Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 665 | 666 | (Page 667) | 668 | 669 | .... | 3284 | newer

  0 0

   
   Meneja Msaidizi wa Uwekezaji na Biashara Kubwa wa Benki ya Exim, Thobius Samwel (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo juu ya huduma za kibenki zitolewazo na benki yake  kwa washiriki wa shindano la Gofu liloandaliwa kwa watendaji wakuu wa makampuni mbali mbali jijini Dar es Salaam lililofanyika katika viwanja vya Gofu vya Lugalo, mwishoni mwa wiki jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Afisa Mauzo, wa benki hiyo Bw. Ishaq Samailla. Benki ya Exim ilikuwa miongoni mwa wadhamini.
   Meneja Msaidizi wa Uwekezaji na Biashara Kubwa wa Benki ya Exim, Joseph Lema (katikati) akichukua moja ya vipeperushi vyenye maelezo juu ya huduma za kibenki zitolewazo na benki yake, kumpatia mshiriki wa shindano la Gofu liloandaliwa kwa watendaji wakuu wa makampuni mbali mbali jijini Dar es Salaam lililofanyika katika viwanja vya Gofu vya Lugalo, mwishoni mwa wiki jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Afisa Mauzo, wa benki hiyo Bw. Ishaq Samailla.Benki ya Exim ilikuwa miongoni mwa wadhamini.

  0 0

  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza (UK Met Office) wamesaini mkataba wa makubaliano ya uboreshaji huduma za hali ya hewa hapa nchini. Mkataba huo umesainiwa tarehe 11 Novemba, 2014 wakati wa kikao cha masuala ya hali ya hewa (IBCS) kilichofanyika mjini Geneva Uswiss.

  Akizungumzia makubaliano hayo Dkt Agnes Kijazi alisema Mamlaka ya Hali ya Hewa ililiomba Shirika la Hali ya Hewa Duniani kuisaidia TMA kuboresha huduma zake ili ziwe za kisasa (Modernization of meteorological services in Tanzania) na ofisi ya hali ya hewa ya Uingereza ilikubali kuisaidia TMA katika zoezi hilo. ‘Makubaliano tunayosaini leo ni sehemu tu ya kazi kubwa ya uboreshaji wa huduma za hali ya hewa nchini ambapo shirika la Kimataifa la Uingereza (DFID) kupitia Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza limeipatia TMA Pound 70,000’ alisema Dkt. Kijazi .

  Akifafanua kuhusu matumizi ya fedha hizo Dkt. Kijazi alisema fedha hizo zitatumika kuijengea uwezo TMA kutunza data za hali ya hewa za kihistoria kwa njia ya digitali na pia kuwajengea uwezo watumishi wa TMA kutoa huduma bora zinazokidhi matarajio ya wadau na hivyo kulinda maisha ya watu na mali zao.

  Kwa upande wake mkuu wa Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza Dkt. Rob Varley alisema anafurahia ushirikiano uliopo kati ya TMA na UK met office na akaahidi kuendeleza ushirikiano huo na pia kuisadia TMA kuboresha huduma zake.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dkt. Agnes Kijazi akisaini mkataba na mtendaji mkuu wa Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza Dkt. Rob Varley. Tukio hilo lilishuhudiwa na Dkt. Ladislaus Chang’a, Mkurugenzi wa Utafiti katika Mamlaka ya Hali ya Hewa na Bi. Jane Wardle mtaalam wa masuala ya hali ya hewa kutoka ofisi ya hali ya hewa ya Uingereza.

  0 0  0 0

  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshirikiana na Timu ya mpira wa miguu ya Sunderland (SAFC) ya nchini Uingereza katika uzinduzi wa utangazaji utalii wa Tanzania pamoja na kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya michezo (Destination Partner in Tourism and Sports Development). Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 29 Novemba, 2014 kwenye kiwanja kinachomilikiwa na timu ya Sunderland “Stadium of Light”

  Kwenye tukio hilo ambalo lilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe pamoja na, maafisa kutoka Bodi ya Utalii, Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza pamoja na watanzania waishio nchini Uingereza. Tukio hili lilifanyika wakati timu ya Mpira ya Sunderland ilipoikaribisha timu ya mpira ya Chelasea Football club.

  Wakati wa uzinduzi huo matangazo ya Utalii yaliweza kurushwa katika kingo za kuta za uwanja wa timu ya Sunderland na kuonesha vivutio vya vivutio vya utalii wa Tanzania na vile vile yalioneshwa kwenye luniga kubwa iliyokuwepo kwenye uwajani huo. Aidha wachezaji wa timu ya Sunderland walivaa jezi maalum zilizoandikwa ‘Visit Tanzania’ wakati wakifanya mazoezi mepesi kabla ya mechi kuanza.

  Bodi ya Utalii Tanzania ilitumia fursa ya uziduzi huu kuhamasisha wataliii kutoka ndani na nje ya Uingereza pamoja na mashabiki wa timu hizo kutembelea vivutio vya utalii wa Tanzania.
  1Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kalaghe na Garry Hutchinson Mkurugenzi wa Biashara wa timu ya ligi kuu ya Uongereza ya Sunderland wakionyesha jezi ya iliyoandikwa Tanzania yenye rangi za timu hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa matangazo ya Utalii wa Tanzania yanayotangazwa katika uwanja wa timu hiyo kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bw. Geofrey Meena, Teddy Mapunda mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya (TTB) na kutoka kushoto ni Mdau wa Utalii Bw. Nestor Mapunda na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi.


  0 0

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB,Bw.Mark Weissing akiongea na wana habari kuhusu makubaliano kati ya NMB na Master Card katika hafla fupi ya kuweka saini makubaliano hayo.
  Daniel Monehin, Rais wa Kitengo, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wa MasterCardalisema (kulia) na Bw.Mark Weissing, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB wakieka saini makubaliano.

  MasterCard na National Microfinance Bank(NMB), benki kubwa zaidi Tanzania,leo wametangaza makubaliano ya kutoa kadi milioni 1.5 za malipo za MasterCard ambazo zitasaidia katika kupunguza utumiaji wa fedha taslimu na kuongeza ujumuishaji wa masuala ya kifedha kwa kutoa malipo ya kielektroni.

  Kama matokeo ya ushirikiano, NMB itatoa chipu salama ya EMV na PinMasterCard ya malipo, kadi za malipo kwa kipindi cha miaka saba ijayo. Kadi itakuwa na teknolojia isiyo na mawasiliano ya MasterCard, na kuonyesha kadi ya malipo isiyo na mawasiliano ya nchini Tanzania hadi sasa.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mkusa Issack Sepetu kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Halima Maulid Salum kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.


  0 0

  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania,Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi  huduma mpya ya HOME WI-FI itakayowawezesha wateja wake watumiaji INTANETI kufurahia kutumia kifurushi kimoja familia nzima kwa kuwaunganisha na Wi-fi watu 32 ndani ya familia na kuunganisha wanafamilia wengine wanne waliopo mahali popote nchini Tanzania  kufurahia internet ya 3.75G.  kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Home WiFi,Gaurav Dhingra.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Airtel Home WiFi,Gaurav Dhingra (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi  huduma mpya ya HOME WI-FI itakayowawezesha wateja wake watumiaji INTANETI kufurahia kutumia kifurushi kimoja familia nzima kwa kuwaunganisha na Wi-fi watu 32 ndani ya familia na kuunganisha wanafamilia wengine wanne waliopo mahali popote nchini Tanzania  kufurahia internet ya 3.75G.  Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania,Jackson Mmbando na kushoto ni Ofisa Masoko wa Airtel Tanzania,Ndevonaeli Eliakimu.

  Airtel Tanzania leo imezundia huduma ya kwanza ya kibunifu nchini ijulikanayo kama “Home WiFi with bundle share” (WiFi ya nyumbani na kufurushi cha pamoja) itakayowawezesha watanzania na wateja wa Airtel kupata huduma ya Wi-Fi na kuunganisha zaidi ya vifaa vingine 32 vitakavyotumia WiFi .

  Huduma hii vilevile itaunganisha hadi simu 4 za mkononi zilizoko kokote nchini kwenye akaunti moja na kuwapatia internet ya kasi ya 3.75G.  hii inamaanisha kifurushi cha internet kilichopo kwenye kifaa cha WiFI ya nyumbani  sasa kitakuwa na matumizi mawili yaani Wifi ya nyumbani na internet kwenye simu za mkononi pindi mteja akiwa  nje ya nyumbani

  kwa sasa wanafamilia na watumiaji wa intenet Tanzania hawana haja ya kununua vifurushi vya intenet kwa kila simu , kompyuta, Television au vifaa vyovyote vinavyoweza kuunganishwa na internet na badala yake watakachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi kwenye WiFi ya nyumbani na kuwawezesha kila aliyeunganishwa na kifaa hicho kupata kifurushi chake kulingana na gawiwo alilowekea na hivyo kutumia kifurushi kimoja

  ili kujipatia kifaa hichi cha HOME WiFi unaweza ukalipia : shilingi 195,000/-  na kupatiwa kifurushi cha kuanzia cha 40 GB  kwa mwenzi au unaweza kulipia shilingi 250,000/- na kupatiwa kifurushi cha kuanzia cha 120 GB  kwa mienzi mitatu, Aina zote mbili za ofa zinatoa huduma ya kutumia kifurushi kimoja na kuunganisha wanafamilia wanne wenye simu za mkononi ya malipo ya awali (prepaid line)

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja masoko na bidhaa hii wa Airtel Bw, Guarav Dhingra alisema” Dunia inabadilika na kukua kwa kasi ndivyo ilivyo kwa matumizi ya internet, kwa sasa internet si kwa ajili ya baba na mama, bali ni muhimu kwa familia nzima ikiwa ni pamoja na watoto kwaajii ya burudani, masomo,  na nyingine nyingi.  Ongezeko kubwa la simu za kisasa, komputa ndogo, Television za Kisasa, saa za kisasa, tablet katika nyumba zetu ni ushahidi tosha wa hili.

  Wakati ongezeko na upatikanaji wa vifaa hivi ukiwa rahisi,  njia za kuunganiswa na huduma za internet zinazidi kuwa ngumu kwa wateja,  kwani inamgharimu mteja kuwa na simcard kwa kila kifaa, na kila simcard inabidi kusajiliwa na kuwekewa muda wa maongezi wakutosha , kisha kuingiza namba maalumu na kuchangua kirufushi na ndipo kuanza matumizi.

  Airtel kwa kuona hii changamoto imekuja na huduma ya WiFi ambapo sasa unaweza kuunganisha vifaa hivi vyote kupitia kifaa cha WiFi cha nyumbani  na kupata intenet ya kasi bila kuhitaji simcard yoyote ya ziada.  Na tumewawezesha wanafamilia kuweza kuongeza kifurushi cha intenet kwa kupiga *148*20# na kuunganishwa na kifurushi kimoja

  Tunaamini familia nyingi zaidi nchini Tanzania watafurahia na kutumia huduma hii ya pekee toka Airtel na hivyo kutuamasisha kuongeza huduma nyingi za kibunifu za  internet” aliongeza Guarav Dhingra

  Huduma hii inapatikana kwa kupiga 0784104800 ambapo utaweka oda yako kwajili ya kupata kifaa hiki cha  WiFi ya nyumbani, na  kisha Airtel itakuletea mahali ulipo na kukunganisha na huduma hii.


  0 0

   
   Sehemu ya meza kuu,kutoka kulia ni Imam Abbasi Maunda  (mdau), Bi Halima Mamuya (mdau), Balozi Amina Salum Ali (mgeni rasmi), Fatma Khalfan (Mwenyekiti wa bodi), Juma Omari (mkuu wa shule) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mahafali hayo ya kidato cha nne,yaliyofanyika mwishoni mwa wiki,Temeke jijini Dar.
  Mkuu wa Shule ya sekondari Twayyibat,Juma Omari akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa mbalimbali,waliofika kwenye hafla hiyo ya mahafari iliyofanyika mwishoni mwa wiki Temeke,jijini Dar.
  Mwenyekiti wa Bodi,Bi Fatma akizungumza machache kwenye hafla ya mahafari ya kidato cha nne ya shule ya sekondari ya Twayyibat,Temeke jijini Dar,iliyofanyika mwishoni mwa wiki. bi
   Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nee wa shule hiyo wakitoa burudan ya igizo
   Mmoja wa wanafunzi aliyehitimu,akipokea cheti chake wakati wa mahafali shuleni hapo
  Pichani ni mmoja wa Wanafunzi,Sada Abubakar akipokea cheti cha Mwanafunzi bora 

  0 0

  Tanzania’s Idris emerged from the Big Brother Hotshots house at the end of Sunday night’s thrilling 2-hour live extravaganza with USD 300 000 in the bank! He picked up an avalanche of viewer votes from the continent after 63 days of fun, drama and intrigue to become the hottest of the Hotshots in the 9th season of the continent’s most epic reality show.

  Idris saw off the challenge of 25 other housemates through 9 weeks of extravaganzas, weekly tasks, ‘freeze’ challenges and even an epic prank in true Big Brother style. After he’d picked himself up off the floor after the announcement, Idris told IK he was feeling exhausted after the “long ride”. “Big love to everyone in Africa, I have so much love out there, I’m going to give back every single day,” said the man from Arusha.

  The show kicked off with a show-stopping performance from 17 evicted housemates, who got the chance to remind the continent of their Hotshots credentials. The glamorous finale was a star-studded affair, also featuring performances by the One Campaign Artists, Nigerian star M.I. and South Africa’s Unathi Msengana. Even the Top 8 housemates got in on the action, with a performance of their own to sum up their time in the house!
   Idris with Endemol SA CEO Sivan Pillay and M-Net Africa’s Regional Director (West) Wangi Mba-Uzoukwu
  IK took viewers back through all 63 days of Big Brother Hotshots, with reminders of the Hotshots’ stellar performances during the extravaganza tasks, the tender moments – and the explosive ones – they all shared, and all the fun they had learning about each other’s cultures, countries and personalities.

  Evictions were never far from everyone’s minds, though, and when the SizweNtsalubaGobodo auditor delivered a bulging envelope to IK on stage, he got down to business. Over the course of the show, he evicted Butterphly, M’am Bea, JJ, Sipe, Nhlanhla and Macky2 from the house in pairs, leaving Idris and Tayo to count their lucky stars as the rest of the Hotshots looked on enviously from the stage.

  As the time for the winner announcement drew near, Big Brother summoned the duo to the Diary Room for a final few words of encouragement before sending them out of the house to join IK on stage, through a curtain of fireworks.
  Wangi Mba-Uzoukwu, M-Net’s Regional Director for West Africa was delighted with the way Big Brother Hotshots played out. “The behind-the-scenes team overcame some astounding obstacles to get this season of Big Brother Africa on-air – and they delivered a show that was bigger, better, more dramatic and more entertaining than ever before,” she said. “Congratulations to Idris on being named the winner of Big Brother Hotshots – and thank you to the rest of the housemates for providing the entire continent with 63 days of phenomenal entertainment”.

  Sivan Pillay, Managing Director of Endemol South Africa said: “We are very proud to have produced another great season of Big Brother Africa. Despite the devastating setback of the fire, it has been a monumental achievement to entertain the continent with our broadcast partner Multichoice”.

  0 0

  Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye miwani katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa alipopokea sehemu ya mabehewa ya kisasa yatakayotumika kuboresha usafiri katika reli ya kati ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
  Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe akiangalia kitu wakati wa kupokea sehemu ya mabehewa ya kisasa yatakayotumika kuboresha usafiri katika reli ya kati ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).kushoto ni Afisa Habari wa TRL,Midraji Mahezi.
  Sehemu ya ndani ya Mabehewa hayo.


  0 0

  Na Marco Mipawa, Accra- Ghana
  Tanzania inaweza kuwa nchi ya kwanza katika maendeleo ya uchumi iwapo itaweka sera madhubuti za uzalishaji wa Gesi na kuwa na viongozi wenye dhamira dhabiti ya kuiendeleza nchi na kuboresha maisha ya watu.
  Haya yamebainishwa na Meneja wa Redio Kahama FM Marco Mipawa leo wakati akiendelea na ziara ya mafunzo nchini Ghana ya kujionea jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi na jamii katika suala zima la maendeleo.

  Mipawa ameyasema hayo baada ya kuona kuwa nchi ya Ghana inalo tatizo kubwa la upatikanaji wa nishati ya umeme hata kuliko Tanzania inavyoathirika na tatizo hilo lakini maisha ya watu ni mazuri na uchumi uko juu.

  Amesema, katika jiji la Accra umeme hukatika takriban robo tatu ya siku na matumizi ya jenerata ni makubwa lakini thamani ya pesa yao iko kubwa ikilinganishwa na ya Tanzania ambapo kukatikakatika kwa umeme ni mara chache.

  Mipawa amesema, dola moja ya marekani inathamanishwa na Sedisi tatu za Ghana ikiwa ni sawa na Shilingi 1770 za Tanzania hali inayoonyesha uchumi wa Tanzania uko chini ukilinganishwa na wa Ghana.

  Baadhi ya wananchi wa Accra wamemwambia Mipawa kuwa, kinachoisaidia nchi ya Ghana ni Uzalishaji mali katika kilimo, madini na ufugaji; huku sera na sheria za nchi zikisimamiwa kwa umakini mkubwa kwa maslahi ya nchi.
  Wamesema suala la kudhibiti rushwa na kusimamia utii wa sheria vikiambatana na uwazi na ukweli wa serikali na viongozi wa Ghana, ndiyo silaha mahususi zilizoifanya Ghana kuwa na uchumi imara na maisha mazuri ya watu.

  Ziara ya mafunzo ya wiki mbili ya kujionea utendaji wa vyombo vya habari nchini Ghana, imehusisha watu tisa kutoka Tanzania wakiwemo waandishi wa habari na viongozi wa vyombo vya habari mbalimbali kwa udhamini wa Tanzania Media Fund (TMF).
  Mipawa to Ghana
  Meneja wa kituo cha Kahama FM Redio, Marco Mipawa (kushoto) akielekea kukwea pipa kuelekea nchini Ghana kwenye ziara ya mafunzo ya wiki mbili.


  0 0

  ZIKIWA zimesalia siku nne  kufikia mpambano  wa  nani mtani jembe kati ya watani wa jadi  Simba na Yanga,  Kocha wa zamani wa kikosi cha Wanamsimbazi Abdallah Kibadeni, amemshauri  kocha mkuu  wa timu ya Simba Patrick Phiri kuimarisha safu ya ushambuliaji na ulinzi.

  Kibadeni alisema Simba wana nafasi kubwa ya kutetea ushindi wao, lakini  wanachotakiwa kuzingatia ni kwenye safu hizo mbili ili waweze kuzuia mashambulizi ya wapinzani wao, vinginevyo itawawia ngumu.

  "Mechi hiyo itakuwa ngumu kwa sababu timu hizo daima zinaushindani wa hali ya juu, lakini maombi yangu ni kuhakikisha Simba inafanikiwa kutwaa ubingwa wa nani mtani jembe, kwa sababu ina uwezo huo," alisema.


   Kibadeni alisema mabeki waliopo Simba pamoja na washambuliaji ni wazuri, ila angalizo wanatakiwa kujituma na kuwa makali zaidi kila wanapopata mipira kwa sababu kosa moja tu linaweza kuwaletea matokeo mengine .  "Watulize presha ili wacheze mpira pia waache kucheza na jukwaa kwani kinachotakiwa pale ni ushindi na sivinginevyo, lakini uwezo wanao wafanye kazi iliyowapeleka uwanjani.


  Aliongeza kuwa " Dany Sserunkuma waliyemsajili katika dirisha dogo ataongeza nguvu ya ushindani katika kikosi hicho kwani ana uwezo wa kuleta madhara katika lango la wapinzani wao, kikubwa ni kujipanga vema pia kujiamini," alisema Kibadeni

  0 0

  Mwanamitindo Mkongwe hapa nchini na nje ya Mipaka ya Tanzania,Asia Idarous a.k.a Mamaa wa Mitindo (pichani) akiwa na tuzo yake ya "Zakhia Meghji Life Time Achievement 2014" alioshinda jana katika Jukwaa kubwa na maonyesho ya Mitindo la Swahili Fashion Week Tanzania.Asia Idarous ambaye ni Mwanamitindo wa miaka mingi aliweza kunyakua tuzo hiyo baada ya kuwepo kwenye tasnia hiyo ya mitindo kwa zaidi ya miaka 35 na amefanya maonyesho ya mitindo mara 150 ndani ya Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania.Globu ya Jamii inatoa pongezi kwa Mamaa wa Mitindo na kumuombea mafanikio zaidi na zaidi

  0 0


  KLABU  ya Simba imeingia kambini leo Zanzibar huku ikimtema mshambuliaji wake raia wa Gambia Omar Mboob.

  Katibu mkuu wa Simba Steven Ally alidhibitisha kuwa mchezaji huyo ameenguliwa kwenye kikosi cha Simba kwa vile ameshindwa kuonyesha kiwango cha kumshawishi kocha Patrick Phiri ili aweze kusajiliwa.

  "Mboob kwa sasa tunamfanyia taratibu ili aweze kurudi nchini kwao, kesho (leo) au kesho kutwa ataondoka, ameshindwa kuonyesha makali."alisema

  Wakati Ally akisema hayo, Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hanspope alisema "Mimi nilikutana na meneja wake katika shughuli zangu za kibiashara akaniambia kijana wake ni mzuri na muda wowote atakwenda kufanya majaribio barani Ulaya. Nikaona si mbaya akaja hapa tukamwangalia, lakini kiwango chake bado” alisema  Hanspope.

  Hata hivyo, tayari Simba imefikisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Ligi ambao ni Dan Sserunkuma aliyechukua nafasi ya Raphael Kiongera, Mganda Emmanuel Okwi, Joseph Owino na warundi Pierre Kwizera na Amissi Tambwe.

  Katika hatua nyingine, Simba imeingia kambini Zanzibar jana jioni kujiandaa na mechi yao dhidi ya Yanga huku makocha wa timu hizo kila mmoja ana matumaini ya kushinda mchezo huo huku kocha wa Yanga Marcio Maximo akiingia mchecheto na kutamka kuwa "Kocha anaajiriwa ili afukuzwe, hayo ndio maisha hasa Afrika, sihofii kufukuzwa iwapo tutafungwa na Simba, ninachoangalia si tu mechi ya mtani Jembe bali na za ligi.

  Kauli ya Maximo aliiotoa baada ya kuulizwa, kocha Ernie Brandts alitimuliwa baada ya matokeo ya mechi ya mtani jembe msimu uliopita, na yeye amejiandaje katika hilo.

  "Kocha anaajiriwa ili afukuzwe, mimi sijali, matokeo yoyote nitayapokea na uongozi utaangalia kama wanifukuzea au la wao ndio wameniajiwa, kikubwa ninachoangalia ni uwezo wa wachezaji wangu na zaidi naangalia mbele."alisema na kuongeza

  "Muhimu ni kushinda, haijalishi ni mechi ya kirafiki au ni Ligi, zinapokutana timu kubwa za watani wa jadi hakuna mechi raisi, nimejipanga vizuri, lengo ni kushinda, nisingependa nipoteze."alisisitiza Maximo.

  Wakati Maximo akisema hayo,  Kocha wa Simba Patrick Phiri alisema timu yake imeingia Kambini Zanzibar  kujiandaa na mechi ya watani zao   Yanga ambao wameshindwa kuwafunga katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Oktoba 18, kwa kutoka suluhu.

  Phiri alisema wameanza kujipanga kwa mazoezi makali ya viungo katika klabu ya mazoezi (gym) ya Chang’ombe, Dar es Salaam kwa ajili ya kuwajengea nguvu ya mwili wachezaji wake na sasa wanfanya mazoezi ya uwanjani.

  “Mechi inayokuja dhidi yetu na Yanga hakuna droo tena, Simba ni timu kubwa tunahitaji kushinda,” alisema Phiri.

  Hata hivyo matumaini makubwa ya Phiri yapo kwa Dan Sserunkuma kwa kile alichoeleza mchezaji huyo ni mzuri na amemfuatilia kwa muda mrefu akiwepo timu ya taifa ya Uganda 'Uganda Crenes' na Gor Mahia.

  “Daniel ni mchezaji mzuri, nimemfuatilia akiwa katika timu yake ya Taifa na hata akiwa Gor Mahia kule Kenya, huyu ni mshambuliaji aliyekamilika… naamini atatusaidia sana,” alisema. 

  " Nataka mashabiki wasihofu juu ya matokeo ya sasa ya Simba na michezo ya kirafiki badala yake nitawafurahisha mwaka ujao utakapoanza. 

  "Kwa sasa nina michezo miwili migumu iliyobaki mwaka huu, tutacheza na Yanga wikiendi hii kisha tutavaana na Azam  kwenye Ligi Desemba 26 mwaka huu. Mwakani nitakuwa nimebakiza michezo 18 ili ligi imalizike  hivyo ninataka kuhakikisha ninafanya vizuri na kuchukua ubingwa tena kwa kupata matokeo mazuri.

  Hivi karibuni Simba imecheza michezo miwili ya kirafiki. Mmoja dhidi ya Express ya Uganda ambao uliisha kwa sare ya 0-0. Kisha wakacheza na Mtibwa na kupokea kipigo cha 4-2.

  0 0

  Waziri mkuu mstaafu  na mbunge wa Monduli Mh edward Lowassa akimjulia hali leo hii askofu mkuu Katoliki jimbo Kuu la Tabora Paul Ruzoka katika hospitali ya TMJ Mikocheni jijini Dar es salaam alikokwenda kufanyiwa vipimo kufuatia ajali aliyoipata Igunga Mkoani Tabora.Mwenye shati jeupe ni Bishop Gwajima.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa hoteli ya Gold Zanzibar Beach hotel  Bw.  Andrea Lottle akishirikiana na Wafanyakazi wa hoteli hiyo wakisherehekea kwa kuzima mshumaa kuadhimisha miaka miwili ya hoteli hiyo iliofanyika katika ukumbi wao kNungwi Kwenda.
   Wageni wa hoteli ya Gold Zanzibar Beach wakipata picha za kumbukumbu ya hafla hiyo ya sherehe za kutimia miaka miwili ya hoteli hiyo iliofanyika katika ukumbi wake kendwa Zanzibar.

   Msanii wa kitaliano Antonela Mignlore akionesha sanaa za utamaduni wa Kitalioano katika hafla hiyo ya kutimiza miaka miwili ya  Gold Zanzibar Beach hotel.
   Wapishi wakiwa katika harakati za kutowa huduma kwa wageni wao wakati wa hafla ya kusherehekea miaka miwili 

   Sehemu ya wageni waalikwa katika hafla hiyo ya kutimiza miaka miwili ya hoteli ya Gold Zanzibaer Beach Kendwa Zanzibar, wakimsikiliza Mkurugenzi Kuu Mr Andrea Lottle, akizungumza katika hafla hiyo .
  Wafanyakazi wa  Gold Zanzibar Beach Hotel wakiwa na keki yao wakisherehekea miaka miwili ya hoteli hiyo tangu kufunguliwa na kutowa huduma kwa Watalii wanaotembelea Zanzibar wakifurahia wakiwa na Keki yao katika ukumbi wa hafla hiyo iliofanyika katika hoteli hiyo na kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali na Maofisa wa Sekta ya Utalii Zanzibar na Wamiliki wa Mahoteli ya Utalii Zanzibar.  
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia kwake) na Naibu Waziri wake, Dkt. Charles Tizeba (kulia) kukagua baadhi ya mabehewa mapya ya Shirika la Reli nchini (TRL) yaliyonunuliwa na kwa fedha za serikali wakati alipokwenda kwenye bandari ya jijini Dar es salaam leo Desemba 8,2014.
  Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akiangalia jiko ambalo liko ndani ya behewa la daraja la pili kwenye moja ya mabehewa 22 yaliwasili nchini mwisho wa wiki, katika bandari ya jijini Dar es Salaam, leo Desemba 8,2014.
  Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akishuka kwenye moja ya mabehewa 22 yakiyowasili nchini mwisho wa wiki, leo mchana katika bandari ya Dar es Salaam.Mh. Pinda alifika Bandarini hapo  kukagua mabehewa hayo. Waziri Mkuu amempongeza Waziri wa Uchukuzi pamoja na watendaji wake kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Kuimarisha usafiri wa Reli nchini. Utekelezaji wa mradi huu ni mojawapo wa Miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa(BRN).


  0 0

  The Permanent Secretary for Treasury from the Ministry of Finance, Dr. Servacius Likwelile addressing the media during a press conference on the upcoming International Conference on Social Protection.

  The Government of Tanzania through the Ministry of Finance, in collaboration with UNICEF, ILO, UNAIDS and the Economic Policy Research Institute (EPRI) based in South Africa, is organizing an International conference on Social Protection from 15th to 17th December 2014 in Arusha, Tanzania. This marks government’s commitment to poverty eradication and achieving growth with fairness and justice for all especially women and children.

  The conference, to be officiated by H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania is aimed at encouraging South-South exchange of knowledge and best practices  to support Tanzania’s efforts in designing policies and programmes for assisting the poor and vulnerable including women, children, elderly, disabled and youth to achieve a basic standard of living.


  0 0

  Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na viongozi wengine waandamizi wa serikali.Katikati wapili kushoto anayeshuhudia ni Katibu mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na watatu kushoto ni Karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gervas Mdemu.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa miongozo ya kazi(Standing Orders) Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda wakati wa hafla ya kuapa iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Mkuu mpya wa mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda wakati wa hafla wa kuapa iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba mtoto Gracious Mathayo Ntebo mjukuu wa wa mkuu mpya wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda wakati wa hafla ya kumuapisha mkuu huyo wa mkoa iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo. (picha na Freddy Maro).

  0 0

  Ankal Michuzi akimpongeza Binti yake Zahra wakati wa hafla ya Maulid ya Kumpongeza baada ya kulamba Nondozz yake ya kwanza ya Biashara na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dodoma hivi karibuni.Hafla hii imefanyika jana Nyumbani kwa Kaka wa Ankal,Tabata Kimanga jijini Dar es salaam.
   Baba Mkubwa wa Zahra,Ismail Michuzi akiongoza dua ya kuwakumbuka ndugu waliotangulia mbele ya haki kabla ya shereha ya Maulid ya kumpongeza Binti Zahra alielamba Nondozz yake ya Biashara na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dodoma,hivi karibuni.Kulia ni Ankal.
   Ankal akiwa na Wanawe,Ramadhan (pili kushoto),Zahra (kulia),Karim (kushoto) na Sellah (alie na Ankal) wakati wa hafla ya Maulid ya kumpoza Zahra alielamba Nondozz yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dodoma hivi karibuni.Hafla hii ilifanyika Tabata kwa Kaka wa Ankal ambaye ni Baba Mkubwa wa kina Zahra.
   Ankal Michuzi (shoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wanafamilia wakati wa hafla ya Maulid ya kumpongeza binti yao,Zahra (kati) baada ya kulamba Nondozz yake ya kwanza ya Biashara na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dodoma hivi karibuni.


older | 1 | .... | 665 | 666 | (Page 667) | 668 | 669 | .... | 3284 | newer