Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 641 | 642 | (Page 643) | 644 | 645 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Katika
  mazungumzo maalum na Kituo cha Mlimani TV cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amewasisitiza waandaaji wa matamasha na mashindano ya Sanaa na urembo kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo katika kuendesha matukio yao.

  Pia,amewataka waandaaji wa mashindano na matamasha katika vitongoji kuwa makini katika kusimamia taratibu kwani ndiyo wanaoandaa washiriki ambao baadaye wanakuja kushiriki kwenye ngazi ya taifa. 

  Katika hili amewataka kutumia upembuzi yakinifu kabla ya kuruhusu washiriki ama wasanii kushiriki katika matukio yao ili kukwepa aibu kwa taifa.

  "Kama kuna vielelezo au nyaraka zinahitajika, waandaaji lazima waziombe kwa washiriki na wazihakiki kikamlifu. Kama kuna utata wahakikishe wanahusisha mamlaka zinazohusika mapema ili kuupata ukweli" aliongeza Mngereza.

  Aidha, amesisitiza kwamba BASATA litaendelea kuwabana waendeshaji/waandaaji wa matukio ya Sanaa kwani ndiyo wenye jukumu la kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na ndiyo wanaopewa idhini ya uendeshaji na Serikali.

  “Kama katika ngazi ya vitongoji,wilaya na kanda waandaaji wangeweka msisitizo, changamoto zisingekuwepo. Kuna ulegelege wa kudhibitiwa” Aliongeza. 

  Amewataka waandaaji wote kusimamia kanuni  na taratibu zao  kwa haraka pasipo kusubili mashinikizo na malalamiko kutoka kwa jamii.

  0 0

  DSC_0317-1024x682
  CEO of MeTL GROUP, Mohammed Dewji.

  0 0
 • 11/15/14--07:30: WANA CCM BEIJING WAKUTANA
 • Wanachama wapya wa Tawi la CCM China waliopo Beijing wakikabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa Tawi Ndugu Boniphace Shija Nobeji.

  Kada na Mtumishi wa CCM Makao Makuu Ndugu Suleiman Serera akitoa semina iliyohusu itikadi na imani ya CCM kwa wanachama wa CCM Beijing.


  Sehemu ya wanachama waliohudhuria wakiuatilia kwa makini semina iliyokuwa ikitolewa.

  Wanachama wa mashina ya CCM Beijing wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza Mkutano wao uliofanyika katika Chuo cha Beijing Normal. 

  0 0

  Mgeni rasmi kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi ambaye ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akitoa nasaha zake kwa washiriki wa Bonanza hilo lililofanyika leo Novemba 15,2014 kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Picha zote na Othman Michuzi.
  Kaimu Mkurugeni wa Elimu na Huduma wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Allan Kiulla (kulia) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi lililofanyika leo kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Bonanza hilo lililogeshwa kufanyika michezo mbali mbali,ikiwepo mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na mingine mingi.Wa pili kulia ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki ambaye ndie alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Bonanza hilo.

  Sehemu ya Wafanyakazi wa  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wafanyakazi wa NSSF ambao ni Waalikwa walioshiriki kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi wakifatilia kwa makini nasaha za Mgeni Rasmi,ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti".
  Mtanange wa kukata na shoka kati ya Timu ya TRA na timu ya NSSF ulipigwa katika Uwanja wa TCC Chang'ombe,Mtanange uliowatoa kifua Mbele vijana wa NSSF kwa Mabao 4-2 dhidi ya wenzao wa TRA.
  Mbio za kuku kwa kina Baba zilikuwa ni sehemu ya michezo iliyofanyika leo Uwanjani hapo.


  Vijana wa Kundi la Wanne Star wakionyesha makeke yao mbele ya wadau wa TRA waliofurika kwa wingi kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo.


  0 0

  Ugandan President Yoweri Kaguta Museveni delivering his Keynote speech during the 39th World Congress of Africa Travel Association (ATA) in Kampala, Uganda.Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu (right) addressing the participants during the 39th World Congress of Africa Travel Association (ATA) in Kampala, Uganda. With him is the Executive Director of ATA Edward Bergman.
  High table stands during the playing of the Ugandan and EAC anthems.
  Part of the Tanzanian delegation attending the 39th World Congress of Africa Travel Association (ATA) in Kampala, Uganda. They are from left: Asantael Melita (Ngorongoro Conservation Area Authority); Philip Chitaunga (Tanzania Tourist Board); Kelvin Nkulila (Tanzania National Parks); Uzeel Kiangi; Lilian Nyaki and Imani Nkuwi from the Ministry of Natural Resources and Tourism.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari (hawapo pichani) wakati alipokutana nao nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana kwa mazungumzo
  Mhariri wa gazeti la Jamhuri, Jackton Manyerere, akichangia mada wakati wa mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, yaliyofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam, jana Novemba 14, 2014
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri, Deodatus Balile na Mhariri wake, Jackton Manyerere (kulia) mara baada ya kumalizika mazungumzo na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari yaliyofanyika kwenye Makazi ya Mhe Makamu wa Rais Oysterbay, jijini Dar es Salaam, jana usiku Novemba 14, 2014.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Wahariri wa Gazeti la Mwananchi mara baada ya kumalizika mazungumzo na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari yaliyofanyika kwenye Makazi ya Mhe Makamu wa Rais Oysterbay, jijini Dar es Salaam, jana usiku Novemba 14, 2014. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wahariri hao baada ya mazungumzo. Picha na OMR. 

  0 0

  Mwandishi Wetu

  VINARA wa Ligi Daraja la kwanza katika kundi A, timu ya Friends Rangers, kesho wanashuka katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kuvaana na timu ya Kimondo, katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza.

  Ofisa Habari wa klabu hiyo, Asha Kigundula, amewataka wapenzi wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo, kuwapa hamasa wachezaji wao. Kigundula alisema kuwa wana amini mchezo huo utakuwa mgumu, lakini kujitokeza kwa wapenzi wengi kutawafanya wachezaji wao wawe na hamasa kubwa na kuweza kupata ushindi katika mchezo huo.

  Alisema kuwa kikosi chao tayari kipo kambini kujiandaa na mchezo huo, ambao ni muhimu kushinda, ili kiweze kupigania nafasi ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao.

  Kigundula alisema kuwa kushinda kwao katika mchezo wao uliopita dhidi ya Majimaji, kumeisaidia timu yao kuzidi kupaa na kukaa juu ya msimamo wa kundi lao.

  Alisema kushinda kwao katika mchezo huo ni juhudi binafsi za wachezaji, viongozi na wapenzi wa timu hiyo kwa sababu walikuwepo na kuwapa ushirikiano mwanzo. Katika mchezo wa huo uliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Friends Rangers iliwapa kichapo cha mabao 2-1 timu ya Majimaji ya Songea. 

   Kwa matokeo hayo Friends Rangers wanaongoza kundi kwa pointi 19 huku maji maji ambao ndio walikuwa wakiongoza ligi hiyo katika kundi hilo wakishushwa na kubakia na pointi zao 18.

  0 0

  Jengo la ofisi ya Mkuu a mkoa wa Kilimanjaro linavyoonekana kwa juu.


  Katikati ya mji wa Moshi


  Jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Moshi linavyoonekana kwa juu.


  Eneo la kati jirani na ofisi za mkuu wa wilaya ya Moshi.


  Ujenzi wa jengo jipya la Ghorofa jirani kabisa na kipta shoto cha Arusha.
  Eneo la katikati ya mji wa Moshi.


  Jengo zilipo ofisi za mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro .


  Eneo la Shanty town linavyoonekana kwa mbali.Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile akizungumza na wafanyakazi wa benki ya Stanbick jana wakati alipotembelea banda lao katika maonesho ya wadau Gesi na Oil yanayoendelea mkoani Mtwara.
  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Wilman Ndile akizungumza na Ofisa wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN, Francis Kihinga wakati walipokutana kwenye mkutano wa wadau wa gesi unaoendelea mkoani Mtwara, TSN ni moja kati ya wadhamini wa mkutano huo.
  Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye maonesho ya bidhaa za wadau mbalimbali wa madini yaliyofanyika sambamba na mkutano huo. Maonesho hayo yalifanyika katika umbi wa Mikutano wa Chuo cha Veta Mtwara wakati Mkutano wa wadau ulifanyika katika hoteli ya Naf.
  Afisa Matekelezi wa NSSF mkoani Mtwara, Jamila Mfanga akimkabidhi wa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile vipeperushi vya bidhaa zake.
  Picha na wadau.
  Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile (kushoto) akiangalia bango la mafunzo ya Chuo Kikuu Huria ambao walifungua chuo chao mkoani humo, nao walikuwa ni baadhi ya waliojitokeza kwenye maonesho hayo pia pembeni yake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Tolly Mbwete.
  Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Ndile (kushoto) akiwaonesha baadhi ya wageni waliohudhuria mkutano wa kujadilia masuala ya gesi na Mafuta unaoendelea mkoani Mtwara, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta binafsi nchini (TPSF) Godfrey Simbeye pembeni Mwenyekito wa Bodi ya Ushauri wa Madini, Richard Kasesela.

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda (Mb) akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Bunge leo na kuainisha hatua madhubuti za kuchukuliwa na serikali ili kukomesha mauaji baina ya wakulima na wafugaji yanayoendelea Mkoani Manyara wilaya Kiteto na sehemu nyingine nchini.
  Wajumba wa Kamati ya Uongozi ya Bunge wakimsikiliza Waziri Mkuu kwa umakini mkubwa alipokuwa akitanabaisha jinsi Serikali isivyopendezwa na mauaji ya Kiteto na jinsi ilivyojipanga kukomesha kabisa mauji hayo.
  Naibu Spika na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwa jinsi walivyozungumza na Mhe, Waziri Mkuu kwa moyo wa kizalendo kwa nchi yao.
  Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah (kushoto) akitoa ushauri kwenye Kamati ya Uongozi jinsi ya kuwasilishwa Bungeni taarifa za Tume mbalimbali leo. Picha na Prosper Minja-Bunge

  0 0

  Wanachama wa Jumiya ya Watu wanaoishi na maradhi ya kisukari Zanzibar na wafanyakazi wa kitengo cha maradhi hayo kutoka Hospitali Kuu ya Mnazimmoja wakiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya kisukari Duniani yaliyoanzia viwanja vya Maisara na kumalia viwanja vya Malindi Novemba 14.
  Wanachama wa Jumuiya hiyo wakionyesha bango lenye ujumbe mahasusi wa kimataifa wa siku ya kisukari Duniani katika maandamano ya kuadhimisha siku hiyo Novemba 14.
  Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (suti nyeusi) akiyapokea maandamano ya wanajumuiya ya watu wanaoishi na maradhi ya kisukari Zanzibar katika viwanja vya Malindi Mjini Zanzibar.Picha na Makame Maelezo Zanzibar.

  0 0

  1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivalishwa Skafu na vijana na wa Chipukizi wakati alipowasili eneo la Somanga wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi akianza ziara yake ya siku 16 katika mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza sughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi, Katibu Mkuu huyo anaongozana naNape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi pamoja na Mjumbe wa NEC mkoa wa Lindi na Mbunge jimbo la Mtama Mh. Bernald Membe.3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kilwa na Mkoa wa Lindi waliofika katika eneo la Somanga kwa ajili ya mapokezi Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliofika kumpokea katika eneo la Somanga wilayani Kilwa kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. 


  0 0


  Here is your chance to be the star among the Developer community and win great prizes including super cool gadgets and an all paid trip to Mobile World Congress, Barcelona, Spain.
  Vodacom App Star is open to all developers that meet the criteria below:
  • Local relevance – the App submitted should be designed to meet local market consumer needs and be relevant to the target demographic social challenges
  • Innovation – the App submitted should be unique, in terms of functionality or purpose and should utilise current device functionality
  • Quality – the App submitted should be produced to high quality, fully functional with minimal errors and would provide a simple and easy to use user experience
  • Business Viability – the App submitted should be suitable as a start-up application that could be profitable and sustainable
  • Submit your idea now here (http://vodacomappstar.com/), before the 25th of November 2014. 

  0 0


  Greetings from the Slipway Cinema Studio, 
  welcome to this months screenings and schedule....

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh Hawa Ghasia na Mwenyekiti wa Bodi ya Watumishi Housing Company (WHC) Bw. Adam Mayingu wakishuhudia Dr Cyiprian Mpemba (CEO- KEC) na Dr Fred Matola Msemwa (CEO- WHC) wakitia saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya WHC na Kibaha Education Centre(KEC)   ambapo KEC itatoa ardhi kwa ujenzi wa nyumba 1150 za watumishi wa umma katika eneo la Mailimoja mjini Kibaha.Waliosimama kusho ni Mwanasheria wa WHC Bw Joel Maeda. Hafla hiyo imefanyika  jijini Dar- Es - Salaam.

  0 0
 • 11/15/14--19:30: KUMBUKUMBU
 • BIBIANA (NKAMALI) PETER BASI KWEKA

  Bibi yangu mpendwa na somo wangu pia.Leo umetimiza miaka 13 tangu ulipoitwa mbinguni kwa BABA. Hatuna cha kusema,tumebaki kushukuru tuu kwani hata miaka ulioishi ilizidi ile ya Upendeleo.

  Tunakumbuka uzuri wako,Ucheshi,Usafi na Ufanyakazi wako bila kusahau jina lako (BIBI SHAMBA). Kweli ulikuwa mfano wa kuigwa  unakumbukwa sana na mimi somo wako JANE,WAJUKUU WOTE WA KWA BASI,MTOTO WAKO WA PEKEE ALIYEBAKI DUNIANI SR.DEVOTA KWEKA CDNK, WA KWEKA WOTE WA NARUMU,WA –ULOMI WOTE WA USWAA,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI ,MISA YA KUMUOMBEA ITAKUWA NYUMBANI KWAKE NARUMU TAREHE 01/01/2015
  , WOTE MNAKARIBISHWA
  RAHA YA MILELE UMPE Ee BWANA


  0 0
 • 11/15/14--19:56: biashara matangazo


 • 0 0


  I Will Survive by Gloria Gaynor

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi wa kwanza kulia akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo barabara ya soko jipya Bagamoyo mjini mwishoni mwa wiki.Wengine katika picha katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia.
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi wa pili toka kushoto akifungua mvinyo(shampeni) kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo barabara ya soko jipya Bagamoyo mjini mwishoni mwa wiki.Wengine kushoto ni Mmiliki wa duka hilo Simon Mwambapa na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia.
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi wa pili toka kushoto,Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(kushoto) Mmiliki wa duka hilo Simon Mwambapa wa tatu toka kushoto na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Rosalynn Mworia wakigonganisha glasi zenye mvinyo kuashiria isharia uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo barabara ya Bagamoyo mjini mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(katika)akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi(kulia) kabla ya kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo barabara ya soko jipya Bagamoyo mjini mwishoni mwa wiki na Kushoto ni Meneja Masoko wa kanda ya Pwani Florantina Urio.
  Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo barabara ya soko jipya mjini Bagamoyo.

older | 1 | .... | 641 | 642 | (Page 643) | 644 | 645 | .... | 3284 | newer