Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 634 | 635 | (Page 636) | 637 | 638 | .... | 3348 | newer

  0 0

   Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi na WanaCCM wa Mikoa ya Pemba katika Uwanja wa Gombani ya Kale Kisiwani Pemba leo

  Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha Katiba Iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba zungumza na wananchi na WanaCCM wa Mikoa ya Pemba katika Uwanja wa Gombani ya Kale Kisiwani Pemba leo.(Picha na Ikulu.)
   Wananchi wa kisiwani Pemba wakiwa katika mkutano wa CCM uliofanyika katika uwanja gombani Wila ya Chake chake Pembe
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (wa tatu kushoto) Makamo wa Pili wa Rais pia Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC Balozi Seif Ali Iddi,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Abdalla mohamed  Mshindo na Mke wa  Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mama Asha Balozi wakiwa katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika uwanja Gombani ya kale Kisiwani Pemba leo.

   Wananchi wa kisiwani Pemba wakiwa katika mkutano wa CCM uliofanyika katika uwanja gombani Wila ya Chake chake Pembe


  0 0

  Winners of Miss Universe Tanzania 2014 Nale, Carolyne and Zara

  0 0

  Our initiative recognises the significant strides that have been made with Bongo Movies agencies; yet recognise the gaps that exist. 
  Most of Tanzania movies describe issues on family matters mostly from low class and traditional societies, with little focus on question of modern power, politics, and complexity of social relations, of which make moving images interesting. 
  "ONE MONTH DATE" is our first movie to launch our initiative. This movie is about the changing structure of family and marriage in urban spaces of Tanzania. Of recent, there have been an increase of divorce rates and birth of children out of wedlock. 
  This has resulted to increase of single parenting phenomena . The movie is written to tease out relationship issues and society values in communities aiming to address society biases toward single parenting and re-marriage . 
   We are proud to announce that the production of  the movie has come to an end. Now we are ready to put it on screen. The launch is scheduled for 5th December, 2014 at  The New Century Cinemax  at Mlimani City in Dar es salaam on 5th December 2014. 

  Thank you and Karibuni wote

  Paul R.K Mashauri 
  Off: Mikocheni B Area, 
  Plot # 320, 
  Off Old Bagamoyo Road Dar es Salaam 
  +255 2700051 
  +255 717 653544/684005839 
  mashauri@eastafricaspeakers.net 
  mashauri@printmediatz.com

  0 0
 • 11/08/14--14:34: ngoma azipendazo ankal

 • Mayaula Mayoni - Mbongo 

  0 0

  Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM ambaye ni mlezi wa Mkoa wa Simiyu,Mh. Jerry Silaa ameanza ziara ya siku kumi katika Mkoa huo wa Simiyu,ambapo ziara yake hiyo ameianzia wilayani Busega kwenye kata za Lamadi ,Kiloleli na Kabita ambapo ameongea na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) toka ngazi ya shina hadi wilaya.
  Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM ambaye ni mlezi wa Mkoa wa Simiyu,Mh. Jerry Silaa akiwa na baadhi ya viongozi wa CCM wilayani hapo.
  Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM ambaye ni mlezi wa Mkoa wa Simiyu,Mh. Jerry Silaa akunzungumza katika moja ya mkutano wake na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) toka ngazi ya shina hadi wilaya.
  Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM ambaye ni mlezi wa Mkoa wa Simiyu,Mh. Jerry Silaa akisalimiana na wazee wa Simiyu.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 7, 2014 katika tafrija ya kumpongeza Spika kwa kuteuliwa kuwa Rais wa Mabunge ya SADEC iliyofanyika mjini Dodoma. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Anna Abdallah na watatu kulia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki.
  Spika wa Bunge, Mh. Anne Makinda akipongezwa na Mbunge wa Viti Maalum Mh. Anna Abdallah  katika tafrija ya kumpongeza Spika kwa kuteuliwa kuwa Rais wa Mabunge ya SADEC iliyofanyika mjini Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda  na watatu kulia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge Anne Makinda (kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa katiba na Sheria, Angela Kairuki (katikati) alipotoa maelezo kuhusu zawadi ya picha ambayo wabunge walimzawadia Spika Makinda katika tafrija ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa spika wa Mabunge ya SADEC iliyofanyia kwenye viwanja vya Bunge mjioni Dodoma Novemba 7, 2014.

  0 0

  Mr Yussuf M. Hassan, the new Manager of Zacadia.
  October 8, 2014.
  The Board of Trustees (BoT) of ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association) is pleased to announce that Mr Yussuf M. Hassan (above) is the new Manager of the Organization. This was the result of the Board’s scrutiny of three applicants during its third meeting since it dissolved the Management Team.

  In his new role as the Manager, Mr Yussuf will be responsible and accountable for providing an able leadership while ensuring proper execution of day to day activities in order to achieve all of Zacadia’s operating objectives, promote a positive Zanzibari culture of “TUPO PAMOJA working toward the same goal”and ensure the welfare of all Zanzibaris living in Canada through the adherence of the fact that we are all NDUGU and that  UMOJA NI NGUVU.

  Yussuf is tasked to manage Zacadia as one high performing team, where respectful, open, positive and dynamic dialogue prevail and members’ ideas and advice are listened to, followed-up on and acted upon as appropriate.

  Yussuf brings to Zacadia progressive growth and rich experience from his career, working and volunteering in a variety of roles which consisted of, University of Toronto Settlement Program Assistant, Legal Assistant with Etienne Law Office (Toronto),  Interpreter with Immigration and Refugee Board of Toronto, Resource Centre Assistant with OASIS Employment Centre in Toronto, and most recently as Engagement & Outreach Assistant with Action  For Neighbourhood Change.

  He holds a Bachelor of Art (BA) degree in Human Rights and Equity Studiesand has just received a Certificate in Public Policy and Law  from the University of York.

  Please join the BoT of Zacadia in congratulating and welcoming aboard Mr Yussuf Hassan. Let’s all give him our genuine support in his new role in our Organization.

  With the Manager in place, BoT is now calling for Zanzibaris living in Canada to apply for the vacant Directors’ positions for the different  Directorates which have been streamlined to three: 
  [1] Directorate of Education; 
  [2] Directorate of Women, Children and the Disabled, and
  [3] Directorate of Business Development.

  Last date to receive the applications is November 21, 2014. 

  All applications to be addressed to: 
  The Secretary, 
  Zacadia, 
  email address:
  <secrzacadia@gmail.com>

  0 0

   Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akichuana na beki wa Mgambo Shooting, Bushiru Mohamed katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
  Golikipa wa Ruvu Shooting, Said Lubawa akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam.

  Andrey Coutinho akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Mgambo.
  Mrisho Ngasa (kulia) akimtoka Bushiru Mohamed.
  Simon Msuva akimiliki mpira mbele ya beki wa Mgambo shooting.
   Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli lililofungwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Simon Msuva wakati timu hiyo ilipopambana na Mgambo Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
   Mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akimtoka, mchezaji wa Mgambo Shooting, Ally Idd katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema inahitajika dhamira ya kweli kutoka kwa wadau wote katika kutekeleza Azimio la Arusha la kukabiliana na ujangili na kuendeleza hifadhi za wanyama katika nchi za Afrika Mashariki na zilizo Kusini mwa Ikweta.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni (Jumamosi, Novemba 8, 2014) mara baada ya kufunga mkutano wa kikanda wa siku mbili uliojadili mbinu za kupambana na biashara haramu ya wanyamapori ulioandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Arusha, Waziri Mkuu alisema: “Suala hili linataka uwajibikaji wa pamoja. Mashirika na taasisi, wananchi na viongozi sote kama wadau wakuu, kila mmoja anapaswa kushiriki vita hii kama kweli tunataka tuitokomeze.”

  “Kwenye hili Azimio la Arusha na nyie waaandishi wa habari pia mna sehemu yenu mmetajwa... wamesema wanatafuta jinsi ya kushirikiana na vyombo vya habari ili visaidie kutoa elimu kwa jamii kama njia ya kuelimisha umma,” alisema.

  Waziri Mkuu aliwaeleza waandishi hao kwamba Azimio hilo lina vipengele 20 ambavyo vinataka utekelezaji katika ngazi ya nchi mojamoja, ngazi na kanda na ngazi ya kimataifa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.

  “Nimepata faraja kwamba mkutano huu haukuisha kijumlajumla tu, bali umekuja na maazimio 20 ambayo yametengwa kwa ajili yetu sisi wa ndani, mengine yanahusisha ushirikiano wa kikanda na yako mengine yanawahusisha wadau wa maendeleo,” alifafanua.

  Ili kutekeleza azimio hili, nimeshauri iundwe timu itakayoshirikisha vyombo vingi zaidi badala ya kuiachia Wizara ya Maliasili na Utalii peke yake. Timu hii ikutane kila baada ya miezi sita ili kufuatilia utekelezaji wa maazimio haya na ikibidi Waziri atoe taarifa bungeni kuhusu utekelezaji huo,” alisema Waziri Mkuu.

  Mapema, akizungumza na washiriki wa mkutano huo wakati wa kuufunga, Waziri Mkuu alisema kuwepo kwa watu wa ngazi tofauti kwenye mkutano huo ni kielelezo tosha cha umakini wao na nia thabiti ya kutokomeza ujangili katika ukanda huu.

  “Tumeanzisha vita, tusisahau kwamba bado kuna kazi kubwa mbele yetu na vita haijaisha. Tuzidishe mapambano katika sehemu tatu: kwenye nchi unakofanyika ujangili, nchi ambazo nyara zinapitishwa na nchi zinazopokea ama kununua hizo nyara,” alisema Waziri Mkuu.

  “Nakubaliana nanyi kwamba hakuna nchi inayoweza kukabili suala la ujangili ikiwa peke yake. Tunahitaji tuwe na sera mahsusi, sera ya pamoja ya kutuunganisha na kutuongoza wakati tukitekeleza Azimio hili kwa kusaidiana na wadau wa maendeleo,” alisema.

  Alisema Azimio hilo litaipa kazi ya ziada ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo kazi kubwa itakuwa ni kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wa wa Azimio hilo unakuwa wa ufanisi.

  Jumla ya nchi tisa zimetia saini azimio hilo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Nchi hizo ni Burundi, Kenya, Uganda, Msumbiji, Tanzania, Sudan Kusini, Zambia, Rwanda na Malawi.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha ambako alifunga Mkutano wa kupiga vita ujangili wa wanayamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori uliofanyika mjini Arusha Novemba 8, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wapili kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aggrey Mwanri (kulia) baada ya kufunga Mkutano wa kupiga vita ujangili wa wanayamapori na kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori mjini Arusha Novemba 8, 2014. Kushoto ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli.Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Dkt Richard Sezibara(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Embedded image permalink
  Gazeti la The Citizen la Tanzania linamwita 'lulu iliyofichika' hidden gem, kwa kimombo). Huyu ni Leo Mkamia, msanii wa Kitanzania na mwanzilishi wa aina ya muziki ujulikanao kama 'Swahili Blues.'

  Siku chache zilizopita, Leo alirekodi wimbo wake mpya uitwao 'Pamoja.' Miongoni mwa yatakayoonekana katika video ya wimbo huo ni performance ya kihistoria ya msanii huyo katika moja ya vyuo vikuu vikubwa hapa Uingereza, Nottingham University, ambapo Leo alifanikiwa kuwaimbisha Kiswahili baadhi ya wahadhiri na wanafunzi wa chuo hicho kikuu. Katika shughuli hiyo, Leo aliimba na kwaya ya Nottingham Academy.

  Kinachomfanya Leo kuwa msanii wa kipekee kutoka Tanzania kuwa na fursa kubwa ya kutawala anga za muziki kimataifa ni ukweli kwamba amefanikiwa kuanzisha kitu kipya- muziki aina ya Swahili Blues- na ambao tayari umeanza kukubalika kimataifa.

  Mtaji mkubwa wa Leo ni ukweli kwamba anatoka familia ya muziki.Unamkumbuka mkongwe wa gitaa Henry Mkanyika? Basi huyo ni baba mzazi wa Leo, ambaye alianza kucharaza gitaa akiwa na umri wa miaka minane tu.

   

  Kwa sasa Leo ni miongoni mwa wasanii wachache mno, sio tu wa Tanzania, bali Afrika nzima kwa ujumla, ambao sura na sauti zao sasa 'zimezoeleka kwenye vituo vya radio na televisheni vya kimataifa kama BBC. Na katika kuthibitisha hjilo, Leo alihojiwa na BBC mara baadha ya performance hiyo ya kihistoria huko Nottingham.  Pamoja na kufanya vizuri kimataifa, Leo bado anathamini asili yake. Kama video ya pili inavyoonyesha, Leo alifanya mahojiano na mtandao mkubwa na maarufu wa burudani Tanzania na Afrika kwa ujumla wa Bongo5. Kadhalika, msanii huyo anapata sapoti kubwa kutoka kwa mmoja wa waasisi wa muziki wa Hip-Hop nchini Tanzania, lejendari @XamiaSiku4Saa4 wa kundi maarufu kabisa la Kwanza Unit. Ieleweke kwamba katika shughuli za muziki, kupata 'endorsement' ya mkongwe wa muziki ni uthibitisho kuwa msanii husika anafanya kazi nzuri mno.
  Kama Watanzania, tuna wajibu na kila sababu ya kumuunga mkono Leo, kwani sio tu anaitangza Tanzania yetu bali pia anautambulisha utamaduni wetu-kwa maana ya lugha ya Kiswahili- kupitia muziki wake wa Swahili Blues.
  Unaweza kufuatilia maendeleo yake ya kimuziki kwa akaunti zake mbalimbali za mitandao ya kijamii: Twitter na Facebook  na katika tovuti yake sambamba na ukurasa wake wa YouTube

  0 0

  KIUNGO mkabaji wa Azam FC, Salum Abubakar”Sure Boy”aliyeibuka Mchezaji Bora wa Oktoba juzi alikabidhiwa zawadi ya shilingi milioni 1/= na kombe dogo 
  Makabidhiano hayo yalifanyika muda mfupi kabla ya mechi ya raundi ya saba kati ya mabingwa watetezi Azam FC na Costal Union katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyochezwa nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam katika uwanja wa Chamanzi, ambapo Azam FC waliichapa Coastal Union 2-1. 
  Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam juzi,Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema kampuni yake itakuwa ikitoa zawadi kila mwezi kwa mchezaji anayefanya vizuri.
   “Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu ina ushindani mkubwa, nasi (Vodacom Tanzania) kwa kushirikiana Bodi ya Ligi (TPLB) tumejipanga vizuri tutakuwa tunatoa zawadi kwa mchezaji anayeng’ara kila mwezi na mwezi uliopita tulitoa zawadi kama hii kwa Antony Matogolo wa timu ya Mbeya City,” alisema Twissa. 
  Baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Salum aliyeonekana mwenye furaha, alisema; “ninawashukuru wachezaji na mashabiki wa Azam FC kwa ushirikiano wanaonipa, hii ni zawadi kwa timu nzima na mashabiki wa timu yetu.” 
  Aidha, Shabiki wa Azam FC Hassan Kihelelo wa kawe jijini Dar es Salaam alisema anaunga mkono juhudi zinazofanywa na mdhamini mkuu wa ligi”Vodacom Tanzania”.
  "Vodacom  imeonesha ukomavu na ubunifu wa hali ya juu katika kuleta maboresho ya ligi msimu huu kwa kweli inastahili pongezi kwani inafanya wachezaji wetu wanaoshiriki ligi kuu kuwa na moyo wa kucheza na kuonesha vipaji vyao vizuri na kujituma zaidi wakiwa uwanjani", alisema Kihelelo.
   Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ligi Stephen Mguto (kulia) akimkabidhi tuzo Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Oktoba,Abubakar Salum "Sure Boy" katika sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar esSalaam jana.
  Afisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 1/=mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Oktoba, Abubakar Salum "Sure Boy" katika sherehe iliyofanyika kwenye uwanja wa Azam eneo la Chamazi jijini Dar es Salaam jana.

  0 0

  IMG_5047
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza kwenye mkutano wa kikanda unaozungumzia ujangili na hifadhi endelevu ulioshirikisha mataifa ya Afrika, wajumbe wa Bunge la Marekani (Congress) Mashirika ya Umoja wa Mataifa, mataifa washirika wa maendeleo, wanazuoni na wawakilishi wa taasisi zisizo za serikali uliomalizika jana jijini Arusha na kufungwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda. 

  Kushoto Mwenyekiti wa mkutano wa kikanda wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ICCF Group, Dr. Kaush Arha na kulia ni Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia Uchumi, Nishati na Mazingira, Bi. Catherine Novelli.

  0 0


  Mwanamuziki Mkongwe kutoka bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta Hamisi Amigolas (pichani kulia enzi za uhai wake) amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

  Taarifa za awali ambazo chumba cha habari cha Globu ya Jamii imezipata kutoka kwa vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa marehemu Amigolas alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Moyo mpaka kufariki kwake.

  Tutaendelea kupeana taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu kwa kadiri zitakavyokuwa zikiingia. 
  Amigolas atakumbukwa kwa sauti yake nzuri na utanashati awapo jukwaani. Wimbo "Aminata" alioutunga na kuuimba akishirikiana na Ally Choki, Msafiri Diof, Lwiza Mbuttu na Jessica Charles ni moja ya nyimbo bora za Twanga Pepeta wakati huo hadi sasa. Usikilize hapo chini.

  Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi
  -Amin

  0 0

  Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda 
  Na Owen Mwandumbya, 
  Lusaka Zambia

  Rais wa Bunge la SADC ambaye pia ndiye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda kesho tarehe 10 Novemba, 2014 ataongoza ujumbe wa Bunge la SADC kushiriki Misa Maalum ya kuombea mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Michael Chilufya Sata katika misa maalum itakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho Mjini Lusaka, Zambia. 
  Katika ujumbe huo wa Bunge la SADC, Makinda ataongozana na viongozi wengine wa Bunge hilo ambao ni Spika wa Zimbabwe Mhe. Jaji Jacob Mudenda, Spika wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Baleka Mbete, Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Richard Msowoya Spika wa Bunge la Angola Mhe. Fernando da Piedade Dias dos Santos na Mwenyeji wao Spika wa Zambia Dkt. Patrick Matibini. 
  Kutoka secretariat ya makao makuu wa Bunge hilo, katibu Mkuu wa Bunge Bunge la SADC Dkt. Essau Chiviya ataambatana na ujumbe huo kuwakilisha sekretariati ya Bunge hilo katika Misa hiyo Maalum Mjini Lusaka, Zambia.

  Kwa mujibu wa ratiba ya awali iliyotolewa na Serikali ya Zambia, Misa hiyo Maalum ya kuombea mwili wa Rais Rata itanyika kesho tarehe 10 Novemba, 2014 na inatarajiwa kuhudhuriwa na Marais kutoka kila kona ya dunia pamoja na viongozi mbalimbali wa Kimataifa watakaoziwakilisha nchi zao kabla ya kufanyika kwa mazishi yake ambayo yamepangwa kufanyika siku ya jumatatu tarehe 11 Novemba, 2014 mjini Lusaka. 
  Sata aliyekuwa na umri wa miaka 77 alifariki tarehe 29 Oktoba, 2014  jijini Londo Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu ambapo kifo chake kilitokea siku chache baada ya Zambia kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo, sherehe ambazo hakuweza kushiriki kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua. 
  Mwanasiasa huyo mkongwe aliingia madarakani mwezi Septemba 2011 baada ya kuongoza chama chake cha Patriotic Front, na kumshinda Rupiah Banda, ambaye alikuwa rais wakati huo na chama chake cha Movement for Multi-Party Democracy, kikiwa madarakani kwa miaka ishirini.

  Sata ambaye alibatizwa jina la "King Cobra" na wafuasi wake wakati alipochaguliwa mwaka 2011, alionekana kama mbadala wa siasa za Zambia na mtu ambaye alikuwa wavitendo licha ya kukosolewa kwa sehemu kubwa na upinzania. 
  Makinda na ujumbe wake wanatarajia kurudi nchi siku ya jumatano baada kushiriki pia mazishi yatakayofanyika tarehe 11 Novemba, 2014. 

  0 0

   Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislam cha Morogoro (MuM),Hajjat Mwantum Malale akiongoza mahafali ya saba ya Chuo Kikuu hicho cha Waislam yaliyofanyika jana Novemba 8,2014 katika viwanja vya Chuo hicho.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Baraza la Shule Chuo hicho,Prof. Mussa Assad.
   Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislam cha Morogoro (MuM),Prof. Hamza Mustafa Njozi (wa pili kulia) akisoma hotuba yake na baadae kuwakaribisha wakuu wa vitivo kuja kuwaorodhesha wahitimu wao wanaostakihi kutunukiwa Shahada mbali mbali.
   Sehemu ya Wahitibu wa Shahada mbali mbali wakiwa katika Mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro.
  Bi. Farida Khalfan akiwa akiwa katika pozz la picha mada baada ya kulamba Nondozz yake ya Sanaa na Ualimu (Bachelor of Arts with Education) katika Mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro.
  Furaha ya kulamba Nondozz.
  Mdau Jaffar Haniu wa TBC akiwa ni mwenye furaha sana baada ya kulambo Nondozz yake ya Sanaa na Mawasiliano ya Umma (Bachelor of Arts in Mass Communication) katika Mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro.
  Mdau Jaffar Haniu wa TBC (katikati) akiwa na wahitimu wenzake. 

  0 0
 • 11/09/14--01:48: mdau deo alamba nondozzzz
 • Mdau mkongwe wa Globu ya Jamii Deogratius Dotto jana kalamba nondozzz ya  Elimu ya Jamii katika Utawala wa Umma (Master of Arts in Public Administration) katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Nasi hapa chumba cha habari tunampa pongezi sana sana na kumtakia safari njema kuelekea PhD ambayo tayari  amekwishaianza...Hongera mdau Deo!

  0 0

   Uganda 
   Kenya
   Burundi
   Rwanda


  0 0


  0 0  0 0

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya afahamikae kwa jina la Zax 4 Real, Anae fanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya jijini mbeya, Amefanya vizuri pia katika show yake ya Usiku Wa Zax 4 Real, iliyo dhaminiwa na vituo vya redio vya Mbeya Fm, Bomba Fm,Rock Fm,G.Fm,Highlands Fm,Sweet Fm,Boys 2 Men Fasheni,Southside Music,Cigger Foundation na Michuzi Media Group. Katika ukumbi wa Nebana pub Soweto jijini Mbeya.Picha na Mr. Pengo wa Globu ya Jamii,Mbeya.
  Msanii Zax 4 Real akiwapagawisha mashabiki wake.
  mwana dada Silvia Green Kutoka jijini mbeya,akikamua katika stage ya Usiku wa zax 4 Real.
  kijana anae kimbiza katika muziki wa kizazi kipya Davy Star akifanya makamuzi katika show hiyo. 

older | 1 | .... | 634 | 635 | (Page 636) | 637 | 638 | .... | 3348 | newer