Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 629 | 630 | (Page 631) | 632 | 633 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Mbunge wa kuteuliwa akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Bweni ;a wavulana katika shule ya sekondari Bishop Moshi.


  Mkuu wa shule ya sekondari Boshop Moshi,Sophia Mushi akisoma risala mbele ya mgeni ,Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia.

  Wanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo walichangia mifuko mitatu ya Sementi ambayo walikabidhi kwa mgeni rasmi Mbunge Mbatia.

  Mbunge Mbatia akichangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Bweni.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Owen Mwandumbya, Victoria Falls, Zimbabwe.

  Aliyekuwa mweka hazina wa Bunge la SADC ambaye pia ni Mbunge kutoka Bunge la Tanzania Mhe. Said Seleman Jaffo ameutaka uongozi mpya wa Bunge la nchi wanachama wa jumuiya ya kusini mwa Africa (SADC PF) kuendeleza mazuri yote yaliyoanchwa na uongozi unaomaliza muda wake ikiwa ni pamoja na kuzingatia matumizi bora ya fedha za Bunge hilo kwa wanachama kwa lengo la kuendeleza Bunge hilo.

  Mhe. Jafo aliyasema hayo hapa mjini Victoria Falls alipokuwa akisomo taarifa ya mapato na matumizi ya Bunge hilo kabla ya kukabidhi madaraka yake kwa uongozi mpya uliochaguliwa jumapili iliyopita tarehe 2 Novemba, 2014.

  Mhe. Jafo amesema, katika kipindi kifupi cha uongozi wake kama mweka hazina ndani ya Bunge hilo,  aliweza kuweka utaratibu madhubuti wa kuzibiti matumizi ya fedha kwa kuanzisha mfumo maalum uliosaidia kuhakikisha kuwa kila matumizi ya fedha ndani ya Bunge hilo yanakuwa ya wazi na yanadhibiti na kirahisi kutokana na mawasiliano yaliyopo:

  “ Mfumo huu umetusaidia sana kuleta uwajibikaji ndani ya Bunge hili na hasa katika kuhakikisha kuwa matumizi ya fedha yote ndani ya Bunge hayaidhinishwi na Sekretariati peke yake bali, Rais wa Bunge hili, Mweka Hazina pamoja kamati tendaji wanakuwa wanapata taarifa za matumizi ya fedha kupitia mtandao jambo ambalo si rahisi kwa mtu mmoja kufuja pesa kirahisi kwa kwa kuwa kila kitu kipo katika mtandao” alisema Mhe. Jafo.

  Mhe. Jafo amsema ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya uanzishwaji wa mfumo huu wa kisasa Bunge hilo limeweza kufanikiwa kuondoa mapungufu yote yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara kama vile upungufu wa fedha na kushindwa kufikia malengo  kutokana na ukosefu wa fedha.

  “ Napenda kuwafahamisha kuwa hadi kufikia mwezi machi, 2014, taarifa ya mkaguzi wa hesabu za Bunge hili zilikuwa zinaonyesha kuwa tunaupungufu wa fedha, lakini hivi ninavyowaambia mwezi huu November, kasoro hizo hamna tena bali tuna fedha zaidi ndani ya bajeti yetu ambazo ni zaidi ya Dola 824,000” aliongeza Mhe. Jafo.

  Akizungumza nje ya ukumbi baada ya kuwasilisha ripoti hiyo ya fedha na baadae kumkabidhi mweka hazina mpya mikoba ambaye ni Mhe. Gary Nkombo kutoka Zambia, Mhe. Jafo amesema uanzishwaji wa mfumo huo wa udhibiti wa matumizi ya fedha, sio tu umelisaida Bunge hilo bali umeipa sana heshima nchi yetu kwa kuwa utaratibu huu ni mpya na umeonyesha mafanikio ndani ya kipindi kifupi sana.

  Anasema zamani, viongozi walikuwa hawana mawasiliano ya moja kwa moja ya nini kinafanyika na fedha za Bunge lakini baada ya kuazishwa kwa mfumo huu kila kitu kipo wazi na hakuna anaweza kufishwa taarifa yoyote inayohusu fedha kama vile manunuzi, mikataba, mikopo, misaada na michango mbalimbali kutoka kwa wahisani nk.

  Mhe. Jafo alichukua nafasi ya uweka Hazina mwezi june mwaka huu baada ya aliyekuwepo katika nafasi hiyo Mhe. Dkt. Titus Kamani kuchaguliwa katika baraza la Mawaziri.
  Aliyekuwa mweka hazina wa Bunge la SADC ambaye pia ni Mbunge kutoka Bunge la Tanzania Mhe. Said Seleman Jaffo akizungumza kwenye mkutano huo.

  0 0  0 0

  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ndio mdhamini Mkuu wa mashindano ya Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa (Shimisemita) inayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro  hadi Novemba 11.


   Katika mashindano hayo NSSF imepata fursa ya kutoa elimu kuhusu Mafao mbalimabli yatolewayo na Shirika hilo ikiwemo Mango mpya kwa ajili ya Wakulima na Wachimbaji wadogo wa Madini.

  Katika mpango huo, Wakulima sasa wanaweza kujiunga na NSSF na kufaidika na Mafao mbalimbali yanayotolewa na NSSF. Pia Wakulima wanaweza kufaidika na mikopo mbalimbali ikiwemo mikopo ya pembejeo na Vifaa.


  Vilevile wakazi wa Mkoa wa Morogoro na wale kutoka Halmashauri mbalimbali Nchini wanaweza kupata elimu kuhusu uchangiaji wa Hiari, Kupitia Mpango huu.


  Wote walio katika sekta isiyo rasmi, wafanyakazi, wafanyabiashara wanaweza kujiunga na NSSF na kufaidika na Huduma  mbalimbali kama vile Mafao ya Matibabu na Mikopo kupitia SACCOS. 
  Ofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Marcel Amani (kulia), akimwelewesha mmoja wa washiriki katika mashindano ya SHIMISEMITA kuhusu Mafao ya muda mfupi yanayotolewa na NSSF yakiwemo mafao ya matibabu, mafao ya Uzazi pamoja na msaada wa mazishi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi. (Na Mpiga Picha Wetu)
  Wachezaji wa Mpira wa Kikapu wakichuana vikali katika mashindano ya SHIMISEMITA yaliyodhaminiwa na NSSF katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Morogoro. Tamasha hilo linahusisha michezo ya aina yote.
  Ofisa wa NSSF  Ahmed Aly akimwandikisha katibu wa SHIMISEMITA, Salehe Lubawa kuwa mwanachama mpya wa NSSF kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari (Hiari Scheme).

  Ofisa wa NSSF, Aisha Sango akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa washiriki wa michezo ya SHIMISEMITA, kuhusu Mpango mpya kwa ajili ya Wakulima (Wakulima Scheme) katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Morogoro.

  0 0  0 0

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaachia huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (Tanzania Petroleum Development Corporation – TPDC) Mh. MICHAEL PETRO MWANDA na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo JAMES ANDILILE kusubiri  ufafanuzi wa Bunge kutokana na tuhuma zinazowakabili. Awali, jana tarehe 03/10/2014 saa tano asubuhi katika ukumbi wa Bunge uliopo jijini Dar es Salaam katika chumba cha mikutano kulikuwa na kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mwenyekiti akiwa ni Mh. ZITTO ZUBERY KABWE (MB) na makamu wake ni Mh. DEO FILIKUNJOMBE (MB).

  Katika kikao hicho agenda ya mkutano ilikuwa ni kuwasilisha mahesabu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika kipindi kinachoishia tarehe 30 June, 2013. Baada ya majadiliano ya muda kuhusu hati mbalimbali zilizotakiwa na Kamati hiyo ya Bunge hatimaye Mwenyekiti wa Kamati Mh.  Zitto Zubery Kabwe alitoa maagizo kwa askari wa Polisi waliokuwepo katika eneo hilo kwa masuala ya ulinzi kuwa Mwenyekiti wa bodi ya TPDC na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wafikishwe kituo cha polisi Kati.

  Kutokana na maelezo ya mashahidi waliokuwepo kwenye tukio hilo katika ukumbi wa Bunge Mwenyekiti Zitto alisema wapelekwe Polisi waende kusubiri mwongozo wa Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye atawasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa maagizo ya mwisho. Mara baada ya agizo hilo watu hao walifikishwa kituo cha Polisi Kati chini ya ulinzi. 

  Uongozi wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ulishindwa kuchukua hatua zaidi ya hapo kwani shauri hilo halikuwa na mlalamikaji aliyekuja kufungua jalada na kutoa ufafanuzi kuhusu mashtaka yanayowakabili viongozi wa TPDC. Aidha, maafisa wawili wa secretarieti ya Bunge waliitwa Polisi kutoa ufafanuzi kuhusu kadhia hii wakiwepo pia mawakili wa watuhumiwa na hatimaye kilifanyika kikao cha dharura ili kupata ufafanuzi wa kisheria.

  Hatimaye iligundulika kwamba katika sheria ya HAKI, KINGA na MADARAKA ya Bunge sura ya 296 Kif 12 (3) kinaonyesha kwamba mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali alitakiwa kwanza apendekeze kwa Mhe. Spika wa Bunge juu ya jambo lolote aliloliona kama ni kosa. 

  Mhe. Spika akisharidhika kuhusu tuhuma zozote zilizoletwa mezani kwake na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, ndipo anamwandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili suala hilo lipate ufafanuzi wa kisheria ikiwa ni pamoja na hatua za kisheria zinazostahili kuchukuliwa. 

  Katika kikao hicho na jopo la wanasheria iligundulika kwamba katika sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya bunge, agizo la kukamatwa watu hao lililotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge  lilihita kuzingatiwa kwa taratibu tajwa hapo juu kwanza kabla ya utekelezaji wake. 

  Hatimaye ilionekana hakuna sababu ya kuendelea kuwashikilia viongozi hao na badala yake wameachiwa huru tukisubiri taratibu na sheria kama ilivyoelezwa hapo juu.


  S.H. KOVA
  KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
  DAR ES SALAAM

  0 0

  Kampuni inayojishughulisha na uboreshaji wa kuku Zanzibar, Zanchick, leo imetoa chanjo 600,000 zilizo na thamani ya Tshs 9,000,000 kwa wafugaji kuku kwa ajili ya kuwalinda kuku wao na ugonjwa wa Mdondo. Utoaji wa chanjo hizo ulifanyika kwa msaada wa wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar ambao wata ratibu na kusimamia zoezi zima.

  Meneja wa Uendeshaji, kutoka Zanchick, Bwana Christopher Kontonasios alisema: “Tunashukuru Wizara ya Ufugaji na Uvuvi kwa kuwa washiriki wakubwa katika kuratibu zoezi hili na tunataraji serikali itazidi kuwasaidia wazalishaji kuku wa kawaida, kwa kuondoa kodi ya kuagiza chakula cha kuku, jambo ambalo litawaruhusu wazalishaji wa kawaida kupata chakula bora cha kuku chenye bei nafuu.

  Hii ndio njia pekee ya kuwawezesha wakulima wa kawaida kuendeleza ufugaji wa kuku, kwa kiwango cha hali ya juu, na pia kuwaruhusu kukidhi biashara zenye faida.

  Mkurugenzi katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Yusuf Hajj Khamis alisema, “Tunafarijika na juhudi za Zanchick katika kuboresha uzalishaji wa kuku Zanzibar, hii ni hatua kubwa kwa wafugaji wa kawaida. Tunatarajia kuongeza juhudi katika kushirikiana kukuza viwango na jitihada za ufugaji kuku kisiwani hapa."

  Kirusi cha ugonjwa wa Mdondo kwa ujumla hakisababishi madhara yoyote kwa afya ya binadamu, lakini kina uwezo wa kuleta maafa makubwa kwa wafugaji wa kawaida, kwa kumaliza kiasi kikubwa cha kuku na hatimaye kuangamiza biashara yao.

  Msaada huu mkubwa na muhimu ni katika juhudi za Zanchick kufanya kazi na wafugaji wa kawaida ili kuongeza, kuboresha na kunadi uzalishaji wa kuku Zanzibar.
  Mkurugenzi wa Kampuni inayojishughulisha na uboreshaji wa kuku Zanzibar(Zanchick) Bw.Issa Khasim Issa akikabidhi chanjo 600,000 zenye thamani ya Tshs 9,000,000 kwa Naibu katibu katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Omar Ali Amir kwa ajili ya kuwalinda kuku na ugonjwa wa Mdondo, anayeshuhudia kulia Mkurugenzi katika kitengo cha kutoa huduma kwa wanyama kutoka Wizara ya Ufugaji na Uvuvi Zanzibar, Dr.Yusuf Hajj Khamis.

  0 0


  Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Profesa Jakaya Mrisho Kikwete mchana huu ataanza kuzungumza na Wazee wa Dodoma  katika ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma wakati wowote kuanzia sasa. Usikose kuangalia mazungumzo hayo ambayo tayari yanaoneshwa moja kwa moja kupitia: 

   TBC One pamoja na mtandao wa www.ikulu.go.tz

  IMETOLEWA NA KITENGO CHA 
  MAWASILIANO YA RAIS IKULU, DAR ES SALAAM

  NOVEMBA 4, 2014

  0 0

   MAKATIBU wa Kata wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Moshi Vijijini wametishia kubwaga manyanga na kurudisha kadi zao ikiwa Katibu wao wa Wilaya ataendelea na jitihada za kutaka kukigawa chama kwa kumuandaa mtu wake kwa ajili ya kugombea Ubunge mwaka 2015.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi hao ngazi ya kata katika wilaya ya Moshi vijijini, walisema migogoro na malumbano ndani ya CCM imekuwa chanzo cha wapinzani kushinda kiurahisi katika Jimbo la Vunjo.  Mmoja wa viongozi wa Makatibu hao ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema, lazima wanachama wa CCM wachague mtu wanayemtaka na siyo viongozi kuwachagulia mgombea.

    Wakizungumza mjini humo,makada hao ambao walikataa kutajwa majina yao kwa sababu za kuepusha malumbano, walidai kuwa  muda mrefu Katibu wao wa Wilaya amekuwa akifanya jitahada za kuhakikisha mtu wake anayemtaka anapita mwaka 2015.

  Mmoja wa viongozi hao ngazi ya kata, alisema Katibu wao wa Wilaya amekuwa hawasikilizi, huku akitumiwa na watu wenye fedha kuwapigia debe wagombea wao wanaowataka hususani katika kuwania ubunge mwakani.

  "Tumekuwa tukimshauri huyu Katibu wetu, lakini hatusikilizi na kuna mtu ambaye mwaka 2010, alikiyumbisha chama na sasa amerudi tena akiwa na mgombea wake na hali ikiendelea hivi chama kitashindwa tena mwakani'', alisema mmoja wa Makatibu Kata

  Alisema kuna kada ambaye anaandaliwa ingawa kwa sasa yupo nje ya wilaya hiyo ili aje kugombea ubunge na kwamba mpango  huo unaratibiwa na watu wenye fedha.


  Aliongeza kuwa wafanyabiashara wasiokitakia mema CCM wanataka wasimamishe mtu ambaye hakubaliki kwa lengo la kukiangusha ili wapinzani waweze kushindwa kiulaini..

  Mmoja wa mwanachana wa CCM, katika jimbo la Vunjo alisema, umefika wakati viuongozi kukaa pembeni na kwaachia wanachama wenyewe waamue kumpitisha mgombea wanayemtaka. Alisema CCM ni chama ambacho kinajali uhuru wa kila mtu, na umefika wakati vijana kupewa kipaumbele katika nafasi za uwakilishi ukiwamo ubunge hapo mwakani.

  Katibu wa CCM  katika wilaya ya Moshi Vijijini, Miriam Kaaya akizungumzia tuhuma hizo, alikanusha madai ya viongozi hao wa Kata na kusema kwamba malalamiko yote yanajadiliwa ndani ya vikao. Alisema hana mgogoro wowote na makada wenzake wa CCM na kwamba siku zote amekuwa akitaka kila mtu anayestahili haki aipate bila mizengwe.

  Alisema hana mpango wa kumbeba mgombea yoyote kwa kuwa muda wa kutafuta wagombea haujafika na kwamba hivi sasa wanashughulika na chaguzi za serikali za mitaa.


  0 0

  Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Miundombinu wamefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata (km 64), inayojengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hii inaunganika na barabara kuu ya Dar es salaa – Chalinze – Arusha katika eneo la Msata. Hivyo ni njia mbadala ya kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya kanda ya Kaskazini na nchi jirani ya Kenya.

  Barabara hii inayojengwa na kampuni ya Estim Construction ltd, na kusimamiwa na mhandisi mshauri kampuni ya JBG Gauff Ingenieure GMBH & Co. Mkandarasi wa barabara hii ya Bagamoyo – Makofia – Msata anatarajia kukabidhi barabara hii Machi, 2016.

  Aidha, kamati hiyo ilipata nafasi ya kutembelea mizani ya kisasa iliyopo eneo la Vigwaza inayojengwa na kampuni ya M/S China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) na mhandisi mshauri kampuni ya Ambicon Engineering Ltd of Tanzania. 

  Mradi huu hadi sasa umekamilika kwa asilimia 95. Ikiwa ni kukamilika kwa barabara ya maingilio, maegesho ya magari, majengo, ofisi, gereji na jenereta, vyoo vya wasafiri pamoja na mizani. 

  Mradi huu unakamilika Novemba 2014. Kwa habari zaidi tazama picha za ziara hiyo.(Imetolewa na kitengo cha mawasiliano serikalini – Wizara ya Ujenzi)
  Naibu waziri wa Ujenzi Mhe. Gerson Lwenge (Mb) akiwasili eneo la mradi akiambatana na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Peter Serukamba.
  Wajumbe wa kamati ya bunge ya Miundombinu wakipata taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya lami Bagamoyo – Makofia – Msata (Km 64) kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale.
  Ramani ya mchoro ambao barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata itaungana na barabara ya Dar es salaam – Bagamoyo.


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Dodoma Balozi Job Lusinde wakati wa mkutano na wazee wa mji wa Dodoma leo  waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wazee wa mji wa Dodoma leo waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.
  Sehemu ya wazee wakati wa mkutano wao na Rais Kikwete mjini Dodoma  waliouitisha ili kuzungumza naye maswala kadhaa ya maendeleo.


  0 0  0 0


  0 0


  Ni Used Noritsu 3501. Ina uwezo wa kuprint size zifuatazo: 
  4×6,5×7, 6×8, 8×10 and 8×12

  Kwa mawasiliano piga no 0684472115 

  0 0
 • 11/04/14--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Marijani Rajabu - Dunia sasa imani imekwisha

  0 0
 • 11/04/14--19:25: Article 17


 • 0 0

  Bondia Iddi Pialali kushoto akipambana na Fadhili Mkunda wakati wa mpambano wao wa kuwania ubingwa wa kanda ya masharika.Mpambano uliofanyika Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani,  Pialali alishinda kwa K.o ya raundi ya tano na kutwaa ubingwa huo .
  Bondia Iddi Pialali kushoto akipambana na Fadhili Mkunda wakati wa mpambano wao wa kuwania ubingwa wa kanda ya masharika mpambano uliofanyika Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani,  Pialali alishinda kwa K.o ya raundi ya tano na kutwaa ubingwa huo.
  Bondia Iddi Piyalali akiwa na mkanda wa ubingwa wa Kanda ya Mashariki Picha na SUPER D BLOG

  0 0

  Bw. Noel Kaganda, Afisa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York; na Bw. Suleiman Saleh, Afisa katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Washington D.C wakiwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha La Verne cha California waliotembelea Ubalozi wa Tanzania Washington D.C. kujifunza namna Tanzania inavyoshiriki katika Umoja wa Mataifa. Wanafunzi hao walipeperusha bendera ya Tanzania katika National Model United Nations (NMUN), iliyofanyika kuanzia tarehe 31 Oktoba hadi 2 Novemba 2014, huko Washington D.C. 
  Bw. Kaganda, akiwasilisha mada kuhusu ushiriki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na vipaumbele vya nchi katika vyombo, kamati, kamisheni, bodi na mikutano ya nchi wanachama wa mikataba mbalimbali ya Umoja wa Mataifa. 

  Programu ya NMUN inatoa fursa kwa wanafunzi wa vyuo zaidi ya 5000 kutoka pembe zote za dunia kuvaa kofia za Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia, ikiwemo migogoro, mabadiliko ya tabianchi, maafa, janga la umaskini, magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza na usawa na uwiano sawa wa kijinsia. Mafunzo haya kwa vitendo yanawajengea uelewa wa shughuli za Umoja wa Mataifa na  kuwapatia kionjo cha shughuli za kidiplomasia.
  Washiriki wakifuatilia kwa makini mada inayowasilishwa. Pamoja na taarifa za kiuwakilishi katika Umoja wa Mataifa, wanafunzi hao walipata wasaa wa kufahamu misingi na mikakati ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania iliyojikita katika kuendeleza mahusiano ya kiuchumi na kibiashara na kukuza fursa za uwekezaji. 

  Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa zinaendelea kupokea wanafunzi kutoka shule na vyuo mbalimbali vya Marekani ambavyo vimeonesha kiu ya kupata uelewa wa shughuli za kidiplomasia na habari za vivutio vya kiutalii vilivyopo nchini. 


  0 0

  BAADA ya matukio ya harusi ya Jumamosi iliyopita natoa onyo ole wake atakayeniomba mchango wa harusi, sitaki utani. Labda kwanza nikueleze jinsi tulivyopata misukosuko sana kwenye uchangiaji wa ile harusi, maana siku hizi hakuna pa kukimbilia, kila asubuhi unaamshwa saa kumi na mbili na meseji kwenye simu;

  “Ndugu rafiki na jamaa wa familia ya Pingapinga inakukumbusha kuwa harusi ya mtoto wao imekaribia hivyo mchango wako unahitajika”, baada ya wiki  meseji huwa kali zaidi;“Siku zinaisha kwa nini hautoi mchango, unajua familia ya Pingapinga ina shughuli ya harusi ya mtoto wao, toa upesi au la usitulaumu.”

  Basi hizi meseji zilikuwa nyingi kuliko zile za kampuni yangu ya simu inayobuni namna ya kunitoa mkwanja kila wiki. Hatimaye nikatoa faini, maana nisiite mchango, maana mchango haulazimishwi.
  Sasa Jumamosi ndiyo ikawa siku ya harusi, kadi nililetewa mapema , nikahakikisha koti langu la kuendea harusini nalicheki vizuri, maana haya makoti yanayokaa kabatini miezi ni muhimu kucheki vizuri maana unaweza kukuta panya kazalia kwenye mfuko halafu wakatimka kutoka  kwenye makazi yao wakati uko katikati ya kucheza mduara wa harusi.

  Kweli tukaingia ukumbini viti vilikuweko swafi, meza zimepambwa kwa maua na MC alitukaribisha kwa maneno mengi yaliyojaa vichekesho visivyochekesha, au vichekesho vingine vimesharudiwa na kila MC hapa mjini halafu akawa analazimisha watu wapige vigelegele! Yote bure watu walikuwa wamenuna maana hakukuwepo na dalili ya hata chupa moja ya kinywaji, ila ahadi kibao zikawa zinatolewa na MC, mara ‘Roli la bia linakuja toka breweries, mara shampeni leo inatoka Ufaransa kwa helikopta.”

  Ghafla wahudumu waliovalia vikofia kichwani wakapitisha sambusa mojamoja kwa kila mtu, wakisindikizwa na MC akituhamasisha tule tufurahi na bwana harusi. Kwa kweli hela yangu ikaanza kuniuma, kwanza nililazimishwa kulipa, halafu sioni chochote hawa jamaa vipi? Wakati ukumbi mzima ukiwa umeendelea kununa utadhani kikao cha msiba, MC akatuambia eti bwana harusi ana machache kabla ya kutuaga kwenda kupumzika na mkewe. Pamoja na kisirani tulikuwa na hamu kumsikia mshenzi huyu anataka kusema nini.

  Bwana harusi akasimama hata suti aliyovaa ilikuwa haijamkaa sawasawa, akakohoa kidogo akaanza, “Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu, kiukweli hapa nimepata mke mtulivu, mpole asiye na makeke, yaani najisikia nina bahati sana.

  “Naomba niwashukuru wakwe zangu kwa kukubali kupokea robo tu ya mahari na kuruhusu ndoa hii ifanyike. Pia nishukuru kwa zawadi zao za kitanda, godoro, kabati na makochi asante sana.  Naomba nimshukuru baba mwenye nyumba wangu kwa kukubali niwe na deni la kodi ya mwaka ili kufanikisha harusi hii, mzee upo juu.

  “Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii, pia wafanyakazi wenzangu kwa zawadi yenu ya jiko la gesi. Namshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa mtengeneza keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana.


  “Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante kwa akina mama jirani kwa kuja na sambusa mlizokula toka makwao ili kufanikisha harusi hii, mradi harusi hii ni furaha tupu. “MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali tulipane kidogokidogo aksante sanaaaaa

  0 0

   Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za uzalishaji Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdullah Makame akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Zanzibar Salum Maulid Salum (kati kati) kufungua warsha ya utaarishaji mkakati Itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wakwanza (kushoto) Makamu wa Rais wa Chamber of Commerce Zanzibar Ali Aboud Mzee.
   Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Zanzibar Salum Maulid Salum akifungua mkutano huo unaofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resourt Mbweni Wilaya ya Magharibi Zanzibar.
   Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria ufunguzi wa Warsha ya utaarishaji mkakati Itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo Zanzibar Beach Resourt Mbweni.
   Baadhi ya washirki wa warsha ya utaarishaji mkakati Itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakimsikiliza Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora alipokuwa akifungua warsha hiyo.
   Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha hiyo na Mgeni rasmi Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu na Utawalaq Bora Salum Maulid Salum (wa katikati) waliokaa. 

older | 1 | .... | 629 | 630 | (Page 631) | 632 | 633 | .... | 3284 | newer