Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 647 | 648 | (Page 649) | 650 | 651 | .... | 3286 | newer

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa akifafanua jambo wakati alipokuwa akifungua Semina ya siku moja ya kutafuta namna ya kukabiliana na Rashwa mbalimbali ikiwemo ya Ngono kati ya viongozi na watendaji wa chini iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).
  Mwenyekiti wa Chama cha Majaji wanawake Tanzania Jaji Engera Kileo akizungumza katika semina hiyo.
  Shekh Husen Kuzungu akifafanua jambo wakati akichangia mada kwenye semina ya kutafuta namna ya kutokomeza Rushwa ya Ngono iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania  (TAWJA) iliyofanyika Dodoma.
  Mahakaimu, Wabunge, na wakuu wa vyombo vya Dora wakifuatilia jambo wakati mkuu wa mkoa wa Dodoma Chiku Galawa akifungua Semina kuhusu namna ya kukabiliana na tatizo la Rushwa ya Ngono linaloendelea kushamili kati ya wenye vyeo na wasio na vyeo, iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA)
  Wajumbe waliohudhuria warsha ya kutafuta namna ya kukomesha Rushwa ya ngono maofisini kati ya mabosi watendaji wa chini ikiwemo vyuoni na mashuleni iliyoandaliwa na chama cha majaji wanawake Tanzania (TAWJA) iliyofanyika Dodoma
  Majaji, mahakimu, viongozi wa Dini na viongozi wa vyombo vya Dora waliohudhuria semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu mpya wa mokoa wa Dodoma Chiku Galawa.

  0 0

  Habari wadau, naomba kuwajulisha kuwa mwili wa mwandishi wa zamani wa michezo, Innocent Munyuku aliyefariki dunia juzi, unaagwa leo Ijumaa kuanzia saa tano asubuhi hospitali ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Morogoro kwa mazishi.
  Pia mwili wa mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Baraka Karashani, aliyefariki juzi utazikwa kesho Jumamosi makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam badala ya leo makaburi Sinza kama ilivyokuwa imetangazwa jana. Msiba upo nyumbani kwa wazazi wa marehemu maeneo ya Mawasiliano Tower, barabara ya Sam Nujoma, Ubungo Dar es Salaam.
  Nawasilisha,
  Katibu Mkuu TASWA
  21/11/2014

  0 0


  0 0
  Nyumba ya Maarifa (NIP) mkabala ATCL House, Ghorofa ya Kwanza, Mtaa wa Ohio,
  S.L.P. 79868, Dar es Salaam. Simu: +255 22 2127464, Nukushi: +255 22 2126399
   Barua pepe: info@tapsea.org, Tovuti: http://www.tapsea.org
   
  VIONGOZI WAPYA WA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA WATAMBULISHA OFISI MPYA ZA CHAMA

  MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA – TAPSEA ANAWAJULISHA MAKATIBU MAHSUSI WOTE TANZANIA KUWA OFISI YA TAPSEA IMEHAMIA KATIKA JENGO LA NYUMBA YA MAARIFA (NIP) MTAA WA OHIO.  WANACHAMA WOTE MNAOMBWA KUKAMILISHA UANACHAMA IKIWA NI PAMOJA NA KULIPIA ADA YA MWAKA KUPITIA AKAUNTI NAMBA 0150031411800 CRDB AZIKIWE BRANCH, AU AKAUNTI NAMBA 2236600363 NMB HOUSE.  

  NA WALE AMBAO HAMJAJIUNGA NA CHAMA MNAOMBWA MJIUNGE, FORM ZINAPATIKANA KWENYE MTANDAO WA TAPSEA, KATIKA OFISI ZA CHAMA NA KWA WAWAKILISHI WA MIKOA.

  OFISI ZIKO WAZI KUANZIA SAA 1:30 ASUBUHI MPAKA SAA 11:00 JIONI. 
  WOTE MNAKARIBISHWA KUPATA HUDUMA ZA CHAMA.


  IMETOLEWA NA

  ZUHURA S. MAGANGA
  MWENYEKITI – TAPSEA


  0 0  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Bw. Abdul Samji, akisaidiana kukata utepe na Meya wa Jiji la Mtwara, Mhe. Seleman Mtalika, wakati wakizindua tawi jipya la benki hio jijini Mtwara. DTB kwa sasa ina matawi 21 nchi nzima, na inapanga kufungua matawi mengine manne (4) kwaka 2015, kuongeza nguvu kwa mtandao wake kwa miji ya Mwanza na Dar es Salaam.

  ========  =======  =======

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Diamond Trust Bank Tanzania Limited (DTBT), Abdul Samji, amezindua tawi la Benki hiyo katika Manispaa ya Mtwara, lililopo katika Barabara ya Tanu, na hivyo kufanya Benki hiyo kuwa na matawi 21 nchini Tanzania.

  Wakati Mwenyekiti Abdul Samji akizindua tawi la kwanza la DTB kwa Mikoa ya Kusini, alionyesha furaha yake kwamba kwa kipindi cha miaka 7 Diamond Trust Bank imefungua matawi mapya yapatayo 17 – wastani wa matawi 2 hadi 3 kwa mwaka. “Benki yetu ilianza na matawi 4 mwaka 2007 na leo ina matawi 21, huku tukiwa na mpango wa kufungua matawi mengine mawili ndani ya miezi mitatu ijayo,” alisema Samji huku akionesha uso wa furaha.

  Akizungumza na wanahabari wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa tawi hilo, Samji amesema Benki yake imejizatiti na mpango wake wa kuendelea kufungua matawi nchini. “Kufunguliwa kwa Tawi la DTB katika Manispaa ya Mtwara ni utekelezaji wa hamu na shauku iliyo nayo benki yatu kuwa sehemu ya ukuzaji uchumi kwa mikoa ya kusini. DTB imekuwa ikitoa misaada ya kibenki kusaidia miradi kadhaa ya maendeleo na ya kimiundombinu ili kuwezesha kampuni zinazoendesha shughuli zao mkoani Mtwara. Tunaamini kuwapo kwa DTB Bank kwenye mkoa huu kutawarahisishia mambo mengi wateja wengi wapya watakaoanza kufanya nasi shughuli za kibenki.”


  Sasa DTB inakuwa benki ya nane (8) ya kibiashara kufungua tawi katika Manispaa ya Mtwara huku ikitoa huduma kikamilifu za kibenki kwa wananchi wa Mtwara, na wakati huo huo ikiwa na mikakati ya kuelekeza nguvu zake kwa wafanyabiashara ndogondogo na wajasiriamali. Samji amesema kwamba DTB imejizatiti katika kuunga mkono biashara ndogondogo ili kuziwezesha kupata haraka mikopo itakayowafaa.


  Akizungumzia mpango wao wa kuungana na Taasisi ya Aga Khan (Aga Khan Foundation-AKF) kuboresha mipango ya uchumi na fedha, kilimo, uboreshaji wa maisha ya wananchi, elimu na afya Kusini mwa Tanzania (kwenye Mikoa ya Mtwara na Lindi), Samji anasema: “Tumekuja Mtwara tukiwa na uhakika wa kazi nzuri iliyofanywa na Taasisi ya Aga Khan (AFK) miongoni mwa familia za wakulima wadogo wadogo katika Mikoa ya Kusini tukiwa tumejizatiti kuunga mkono juhudi zao hizo za pamoja. Tunatarajia kwamba kufunguliwa kwa Tawi la DTB la Mtwara, kutakuwa kama changamoto kwa programu ya maendeleo ya Taasisi ya Aga Khan ambayo imedhamiria kuboresha maisha ya wananchi wengi waishio vijijini katika eneo hili.”

  DTB inachukuliwa kuwa ni Benki inayokua kwa kasi kubwa sana nchini Tanzania; ikiwa na utendaji wa kiwango cha hali ya juu sana katika tasnia ya viwango vya kibenki. DTBT imeripotiwa kuwa na kiwango cha juu sana cha utendaji hadi kufikia mwishoni mwa Septemba 30, 2014 ikiwa nyota katika ukuaji wa Faida Kabla ya Kukatwa Kodi (Profit Before Tax-PBT) ya 37.5% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2013. Faida kabla ya kodi ilifikia kiwango cha TZS 15.4 bilioni hadi robo ya tatu mwaka 2014 ikiwa na maongezeko ya kuvutia kutoka ukopeshaji na shughuli za fungani (treasury activities).

  Mali za Benki zimeongezeka kwa TZS 128 bilioni kutoka TZS 505 bilioni mwezi Desemba 2013 hadi kufikia TZS 633 bilioni mwishoni mwa Septemba 2014, wakati mikopo kwa wateja (Net Advances to Customers) imeongezeka kwa TZS 62 bilioni.

  DTB kwa sasa ina matawi 21 nchi nzima, matawi 8 yakiwa katika jiji la Dar es Salaam; mawili (2) jijini Arusha na tawi moja moja katika miji ya Zanzibar, Tanga, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Moshi, Morogoro, Iringa, Tabora, Kahama na ongezeko la tawi jipya la Mtwara. Benki inapanga kufungua matawi mengine manne (4) mwaka 2015, kuongeza nguvu kwa mtandao wake kwa miji ya Mwanza na Dar es Salaam huku kukiwa na uwezekano wa kupata matawi mapya kwa miji ya Singida na Kigoma katika mwambao wa Ziwa Tanganyika. Benki inaangalia kwa karibu uwezekano wa kupanua mtandao wake  maeneo ya Kusini mwa Tanzania katika miji ya Masasi, Lindi na Songea.


  DTB Tanzania ni kampuni tanzu ya makampuni ya DTB (DTB Group) kiuhusiano na East African Bank, na kufanya shughuli za kibenki kibiashara na Kenya, Uganda na Burundi ikiwa na mtandao wa matawi 107 kwenye ukanda huu.


  DTB ni kampuni tanzu ya Mfuko wa Aga Khan wa Maendeleo ya Kiuchumi (the Aga Khan Fund for Economic Development-AKFED), ambayo ni tawi la Mtandao wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Aga Khan (Aga Khan Development Network-AKDN).  0 0


  0 0

  Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
   Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
   Matinyi akisoma wasifu wa marehemu.
    Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando akitoa salama za rambirambi.
   Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda akitoa salam za rambirambi.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


   Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea ofisini kwake wakati akikabidhi Vifaa mbalimbali kwa wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini Ikiwa ni Utekelezaji wa Ahadi zake alizotoa Kipindi Akiomba kura ya Kuwa Mbunge wa Jimbo Hilo Pamoja za Ahadi anazotoa kwenye Mfululizo wa Ziara zake anazofanya Mara kwa mara katika Kata Mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mjini.
   Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood akikabidhi Mboa kwa Viongozi wa Msikiti kwajili ya Kumalizia ujenzi wa Msikiti ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa ziara zake za mara kwa mara. 
    Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akikabidhi Tani 2O za Saruji kwa viongozi wa Kanisa la agae la Mjini Morogoro Kwajili ya kufanikisha Ujenzi wa Kanisa Hilo.
   Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akimkabidhi Tank la Maji Diwani wa kata ya Bigwa kwa niaba ya wakati wa kata hiyo Ili kutatua kereo ya Maji katiaka kata hiyo 
    Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akikabidhi Hundi ya Shilingi Laki Tano kwa kikundi cha wa mam wajasiriali Kutoka kata ya Kihonda  Magorofani
   Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikabidhi Hundi   
  Katika Shuguli yake ya kukabidhi Vifaa mbalimbali Mh Abood alikabidhi vifaa vyenye Jumla ya Shilingi Milioni 1756OOOO/= Katika vikundi Mbalimbali vya Wajasiriamali,Vya Kidini kutoka kata za Jimbo la Morogoro Mjini.Baadhi ya Vifaa alivyokabidhi Mh Abood ni amoja na Matofali ,Vifyuko ya cement,Mabati Mbao na Hundi.
  Akielezea zaidi Mh Abood alisema Maka sasa ameweza Kuchimba Visima  24 Kati ya 36 Vitakavyogharimu Kiasi cha Shilingi Milioni 365. Karibu  kata  Zote za Manisaa ya Morogoro Kwasasa Zina Kisima Kwajili ya kutatua changamaoto Kubwa ya maji inayowakumba wakazi wa Jimbo la Morogoro  Mjini.

  Akielezea zaidi Mh Abood Alisema Anapambana usiku na Mchana 
  kutatua Kero Zote zinazowakumba wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini..
  Akielezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na Ahadi zake alizotoa kwa wananchi wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Abood Amesema karibu ahadi zake zote alizoahidi Amezitekeleza ,Amewaomba wakati wa manisaa ya Morogoro Kushikiana nae Bega kwa Bega katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mainduzi.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Mkutano wa pili wa Kimataifa kuhusu Lishe na Virutubisho (ICN2) uliofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Rome, Italia juzi Novemba 19, 2014.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakati wa mkutano huo wa ICN2 (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, James Nsekela na Msaidizi wa Rais katika Masuala ya Lishe Dkt. Wilbald Lorri.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango Maalum wa Chakula Duniani (WFP) Ethria Cousin (kushoto) na Balozi Wilfred Ngirwa wakati wa mkutano huo wa ICN2, uliofanyika juzi Novemba 19, 2014, Jijini Rome Italy.
   Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi walioshiriki katika Mkutano huo wa ICN2. Kulia ni Mfalme Letsie III wa Lesotho.
  Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa FAO Jose Graziano da Silva, wakati alipomtembea ofisini kwake na kufanya naye mazungmzo, juzi Novemba 19, 2014. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid. Picha na OMR.

  0 0  Dar es Salaam. Mbunifu wa mitindo na muigizaji wa filamu nchini, mrembo Jokate Mwegelo kwa kushirikiana na mshiriki maarufu wa Big Brother Africa, Mganda Gaetano Kagwa wameteuliwa kuendesha kipindi kipya cha Maisha kijulikanacho kwa jina la “Beat the Challenge” kupitia M-Net East Africa.

  Kipindi kitashindanisha familia mbalimbali katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda na mshindi atapewa gari jipya kabisa kutoka kwa waandaaji.  
  Katika mashindano hayo, kila  familia inatakiwa kuwa na watu wanne ambao ni Baba, Mama na watoto wawili wenye umri kati ya miaka 12 na 17.Familia hizo zitashinda katika kutatua changamoto mbalimbali zitakazowasilishwa na waandaaji na kila familia itakuwa na jukumu la kutatua hiz changamoto kwaa kutumia nguvu kuliko ufahamu wa akili.

  Akizungumza jana, Jokate alisema kuwa amejisikia faraja kubwa kupewa nafasi hiyo ambayo itampa uzoefu zaidi katika fani ya utangazaji na kujipanua kimawazo.Jokate ambaye pia ni Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006 alisema kuwa anajisikia faraja kubwa kwa kuzidi kuongeza wigo wa mawasiliano kwani hii si mara yake ya kwanza kuendesha vipindi katika televisheni baada ya kutamba katika kipindi cha Chaneli O.


  “Kama nilivyosema, nataka kuishi kwa kutegemea vipaji vyangu na wala si vinginevyo, nimeanza katika urembo, nikaja katika ubinifu na uanaminitindo, MC, muigizaji wa filamu na sasa mtangazaji, kote huko nimefanikiwa, ni faraja kubwa kwangu,” alisema Jokate.

  Alisema kuwa anashukuru kuona kuwa filamu yake ya Mikono Salama kwa sasa inatamba sana na inamuongezea sifa kubwa katika fani hiyo. “Hata kidoti Fashion nayo inatamba, hivyo kwa nashukuru Mungu kwa kuniwezesha,” alisema.

  Kwa upande wa Tanzania, utafutaji wa washiriki utafanyika Jumamosi Novemba 22), New Africa Hotel, wakati Uganda watafanyia kwenye hotel ya Silver Springs, Kampala na Kenya kwenye studio za Supersport zilizopo katika Barabara ya Jamhuri.Kipindi cha kwanza kitarushwa Desemba 13 kupitia chaneli ya Maisha Magic 161 kuanzia saa 2.30 usiku kwa mujibu wa Jokate.


  0 0
 • 11/21/14--05:14: Article 12


 • 0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani ya nchi Mbaraka Abdualwakili, akizindua chapisho la tathmini ya Polisi Jamii nchini, hafla hiyo ilifanyika jana Makao Makuu ya Polisi  Jijini Dar es Salaam. Picha Alexander Mpeka – Jeshi la Polisi
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Bw.  Mbaraka Abdualwakil, Mwakilirishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia  ambaye ni Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu, Bi Selina Lyimo wakiwa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Abdulrahaman Kaniki pamoja  timu iliyoshiriki katika utafiti wa tathmini ya Polisi jamii. Picha na Alexander Mpeka – Jeshi la Polisi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Bw.  Mbaraka Abdualwakil, Mwakilirishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia  ambaye ni Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu, Bi Selina Lyimo wakiwa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Abdulrahaman Kaniki pamoja  makamishina wa Jeshi la Polisi wakati wa hafla ya makabidhiano ya chapisho la utafiti wa tathmini ya Polisi jamii . Picha na Alexander Mpeka – Jeshi la Polisi.

  =======  =======  =======


  Na. Tamimu Adam - Jeshi la Polisi.

  Jeshi la Polisi nchini  limetakiwa kutumia matokeo ya utafiti  wa tathmini ya Polisi Jamii  uliofadhiliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya taifa ya Sayansi na teknolojia( COSTECH) katika kuboresha mkakati wa Polisi jamii ili kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kwani matokeo hayo yana manufaa makubwa katika kubaini, kuzuia, na kutanzua uhalifu na kero mbalimbali katika jamii.

  Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bi. Selina Lymo  kwa niaba ya  Katibu  Mkuu wa  Wizara ya Mawasiliano, Sayansi  na teknolojia wakati wa hafla ya kukabidhi chapisho la  utafiti  wa matokeo ya tathmini ya Polisi jamii  nchini kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Bw. Mbaraka Abdulwakili . 

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Bw. Mbaraka  Abdulwakili alisema atahakikisha utafiti huo unafanyiwa kazi ipasavyo na amewataka watendaji wa Jeshi la Polisi kutumia utafiti huo katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kuwa askari waliopo hawatoshi na Polisi jamii imeonyesha  mafanikio makubwa katika kuzuia vitendo vya uhalifu na wahalifu.

  Naye, Mtaalum Mwelekezi wa Utafiti wa Tathmini ya Polisi Jamii ambaye pia ndiye Mtafiti Mkuu   Dkt  Haji Semboja alisema kuwa utafiti huo ulifanyika katika kanda saba ambapo matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa uhusiano wa kiutendaji baina ya wananchi na Jeshi la Polisi umeboreshwa kwa kiwango kikubwa kupitia dhana ya Polisi jamii.

  Alisema kuwa jambo hilo linasaidia katika kutengeneza mazingira ya amani na hivyo shughuli nyingine za kiuchumi  na kijamii zinaweza kuendelea kufanyika bila hofu na kwa uhakika wa ulinzi na usalama.

  Aliongeza kuwa, utafiti huo umeonyesha kwamba, watu wengi wanaamini kuwa, matokeo ya kuanzishwa kwa Polisi jamii katika maeneo yao  kuna mafanikio makubwa katika kuhimiza na kutia moyo uvumbuzi wa njia mpya za kukabiliana na vitendo vya uhalifu ambapo wananchi wamekuwa wakihimizwa utoaji wa taarifa za uhalifu kupitia njia mbalimbali ikiwemo njia ya ujumbe mfupi. 

   Naye, Naibu Inspekta Jenerali  wa Polisi, Abdulrahman Kaniki aliipongeza timu nzima iliyofanya utafiti huo na kusema kuwa Jeshi la Polisi kama watekelezaji wakuu wa Programu ya maboresho  yaliyojikita katika mihimili mikuu mitatu ambayo ni Weledi, Usasa na Polisi jamii,  wanatambua na kuthamini kazi nzuri iliyofanywa na watafiti hao na amewaomba kuangalia namna wanavyoweza kufanya utafiti katika mihimili  mingine miwili iliyobaki ambayo ni Usasa na Weledi ili Jeshi  Polisi  liweze kuwa na tathimini halisi ya Maboresho yake.

  Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dr. Flora Tibazarwa alisema kuwa madhumuni ya mpango wa utafiti huo yalikuwa ni kuimarisha uhusiano baina ya  Jeshi la Polisi na wananchi katika kuzuia na kutatua matatizo ya jamii, msisitizo ukiwa kuzuia uhalifu kabla haujatokea.

  Aliongeza kuwa matokeo ya utafiti huo yatawasaidia watunga sera na watoa maamuzi kutoa maamuzi na kutunga sera mbalimbali za usalama wa raia na mali zao kwa faida ya taifa letu.   

  0 0

  Mkurugenzi  wa makampuni ya  Asas  Bw  Salim Abri  Asas  kushoto akipokea cheti  maalum kutoka kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Letici Warioba  baada ya  kuibuka  mshindi wa kwanza katika  ulipaji kodi mkoa wa Iringa leo.
  Meneja  wa TRA mkoa wa Iringa Rosalia Mwenda akimpongeza  Bw  Asas  kwa ushindi katika ulipaji kodi
  Cheti  kilichotolewa kwa  kampuni ya Asas
  Salim Asas  akionyesha  cheti kwa wanahabari  baada ya  kukabidhiwa  cheti  hicho kwa kuwa mlipaji  kodi mzuri.
  KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi,Waziri Kiongozi (Mstaafu),Mh. Shamsi Vuai Nahodha akitoa hotuba yake katika kilele cha Maadhimisho hayo yaliyofanyika leo Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Othman Michuzi.
  Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Adam Malima akitoa nasaha zake kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi yenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti",yaliyofanyika leo Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Bernard Mchomvu akitoa hotuba yake kwenye kilele cha Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi yenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti",yaliyofanyika leo Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade akitoa hotuba yake kwenye kilele cha Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi yenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti",yaliyofanyika leo Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Wageni waalikwa kutoka nchi mbali mbali wakifatikia kwa makini hotuba ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade (hayupo pichani) aliyokuwa akiitoa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi yenye kauli mbiu isemayo "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti",yaliyofanyika leo Novemba 21,2014 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
  Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya nane ya Siku ya Mlipa Kodi,Waziri Kiongozi (Mstaafu),Mh. Shamsi Vuai Nahodha (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Washiri watatu wanaolipa kodi vizuri.Washindi hao ni TBL (kulia),Vodacom (pili kushoto) na TCC (kushoto).


  0 0

   Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt. Fatma Mrisho akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani isemayo, Tanzania Bila Maambukizi Mapya ya VVU, Vifo vitokanavyo na Ukimwi na Ubaguzi na Unyanyapaa inawezekana inayolenga kupunguza maambukizi Mapya ya Ukimwi, kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi na kukomesha vitendo vya unyanyapaa kwa asilimia Sifuri.
   Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani yatakayofanyika kitaifa mkoani Njombe kuanzia Novemba 24, 2014 na kufikia kilele chake Desemba 1, 2014.
   Mkurugenzi wa ufuatiliaji wa Tathmini wa Ofisi ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi  Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu utoaji wa huduma na upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi kwa watu wanaoishi na VVU katika maeneo mbalimbali nchini.

   Mkurugenzi wa ufuatiliaji wa Tathmini wa Ofisi ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi  Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu utoaji wa huduma na upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi kwa watu wanaoishi na VVU katika maeneo mbalimbali nchini.
  Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa TACAIDS akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mbinu na elimu inayotolewa na TACAIDS katika maeneo mbalimbali ikiwemo matumizi ya mipira ya kike kwa wanawake ili kuzuia maambukizi mapya ya VVU.


  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Lazaro Nyalandu akizungumza na Waandishi wa Habari (hawako pichani) katika Ukumbi wa Habari wa Bunge Mjini Dodoma leo Novemba 21,2014, kuhusu Uvumi ulioanza kuenea kuwa jamii ya wamasai wanaoishi katika hifadhi ya Hifadhi ya Ngorongoro kuwa watahamishwa.

  0 0

  Balozi wa Tanzaniania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyabiashara kutoka Ubeligiji baada ya kutembelea bandari ya nchi kavu ya PMM- Dar es salaam.

  0 0

  BENDI Kongwe ya muziki wa dansi, Sikinde pamoja na Malkia wa muziki wa Taarab Afrika Mashariki, Khadija Kopa ni miongoni mwa wanamuziki watakatoa burudani kwenye Tamasha la Sanaa na Ubunifu wa Mswahili (Swahili Arts and Creative Carnival).

  Akizungumza na mtandao wa jamii,  mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, Ahadi Kakore amesema kuwa Sikinde ni miongoni mwa bendi zinazopiga muziki wa Kiswahili asilia ndiyo maana wameamua kuiweka kuwa bendi rasmi ya dansi ya tamasha hilo.

  Aliongeza kuwa kwa upande wa Khadija Kopa naye atakuwa na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic ambayo siku hiyo imeahidi kuimba nyimbo zake mpya ambazo nyingi zitaimbwa kwa mara ya kwanza siku hiyo.

  “Mbali ya kuwepo kwa burudani hizo za muziki lakini haina maana kuwa ndiyo tumefunga mlango kwamba hatutakuwa na wasanii wengine ila bado tupo kwenye mazungumzo na wanamuziki nyota wa kizazi kipya kwani tumelenga kuwafikia watu wa rika zote.
  “Pamoja na burudani za watu wazima pia watoto nao hawajaachwa nyuma kwa sababu kutakuwa na michezo maalum kwa watoto na zawadi nyingi zipo kwa ajili yao ili kuhakikisha wanafurahia siku hiyo.

  Mbali na muziki, burudani nyingine zitakazokuwepo siku hiyo ni maonyesho ya filamu za Kiswahili, maonyesho ya mavazi, vyakula, nyama choma, vinywaji pamoja na michezo ya watoto na maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali na watu 1,000 wa kwanza watapata zawadi langoni,” alisema Kakore.

  Swahili Arts and Creative Carnival linatarajiwa litafanyika Novemba 29 mwaka huu kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku likiwalenga watu wazima na watoto kuanzia saa 4:00 asubihi hadi usiku wa manane.

  Tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Swahili Arts & Creative Carnival kwa kushirikiana na Hildelly Solution na Wazalendo Bright Media kwa udhamini wa Amo Transport Solutions, Coca Cola, Tigo, Oriflem, Chibuku, Global Publishers, CTN na Sibuka TV. 

  0 0

   Waziri kiongozi mstaafu Shamsi Vuai Nahodha(kulia) akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza, kombe la mshindi wa pili kwa walipa  kodi wakubwa nchini wakati wa maadhimisho ya nane ya siku ya mlipa kodi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.Vodacom imeongoza katika kundi la sekta ya mawasiliano nchini.
   Waziri kiongozi mstaafu Shamsi Vuai Nahodha(wapili kutoka kulia)akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu bora wakubwa walipa kodi kutoka kushoto ni Meneja wa maswala ya kodi wa kampuni ya sigara Tanzania(TCC) Godfrey Ferdinand,wapili ni Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza,kulia Meneja huduma wa kampuni ya Tanzania Breweries Alois Qande,wakati wa maadhimisho ya nane ya siku ya mlipa kodi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
   Waziri kiongozi mstaafu Shamsi Vuai Nahodha(wanne kutoka kushoto waliokaa)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi walipa kodi ambapo Vodacom Tanzania imeongoza katika kundi la sekta ya mawasiliano nchini.
   .Wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya nane ya siku ya mlipa kodi nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam,ambapo Vodacom Tanzania imeongoza katika kundi la sekta ya mawasiliano nchini.

older | 1 | .... | 647 | 648 | (Page 649) | 650 | 651 | .... | 3286 | newer