Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

Mh. Suluhu akutana na balozi wa Norway Nchini,Pia afanya mazungumzo na Mchungaji Stella Matte

$
0
0
Barozi wa Norway Nchini Tanzania Anne - Marie Kaarstad akizungumza na waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu (kulia), alipomtembelea Ofisini kwake, mtaa wa Ruthuli jijini Dar es Salaam leo.
Anne Kristin Hermansen (kushoto),akiwa pamoja na Elisabeth Schwale wakisikiliza mazungumzo baina ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu na Barozi wa Norway Nnchini Tanzania Anne - Marie Kaarstad (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini hapo leo.
Mchungaji Stella Matte akitoa shukrani kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu (kulia), kwa kuhudhulia semina waliyoandaa iliyohusu maswala ya uongozi, alipomtembelea ofisini kwake leo mtaa wa Ruthuli jijini Dar es Salaam.

BEI YA MADAFU LEO

UNFINISHED HOUSE FOR SALE

$
0
0
LOCATION: Tegeta, Mivumoni (Few kilometers from Wazo Cement factory)

 PLOT SIZE: Eight hundred square meters (800m2

OTHER DETAILS: Owneship documents from local government (Neighbouring plots are surveyed) BUILDING STRUCTURE: 4 bedrooms of which 2 are self contained, lounge, dinning, kitchen, public toilet and bathroom, 2 verandas (Reached roofing stage) SURROUNDINGS: Ideal for residencial and commercial use. Electricity and Water accessible.

Neighbouring landmarks are residencial houses, secondary school, vocational training college, dispensary, church.

PRICE: 35,000,000/= (Thirty Five Million Tanzanian Shillings) Negotiable.

CONTACTS: Mobile: +255766669271. Email: nachaliddy@gmail.com )


JK alipowatunuku Kamisheni maafisa wa ngazi ya chini 437 wa Jeshi la Kongo na JWTZ Monduli Arusha

utitiri wa bodaboda jijini Hanoi, Vietnam, na nidhamu ya waendeshaji wake...

UJUMBE WA TPDF WATEMBELEA OFISINI KWA BALOZI PATRICK TSERE NCHINI MALAWI

$
0
0
Balozi Tanzania nchini Malawi,Mh. Patrick Tsere akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa wanajeshi sita wakiongozwa na Brigedia Generali ERNEST GALINOMA ( mstaafu) wakiwa na Makombe yao waliyoshinda baada ya kushiriki mashindano ya mchezo wa gofu yaliofanyika mwishoni wa juma, mjini Lilongwe Malawi. Ujumbe huo ulikuwa umealikwa na uongozi wa jeshi la Malawi kucheza gofu ikiwa ni maadhimisho ya kuwakumbuka waafrika walioshiriki vita vya pili vya dunia na kutimiza miaka mia baada ya vita vya kwanza. Sherehe hizo zilifanyika mwishoni mwa juma.

KOCHA NOOIJ KUTAJA KIKOSI CHA STARS NOVEMBA 4

$
0
0
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij keshokutwa (Novemba 5 mwaka huu) atatangaza kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itakayochezwa ugenini Novemba 16 mwaka huu.

Nooij atatangaza kikosi hicho mbele ya waandishi wa habari katika mkutano utakaofanyika saa 4.30 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizoko ghorofa ya tatu, Jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Swaziland, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Mbabane.

Makamu wa Rais wa Afrika Kusini awasili nchini kwa ziara ya siku moja

$
0
0

Makamu wa Rais wa  Afrika Kusini, Mhe. Matamela Cyril Ramaphosa akiteremka katika ndege mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere Jijini  Dar es Salaam.  Mhe. Ramaphosa yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo pamoja na mambo mengine atazungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,  Mahusiano , Mhe. Stephen Wasira kwa pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt.  Mahadhi Juma Maalim (Mb), na Bi. Zuhura Bundala, Kaimu Mkurugenzi   wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa mapokezi ya  Makamu wa Rais wa Afrika Kusini.  
Mhe. Ramaphosa akilakiwa na Mhe. Wasira mara baada ya kuwasili.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA MSIBA WA RAIS WA ZAMBIA, MICHAEL CHILUFYA SATA

$
0
0
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Rais wa Zambia, Michael Chilufya Sata, wakati alipofika nyumbani kwa Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Judith Kapijimpanga, jijini Dar es Salaam, leo Novemba 3, 2014.
Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Judith Kapijimpanga, baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Rais wa Zambia, Michael Chilufya Sata, nyumbani kwa, Balozi huyo jijini Dar es Salaam, leo Novemba 3, 2014. Picha na OMR

Baraza la michezo ya Majeshi Tanzania ladhamiria kutatua changamoto ya michezo nchini

$
0
0
Wajumbe wa Kamati Tendaji ya BAMMATA katika picha ya pamoja mara baada ya kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika jijini Mbeya katika Bwalo la Magereza la Chuo Ruanda.Wa tatu kutoka kushoto mstari wa mbele ni mwenyekiti wa Baraza hilo Brigedia Jenerali CIRIL MHAIKI.

Tanzania imekuwa haifanyi vizuri sana katika michezo mingi ya Kimataifa inayoshiriki kwa hivi sasa.Hii inatokana na changamoto nyingi zinanazoikabili Taifa  miongoni mwake ikiwa ni kutokuwapo kwa   michezo ya majeshi kama ilivyokuwa hapo awali. 

Michezo hiyo ambayo ilikuwa inasimamiwa na Baraza la michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) ilikuwa inatumika kubaini na kuendeleza vipaji vya wanamichezo wanajeshi ambao walitumika kuitangaza Tanzania kimichezo nje ya nchi na hivyo kuliletea heshima na sifa maridhawa Taifa letu.

Baadhi ya wachezaji walioliletea taifa sifa kwa uchache ni pamoja na Filbert Bay, Juma Ikangaa, Samson Ramadhan, Iswege Christopher,Nasser Mafuru, Samuel Mwang’a , Hitii Shamba na Restuta Joseph ambao wote ama wametokea Majeshini au wamepata mafunzo na wakufunzi wa majeshini.

Mkuu wa wilaya Arumeru Mhe Nyirembe Munasa afungua Tamasha la Vijana katika nchi za Afrika Mashariki leo

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,mkoa wa Arusha, Mhe.  Nyirembe Munasa akitoa hotuba kwa vijana kutoka nchi za Afrika Mashariki katika Tamasha linalowakutanisha Vijana wapatao 250 ,Tamasha hilo linafanyika  kwa siku tano katika taasisi ya

 MS -TCDC mkoani Arusha

 Vijana kutoka nchi za Afrika Mashariki wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye Tamasha la vijana.
 Mkuu wa Wilaya Arumeru,mkoa wa Arusha, Mhe Nyirembe Munasa (kulia mbele) akibadilishana mawazo na mmoja wa vijana kutoka Uganda wanaohudhuria Tamasha la Vijana kutoka nchi za Afrika Mashariki.
 Mkuu wa Wilaya Arumeru,mkoa wa Arusha,Nyirembe Munasa akiwa katika picha ya pamoja na washiriki  wa Tamasha la Vijana. Picha na Emmanuel Filbert

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAJUMBE WA ILIYOKUWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, SERENA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuzungumza na aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, walipokutana katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Novemba 3, 2014 baada ya kuzindua rasmi utoaji wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi) uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waliokuwa wajumbe wa Tume ya Katiba mpya, kutoka (kushoto) ni Humphrey Polepole, Mwenyekiti wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Julius Butiku na Prof. Mwesiga Baregu, baada ya kuzindua rasmi utoaji wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi) uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani. Picha na OMR

MBUNIFU WA MAVAZI WA KIMATAIFA SHERIA NGOWI AFUNIKA KATIKA MAONYESHO YA MAVAZI YA 'MERCEDES BENZ FASHION WEEK AFRICA 2014' NCHINI AFRIKA KUSINI

$
0
0
Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014012
Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014013
Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014014
 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014015
 Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014016
 Na Mwandishi wetu 
 Mbunifu wa kimataifa wa mavazi kutoka Tanzania, Sheria Ngowi (picha ya mwisho hapo juu) amedhihirisha kuwa yeye ni nguli katika ubunifu baada ya kufinika katika onyesho la mavazi la kimataifa lijulikanalo kama Mercedes Benz Fashion Week Africa 2014 lililofanyika juzi Ijumaa mjini Johannesburg, Afrika Kusini. 
Ngowi alionyesha mkusanyiko wa mavazi aliyoyaita 'PRIDE' yaani kujivunia, kama moja ya njia za kumuenzi Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere pamoja na viongozi mashuhuri waliopigania uhuru Afrika. Afrika Kusini ilizizima na kuduwaa kwa muda usiopungua dakika 15 pale ambapo mavazi mbali mbali yaliyobuniwa na Ngowi yalipokuwa yakioneshwa katika ukumbi wa Melrose Arch. 
Sheria Ngowi alionyesha mkusanyiko wa mavazi aina ya suti yenye ubunifu na ueledi wa hali ya juu kwa kutumia vitambaa vya kisasa na kale vilivyonakshiwa kwa maua na rangi za kuvutia kama nyekundu, zambarau, machungwa, nyeupe na nyeusi huku mengine yakiwa bila maua lakini yaliyong'aa kwa kutumia rangi imara kama blu, kahawia na kijivu. 
Onyesho hilo la Mercedes Benz Fashion Week Africa 2014 lilihudhuriwa na watu mbali mbali wakiwemo viongozi wa umma kutoka Afrika kusini, Balozi wa Tanzania Afrika Kusini, Radhia Msuya, wabunifu wa mavazi kutoka nchi za Afrika kama Taibo Bacar kutoka Mozambique, David Tlale kutoka Afrika Kusini, waandishi wa habari kutoka sehemu mbali mbali za dunia na wadau wa mitindo. 
 Mercedes Benz Fashion Week Africa 2014 ni onyesho la kimataifa linalofanyika nchini Afrika Kusini mara moja kwa mwaka likikusanya zaidi ya wabunifu wa mavazi 35 kutoka Afrika kwa ajili ya kuonesha ubunifu wa mavazi yao ambapo kwa mwaka huu Sheria Ngowi ni mbunifu pekee aliyechaguliwa katika onyesho hilo kutoka Tanzania. Sheria Ngowi anasifika kwa ubunifu wa mavazi aina ya suti, kanzu,sare za makampuni, mashirika, shule na hafla mbalimbali kama harusi.
Mbunifu huyu alifungua rasmi ofisi zake zilizopo Masaki, mtaa wa Buzwagi mkabala na Ubalozi wa Angola mwaka mmoja na nusu uliopita ambapo alianza kazi kwa kuwatengenezea mavazi watu kutoka nchi mbalimbali duniani. Pongezi nyingi kwa Sheria Ngowi, unaipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kipaji chako na kazi zako nzuri.

JENGA TANZANIA FOUNDATION YAWALETEA KIPIMO CHA MALARIA PAPO HAPO !.

$
0
0
Mwanadiaspora Mtanzania na Mkurugenzi wa JENGA TANZANIA FOUNDATION Bw. Nasoro Ally akitambulisha rasmi Home Malaria Kit katika mkutano wa  Africa Diaspora Market Place (ADMP III) uliofanyika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani tarehe 10/27/2014.
Akizungumza katika mkutano huo, Bw.. Nasoro Ally alieleza  kuwa bado Malaria ni tishio kubwa la uhai kwa Sub-Sahara Africa na ni chanzo cha vifo vya watoto wadogo hasa chini ya umri wa miaka 5 . 
Kipimo hicho chenye uwezo wa kugundua vijidudu vya Malaria mwilini kati ya dakika 5 hadi 10 kimekubalika na shirika la World Health Organization (WHO) kama kipimo sahihi na cha haraka kwa upimaji wa Malaria nyumbani. Bw. Nassoro aliongeza kusema, kipimo hicho kitatolewa bure nchini Tanzania kwa familia zisizojiweza na kuhakikisha kinafika  sehemu mbali mbali za ndani hasa mikoani na vijijini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma sahihi za afya na kufupisha safari ndefu na zenye milolongo.


Mkurugenzi wa JENGA TANZANIA foundation Bw. Nasoro Ally na Mwanasayansi msaidizi wa JENGA TANZANIA, Da. Asha Nyanganyi wakitambulisha rasmi kipimio cha nyumbani cha Malaria kwa  Mhe. Balozi Liberata Mumulala na wawakilishi wa USAID waliohudhuria mkutano huo.

VIDEO YENYE MAELEZO KUHUSU KIPIMO CHA NYUMBANI CHA MALARIA
Kipimo cha  Nyumbani cha Malaria Chenye Uwezo wa Kugundua Vijidudu  vya Malaria Vikiwemo Plasmodium Falciparim (PF) Vivax(PV)  Ovale (Po) na Malariae(Pm) antigen kati ya dakika 5 hadi 10 .


Mhe.Balozi Liberata Mulamula akipata kipimo cha  Malaria Mara moja kutoka kwa Mwanasayansi msaidizi wa JENGA  Asha Nyanganyi



Baadhi ya watu wachache walioshiriki katika kipimo hicho.

Shukrani; Images
Sunday Shomari
Jenga Tanzania Foundation
Story;
NesiWangublogspot.com

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 12 WA SHIRIKISHO LA TAASISI ZA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA KWA NCHI ZA SADC

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Angel Magati ambaye aliimba wimbo maalum wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana  na Rushwa kwa nchi za SADC (Southern African Forum Against Corruption) ulioanza leo ukitarajiwa kumalizika Ijumaa ya tarehe 07/11/2014 Katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza. Angel, mwenye umri wa miaka 22, na  mwanafunzi katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM, ameshatoa albamu yake ya kwanza iitwayo "Umefanya Tena" yenye nyimbo tisa kali za Kiswahili na Kiingereza.


Meza kuu ikiungana na wajumbe kusimama kimya kwa muda wa dakika moja kumkumbuka Rais wa Zambia Marehemu Michael Satta kabla ya ufunguzi wa  Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana  na Rushwa kwa nchi za SADC (Southern African Forum Against Corruption) ulioanza leo ukitarajiwa kumalizika Ijumaa ya tarehe 07/11/2014 Katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa nchi za SADC (Southern African Forum Against Corruption) ulioanza leo ukitarajiwa kumalizika Ijumaa ya tarehe 07/11/2014 Katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.
  Sehemu ya wadau toka nchi mbalimbali barani Afrika wameshiriki Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa nchi za SADC (Southern African Forum Against Corruption) ulioanza leo ukitarajiwa kumalizika Ijumaa ya tarehe 07/11/2014 Katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.
 Kutoka kushoto ni Mbunge wa Sengerema William Ngeleja, Meya wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Amina Masenza wakisikiliza kwa umakini yanayojiri ndani ya Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa nchi za SADC (Southern African Forum Against Corruption) ulioanza leo ukitarajiwa kumalizika Ijumaa ya tarehe 07/11/2014 Katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Utawala Bora Kapt.George Mkuchika katika Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa nchi za SADC (Southern African Forum Against Corruption) ulioanza leo ukitarajiwa kumalizika Ijumaa ya tarehe 07/11/2014 Katika Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.PICHA NA IKULU.

PAUL MAKONDA: SIKUVURUGA MKUTANO WA TAASISI YA MWALIMU NYERERE

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
SIKINDE- TUFURAHI NA WANA SIKINDE

USED CARS BUYERS SEMINAR

$
0
0


 GET YOURSELF TRAINED ON HOW TO BUY A USED CAR RIGHT FROM JAPAN THROUGH SAMURAI JAPAN TRADING.  

MR SHIMBUTSU - A CONSULTANT IN CAR SELLING BUSINESS FROM JAPAN WILL BE OFFERING FREE SEMINARS EVERY SATURDAY FOR THE MONTH OF NOVEMBER 2014.

TIME: 3 TO 4 PM

VENUE: SAMURAI JAPAN TRADING OFFICES MAKTABA COMPLEX 3 RD FLOOR BIBI TITI MOHAMED ROAD



'' GET A CHANCE TO EXPAND YOUR KNOWLEDGE FOR FREE''

MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA BW. KYLE PETERS ATEMBELEA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOETEKELEZWA NA TASAF WILAYANI BAGAMOYO.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bwana Kyle Peters amefanya ziara katika kijiji cha Buma wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ambako ameshuhudia walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF na kuridhishwa kwake na namna mpango huo ulivyowanufaisha walengwa ambao wameanza kuondokana na umaskini.

Akiwa kijijini hapo Bwana Peters alitembelea moja ya nyumba iliyoboreshwa na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini Bwana Bakari Rajabu Bakari ambaye kwa kutumia fedha za ruzuku kupitia Mpango wa kunusuru kaya maskini ameweza kuboresha maisha yake ikiwa ni pamoja na kununua Luninga(TV) huku akimudu pia kusomesha watoto wake.

Bwana Peters amesema utekelezaji wa Mpango huo umeanza kuonyesha mafanikio nchini TANZANIA  jambo ambalo litatumiwa na Benki ya Dunia kuendelea kuufadhili huku mfano huo ukisambazwa katika nchi nyingine ili kazi ya kuutokomeza umaskini iwe na mafanikio.

Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema mafanikio ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini yanatokana na taasisi yake kuamini na kutekeleza majukumu yake kwa uwazi na kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo walengwa katika hatua za utekelezaji wake.

Zifuatazo hapo chini ni baadhi ya picha za ziara ya makau huyo wa Rais wa Benki ya Dunia katika kijiji cha Buma wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
    Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters akiwahutubia wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini katika kijiji cha Buma wilayani Bagamoyo.
    Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa masuala ya mpango wa kunusuru kaya masikini kwa walengwa (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters.
0Baadhi ya wanuafaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF katika kijiji cha Buma wilyani Bagamoyo wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga.

    Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi akimkaribisha Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kyle Peters alipotembelea miradi ya TASAF wilayani humo. Kushoto kwake Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Article 8

Viewing all 110021 articles
Browse latest View live




Latest Images