Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

ZIETLOF AVUNJA REKODI NYINGINE YA DUNIA AKIWA TANZANIA

0
0


 Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiwa na Meneja mkuu wa Alliance Autos Bwana Wayne Mcintosh(wa pili toka kulia)wakipata picha ya pamoja na wanahabari
 
Meneja Mkuu wa Alliance Autos Wayne Mcintosh(kushoto) Akipata picha na Dereva Toka  Nchini Ujerumani Rainer Zietlof


 Meneja Masoko wa Alliance Autos Tharaia Ahmed(kushoto)akipata picha na Dereva Rainer Zietlof



Meneja mkuu wa Alliance Autos Bwana Wayne Mcintosh akisoma cheti cha rekodi ya dunia alichopewa dereva toka ujerumani 
-----------------------------------------

DEREVA raia wa Ujerumani Rainer Zietlof yuko mbioni kuvunja rekodi ya dunia ya kuendesha gari kwa kilometa 17,000 kutoka Ulaya hadi Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Zietlof alisema kuwa hiyo itakuwa ni rekodi yake ya tatu baada ya zile za awali alizovunja mwaka 2011 na 2012.
Awali alivunja rekodi baada ya safari iliyojulikana kama 'Panamerica'ambayo ilimchukua kutoka Tierra del Fuego hadi Alaska kwa siku 11 na saa 17 wakati ile ya 'Russtralia' ilimtoa Melbourne, Australia hadi St.Petersburg nchini Urusi ambako alitumia saa 18.
Zietlof anayetumia gari aina ya VW Touareg V6 TDI alianza rasmi safari yake Septemba 21 mwaka huu huko North Cape nchini Norway na anatarajia kuikamilisha nchini Afrika Kusini, ambako atakuwa ametembea kwa kilometa 17,000.
Kwa mujibu wa dereva huyo, safari hiyo ndefu imempitisha katika nchi za Norway, Finland, Sweden, Denmark, Ujerumani, Jamhuri ya Czech, Slovakia, Hungary, Serbia, Bulgaria, Uturuki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya na sasa Tanzania.
Dereva huyo alizungumza na wandishi wa habari katika makao makuu ya Alliance Autos iliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa atachangia kiasi cha senti 20 za euro kwa kila kilomita, kwa vijiji nchini Tanzania na Zambia.
Mbali na kuahidi kuvichangia vijiji hivyo, Zietlot pia amesisitiza kuvitembelea vijiji hivyo atakavyo vichangia.
Aidha, amelisifia gari hilo kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na mazingira tofauti tofauti ya hali ya hewa kama baridi kali na joto pamoja na barabara mbovu.
Mradi huu wa kuzunguka sehemu mbalimbali za dunia kwa gari hilo umedhaminiwa na makampuni makubwa ya magari ya Tehama na Volkswagen nchini Ujerumani, Slovakia na Afrika Kusini.
Katika safari hiyo Zietlow yuko na wasaidizi wake wawili, Marius Biela ambaye ni mpiga picha na mchukua video huku Matthias Prillwitz ni mzoefu wa mbio
za magari nchini Ujerumani.

Dereva huyo alianza safari zake za barabarani mwaka 2005 na ameoa na ana mtoto mmoja. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA.

TAARIFA YA MSIBA

0
0
Familia ya Stambuli inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao Idrissa Stambuli (32) kilichotokea Jumatatu tarehe 03/11/2014 huko Tanzania. Mazishi yatafanyika Jumatano tarehe 5/11/2014 baada ya salatul dhuhri huko Mbagala, Dar es salaam, Tanzania. 
Kwa hapa Marekani msiba upo nyumbani 
17 Walsh Street, 
Springfield, 
Massachusetts 01109. 
Tutafanya kisomo cha kumuombea marehemu Jumamosi Novemba 8, 2014 kuanzia saa kumi jioni (4pm) mpaka saa Tatu usiku (9pm) katika 
Masjid Al Baqi 
148 Fort Pleasant Avenue, 
Springfield, 
Massachusetts 01118 
Kama ilivyo desturi yetu unaweza kutoa mkono wa pole kwa wafiwa kwa
 mama mzazi wa marehemu 413 783 3069 
Dada wa marehemu Zaidani Stambuli na mumewe 
Wally Masesa 413 272 5036 
Kwa taarifa zaidi wasiliana na Baraka Baraka 413 285 4544 
Maria Sombe 413 364 8146 
Hidaya Masesa 413 737 7186

Balozi Mpya wa Norway aKukutana na Dk.Shein Zanzibar

msanii chipukizi angel magoti atia fora na wimbo wake wa "say no to corruption"

Shukrani za DJ John Dilinga kwa wadau

0
0
Big up na special thanks zifike kwa marafiki Juma Rajabu wa Max malipo, Mwinchade Chambuso wa hella investment, Richard Orombe wa hot shot production, Robby wa Robby One Fashion, Bakari Madega wa Rangers bureau de change, Harisday na Evance Bukuku kutoka event light, Muhidini Michuzi wa Michuziblog, Radio One Mtaa wa Mangoma, East Africa Radio pamoja na E fm kwa kuthubutu kuiboost THE LEGEND 2nd anniversary kwa moyo mmoja na bila kipingamizi chochote kile. 

Sina maneno ya kuweza kuelezea faraja gani niliyonayo moyoni except to say, thank you very much and God bless you. 
John Dillinga Matlou aka THE LEGEND

Dodoma Kaa Tayari 8 Novemba Kwa Nyama Choma Festival/ Dar 6 December

tangazao la msiba musoma

0
0
Bwana Abiud Maregesi wa Kijitonyama Dar Es Salaam, anasikitika kutangaza kifo cha Mama yake mzazi, Mama Martha Maregesi, kilichotokea Jumanne, tarehe 04 Novemba 2014 katika Hospital ya Rufaa ya Musoma.  
Mazishi yatafanyika Alhamisi tarehe 06 November 2014 kijiji Seka Majita Musoma.  Habari ziwafikie Ndugu, Jamaa na Marafiki popote walipo.

UDA yawanoa madereva, makondakta kuleta ufanisi

0
0
Fundi wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) akifanyia marekebisho moja ya mabasi ya shirika hilo.
 

Wakazi wa Dar es Salaam wataanza kupokea huduma zilizoboreshwa zaidi kila watakapotumia mabasi yanayomilikiwa na Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), hii inatokana na mafunzo ya mwezi mmoja yanayotolewa na shirika kwa madereva, makondakta pamoja na wafanyakazi wengine wa shirika hilo.

Akizungumza wakati wa ziara fupi ya waandishi wa habari katika makao makuu ya UDA jijini Dar es Salaam Jana, Mkuu wa kitengo cha mahusiano ya umma wa UDA, Bw.  George Maziku alisema kuwa miongoni mwa mambo mengine, kampuni yake imejikita katika utoaji wa mafunzo madhubuti kwa wafanyakazi wake ili kuboresha huduma zote zinazotolewa kwa wateja wa UDA.

“Uongozi wa UDA unalichukulia kwa uzito mkubwa sana suala la usalama. Tumeupitia mtaala wa utoaji elimu kwa wafanyakazi wetu lengo likiwa ni kuboresha usalama na kufanya wateja wetu wafurahie huduma zinazotolewa na shirika. Tunatoa mafunzo haya kwa madereva wetu ili kuinua hali yao ya uzingatiaji wa usalama,” alisema Maziku.  

Mbali na masuala ya usalama, mkuu huyo wa kitengo cha uhusiano aliahidi uboreshaji wa huduma kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuwajali wateja, suala ambalo limekua likizua mjadala mkubwa.

Bw. Maziku alisema kuwa kampuni yake ina mabasi yapatayo 400 jambo linayoifanya UDA kuwa kampuni ya kwanza Tanzania kuwa na magari mengi yanayofanya kazi kwa mkupuo, hivyo kuna uhitaji mkubwa sana wa kuweka viwango thabiti ambavyo vinaweza kuigwa na makampuni mengine.

“Tunalenga kuwa na mabasi 3000 ifikapo mwakani lakini kikubwa zaidi kabla hata ya kupata idadi hiyo ya mabasi ni kuwapa mafunzo madereva wetu ili wawe na elimu ya kutosha na uzoefu wa kutosha katika sekta ya usafirishaji wa umma.

“Kwa kulitambua hili, kampuni imeajiri wakufunzi kutoka ndani na nje ya nchi, ili kutoa mafunzo kwa madereva wetu na wafanyakazi wengine wanaojihusisha na usafirishaji, mafundi na wafanyakazi wote (hasa makondakta) katika kuwajali wateja,” alisema.

Bw. Maziku alisema kuwa mbali na mafunzo hayo, kampuni imekuwa ikifuatilia kwa karibu sana tabia na  mienendo ya madereva na makondakta wake mara kwa mara kwa kuwatumia wasimamizi ambao hupanda mabasi ya kampuni hiyo bila ya makondakta na madereva kupewa taarifa.

Kwa sasa, mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na kampuni hapo awali, yameonyesha kuzaa matunda yaliyotarajiwa kwa kuwabadilisha baadhi ya madereva na makondakta wa kampuni hiyo.

Hii ilibainika baada ya mkazi wa Dar es Salaam, ambaye amekuwa akitumia huduma za UDA kwa nyakati tofauti, Bw. Andrew Sanga , kukiri kuwa madereva wa UDA wapo tofauti ukilinganisha na madereva wengine wa mabasi ya abiria.


“Ilikuwa ni adha kubwa kutumia usafiri wa umma kutokana na huduma mbovu ambazo abiria tulikua tukikumbana nazo. Madereva wengi wa abiria hawazingatii suala la usalama barabarani. Wanaendesha hovyo  bila kujali kuwa kuna watumiaji wengine wa barabara. Lakini nina furaha kusema kuwa madereva wa UDA wapo tofauti sana na wenzao,” alifafanua.

SHUKURANI TOKA FAMILIA YA MAREHEMU MZEE ANGULILE MWASUMBWE WA TUKUYU

0
0
Kwa niaba ya familia ya mzee Angulile Mwasumbwe wa Kanyelele Tukuyu Mbeya, tunawashukuru ndugu, marafiki na jamaa zetu wote walioungana nasi kwa hali na mali katika msiba wa baba yetu uliotokea 23/09/2014. 
Mungu hatawapungukia wala kuwaacha.
 Tunamtukuza Bwana awezaye kutufanyia mambo ya ajabu kuliko vile tuwazavyo na tuombavyo (Efeso 3:20); tunamtukuza Mungu kwa kumtwaa Baba yetu katika uzee mwema - Marehemu ameishi miaka 100 kamili (1914 - 2014)
Mbarikiwe Mungu aliye Juu na jina la Bwana lihimidiwe!
 Michael Mwasumbwe Angulile
Marehemu Mzee Angulile Mwasumbwe enzi za uhai wake
Mdau Michael Angulile Mwasumbwe akiwa na babayake enzi alipokuwa hai
Michael na baba
Wakati wa mazishi huko kijijini Manyele, Tukuyu, Mbeya

BENKI YA CRDB YASHIRIKI KONGAMANO LA VIJANA LA BIASHARA LILILOANDALIWA NA TAASISI YA AIESEC JIJINI ARUSHA

0
0
Jumla yaVijana 150 kutoka ndani na nje ya nchi wameudhuria Kongamano la Biashara kwa Vijana lililofanyika jijini Arusha ambapo Benki ya CRDB wakiwa ni miongoni mwa wadhamini wa  kongamani hilo.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na Vijana kutoka katika Vyuo Vikuu vya nchi za Afrika Mashariki na kuandaliwa na Taasisi ya AIESEC ambalo hujihusisha na ubunifu wa vipaji vya uongozi miongoni mwa vijana lililofanyika jijini Arusha hivi karibuni katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Hall CDTI- TENGERU, Arusha ambalo lilihudhuriwa na wanafunzi 150 kutoka nchi tofauti za kimataifa na 150 kutoka vyuo vya elimu ya juu ndani ya Tanzania.
Benki ya CRDB kama miongoni mwa makampuni yaliyodhamini kongamano hilo, ilialikwa kuweza kutoa elimu juu ya “Teknolojia na Ubunifu” ambapo  Mkurugenzi wa mikakati na ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini aliweza kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi walengwa.
 Katika kongamano hilo washiriki walipata nafasi ya kuelemishwa kuhusu huduma za kibenki kwa njia ya kieletroniki zilizotolewa na Mangire Kibanda (Meneja huduma za kibenki kwa njia ya kielektroniki) ambaye alitoa elimu kuhusu huduma za kibenki kwa njia ya simu (SimBanking), kwa njia ya Internet (Internet Banking), mashine za mauzo (Pos), Wakala wa Benki (FahariHuduma).
Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akitoa mada kuhusu teknolojia  na ubunifu.
Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akitoa mada.
Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akijibu maswali ya wanafunzi.
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Alma Ally (kushoto) akifafanua jambo kuhusu akaunti ya Scholar ambayo ni maalumu kwa wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi wakipata elimu kuhusu huduma za kibenki.
Meneja wa Huduma za Kibenki za Kieletroniki, Bw. Mangire Kibanda (kulia) akitoa elimu kuhusu huduma za kibenki za kielectroniki kwa njia ya simu (SimBanking), kwa njia ya Internet (Internet Banking), mashine za mauzo (Pos), Wakala wa Benki (FahariHuduma) kwa wanafunzi waliohudhuria kongamano hilo.
Baadhi ya wanafunzi wakipata elimu kuhusu huduma za kibenki zitolewazo na Benki ya CRDB.
Wanafunzi kutoka vyuo vya nchi za Afrika Mashariki na Kati wakisikiliza mada kutoka kwa Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini (hayupo pichani).
Ofisa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Bw. Petro Kasindya (kulia), akitoa ufafanua kwa walengwa kuhusu mfumo wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB. 

MUWSA YASAMBAZA BOMBA ZA MAJI MRADI MKUBWA WA MAJI MTO KARANGA

0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

TATIZO la upungufu wa maji katika Manispaa ya Moshi linaelekea kuwa historia ifikapo mwezi Desemba mwaka huu kufuatia kukamilika kwa utekelezaji wa  mradi mkubwa wa maji uliopo katika chemchem ya Mto Karanga ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni 382.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira ( MUWSA), Mhandisi Cyprian Luhemeja amefafanua kuwa, mradi huo utakapokamilika utahudumia maeneo ya Bomambuzi, Pasua , Matindigani na meneo ya katikati ya mji.

Mhandisi Luhemeja amesema maeneo hayo kwa sasa yana mgawo wa maji kutokana na uwepo wa maji kidogo ambapo pindi mradi huo utakapokamilika utawezesha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa maji katika maeneo hayo kwa saa 24.

Amesema mradi huo utasaidia kuongeza  kiwango cha upatikanaji wa maji kwa mita za ujazo zipatazo 2,592 kwa siku katika mfumo wa kusambazia maji ambapo kwa sasa umeshakamilika kwa asilimia 99.

Amefafanua kuwa gharama za mradi huo ni kubwa lakini gharama za uendeshaji ni ndogo kutokana na chanzo cha maji hayo kutoka katika chemchem ya mto karanga ambapo itasaidia upatikanaji wa maji saa 24.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA ,Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwaonesha wanahabari chanzo cha maji kilichopo Mto Karanga .
Wanahabri wakipita juu ya Bomba zilizoanza kusambazwa kutoka katika chanzo cha maji cha Mto Karanga.

COURT ALLOWS WITHDRAW OF A TANZANIAN RESIDENT’S APPLICATION AGAINST THE GOVERNMENT OF KENYA AS IT RESUMES SESSIONS

0
0
The East African Court of Justice 5th November 2014: The First Instance Division yesterday resumed its month long sessions and granted leave to withdraw an Application filed by a Tanzanian resident, Mr. James Alfred Koroso, seeking an interim order that the Government of Kenya does deposit the amount of Kshs 28,475,737 being the decretal amount awarded to the Applicant by the High Court of Kenya.

The Applicant sought leave of Court to withdraw the application under Rule 51(b) of the Rules of Procedure of the East African Court of Justice which provides that, “An Applicant or a claimant may discontinue its reference or claim against all or any of the respondents or may withdraw any part of the Reference or claim; and the respondent may in similar manner discontinue or withdraw its counter claim”.

Counsel for the Applicant told the Court that he should be allowed to withdrawal the Application because the prayers that sought will be addressed with in the main Reference.

The Court therefore declared the Application as withdrawn and ordered the costs to abide the outcome of the main Reference.

The subject of the main Reference (Case) is that the Applicant (Alfred Koroso) a businessman from Moshi, Tanzania, was arrested and placed in custody at Taveta Police Station in Kenya on 17 December 1993 under charges of robbery with violence.  The Applicant was acquitted on 7 December 1995 after a not guilty verdict. The Applicant thereafter filed a case in the High Court Kenya in Nairobi on 15 November 1996 for payment of damages for wrongful arrest, confinement and prosecution by the Government of Kenya. His claim was successful and the High COurt of Kenya ordered compensation of Kshs 21,000,000 plus interest and cost be paid to Mr. Koroso (the Applicant). 

The Applicant claims that the amount awarded to him was supposed to be paid within 30 days from the Date of the judgment of the High Court of Kenya on 25th March 2013 but it has never been paid to date.

Mr. Koroso (the Applicant) therefore alleges that the refusal, failure and frustration of the decree by the Government of Kenya is an infringement of Articles 6 (d) and 7 (2) of the Treaty for the Establishment of the East African Community.

He further alleges that he has continued to suffer and is incurring more damages and he is therefore claiming the said decretal sum and an additional amount of Kshs 5,086,465 as liquidated damages.

The Reference will be heard  at a later date.

The Counsels present in Court were Mr. Selemani Kinyunyu Lawyer for the Applicant and Mr. Charles Mutinda Princple Litigation representing the Attorney General of Kenya both appeared before the Bench of the First Instance Division, Honourable Justices, Jean Bosco Butasi (Principal Judge), Isaac Lenaola Deputy (Principal Judge), Dr. Faustin Ntezilyayo, Lady Justice Monica Mugenyi and Justice Fakihi A. Jundu in open Court.

EACJ Rules Of Procedure
Rule 51 (1) Provides that;  An Applicant or a claimant may discontinue its reference or claim against all or any of the respondents or may withdraw any part of the Reference or claim; and the respondent may in similar manner discontinue or withdraw its counter claim”.

EAC Treaty
Article 6 (d) of the Treaty provides that, good governance including adherence to the principles of democracy, the rule of law, account ability, transparency, social justice, equal opportunities, gender equality, a s well a s the recognition, promotion and protect ion of human and peoples right s in accordance with the provisions of the African Charter on Human and Peoples’ Rights;

Article 7 (2) provides that; The Partner States under take to abide by the principles of good governance, including adherence to the principles of democracy, the rule of law, social justice and the maintenance of universally accepted standards of human rights.

ZIARA RASMI YA RAIS KIKWEETE NCHINI CHINA - SEHEMU YA KWANZA

BENKI YA CRDB YASHIRIKI KONGAMANO LA VIJANA LA BIASHARA LILILOANDALIWA NA TAASISI YA AIESEC JIJINI ARUSHA

0
0
Jumla yaVijana 150 kutoka ndani na nje ya nchi wameudhuria Kongamano la Biashara kwa Vijana lililofanyika jijini Arusha ambapo Benki ya CRDB wakiwa ni miongoni mwa wadhamini wa  kongamani hilo.


Kongamano hilo lilihudhuriwa na Vijana kutoka katika Vyuo Vikuu vya nchi za Afrika Mashariki na kuandaliwa na Taasisi ya AIESEC ambalo hujihusisha na ubunifu wa vipaji vya uongozi miongoni mwa vijana lililofanyika jijini Arusha hivi karibuni katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Hall CDTI- TENGERU, Arusha ambalo lilihudhuriwa na wanafunzi 150 kutoka nchi tofauti za kimataifa na 150 kutoka vyuo vya elimu ya juu ndani ya Tanzania.


Benki ya CRDB kama miongoni mwa makampuni yaliyodhamini kongamano hilo, ilialikwa kuweza kutoa elimu juu ya “Teknolojia na Ubunifu” ambapo  Mkurugenzi wa mikakati na ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini aliweza kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi walengwa.


 Katika kongamano hilo washiriki walipata nafasi ya kuelemishwa kuhusu huduma za kibenki kwa njia ya kieletroniki zilizotolewa na Mangire Kibanda (Meneja huduma za kibenki kwa njia ya kielektroniki) ambaye alitoa elimu kuhusu huduma za kibenki kwa njia ya simu (SimBanking), kwa njia ya Internet (Internet Banking), mashine za mauzo (Pos), Wakala wa Benki (FahariHuduma).
Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akitoa mada kuhusu teknolojia  na ubunifu.
Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Bw. Goodluck Nkini akijibu maswali ya wanafunzi.
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Alma Ally (kushoto) akifafanua jambo kuhusu akaunti ya Scholar ambayo ni maalumu kwa wanafunzi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO


DCB yatoa msaada wa vifaa vya maabara kwa ajili ya Shule ya Sekondari Kinyerezi

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymund Mushi (wa pili kulia), akipokea sehemu ya msaada wa vifaa vya maabara kwa ajili ya Shule ya Sekondari Kinyerezi, kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Plc, Edmund Mkwawa, wakati wa makabidhiano yaliyofanyika Dar es Salaam juzio. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Judith Charamila na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Balozi Paul Rupia.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA MITAJI HISA JIJINI DAR

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa TPSF, Dkt. Reginard Mengi, wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Novemba 5, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaji Hisa, lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta isiyo rasmi ya TPSF.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaji Hisa, lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta isiyo rasmi ya TPSF, lililofanyika leo Novemba 5, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo waliohudhuri ufunguzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia.

Madereva watakiwa kutotumia simu wakati wanaendesha vyombo vya moto

0
0
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani nchini Kamanda Mohamed Mpinga,amewataka madereva nchini kuzingatia sheria za barabarani na kuacha tabia ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.

Kamanda Mpiga, alitoa wito huo leo katika hafla ya kupokea pete maalum kutoka kampuni ya Vodacom ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayojulikana kama “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya magari kuacha matumizi ya simu wanapokwa wanaendesha.

Pete hizo maalum ni za kuvaa kwenye kidole gumba ambapo madereva wanatakiwa kuzivaa wakiwa wanaendesha magari yao ili kuwakumbusha pindi wanapotaka kutumia simu

Alisema madereva wakizingatia sheria za barabarani  kwa kiasi kikubwa ajali zinazoendelea kutokea kila siku zitapunga na aliipongeza kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania na kampuni ya mafuta ya puma kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu.

Kwa upande wake,Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia alisema kampuni yao itaendelea kuunga mkono jitihada za kuondoa  matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.”Tunaomba madereva kufuata sheria za barabarani kwa usalama wenu na watumiaji wengine wa barabara.

Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu  ya mkononi  kupitia kampeni ya Wait to Send.Mbali na kampeni hii hii alisema kwa mwaka huu kampuni ilidhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.
Kamanda wa polisi wa usalama barabarani Mohamed Mpinga(katikati)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla maalumu ya kikabidhiwa stika na pete za kuvaa kwenye kidole gumba kwa madereva zenye ujumbe wa”wait to send” ukiwa na maana ya wateja wa simu za mkononi wasitumie simu zao za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo vya moto. kampeni hiyo imeanzishwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la usalama barabarani kupambana na janga la ajali barabarani.kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia na kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya mafuta ya puma Philippe Corsaletti.
Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(kushoto)akimkabidhi stika Kamanda wa polisi wa usalama barabarani Mohamed Mpinga wakati wa hafla maalumu ya kikabidhiwa stika hizo na pete za kuvaa kwenye kidole gumba kwa madereva zenye ujumbe wa”wait to send” ukiwa na maana ya wateja wa simu za mkononi wasitumie simu zao za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo vya moto. kampeni hiyo imeanzishwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la usalama kupambana na janga la ajali barabarani nchini.
Kamanda wa polisi wa usalama barabarani Mohamed Mpinga,akionesha stika alizokabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(kushoto) wakati wa hafla maalumu ya kikabidhiwa stika na pete za kuvaa kwenye kidole gumba kwa madereva zenye ujumbe wa”wait to send” ukiwa na maana ya wateja wa simu za mkononi wasitumie simu zao za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo vya moto. kampeni hiyo imeanzishwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la usalama barabarani kupambana na janga la ajali barabarani nchini.
Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kushoto) na Kamanda wa polisi wa usalama barabarani Mohamed Mpinga wakionesha pete zenye ujumbe wa”wait to send” wakati wa hafla maalumu ya kikabidhiwa stika na pete hizo za kuvaa kwenye kidole gumba kwa madereva zenye ujumbe huo wenye maana ya wateja wa simu za mkononi wasitumie simu zao za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo vya moto. kampeni hiyo imeanzishwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la usalama kupambana na janga la ajali barabarani nchini.

Irene Kiwia alivyoiwakilisha Tanzania katika moja ya Mikutano ya Umoja wa Mataifa

0
0
Rais wa Taasisi ya kijamii ya Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (Tanzania Women of Achievement ),Bi. Irene Kiwia (wa pili kushoto) akizungumza kwenye moja vikao vya Mkutano wa  69 wa Umoja wa Mataifa (Unga) kwa kushirikiana na Clinton Global Initiative (CGI) uliofanyika mwezi uliopita nchini Marekani.Bi. Kiwia alipata nafashi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye Mkutano huo uliokuwa na ukijadili maswala mbali mbali ya wanawake na maendeleo, swala ambalo liko karibu sana na kazi zake akiwa kama mmoja wa Wanadiplomasia wa mambo ya Afya Ulimwenguni.Wengine pichani ni Bi. Sheila Tlou (Mwakilishi wa UNAIDS Mashariki na Kusini mwa Africa),Bi. Catharine Taylor (MSH),Bi. Kate Gilmore (UNFPA). 
Sehemu ya Wadau wa Mkutano huo.

Watanzania watakiwa kudumisha Amani na Mshikamano

0
0
Frank Mvungi-Maelezo

Watanzania wametakiwa kuendeleza amani na mashikamano uliopo kwa maslahi ya Kizazi hiki na Kizazi Kijacho kwa kuenzi misingi ya Amani na Uzalendo iliyojengwa na Waasisi wa Taifa hili.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na aliyekuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni mwenyekiti wa wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania.

Nchi ni zaidi ya itikadi na Mihemko ya watu wachache hivyo ni lazima tuwaepuke wote wanaotaka kuvuruga amani na utulivu uliopo alisema Mpanju.

Akifafanua Mpanju amesema hali iliyojitokeza katika moja ya midahalo iliyofanyika jijini Dar es salaam hivi karibuni ni ya kukemewa na watu wote wanaopenda amani na wazalendo kwa kuwa vitendo hivyo vinaweza kuleta madahara katika jamii hasa kwa makundi maalum kama walemavu,wanawake na wataoto.

Akizungumzia Katiba inayopendekezwa Mpanju amesema ni vyema Watanzania wakaisoma na kuilewa ili kuepuka upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi.

Aliongeza kuwa ni vyema kuepuka kauli zinazoweza kuleta uchochezi katika jamii hasa katika kipindi hichi ambapo baadhi ya watu wamekuwawakitumia mwavuli wa Kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Katiba inayopendekezwa na kufanya vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.

Pia Mpanju alitoa wito kwa vijana kuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo vyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani hapa nchini kwa kuweka uzalendo mbele na kujali maslahi mapana ya Taifa na si ya Kikundi Fulani cha watu.

Katika Hatua nyingine Mpanju alikanisha kuhusika na vurugu zilizotokea katika moja ya midahalo hapa jijini Dar es salaam na kudai hahusiki na tukio hilo kwa namna yoyote kama ilivyoripotiwa .
Aliyekuwa MJumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Amon Mpanju ambaye pia ni mwenyekiti wa wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa Vijana kuwa wazalendo na kulinda amani iliyopo hapa nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images