Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

TBL YAWA KINARA ULIPAJI KODI TANZANIA

$
0
0
Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, akikabidhi Kombe la mshindi wa Meneja wa Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Alois Qande, wakati wa maadhimisho ya nane ya mlipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, Dar es Salaam hivi karibuni.


Michuzi Blog Exclusive: super model flaviana matata achumbiwa, mchumba kapuni kwa sasa....

JK apokea salamu za kheri toka kwa Rais Barack Obama wa Marekani

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete salamu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwa furaha na ujumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Washington DC uliomtembelea kumjulia hali na kwasilisha salamu maalumu za pole  za Rais Barack Obama jijini Baltimore, Maryland.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea salamu maalumu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na maafisa waandamizi  wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington D.C. wakati walipomtembelea mjini Baltimore Maryland ambapo balozi Liberata Mulamula aliwasilisha kwa Rais Kikwete Salamu maalum za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama leo jijini Baltimore, Maryland, Marekani. Picha na Freddy Maro

Taarifa ya msiba wa Kamishna Msaidizi wa Polisi mstaafu Leonard Mashaka

$
0
0
Kamishna Msaidizi wa Polisi mstaafu,Marehemu Leonard Mashaka enzi za uhai wake. 

Mheshimiwa Jaji Lillian Mashaka anasikitika kutangaza kifo cha Mume wake Kamishna Msaidizi wa Polisi mstaafu Leonard Mashaka kilichotokea siku ya Jumapili tarehe 23/11/2014. 
Msiba upo nyumbani kwake Mikocheni Dar es Salaam(nyumba za serikali).



Mazishi yatafanyika Jumatano tarehe 26/11/2014.
Ratiba itaanzia nyumbani saa 4 asubuhi na hatimaye misa takatifu katika kanisa la Mt. Martha Mikocheni, Saa 7 mchana.



Mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kinondoni (yazamani)kuanzia saa 9 mchana.

Taarifa ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote walipo.

Raha ya milele umpe e Bwana na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa amani.

KANDA YA KASKAZINI WAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

$
0
0
Wanaharakati kutoka shirika la Kwieco la mkoani Kilimanjaro wakiwa katika maandalizi ya maadhimisho ya siku 16 za kupingaukatili wa kijinsia.
Maandamano ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yakipita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Moshi.
Mkurugenzui wa shirika la KWIECO ,Elizabeth Minde (mwenye miwani myeusi) akiwa katika maandamano hayo.
Brass Band ya Chuo cha Polisi ikiongoza maandamano ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kanda ya kaskazini yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.
Picha zaidi BOFYA HAPA

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA AHMED .Z. MSANGI-SACP ANAWATANGAZIA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014 NA KIDATO CHA NNE MWAKA 2013 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI BAADA YA USAILI KUKAMILIKA

$
0
0
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA AHMED .Z. MSANGI-SACP 

Maelekezo Muhimu.
Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014, kidato cha nne mwaka 2013 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo, Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita, Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani, Oljoro, Rwankoma na Kimbiji wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi.
  1. Wahitimu hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti tarehe 28/11/2014 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wa kuwapeleka Shule ya Polisi Tanzania tarehe 30/11/2014.

  2. Zoezi la usajili litaanza shuleni hapo tarehe 01/12/2014 hadi tarehe 15/12/2014. Atakaefika kuanzia tarehe 16/12/2014 hatapokelewa.

  3. Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Shule ya Polisi Tanzania mjini Moshi.

  4. Vijana hawa watalazimika kufika shuleni wakiwa na mahitaji yafuatayo:

    1. Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

    2. Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)

    3. Chandarua chenye upana futi tatu

    4. Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)

    5. Pasi ya Mkaa

    6. Ndoo moja

    7. Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=).

    8. Pesa kidogo ya kujikimu.

  5. Kwa mujibu wa kanuni za shule ya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa shuleni hapo. Shule itaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.

  6. Angalia orodha kwenye tovuti ya www.policeforce.go.tz au fika Ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya iliyopo Forest barabara ya mahakama kuu.

DKT. SHEIN AENDELEA NA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA,AKUTANA NA MABALOZI WILAYA KATI,UNGUJA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Ngazi mbali mbali za Chama cha Mapinduzi alipofika katika viwanja vya Tamarind Hotel Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Unguja alipofika kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Mkutano maalum wa mwendelezo wa ziara zake za kumarisha Chama.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Ngazi mbali mbali za Chama cha Mapinduzi alipofika katika viwanja vya Tamarind Hotel Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Unguja alipofika kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Mkutano maalum wa mwendelezo wa ziara zake za kumarisha Chama.
Kikundi cha Ngoma ya Benibati wakitumbuiza kwa Ngoma hiyo wakati wa Mkutano maalum wa mwendelezo wa ziara za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika kumarisha Chama uliofanyika jana katika viwanja vya Tamarind Hotel Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Unguja kwa kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapongeza wasanii wa kikundi cha Benibati kilipotumbiza kwa wajumbe wa Mkutano maalum wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani kabla ya kuzungumza nao katika kuimarisha Chama jana viwanja vya Tamarind Hotel Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Unguja ikiwa ni mwendelezo wa ziara katika Mikoa ya Unguja.

Miss Ilala 2014 ashiriki chakula cha mchana na Watoto wa Kituo cha Mwana Orphans Centre

$
0
0
Miss Ilala 2014 Jihan Dimack, akiwanawisha mikono watoto yatima wa kituo cha Mwana Orphans Centre kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam katika hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika katika hoteli ya Cape Town Fish Market.  (Picha na John Dande)
Miss Ilala 2014 Jihan Dimack, akiwagawia chakula watoto wanaolelewa na kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwana Orphans Centre kilichopoVingungutijijini Dar es Salaam katikahaflayachakula cha mchanailiyofanyikajuzikatikahoteliya Cape Town Fish Market. 
Miss Ilala 2014, Jihan Dimack akila chakula pamoja na watoto hao.
Miss 2014 Jihan Dimack akitoa zawadi kwa watoto hao.

Miss Ilala mwaka 2014 Jihan Dimack akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa na kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwana Orphans Centre kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam katika hafla ya chakula cha mchana,iliyofanyika katika hoteli ya Cape Town Fish Market.
Miss Ilala 2014 Jihan Dimack akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa hoteli ya Cape Town Fish Market.

KONGAMANO LA 31 LA KISAYANSI LAENDELEA MJINI BAGAMOYO

$
0
0
Na Andrew Chale, Bagamoyo
 Kongamano la Kisayansi la 31, '31th Annual Scientific Conference and Annual General Meeting'.. lililoandaliwa na Tanzania Public Health Association (TPHA),linaendelea kwa siku ya pili katika Ukumbi wa Stella Maris Mjini Bagamoyo,mkoani Pwani.

Kongamano hilo la kisayansi la 31, limeanza Novemba 24 linatarajia kuwa la siku tano na kutarajia kumalizika Novemba 28 ambapo wataalamu wa afya na wadau watajadilina mambo mbalimbali ya afya hapa nchini.
DSC_0825
Maximilian Mapunda kutoka shirika la Afya Duniani (WHO-Country Officer) akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.
DSC_0830
Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga akiwasilisha mada maalum kwenye kongamano hilo.
DSC_0852
Dk. Ali Mzige mshiriki wa Kongamano la Kisayansi la 31, akiwasilisha mada maalum.
DSC_0848
Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe akitoa ufafanuzi kwenye mada zinazotolewa na wajumbe kwenye kongamano hilo.
DSC_0856
Wajumbe wa kongamano hilo wakichangia mada.
DSC_0857
Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga (kushoto) akifuatilia kwa makini kongamano hlo.

SHIRIKA LA WANAWAKE KATIKA SHERIA NA MAENDELEO AFRIKA (WiLDAF) LAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DAR

$
0
0
Wanaharakati kutoka shirika la WiLDAF wakiwa katika maandalizi ya matembezi ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliayoanzia viwanja vya Mnazi mmoja na kuishia katika Ukumbi wa Karimjee hapo jana.
Maandamano ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yakipita katika mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam hapo jana
Maandamano ya kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yakipokelewa na Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe
Mgeni rasmi katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe ambaye alikuwa anamuwakilisha Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akitoa hotuba yake.
Mratibu wa Kitaifa shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Ndugu Judith Odunga akitoa hotuba yake katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Khadja Kopa, Bilal Mashauzi kuwasha moto USIKU WA KHANGA PARTY NOV 29

$
0
0
Na Andrew Chale

ASIA Idarous Khamsin na Safari  Carnival  wanakuletea usiku wa Khanga Party na Spice Modern Taarab watakaowasha moto wa burudani sambamba na gwiji wa mipasho nchini Khadija Kopa pamoja na Bilal Mashauzi,  Jumamosi ya usiku wa Novemba 29, ndan ya ukumbi wa Safari Carnival, Mikocheni B.

Kwa mujibu wa  mmoja wa wandaaji wa usiku huo, Asia Idarous Khamsin,  amesema tayari maandalizi yake yamekamilika na amewasihi wadau kujitokeza kwa wingi katika onesho hilo la aina yake  kwa kiingilio cha sh 10,000 na 20,000 kwa V.I.P.

Asia Idarous Khamsin alisema Usiku wa Khanga, itaanza kuanzia usiku wa saa mbili  na kuendelea huku vazi maalum likiwa ni Khanga.

"Usiku huu ni maalum kulienzi vazi la khanga, ambalo pia ndilo vazi maalum la usiku huo. Pia watafurahia muziki mzuri kutoka kwa magwiji wa taarab hapa nchini akiwemo Khadija Kopa, Spice Modern taaba na Bilal Mashauzi." alisema Asia Idarous Khamisin  ambapo pia alisisitiza vazi la khanga ni la heshima hasa kwa mwanamke wa Kitanzania hivyo kila mmoja atakapolitengeneza vizuri ama kufunga litamweka malidadi.

Aidha, alibainisha kuwa, usiku huo pia kutakuwa na  zulia jekundu 'Red Carpet' ambapo watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa na watu maalufu watakao jitokeza usiku huo.

Pia alibainisha kuwa, tayari tiketi zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Fabak fashions Mikocheni na Safari Carnival  kwa mawasiliano piga 0754263363 au 0713263363

Bondia Zumba Kukwe ataka kuzichapa na Thomas Mashali au Kalama Nyilawila

$
0
0
Mabondia Sweet Kalulu wa Dar es Salaam kushoto na Zumba Kukwe kulia na katikati ni mwandaaji wa pambano hilo George Nyasalu akishuhudia mabondia hao baada ya kupima uzito na afya jana.

Na John Gagarini, Kibaha

BONDIA Zumba Kukwe wa Maili Moja wilayani Kibaha Mkoani Pwani ambaye leo anapambana na bondia Sweet Kalulu amesema kuwa lengo lake kubwa ni kupambana na Thomas Mashali au Kalama Nyilawila.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Kibaha wakati wakipima uzito na kupima afya kwenye ukumbi wa Container Bar alisema kuwa leo atamshinda mpinzani wake raundi ya tatu.

Kukwe alisema kuwa kwenye pambano lake la leo anatarajia kufanya vizuri kwa kumpiga mpinzani wake na kuwapa raha wapenzi wa ngumi wa mkoa wa Pwani.

“Nimejipanga vizuri kwenye pambano langu na sitawaangusha wapenzi wangu kwani niko kwenye uwanja wa nyumbani, naangalia mbele zaidi ninaowataka ni Mashali au Nyilawila,” alisema Kukwe.
Aidha alisema kuwa anatarajia kuiweka Pwani kwenye ramani ya mchezo huo wa ngumi hivyo malengo yake ni kupambana na mabingwa wa Tanzania.

“Najiamini kuwa nina uwezo na baada ya pambano la leo safari yangu ya kuanza kutamba kwenye ulimwengu wa ngumi itaanza na nitahakikisha ngumi inakuwa juu mkoani Pwani,” alisema Kukwe.
Kwa upande wake Kalulu alisema kuwa yeye hana maneno mengi anachosubiri ni muda tu ufike na kila mtu atajua  nini kilichomleta Kibaha kwnai anauwezo.

Naye muandaaji wa pambano hilo George Nyasulu alisema kuwa lengo la kuandaa pambano hilo ni kuwahamasisha vijana wanaopenda mchezo huo kujitokeza ili kucheza mchezo huo.

Nyasulu alisema kuwa huo ni mwanzo kwani baadaye ataandaa mapambano mengi zaidi na nia ni kutoa bingwa wa ngumi Taifa kwani vijana wana uwezo.Jumla ya mapambano saba ya utangulizi yatachezwa.

Washindi 62 wamejinyakulia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya “shinda na kabumbu” ya Vodacom

$
0
0
Jumla ya washindi 62 mpaka sasa wamejishindia zawadi ya shilingi 50,000 kila mmoja na wateja wawili wakubwa wa wiki wamejishindia 1,000,000 kila mmoja katika droo ya kwanza na ya pili ya promosheni ya “SHINDA NA KABUMBU” iliyozinduliwa hivi karibuni ikiwa inawalenga wapenzi wa soka.

Washindi wa shilingi 1,000,000/-katika droo ya kwanza ni Salome Mayoba mkazi wa Kahama,na mshindi wa droo ya pili ni na Raymond Mwegoha mkazi wa Dar es Salaam ambapo washindi wa shilingi 50,000/- wametangazwa kuwa ni Hapifania Msack,Elick Mgecha,Jene Msangi,Pereus Ngambeki,Hassan Lugwisha, Wengine ni John Nkurlo,Makere Bairi,Jenro Ndimbudzi,Monica Mchilo,Ferida Nywage,Joseph Samwel,Yona Gilayo,Emil Mlutie,Batoromeo Nyerere,Peter Mbuya,Dismas Kimario,Vicent Mangesho,Sophia Segu,Omary Oswald,Zuberi Mwamba,Moses Mwambene,Wallace Ngalomba,Martin Dominick,Deusdediti Ziguye,Idd Joche,Swahab Said,Cleophace Gatahwa,Maneno Mwangosi,Peter Gabagambi,na Michael Kissla.

Promosheni hii ambayo itadumu kwa kipindi cha mwezi mmoja washindi wake wanapatikana kwa kujibu maswali mbalimbali kuhusiana na ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Ligi kuu ya Uingereza,na masuala mengine mengi yanayohusiana na Kombe la Dunia na mengine mengi yanayohusiana na mchezo wa soka kwa ujumla.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema kila siku wapenzi wa soka au wateja 5 watajinyakulia shilingi 50,000 pia atakuwepo mshindi mmoja wa wiki atakaejinyakulia shilingi Milioni 1. Na droo ya mwisho katika promosheni hii atapatikana mshindi wa jumla atakayejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 pesa taslimu. Ili kushiriki katika promosheni hii mpenzi wa soka au mteja yeyote wa mtandao huu anachopaswa kufanya ni kutuma neno SOKA kwenda namba 15725 na hapo mteja atakatwa kiasi cha shilingi 99 tu kwa kila meseji.

Amesema kila wiki washindi watakuwa wakitangazwa na kupigiwa simu moja kwa moja baada ya kufanyika droo za kila wiki na kutumiwa fedha zao kwa njia ya M pesa.

Vodacom imekuwa ikiandaa promosheni mbalimbali kwa wateja wake na moja ya promosheni ambayo imewafanya wateja wake maisha yao kuwa murua ni ile ya Timka na bodaboda na Vodacom milionea ambapo washindi waliweza kujishindia pikipiki na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 100.
Humudini Abdulhussen Ofisa Mwandamizi wa Bodi ya Kusimamia Michezo ya Kubahatisha Tanzania (kushoto) akihakiki moja ya namba za simu anazoonyeshwa kwenye kompyuta mpakato na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati) na Ofisa Masoko wa kampuni hiyo Prestin Lyatonga (kulia) wakati wa droo ya pili ya shindano la “Shinda na Kabumbu” inayowawezesha wadau wa soka na wateja wa kampuni hiyo kushiriki kwa kutuma neno SOKA kwenda namba 15725 na kujibu maswali mbalimbali yanayohusiana na soka. Zaidi ya wadau 60 wamejinyakulia pesa taslimu kupitia promosheni hii.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati) akiongea kwa simu na Raymond Mwegoha mkazi wa Dar es Salaam aliyeibuka mshindi wa wiki na kujishindia kitita cha shilingi Milioni 1/= katika promosheni ya “SHINDA NA KABUMBU” inayoyawezesha wadau wa soka na wateja wa kampuni hiyo kushiriki kwa kutuma neno SOKA kwenda namba 15725 na kujibu maswali mbalimbali yanayohusiana na soka. Zaidi ya wadau 60 wamejinyakulia pesa taslimu kupitia promosheni hii. Wanaoshuhudia kushoto ni Ofisa Mwandamizi wa Bodi ya Kusimamia Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudini Abdulhussen na Ofisa Masoko wa kampuni hiyo Prestin Lyatonga (kulia).

Article 15

KAMPUNI YA NABAKI AFRIKA WAFUNGUA TAWI KUBWA JIJINI ARUSHA

$
0
0
SAM_0100
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa kampuni ya Nabaki Afrika Hamish Hamilton akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa tawi kubwa la Arusha uliofanyika hivi karibuni
SAM_0113
SAM_0109
Kulia niTania Hamilton akiwa na mumewe mwenyekiti wa kampuni Nabaki Afrika Hamish Hamilton
SAM_0128
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa kampuni ya Nabaki Afrika Hamish Hamilton akiwa anampa maelekezo mteja aliyetembelea tawi hilo siku ya ufunguzi hivi karibuni Nabaki Afrika imefungua rasmi tawi kubwa jijini Arusha eneo la njiro nyuma ya petro stationya BP katika jingo la RSA

Aidha mafanikio hayo yamepatikana baada ya kutoa huduma yake Arusha kwa miaka miwili katika tawi eneo nane nane njiro Arusha,Sambamba na kuzinduzindua tawi hili Nabaki Afrika imesherehekea miaka 20 tangu kuzaliwa kwake hapa Tanzania jijini Dar es saalam

Katika hatua nyingine Nabaki Afrika imejipanga zaidi katika kuboresha zaidi huduma kwa wateja wake ili kuwawezesha watanzania wote kufanya ujenzi bora na si bora ujenzi

Kwa upande wake msimamizi mkuu wa tawi hilo Jesse Madauda alisema kuwa watu mbalimbalii wajitokeze katika tawi hilo ili waweze kupata msaada zaidi katika ushauri na bidhaa zenye ubora wa hali ya juukatika ujenzi

Naye mwanzilishi wa kampuni hiyo Hamish Hamilton alisema changamoto pamoja na mafanikio waliyoyapata kupitia wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwa ni watu wakujituma katika kazi


Pia alisema kuwa kauli mbiu ya kampuni hiyo ni kuwa imejaribiwa imepimwa imeaminiwa na watanzania kwa mda mrefu sasa(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge, Mh. Mussa Azan Zungu akiongozwa na Mpambe wa Bunge kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati alipositisha kikao cha Bunge cha asubuhi leo Novemba 26, 2014.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Mbunge wa Urambo, Mh. Samuel Sitta (katikati) akizungumza na baadhi ya wabunge wa Upinzani, Bungeni mjini Dodoma leo Novemba 26, 2014.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizugumza na Mbunge wa Viti Maalum Rachel Mashishanga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo Novemba 26, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Programu ya Safaari Lager Wezeshwa msimu wa nne yazinduliwa mkoani Morogoro

$
0
0
Balozi wa Programu ya Safaari Lager Wezeshwa msimu wa nne, Samira Kadelwa akigawa vipeperushi kwa wajasilamali mbalimbali wa Mkoa wa Morogoro wakati wa uzinduzi wa Proramu hiyo mkoani humo uliofanyika jana.Jumla ya milioni 220 zinatarajiwa kugawiwa kwa wajasiliamali kwa awamu hii ya nne chini ya bia ya Safari Lager.
Balozi wa Programu ya Safaari Lager Wezeshwa msimu wa nne, Catherine Oden akigawa vipeperushi kwa wajasilamali mbalimbali wa Mkoa wa Morogoro wakati wa uzinduzi wa Proramu hiyo mkoani humo uliofanyika jana.Jumla ya milioni 220 zinatarajiwa kugawiwa kwa wajasiliamali kwa awamu hii ya nne chini ya bia ya Safari Lager.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Kimataifa la kuchochea mwamko wa nafasi ya mabingwa wa uchunguzi tiba katika kuboresha huduma za tiba. Kongamano hilo linalofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, limewakutanisha mabingwa wa tiba za afya kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika.

baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia katika ufunguzi wa Kongamano hilo leo Novemba 26, 2014.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU KUADHIMISHA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA KESHO

$
0
0
 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephrahim Kwesigabo, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu Siku ya Takwimu Afrika itakayo adhimishwa Dar es Salaam kesho. Kulia ni Mtakwimu Mkuu, Adella Ndesengia.
 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephrahim Kwesigabo, akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kuhusu Siku ya Takwimu Afrika itakayo adhimishwa Dar es Salaam kesho.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephrahim Kwesigabo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kuhusu Siku ya Takwimu Afrika itakayo adhimishwa Dar es Salaam kesho. (PICHA NA VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO).

Tanzania itaungana na nchi nyingine barani Afrika katika kuadhimisha Siku ya Takwimu Afrika ambayo itafanyika tarehe 27 Novemba, 2014 katika ukumbi wa mikutano uliopo Jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema lengo la kuadhimisha siku hiyo ni kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa tasnia ya takwimu katika kuleta maendeleo  ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.Kwesigabo amesema kuwa, Kaulimbiu ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka 2014 ni “Takwimu Huria kwa Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa Wadau wote”.

“Kaulimbiu ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka huu imebeba ujumbe muafaka ambapo kwa kuwa sasa maendeleo ya Afrika yanategemea takwimu huria katika kuongeza uwajibikaji na ushirikishwaji katika kuandaa sera, kupanga na kutathmini mipango mbalimbali ya maendeleo na kufanya maamuzi sahihi, amefafanua Kwesigabo”.

Takwimu huria ni takwimu na taarifa zinazozalishwa kwa ubora na viwango kutokana na tafiti au taarifa za kiutawala ambazo zinatolewa, kusambazwa na kutumiwa na mtu yeyote bila kikwazo chochote.  Akielezea baadhi ya sifa za takwimu huria Mkurugenzi Kwesigabo amesema ni pamoja na upatikanaji wake kwa urahisi kulingana na mahitaji ya watumiaji, ziwe kamilifu kwa kutoa ujumbe sahihi na unaoeleweka na ziwe katika mfumo 

utakaomrahisishia mtumiaji kuzitumia kulingana na mahitaji yake pasipo kizuizi chochote.  Sifa nyingine za takwimu huria ni kutokuwa na ubaguzi, zitolewe kwa wakati, na muundo wa uhifadhi wake uwe rahisi ambao unaweza kusomeka katika programu mbalimbali za kompyuta.

Kwesigabo ameongeza kuwa Serikali ya nchi yoyote inapokuwa na mfumo wa takwimu huria, huwezesha wananchi na wadau wengine kupata taarifa na takwimu zinazozalishwa katika nchi hiyo bila kizuizi chochote. Aidha, huongeza uwazi na ushirikishwaji wa wananchi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali.

Washiriki mbalimbaliwa kutoka katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wadau wa Maendeleo, Vyuo vya Elimu ya Juu, Wanafunzi wa Shule za Sekondari pamoja na Wadau wengine wa takwimu nchini wanatarajia kuhudhuria katika maadhimisho hayo. Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika hufanyika tarehe 18 Novemba, kila mwaka lakini kwa Tanzania maadhimisho hayo yatafanyika kesho tarehe 27 Novemba, 2014.

msikilize mwenyekiti wa PAC MHE ZITTO KABWE AKISOMA RIPOTI YA ESCROW BUNGENI SASA KUPITIA KWANZA JAMII RADIO

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images