Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 648 | 649 | (Page 650) | 651 | 652 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Watoto wenye umri chini ya miaka 12 wa Mkoa wa Dar es Salaam wanakusanyika kesho Jumamosi (Novemba 22 mwaka huu) asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa ajili ya kusaka kombaini ya mkoa.

  Mkusanyiko wa kusaka kombaini hiyo kwa ajili ya timu itakayoshiriki mashindano ya Taifa yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao uko chini ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).

  Wachezaji hao wataanza kujaribiwa saa 1 hadi saa 5 asubuhi. Mashindano ya Taifa yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 28 mwaka huu.  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM,Mh. Balozi Seif Ali Iddi (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya makada wa CCM-China wakati alipokutana nao.
  Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM,Mh. Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Tawi la CCM-China Bw. Olivo Mtunge wakati alipokutana nao kwa mazungumzo ikiwa ni pamoja na kufungua tawi jipya la Chama hicho,nchini humo.
  Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM,Mh. Balozi Seif Ali Iddi  akisabahiana na Mwenyekiti wa Tawi la CCM-China Bw. Boniphace Chija Nobeji.
  Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM,Mh. Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mfanyakazi wa CCM Makao Makuu, Bw. Seluman Serela. 

  0 0  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amesema elimu imekomboa wanawake nchini Tanzania kwa kuwapa uwezo wa kushiriki sawa sawa na wanaume kwenye fursa za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

  Mhe. Membe, ambaye alikuwa akihutubia kwenye mahafali ya 11 ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Jijini Dar es Salaam leo, aliwataka wanawake kutumia kikamilifu fursa za elimu ya juu ili wajitegemee kiuchumi na kuondokana kabisa na unyanyasaji wa kijinsia.

  Alielezea kuridhishwa na uwezo ulioonyeshwa na wahitimu wa kike katika chuo hicho. Kati ya wahitimu 902 waliotunukiwa Shahada na Stashahada na Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, 423 ni wanawake.

  Mhe. Membe aliwataka wahitimu hao watumie elimu yao vizuri katika kuiendeleza jamii na taifa, kufanya kazi kwa bidii na kutii sheria za nchi.
   Brass Band ya Jeshi la Magereza ikiwaongoza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Kampasi ya Dar es Salaam , Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, Maafisa, Wahadhiri,Wahitimu pamoja na Wageni Waalikwa kuingia katika Viwanja vya Chuo Kikuu  hicho katika sherehe za Mahafali ya Kumi na Moja ya chuo hicho yaliyofanyika tarehe 21.11.2014.
    Mhe. Membe (mwenye joho la bluu) akiongozana na baadhi ya Wahadhiri kuingia katika viwanja yalikofanyika mahafali ya kumi na moja ya chuo kikuu cha Kimataifa cha Kampala Kampasi Dar es Salaam huko Gongo la Mboto.
   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mhe. Ally Hassan Mwinyi  (mwenye kofia ya njano) akiwa pamoja na mgeni rasmi  Mhe. Membe (wa pili kutoka kushoto) wakiwa wamesimama kwa heshima ya Wimbo wa Taifa kama ishara ya kuanza kwa mahafali hayo ya kumi na moja.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0  0 0  0 0


  0 0

  Na hiki ni kipindi kilicho enda hewani Mwezi wa 12 mwaka jana katika televisheni ya Taifa nchini Japani ya NHK. Kipindi hiki kilihusu safari ya Bi Radhia Kipozi-Suzuki alipo tembelea kijiji cha Umaji kilichopo Kouchi Japani. Hapa naongelea kuhusu utamaduni mbalimbali wa Tanzania.

  0 0


  0 0


  Chaka Khan - Ain't Nobody

  0 0

  Na Profesa Joseph Mbele
  Nimewahi kuandika kuwa kama mwandishi, najikuta nikialikwa kuongelea maandishi yangu, na pengine kuongelea kitabu maalum. Hayo niliandika katika blogu yangu.
  Wakati mwingine, mwandishi unaalikwa kwenye mahojiano katika vyombo vya habari. Nami nimewahi kuhojiwa katika redio, blogu, na magazeti.
  Hapa naleta mahojiano niliyofanyiwa mwaka 2006 na m-Tanzania Deus Gunza, ambaye alikuwa anamiliki na kuendesha Radio Butiama, kule Columbus, Ohio. Mahojiano hayo ya papo kwa papo yalihusu kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences

  Yasikilize mahojiano haya hapo:

  http://butiama.podomatic.com/entry/2006-09-02T06_26_37-07_00

  0 0

  At least 14 people have been injured in a suspected gas explosion at a central London hotel, ambulance officials say.
  The Hyatt Regency London - The Churchill, in Portman Square, Marylebone, was evacuated following the blast shortly before midnight.
  London Ambulance Service said five of the injured were taken to hospital, including two with leg wounds.
  Fire officers and gas engineers are ensuring the scene is safe so guests can be allowed back into the hotel.
  Another nine people who sustained injuries were treated at the scene.
  London Fire Brigade said the explosion happened at about 23:40 GMT in the basement of the five-star hotel, causing part of the building to collapse.

  0 0


  0 0
 • 11/22/14--02:08: IN LOVING MEMORY
 • THE LATE SABINUS PETER KWEKA

  Father, we cannot believe that ten years has  passed already, since you left us suddenly on 22ND November 2004.  There are no words to express the pain and emptiness you have left in our hearts. Our lives have changed and we will never be the same again, without you in our lives.

  We pray for you every day and we know you are in better place and continue to praise our LORD JESUS CHRIST just like you taught us when you were with us.We thank GOD for the time he gave us to be with you those days. GOD be with you, till we meet again.

  You are missed by your children JANE, FESTO,EUGENIA,ELIZABETH, CECILIA  and THADEI, your in – Laws – OTTO, IBRAHIM,JOHN,VALENTINA  and COSTANCIA; your only sister remained – SR.DEVOTHA KWEKA CDNK,
  Grand children and all relatives, ESPECIALLY KWEKAS from NARUMU, neighbours and Family friends.

  MAY OUR LORD REST YOUR SOUL  IN ETERNAL PEACE,
  AMEN

  NB: THERE WILL BE A HOLY MASS FOR REMEBERANCE AT HIS HOME – NARUMU.
  YOU ARE ALL WELLCOME.


  0 0

  Kanisa  la  HHC Catherdral  lilopo  Ilemela  Mwanza  linakukaribisha  kwenye  kongamano  baraka  la  kujengwa  kiuchumi  tarehe  3-12-2014  na  4-12-2024  .Wahubiri ni  Bishop  Joseph  Njoroge  toka  Nairobi  Kenya  na  Bishop  Eugene  Murisa  wa  HHC  Mwanza.
  Mahali:  Gold Crest  Hotel kuanzia
  Saa  9.00  Alasiri hadi  12.30  jioni.
  Hakuna  Kiingilio wote mnakaribishwa.

  0 0

  Mkuu wa kwanza wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) Askofu Dkt. Saimon Chiwanga akitoa neno baada ya Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene kumaliza shudhuli ya kutunuku vyeti kwa wahitimu wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimtukuku Shahada ya Uzamili katika Uchumi wa Maendeleo Amina Salum Mwanja wakati wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
  Baadhi ya wahitimu wa mahafali ya 28 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) iliyofanyika jana mjini Dodoma.
  Mwanafunzi wa mwaka wa pili anayesomea Shahada ya kwanza ya Mipango ya Usimamizi wa Mazingira katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vjijini (IRDP) Azizi Mshau akimweleza Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene namna bora ya kundaa mipango miji inayokuwa rafiki kwa mazingira.


  0 0
 • 11/22/14--06:56: TAARIFA YA MSIBA
 • Uongozi wa Azania Bank Ltd unasikitika kutangaza kifo cha Mfanyakazi mwenzao,Ndg. George Godwin Njabili kilichotokea jana Novemba 21,2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

  Mipango ya Mazishi inafanya nyumbani kwa Marehemu,Tabata Bima jijini Dar es Salaam.

  Taarifa hii iwafikie Ndugu,Jamaa na Marafiki wote wanaomfahamu Marehemu Njabili,na tunamuombea kwa Mungu aiweke roho yake mahala pema Peponi,Amin.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Taasisi ya ESAMI iliyopo Njiro Hill Mkoani Arusha alipowasili kwenye Taasisi hiyo leo Novemba 22,2014 kuhudhuria Mahafali ya nane ya Taasisi hiyo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal wa pili kulia na Viongozi wa Taasisi ya ESAMI iliyopo Njiro Hill Mkoani Arusha akiongoza maandamano ya mahafali ya nane ya Taasisi hiyo yaliyofanyika leo Novemba 22,2014 Njiro Hill Mkoani Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti Witness Steven mhitimu wa Shahada ya MBA katika Taasisi ya ESAMI Kampas ya Dar es salaam kwenye mahafali ya nane ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Novemba 22,2014 Njiro Hill Mkoani Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti Leah Mumbua mhitimu wa Shahada ya MBA katika Taasisi ya ESAMI Kampas ya Nairobi kwenye mahafali ya nane ya Taasisi hiyo iliyofanyika leo Novemba 22,2014 Njiro Hill Mkoani Arusha.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akisalimiana na Viongozi wakiwemo wawekezaji Kampuni na wadau wa maendeleo wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar”uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Tamasha la Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akipata maelezo kutoka kwa Taki Dewji wa banda la Shell wakati alipotembelea mabanda mbali mbali mara baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamd Shein akipata maelezo kutoka kwa Rose Tesha Meneja Vipindi katika banda la VSO wakati alipotembelea mabanda mbali mbali mara baada ya kuzindua rasmi Maonesho ya Fursa za Ajira na Uzalishaji kwa vijana “Youth Development Carrier Fair in Zanzibar” uzinduzi uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama,Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.


  0 0

  Dk. Kitindi Hemedi Kumpuni

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, anasikitika kutangaza kifo cha Dk. Kitindi Hemedi Kumpuni (Mhadhiri Idara ya Magonjwa ya akina Mama), kilichotokea tarehe 21 Novemba 2014, saa 8:30 mchana, katika Hospitali ya Kairuki, baada ya kuugua kwa muda mfupi. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Oysterbay, barabara ya Bongoyo.  

  Marehemu atazikwa siku ya Jumapili tarehe 23.11.2014, Saa 10 jioni katika makaburi ya Kisutu DSM. 

  Kwa taarifa zaidi piga simu namba 0713278060, au 0754309869.

  MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMINA.

older | 1 | .... | 648 | 649 | (Page 650) | 651 | 652 | .... | 3272 | newer