Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 642 | 643 | (Page 644) | 645 | 646 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 49 ya Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam akiimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi rasmi wa mahafali hayo jijini Dar es salaam. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Mathew Luhanga (katikati) na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema.
  Baadhi ya wahitimu wa shahada ya Uhasibu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam mwaka 2014 wakisubiri kutunukiwa shahada zao wakati wa mahafali ya 49 yaliyofanyika katika ukumbi wa Blue Pearl,Ubungo jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam waliohitimu masomo yao kwa mwaka 2014. Takribani wahitimu 3459 wametunukiwa Astashahada, Shahada na Stashahada za fani mbalimbali.
  Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema akizungumza na wahitimu 3459 wa fani mbalimbali wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam waliohitimu masomo yao mwaka 2014.


  0 0


  MWANAMICHEZO ambaye anacheza kwa kutumia pikipiki Bian Capper kutoka nchini Afrika kusini ametoa wito kwa watanzania kucheza mchezo huo ambao mbali ya kufurahisha pia unatumia akili na kukufanya uwe mkakamavu wakati wote.
  Akizungumza jana kabla kuonesha umahiri huo mchezaji wa pikipiki ambaye ni raia wa Afrika Kusini anayefanya ziara katika nchi za Afrika kwa udhamini wa kinywaji cha Redbull atakuwa nchini kwa ziara za ya maonesho ya kuonesha namna ya kucheza na pikipiki kwa siku tatu.
   Onyesho la kwanza lilianza jana kwenye viwanja vya Coco beach , leo Jumapili atakuwa Mlimani City na kesho Jumatatu atakuwa katika eneo la Ubungo Tanesco ambako litakuwa onyesho lake la mwisho.
  Capper amesema kwamba amefurahia kuweza kufika nchini pia tayari ameshafanya maonyesho yake katika nchi za Kenya na Uganda.

  Wakati huohuo Rais wa Tanzania Motorcross Acrobatic Club Blagina Mwihava alisema kwamba wamemleta mwanamuchezo huyo ambaye wana imani kubwa ataleta msisimko mkubwa kwa vijana wa kitanzania kuweza kupata hamasa ya kucheza mchezo huo wenye mvuto.
  “Hii itakuwa ni shoo kwa watanzania ili waweze kuvutika kucheza mcheo huu wa aina yake .

  Ziara ya mchezaji huyo imeratibiwa na Kampuni ya Mohans inayosambaza kinywaji cha Redbull nchini maonesho hayo yote ni ya wazi. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG

  0 0

   Mdau Meshack Ndoje jana Novemba 15, 2014 kwenye mahafali ya arobaini na nne (44) ya chuo kikuu cha Dar es Salaam katika ukumbi wa mlimani city alikuwa ni mmoja wa walamba nondozz waliotunukiwa Nondozz zao,Mdau Meshack amelamba nondozzz ya Takwimu yaani B.A. Statistics.
  Mdau Meshack Ndoje akiwa na baadhi ya ndugu zake waliofika kumsapoti kwenye mahafali hayo.

  0 0

   Nani kasema Old School ni kwa muziki peke yake? Mdau mwandamizi wa Globu ya Jamii Nathan Chiume na mai waifu wake wanakupa jibu la swali hilo wakiwa katika mfano wa studio za mpiga picha maarufu wa miaka ya sitini wa jijini Bamako, nchini Mali, Malick Sidibe, iliyo katika kituo kipya cha utamaduni wa Afrika (The Africa Centre: BOFYA HAPA) katika barabara ya tano na ya 110 (Fifth Avenue and 110th street) kitongoji cha Manhattan  hapo jijini New York kilichoanzishwa na bilionea Mo Ibrahim
   Hapo Nathan na Mai Waifu wake wanaonesha mapozi ya wapendanao walipokwenda studio hiyo. Yaani bila kuwa na redio, baiskeli ama pikipiki studio kulikuwa hakunogi.   Hehehe...si mchezo enzi hizo. Namna ya kuliingiza na kulitoa hilo bodaboda humo studio ni hadithi ingine. Kwa leo furahia taswira hizo huku ukijiuliza kuna ubaya wa kurudia huko?

  0 0

  Makamu wa Rais wa Kiwanda cha Dawa za Binaadamu cha Shuangcheng Bwana Jianlin Yuan akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake wakati walipotembelea kiwanda hicho wakiwa katika ziara ya Kiserikali Katika Jimbo la Kisiwa cha Hainan.
  Ujumbe wa Zanzibar Ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif ukifanya mazungumzo na Ujumbe wa Makampuni ya uwekezaji vitega uchumi katika Jimbo la Hainan ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji ya Hainan.
  Balozi Seif na Ujumbe wake wakiwa katika kikao cha pamoja cha ushirikiano kati ya Zanzibar na Uongozi wa Manispaa ya Mji wa Haikou ukiongozwa na Meya wa Mji Huo Mstahiki NI Qiang.
  Mwenyekiti wa Kiwanda cha kusindika bidhaa za nazi pamoja na matunda kiliopo Haikuu Bwana Huang Chunguang akimfahamisha Balozi Seif na Ujumbe juhudi zinazochukuliwa na Kiwanda hicho katika kulitumia vyema zao la nazi. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na Kulia yake ni Waziri wa Ardhi Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban na Waziri wa Habari Mh. Sai Ali Mbarouk. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Maofisa wa Uhamiaji kutoka Dar Es Salaam na Zanzibar wameanza zoezi la kupokea maombi ya pasipoti kutoka kwa Watanzania waliopo nchini Italy. Maofisa hao wanategemewa kuelekea katika nchi za Turkey na Greece,kwa ajili ya zoezi hilo hilo.

   Haya ni matunda ya Kamati ya Diaspora iliyokutana na Mh Balozi James Alex Msekela, mwezi juni mwaka huu. Kamati ilikutana na balozi na maofisa wa juu wa kibalozi kwa ajili ya kutambulisha kamati na uongozi wake,na pia kuwakilisha kero na matatizo ya watanzania wanaoishi Italy . 

  Mkutano huo uliisha kwa mafanikio makubwa. Kwa hiyo haya ni matokeo ya uchapa kazi wa kweli wa mh Balozi Dkt James Alex Msekela, kwani katika mapumziko yake nchini Tanzania mwezi August mwaka huu alitumia muda wake kukutana na Kamishna wa Uhamiaji Tanzania kujadili suala la matatizo ya Pasipoti kwa watanzania wa Maeneo ya uwakilishi wake.
  Baadhi ya Maofisa wa Uhamiaji ambao wako nchini Italy hivi sasa,wakiendelea na kazi rasmi ya  kutatua matatizo ya pasipoti kwa watanzania waishio nchini humo, wakiwa katika siku ya pili ya zoezi hilo,ambalo linaanzia asubuhi mapema saa 3 hadi saa kumi na mbili jioni.
  Afisa Uhamiaji akichukua maelezo ya mmoja wa Watanzania waishio nchini Italy wakati wa zoezi la kutatua matatizo ya pasipoti kwa watanzania hao.

  Sehemu ya Watanzania hao wakisubiri kutatuliwa matatizo yao ya pasipoti.

  0 0

  Waziri wa Afya Mhe.Dkt Seif Rashidi aongoza zoezi la kupima afya za Wabunge katika Ukumbi wa Msekwa jana.Upimaji wa afya za Wabunge umefanywa na Madaktari wa Aga Khan kutoka Morogoro,Dar. na Dodoma.
  Waziri wa Afya Mhe.Dkt Seif Rashidi (kulia) akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Agha Khan,Sisawo Konteh wakati wa zoezi la upimaji wa Afya kwa Waheshimiwa Wabunge,Mjini Dodoma jana.Katikani ni Mmoja wa Maafisa waandamizi wa Hospitali ya Agha Khan.
  Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini,Mchungaji Luckson Mwanjale akimsikiliza kwa Makini Mtaalam wa Maswala ya Afya kutoka Hospitali ya Agha Khan wakati wa zoezi la kupima Afya kwa waheshimiwa Wabunge,Mjini Dodoma jana.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (kazi maalum),Prof. Mark Mwandosya akijiandaa kupima uzito wake.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma akipima akichukuliwa vipimo na Daktari kutoka Hospitali ya Agha Khan.


  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kaimu Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimuapisha Dkt. Adelhelm James Meru kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Novemba 17,2014 Ikulu Dar es salaam.
  Makamu wa Rais na Kaimu Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Dkt. Adelhelma James Meru wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuapishwa leo Novemba 17, 2014 Ikulu Dar es salaam.
  Makamu wa Rais na Kaimu Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Dkt. Adelhelma James Meru wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya kuapishwa leo Novemba 17, 2014 Ikulu Dar es salaam.
  Makamu wa Rais na Kaimu Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Dkt. Adelhelma James Meru wakiwa katika picha ya pamoja na Familia mara baada ya kuapishwa leo Novemba 17, 2014 Ikulu Dar es salaam. (Picha na OMR)

  0 0

  Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili viwanja vya Ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Unguja kuzungumza na Mabalozi wa Wilaya ya Mjini CCM katika kuimarisha Chama alipoanza ziara maalum kwa mikoa mitano ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani katika mkutano wa Mabalozi wa CCM Wilaya ya Mjini Unguja,alipofika kuzungumza nao akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi kwa Mikoa mitatu ya Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Mabalozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mjini katika Ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Unguja leo akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama katika Mikoa ya Unguja (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na (kushoto) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mjini Juma Faki Chum
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Mabalozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mjini katika Ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Unguja leo akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama katika Mikoa ya Unguja.
  Baadhi ya Viongozi na Mabalozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mjini wakiwa katika Mkutano uliohutubiwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Unguja leo.[Picha na Ikulu.]

  0 0

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa GHASIA akiwahutubia Viongozi wa mkoa wa Mtwara pamoja na wananchi wa mkoa wa Mtwara walio shiriki katika uzinduzi wa majengo ya tawi la Chuo kikuu huria Tanzania kushoto kwa waziri ni Makamu wa chuo kikuu huria Tanzania Profesa Tolly Mbwete kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego Waziri Hawa Ghasia alimuakilisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika uzinduzi wa majengo ya tawi la chuo kikuu huria Mtwara.
  Makamu mkuu wa Chuo kikuu huria Tanzania Profesa Tolly Mbwete aliye vaa koti akimuonyesha WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa GHASIA Vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufundisha kwakutumia Intarnet katikati ni Mhadhiri wa taluma ya sayansi ya mtandao Dr Edephonce Ngemera Waziri Hawa Ghasia alikuwa akimuakilisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika uzinduzi wa majengo ya tawi la chuo kikuu huria mkoani Mtwara.
  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa GHASIA akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Serikali pamoja na viongozi wa chuo kikuu huria mkoani Mtwara.Picha na Chris Mfinanga 

  0 0

  Wadau wa soka nchini na wateja Vodacom Tanzania kwa ujumla wameletewa Promosheni mpya na ya aina yake iliyozinduliwa jana na kampuni hiyo ambapo imewalenga wapenzi wa soka na wateja wa kampuni hiyo kushiriki katika Promosheni ya “SHINDA NA KAMBUMBU”

  Promosheni hii ambayo itadumu kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo itawafanya wapenzi wa soka kuchemsha bongo kujibu maswali mbalimbali kuhusiana na ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Ligi kuu ya Uingereza,na masuala mengine mengi yanayohusiana na Kombe la Dunia na mengine mengi yanayohusiana na mchezo wa soka kwa ujumla.

  Kila siku wapenzi wa soka au wateja 5 watajinyakulia shilingi 50,000 pia atakuwepo mshindi mmoja wa wiki atakaejinyakulia shilingi Milioni 1. Na droo ya mwisho katika promosheni hii tutapata mshindi wa jumla atakaejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5 pesa taslimu. Ili kushiriki katika promosheni hii mpenzi wa soka au mteja yeyote wa mtandao huu anachopaswa kufanya ni kutuma neno SOKA kwenda namba 15725 na hapo mteja atakatwa kiasi cha shilingi 99 tu kwa kila meseji.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hii Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amewasihi wapenzi wa soka na watanzania kwa ujumla kushiriki katika promosheni hii na kutuma meseji nyingi za kujibu maswali yanayohusiana na soka ili waweze kujishindia zawadi na kufanya maisha yao kuwa murua.

  “Wakati umefika tena kwa wateja wa Vodacom na wapenzi wa mpira wa miguu kujishindia zawadi kemkem kupitia promosheni hii kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote,na kupitia promosheni mbalimbali za kampuni hii wateja wetu wengi wameweza kunufaika na maisha yao kuwa murua kwa kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu”.Alisema Nkurlu.

  Amesema kila wiki washindi watakuwa wakitangazwa na kupigiwa simu moja kwa moja baada ya kufanyika droo za kila wiki na kutumiwa fedha zao kwa njia ya M pesa na alitumia nafasi hiyo kuwapa tahadhari na matapeli ambao wamekuwa wakitumia promosheni kama hizi kuwarubuni wateja kuwa wawatumie fedha ili waweze kushinda zawadi wakati hawahusiki na promosheni hii.

  Vodacom imekuwa ikiandaa promosheni mbalimbali kwa wateja wake na moja ya promosheni ambayo imewafanya wateja wake maisha yao kuwa murua ni ile ya Timka na bodaboda na Vodacom milionea ambapo washindi waliweza kujishindia pikipiki na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 100.
  001&002.Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(kushoto)akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya ”SHINDA NA KABUMBU”inayolenga kuwawezesha wadau wa soka na wateja wa kampuni hiyo kushiriki kwa kutuma neno SOKA kwenda namba 15725 ambapo mteja atakuwa akiulizwa maswali mbalimbali kwa njia ya ujumbe kuhusiana na maswala ya soka na kuweza kujishindia fedha taslimu kuanzia shingili elfu 50 mpaka Milioni 5/= kulia ni Afisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe,hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0
 • 11/17/14--02:59: Article 19

 • 0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa pongezi kwa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kufuatia timu yake ya Taifa (Bafana Bafana) kufuzu kucheza fainali zijazo za AFCON nchini Equatorial Guinea.

  Afrika Kusini iliifunga Sudan mabao 2-1, hivyo kufuzu kabla ya kukamilisha michezo yote. Bafana Bafana bado imebakiza mchezo mmoja katika hatua hiyo.

  Wakati huo huo, TFF imeipeleka barua ya shukrani kwa Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kwa kufanikisha kambi ya Taifa Stars nchini humo kabla ya kwenda kucheza Swaziland.

  SAFA ilitoa viwanja vya mazoezi kwa Taifa Stars na usafiri wa basi la kisasa kutoka Johannesburg kwenda Swaziland na kurudi, hivyo kuokoa zaidi ya dola 15,000 ambazo TFF ingetumia kama ingegharamia yenyewe safari hiyo au kuweka kambi ya timu hiyo nyumbani.

  Awali Benchi la Ufundi la Taifa Stars chini ya Kocha Mart Nooij lilipendekeza timu kufika Swaziland mapema au kuweka kambi nchini Afrika Kusini. SAFA ikajitolea kusaidia kambi hiyo.

  Pia TFF inakanusha madai ya gazeti moja la kila siku lililodai kuwa wakaguzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wamevamia/wamefanya ukaguzi wa siri kukagua fedha za udhamini wao kwa Taifa Stars.

  Ukaguzi wa hesabu ni utaratibu wa kawaida wa kila robo ya mwaka wa fedha. TFF ndiyo huwaalika TBL kutuma wakaguzi wao ili kuhakiki vitabu vya fedha. Uhusiano kati ya TFF na TBL ni mzuri, na kila kinachofanyika ni kwa nia njema kwa makubaliano ya pande zote mbili.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege (kulia) akitoa maelekezo kwa baadhi ya wawasilishaji mada katika mafunzo yanayoshirikisha maafisa mazingira katika mikoa ya Iringa na Mbeya yanayofanyika jijini Mbeya leo. Lengo la mafunzo hayo ni kuwashirikisha mpango kazi wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na kupata michango yao. Kushoto ni Meneja wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Nyanda za Juu Kusini David Elias. Katikati ni Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Abdullatif Nassor.
  Afisa Misitu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Theodore Silinge akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
  Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege (kulia) akielezea shughuli za Kitengo chake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi ili aweze kufungua mafunzo hayo.
  Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa madini hotuba iliyokuwa inawasilishwa na mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi (hayupo pichani).
  Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi (katikati) akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
  Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi ( wa nne kutoka kushoto waliosimama mbele); Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege ( wa tatu kutoka kushoto waliosimama mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

  0 0


  Na Mwandishi wetu,Kagera.


  KIKUNDI cha Wanaume wapiga kasia cha Nichoraus Ngoroma Kisiwa cha Ukerewe kimeibuka na ubingwa katika fainali za mashindano yambio za mitumbwi chini ya udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager zijulikazo kama “Balimi Boat Race 2014” na hivyo kikundi hicho kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na kuwakilisha Kisiwa hicho kwenye fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Desemba 6 mwaka huu jijini Mwanza.

  Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Kapina Kagari ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/= pamoja na kuwakilisha Kisiwa cha Ukerewe katika fainali za Kanda jijini Mwanza pia, wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Athumani Malemo ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Mashauri Saidi ambacho kilizawadiwa Shilingi 400,000/=

  Nafasi ya tano hadi ya tisa walipewa kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi ambavyo ni Asante Robert, Ladsilaus Musimu, Benedicto Aniseti, Gervas Kulwa, Simon Fundi na Silvari Sasieli.

  Upande wa Wanawake kikundi cha Muhate Mwocha kilifanikiwa kutwaa ubingwa na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza.Nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Mlanzi Mussa ambao walizawadiwa Shilingi 600,000/=,washindi wa tatu ni kikundi cha Joyce Makalu ambao walizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Beatrice Kalomba ambao walizawadiwa Shilingi 300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 200,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Pili Masitu, Adventina Elias, Jesca Jose, Veronica Machumu,Juliana Petro na Maria Mabagara.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mery Tesha kwanza alitoa shukrani kwa Kampuni ya bia nchini(TBL) kupitia bia ya Balimi Extra Lager ambao ndio wadhamini wa mashindano hayo na kuwaomba waendelee kudhamini kwani yanaleta hamasa umoja na udugu kati yetu kuiachilia mbali afya na kipato kinachopatikana kama zawadi mara baada ya mashindano.

  Tesha alisema washindi waliopatikana wakaiwakilishe vyema Ukerewe na wahakikishe wanarudi na ushindi na wale ambao hawakupata nafasi ya kushinda wajiandae kwa mashindano mengine mwakani.

  Tesha alimaliza kwa kuwaomba zawadi walizopewa wakazitumie kwab maendeleo yao kwani huo ni mtaji tocha kwa mtu anayeweza kujishughulisha.

  Fainali za Kanda za mbio za mitumbwi zijulikanazo kama “Balimi Boat Race 2014” zinatarajiwa kufanyika Desemba 6, mwaka huu jijini Mwanza katika ufukwe wa Mwaloni.
  Washindi wa kwanza wa mbio za makasia wa Kisiwa cha ukerewe kikundi cha Nichoraus Ngoroma wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi mwishoni mwa wiki.

  0 0

  After 42 days in the Big Brother Hotshots house, Mr. 265 (Malawi) and Samantha (South Africa) were evicted on Sunday night after not picking up enough votes from the continent. The 12 housemates who are left in the game are on high alert though, as Big Brother introduced a twist which they think puts them all in danger of leaving next week and surrendering their shot at the USD300 000 prize.

  After Samantha and Mr. 265 were evicted, IK took viewers into the house for a special announcement from Big Brother. Biggie told the housemates that there were to be no nominations after the live show, but that instead, all of them were up for eviction next Sunday. On top of that, he announced that ten housemates from previous seasons of Big Brother Africa would be entering the game. Each current Hotshots housemate will have to compete against an ex-housemates in order to stay in the game. At the end of the week the audience will decide whether to keep the Hotshots housemate or to swop them with an ex-housemate from their country.   As the housemates caught their breath, IK informed viewers that Big Brother was playing a prank on the housemates – there is no voting this week, and nobody is in danger of leaving on Sunday. The returning housemates are not eligible for the USD300 000 prize and are in on the prank – but the Hotshots think they need to fight for their lives in the game.


  IK then went back into the house and introduced the returning housemates one by one. The ‘match-ups’ are: Idris vs Feza from BBA: The Chase; Macky2 vs Sulu from BBA: the Chase; Goitse & Sheillah vs Miss P from BBA Amplified; Sipe vs Natasha from BBA: The Chase; Tayo vs Uti from BBA 3 & All Stars; JJ & Butterphly vs Vimbai from BBA Amplified; M’am Bea vs Elikem from BBA: The Chase; Ellah vs Denzel from BBA: The Chase; Trezagah vs Leonel from BBA Revolution and Nhlanhla vs Luclay from BBA Amplified. The returning housemates are back in front of the Big Brother cameras for one week and will enter the Big Brother House on Monday, 17 November 2014 at 20h30 CAT right after the conclusion of the Nomination show broadcast.It’s going to be a tough week for the Hotshots!


  Unfortunately for Samantha and Mr. 265, their eviction was no prank and they joined IK on stage after he revealed that they’d received the fewest viewer votes this week. Samantha was only in the firing line after being ‘added’ by Head of House Sipe, who stood and told the housemates that her decision was nothing personal. “I added Samantha because I was looking at the strongest people from the other group because most the people in my group were already up,” said the Malawian with a shrug.

  Out on stage with her co-evictee, Samantha said that she had a feeling she’d be leaving and had even gone as far as packing up all her personal items. “I always felt there were some underlying issues with Sipe and I and that she’d put me up. Also compared to the people I was put up against, I felt they were very strong,” she said. IK quizzed her about the effect of the ‘strike’ she received early on in the game for conspiracy. “I got to a point where I didn’t know if I should speak about certain things – I was very paranoid,” said Samantha. After showing her, her highlights package, IK asked about JJ and Idris, who featured quite heavily towards the end. “It seemed like Idris, outside the house and away from cameras, would be someone that you’d date?” asked IK. “Yes, I would say that,” was her response. “But Not JJ?” teased IK. “No!” she said, with a laugh and a shake of her head. 


  Mr. 265 said he had mixed feelings about being evicted. “ Being put up, there’s a possibility you survive or not, so it’s all cool,” said the Malawian. IK quizzed him on his ‘altercation’ with Tayo, where he had to ask the Nigerian to stop singing loudly while his team was trying to prepare for a task, but he brushed it off. “What’s this show going to do for your career as a radio and television presenter?” asked IK. “We’ll have to see how things have changed outside the house,” said Mr. 265. “As Figgie said, we’re quite lazy and there’s a lot of work we have to do after this – I think the chapter begins now.”


  It had been a busy week for the housemates. Big Brother came up with a unique punishment for Butterphly, who had been seen to move during the ‘freeze’ stripper task. Every time Big Brother played a specific musical riff for a period of 48 hours, she was to stop what she was doing and give the nearest male housemate a lap dance. On Tuesday, Big Brother was replaced by a flirtatious imposter – a female Biggie called ‘Figgie’. She was a little harsh on some of the housemates and a little flirty with others, constantly asking the guys to take their shirts off in the Diary Room and teasing the housemates about their weight.

  During this week’s Modern Drama Extravaganza, the housemates were told that they were not playing for immunity as usual, but rather for a team reward – the chance to receive messages from home. The StarMeter question for the past week was “Which Big Brother Hotshots housemate is the funniest” – a title that went to Macky2. This week, the question to be answered by social media buzz is “Which Big Brother Hotshots housemate is the craziest?”

  The musical accompaniment to the live show was provided by Zambian duo JK, who kicked off the show with ‘Telemundo’ and Kay Figo who added a bit of spice with ‘Kanyelele’ later on. 

  Stay in touch with Big Brother Hotshots on social media - follow @bigbroafrica on Twitter, @bigbro_africa on Instagram and on Facebook at facebook.com/bigbrotherafrica.

  Big Brother Hotshots is produced by Endemol South Africa.

  0 0

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Job Ndugai akikabidhi Ripoti maalumu ya  CAG Kuhusu akaunti ya ESCROW kwa Mwenyekiti wa PAC Mhe. Zitto Kabwe na Kaimu wake Mh. Deo Filikunjombe,Bungeni mjini Dodoma leo.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Job Ndugai akikabidhi Ripoti maalumu ya  CAG Kuhusu akaunti ya ESCROW kwa Mwenyekiti wa PAC,Mhe. Zitto Kabwe 
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Job Ndugai akiwa ameshikilia vitambu vilivyo Beba ripoti ya CAG kuhusu akaunti ya ESCROW Kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa PAC Mhe.Zitto Kabwe leo.Picha na Deusdidus Moshi,Globu ya JAmii Kanda ya Kati.

  0 0

  Kampuni ya Bima ya Resolution leo hii imeaanda siku maalum ya familia kwa ajili ya wateja wake katika viwanya vya Posta jijini Dar es Salaam.

  Hii ni mara ya kwanza kampuni hiyo imeaanda siku hii maalum kwa ajili ya wateja wake na kulikuwa na burudani ya kutosha kutoka bendi ya Borabora, DJ maalum na vichekesho kutoka MC Pilipili. Kulikuwa pia na michezo mbalimbali ya watu wazima na watoto kama vile: soka, dance limbo na tug of war. Wateja waalikwa walipata chakula kwani kulikuwa na chakula cha kutosha.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution Bwana Oscar Osir alisema, “ Tukiwa tunaelekea kumaliza mwaka wa 2014 tuliona muhimu kumaliza mwaka kwa furaha na ndio maana tumejumuika na wateja wetu leo katika siku hii ya familia

  “ Kadri kampuni yetu inavyozidi kukua mchini Tanzania tunatarajia kuwa na siku maalum zingine kama hizi ili kufurahi pamoja na wateja wetu. Wateja wetu wametuamini kuwapa bima ya afya bora na kwa familia zao na hivyo basi ni vizuri kuwaonyesha jinsi tunavyowathamini” Bwana Osir alisema

  Kampuni hiyo pia ilitoa huduma ya afya na kuwapa wateja wao fursa ya kujadiliana maswala tofauti ya afya.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Resolution Insurance, Oscar Osir (kushoto)akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya Wanafamilia wa kampuni hiyo iliyofanyika mwiashoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Kulia ni Watoto wa wakisubili keki ikatwe wale.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Resolution Insurance, Oscar Osir(katikati) akikata keki wakati wa hafla ya kampuni hiyo kwa wafanyakazi na wateja iliyofanyika Viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam.
  Mchezaji Abdalah Abdul(kulia) akijaribu kumtoka Hilari Salehe wakati wa hafla kwa nafamilia wa Resolution Insurance(Bima ya Afya) iliyofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Baadhi zya washiriki wa mbio za Magunia wakishindana wakati wa wa hafla kwa nafamilia wa Resolution Insurance(Bima ya Afya) iliyofanyika katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Robert Kishiki alishinda mbio hizo.
  Wafanyakazi wa Resolution Insurance wakiwaburuza wateja wakati wa mpambano wa kuvuta kamaba baina ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wateja uliofanyika viwanja vya kijitonyama jijini Dar es Salaam mwioshoni mwa wiki.Wafanyakazi wa Resolution Insurance walishinda.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alphonso Rodrudges(suti ya bluu) akikabidhi mfano wa hundi yenye kiasi cha Tsh. Millioni Miamoja kwa Uongozi wa Jeshi la Magereza zitakazotumika katika ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni (wa pili kulia) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil(wa tatu kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja. hafla hiyo imefanyika leo Novemba 17, 2014 katika viwanja vya Gereza Wazo, Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil hotuba yake fupi katika hafla ya kupokea vifaa vya ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni, hafla hiyo imefanyika leo Novemba 17, 2014 katika viwanja vya Gereza Wazo, Jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi katika hafla ya kupokea vifaa vya ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni, hafla hiyo imefanyika leo Novemba 17, 2014 katika viwanja vya Gereza Wazo, Jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Vifaa vya ujenzi vilivyokabidhi leo na Kampuni ya Twiga Cement. Kampuni hiyo imekabidhi mifuko 1200 ya saruji pamoja na fedha Tsh. Millioni Miamoja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil(kushoto) akikata utepe kabla ya kukabidhiwa rasmi vifaa vya ujenzi pamoja na hundi yenye kiasi cha Tsh. Millioni Miamoja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulawakil(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza mara baada ya kukabidhiwa rasmi vifaa vya ujenzi pamoja na hundi yenye kiasi cha Tsh. Millioni Miamoja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zenye hadhi kwa Maofisa na Askari wa Gereza Wazo,Wilayani Kinondoni(wa tatu toka kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Magereza Huduma za Urekebishaji, Injinia. Deonice Chamulesile(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

older | 1 | .... | 642 | 643 | (Page 644) | 645 | 646 | .... | 3283 | newer