Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 643 | 644 | (Page 645) | 646 | 647 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kushoto akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki Meli kubwa ya mizigo iliyobeba Kivuko kipya cha MV Dar es Salaam ilipokuwa inakaribia kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam.
  Taaswira ya Kivuko cha MV Dar es Salaam kama kinavyoonekana juu ya Meli kabla ya kushushwa majini katika bandari ya Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akionesha furaha yake ndani ya Kivuko hicho cha MV Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki kulia akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka TEMESA Eng. Japhet Masele kuhusu vitu mbalimbali ndani ya Kivuko hicho cha MV Dar es Salaam.


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa kauli kuhusu mgogoro wa wakulima na wafugaji wilayani Kiteto , Bungeni mjini Dodoma Novembe 17, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Fedha,Saada Mkuya (kulia) na Naibu wake, Mwigulu Lameck Nchemba kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 17, 2014.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dr, Florance Turuka kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 17, 2014. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Juliet Kairuki.
  Waziri wa Fedha, Saada Mkuya (kushoto) akizungumza na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dr, Florance Turuka kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 17, 2014. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Juliet Kairuki.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanafunzi wa shule ya rwekiza ya Bukoba Vijijini kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 17, 2014. Kulia kwake ni Mbunge wa Bukoba Vijijini na mmiliki wa Shule hiyo, Jasson Rwekiza.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dr. Florance Turuka (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanznaia (TIC), Juliet Kairuki kutoka wenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Novemba 17, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  0 0

  Ecobank, the leading pan-African banking group, has joined forces with the African Guarantee Fund, the first continent-wide guarantee fund, and AfricSearch, the recruitment firm, in co-hosting the first Africa Champions’ Forum in Senegal. This forum brings together leading lights from the private sector and development agencies, together with influential political decision-makers, all united around a single cause: to promote the growth of the continent by providing finance and advisory services to Africa’s emerging small and medium enterprise (‘SME’) champions. 

  The objective of the forum is to enable some 300 SME leaders, from the five regions of Africa, to interact with more than 100 representatives of reputable financial institutions and around 50 small business consultants. The forum also aims to celebrate the achievements of Africa’s finest entrepreneurs, and the leading financial institutions that support them, by presenting awards in the following categories:

  SME of the Year
  Regional Development Prize 
  Young Entrepreneur Of the Year
  Best SME Bank

  SMEs were invited to make award submissions, provided that they met the following criteria: a minimum of 3 years of legal existence, with at least 10 full-time or equivalent employees and a turnover of between USD 250,000 and USD 15 million. 
  Mr. Albert Essien, Ecobank’s Group CEO, commented: “The private sector and, in particular, SMEs are the lifeblood of any economy. SMEs are also the largest providers of direct employment, so it is important to support Africa-wide initiatives to drive their development, thereby deepening financial inclusion. Ecobank is delighted to be able to bring together private and public institutions in such a way to maximize the impact of the Africa Champions’ Forum.”

  Patrick Akinwuntan, Ecobank’s Group Executive for Domestic Bank, added: “Supporting SMEs is in line with our vision of contributing positively to Africa’s development. In addition to providing access to finance through credit facilities, collections, trade and cash management products and services, Ecobank also provides significant access to market to SMEs through our unparalleled network of multinational and large corporates across 36 countries in Africa.”

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akitoa hotuba ya ufunguzi wa   Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili kuhusu Sauti ya Kwanza ya Sayansi ya Jamii. Mkutano  huo ambao unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani  chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unawashirikisha Wajumbe kutoka  Tanzania, Kenya, Uganda, Ghana, Nigeria na Canada. Katika hotuba yake Mhe. Membe alisisitiza umuhimu wa Wasomi na Wanazuoni kujikita katika Tafiti za Kisayansi ili kuja na majibu yatakayoisaidia nchi kuondokana na umaskini, utunzaji wa mazingira na masuala mengine ya manufaa kwa nchi.
  Mhe. Membe akikaribishwa na Prof. Florence Luoga ambaye ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili kuhusu Sauti ya Kwanza ya Sayansi ya Jamii  ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
  Mhe. Membe akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mkutano huo
  JUU NA CHINI: Ni sehemu ya Wajumbe wakifuatilia mkutano huo kuhusu masuala ya Sayansi ya Jamii.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Mkurugenzi wa Shule za St Mary's, mama Getrude Lwakatare akizungumza na wanafunzi wa Shule za St Mary's International za Dar es Salaam wakati akizundua tamasha la kuonyesha vipaji vya wanafunzi wa Shule za St Mary's International za Dar es Salaam lililofanyika mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.PICHA NA PHILEMON SOLOMON
   Mkurugenzi wa Shule za St Mary's, mama Getrude Lwakatare (kushoto), akikabidhiwa baadhi ya Peni na Meneja Masoko wa Kampuni ya SILAFRICA, Salman Pathan kama mchango wake kwaajiliya shule za St Mary's International.
   Wanafunzi kutoka shule za St Mary's International za Dar es Salaam wakitoa burudani wakati wa tamasha la kuonyesha vipaji.
    Mkurugenzi wa Shule za St Mary's, mama Getrude Lwakatare (wakwanza kulia), akiwa na Walimu wa shule hizo wakifuatilia burudani wakati wa tamasha hilo.
   Wanafunzi kutoka shule za St Mary's International za Dar es Salaam wakiwa kwenye tamasha hilo.

  0 0
 • 11/17/14--12:35: the isumba shout this week..
 • Wanaotambua good music wanajua kuwa unapatikana ndani ya isumba lounge (jollies club) kila ijumaa na jumamosi; chini ya usimamazi wa DJ JOHN DILLINGA na DJ FAST EDDIE doors open 9pm entry 10. Karibu na wewe tule oldies, old scul, soca rumba, charanga, chacha na nyingine kibao.

  0 0


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Milola jimbo la Mchinga ambapo aliwaambia wapinzani wamekosa sera mbadala matokeo yake wamekuwa wakitumia muda mwingi kuishambulia CCM
   Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ,Mbunge wa Jimbo la Mtama na mlezi wa wilaya Kilwa na Waziri wa Mambo ya Nje Ndugu Bernard Membe akiwasalimia wakazi wa Milola waliojitokeza kwa wingi kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman.
   Sehemu ya wananchi wakifuatilia mkutano.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye pich ya pamoja baada ya kuwakabidhi vyeti vya kuhitimu mafunzo ya kuendesha boda boda.
  Wananchi wa Milola wakiomba kupatiwa kad za uananchama wa CCM kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana.

  0 0

  Marehemu Omar Ndege Mgori
  Familia ya  Mzee Ndege inatoa shukurani nyingi kwa ndugu, jamaa marafiki ma majirani waliokuwa nao bega kwa bega tokea ndugu yao mpendwa Marehemu Omar Ndege Mgori kilichotokea mwezi wa jana huko  India  na hatimaye kuzikwa  siku ya jumatatu Oktoba 13, 2014 kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Familia inasema haina cha kuwalipa zaidi ya  AHSANTE SANA na kumuomba Mola awajazie pale palipopungua.

  Dua maalumu ya kumuombea Marehemu Omar Ndege Mgori imepangwa kufanyika  siku ya tarehe 23 mwezi huu, huko Mbezi  jijini Dar es salaam nyumbani kwa marehemu  kuanzia saa sita mchana. Familia inawakaribisha ndugu, jamaa, marafiki na majirano wote siku hiyo  0 0


  Vijana kutoka Tanzania.(Picha ya UNFPA/Tanzania
  Tarehe 18 Novemba kila mwaka ni siku ya kimataifa ya idadi ya watu. Siku hii hutumiwa kufahamu idadi ya watu duniani na  huku takwimu hizo zikitumiwa kupanga  mikakati ya ustawi wa watu  duniani kote. Maudhui ya siku hiyo mwaka huu ni ustawi wa vijana kundi ambalo ni nguvu kazi katika jamii.
  Shirika la idadi ya watu duniani UNFPA ndilo linaloratibu kazi hiyo ambapo nchini Tanzania shirika hilo hilo linatarajia kuitumia siku hiyo kuwanufaisha vijana. Katika mahojiano na afisa mawasiliano wa UNFPA Tanzania Sawiche Wamunza, afisa wa idadi ya watu na maendeleo
   Samweli Msokwa anaanza kwa kueleza kauli mbiu ya siku hiyo.
  (SAUTI MAHOJIANO)
  Kusikiliza bofya hapa

  0 0


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu waTanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake walipomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  

  Jaji Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya rufani Mhe Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi,daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama
  Mhe Hussein Katanga.

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.
   Rais Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York 
  Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge, jana jumatatu, imeanza mkutano wake wa pili na wa siku mbili unaofanyika hapa Umoja wa Mataifa. 
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda ( Mb) ni miongoni mwa washiriki wa Kamati hiyo ya Maandalizi ukiwahusisha maspika kadhaa kutoka mabunge mbalimbali duniani.
  Katika mkutano huo wa siku mbili ambao umeandaliwa na Inter-Parliamentary Union ( IPU), wajumbe wa kamati hiyo wanajadili mapendekezo ya Maudhui na Tamko la Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge unaotarajiwa kufanyika mwaka 2015. 
  Aidha wajumbe hao wanatarajiwa pia katika siku mbili hizi kutoa uamuzi wapi kutakakofanyikia mkutano huo. 
  Maudhui na Tamko la mkutano huo wa Nne pamoja na mambo mengine yanatarajiwa kuwa yatazingatia vipaumbele au mambo muhimu na ya msingi ya mahitajo ya mwanadamu katika dunia ya sasa. 
   Mambo ambayo pia ni ajenda muhimu katika Umoja wa Mataifa Baadhi ya mambo hayo na ambayo wajumbe wa kamati ya Maandalizi wanayapitia ni pamoja na, tathimini ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs), Mapokeo ya Agenda Mpya za Maendeleo Endelevu baada ya 2015, na maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa wa Umoja wa Mataifa. 
  Katika siku ya kwanza ya mkutano wao wajumbe wamesikiliza thathmini ya utekelezaji wa MDGs, tathmini iliyotolewa na Spika wa Bunge la Iceland ambaye ameainisha mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa malengo hayo ambayo yanafikia ukingoni mwakani. 
  Pamoja na kusikiliza tathimini ya MDGs, Maspika hao pia wamepata fursa ya kubadilishana mawazo na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja anayehusika na SDGs, 
   Bi Amina Mohammed ambaye ametoa muhtasari wa ajenda na malengo mapya ya SDGs baada ya 2015. Katika maelezo yake Bi Amina ametilia mkazo ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa, Serikali na nafasi ya Mabunge katika utekelezaji wa SDGs huku akisisitiza kwamba changamoto kubwa na muhimu katika utekelezaji wa SDGs hizo ni suala na uwezeshaji wa raslimali fedha, suala ambalo amesema linahitaji ushirikiano wa pamoja katika kulipatia muelekeo wake. 
  Aidha amewaeleza wajumbe wa Kamati kuwa Maspika na wabunge katika kila Bunge duniani kote wanapashwa kuwa weledi na wenye ufahamu mkubwa kuhusu SDGs yenye ajenda 17 na malengo 169 kwa kuwa wao ndio wawakilishi halisi wa wananchi waliowachagua. 
   Akasisitiza kuwa wabunge wanapashwa kushirikiana kikamilifu na serikali katika utekelezaji wa SDGs na huku au kubemba ujumbe wa mambo muhimu na ya msingi kwa mahitajimasuala ambayo ni muhimu kwa maisha yana Maspika kadhaa ambao ni wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabungo utaofanyika mwakani.
   Mhe. Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda ( Mb) akifuatilia majadiliano yaMkutano wa  Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Dunia wa Maspika wa Mabunge, Mkutano  huu wa siku mbili unafanyika hapa Umoja wa Mataifa.
   Mhe. Spika akibadilisha mawazo na   viongozi wa IPU
    Mhe. Spika akisalimiana na  Spika wa Bunge la India
  Mhe, Spika  Anne Makinda akisalimia kwa furaha na  Spika wa Bunge la Uruguay

  0 0  0 0  0 0


  Toni Braxton - Breathe Again

  0 0

  Picha ya pamoja, Baadhi ya wana kikundi cha UWF, mwakilishi kutoka Tanzania Women Bank (TWB), Bi Khadija na Baadhi ya washindi wa mradi huo wa Mwanamakuka tangu mwaka 2012 wakiwa katika picha pamoja.
   Pichani kulia ni Mwenyekiti wa UWF na Meneja Mradi wa Mwanamakuka,Bi.Maryam Shamo, akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) Mikocheni jijini Dar,mwishoni mwa wiki,kuhusiana na hafla fupi ya kumkumbuka Marehemu Aziza Mbogolume,ambaye alikuwa mshindi wa kwanza wa shindano la MWANAMAKUKA 2013.
  Shindano hilo huandaliwa na kikundi cha UNITY OF WOMEN FRIENDS (UWF),kupitia mradi wao wa MWANAMAKUKA, hafla hiyo pia iliwakutanisha wadau mbalimbali wa kikundi hicho wakiwemo na washindi wa mradi huo ambao umekuwa ukifanya vyema kila mwaka,Anaefutia pichani ni Bi Jane Magembe, , Mwate Madinda na Martha Kalaghe. 
  Mwenyekiti wa UWF na Meneja Mradi wa Mwanamakuka,Bi.Maryam Shamo,akionesha moja ya, kipaji cha marehemu Aziza, ambacho kilikuwa ni uchoraji.
   Baadhi ya washindi wa mradi huo wa Mwanamakuka tangu mwaka 2012 wakijadiliana jambo,ambapo walikukutana kwa madhumuni ya kumkumbuka Mwanamakuka mwenzao aliyefariki. 


  0 0

   Meneja wa Airtel Simiyu Bw. Ezekiel Nungwi akikabidhi msaada wa vitabu vya sayansi kwa Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima.
   Mkuu wa shule ya sekondari ya Bariadi Bw. Pawa Lutema akipokea msaada wa vitabu vya sayansi kutoka kwa mkuu wa wilaya Bariadi.
   Mkuu wa wilaya ya  Bariad Bw. Erasto Sima akisoma Hotuba katika makabidhiano ya msaada wa vitabu vya masomi ya sayansi kwa shule ya sekondari Bariadi uliotolewa na kampuni ya Airtel Tanzania

  ========  =======  ========
  Airtel Yaendelea Kusaidia Sekta ya Elimu hapa Nchini
  ·       Shule ya Sekondari Bariadi yanufaika na msaada huo

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imepiga jeki jitihada za serikali za kuhamasisha masomo ya sayansi kwa kutoa msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule ya sekondari ya Bariadi iliyopo Mkoani Simiyu.

  Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 1.5 unahusisha vitabu vya fizikia, hisabati, baiolojia na kemia kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo shuleni hapo.

  Akipokea msaada huo mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima amesema shule nyingi wilayani hamo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitabu vya masomo ya sayansi licha ya kwamba kuna uhaba pia wa walimu wa masomo hayo.

  “Ni kweli kwamba uhaba wa vitabu unakwamisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi kujifunza kwa ufasaha masomo ya Sayansi wilayani Bariadi hali inayorudisha nyuma ukuaji wa elimu ya sayansi wilayani hapa”. Alisema Bwana Sima.

  “uhaba wa vitabu ni moja ya changamoto, lakini uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ni kikwazo kikubwa kwa utoaji wa elimu ya sayansi kwa wanafunzi wetu hapa Bariadi” aliongeza Bwana Sima.

   Aidha Bw. Sima ameishukuru kampuni ya simu ya airtel  kwa kuona umuhimu wa kuboresha masomo ya sayansi ambayo  ufaulu wake umekuwa mdogo hali ambayo inayotoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa umakini zaidi.

  “Msaada huu utaongeza hamasa kwa wanafunzi wetu kujifunza masomo ya sayansi hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kuona umuhimu wa kusaidia shule hii na hasa vitabu vya sayansi” alimalizia Bwana Sima.

  Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekonderi Bariadi Bw. Pawa  Lutema akipokea vitabu hivyo, amesema hatua hiyo ni sehemu ya utatuzi wa changamoto ya vitabu vya sayansi na kisha kuahidi kuvitunza ili viwe msaada kwa wanafunzi watakaosoma shuleni hapo.

   Awali  meneja wa Airtel Mkoani Simiyu Bw. Ezekiel Nungwi  akikabidhi  msaada huo wa vitabu  amesema kuwa kampuni yake inaendelea na mpango wake wa kutoa msaada wa vitabu kwenye shule mbalimbali nchini kwa lengo la kusaidia ukuaji wa elimu nchini.

  Msaada huo wa vitabu vya masomo ya hisabati,kemia,fizikia na Bailojia utasaidia kupunguza uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye shule hiyo.
    

  0 0

      Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza (Kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii wa batiki yaliyoanza mapema wiki hii kwenye Ofisi za Baraza hilo zilizoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni  Bi. Leah Ruhimbi
       Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla akiongea na Wasanii (hawako pichani) waliohudhuria kwenye mafunzo ya wiki moja ya utengenezaji batiki yanayoandaliwa na kituo chake kwa kushirikiana na BASATA na kufanyika makao makuu ya BASATA. Mwingine katika picha ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi. Leah Ruhimbi
        Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi. Leah Ruhimbi akifungua mafunzo ya utengenezaji batiki kwa wasanii wa Sanaa za Ufundi yanayofanyika kwa wiki moja makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba. Wengine kutoka kulia ni  Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka BASATA Bi. Vivian Shalua na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ujereum Bi. Eleonore Sylla
      Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Sanaa kutoka BASATA Bi. Vivian Shalua akiwaelekeza jambo wasanii wanaoshiriki mafunzo ya utengenezaji batiki
  Sehemu ya Wasanii wa utengenezaji batiki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo. Picha, habari na Aristide Kwizela-Afisa Habari BASATA


  ======  ======  ======== =====
  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Ujeruman maarufu kama Goeth Insitut wameendesha mafunzo ya utengenezaji batiki kwa wasanii wa Sanaa za mikono yanayofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA jijini Dar es Salaam.

  Mafunzo hayo yanayotazamiwa kudumu kwa siku tano yaani kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa yanalenga kuongeza ubunifu na weledi miongoni mwa wasanii wa Sanaa za mikono ili kuongeza ubora na tija katika uzalishaji.  

  Mapema akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Leah Ruhimbi alisema kwamba mafunzo hayo yatasaidia kuongeza tija kwa wasanii hao na kuwawezesha kubuni Sanaa zenye ubora zitakazopenya masoko mbalimbali ya Sanaa.“Ni matarajio ya BASATA na wizara kwamba mafunzo haya yatakuwa yenye tija kwa wasanii na yatawawezesha kusambaza ubunifu na uzoefu kwa wasanii wengine nchini. Lengo ni kuwa na sanaa zenye ubunifu na ubora” alisisitiza.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Goeth Institut Bi. Eleonore Sylla alisema kwamba mafunzo hayo yanahusisha wasanii wenye uwezo wa kutengeneza batiki na lengo kuu ni kuwaweka pamoja ili wachangie uzoefu na baadaye kutengeneza batiki zenye ubora zaidi.“Tunajua mnatoka sehemu mbalimbali nchini na wote mna uzoefu katika utengenezaji wa batiki lakini kuwa kwenu pamoja kwenye mafunzo haya kutawafanya mpate uzoefu zaidi na hatimaye kubuni batiki zenye ubora” aliongeza Sylla.
  Naye Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza alisema kwamba BASATA kwa kushirikiana na Goeth Insitut wameona kwamba kuna haja ya mafunzo hayo ya wasanii na kwamba baraza litaendelea kuboresha ubora wa kazi za Wasanii kupitia kuwajengea uwezo.

older | 1 | .... | 643 | 644 | (Page 645) | 646 | 647 | .... | 3284 | newer