Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 646 | 647 | (Page 648) | 649 | 650 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Chumba cha Globu ya Jamii Kimepokea picha ya tukio la ajali ya Lori lililokuwa limebeba mapipa ya lami ambalo limeshika moto mapema leo asubuhi maeneo ya Mikumi,Morogoro.chanzo cha mlipuko huo bado hakijafahamika mpaka sasa na bado hatujapata taarifa kama kuna aliepoteza maisha au kupatwa kwa majeruhi.Chini ni ujumbe kutoka kwa mdau wa Globu ya Jamii alietuletea taswira hizi kuhusiana na hali ya barabara hiyo.

  ''Kama una safari ya kwenda Iringa-Mbeya au kama unapokwenda utapita mikumi basi sitisha safari kwani njia inefungwa tangu saa mbili asubuhi. Kuna lory linawaka moto mpaka sasa. Lilikuwa limebeba lami so lami bado inawaka na inesambaa sehemu kubwa''
  Baadhi ya watu wakishudia tukio hilo la ajali.

  0 0

  MKUTANO wa kwanza wa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation uliyofanyika juzi Novemba 19, katika kijiji cha Misima, wilayani Handeni, mkoani Tanga na kuwakutanisha wananchi wote umeibua kero nyingi za wananchi, ikiwamo ya kijiji chao kuingizwa kwenye Halmashauri ya Mji bila ridhaa yao. 
  Mmoja wa wakazi na wananchi wa kijiji cha Misima, akilalamikia eneo lao kuingia kwenye Halmashauri ya Mji kinyume cha sheria ya utawala bora, ikiwa ni pamoja na kutoshirikishwa kwa lolote na viongozi wa juu.
   
  Taasisi hiyo ilianzishwa mapema mwaka huu na kuzinduliwa Mei 8 jijini Dar es Salaam, ilifanya mkutano mkubwa wa hadhara Misima, ambapo umati wa wanchi ulihudhuria, huku kero nyingi zikiwasilishwa na kudhihirisha changamoto za utawala bora zinazoathiri maendeleo ya Tanzania.
   
  Wakizungumza kwa uchungu mkubwa, mwananchi wa Misima aliyejitambulisha kwa jina la Mhina Ally, alisema viongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na madiwani waliamua kuingiza kijiji chao katika Halmashauri ya Mji bila ya kuwashirikisha, ikiwamo kubandika tangazo la pingamizi kwa siku 90 katika maeneo yao kama sheria inavyotaka.
   
  Alisema kutoka Handeni Mjini hadi katika eneo lao ni kilomita 16 zilizozunguukwa na mapori yanayowafanya wananchi wajihusishe na kilimo kwa asilimia 99, hivyo kuingizwa kwenye sheria za mji ni kusababisha ugumu wa maisha.
   
  “Inashangaza mno kusikia Tanzania kuna utawala bora wakati viongozi wachache wanaweza kufanya watakavyo; hali inayoweza kuleta mapigano makubwa, endapo wananchi tutasimama kidete kudai haki zetu zinazokandamizwa na viongozi kila siku,” alisema.
   
  Ally alifika mbali zaidi kwa kusema walisikia tangazo redioni la kuingizwa kwenye Halmashauri ya Mji, huku tangazo la pingamizi likishindwa kuwekwa kijijini kwao kwa hofu ya kupingwa na wananchi wao.
   
  “Viongozi wa serikali ya kijiji waliamua kutoliweka tangazo la pingamizi kijijini kwetu kwasababu wanajua fika tusingekubali, hivyo inashangaza malalamiko yetu kufumbiwa macho na serikali inayoitwa sikivu, licha ya kuzunguuka sehemu nyinyi, kama kwa Mkuu wa wilaya na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa Tanga, alipokaimu DC Halima Dendego, ambaye sasa amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,” aliongeza.
   
  Naye Naye Idd Kisege alisema kuwa ili kuona viongozi wanaogopa kufika Misima, hata namba kwenye nyumba zao hakuna ingawa wanatangaza uchaguzi kwa sheria za mji katika kijiji chao, jambo lisiloweza kuvumiliwa na kila mpenda maendeleo ya Misima.
   
  “Watu wa Misima tunaambiwa sisi ni watata, wakorofi tunapodai haki zetu, ili waendelee kutuburuza, ndio maana kwenye ziara ya Mheshimiwa Rais, Profesa Jakaya Mrisho Kikwete waliniburuza Polisi kwasababu ya kuonyesha bango kwa mheshimiwa ili kuona kero zetu,” alisema Kisege.
   
  Naye Mkomwa Athuman alisema kuwa Misima haipo tayari kutumikia sheria za Mji kwakuwa ni mapema mno kwao, hivyo wanaomba serikali, ikiwamo ofisi ya Waziri kulifuatilia suala hilo kwa kina.
   
  “Mzozo huu umeshakuwa mkubwa na kuondoa ushirikiano kabisa kwa viongozi na wananchi wa hapa Misima, hivyo tayari malalamiko yetu yamefikishwa Ofisi ya Waziri Mkuu kulishtakia suala hilo kwasababu sheria ya kuingia kwenye Mamlaka ya Mji Handeni haijafuatwa na imeanzishwa na watu wachache ili kuzima uozo wa ardhi waliyoufanya kwenye kijiji chetu,” alisema.
   
  Katika kila mwananchi aliyezungumza kwenye mkutano huo alionyesha kuguswa na kero hiyo ya mji, huku wakisema kutoka Handeni Mjini hadi Misima ni mbali pamoja na viongozi kushindwa kufuata sheria za utawala bora.
   
  Awali, mkutano huo ulioanza saa tisa alasiri ulifunguliwa na mtoa mada wa kwanza, Kambi Mbwana, ambaye ndiye Msemaji Mkuu wa taasisi hiyo, aliyejikita sababu na dhamira kuu ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo.
   
  Mbwana alisema kuwa sababu kubwa ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kutoa elimu ya uraia na kuhamasisha utawala bora, ikiwa ni njia moja wapo ya kuwafanya Watanzania wote wajiletee maendeleo kwa kushirikiana baina yao na viongozi wote.
   
  Akizungumzia utawala bora, Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Adam Malinda, alisema kwamba matatizo mengi katika jamii yamekuwa yakichangiwa na viongozi wasiojua nini maana ya utawala bora.
   
  “Utawala bora ni somo muhimu na lazima lipigiwe kelele na watu wote, maana malalamiko mengi ya watu wa Misima yamesababishwa na tatizo hilo, ndio maana unaona kero zimepamba moto,” alisema.
   
  Malinda aliwataka viongozi wa juu, wakiwamo wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kuzungumza na wananchi wa Misima ili kutatua mtafaruku huo kwa ajili ya kuwafanya wananchi waendelee na shughuli za kujiletea maendeleo, sambamba na serikali kuwafanyia kazi watendaji wabovu.
   

  Kuhusiana na mzozo huo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas Mzinga, alikaririwa akisema kuwa utaratibu ulifuatwa, ikiwamo kutoka kwa siku 60 za pingamizi, ingawa wananchi hao walishindwa kupita njia hiyto kwa ajili ya kufanikisha malengo yao.

  0 0

  Nafasi Art Space kwa kushirikiana na Tunawea leo wameendesha Warsha ya siku mbili ya Sanaa na Harakati iliyowakutanisha baadhi ya Wasanii, Waandishi wa Wanaharakati nchini Tanzania ambapo Mpiga picha na Mwanaharakati Boniface Mwangi kutoka Kenya ndio mwezeshaji katika warsha hiyo
   Mpiga picha na Mwanaharakati Boniface Mwangi kutoka Kenya, akizungumza na washiriki wa warsha hiyo
   Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada mbalimbali
   Mpiga picha na Mwanaharakati Boniface Mwangi kutoka Kenya, akizungumza na washiriki wa warsha hiyo
   Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo
  Mwazilishi wa Change Tanzania, Maria Sarungi Tsehai akichangia mada wakati wa warsha ya Sanaa na Harakati iliyofanyika jijini Dar es Salaam


  0 0

         Benki ya NMB juzi ilifungua tawi jipya maeneo ya Tandika- Dar es Salaam tawi linalokadiriwa kuhudumia Zaidi ya wateja 300 kwa siku. Tawi la NMB Tandika lipo maeneo ya Sokoni karibu na kituo cha polisi Tandika katika makutano ya mtaa wa Chihota na Ugweno.Tawi hili linatoa huduma kwa wakazi wa Tandika, Yombo,Buza,Mtongani na maeneo mengineyo.
   Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema akikata utepe kuashiria  uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Tandika.  Kutoka kushoto  ni; Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Temeke Bw.Bakari Kombo , Meneja wa NMB tawi la Temeke Bw.Harold Lambileki na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salam Bw, Salie Mlay wakishuhudia uzinduzi huo.
   Meneja wa tawi la NMB Tandika  Bw.Cosmas Peja akimwonyesha Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema idara mbali mbali zilizopo ndani ya tawi la NMB Tandika.Sambamba na uzinduzi wa tawi la NMB Tandika, NMB imetoa msaada wa vifaa vya hospitali katika hospitali ya Wilaya ya Temeke vyenye thamani ya Shilingi Milioni 5 na Madawati kwaajili ya Shule ya Sekondari Tandika  yenye thamani ya Shilingi Milioni 5.
   Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema akiongea na Fatuma Said Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari  Tandika mara baada ya kupokea madawati kutoka NMB wakati mwanafunzi Joachim Richard akisikiliza kwa makini. 
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema akipokea sehemu ya vifaa vya Hospitali kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salam Bw, Salie Mlay wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya hospitali ya Temeke iliyofanyika leo katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es salam.Kwanza kushoto ni: ni; Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Temeke Bw.Bakari Kombo na Mganga  Mkuu wa Hospitali ya Temeke Dk.Amaan Malima wakishuhudia makabidhiano.

  0 0

   Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Bwn. Suleiman Saleh(kulia) akimwakilisha Balozi Liberata Mulamula kwenye tafrija ya siku ya Uhuru wa nchi ya Oman iliyofanyika Washington, DC siku ya Jumanne Novemba 18, 2014. Mwingine katika picha ni Seif Ameir ambaye ni mfanyakazi kwenye Ubalozi huo.
   Toka kushoto ni Bi. Farida Saleh na Bi. Nargis Ameir wakiwa katika picha ya pamoja walipohudhuria sharehe ya uhuru wa nchi ya Oman iliyofanyika siku ya Jumanne Novemba 18, 2014 jijini Washington, DC.
  Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Bwn. Suleiman Saleh(kulia) akimwakilisha Balozi Liberata Mulamula kwenye tafrija ya siku ya Uhuru wa nchi ya Oman iliyofanyika Washington, DC siku ya Jumanne Novemba 18, 2014. Wengine katika picha toka kushoto ni Bwn. Seif Ameir akifuatiwa na mama mwenye nyumba wake Bi. Nargis Ameir na  Bi. Farida Saleh ambaye ndiye barafu ya moyo wa  Afisa Suleiman Saleh.

  0 0

   Maziwa yakiwa tayari yamekamliwa na kuhifadhiwa kwenye majokovu kabla ya kwenda kwa walaji. Shamba hilo la Uzalishaji ngo'mbe wa maziwa la Gereza Mtego wa Simba limekuwa likipigiwa mfano hapa nchini(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
   Sehemu ya Wanyama kazi katika Shamba Kubwa la Uzalishaji wa ngo'mbe wa nyama katika Gereza Ubena lililopo Mkoani Pwani. Shamba hilo lina takribani jumla ya ngo'mbe zaidi ya 1500. Uzalishaji wa ngo'mbe umekuwa ukiongezeka kwa mafanikio makubwa kila Mwaka hivi karibuni kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Uongozi wa Jeshi la Magereza katika kuyahudumia mashamba hayo Nchini.
   Lango Kuu la kuingilia Gereza la Mifugo Ubena lililopo Mkoani Pwani ambalo linashughulika zaidi  na Uzalishaji wa Mifugo. Wafungwa katika Gereza hilo wanapata elimu ya Ufugaji bora unaozingatia Kanuni za Ufugaji wa Kisasa ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa jukumu la Urekebishaji kwa Wafungwa.

   Kundi la ndama wakiwa zizini katika Shamba la Uzalishaji wa Mifugo Gereza la Mifugo Ubena, Mkoani Pwani.

  Kundi la ngo'mbe wa maziwa katika Shamba la Mifugo la Mtego wa Simba lililopo Mkoani Morogoro. Shamba hili la Mifugo ni Maalum kwa Uzalishaji wa Ngo'mbe wa maziwa kama inavyoonekana katika picha na Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1944.
  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Temeke Shophia Mjema wa kwanza (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.Hafla hiyo imefanyika leo.
   Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(katika)akimfafanulia jambo kuhusiana na simu aina ya Vodafone smart kicka Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema(kulia) alipofika  kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
   Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(kushoto)na Matina Nkurlu Meneja uhusiano wa kampuni hiyo(katikati)wakimsikiliza jambo kwa umakini Mkuu wa Wilaya ya Temeke Shophia Mjema(kulia)mara baada ya kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam leo.
   Mkuu wa Wilaya ya Temeke Shophia Mjema wane toka kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania mara baada ya kuzindua duka jipya la kampuni hiyo lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam leo.

  =========  =======  ========
  Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema ametoa ushauri kwa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kufungua zaidi  vituo vya kutoa huduma kwa wateja wilayani humo ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa karibu badala ya kuzifuata mbali na kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kufanya shughuli za uzalishaji.Alitoa ushauri huo wakati akifungua duka la Vodacom la Mbagala ambapo pia alitoa pongezi kwa hatua hiyo.
   
  Katika kuhakikisha wakazi wa vitongoji vya Mbagala na maeneo jirani ya Mtoni,Temeke na Tandika  wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imefungua duka jipya  katika  eneo la Mbagala Zakiemu.

  Mbagala ni moja ya kitongoji maarufu katika cha jiji la Dar es Salaam ambacho kinakuwa kwa kasi kwa maendeleo na kuwa kivutio cha wawekezaji wengi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu na shughuli mbalimbali za kibiashara ikiwemo kituo kikubwa cha mabasi yanayoelekea mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara.

  Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma  kwa mawakala wa Mpesa na uuzaji wa bidhaa  za Vodacom na litawawezesha wateja wa  Mbagala na vitongoji vyake   wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa ya Kusini  na wateja kutoka maeneo ya Temeke,Kurasini,Mtoni  na Tandika.Mtandao wa Vodacom unaongoza  kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika wilaya ya Temeke.

  Hassan Saleh Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Vodacom Tanzania,alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa  ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza  kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya  ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha wakulima nchini.

  “Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora kwa gharama nafuu.”Anasema Saleh.


  Vodacom ina mtandao wa maduka  84 nchi nzima na wakala mbalimbali wakuuza bidhaa zake nchini na  duka lililofunguliwa leo ni la 5 kufunguliwa katika wilaya ya Temeke.

  0 0  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dimani Mkoa wa Magharibi CCM katika viwanja vya Ofisi ya Mkoa Amani leo alipofika kuzungumza na Mabalozi na wenyeviti wa maskani katika mfululizo wa ziara zake za mikutano ya kuimarisha Chama katika Mikoa ya Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dimani Mkoa wa Magharibi CCM katika viwanja vya Ofisi ya Mkoa Amani leo alipofika kuzungumza na Mabalozi na wenyeviti wa maskani katika mfululizo waziara zake za kuimarisha Chama Mikoa ya Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wanachi na Wanachama wa CCM katika Mkutano wa Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani za CCM Wilaya ya Dimani katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama katikaMikoaya Unguja.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng. Ngosi Mwihava akizungumza kabla ya kuanza kwa mnada wa kwanza wa madini yaliyokamatwa yakisafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Bruno Mteta (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini Tanzania, Richard Kasesera (wa pili kulia), Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim (wa tatu kushoto), Meneja Usafirishaji Madini wa TMAA, George Kaseza (wa pili kushoto), na maafisa wengine kutoka TMAA, Eng. Charles Shamika (wa nne kushoto) na Flora Kisena (wa kwanza kushoto).
  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Bruno Mteta (wa nne kulia), akisoma moja ya zabuni (bid) ya ununuzi wa madini yaliyokuwa yakipigwa mnada jijini Arusha. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng. Ngosi Mwihava (wa tano kulia), Zabibu Napacho, Afisa Mfawidhi Ofisi ya TMAA-Arusha (wa kwanza kulia), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari TMAA, Eng.Yisambi Shiwa (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini Tanzania, Richard Kasesera (wa tatu kulia), Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Salim Salim (wa tatu kushoto), Meneja Usafirishaji Madini wa TMAA, George Kaseza (wa pili kushoto), na Eng. Charles Shamika (wa nne kushoto), Flora Kisena (wa kwanza kushoto) kutoka TMAA.
  wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito ya Arusha, wakishuhudia mnada wa kwanza wa madini yaliyokamatwa yakisafirishwa nje ya nchi bila kuwa na vibali husika.Aliyenyanyua karatasi ya maombi ya zabuni (bid) ya madini hayo ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Bruno Mteta.
  Meneja Usafirishaji Madini kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), George Kaseza (katikati),akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha, mara baada ya kumalizika kwa mnada wa kwanza wa madini yaliyokamatwa yakisafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.

  Na Teresia Mhagama

  Madini yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100 yaliyokamatwa wakati yakisafirishwa nje ya nchi bila kufuata taratibu za nchi za usafirishaji madini yamepigwa mnada na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

  Madini hayo yamepigwa mnada jijini Arusha katika Maonesho ya Tatu ya Kimataifa ya Vito yaliyofanyika katika hoteli ya Mount Meru ambapo mnada huo wa kwanza kufanyika nchini ulishuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eng.Ngosi Mwihava, Mwenyekii wa Bodi ya Ushauri wa Madini, Richard Kasesera, Makamishna Wasaidizi wa Madini nchini na wananchi waliohudhuria maonesho hayo.


  0 0

  Tanzania Portland Cement Co Ltd Managing Director, Alfonso Rodriguez (2nd L) hands over a dummy of cheque Euros 5000 (Tsh 11.5 million) to the first winner of TPCC Quarry Life Awards competition, Siajali Pamba (L) in Dar es Salaam yesterday. Second right is University of Dar es Salaam College of Natural & Applied Sciences Head of Aquatic Sciences & Fisheries Department, Dr. Charles Lugomela and TPCC Environment Manager, Richard Magoda.
  University of Dar es Salaam College of Natural & Applied Sciences Head of Aquatic Sciences & Fisheries Department, Dr. Charles Lugomela (3rd L) awards the second winner of TPCC Quarry Life Awards competition, Singira Ngoishiye (L) in Dar es Salaam yesterday. Second left is Tanzania Portland Cement Company Managing Director, Alfonso Rodriguez and TPCC Environment Manager, Richard Magoda. He went away with Euro 3000 (Tsh 6.9 million).
  Tanzania Portland Cement Co Ltd Managing Director, Alfonso Rodriguez (2nd L) hands over a dummy of cheque Euros 1500 (Tsh 3.5 million) to the third winner of TPCC Quarry Life Awards competition, Kelvin Ngongolo. Right is University of Dar es Salaam College of Natural & Applied Sciences Head of Aquatic Sciences & Fisheries Department, Dr. Charles Lugomela and TPCC Environment Manager, Richard Magoda.
  Tanzania Portland Cement Co Ltd Environment Manager, Richard Magoda (R), congratulates the TPCC Quarry Life Awards first winner, Siajali Pamba. Looking on are TPCC MD, Alfonso Rodriguez and University of Dar es Salaam College of Natural & Applied Sciences Head of Aquatic Sciences & Fisheries Department, Dr. Charles Lugomela and TPCC Environment Manager, Richard Magoda.
  TPCC some management team in a group photo with the winners.

  0 0


  0 0

   Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Job Ndugai akiongoza Kikao cha Bunge leo Novemba 20,2014 mjini Dodoma.

  Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akizungumza, Bungeni Mjini Dodoma leo Novemba 20, 2014.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiteta na Baadhi ya wabuge na Mawaziri, Bungeni mjini Dodoma leo Novemba 20, 2014.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiteta jambo na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Mbunge wa Urarmbo, Mh. Samuel Sitta, Bungeni Mjini Dodoma leo Novemba 20, 2014.
   Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Mbunge wa Urarmbo, Mh. Samuel Sitta (kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya Wabunge wa Upinzani kutoka kulia kwake ni Mh. David Kafulila,Mh. David Silinde na Mh. Tundu Lissu.
   Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Singida Mashariki,Mh.Tundu Lissu (kulia) akimwonyesha nyaraka fulani Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mh. Fredrick Werema,nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Novemba 20,2014.
  Mhe Andrew Chenge na Mhe. Richard Ndassa wakitafakari jambo wakati wakitoka katika ukumbi wa Bunge mjini Dododma leo Novemba 20,2014.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiteta na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Mh. Aggrey Mwanri (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mh. Chiku Galawa, kwenye viwanja vya hoteli ya St. Gaspar Mjini Dodoma baada ya kufungua Kongamano la Ajira la Wakuu wa Mikoa, leo Novemba 20, 2014.

  0 0
 • 11/20/14--10:10: ZIFF SUBMISSIONS NOW ONLINE
 • The Zanzibar International Film festival (ZIFF) has hit a new landmark for African film festivals as it becomes the first festival on the continent to have their film submissions totally online, and for a very low fee.

  With the growth of the Internet many film festivals have utilised the new found capacity to receive films online and reduce the time it took to select films. Festival programmers will now begin to watch films before the end of the submission period and give themselves ample time to watch films carefully and diligently.

  “The Festival is no longer accepting film submissions in hard copy for filmmakers outside Tanzania. Tanzanian filmmakers and producers will have one year of grace to submit their films both electronically and in hard copy and they won’t be charged a fee”, said Daniel Nyalusi ZIFF Festival Manager.

  “ZIFF has signed with Festhome, an international platform through which filmmakers from all over the world submit films to film festivals”, explained Nyalusi, “For less than the cost of a typical festival submission, we guarantee that your film will be viewed and in good time”.

  Now people can send a Password protected Vimeo file of any format and submit it online.

  The ZIFF festival provides an invaluable platform for filmmakers to showcase their craft to an international viewing audience.

  ZIFF2015, still sponsored by ZUKU, will take place between and 26th 18th January, 2015, this includes Bongo Movies. July 2015. Deadline for Submission is 31st

  0 0

  Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wameaswa kuendeleza ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao ili kutimiza malengo ambayo Wizara imejiwekea.

  Akizungumza na watumishi wa makao makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Novemba 20, 2014), Katibu Mkuu Bi.  Maimuna Tarishi amesema ushirikiano na upendo ni ngunzo muhimu za mafanikio katika taasisi yoyote.

  “Watumishi wa umma, hasa tuliopo Dar es Salaam, tunatumia muda mrefu tukiwa kazini hivyo tunatakiwa tupendane na tushirikiane katika kutekeleza majukumu yetu kama timu moja,” amesema Bi. Tarishi.

  Katibu Mkuu huyo alikuwa alikuwa akizungumza na watumishi hao kwa mara ya kwanza tangu alipohamishiwa Wizarani hapo hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii ambako alikuwa Katibu Mkuu.

  Aliongeza: “Tufanye kazi kwa malengo na kasi… tujiulize, wiki hii nimefanya nini, nimetekeleza nini,” alisema kiongozi huyo na kusisitiza kuwa watumishi wa Wizara ya Katiba wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Wizara.

  Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara hiyo Bi. Theresa Mghanga alimshukuru Katibu Mkuu kwa kutenga muda kukutana na watumishi na kusisitiza umuhimu wa watumishi wote wa Wizara kuzingatia sheria, kanuni na miongozo katika utumishi wao.

  “Tuwahi kazini na kutimiza wajibu wetu na tujione kuwa tuna deni kwa nchi yetu,” alisema Bi. Theresa katika mkutano huo uliohudhuriwa na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na watumishi wote wa Wizara waliopo makao makuu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Maimuna Tarishi akiongea na wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Nov. 20, 2014).
  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Theresa Mghanga (aliyesimama) akiongea katika mkutano kati ya Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi na watumishi wa Wizara hiyo.
  Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Maimuna Tarishi (hayupo pichani) leo (Alhamisi, Nov. 20, 2014). (Picha na Said Benjamin).

  0 0

  Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Dkt. Abdallah Kigoda akipata maelezo ya namna ya kunufaika baada ya kujiunga na Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF kutoka kwa Afisa Masoko wa Mfuko huo, Albert Kitunga, wakati alipotembelea banda la maonesho la GEPF kwenye maonyesho ya siku ya viwanda yanayoendelea kwenye viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ‘sabasaba’ Dar es Salaam.
  Afisa Masoko wa Mfuko wa GEPF, Albert Kitunga akimuonyesha Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Dkt. Abdallah Kigoda fomu za kujiunga na Mfuko huo wakati alipotembelea banda la maonesho la GEPF kwenye maonyesho ya siku ya viwanda yanayoendelea kwenye viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ‘sabasaba’ Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Mfuko wa Mafao ya Kustaafu GEPF wakitoa huduma kwa mmoja wa wateja wao mbalimbali kwenye maonyesho ya siku ya viwanda yanayofanyika kwenye viwanja vya maonesho ya Biashara ya Kimataifa ‘sabasaba’ Dar es Salaam.

  0 0

  Wiki hii, Ubalozi ukiongozwa na Mama Balozi Rose Mero umeshiriki kwenye maonyesho ya UN ya kina mama, Geneva (United Nations Women's Guild 2014), yenye lengo la kukusanya pesa za kusaidia miradi ya kuendeleza watoto wenye mahitaji mbalimbali duniani kote.

  Kwenye maonyesho hayo, banda la Tanzania lilijumuisha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kutengenezwa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kahawa, majani ya chai, khanga, vitenge, vinyago, korosho n.k

  Watu mbalimbali walipata nafasi ya kujipatia chakula cha kitanzania kama vile maandazi, chapatti, samaki wa kukaanga, maharage ya kuungwa na Nazi, chai yenye viungo vya tangawizi, sambusa, pilau, n.k
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alipata nafasi ya kutembelea banda la Tanzania akiwa Geneva kuhudhulia kikao cha Bodi ya " Water Supply and Sanitation Collaborative Council", ofisi zake Geneva, kwa nafasi yake kama Mwenyekiti.Kulia ni Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva, Mhe. Modest Mero


  0 0


  0 0  0 0

  1
  Doris Mollel akikabidhiwa vitabu 200 na mkurugenzi wa MAK Solutions Bi Meetal Kirubakaran. Vitabu hivyo vilikabidhiwa kwa shule ya msingi Mpunguzi iliyopo Dodoma kama mchango wa kuadhimisha siku ya watoto duniani.(Picha zote na Albert Manifester).
  Dodoma, Novemba 2014.
  Katika kuadhimisha siku ya watoto duniani inayofanyika tarehe 20 Novemba kila mwaka,  Miss central Zone 2014 Doris Mollel amechangia Vitabu vyenye thamani ya Shilingi Milioni moja (1,000,000/=) katika shule ya msingi Mpunguzi iliyopo katika kijiji cha Mpunguzi mkoani Dodoma.
  Doris, ambaye pia ni mshindi wa tatu kwenye Miss Tanzania 2014 amejikita katika sekta ya elimu kama sehemu ya huduma zake za jamii ambapo amedhamiria kuendeleza mchango kwenye elimu ya msingi kwa kuchangia vitabu kwenye shule zenye uhitaji zaidi.
  Msaada huo wa Vitabu 200 vya kiada na ziada ameutoa kwa ushirikiano na kampuni ya uuzaji wa Vitabu ya MAK Solutions yenye duka lake Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bi Meetal Kirubakaran alisema MAK solutions wanafurahi kutoa vitabu hivyo kama mchango wao katika kusaidia sekta ya elimu Tanzania.
  2
  Doris akijadiliana jambo na Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda (Katikati) mjini Dodoma kabla ya kuelekea Mpunguzi. Wa kwanza kushoto ni Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo na anayefuata ni Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela.
  Akizungumza kwenye hafla iliyofanyika shuleni hapo, Mollel alisema ‘Ni muhimu kuwajengea watoto wetu utamaduni wa kujisomea tangu wakiwa wadogo ili kuwakuza kukabiliana na changamoto za dunia ya sasa ambayo inahitaji uelewa mpana. Najivunia kuwa sehemu ya kampeni hii na nitaendelea kuongeza jitihada za kuwafikia watoto wengi zaidi’
  Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Bw. Juma Kaponda amempongeza Doris kwa juhudi zake za kusadia jamii hasa sekta ya elimu na ameomba wadau wengi kuiga mfano huu kuendeleza sekta hii.
  Hafla hiyo ya makabidhiano ilihuduriwa na mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mpunguzi Bi Neema Mando, Makamu mwalimu mkuu wa shule Bw Danctan Chipalo, Afisa elimu - ufundi manispaa ya Dodoma Bw Mnyagatwa Mazengo, Afisa elimu – Taaluma wa mkoa Bw Eliud Njogela pamoja na wanafunzi wote wa shule ya Mpunguzi.
  10
  Doris akiwa na baadhi ya wanafunzi baada ya kugawa vitabu.
  Alipokuwa njiani kuelekea mpunguzi, Doris alipata nafasi ya kuongea machache na baadhi ya wanafunzi wa vijiji vya jirani. 

older | 1 | .... | 646 | 647 | (Page 648) | 649 | 650 | .... | 3270 | newer