Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 653 | 654 | (Page 655) | 656 | 657 | .... | 3270 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Jumanne Sagini akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) Daftari la Wapiga Kura linalotumika kuandikisha wananchi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa.

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akiongea na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Desemba 14 mwaka huu ambapo amesema hadi sasa maandalizi yote yamekamilika. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa na kulia ni Afisa Mwandamizi wa TAMISEMI Bw. Mohamed Mavura.

   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye  Daftari la Wapiga Kura ili waweze kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu. Pia Katibu Mkuu huyo amewataka Viongozi wote wanaosimamia uchaguzi huo kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa na kulia ni Afisa Mwandamizi wa TAMISEMI Bw. Mohamed Mavura.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini  akitoa wito kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wagombea na Washabiki wao kuendesha kampeni kwa amani, utulivu na ustaarabu bila kukiuka kanuni na taratibu zilizowekwa. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Jumanne Sagini akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Mwaka 2014 ambazo tayari zimesambazwa kwa wadau wote wa uchaguzi huo. Aidha amesema kuwa Kanuni hizo zimewekwa katika Tovuti ya TAMISEMI ambayo ni www.ps@pmoralg.go.tz . Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa.  Mratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kutoka TAMISEMI Bw. Denis Bandisa akifafanua utaratibu wa kumuandikisha Mpiga Kura katika Daftari laWapiga Kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 20 kwa ajili ya Uchaguzi huo. (PICHA NA MAELEZO).

  0 0

   Mchezaji mpya wa Yanga, Emerson Oliveira Neves Roque akiwasalimia mashabiki wake timu hiyo, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
    Mchezaji mpya wa Yanga, Emerson Oliveira Neves Roque akiwasalimia kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
    Mchezaji mpya wa Yanga,Emerson Oliveira Neves Roque (katikati) mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere. Kushoto ni Andrey Coutinho

   Mchezaji mpya wa Yanga, Emerson Oliveira Neves Roque (kushoto) akiwasalimia mashabiki wa timu hiyo, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na mchezaji mwenzake Andrey Coutinho (katikati).

  Mchezaji mpya wa Yanga, Emerson Oliveira Neves Roque (kulia) akiwa na wadau wa Klabu ya Yanga.
  Maximo akiwasili. 

  0 0

   Ndugu wa Marehemu Sebastian Mgimba Philipo Mgimba (katikati) akiwa amebeba msalaba huku pembeni ndugu mwingine akiwa pamoja na picha ya marehemu wakati wa misa fupi ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam leo.
  Dada wa Marehemu Sebastian Mgimba, Mariam akiwa na ndugu zake wakati wa sala ya mazishi iliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni leo
   Rafiki wa Marehemu akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Sebastian Mgimba mara baada ya sala fupi ya mazishi kufanyika
   Baba Mzazi wa Marehemu Sebastian Mgimba, Mzee Mgimba pamoja na Mama wakiwa na shada la maua tayari kwa kuweka juu ya kaburi la Mtoto wao Marehemu Sebastian Mgimba.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   ·         Wafanyakazi wa Airtel kutembea ili kukusanya jumla ya zaidi ya milioni 10.
  ·         Wafanyakazi wa Airtel kukarabati darasa na kununa madawati shule ya kumbukumbu.

  Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake maalumu wa “Airtel tunakujali” imeandaa matembezi ya hisani huku ikialika wadau wote wenye wito wa kuchangia elimu kuungamkono jitiada hizo ili kukamilisha lengo la kuikarabati shule ya msingi kumbukumbu iliyopo kinondoni jijini Dar es Saalam.

  Matembezi hayo yanayoandaliwa na wafanyakazi wa Airtel yatashirikisha wadau mbalimbali na yatafanyika siku ya Jumamosi tarahe 29/11/2014 kuanzia saa moja asubuhi katika viwanja vya ofisi ya Airtel Makao makuu Morocco.

  Akiongea kuhusu Matembezi haya Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema “wafanyakazi wa Airtel nao wameona mapungufu yaliopo shuleni hapo na kuamua kujitosa kwa kutumia sehemu ya kipato chao kuihudumia jamii kwa njia hii, kila mfanyakazi wa airtel ambae amehamasika tayari ameshachangia.

  Na sasa tumeona ni vyema kuishirikisha jamii pia wakiwemo wanafamilia, marafiki na wote wenye wito wa kuchangia elimu kuungana nasi kuhakikisha watoto wanaosoma shule ya kumbukumbu wanasoma katika mazingira mazuri

  “Lengo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 10 ili kukarabati darasa moja na kununua madawati kwa ajili ya darasa la wanafunzi wa darasa awali”  
  Tutafanya Matembezi ya Kilomita 5 ambapo ni ya wazi ili kila mtanzania aweze kushiriki na kuchangia, pia kutakuwa na Tshirt maalumu zinapatikana katika ofisi ya Airtel Makao Makuu kwa gharama ya shilingi 15,000. Kwa kununua lengo ni kumfanya kila mmoja aweze kuchangia.

  Tunatoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kuungana nasi katika matembezi haya kwa kununua tshirt hizi maalumu na kwa kujitokeza kutembetea nasi ili kuwezesha vijana wetu ambao ni taifa la kesho kupata elimu bora ,katika mazingira mazuri  na yaliyoboresha zaidi. Aliongeza Hawa

  Airtel chini ya mpango wa”Airtel Tunakujali” unaoendeshwa na wafanyakazi katika vitengo mbalimbali umeshika kasi ambapo kitengo cha huduma kwa wateja kilifanya burudani na kumshirikisha banana zoro na mzee king Kikii na sasa kitengo cha rasilimali watu na ofisi ya mkurugenzi imeandaa matembezi ya hisani lengo likiwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayozunguka jamii hususani kwenye elimu ambapo utekelezaji wake unategemea kutafanyika mapema mwakani.

  0 0

   
   Bibi Harusi Mtarajiwa Noreen Mhina  akiwa katika nyuso ya Furaha, jana tarehe 25.11.2014
    
   Bibi Harusi Mtarajiwa Noreen akiwa amempata Mume wake mtarajiwa Leonard  Baada ya kumsaka ukumbi Mzima kwa ajili ya kumtambulisha kwa wageni waalikwa .
   Bibi harusi Mtarajiwa Noreen akimvisha Mume wake mtarajiwa Leonard  zawadi ya Saa Mara baada ya kutambulishwa Rasmi wa wageni waliofika katika Sherehe ya kumuaga.


  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Jumanne Sagini akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) Daftari la Wapiga Kura linalotumika kuandikisha wananchi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akiongea na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Desemba 14 mwaka huu ambapo amesema hadi sasa maandalizi yote yamekamilika. Kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi huo Bw. Denis Bandisa na kulia ni Afisa Mwandamizi wa TAMISEMI Bw. Mohamed Mavura.

  0 0

   Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Industries Group), mfanyabiashara maarufu Afrika, Alhaji Aliko Dangote akitumia gari kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda chake kikubwa cha saruji katika Kijiji cha Msijute, mkoani Mtwara leo.
   Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Industries Group), mfanyabiashara maarufu Afrika, Alhaji Aliko Dangote (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara leo.


  0 0

  Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe Zitto Kabwe akisoma Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya ESCROW Bungeni Mjini Dodoma leo.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati akiendesha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
  Baadhi ya wahudumu wa Bunge wakigawa Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW kwa Wabunge
  Waheshimiwa Wabunge wakipitia ripoti ya GAG kwa makini wakati ikisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe.

  0 0

  Mgeni Rasmi Waziri wa Maendeleao ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (MB) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki ndani ya Ziwa Viktoria Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya ya vizimba (Cages). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe.John Henjewele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael M. Muhuga.
  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani akipandikiza vifaranga vya samaki ndani ya Ziwa Victoria, mradi unaotekelezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kutumia teknolojia mpya hapa nchini ya kuzalisha samaki kwenye vizimba.
  Picha ya vizimba ambavyo ufugaji wa samaki umeanza mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuzindua mradi huo na kupandikiza vifaranga vya samaki. Mradi unatekeleza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Wilaya ya Bunda, Kiteule cha Bulamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Economic Social Research Foundation (ESRF), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Ufugaji wa samaki kwa kutumia teknolojia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria, umekuwa ukitekelezwa pia na wenzetu wa Kenya na Uganda ambao wamepiga hatua kubwa.


  0 0


  Amref Health Africa in partnership with Ministry of Health, TACAIDS,UNAIDS in Tanzania and Salama Foundation will offer free HIV testing in multiple selected sites in Dar es salaam City on 29thNovember 2014. This is part of the national HIV Testing Campaign to mark the World AIDs Day in 2014.


  In Tanzania, sixty-two percent (62) of women and 47 percent of men have ever been tested and received the results of their HIV test according to the THMIS 2011/12. The results lead to a gap of 53% for men and 38% for women that needs HTC services.So, let us join together during this World AIDS Day to close the gap


  Knowing one’s status is the first step in getting to early treatment. Earlier testing leads to earlier diagnosis and better health outcomes. However, significant numbers of people living with HIV continue to present themselves for testing at a late stage, leading to adverse health outcomes. 
  In Dar es Salaam we will be commemorating the World AIDS Day on 29 of November by engaging community members including Public and Private sector for free HIV Testing and Counseling. Servises will be provided in the frollowng areas from 9.00AM to 5.00 PM.

  1: Mawasiliano Bus Stand: Behind Mawasiliano Towers, 
  Sam Nujoma Road

  2. Buguruni Market: Buguruni Market Bungoni Street

  3. Kariakoo Market: Kariakoo Market (Tandamuti street 
  and Swahili street)

  4. Mwembeyanga Ground: Tandika Mahunda Street

  5. Tandika Market: Tandika Sokoni Kivungo street

  6. Manzese: Mpakani Primary school. 

  Protect your Goal’ Campaign in Tanzania. ‘”LINDA GOLI LAKO is a UNAIDS global initiative to raise HIV awareness worldwide through the use of sports and the music industry. The campaign aims to raise awareness of HIV and to mobilize community  including young people to commit to HIV Prevention (Use of Condom, HIV Testing, and in reducing the number of sexual partners).


  0 0
 • 11/26/14--20:00: KUMBUKUMBU
 • MAREHEMU EMMANUEL ASUMWISYE MWASANGUTI

  Mpendwa wetu EMMANUEL (Ima), Siku zimepita na hatimaye zikawa wiki, na wiki ziKawa miezi. Leo tarehe 27 Novemba 2014 unatimiza MWAKA MMOJA tangu ulipotutoka kwa majonzi makuu kwa ajali ya gari iliyotokea Dar es Salaam.

  Tukikukumbuka machozi yangali yanatutiririka na kumbukumbu zingali mbichi kama vile ajali imetokea jana tu, hata hivyo tunamshukuru MUNGU mwenye uwezo wote kwa kutupigania hadi hivi leo. Kama familia tuna kumbukumbu nyingi juu yako kwa njia ya picha, utani na ucheshi wako, ndoto na matarajio yako mengi ya maisha ambavyo kwa ujumla wake tunavithamini sana. Safari yako hapa duniani japo ilikua fupi, imegusa maisha ya watu wengi na tunashukuru MUNGU kwa miaka aliyotuzawadia kuishi nawe katika familia yetu.

  Kwa upendo unakumbukwa na watoto wako uliowapenda sana JOSHUA and JOEL. Joshua, ingawa taratibu anakubaliana na kutokuwepo kwako, haachi kuuliza utarudi lini! Joel, mtoto uliyemwacha akiwa angali hajazaliwa, kwa neema na rehema za MUNGU mnamo tarehe 4 Aprili, 2014 alizaliwa akiwa na afya njema, alipewa jina la Joel Asumwisye.

  Unakumbukwa kwa uchungu na maumivu na wazazi wako – Asumwisye Sobha Mwasanguti na Twandege Kissale Mwasanguti, mke wako mpenzi Christabella Gonelimali, kaka na dada zako. Pia unakumbukwa na ndugu, jamaa, marafiki, majirani na pia wafanyakazi wenzako wa CRDB Bank Plc zaidi sana wale wa idara ya Treasury.

  Pengo uliloliacha halitazibika kamwe. Kwa ghafla, kufumba na kufumbia ulitutoka tukibaki kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu lakini ni MUNGU pekee anayejua ni kwanini aliruhusu haya yatokee!. Ingawa hatuko pamoja nawe, roho yako itaendelea kuishi ndani ya mioyo yetu milele! Tulikupenda sana lakini MUNGU alikupenda zaidi. Katika mikono ya BWANA unapumzika, katika mioyo yetu unaishi milele! 

  AMINA!

  0 0

  Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania nchini Marekani amemkaribisha Mhe. Ammon Mutembwa, Balozi mpya wa Jamhuri ya Zimbabwe Ubalozini Tanzania House, Washington DC, Marekani, Jumatano Novemba 26, 2014. 
  Katika mazungumzo yake na Balozi Mutembwa, Mhe. Balozi Mulamula alimweleza Balozi huyo kwamba ajisikie kwamba yuko nyumbani. 
  Mhe. Mulamula aliendelea kwa kusema kwamba Tanzania na Zimbabwe zina mahusiano ya kihistoria na kwa msingi huo ni vyema kutafsiri kwa vitendo mahusiano hayo kwa kujenga mashirikano zaidi baina yao. 
  Mhe. Mulamula alifurahishwa na ziara hiyo ya Balozi Mutembwa Ubalozini na kuahidi kwamba kupitia kwa Jumuia ya Ushirikiano wa Nchini za Kusini mwa Afrika (SADC), Tanzania na Zimbabwe zina fursa ya kutosha kuziwakilisha nchi zao nchini Marekani kwa manufaa ya Serikali na wananchi wao. 
   Kwa upande wake, Mhe. Balozi Mutembwa alimshukuru Mhe. Balozi Mulamula kwa kumkaribisha Ubalozini na kwamba kwa vile ndio kwanza ameripoti katika kituo chake kipya cha kazi atashukuru sana kupata mwongozo wake na ushauri kutoka kwake ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kiuwakilishi nchini Marekani kwa ufanisi. Balozi Mutembwa alisema pia kwamba moja ya jukumu lake kubwa ni kuhakikisha vikwazo ilivyoekewa nchi yake na Marekani vinaondolewa kupitia mazungumzo na kujenga maelewano mazuri baina ya nchi yake na Marekani.
   Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico(Kulia) akimkaribisha Mhe. Ammon Mutembwa,(Kushoto). Balozi  Mpya wa Jamhuri ya Zimbabwe nchini Marekani Ubalozini Tanzania House Washington DC,Marekani.
   Mhe.Balozi  Mulamula na Mhe. Balozi Mutembwa katika picha ya kumbukumbu baada ya kusaini kitabu cha wageni.
   Mhe. Balozi Liberata Mulamula(Katikati) akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mhe.Balozi Ammon Mutembwa (Wa pili kushoto) huku Maofisa wao Bw. Suleiman Saleh (Wa kwanza kulia) na Bw. Whatmore Goora (Wa kwanza kushoto) wakifuatilia. Picha na Mugendi Zoka

  0 0

   Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto (kulia). 

  WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda ametajwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ‘Usilie’ ambayo itapatikana kwenye DVD Desemba 7, mwaka huu.
  Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto, alisema hafla hiyo itafanyika kwenye Ukumbi wa PTA uliopo Uwanja wa Sabasaba, Dar es Salaam.
  Mbali ya uzinduzi huo Misheto alisema pia wasanii mbalimbali wa filamu watanogesha siku hiyo.
   Aliwataja waimbaji wa injili ambao watakuwepo siku hiyo kuwa ni Leah Mudy, AIC (T) Vijana Chang’ombe, Accasia Singers, Papson Mastaki kutoka Kenya na Frank Hume kutoka Boston nchini Marekani watatumbuiza.
  Uzinduzi huu umeratibiwa na Misheto Promotion, ambapo kabla ya uzinduzi huo kutafanyika huduma za bila malipo za kiafya na kitabibu kutoka kwa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali, ambayo yamekuwa yakiikabili jamii.
  Misheto ameyataja magonjwa hayo kuwa ni moyo, figo, kisukari na mengineyo ambapo huduma hiyo itatolewa na madaktari bingwa nchini. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
  “Huduma hii itaanza saa mbili asubuhi na itatolewa bure, ikiwemo ushauri na kwa wale ambao wataweza kutibika watatibiwa, ila ambao watakuwa kesi zao zimekuwa ni kubwa zaidi watapewa ushauri wa bure wa kuendelea na matibabu katika hospitali kubwa na hakutakuwa na kiingilio," alisema Misheto.

  0 0
  0 0

   Balozo Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga na Dkt. Asghar Farshad wa hospitali ya Iran huko Dubai wakitia saini makubaliano ambapo hospitali hiyo imetoa ofa ya punguzo la asilimia 40 ya malipo ya matibabu kwa Mtanzania yeyote atayekwenda kutibiwa hapo Iranian Hospital Dubao
   Balozo Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga na Dkt. Asghar Farshad wa hospitali ya Iran huko Dubai wakibadilishana hati za makubaliano ambapo hospitali hiyo imetoa ofa ya punguzo la asilimia 40 ya malipo ya matibabu kwa Mtanzania yeyote atayekwenda kutibiwa hapo Iranian Hospital Dubao
  Balozo Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga na Dkt. Asghar Farshad wa hospitali ya Iran huko Dubai wakionesha hati za  makubaliano ambapo hospitali hiyo imetoa ofa ya punguzo la asilimia 40 ya malipo ya matibabu kwa Mtanzania yeyote atayekwenda kutibiwa hapo Iranian Hospital Dubao

  0 0
 • 11/26/14--23:35: UNCDF VACANY ANNOUNCEMENT
 • vacancies
  Basically, professionals with this background:
  Required Skills and Experience
  Education:
  At least a Master’s Degree in Business Administration, Finance, Banking or related areas, plus preferably a Bachelor Degree in engineering, finance or economics.
  Experience:
  Preferably a minimum of 5 years of relevant experience;
  Ability to build partnerships and deliver results that meet the needs and long-term interest of clients within and outside the institution;
  Demonstrated experience in preparation of project financial analysis and creation/evaluation of advanced and complex Ms Excel spread sheet financial models;
  Demonstrated experience with private equity/venture investments, credit and risk assessment, with solid financial modelling and risk assessment skills. Project financing experience in the private sector is a plus;
  Demonstrated experience in preliminary evaluation of project proposals for assessing their feasibility for private sector funding and/or technical support by LFI.
  Here is the link with more information


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Canada Jack Mugendi Zoka alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo kwa Rais baada ya kuteuliwa rasmi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Canada Jack Mugendi Zoka aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha kwa Rais baada ya kuteuliwa.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi Mpya wa Tanzania Nchini Canada Jack Mugendi Zoka baada ya mazungumzo alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar baada ya kuteuliwa.[Picha na Ikulu.]

  0 0


  0 0

  Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu has commended a remarkable initiative by Tanzania National Parks in introducing new tourism products at Lake Manyara National Park. Nyalandu said this during the official launching of the hot springs boardwalk way and hippo pool viewpoint projects at the park yesterday. Nyalandu said that the two projects will add value to the tourism sector by increasing the number of tourist arrivals in the country and urged other stakeholders to be innovative in introducing products that will attract more tourists.

  The Manyara boardwalk way and hippo pool viewpoint projects worth about 200 millions were initiated to counter the decreased trend of tourist numbers in the park following the flashfloods hit the park in March 2013 which damaged most of tourist infrastructures.

  The first ever tourism product in the national parks, the boardwalk way is featured with 1.5 meters wide impressive wooden structure, creating a 300 meters long trail standing 1.5 meters above ground winding up in an observation platform that is 15 meters long and 2.5 meters wide. The trail meanders through the hot springs and lakeshore around a marsh and finally into the lake. The boardwalk will give visitors a unique view and wonderful photo opportunities at every turn of the boardwalk trail.

  Hot springs boardwalk way is designed to simply give people a nice place to walk along the numerous hot springs and be close to the attractions and enjoy the wide view of the lake.

  Visitors will use the facilities boardwalk way for free and have opportunity of walking around 600 meters on a return trip to the lakeshore and over the hot springs. Educational signage with entertaining themes will be erected in key locations to allow visitors’ easy reading and understanding of the nature and the resources found in the area. These signs will educate visitors about the ecology and adaptation of plants and animals to the area. Moreover, it will explain the fragility of the ecosystem and why it is so important to use the boardwalks to avoid, as much as possible, disturbing the environment.

  Moreover, the viewpoint is a freestanding wooden platform rising by 8 feet above the ground measuring 56 feet in length and 5 feet in width. It is about 8 km away from main gate. Standing at the top of the viewing platform enables the viewer a spectacular view of the marshland and its inhabitants – waterfowl, hippo, buffalo and wildebeest – from a point of vantage while affording the visitor a high sense of security.
  Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu unveils the foundation stone of the Lake Manyara hot springs boardwalk way yesterday.
  Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (2nd left) cut off ribbon to officially launch Lake Manyara hot springs boardwalk way and hippo pool view point in Lake Manyara. Others in the picture from left are Manyara Regional Commissioner Hon. Elaston Mbwilo; Director General of TANAPA Allan Kijazi and the Chairman of the Parliamentary Committee on Lands, Natural Resources and Environment Hon. James Lembeli.


  0 0
 • 11/27/14--01:34: ENEO LA SHULE LINAUZWA

 • VIWANJA HIVI VIPO KIGAMBONI,KATA YA PEMBA MNAZI,MTAA WA MUHIMBILI (TUNDWI CENTER),VIPO UMBALI WA MITA 600 - 700 KUTOKA BARABARA KUU,NI VIWANJA VILIVYOPIMWA.

  ENEO  LA SHULE NI KWA AJILI YA CHEKECHEA,PRIMARY PAMOJA NA SEKONDARI ,UKUBWA WA ENEO HILO NI  35,022 SQM.
  KWA MAELEZO ZAIDI JUU YA VIWANJA HIVYO,WASILIANA NA NDG. JAMES MPAYO KWA NAMBA HIZO HAPO CHINI.
  0784 207877 NA 0754 780878
  PIA UNAWEZA KUMTUMIA EMAIL: 
  JMPAYO@OVI.COM

older | 1 | .... | 653 | 654 | (Page 655) | 656 | 657 | .... | 3270 | newer