Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Chuo Kikuu cha Dodoma kuzinduliwa kesho jijini Dar

$
0
0
 Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),Balozi Juma Mwapachu (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) juu ya Uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko maalum wa Chuo Kikuu cha Dodoma,unatarajia kuzinduliwa rasmi kesho Novemba 8,2014 kwenye hoteli ya Golden Tulip,Jijini Dar es Salaam,ambapo Mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa Awamu tatu na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Mh. Benjamin W. Mkapa.Dhumuni la Mfuko huo ni kuweza kukisaidia Chuo hicho katika kukabiliana na mahitaji ya kifedha na vifaa mbali mbali chuoni hapo.Wengine Pichani ni Kaimu Mkuu wa Chuo hicho,Prof. Idris Kikula (katikati) na Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM,Prof. Ludovick Kinabo.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Prof. Idris Kikula akisisitiza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) wakati wa kuzungumzia Uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko maalum wa Chuo Kikuu cha Dodoma,unatarajia kuzinduliwa rasmi kesho Novemba 8,2014 kwenye hoteli ya Golden Tulip,Jijini Dar es Salaam.Katiki ni  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),Balozi Juma Mwapachu na kulia ni Katibu wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),Bi. Christina Silvester.

MASHINDANO YA MALECELA CUP 2014 YAMALIZIKA JIMBO LA SAME MASHARIKI

$
0
0
Mgeni rasmi katika mashindano ya John Sawel Malecela 2014,mbunge wa viti maalum Ester Bulaya(mwenye kofia) akiwa na mbunge wa jimbo la Same Mashariki Anne Kilango Malecela wakati wa fainali ya mshindano hayo iliyofanyika katika uwanja wa Mamba Myamba wilayani Same. 
Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela akiongozwa na katibu wa chama cha soka wilaya ya Same Nathaniel Msangi kwenda kukagua timu za sekondari ya Parane na Ntenga zilizokuwa zikicheza mchezo wa fainali ya kwanza.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KAULI YA WAZIRI MEMBE BUNGENI KUHUSU BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA NDOVU

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe.

I-TECH TZ YAKABIDHI TABLET ZA MAFUNZO YA MATATIBU

$
0
0
Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Otilia Gowelle (kushoto) akizungumza jambo kuhusu msaada wa vifaa na vitabu vya miongozo kwa ajili ya mafunzo ya matabibu wasaidizi kwenda kwenye ngazi ya Tabibu viliovyokabidhiwa kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mafunzo na Elimu( I-TECH TZ), Dkt Fatma Kabore(kulia) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
Mwakilishi Mkazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mafunzo na Elimu( I-TECH TZ), Dkt Fatma Kabore(kushoto) akimkabidhi tablet kwa ajili ya mafunzo ya masafa ya matabibu wasaidizi kwenda kwenye ngazi ya Tabibu Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Otilia Gowelle wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika leo jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. Kituo hicho kimekabidhi tablet 71 zenye thamani ya Sh. milioni 24 kati hizo 60 zitatumia na wanafunzi wa fani hizo kwenye vyuo vya Mtwara, Kilosa na Mafinga na nyingine zitatumiwa na wakufunzi.
Mwakilishi Mkazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mafunzo na Elimu( I-TECH TZ), Dkt Fatma Kabore(wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Otilia Gowelle(wa nne kutoka kulia) wakiwa na watendaji wengine wa wizara hiyo na kutoka kituo hicho.

DANGOTE AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KIWANDA CHAKE KIKUBWA CHA SARUJI MTWARA

$
0
0
 Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria, akiteremka kwenye ndege alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara, kwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha saruji kinachojengwa mkoani humo.
 Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria, akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa kampuni hiyo nchini, Esther Baruti (katikati) pamoja na Balozi Mdogo  wa Nigeria nchini, Adamu Mussa alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho, mkoani Mtwara
 Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote akiwa kwenye gari huku akipata maelezo ya ujenzi wa kiwanda hicho kutoka kwa mafundi na wahandisi ya Dil & Sinoma inayojenga kiwanda hicho kitakachokuwa cha tatu kwa ukubwa Afrika.
 Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria, akizungumza na Meneja Mkuu wa Kiwanda kikubwa cha cha saruji cha Dangote Tanzania, Daljit Singh (katikati), alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho,mkoani Mtwara. Kushoto ni Kenneth Kasigila ambaye ni Msaidizi Maalumu wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, iliyopewa fursa ya kwanza kujenga benki karibu na kiwanda hicho.

Serikali ya China yalaani vikali tuhuma za kuhusishwa kwa Ndege ya Rais wake kubeba meno ya ndovu kutoka nchini

$
0
0
Serikali ya China imelaani vikali uzushi uliotolewa na vyombo vya magharibi kutuhumu ndege ya Rais huyo kutumika kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.

Akizungumza leo mjini Arusha Balozi wa China Lu Youqing alisema kuwa huo ni uongo mkubwa ambao ulikuwa na nia ya kutia aibu taifa lake na Tanzania kwa ujumla.

Alisema kwamba Taifa lake hutoa adhabu kali kwa mtu anayefanya uovu kama ujangili, "Kama mwandishi angeweza kuthibitisha hao maafisa wangechukuliwa hatua kali, na hilo liko ndani ya uwezo wangu kwanini ameshindwa kuwataja?"

Lu alisema kwamba Adhabu kama hiyo si kwa mtu aliyekutwa na nyara tu bali hata kwa muongo, "Mwandishi huyo ni muongo na anatakiwa aadhibiwe".

Waziri wa maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu aliunga mkono kauli hiyo na kusema kuwa ilikuwa na nia ya kuchafua hali ya hewa kutokana na mkutano wa kimataifa ulioanza leo jijini Arusha.

"Hata tulipokwenda na rais Kikwete jijini London kwa mkutano wa kimataifa juu ya ujangili gazeti la Dail Mail lilitoa habari za kashfa kuhusu Tanzania siku moja kabla ya mkutano na hii leo ndio limetokea"

Alisema nashukuru wadau wa uhifadhi ambao kwa kiwango kikubwa wamehudhuria kikao chetu muhimu cha leo ambacho kitaleta mabadiliko makubwa katika vita dhidi ya ujangili.

Kikao hichio kilihudhuriwa na mawaziri kutoka nchi tisa za Afrika ukanda wa bahari ya Hindi na afrika mashariki na Kati pamoja na wawakilishi wa mashirika mbalimbali na balozi wa nchi nyingi wanaowakilisha nchi zao.
Balozi wa China nchini Tanzania,Mh. Lu Youqing akizungumza na vyombo vya habari mjini Arusha leo juu ya tuhuma za kuhusishwa kwa Ndege ya Rais wa China kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii,Mh. James Lembeli.

kikao cha kupitia Rasimu ya Sera ya Taifa ya Mazingira chafanyika jijini Dar leo

$
0
0
Profesa Richard Kangalawe akiwasilisha maoni kuhusu Rasimu ya Sera ya Mazingira katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa NIMR Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete akifungua kikao cha kupitia Rasimu ya Sera ya Taifa ya Mazingira jijini Dar es Salaam.
Wajumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakisikiliza maoni kuhusu mapitio ya Rasimu ya Sera ya Taifa ya Mazingira iliyowasilishwa na jopo la Wataalamu katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa NIMR Jijini Dar es Salaam.

JK AOMBA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KUKABILI UJANGILI

$
0
0
GU9A8625
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog)
Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete ameitaka jumuiya ya kimataifa kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na majangili wanaomaliza tembo kwa lengo la kupata pembe zao.
Alisema kutokana na biashara nzuri ya pembe hiuzo duniani majangili wamekuwa na soko tayari kiasi cha kuendeleza vitendo vyao.
Alisema mitandao iliyopo inawezesha kuuawa kwa tembo hao na kufikishwa bidhaa za pembe katika soko haramu ambalo lipo duniani na hivyo bila ushirikiano wa kimataifa wanyama hao ambao ni urithi wa dunia watatoweka kabisa katika miaka ijayo.
Amesema takwimu zilizopo sasa nchini za tembo zinatisha.
Alisema mathalani kwa ujangili pekee kwenye mfumo wa ekolojia wa Selou-Mikumi tembo waliobaki ni 13,084 kwa mwaka jana kutoka Tembo 109,419 waliokuwepo mwaka 2006.
Alisema mfumo uliopo wa ujangili na soko la bidhaa hizo unafanya vita inayoendeshwa na Tanzania kuwa ngumu kama haitapata ushirikiano na mataifa mengine.
Alisema kutokana na ukweli huo wanataka mataifa jirani na jumuiya ya kimataifa kuingia katika mapambano ya kudhibiti biashara hiyo na hivyo kuwamaliza majangili na kuendelea kuhifadhi Tembo.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori, alisema serikali ya Tanzania imeanzisha mchakato wa kulinda wanyama pori.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Patrick Balisidya & Afro 70 - Weekend

MSHINDI WA TMT 2014 MWANAAFA MWINZAGU AFAULU MITIHANI YAKE YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2014.

$
0
0
Pichani (Katikati) ni Mwanaafa Mwinzagu ambae ni Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya wafanyakazi na Wadau wa Kampuni ya Proin Promotions ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la TMT mara baada ya kutangazwa mshindi wa Kitita cha Milioni 50 za Kitanzania katika fainali ya shindano la TMT lililomalizika Mnamo tarehe 30 Aug 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City na Kumtangaza Mwanaafa Kuwa Mshindi kwa Mwaka 2014.
Mwanaafa Mwinzagu akiwa amembeba Mdogo wake mara baada ya kutangazwa mshindi wa Shindano la TMT 2014 lilifanyika tarehe 30 August 2014 katika Ukumbi wa Mlimani city.Picha na Josephat Lukaza.

Na Josephat Lukaza 
Mwanaafa Mwinzagu ambae alishiriki Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) huku akiwa ni Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Tandika iliyopo Mjini Mtwara katika Manispaa ya Mtwara amefaulu mitihani yake ya kumaliza elimu ya Msingi Kwa Kupata daraja C huku Masomo ya Hesabu na Sayansi akiwa kafanya vizuri sana kwa Kupata Daraja B.
 Wakati Shindano la TMT lilipofika Mtwara kwaajili ya kusaka vipaji vya kuigiza Ndipo Mwanaafa alipojiunga na Kuja kushiriki Katika SHindano hilo Kubwa na lenye mvuto wa Pekee Afrika Mashariki na Kati. Wakati akihojiwa mara baada ya Kutoka katika hatua ya Kwanza ya Shindano hilo lililofanyika Mtwara na kuhojiwa Mwanaafa Mwinzago alisema "Hiki ni Kipaji kwahiyo sina haja ya kuficha na pia naweza Kukosa kwenye Shule nikapata Kwenye Kuigiza na ndio maana nimekuja Kushiriki" Vilevile alipoulizwa Je Ikitokea Ukashinda itakuwaje Shule na Sanaa? Alijibu kuwa "Ikitokea nikashinda katika ngazi ya Kanda ya Kusini Nitaenda Kambini Dar Es Salaam na kuacha Shule kwanza, Maana Shule Ipo ila Shindano hili linapita tu Kwahiyo Naweza kupata kwenye Sanaa na nikishinda basi nitarudia Darasa".
Mara baada ya Kuibuka MShindi katika Kinyanganyiro Hiko Katika Ngazi ya Kanda ya Kusini, Timu nzima ya TMT iliweza kumuhoji Mwalimu wake Mkuu ambapo alisema yafuatayo "Huyu Ni mwanafunzi wa Darasa la Saba Kwa Sahivi na Hiki pia ni kipaji lakini Sisi kama Wazazi hatuwezi kuzuia Mtoto kuonyesha Kipaji chake yeye alichofanya alishiriki Mashindano na ameshinda kwahiyo sisi kama walimu wake tutajadiliana jinsi ya kulitatua hili kwa maana hatuwezi kujua labda mshindi wa Milioni 50 hatakuwa yeye"
Mara baada ya Shindano la TMT kumalizika tarehe 30 August 2014 wiki moja baadae Mwanaafa aliweza Kurejea Mjini Mtwara kwaajili ya Kufanya mitihani yake ya Kuhitimu Elimu ya Msingi na Hatimae mara baada ya kuwasili nyumbani kwao Mwanaafa aliweza kwenda shule kwao kwaajili ya kukamilisha taratibu za kufanya mtihani na kesho Mwanaafa akaweza kufanya Mitihani yake vizuri kwa muda wa siku mbili na alipomaliza Alirejea Jijini Dar Es Salaam ambapo Aliendelea na zoezi la Kurekodi filamu ya Pamoja Ya Washindi wa TMT waliofanikiwa kuingia Hatua ya Kumi Bora huku yeye akiwa ni kinara katika filamu hiyo ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Mapema Mwezi wa Kumi na Mbili katika Mikoa yote ambayo TMT ilipita kwaajili ya kusaka Vipaji.
Hapo Majuzi kupitia Vyombo mbalimbali vya habari kupitia Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lilitangaza matokeo ya Mitihani ya Elimu ya Msingi na Ndipo tulipofahamu kuwa Mwanaafa ameweza kujitahidi sana katika Mitihani huku akiwa kafanya Vizuri sana katika Masomo ya Hesabu na Sayansi ambapo amepata daraja B huku masomo mengine akiwa amepata daraja C na Kupelekea kupata wastani wa daraja C.
Kwa Matokeo hayo tunapenda kumpongeza Mwanaafa kwa kuonyesha uwezo wake katika Masomo na hatimaye kufanya vizuri katika Mitihani yake ya Mwisho ya Kumaliza Elimu ya Msingi
Ikumbukwe kuwa hapo awali Mwanaafa alisema kuwa endapo atashinda Milioni 50 katika fainali ya Shindano la TMT lililomalizika tarehe 30 August 2014 basi atatumia Kiasi hiko cha pesa kwaajili ya kujiendelea kielimu lakini Wakati wa Fainali hiyo Kampuni ya Proin Promotions Ltd iliahidi kumsomesha Mwanaafa hata Kama asingeshinda katika Shindano hilo.
Kwasasa Mwanaafa yupo chini ya Uangalizi wa Kampuni ya Proin Promotions ambapo kampuni hiyo itamsomesha Kuanzia Kidato cha Kwanza hadi Cha Nne.
Kampuni ya Proin Promotions Ltd inapenda kumpongeza Mwanaafa kwa kufanya Vizuri katika Mitihani yake ya Kumaliza Elimu ya Msingi na kuonyesha Kuwa Kumbe Bado ni Mshindi hadi Darasani.

Ashura Day 1436 November 2014 in BUKOBA

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA IJITIMAI YA KIMATAIFA MJINI MOROGORO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi semina ya mafunzo ya Kiislamu (IJITIMAI) iliyofunguliwa jana Novemba 7, 2014 kwenye Msikiti wa Jabalhira, mjini Morogoro
  
 Sehemu ya waumini wa dini ya kiislam waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa IJITIMAI, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi IJITIMAI hiyo katika msikiti wa Jabalhira, mjini Morogoro. Picha na OMR 

TASAF YAENDESHA WARSHA YA MAFUNZO KWA WAWEZESHAJI NGAZI YA TAIFA KUHUSU TUKIO LA UTAMBUZI WA KAYA MASKINI UKUMBI WA TEC DSM

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini linalotarajiwa kuanza Novemba 10 katika halmashauri 16. Wengine (walioketi) ni Mkurugenzi wa fedha wa TASAF Bw. Isaya Wambura (wa pili kushoto), meneja masijala ya walengwa Philipine Mmari (wa kwanza kushoto), Mtaalamu wa Mafunzo Mercy Mandawa (wa pili kulia) na Meneja Rasilimali watu Tecla Makundi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiri wa mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini.



Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akitoa neno la ufunguzi wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa (hawapo pichani) kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini linalotarajiwa kuanza Novemba 10 katika halmashauri 16 nchini . Aliyekaa kushoto ni  Mkurugenzi wa fedha wa TASAF Bw. Isaya Wambura.
 Afisa Ufuatiliaji na tathmini wa TASAF Bw. Paul Luchemba akitoa mada juu ya malengo ya warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini katika ukumbi wa AMECEA Kurasini Jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo kwa wawezeshaji ngazi ya taifa kuhusu tukio la utambuzi wa kaya maskini unaotekelezwa na TASAF kupitia Mpango wa kunusuru kaya maskini  PSSN wakifuatilia mjadala baada ya uwasilishaji wa madajuu ya mwongozo wa mpango katika ukumbi wa TEC-Kurasini jijini DSM.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

NEWZ ALERT:SITTI MTEVU ALIVUA TAJI LA MISS TANZANIA 2014,LILIANI KAMAZIMA AMRITHI.

$
0
0


Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) aliyechukua nafasi yake pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk.
Sitti Abas Mtemvu amelivua taji hilo baada ya kuiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania, November 5 mwaka huu, kuhusiana na uamuzi wake huo.
Mrembo huyo alikuwa akikabiliwa na shutuma za kudanganya umri wake, jambo ambalo lilililazimu Baraza la Sanaa la Taifa, (Basata) kutokana na agizo la wizara  husika kufuatilia ukweli wake.
“Baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali dhidi yangu. Wameniwekea maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema wakati siyo,” amesema kwenye barua hiyo.
Miss Tanzania aliyechukua nafasi ya Sitti Mtemvu, Lilian Kamazima pichani kulia.
“Shutuma hizo zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao ya kijamii, kiasi ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu. Sasa kwa hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014,” ameongeza.

“Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa. Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.”
Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi. 
“Leo nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo niliochukua.” Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamazima.

Salumu "Manywele" wa Michuzi media group na Kurthum Wameremeta

$
0
0
 Mfanyakazi wa Michuzi Media Group Bw. Salumu Mwingiriko a.k.a Manywele akifungua dansi na mkewe Kurthum Abubakar usiku wa kuamkia leo katika sherehe ya kumeremeta kwao iliyofana sana katika ukumbi wa Kilimanjaro katika Uwanja wa Sabasaba jijini Dar es salaam
 Ankal na mai waifu wake wakipokea keki toka kwa maharusi kwa niaba ya wafanyakazi wa Michuzi Media Group
 Picha ya pamoja na maharusi. Kulia ni Hamisi Makuka mpiga picha wa MMG
Maharusi wakiserebuka kwa furaha. 

Taarifa ya Uzinduzi wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA MAHAKAMA YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA ICTR JIJINI ARUSHA.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitazama baadhi ya picha za kumbukumbu za Mahakama ya Kimbari zilizo katika ukumbi huo wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ICTR, ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
  Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

HII NDIO BARABARA ILIYOKARABATIWA KWA MILIONI 90 UKONGA MAZIZINI- MOSHI BAR

$
0
0
 Hii ndio ile barabara ya Ukonga Mazizini- Moshi Bar ambayo inadaiwa kugharimu kiasi cha shilingi Milioni 90 kuikarabati kwa kiwango cha changarawe kwa umbali wa kilometa tatu. Picha hizi ni madimbwi ya mwanzo tu ya hizo kilometa tatu.(Picha na Father Kidevu Blog).
Meya Jerry Silaa wa Ilala ambaye ni Diwani wa Gongo la Mboto alipotembelea aliwaambia wananchi kuwa fedha za ujenzi huo ni kutoka mfuko wao ni . PICHA ZA CHINI NI SIKU MEYA SILAA ALIPOTEMBELEA UJENZI WAKE.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibarkilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza. Ikiwa ni utekelezaji wa miradi yadharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinuulitokea baada ya Mvua kubwa. Mradi huoambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za Ujenzi huohizo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.
Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar
Mwonekano wa Bara barabara hiyo

Ofisi ya Taifa ya Takwimu yatoa taarifa za mfumuko wa bei nchini.

$
0
0
 
 Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumuko wa bei nchini.
Baadi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumzia suala la mfumuko wa bei nchini.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO).


Wananchi wameombwa kutoa ushirikiano wa dhati kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupitia ofisi za takwimu za mikoa wakati wa ukusanyaji wa takwimu mbalimbali kwa lengo la kutoa taarifa zilizo sahihi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Kwesigabo amesema kuwa pamoja na mambo mengine Ofisi ya Taifa ya Takwimu ndiyo yenye mamlaka ya kutoa taarifa za mfumuko wa bei nchini ambapo kwa mwaka huu unaonesha umepungua kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kuanzia kipindi cha mwezi Oktoba 2013 hadi Oktoba 2014.

Kwesigabo amesema kuwa mwenendo wa bei za bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua bei kwa mwezi Oktoba 2014 zikilinganishwa na mwezi Oktoba 2013 ni pamoja na bei za mahindi asilimia 7.2, unga wa mahindi asilimia 5.5 na unga wa ngano asilimia 4.4.

Bidhaa nyingine za vyakula zilizoonesha kupungua bei ni ulezi asilimia 3.5, tambi asilimia 2.2, samaki asilimia 4.6, mihogo asilimia 2.1 na sukari imepungua kwa asilimia 4.6.

Aidha, Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba 2014 umepungua hadi asilimia 5.9 kutoka asilimia 6.6 tofauti na hali ilivyokuwa mwezi Septemba 2014.  “Hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Oktoba 2014 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwaka ulioishia mwezi Septemba 2014” alisema Kwesigabo.

Kwa upande wa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi Bw. Kwesigabo amesema kuwa umepungua kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na kupungua kwa asilimia 0.4 kama ilivyokuwa kwa mwezi Septemba mwaka huu, huku fahirisi za bei za taifa zimepungua hadi kufikia 149.70 kwa mwezi Oktoba 2014 kutoka 149.93 za mwezi Septemba 2014.  

Kwesigabo amezitaja bidhaa zilizochangia ongezeko la fahirisi za bei nchini kuwa ni pamoja na vitafunwa vinavyotokana na unga wa nagano kwa asilimia 2.4, unga wa mahindi kwa asilimia 0.1, samaki kwa asilimia 1.7,ndizi za kupika kwa asilimia 7.5, mbogamboga kwa asilimia 2.2, viazi mviringo kwa asilimia 1.5 na sukari kwa asilimia 1.6.

Aidha, amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii umefikia shilingi 66 na senti 80 kwa mwezo Oktoba 2014 kutoka mwezi Septemba 2010.

Kuhusu ulinganifu mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana na kueleza kuwa mfumuko wa bei nchini Kenya umepungua hadi kufikia asilimia 6.43 kwa mwezi Oktoba 2014 ikilinganishwa na asilimia 6.60 za mwezi Septemba mwaka huu, huku Uganda ikiwa na mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 1.8 kwa mwezi Oktoba mwaka huu ikilinganishwa na 1.4 za mwezi Septemba. 





shindano la ubunifu wa jezi ya Taifa Stars

$
0
0
Katika kuelekea shindano la kubuni jezi mpya ya Taifa Stars, huyu mdau ametutumia  picha hii ikionyesha ubunifu wake... je mnasemaje?
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images