Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 651 | 652 | (Page 653) | 654 | 655 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akiliongoza Bunge mjini Dodoma leo,wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mtu mmoja kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kosa la kupatikana akisambaza Ripoti ya (ESCROW) ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kinyume na Sheria Baada ya Hoja iliyoibuliwa na Mbunge wa Kuteuliwa Mhe.James Mbatia.
  Mbunge wa Kuteuliwa Mhe.James Mbatia akiwa amekaa na Hasimu wake wa Siasa jimbo la Vunjo Mhe.Agustino Mrema wakimsikiliza kwa makini Spika wa Bunge Mhe.Anna Makinda.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisalimiana ya wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka Katoro-Busanda. Aliye valia gauni la njano ni Mbunge wa Busanda Mhe.Lolesia Bukwimba.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka Katoro-Busanda.
  Mbunge wa Busanda Mhe. Lolesia Bukwimba (kushoto) akimueleza jambo Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya juu ya ugeni wake wa wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka Katoro-Busanda,waliotembelea Bungeni Mjini Dodoma leo.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa chama cha kuweka na kukopa (SACCOS) kutoka Katoro-Busanda,waliotembelea Bungeni Mjini Dodoma leo.
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe. Sofia Simba (kushoto) akifurahia jambo na Mhe.Anna Mkinda wakati wakitoka katika kikao cha Bunge leo. Picha zote na Deusdedit Moshi

  0 0

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa tahadhari kwa wanawake wa jiji la Dar es Salaa hususani wasichana kuwa makini na wanaume wanaowataka kimapenzi na baadaye kuwauwa na kutelekeza miili yao.

  Zimekuwepo taarifa juu ya kuwepo kwa wanaume wawili wanaoshawishi wanawake kuwa nao kimapenzi na baada ya muda huwauwa. Hivyo natoa tahadhari kwa wanawake wa jiji la Dar es Salaam kuchukua tahadhali juu ya watu hawa maana huatarisha maisha yao au ya familia zao.

  Inaaminika watu hao huwashawishi akina dada au wanawake kwa jumla ili wawe nao kimapenzi huku wakiwasaidia kwa huduma mbalimbali za kimaisha na kisha kuwauwa.

  Natoa wito kwa wanawake wote kutokukubali kushawishiwa kirahisi na wanaume wasiowajua ambao wanataka kuwa nao kimapenzi na starehe kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kuingia katika mtego mbaya na pengine hata kuyaweka maisha yao rehani.

  Aidha, katika siku za hivi karibuni yameripotiwa matukio kadhaa ya mauaji ya aina hiyo ambapo kwa sasa wanawake wapatao sita tayari wamepoteza maisha. Haijafahamika madhumuni ya wauaji hao na huenda ni mambo ya ushirikina n.k.

  Msako mkali unaendelea ili kuwabaini na Jeshi la Polisi Kanda Maalum linatoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kutoa taarifa sahihi kwa Jeshi hilo na vyombo vingine vya usalama ili kuwabaini na kuwakamata ili sheria ichukue mkondo wake dhidi ya wahusika.

  S. H. KOVA
  KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
  DAR ES SALAAM

  0 0

  Na Asteria Muhozya, Dare s Salaam

  Wizara ya Nishati na Madini imekutana na wadau wa madini ya Shaba katika mkutano wa siku mbili ulioanza tarehe 24- 25 Novemba, 2014 na kuwashirikisha wafanyabiashara wa madini hayo, wachimbaji wadogo, viwanda vya kuyeyusha madini ya Shaba, Makamishana Wasaidizi wa Madini kutoka Kanda mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa Madini Wakaazi.

  Akifungua mkutano huo, unaolenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ndogo ya madini ya Shaba na namna ya kuyaongezea thamani madini hayo, Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja amewataka wachimbaji wadogo nchini kutumia fursa zinazotolewa na Wizara ya Nishati na Madini ikiwemo kupata ruzuku ili waweze kuendeleza shughuli za uchimbaji wa madini jambo ambalo litasaidia kuyaongezea thamani madini hayo.

  Aidha, Kamishna Masanja ametumia fursa hiyo, kuwataka wachimbaji na wafanyabiashara kuacha kufanya biashara kinyume na sheria na taratibu kwa kuwa jambo hilo linaikosesha Serikali mapato ikiwemo kuchangia madini hayo kutokupata thamani halisi.

  Vilevile Kamishna Masanja ameeleza kuwa, Serikali itaendelea kuzuia usafirishaji madini ghafi ya Shaba na kueleza kuwa, “Haturuhusu madini ghafi ya shaba kutoka nje, tunataka yatoke yakiwa tayari ni madini, kwasababu kuna zaidi ya shaba hivyo tunapoteza, tunataka kuyaongeza thamani madini yetu hapa hapa nchini”, alisisitiza Masanja.
  Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja (katikati) akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba. Wengine kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Dominick Rwekaza, Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje, Kaimu Kamishna Msaidizi sehemu ya Uongezaji Thamani Madini, Latifa Mtoro na Mwakilishi wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA), John Mvumula.
  Mfanyabiashara wa madini ya Shaba kutoka Kanda ya Kati Doreen Kisia, akisistiza jambo wakati akichangia hoja katika mkutano huo.
  Mmoja wa washiriki wa mkutano huo, akiongea jambo wakati akichangia mada kuhusu madini ya Shaba.
  Kamishna Msaidizi Kamishna Msaidizi wa Madini na Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje, akisalimiana na baadhi ya wadau wa madini ya Shaba waliohudhuria mkutano huo.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Dominick Rwekaza, (kulia) akiongea jambo wakati wa mkutano huo.
  Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja (katikati) katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa wadau wa madini ya Shaba ambao umewajumuisha wafanyabiashara wa madini ya Shaba, wachimbaji wadogo, viwanda vya kuyeyusha madini ya Shaba, Makamishna Wasaidizi wa Madini kutoka Kanda mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa Madini Wakaazi.

  0 0
 • 11/24/14--23:30: Article 22


 • 0 0

  Marehemu Mathew Sebastian Mgimba Enzi za Uhai Wake.

  2Timotheo 4:7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza Imani nimeilinda.

  Familia ya Ndugu Sebastian Mgimba inasikitika kutangaza kifo cha Mpendwa wao Mathew Sebastian Mgimba kilichotokea Nchini Malaysia tarehe 20/11/2014.
  Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili leo tarehe 25/11/2014 na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwao Sinza Kumekucha.
  Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi - Amina

  0 0

  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF umekuwa Mshindi wa kwanza miongoni mwa taasisi za serikali na mashirika ya umma yanayofanya manunuzi makubwa nchini na hivyo kutunukiwa tuzo ya uzingatiaji wa taratibu na kanuni za manunuzi kwa kipindi cha mwaka 2013/2014.

  TASAF imekuwa miongoni mwa taasisi zilizoshinda tuzo ya ubora wa manunuzi kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka 2013/2014 na kukabidhiwa tuzo katika hafla iliyofanyika mjini Nairobi nchini Kenya ambako Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga aliipokea tuzo kwa niaba ya taasisi hiyo ambayo kwa sasa iko katika jitihada kubwa za kulisaidia taifa kuondokana na umaskini kupitia mpango wake wa kunusuru kaya maskini PSSN.

  Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus Mwamanga  amesema licha ya taasisi yake kufanya manunuzi makubwa kutokana na uwingi wa shughuli za kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya maskini, kanuni, taratibu na sheria za manunuzi ya umma zimekuwa zikizingatiwa kwa kiwango kikubwa. Bw. Mwamanga amesema kwa takribani miaka mitatu mfululizo TASAF imekuwa ikipata hati safi ya manunuzi na kuwa miongoni mwa taasisi za serikali na mashirika ya umma zinazofanya vizuri katika uzingatiaji wa sheria ya manunuzi nchini.

  Zifuatazo ni picha za upokeaji wa tuzo hiyo zilizofanyika Nairobi-Kenya
   Mkurugenzi  Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (mwenye Kaunda suti) akiwa  na ngao ya ushindi wa kwanza ya uzingitiaji wa kanuni za manunuzi nchini kwa mwaka 2013/14

   Mkurugenzi  Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (kushoto) aliyeshika ngao ya ushindi  wa kwanza (kulia kwake) ni  Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA Bw. Marten Lumbanga.

  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Susan Mlawi (kushoto) alikuwa miongoni  mwa wageni walioalikwa kwenye hafla ya kukabidhi  tuzo ya manunuzi kwa taasisi za Serikali na mashirika ya umma kwa nchi za Afrika Mashariki iliyofanyika mjini Nairobi, Kenya
   Baadhi ya viongozi wa taasisi zilizo shinda tuzo ya manunuzi  kwa mwaka  2013/14 kutoka nchi za Afrika Mashariki.

  0 0  Sekretariet ya jumuiya ya waliosoma shule ya sekondari Mzumbe (Mzumbe Secondary School Alumni) inawataarifu wanajumuiya wote kuwa Jumamosi ya Tarehe 29 mwezi Novemba 2014kutafanyika mkutano wa wanachama wote jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Jolly Club - Isumba Lounge kuanzia saa nane mchana.

  Tangu kuanzishwa kwake Jumuiya ya waliosoma Mzumbe Sekondari imeshirikiana na uongozi wa shule hiyo kuainisha maeneo mbalimbali ambayo jumuiya hiyo itashiriki kuyaboresha.
  Katika mkutano huo wa wanachama wote, uongozi wa jumuiya utachaguliwa na mpango mkakati wa miaka mitano utajadiliwa.


  Mafanikio ya malengo ya kuiboresha Shule ya Sekondari Mzumbe yanaanza na ushiriki wa kila aliyesoma Mzumbe. Upatapo ujumbe huu, tafadhali wafikishie taarifa wanajumuiya wengine.


  Kuthibitisha ushiriki wako wa kikao tuma ujumbe kwa etalawa@gmail.com , au SMS to 0784 250 5040652 429 308 ; 0767 210 827

  Eddy Talawa
  Mwenyekiti wa muda,
  Jumuiya ya waliosoma shule ya sekondari Mzumbe‍

  0 0

  Mkutano wa 16 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika Tarehe 30 Novemba, 2014 Nairobi, Kenya. 

  Kwa mujibu wa Mkakaba Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri la
  Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Tarehe 20 – 27 Novemba, 2014 katika  ngazi ya Wataalam, Makatibu Wakuu na Mawaziri. Aidha, katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa uwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha mwaka mmoja na Jamhuri ya Kenya inayomaliza kipindi chake, Ikiwa ni utekelezaji wa Ibara ya 12 (2) ya Mkataba wa Uanzishaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Akizungumzia Tanzania kuchukua Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika  Mashariki Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo alisema, “Katika kipindi cha uenyekiti wake, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendeleza mafanikio yaliyopatikana wakati wa kipindi cha uenyekiti wa Jamhuri ya Kenya. Aidha, mkazo utawekwa katika kuhakikisha mtangamano wa Afrika Mashariki unaendelezwa kwa kuzingatia matakwa ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya pamoja na Kanuni na Taratibu za Jumuiya. 

  Aidha, mkazo utawekwa katika kuhakikisha Sekta binafsi na Wadau wengine wanashirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wa mtangamani wa Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuzitumia fursa zitokanazo na Jumuiya ya Afrika Mashariki,”


  0 0

  Tembelea Vituo Vya Mauzo 
  Ujipatie Tiketi Yako Sasa.
  1.Samaki Samaki-Mlimani City na Posta
  2.Tripple 7  - Kawe
  3.Didis - Oysterbay
  4.Born 2 Shine - Mwenge

  0 0

  _N0A0439
  Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Habari, vijana, utamaduni na michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, akiongea neno wakati wa uzinduzi.

  _N0A0239
  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba akielezea jambo katika hafla za uzinduzi wa Tuzo za Filamu Tnzania zilizofanyia mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam._N0A0270 Vijana kutoka Kigamboni Community Center wakitoa burudani wakati wa hafla za  uzinduzi wa Tuzo za Filamu Tnzania zilizofanyia mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mwenyekiti Mteule katika Uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi,Ndg. Zefrin Lubuva (kulia) akirejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi,Bi. Vicky Mwakasonda katika ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Oysterbay,jijini Dar es Salaam jana.
  Mwenyekiti Mteule katika Uchaguzi wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi,Ndg. Zefrin Lubuva akisaini fomu mbele ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi,Bi. Vicky Mwakasonda wakati alipozirudisha katika ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Oysterbay,jijini Dar es Salaam jana.Kulia ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Oysterbay,Ndg. Joackim Ngonyani.


  0 0

   Mkurugenzi wa Airtel Huduma kwa Wateja,Bi.Adriana Lyamba akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Simba ya UDOM kwa kuibuka washindi wa mashindano ya Airtel Uni 255,yaliyofanyika katika viwanja vya michezo ndani ya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),Mashindano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
   Timu ya Simba ikishangilia mara baada ya kukabidhiwa kombe lao mara baada ya kuibuka kinara katika mashindano ya Soka ya Airtel 255.
   Aidha Aneth Mugha ambaye ni Meneja Masoko wa Airtel alikifafanua mbele ya Wanafunzi wa UDOM (hawapo pichani),namna vocha mpya ya Airtel Uni 255 inavyoweza kuwanufaisha katika suala zima la kuperuzi kwa gharama nafuu kuliko zote wakiwa chuoni hapo.Bi, Aneth alisema kuwa Airtel Uni 255 ni huduma maalum kwa vyuo vikuu inayomuwezesha mwanafunzi kupata huduma nafuu ya mawasiliano ikiwemo kupiga simu, sms, na intanet ili kwasaidia wanafunzi kutumia huduma hiyo kujiendeleza kimasomo.
   Baadhi ya Wanafunzi wakishuhudia burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye jukwaa la Airtel Uni 255,baada ya mashindano ya Soka kumalizika na kumpata mshindi,Wasanii waliotoa burudani kwenye jukwaa hilo ni Roma,Ney wa Mitego pamoja na Vanessa Mdee a.k.a V-Money na burudani nyingine,ambapo wasanii chipukizi walishindana kughani na kuibuka na zawadi mbalimbali zikiwemo simu za mikononi,fulana na nyinginezo.
   Baadhi ya Wanafunzi wa chuo cha Dodoma (UDOM) wakiwa jukwaa wakijiunga na huduma maalum ya UN 255,ambayo imetolewa kwa ajili yao.Airtel Uni 255 ni huduma maalum kwa vyuo vikuu inayomuwezesha mwanafunzi kupata huduma nafuu ya mawasiliano ikiwemo kupiga simu, sms, na intanet ili kwasaidia wanafunzi kutumia huduma hiyo kujiendeleza kimasomo.

  Aidha Aneth Mugha ambaye ni Meneja Masoko aliwatangazia Wanafunzi wa UDOM,namna vocha mpya ya Airtel Uni 255 inavyoweza kuwafaidisha kuperuzi kwa gharama nafuu kuliko zote wakiwa chuoni hapo.
   Baadhi ya Wanafunzi wa UDOM wakishangilia burudani iliyokuwa ikitolewa kweye jukwaa la burudani la Airtel Uni 255,ambapo wasanii mbalimbali walitumbuiza akiwemo Ney wa Mitego,Roma Mkatoliki pamoja na Vanessa Mdee a.k.a V-Money.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya Wanawake  Tanzania (TWB), Magareth Chacha  (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichai) wakati wa hafla ya kukabidhi hati za viwanja kwa wateja walionunua na waliomaliza kulipa mikopo yao, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Benki hiyo, Aaron Nyanda na Mwanasheria wa Ardhi Plan Ltd, Musa Maghimbi. (Picha na Francis Dande) 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya Wanawake  Tanzania (TWB), Magareth Chacha  (wa pili kushoto) akimkabidhi hati ya kiwanja, Mhindi Mayenga wakati wa hafla ya kukabidhi hati za viwanja kwa wateja walionunua na waliomaliza kulipa mikopo yao, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Benki hiyo, Aaron Nyanda na kulia ni Mwanasheria wa Ardhi Plan Ltd, Musa Maghimbi. 
  Wateja wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) wakiwa wameshika hati zao za viwanja baada ya kukabidhiwa na uongozi wa benki hiyo. Kutoka kushoto ni Belinda Rweyemamu, Mhindi Mayenga na Gabriel Kameka.

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation) na Miss Tanzania 2012,Bi. Brigitte Alfred akimtumza mmoja wa vijana wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao wako chini ya Taasisi hiyo,aliekuwa akighani shairi alilolitunga,wakati wa hafla ya kusherehekea Mafanikio ya Vijana hao iliyofanyika leo kwenye Viwanja Makumbusho,Jijini Dar es Salaam.Taasisi ya BAF kupitia Mpango wake wa JA (Juniour Achievement) imeweza kuelimisha vijana 50 wenye ulemavu wa ngozi katika mpango wa kutoa elimu ya kujitambua, ujasiriamali na stadi za biashara ili waweze kuthubutu, kuanzisha na kuendeleza biashara na shughuli nyingine za kiuchumi zitakazo wapa ajira, kipato na kuinua ustawi wa maisha yao na familia zao.

  Kijana mwenye ulemavu wa ngozi (albino) akighani mashairi yake.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation) na Miss Tanzania 2012,Bi. Brigitte Alfred akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pugu waliofika kwenye hafla hiyo ya kusherehekea Mafanikio ya Vijana,yaliyofanyika leo kwenye Viwanja Makumbusho,Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation),Bi. Brigitte Alfred akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vijana wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao wako chini ya Taasisi hiyo.
  Baadhi ya Wanahabari waliohudhulia hafla hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation) na Miss Tanzania 2012,Bi. Brigitte Alfred pamoja na baadhi ya vijana wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao wako chini ya Taasisi hiyo.

  0 0

  Watanzania wanatakiwa kupigia kura jezi ya timu ya Taifa ya nyumbani na ugenini kupitia mtandao wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa www.tff.or.tz ambapo jezi hizo zimewekwa.

  TFF ilipokea mapendekezo ya mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa kutoka kwa Watanzania 86. Jezi 11 za nyumbani, bukta nane za nyumbani, jezi nane za ugenini na bukta tano za ugenini ndizo zimepitishwa kwa ajili ya kupigiwa kura.

  Mwisho wa kupiga kura ni Desemba 31 mwaka huu. Mpigaji kura anatakiwa kubonyeza kwenye jezi na bukta ambayo ameichagua. Anatakiwa kufanya hivyo kwa jezi ya nyumbani na jezi ya ugenini.

  Tunawashukuru wote waliojitokeza kupendekeza mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa.


  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


  0 0

  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeendesha mafunzo ya Maadili kwa maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi walioko Zanzibar. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano ulioko katika Chuo cha Polisi mjini Zanzibar.

  Mafunzo hayo yana lengo la kuwasaidia watendaji hao wa Jeshi la Polisi walioko Zanzibar kuweza kuondokana na changamoto nyingi za uvunjifu wa maadili ambazo watendaji hao wamekuwa wakikabiliana nazo.

  Mafunzo hayo pia yana lengo la kuwakumbusha watendaji hao jinsi ya kuboresha na kuimarisha utendaji kazi ndani ya jeshi hilo huku wakizingatia maadili wakati wa utendaji kazi zao katika utumishi wa umma.

  Akifungua mafunzo hayo Kwa niaba ya Kamishna wa Maadili, Mjumbe wa Baraza la Maadili Mhe. Hilda Gondwe aliwakumbusha watendaji hao wa Jeshi la Polisi Zanzibar na watendaji wengine kuwa wana wajibu mkubwa wa kulinda na kusimamia maadili ndani ya jeshi hilo ili kulinda imani ya wananchi kwa jeshi la polisi

  Aliwataka watendaji hao kuzingatia maadili kwani kwa kufanya hivyo kutaimarsiha utawala bora nchini na kuimarisha utendaji kazi kwa ujumla na hivyo kuboresha utendaji kazi katika maeneo yao.

  Mafunzo hayo yamewashirikisha watendaji waandamizi wa jeshi la polisi walioko Zanzibar kutoka katika mikoa mitatu ya kipolisi ya Kusini, Kaskazini na Mjini Magharibi kama OCD, RCO ambapo maafisa 35 walitarajiwa kuhudhuria mafunzo hayo.

  Katika mafunzo hayo jumla ya mada tatu za Sheria ya Maadili, Fomu ya Tamko la Mali na Madeni na Mgongano wa Maslahi ziliwasilishwa na wataalamu kutoka Sekretarieti ya Maadili
  Mjumbe wa Baraza la Maadili Mhe.Hilda Gondwe akifungua rasmi mafunzo ya MAADILI kwa maafisa wa Polisi mjini Zanzibar.
  maafisa wa Polisi wakimsikiliza mgeni rasmi wakati akifungua mafunzo ya MAADILI katika chuo cha Polisi Zanzibar.
  washiriki wa mafunzo ya MAADILI kwa maafisa wa Polisi mjini Zanzibar katika picha ya pamoja na mgeni rasmi baada ya kufungua mafunzo hayo.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya Wanawake  Tanzania (TWB), Magareth Chacha  (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichai) wakati wa hafla ya kukabidhi hati za viwanja kwa wateja walionunua na waliomaliza kulipa mikopo yao, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Benki hiyo, Aaron Nyanda na Mwanasheria wa Ardhi Plan Ltd, Musa Maghimbi. (Picha na Francis Dande) 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya Wanawake  Tanzania (TWB), Magareth Chacha  (wa pili kushoto) akimkabidhi hati ya kiwanja, Mhindi Mayenga wakati wa hafla ya kukabidhi hati za viwanja kwa wateja walionunua na waliomaliza kulipa mikopo yao, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Benki hiyo, Aaron Nyanda na kulia ni Mwanasheria wa Ardhi Plan Ltd, Musa Maghimbi. 
  Wateja wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) wakiwa wameshika hati zao za viwanja baada ya kukabidhiwa na uongozi wa benki hiyo. Kutoka kushoto ni Belinda Rweyemamu, Mhindi Mayenga na Gabriel Kameka.

  0 0

  Wakati usajili kwa watu wanaotaka kushiriki mbio ndefu za Uhuru, maarufu kama Uhuru Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Desemba 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam ukiendelea kwa kasi kubwa waandaaji wa mbio hizo wamezindua mpango wa kujenga kituo cha michezo eneo la msoga mkoani pwani.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya mbio hizo, Innocent Melleck alisema,kamati ya uhurumarathon imeona umuhimu wa kuanzisha kituo hicho ambapo jumla ya shilingi bilioni  nne nukta nane (4.8bl) zinatarajiwa kutumika katika kukamilisha mpango huo

  “Tunapenda kutangaza rasmi kwamba Uhurumarathon imenunua shamba eneo la msoga mkoani pwani lenye ukubwa wa ekari ishirini na tano kwa lengo la kujenga kituo kikubwa cha kukuza vipaji vya wanamichezo mbalimbali mkoani pwani eneo la msoga na kitajulikana kwa jina la Jakaya Kikwete Uhuru Sports Accademy na jumla ya michezo kumi na moja itahusishwa katika mkakati huo.

  Tunatarajia kumkabidhi mheshimiwa Rais Kikwete mpango huu wenye lengo la kuleta mafanikio makubwa ya michezo nchini ambapo watoto wenye vipaji watapata nafasi ya kusoma na kukuzwa katika utaratibu wa michezo na tunaamini kuwa baada ya miaka mitano hadi kumi tutaweza kuanza kupata mafanikio.

  Kituo hiki ndicho kituo pekee katika ukanda wan chi za Afrika mashariki na kati ambapo jumla ya wanamichezo 2300 wataweza kuwa katika mpango wa awali.

  Tunatarajia kupata nguvu toka katika wahisani mbalimbali wa ndani nanje ya nchi kwa kuwa wapo wanaohitaji kuona Tanzania ikipata mafanikio kupitia michezo.

  Wakati huo huo Zaidi ya wakimbiaji 2700 wameshachukua form kwaajili ya kushiriki mbio za mwaka huu huku malengo makuu yakiwa ni kuhitaji kushirikisha Zaidi ya wakimbiaji elfu kumi na tano.

  Vituo vitakavyokuwa vikiuza fomu za ushiriki ni 1.Triple seven Mikocheni.2.maduka ya TSN,Uchumi supermarkets,Uwanja wa Leaderds Club,Ofisi za Rt Taifa,Standi kuu ya mabasi moshi mjini,Arusha na katika tovuti ya WWW.UHURUMARATHON.COM au kwa kupiga simu 0688108384.
  Mratibu wa Uhurumarathon Innocent Melleck kulia akizungumza na waandishi habari jijini Dar Es Salaam juu ya Mbio za uhuru kuanzisha mpango wa kuzindua kituo cha michezo eneo la Msoga linalijulikana kwa jina la Jakaya Kikwete Uhuru Sport Accademy ambapo kituo hicho kitagarimu jumla ya shilingi 4.8Bil ambapo kitashirikisha jumla ya michezo kumi na moja na madarasa kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita,Kulia ni Katibu mkuu wa chama cha riadha Tanzania Selemani Nyambui.
  Katibu mkuu wa chama cha riadha Tanzania Selemani Nyambui akizungumza na waandishi habari jijini Dar Es Salaam juu ya Mbio za uhuru kuanzisha mpango wa kuzindua kituo cha michezo eneo la Msoga linalijulikana kwa jina la Jakaya Kikwete Uhuru Sport Accademy ambapo kituo hicho kitagarimu jumla ya shilingi 4.8Bil ambapo kitashirikisha jumla ya michezo kumi na moja na madarasa kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita.

  0 0

  DSC_0684
  Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando akifungua kongamano hilo la kisayansi.

  Na Andrew Chale, Bagamoyo
  SERIKALI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepongeza juhudi za makusudi zinazofanywa na Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) katika kushughulikia masuala ya afya kwa jamii huku ikiahidi kushirkiana kwa ukaribu.

  Hayo yalisemwa jana mjini hapa na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk.Donan Mmbando wakati wa ufunguzi wa kongamano la 31 la Kisayansi na Mkutano mkuu wa mwaka wa TPHA unaoendelea katika ukumbi wa Stella Maris, Bagamoyo.

  Dk.Margaret Mmbando alisema kuwa juhudi za dhati zinazofanywa na wadau wa afya serikali inazitambua na watahakikisha wanaendelea kuungana nao kwa hali na mali ilikuisaidia jamaii kwenye mambo yote ya msingi hususani masuala ya afya.

  "Tunaipongeza TPHA kwa juhudi hizi za dhati kabisa katka ukuaji na ustawi wa sekta ya afya. Hivyo pia naamini baada ya kongamano hili kwa muda wa siku tano kila atakayetoka hapa atajifunza mambo makubwa na ya msingi katika mustakaba wa sekta hii" alisema Dk.Margaret Mhando.
  DSC_0697
  Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga (kulia) akimkaribisha, Dk. Margaret Mhando kwenye ufunguzi huo.


older | 1 | .... | 651 | 652 | (Page 653) | 654 | 655 | .... | 3285 | newer