Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

mdau mama mutaki akiwa malta kula nomndozzz ya sheria ya maritime

0
0
 Mdau Mrs Leticia Mutaki (wa pili kushoto) akiwa na wanafunzi wenzake wanawake kwenye ufunguzi wa kula nondozzzz  ya  sheria ya Masters in  maritime law nchini Malta.
 Mdau Mrs Leticia Mutaki (wa pili kushoto) akijidai na bendera ya Tanzania kwenye ufunguzi wa mafunzo ya nondozzz  ya sheria ya Masters in  Maritime law nchini Malta.

pre-wedding party ya jacqueline yafana sana

0
0
 Bi Harusi Mtarajiwa Jacqueline Dillip Sing (katika bluu tupu) akiwa na dada zake kwenye mnuso wa pre-wedding party usiku wa kuamkia leo ukumbi wa VIP Diamond Jubilee hall jijini Dar es salaam. Chini Ankal na wadau waalikwa wenzie katika mnuso huo

supu ya pweza, karanga mbichi, muhogo mbichi, mbata, korosho havisaidii urijari - Daktari

0
0
Dk Cuthbert Maendaenda akiwatwanga
lekcha wahariri mbalimbali mjini Morogoro

ULAJI wa supu ya pweza, karanga mbichi, muhogo mbichi, mbata kwa dai kwamba vinaongeza urijali kwa wanaume kumeelezwa kuwa ni dhana potofu inayostahili kupigwa vita kwa kuwa haina uhusiano kati ya urijali wa mwanaume na virutubisho vinavyotolewa na vyakula hivyo.


Kauli hiyo imetolewa na Dk Cuthbert Maendaenda wakati akitoa mada yake katika semina ya wahariri iliyofanyika mkoani Morogoro iliyojadili nafasi ya wanaume katika kuleta mabadiliko katika jamii juu ya afya ya uzazi na ujinsia.
Dk Maendaenda ambaye alikuwa akijibu maswali pia kuhusiana na dhana hiyo iliyozoeleka kuhusu nguvu ya supu ya pweza, alisema ipo haja ya wanaume kuangalia sababu za kudorora kwa uwezo wao na kufanya marekebisho badala ya kudhani kwamba kuna dawa kutoka katika vyakula hivyo.
Miji mingi nchini kwa sasa nyakati za jioni kuna supu ya pweza na mauzo ya karanga mbichi ambao wauzaji wamekuwa wakinadi kama msaada wa kurejesha heshima katika ndoa.
Alisema ufanyaji mapenzi unaathirika na vitu vingi na jamii lazima kuangalia ukweli huo ili kuwa na watu wanaojiamini katika mapenzi na wale ambao wanamatatizio kupata ushaudi wa kidaktari.



Mwezeshaji huyo kutoka Taasisi ya sweden inayohusu haki za afya ya uzazi na ujinsia (RFSU) tawi la Tanzania ambalo linaendesha mradi wa TMEP wenye lengo la kuwaamsha wanaume  kuwa chachu ya mabadiliko na hivyo kuwa na uelewa mpana kuhusu haki za ujinsia. 

NEWS ALERT: Rais Kikwete afanyiwa upasuaji wa tezi dume Marekani, hali yake inaendelea vyema

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani. 
 Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo. 
 Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. 
Hali ya Mheshimiwa Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba. 
 Wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete kwa kadri zitakavyokuwa zinapatikana. 
 Imetolewa na
 KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS,
 IKULU DAR ES SALAAM, NOVEMBA 9, 2014
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na  Dkt.Edward Shaeffer wa  hospitali ya Johns Hopkins (kushoto) na Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi  (kulia) muda mfupi baada ya kuwasili ili kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland Marekani Jumamosi asubuhi.Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa Mpasuaji Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland nchini Marekani Jumamosi asubuhi(picha na Freddy Maro)

DJ JD na DJ FAST EDDIE WAFANIKIWA KUREJESHA MUZIKI WA DISKO KILELENI TENA, NYOMI ISUMBA LOUNGE KILA IJUMAA NA JUMAMOSI

0
0
 DJ JD akiwa kazini katika ukumbi wa Isumba Lounge jijini Dar es salaam usuiku wa kuamkia leo. Yeye na DJ Fast Eddie wameweza kurejesha utamu wa wapenzi wa muziki kwenda disco kwa wingi kama ilivyokuwa enzi hizo. Hapo Isumba ni mambo ya Old Skul na Mayenu kwa kwenda mbele kila Ijumaa na Jumamosi ambapo vijana wa zamani na wapya huruka majoka hadi lyamba.

TAMASHA LA TIGO LAFANA BUKOBA LEO! WASANII WA ORIGINAL COMEDY WAFUNIKA MJINI BUKOBA!

0
0
Mpoki(kulia) akitamba!!Wasanii wa Original Comedy wakiwapa buradani wananchi waliohudhuria Tamasha hilo katika uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini leo Jumapili Novemba 9, 2014. Nani zaidi??Mwana-FA akiimba mbele ya umati wa wakazi wa Bukoba leo kwenye Tamasha la Tigo lililofanyika leo Jumapili jioni kwenye Uwanja wa Kaitaba.Kiingilio ilikuwa ni wewe kuvaa uhusika wa Tigo!!Mwana-FA

Top 10 Reasons to drink ARGI+

0
0


Top 10 Reasons to drink ARGI+

In summary, what are the benefits of taking ARGI+?

1. Is a marvelous daily supplement that supports better health throughout many systems of the body, delivering optimal performance.
2. Supports the immune system. Nitric oxide derived from L-Arginine, is used by white blood cells to attack bacterial etc. as it is toxic to them and makes these immune cells more lethal.
3. Helps maintain a healthy blood pressure and cardiovascular system.
4. Aids bone and tissue growth and repair, so is particularly appropriate after fractures and soft tissue injury.
5. The nitric oxide formed, permits greater blood flow and may improve sexual function.
6. Increases muscle mass and strength, whilst reducing the amount of fatty tissue. A welcome benefit for sports men and women.
7. The pomegranate and fruit components are a rich source of antioxidants, needed to fight the damaging effects of free radicals.
8. Contains an extract of red wine, which helps to reduce blood cholesterol levels.
9. Affects insulin sensitivity so is particularly useful in maintaining blood glucose control.
10. Acts to release anti-ageing hormones. Who wants to look older than their years?

What Vitamins are in ARGI+?

1. Vitamin C-for immune system, a healthy nervous system, concentration sleep and healthy bones and skin.
2. Vitamin K2 – for bone formation, blood clotting, healing and vitality.
3. Vitamin B6 for immune system, a healthy nervous system brain, muscles, oxygen transportation, protein, fat and carbohydrate metabolism.
4. Vitamin D3 – for the immune system, bones, a healthy nervous system and positive mood.
5. Vitamin B9- for new cells, brain, nerves and growth.

WITH SO MANY HEALTH BENEFITS, IT’S NO WONDER L-ARGININE IS GENERATING SO MUCH EXCITEMENT AT ONLY TSH 132,000. CALL 0786139316/0769888605 FOR MORE INFORMATION.  

ngoma azipendazo ankal

0
0
Orchestre Veve - Muana Mburu

WORLD-CLASS TRAINING ON INFORMATION SECURITY RISKS AND MANAGEMENT TECHNIQUES

0
0
World class Information Security training experts of Koening- Solutions, India (www.koenig-solutions.com) in collaboration with Auditec Consulting Company, Tanzanian local partners, welcome all information systems practitioners to attend this unique IT Security career opportunity.

DATE:1st – 5th December 2014,
TIMEFrom 0800 to 16OO Hrs 
VENUENASHERA HOTEL, MOROGORO

TARGET GROUPChief Information Officers/Heads of IT/Information Security officers
Auditors/ System Administrators/ System Engineers
Database Administrators/ Application Administrators
Network Administrators/ Programmers
MAJOR COURSE FOCUS
Information Security  fundamentals, threats and vulnerabilities
Network scanning and advance sniffing techniques
System hacking and virus/Trojan/spyware attacks
Computer and windows forensics investigation process
AWARDCertificates of Attendance

TRAINERS. S. Sandhu (CCNA, CEH, ECSA, EDRP, CHFI, CompTIA Security+ Certified)

FEETshs. 1,500,000 to cover tea break, lunch, training materials, certificates and social gathering events.

Deposit your fee (cash) to Auditec account number 0150237529000 CRDB Bank and send a scanned copy to Auditec through email or submit original pay in slip to Auditec offices.
Cheques should be submitted to Auditec at least 1 week before training date.
Please confirm your participation before November 21, 2014

All enquiries should be addressed to:
TRAINING COORDINATOR
AUDITEC CONSULTING COMPANY
PLOT 2478/5- OCEAN ROAD/OBAMA DRIVE
P. O. BOX 34702, DAR ES SALAAM- TANZANIA,
TEL: 0757 642389.
EMAIL: info@auditec.co.tz; 

DON’T MISS THIS CARRER CHANGING OPPORTUNITY!
LEARN FROM THE BEST!

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA MPYA YA AIRTEL MONEY TIMIZA MJINI DODOMA

0
0
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia), Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi (wa tatu kushoto), Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel, Arindam Chakrabarty (kulia) wakipiga makofi baada ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Airtel Money Timiza, katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia) baada ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Airtel Money Timiza mjini Dodoma jana. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk. Rehema Nchimbi, Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel, Arindam Chakrabarty (kulia).
  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
Meneja Uendeshaji kutoka kampuni ya Airtel Tanzania,Bwa.Asupya Naligingwa akitoa maelekeo mafupi namna ya kutumia huduma hiyo mpya ya Timiza wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza, katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano.
   Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia  uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money Timiza katika viwanja vya Nyerere Square, mjini Dodoma jana.
HABARI NA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MASHINDANO YA MASHUA YA MERCEDES BENZ CUP 2014 YAFANA JIJINI DAR

0
0
mashua
Moja ya mashua ikisukumwa kurejeshwa katika eneo lake la hifadhi baada ya kumaliza mashindano hayo.
-----------------------------
MICHUANO ya siku 2 mwaka ya waendesha mashua za kisasa kuwania kombe la Mercedes Benz kwa mwaka huu imemalizika juzi jioni kwa waendesha mashua Al Bush akisaidia na  Pugwash wakitwaa ushindi wa jumla na kutwaa kombe la Mercedes Benz.
Waendesha mashua hao yenye jina la Strophic aina ya Hobie Tiger ikiwa na namba 2653 wakikabidhiwa kombe hilo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CFAO, Wayne McIntosh ambao ndio mawakala pekee wa Mercedes Benz nchini Tanzania.
Akizungumzia mashindano hayo Mratibu wa waendesha mashua hao Michael Sulzar alisema yalikuwa na ushindani mkubwa na kwamba ingawa siku ya kwanza bahari ilikuwa shwari siku ya pili bahari ilikuwa chafu na kufanya  wenye mashua kuwa na kazi ya ziada.
Alisema kwa kawaida mchezo huo unakuwa mtamu pale ambapo bahari inakuwa ‘ngumu’ ambapo waendesha mashua hao ni kama vile wanataka kutemwa kutoka kwenye mashua, hivyo wakilazimika kutumia maarifa yao kuidhibiti.
mratibu
Mratibu wa waendesha mashua Michael Sulzar akitangaza matokeo ya mashindano ya kuwania kombe la Mercedes Benz 2014 yaliyofanyika katikati ya wiki. Jumla ya timu kumi na nne (Mashua) zilishiriki katika michuano hiyo ya siku mbili.

Pamoja na washindi hao wa jumla ambao walikuwa katika mashua ya kisasa zaidi yenye Tanga mithili ya baluni  washindi wengine ni Tony Hughes na Richard Stanley wakiendesha mashua Popo bawa yenye namba 2648 aina ya Hobie Tiger.
Mshindi wa tatu alikuwa Cyrille Girardin akiwa na Olivier Praz waliokuwa na mashua ya Theluji  namba 72 aina ya Hobie 16.
Michael Sulzer na Andreas Schimidt wao walipata tuzo ya wawili waliofanya vyema. Wawili hao walikuwa katika mashua Die Wilde 13 yenye namba 1659 aina ya Nacra Infusion.
Aliyetwaa tuzo ya uanamichezo bora ni Mark Henderson na Shane Rumbold waliokuwa katika mashua Shark aina ya Hobie  tiger.
kombe
Waendesha mashua Al Bush na mwenzake Pugwash wakiwa na  kombe la ushindi la  Mashindano ya mashua ya siku mbili ya kombe la Mercedes Benz yaliyofanyika jijini Dar es salaam Yatch Club.Washindi hao walikuwa wakiendesha mashua yao yenye jina la Strophic aina ya Hobie Tiger ikiwa na namba 2653.Walikabidhiwa kombe hilo hivi karibuni na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya CFAO Motors, Wayne McIntosh (kulia) ambao ndio mawakala pekee wa Mercedes Benz nchini Tanzania.Wa Pili kulia ni Meneja Masoko wa CFAO Motors,  Tharaia Ahmed.
Mshindi wa kwanza katika mashua za kawaida alikuwa David Scott akiwa na Christina waliokuwa na mahsua  Alphacrucis yenye namba112483 aina ya Hobie16. Mshindi wa pili wenye mashua Polo aina ya Hobie 16 yenye namba 111206 Andrew Boyd na Kim Troll.
 Mshindi wa tatu alikuwa Roland Van de Ven akiwa na Peter Scheren waliokuwa katika mashua namba 2657 aina ya Hobie Tiger iliyojulikana kama 1.
Jumla ya Mashua 14 zilishindana katika michezo iliyoandaliwa katika klabu ya Yatch ya Dare s salaam Msasani.
Baada ya shamrashamra za kupeana vikombe na tuzo nyingine Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh alipata nafasi ya kuzungumzia michuano hiyo ambayo imekuwa ikidhaminiwa na Mercedes Benz kwa miaka zaidi ya sita sasa.
mtoto
Mtoto wa mshindi wa kwanza katika mashua za kawaida David Scott (ambaye aliendesha mashua hiyo akiwa na Christina) akimsalimia Ofisa Mtendaji mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh kabla ya kukabidhiwa tuzo ya wazazi wake ya ushindi.
tuzo
Mark Henderson na Shane Rumbold wakikabidhiwa tuzo ya uanamichezo bora, walikuwa katika Mashua Shark aina ya Hobie Tiger.
ofisa
Ofisa Mtendaji Mkuu wa CFAO Motors, Wayne McIntosh akizungumza kabla ya kukabidhi kombe la Mercedes Benz kwa washindi wa jumla Al Bush na mwenzake Pugwash. Michuano hiyo ilianzia na kumalizikia Dar Yatch Club Msasani. Kulia aliyebeba kombe hilo ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed.

Shy-Rose Bhanji Akutana na Waandishi wa Habari Jijini Dar kufafanua Uzushi Unaoenezwa Kuhusu Yeye

0
0

Mbunge wa  Bunge la Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam jana kufafanua uzushi unaoenezwa na baadhi ya wabunge wa bunge hilo kuhusu yeye, na baadhi yao wakisusia kushiriki vikao vya bunge hilo kushinikiza aondoshwe kwenye kamati ya uongozi kitu ambacho amekipinga akitaka wenye madai hayo wawasilishe kwanza madai yao yajadiliwe na yeye ajitetee. mazungumzo hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mbunge wa Bunge hilo Twaha Taslima, aliyekuwa akifafanua mambo ya kisheria kuhusu bunge hilo.
Mbunge wa Bunge hilo Twaha Taslima, aliyekuwa akifafanua mambo ya kisheria kuhusu bunge hilo.

IN LOVING MEMORY

Siku ya tatu ya ziara ya Ndg Jerry Silaa mkoani Simiyu

0
0
 Ziara ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ndg.Jerry Silaa imeingia siku ya 3 kwa kutembelea wilay ya Maswa ambapo ameongea na viongozi wa CCM wa ngazi za Vijiji na Vitongoji na amehutubia mkutano wa hadhara kata ya Malampaka. 
 Ndg Jerry Silaa akisalimiana na wananchi wa Malampaka
Wananchi wa Malampaka wakimsikiliza Ndg Jerry Silaa

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA AHMED .Z. MSANGI-SACP ANAWATANGAZIA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014 NA KIDATO CHA NNE MWAKA 2013 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI BAADA YA USAILI KUKAMILIKA

0
0
Maelekezo Muhimu.

  1. Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014, kidato cha nne mwaka 2013 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo, Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita, Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani, Oljoro, Rwankoma na Kimbiji wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi.

  2. Wahitimu hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti tarehe 28/11/2014 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wa kuwapeleka Shule ya Polisi Tanzania tarehe 30/11/2014.

  3. Zoezi la usajili litaanza shuleni hapo tarehe 01/12/2014 hadi tarehe 15/12/2014. Atakaefika kuanzia tarehe 16/12/2014 hatapokelewa.

  4. Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Shule ya Polisi Tanzania mjini Moshi.

  5. Vijana hawa watalazimika kufika shuleni wakiwa na mahitaji yafuatayo:

    1. Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

    2. Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)

    3. Chandarua chenye upana futi tatu

    4. Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)

    5. Pasi ya Mkaa

    6. Ndoo moja

    7. Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=).

    8. Pesa kidogo ya kujikimu.

  6. Kwa mujibu wa kanuni za shule ya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa shuleni hapo. Shule itaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.

  7. Angalia orodha kwenye tovuti ya www.policeforce.go.tz au fika Ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya iliyopo Forest barabara ya mahakama kuu.



U.S. Under Secretary of State for Economic Growth, Energy, and Environment visits Burunge Wildlife Management Area

0
0
November 10, 2014 - The United States under Secretary of State for Economic Growth, Energy, and the Environment, Catherine Novelli (pictured), recently visited the Burunge Wildlife Management Area (WMA) in the Manyara Region.  Under Secretary Novelli visited Burunge WMA to learn first-hand about the challenges facing community based wildlife conservation efforts.


Burunge WMA lies between Tarangire and Lake Manyara National Parks, and is an area of critical importance to the Tarangire – Manyara ecosystem.  Burunge WMA is one of nineteen WMAs established through collaborative efforts between the U.S. Government through United States Agency for International Development (USAID), the Government of Tanzania, other development partners, and local communities. 
At the Burunge WMA, Under Secretary Novelli received a briefing from Mr. John Salehe, the Tanzania Country Director for the African Wildlife Foundation (AWF), on the WMA community conservation model that the U.S. Government has implemented in Tanzania over the last decade.  She also met with Village Game Scouts and toured U.S. supported projects.



During the visit, Under Secretary Novelli noted that wildlife trafficking is a global issue that requires a global response, and that local communities are key partners with governments in the fight against poaching.  She reiterated U.S. Government commitment to support innovative wildlife protection and conservation initiatives that benefit local communities sharing environments with wildlife, and emphasized that greater success in wildlife conservation can only be won through collaborative efforts between public, private and civil society partners.  

save the date: 5th December, 2014 @ Century Cinemax Mlimani city, dar es salaam

Mtwara Festival is Back Again – This December

KIKUNDI CHA COSTANTINE LUSALAGE MABINGWA MBIO ZA BALIMI MITUMBWI MWANZA.

0
0
Baadhi ya Wakimbia mbio za Makasia Wanaume wakichuana wakati wa fainali za mbio za Mitumbwi zinazodhaminiswa na Bia ya Balimi Extra Lager zijulikanazo kama “ Balimi Boat Race 2014” Mkoa wa Mwanza zilizofanyika mwishoni mwa wiki ambapo kikundi cha Costantine Lusalage kutoka Sengerema kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa upande wa Wanaume.
Baadhi ya Wakimbia mbio za Makasia Wanawake wakichuana wakati wa fainali za mbio za Mitumbwi zinazodhaminiswa na Bia ya Balimi Extra Lager zijulikanazo kama “ Balimi Boat Race 2014” Mkoa wa Mwanza zilizofanyika mwishoni mwa wiki ambapo kikundi cha Joyce Alon kutoka Misungwi kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa upande wa Wanawake.
Meneja wa bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa(kulia) akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbio la Mitumbwi zilizodhaminiwa na bia hiyo zilizofanyika Mwanza mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Meneja Masoka wa TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki.

WAZIRI MIGIRO AFUNGUA RASMI MKUTANO WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA TANZANIA KATIKA HOTELI YA MALAIKA JIJINI MWANZA

0
0
Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro, WAZIRI wa Katiba na Sheria akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Majaji katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza,Maudhui ya Mkutano huo ni kujitathmini Kama njia bora ya kuboresha Mahakama. Mhe. WAZIRI amefungua Mkutano huo kwa niaba ya Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akitoa Mada katika Mkutano wa Majaji unaofanyika mkoani Mwanza.
Mhe. Jaji Sauda Mjasiri, Jaji wa Mahakama ya Rufani, (aliyeketi mbele, wa kwanza kushoto), Mhe. Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar (wa kwanza kulia) pamoja na Mhe. Shaaban Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (katikati) wakiwa pamoja na Wahe. Majaji wengine wa Mahakama ya Tanzania wanaohudhuria katika Mkutano huo. 
Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro, Waziri wa Katiba na Sheria (wa nne kushoto), Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (wa tatu kushoto), Mhe. January Msoffe, Jaji wa Mahakama ya Rufani (wa pili kushoto), Mhe. Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar, (wa pili kulia), Mhe. Shaaban Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (wa kwanza kushoto) pamoja na Mhe. Jaji Mwangesi, Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa ni baadhi ya Majaji wote waliohidhuria katika Mkutano huo Mkuu wa mwaka unaofanyika jijini Mwanza.(Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania).
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images