. Mehmet Müezzinoğlu. Kushoto ni Dr. Athuman Ngenya na washiriki wengine kutoka Tanzania. 

FID-Q AZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAIFA LETU.

$
0
0
Msanii nguli wa miondoko ya Hip-hop Fareed Kubanda – Fid Q amekutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge katikakati ya jiji la Dar es Salaam, kujadili maswala ya msingi yenye mustakabali chanya kwa maendelo ya taifa hili. Ameitisha mkutano huu akiwa kama kijana na mwenye nafasi na ushawishi kwa vijana wenzie katika ushiriki wa kuleta mabadiliko chanya na maendeleo ya nchi yetu.

Fid Q amesukumwa kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kutanabai kwamba vijana japo ni asilimia 80 ya taifa lakini hawana mwamko na msukumo wa kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi wa viongozi waowataka na wanaowaamini wanauwezo wa kuleta mabadiliko ya ki nidhamu kwenye masuala ya msingi ya taifa letu.

“Kuna kitu kimoja ambacho watu wengi hasa hasa vijana wenzangu hawakifahamu, Nchi yetu ni changa sana. Vijana nchi hii chini ya umri wa miaka 35 ni zaidi ya asilimia 80 ya idadi ya watu, wakati watu wazima zaidi ya miaka 60 ni asilimia chini ya 5 ya watanzania wote. 

Hizi ni takwimu za sensa iliyopita. Nimetanguliza takwimu mapema kwa sababu, twakimu huwa hazisemi uwongo. Changamoto zinalolikumba taifa hili kwa kiasi kikubwa zinatuathiri sisi vijana wa nchi hii ambao ndio wengi wetu. Madhara yanayotokana na uongozi mbovu, vile vile yanatuathiri sana sisi vijana kwa wingi wetu. Tutake tusitake, ustawi na kunawiri kwa vijana ndio kutaamua mustakabali wa Tanzania, vijana tukilala basi na Tanzania pia italala.” Alisema Fid Q.

Bado kuna changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana. Vijana wengi wamezagaa mitaani bila shughuli za kufanya. Hata wale wenye degree hawana kazi. Vijana wanakata tama na kuona kwamba wao sio sehemu ya taifa hili. Kuna changamoto ya viongozi waadilifu watakaosimamia kuhakikisha kwamba keki ya taifa inagawanywa kwa Watanzania wote na hailiwi na wachache.

Baada ya utangulizi huo, ni dhahiri kwamba kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa unaoendelea, na uchaguzi mkuu wa 2015 lazima vijana tuamke na tushiriki kikamilifu. Kwanza, vijana wenye uwezo na sifa za kugombea nafasi za uongozi ni lazima wafanye hivyo, pili vijana wenye vigezo vya kupiga kura pia ni lazima wafanye hivyo maana ni wajibu wetu, tatu, vijana ni lazima tushiriki kikamilifu katika mchakato wa kampeni ili kuhakikisha ishu zetu za msingi zinajadiliwa na wagombea na zinapewa kipaumbele.

Kama vijana wanakuwa na hofu basi niwakumbushe kwamba, Mwalimu Nyerere alikabidhiwa nchi hii akiwa na miaka 39 tu na kuanza harakati za kupigania Uhuru ambao tumeuenzi jana. Alikuwa ni kijana mdogo tu. Mzee wetu Dr. Salim Ahmed Salim alianza kuwa mwanadiplomasia mahiri akiwa na rika dogo tu, akiwa na umri wa miaka 22 alikuwa Balozi wa Tanzania, nchini Misri. Mifano ipo mingi, hivyo vijana tusipate woga – Tumechangia kupatikana kwa Uhuru na kujenga nchi hii, na sasa ni wakati mwingine tena wa kuibadilisha nchi yetu.

“Hivyo mimi Fareed Kubanda, nimeamua kufanya matamasha ili kusimamia haya niliyoyasema hapo juu. Kwa kutumia nafasi zenu ndugu wana habari naomba mnisaidie kutangaza azma yangu hii pamoja na nitawapigia baadhi ya wasanii wenzangu kuwaomba waniunge mkono ili tufanikishe hili na tushiriki katika kuleta uongozi utako leta mabadiliko tunayoyataka na kwa kasi yetu sisi vijana.”

Fid Q aliendelea “Ninatumaini kwamba wasanii wenzangu wataniunga mkono, ili kuanza kuwaamsha vijana wenzetu, tuweze kutimiza wajibu wetu wa kihistoria wa kufanya mabadiliko katika nchi yetu, hasa pale tunapokuwa tunahitajika sana na jamii. Tayari nimefanya mazungumzo na Mkubwa Fela, Babu Tale, Mwana FA, Nick wa Pili, Lamar, P-Funk, Mwasiti, Barnaba, Ditto ambao wamekubali kuwa sehemu ya harakati hizi. Bado nahitaji wasanii wengine wengi washiriki ki mawazao, hali na mali kufikia lengo kuu la Tanzania mpya na bora zaidi”.


Huu ni mwanzo wa harakati hizi, mwakani tutafanya amsha amsha kubwa ya vijana. Mwaka huu tunasema Tuonane January (#Tuo8January). Tutengeneze nchi yetu!! Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania!

 Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Farid Kubanda Fid Q akizungumza na waandishi wa habari kwenye mgahawa wa City Sports Lounge wakati akitangaza kuanza kwa kampeni maalum ya kuhamasisha vijana kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa njia ya matamasha  inayoitwa(#Tuo8January),inayotarajiwa kuanza  jumamosi mkoani Njombe  kutoka kulia ni Promota  Tale Msanii Dito na kutoka kushoto ni mtayarishaji wa muziki  Lamar kutoka Studio ya Fishcrab Music na Promota Said Fella wakiwa katika mkutano huo.

ZIARA YA NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS

$
0
0
Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb) Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais alifanya ziara ya kukagua Mazingira Mkoani Mtwara hususan katika eneo la Mdenga, Manispaa ya Mtwara. Chimbuko la ziara hii ni malalamiko yaliyotolewa na wananchi kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Abdulrahman Kinana alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo
Afisa Uhusiano wa kampuni ya SBS, Bw. Geofrey Kanenge (katikati) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb) (wa pili kushoto) kuhusu udhibiti wa utiririshaji wa maji taka yatokanayo na usafishaji wa mapipa yenye kemikali unavyofanywa na kampuni hiyo wakati wa ziara ya ukaguzi wa mazingira mkoani Mtwara.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (katikati) akipata maelezo kuhusu ubanguaji wa korosho kutoka kwa Uongozi wa Kiwanda cha Micronix kilichopo mkoani Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya mkoani humo.
Sehemu ya Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kukagua hali ya Mazingira ya viwanda aliyoifanya mkoani Mtwara.
Eneo la bwawa la asili la Mdenga lililofukiwa kinyume cha sheria na kampuni ya SBS inayojishughulisha na urejelezaji wa taka mkoani Mtwara na kusababisha uharibifu wa mazingira katika eneo hilo.

KAMERA YA MTAA KWA MTAA NA TASWIRA ZA AJALI YA KUTATANISHA

$
0
0
 Katika pita pita zetu za Mtaa kwa Mtaa,tuliibuka maeneo ya Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam na kukutana na mziki huu mnene na wakutatanisha uliozikutanisha gari mbili,ukiangaliwa kwa makini utabaini kuwa hili gari kubwa lenye nambari za Usajili T 544 CKG mali ya Kampuni ya Azania lilikuwa lipo kwenye njia yake halali kabisa kuelekea Buguruni na huyo mwenye Gari ndogo lenye nambari za Usajili T806 AVT anaonekana akielekea Ubungo lakini katika njia ambayo haimruhusu yeye kupita.Kilichotokea hapo ndio kama inavyoonekana pichani.Sasa sijui huyo mwenye hiyo gari ndogo alijiona anaendesha Boda boda....!!! Maana hapo alipotaka kupita hata hapaelezeki.
 Hapa hata sijui walitaka kupishana vipi??

CAG AHUDHURIA KIKAO CHA BODI YA WAKAGUZI YA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Mussa Juma Assad na ambaye kwa wadhifa wake ni Mkaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa akiwa na baadhi wa wasaidizi wake katika Kikao cha Bodi ya Wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kilichofanyika jana ( Jumanne) Hapa Umoja wa Mataifa.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mwenye tai nyekundu akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu kutoka Uingereza aliyekuwa akimkaribisha kwenye Bodi hiyo, upande wa kulia ni Ujumbe wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka India. Uingereza, India na Tanzania ndiyo inayounda Bodi ya Wakaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa na Mashirika yake. Katika mkutano huo ilielezwa kuwa Tanzania kwa maana ya CAG itachukua uenyekiti wa Bodi ifikapo Januari Mosi mwakani, uenyekiti huo ni wa miaka miwili.
Pamoja na Kushiriki Vikao vya Bodi, CAG alipata nafasi ya kufika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambako alipokelewa na Mwenyeji wake, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Ramadhani Mwinyi. Akiwa katika Uwakilishi wa Kudumu CAG alijionea maendeleo ya ukarabati wa Jengo la Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa

TASAF yamuaga Bi. Manjolo

$
0
0
Mfuko wa Maendeleo ya jamii-TASAF kwa ushirikiano na Wizara ya Fedha umempongeza na kumuaga rasmi Afisa aliyestaafu kutoka Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania ambaye alikuwa akisimamia  shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo.
Bi. Manjolo ambaye amefanya kazi hapa nchini kwa miaka kumi amepongezwa kwa kushiriki kikamilifu katika kuchochea kasi ya utekelezaji wa shughuli za TASAF za kupambana na umaskini nchini .
Akizungumza katika hafla ya kumuaga na kumpongeza Afisa aliyestaafu kutoka Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania ambaye alikuwa akisimamia  shughuli za TASAF (Task team Leader-TTL) Bi. Manjolo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga alibainisha kuwa Afisa huyo alikuwa akitumia falsafa yenye maneno ya "hakuna kulala hadi kieleweke" katika kuwapa moyo watendaji na wadau wa mfuko huo katika kuwahudumia walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini unaosimamiwa na TASAF.
"Wote tunafahamu kuwa katika kipindi ambacho tumekuwa naye, TASAF sasa imepanda chati sana na siyo ndani ya nchi tu, lakini pia hata nje ya nchi huko kwingineko Duniani, na maendeleo ya mpango wa kunusuru Kaya Maskini umekuwa ukiongelewa kwamba ni mpango unaofanya vizuri, lakini haya yote ni kwa sababu ya ushiriki wake mzuri ambao ulikuwepo na amehusika kwa kiasi kikubwa kuuandaa na kuufikisha mahala hapa pazuri tulipo" alifafanua Bw. Mwamanga.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha Dakta Servacius Likwelile amemtaja Bi Manjolo kama kiongozi hodari ambaye wakati wote amekuwa akitekeleza majukumu yake kwa ukamilifu na kuhakikisha kuwa mafanikio yanapatikana.
"Tumekuwa katika safari ndefu lakini yenye mafanikio makubwa kutokana na umakini wa mmoja wa madereva wetu ambaye ni Bi. Manjolo , tulianza naye akiwa ni msaidizi wa TTL hadi akawa TTL na katika kipindi chake chote cha miaka kumi ameiwezesha TASAF kufikia mahala hapa kwa sababu ya uwazi , wepesi na ukarimu wake wa kutaka kuona kwamba tunafanikiwa". Alibainisha Dr. Likwelile.
 Dr. Likwelile ambaye pia amepata kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha hakusita kutoa shukrani zake za dhati kwa mafanikio yaliyopatikana kutokana na ushiriki wa Bi. Manjolo.
"Tunamshukuru Aida kwa uadilifu, uaminifu, ukaribu, udugu na kupenda kutimiza wajibu na akaongeza kuwa siyo rahisi kutekeleza mpango kama huu na ukaleta maana kwa jamii kama hakuna uongozi mzuri na mshauri mzuri". alisisitiza Dr. Likwelile. 
 Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo akifurahia tuzo aliyopewa na TASAF kama ishara ya mafanikio makubwa kufuatia ushirikiano alioutoa kwa TASAF katika kutekeleza mipango ya maendeleo.
 Menejimenti ya TASAF ikiwa katika picha ya pamoja na Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (wa tatu toka kulia walioketi).
Baadhi ya wafanyakazi wa TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (wa tatu toka kulia walioketi) wakati wa hafla ya kumuaga Bi. Manjolo.
 Afisa aliyestaafu wa Benki ya Dunia aliyekuwa akisimamia shughuli za TASAF Bi. Ida Manjolo (wa tatu toka kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dokta Servacius Likwelile,   Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya Fedha Bw. Said Magonya (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (wa kwanza kushoto). Wengine ni walioketi toka kulia ni Afisa mpya wa Benki ya Dunia anayesimamia shughuli za TASAF Bw. Mohamed Muuderis na Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Ikulu Bi. Suzan Mlawi pamoja na baadhi ya wanafamilia ya Bi Manjolo (waliyosimama).

Mrwanda: Simba longo longo nyingi

$
0
0
Mshambuliaji Mpya wa timu ya Yanga, Danny Mrwanda amevunja ukimya kwa kusema hakutaka kusajiliwa Simba kwa mali kauli anachoangalia na 'njuru'.

Mrwanda ambaye ameanza mazoezi na Yanga jana jioni na kukabidhiwa jezi namba 24 alisema walishindwana dau na Simba  hivyo anaangalia kwenye maslahi.

"Mpira ni kazi yangu, naishi kwa ajili ya kutegemea mpira, sasa wao wameleta longo longo, Yanga wamekuja nikawapa dau wakakubali nikasaini mkataba, sasa hivi maisha yangu ni Yanga na akili zangu naelekeza kwenye timu yangu mpya na si mambo mengine, ninachangamoto ya kuhakikisha Yanga hawajuti kunisajili.

Kuhusu kusaini mkataba wa miezi sita Simba kama kocha wa wekundu hao wa Msimbazi Patrick Phiri alivyowahi kusema wiki iliyopita alisema "Nilifanya mazungumzo na Simba, na Phiri ananitaka hata leo hii, lakini viongozi wake longo longo, wanataka kunipa hela wanayotaka wao, hapo ndio tumeshindwana."alisisitiza Mrwanda huku akigoma katu katu kutaja kiasi alichoitaji Simba wakashindwa kumpatia.

Hata hivyo Mrwanda alisema kuwa mkataba wake wa  Polisi Morogoro ambayo inadai Yanga imemsajili mchezaji huyo kinyemela alisema "Habari za mkataba wangu na Polisi nisingependa kuzungumzia, viongozi wa Yanga watamalizana wenyewe na Polisi."alisema.

Naye kocha wa Yanga Mbrazil Marcio Maximo alisemaa ameshafanya kazi na Mrwanda wakati akiinoa timu ya Taifa, Taifa Stars, anamjua vizuri Danny na anajua ni kitu gani anaweza kukipata kutoka kwa mchezaji huyo.                                                                                                                                                                                                    
"Mrwanda ni mshambuliaji mzuri ana uwezo wa  kumiliki mpira, kukimbia katika nafasi, kufunga na kupiga pasi. Ingawa Danny ana udhaifu wake, hasa kuinama sana chini, ninalitambua tatizo hilo na nitalifanyia kazi, naamini ataifanya safu yangu ya ushambuliaji iwe yenye kasi zaidi.

Katika mazoezi ya jana jioni, Maximo aliweka wazi kikosi chake cha kwanza ambacho kitaanza katika mechi ya Nani mtani Jembe dhidi ya mahasimu wao Simba ambapo langoni alisimama Deogratius Mushi 'Dida' Juma Abdul, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub 'Canavaro' Mbuyu Twite, Simon Msuva, Emerson de Oliveira Neves Roque, Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima na Andrey Coutinho.

Katika mazoezi hayo ambayo Maximo alitumia mfumo wa 3-4-3  huku wapiga penati katika kikosi hicho ni  Canavaro, Msuva, Ngassa, Joshua na Mrwanda, kwa maana hiyo, katika mechi hiyo ya Jumamosi Ngasa na Mrwanda wataingia wakitokea benchi na kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza na Andrey Countinho   .

DKT. SHEIN KUWA MGENI RASMI UTOAJI TUZO ZA TASWA

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania Ijumaa wiki hii.

Tuzo hizo zinaandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na mwaka huu zimedhaminiwa na Selcom Wireless, Said Salim Bakhresa & Co Ltd - Bakhresa Group, IPTL, mifuko ya hifadhi ya jamii, PSPF na NSSF.

TASWA inaishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano wake na kukubali Rais Dk. Shein aje katika tuzo zetu, ambazo zitafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, VIP Dar es Salaam.

Kukubali kwa Dk. Shein kuwa mgeni rasmi kunaonesha jinsi gani alivyokuwa mwanamichezo wa kweli na mwenye nia ya dhati ya kushirikiana na wadau wa michezo nchini.

Wanamichezo 44 wanatarajiwa kupewa tuzo siku hiyo baada ya kufanya vizuri katika michezo mbalimbali kuanzia Juni 2013 hadi Juni 2014. Pia itatolewa Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa jumla na Tuzo ya Heshima.

TASWA imewahi kutoa Tuzo ya Heshima kwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, pia imewahi kutoa Tuzo ya Heshima kwa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliyokuwa ikicheza mechi za kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwaka 1980 zilizofanyika Lagos, Nigeria.


Tunaamini zitakuwa tuzo za aina yake, ambapo tayari Kamati ya Kusimamia Tuzo hizo imeshatangaza majina ya wanamichezo zaidi ya 100 wanaowania tuzo mbalimbali.

Ahsanteni
Egbert Mkoko
Makamu Mwenyekiti TASWA
10/12/2014

BALOZI KALLAGHE ASHIRIKI UZINDUZI WA RIPOTI KUHUSU MALARIA DUNIANI

$
0
0
Tarehe 9 Desemba 2014, ripoti ya mwaka ya dunia ya malaria (World Malaria Report 2014) ilizinduliwa rasmi katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za bunge la Uingereza zilizopo Portcullis House, Westminster jijini London.

Katika hafla hiyo, Tanzania ilitajwa kama mfano wa nchi inayoendelea kupata mafanikio barani Afrika katika kupambana na ugonjwa wa Malaria hasa kwa upande wa Zanzibar.

Tanzania ilipongezwa kwa mchango wa kisiasa wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika kuhakikisha agenda ya mapambano dhidi ya Malaria inapewa kipaumbele na katika eneo la utafiti wa kisayansi unaofanyika katika Taasisi ya Utafiti ya Ifakara.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa mtoto wa Malkia, Prince Andrew. Wengine waliohudhuria ni pamoja na wabunge kutoka vyama vya kisiasa nchini Uingereza,wawakilishi wa taasisi za kitafiti na wadau kutoka sekta binafsi. Tanzania iliwakilishwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe.
Balozi wa Tanzania, Mhe. Peter Kallaghe, akichangia machache katika hafla fupi ya Uzinduzi wa Ripoti kuhusu Malaria Duniani, uzinduzi huo ambao ulifanyika katika Ofisi za Bunge la Uingereza.
Balozi wa Tanzania, Mhe. Peter Kallaghe, akimsikiliza kwa makini mmoja wa wawakilishi wa Ripoti kuhusu Malaria Duniani, katika uzinduzi ambao ulifanyika jana katika Ofisi za Bunge nchini Uingereza.
Balozi wa Tanzania, Mhe. Peter Kallaghe (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wawakilishi kutoka shirika la Afya Duniani na washiriki wengine katika Uzinduzi wa Ripoti kuhusu Malaria Duniani, uzinduzi ambao ulifanyika tarehe jana tarehe 9 Desemba 2014 katika Ofisi za Bunge la Uingereza.

Tathimini ya ripoti mradi wa GEWE yazinduliwa Dar

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC), Bi. Gladness Munuo (wa kwanza kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam
Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC), Bi. Gladness Munuo (wa kwanza kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam.

VETA WATAKIWA KUHAKIKISHA WANASIKILIZA MAONI YA WADAU WAO ILIKUJUA MAHITAJI YAO SANJARI NA KUBADILISHA MITAALA YA ELIMU

$
0
0
WAZIRI wa Kazi na Ajira Mhe.  Gaudensia Kabaka  akizindua Kongamano la siku mbili jijini Arusha leo linaloshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwa ajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku mbili linaloshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwa ajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao na nini cha kuongeza kwa vijana wanaopitia Veta na kupata ajira katika sekta mbalimbali sanjari na kuzindua kitabu kinachoanisha mahitaji ya soko la ajira kwa vijana. 
 Mkurugenzi wa Veta, Mhandisi Zebadiah Moshi akiwa anaongea katika kongamano hilo 
Waandishi  wa habari wa Mkoa wa Arusha wakimuoji mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa VETA Profesa Idrissa Mshoro wakati wa mapumziko wa kongamano lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwaajili ya kujadili changamoto wanazozipata wadau hao na nini chakuongeza kwa vijana wanaopitia Veta na kupata ajira katika sekta mbalimbali sanjari na kuzindua kitabu kinachoanisha mahitaji ya soko la ajira kwa vijana.
Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA





Viewing all 109975 articles
Browse latest View live




Latest Images