Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA BENDI YA MSONDO NGOMA ZAFANA SANA

$
0
0
 Bendi Kongwe ya Muziki wa Dansi hapa nchini iliyodumu kwa miaka 50 toka kuanzishwa kwake mwaka 1964,Msondo Ngoma Music Band imesherehekea jubilei yake hiyo iliyofanyika Novemba 1,2014 katika viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha mashabiki wake lukuki kutoka sehemu mbali mbali.

Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo za kusherehekea Jubilei ya miaka 50 ya Bendi ya Msondo Ngoma,alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye aliweza kuwatunuku vyeti vya heshima wanamuziki mbali mbali walioitumia Bendi hiyo toka ilipoanzishwa mpaka sasa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea Cheti cha heshima kutoka kwa Muwakilishi wa Mfuko wa PSPF,Abdul Njaidi ambao ni sehemu ya Wadhamini wa Bendi hiyo ikiwa ni sehemu ya heshima kwa Mh. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake mkubwa kwa wasanii mbali mbali hapa nchini.Cheti hicho kimetolewa na Bendi ya Msondo Ngoma.Picha Zote na Othman Michuzi.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimkabidhi Cheti cha heshima Kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma,Mzee Said Mabela.
Mmoja wa Waanzilishi wa Bendi hiyo,John Simon (Kapten Mstaafu) akizungumza machache pamoja na kutoa historia fupi ya kuanza kwa bendi hiyo.
Safu ya waimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma ikiongozwa na Nguli Shaaban Dede (katikati) wakifanya vitu vya mbele ya mashabiki wao lukuki waliofika kwenye Viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar.
Mpiga Tumba wa Msondo Ngoma akifanya yake.
Hassan Moshi William (mtoto wa Marehemu TX Moshi Willian) akionyesha uhodari wake kiasi kwamba hata pengo la mzee wake kuhisi limezibwa.
Rapa wa Bendi ya Msondo Ngoma,Roman Mng'ande akifanya mambo.

BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA PICHA ZAIDI

msaada tutani: Je, unajua waliko hawa watoto?

$
0
0
Hii picha imekuwa ikisambaa sana kwenye mitandao ninaomba kama kuna mtu anafahamu uwezekano wa kupatikana kwa watoto hawa kwenye hii picha. Msamaria mwenye nia ya kuwasaidia ameomba jina lake lisitajwe bali anaomba yoyote anayefahamu jinsi ya kuwapata hao watoto atume email kwa
Asante sana!

SURPRISE BIRTHDAY PARTY YA DESIGNER PETER WALDEN YAFANA HUKO BOWIE, MD

$
0
0
IMG_5947Designer wa nguo (PSW) Peter Walden na mkewe Frida Walden wakiwa wenye nyuso za furaha wakati kusheherekea Birthday yake nyumbani kwake huko Bowie MD Jumamosi Novemba 1, 2014. IMG_5937Birthday boy akiwa na mama yake. IMG_5965Cake ya Birthday iliyowekwa nembo ya nguo za Peter (Perfect Gentleman by PSW. Picha zaidi BOFYA HAPA

NEWS ALERT: Mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuzingatia Mambo ya msingi katika katiba wavunjika kwa tafrani kubwa

$
0
0
Tafrani kubwa imezuka jioni ya leo wakati wa Mdahalo uliondaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere wa kujadili umuhimu wa kuzingatia Mambo ya msingi katika katiba inayopendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliokuwa ukifanyika kwenye Ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza, Jijini Dar es salaam.

Chanzo cha Tafrani hiyo, inaelezwa kuwa wakati Jaji Warioba akiongea, baadhi ya watu waliokuwepo kwenye mdahalo huo  walisimama na kuinua mabango yasemayo pamoja na mambo mengine kwamba iweje wajadili mapendekezo ya rasmu ya katiba ambayo wao wameshaikubali?

Likaanza zogo ambapo watu wengine walijaribu kuwanyang'anya yale mabango na kuyachana na wao wenye mabango kujihami. Ndipo vurugu/kashfa/matusi vikaanza kutolewa. Hali hii ilisababisha kushikana mnashati, kusukumana na kurushiana viti. 

 Mkutano huo, ambao ulihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali sambamba na itikadi tofauti za kisiasa, ulirushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV kwa kile kilichoelezwa kuwa maudhui ya kimtazamo uliolenga kuoanisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya Tume ya Warioba na ile ya Bunge Maalum la Katiba. 
Jaji Mstaafu Mh. Joseph Sinde Warioba akisaidiwa kuondolewa kwenye Mdahalo huo mara baada ya kuzuka kwa tafrani hiyo.
Jaji Mstaafu Mh. Joseph Sinde Warioba akisaidiwa na Wanausalama  kuondolewa kwenye Mdahalo huo mara baada ya mambo kuharibika kutokana vurugu kubwa.
Ilikuwa ni mshikemshike na tafrani tupu.
Mdahalo ukiwa umesitishwa kwa vurugu hizo

IGP MSTAAFU MZEE PHILEMON MGAYA ASHEREHEKEA MIAKA 85 YA KUZALIWA

$
0
0
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dkt. Alex Malasusa akiwa pamoja na IGP mstaafu Mzee Philemon Mgaya wakati wa sherehe hiyo iliyofana sana iliyofanyika katika Hotel ya Protea Court Yard ya jijini Dar es Salaam.
IGP Mstaafu Mzee Philemon Mgaya akipokea zawadi

IGP Mstaafu Philemon Mgaya akikata keki huku akiwa amezungukwa na wajukuu wake. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AZINDUA HARAMBEE YA UJENZI WA KITUO CHA WATOTO NA VIJANA-UDSM

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na watoto baada ya kuzindua harambee ya ujenzi wa Kituo cha Watoto na Vijana cha Kanisa la Umoja la Chuo Kikuu cha Dar es salaam Novembe 2, 2014. Kulia Kwake ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Titus Mdoe na kushoto kwake ni Askofu Charles Salala wa Kanisa la Afrikani Inland Church. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Bw. Frederick Msagala CD ya kwaya ya Kanisa la Umoja la Chuo Kikuu cha Dar es salaam baada ya kuinunua kwa sh. 700,000 katika uzinduzi wa Halambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Watoto na Vijana cha Kanisa iliyo mjini Dar es slaam Novemva 2, 2014.
Waziri Mkuu, Mkzengo Pinda akisalimiana na viongozi wa Kanisa la Umoja la Chuo Kikuu cha Dar es salaa baada ya kuwasili chuoni hapo ili kuzinduaa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Watoto na Vijana cha Kanisa hilojijini Dar es salaama Novemba 2, 2014.

Ma-sensei watano waliotunukiwa ngazi za juu za karate watoa shukurani kwa Shirikisho la Karate Tanzania

$
0
0
 Walimu  (ma-Sensei) watano toka Tanzania, yaani Sensei Dudley Mawalla, Sensei Daud Magoma, Sensei Kheri Kivuli, Sensei Edgar Kaliboti na Sensei Rumadha Fundi, wanatoa shukrani  nyingi sana kwa  kupewa dhamana kubwa ya heshima na vyeo vya ngazi za juu toka shirikisho la Karate Tanzania (Tanzania Karate-Do Federation). 
 Chini ya uongozi wa mwenyekiti Sensei Geofrey Kalonga na katibu mkuu wake Sensei Phillip Chikoko, wana-sema ma-Sensei hao katika waraka ulioandikwa na Sensei Rumadha Fundi kwa niaba ya wote kuwa wao hawana  budi kuitikia wito wa kuchangia maendeleo ya sanaa ya Karate inayohitaji nidhamu na mifano ya ujasiri wa hali ya juu kwenye kizazi kipya cha taifa letu. 
 Sensei Dudley Mawalla na Sensei Daudi Magoma, walitunukiwa shahada au Dan ya Saba kila mmoja, wakati  Sensei Kheri Kivuli, Sensei Kaliboti na Sensei Rumadha Dan sita kila mmoja.
Sensei Dudley Mawalla, mwanzilishi wa Japan Shotokan Tanzania. Sensei Kaliboti, mkufunzi wa Gracie Ju jitsu, Australia, Sensei Rumadha, Okinawan Goju Ryu Jundokan KyoKai, Texas, USA, Sensei Daudi na Sensei Kivuli, wakufunzi wa Okinawa Goju Ryu, Dar Es Salaam, Tanzania.
 Sherehe hizo zilifanyika uwanja wa ndani wa taifa kuadhimisha siku ya baba wa taifa Mwalimu Nyerere, kushirikishwa na zaidi ya wana-Karate 50 wa ngazi mbalimbali toka shule na mikoa tofauti hapa nchini. 
"Wote tuliotunukiwa heshima hiyo, hatunabudi kusema asante zetu katika shirikisho la Karate Tanzania(Tanzania Karate-Do Federation", unamalizia waraka huo ambao Globu ya Jamii ina nakala yake
Katibu Mkuu wa Tanzania Karate Do Association Sensei Philip Chikoko (kushoto) akimtunuku  Sensei daudi Magoma shahada au Dan ya Saba

Katibu Mkuu wa Tanzania Karate Do Association Sensei Philip Chikoko (kulia) akimtunuku  Sensei Kheri Kivuli  shahada au Dan ya Sita
Sensei Edgar Kaliboti akiwa anasimamia mafunzo ya mtindo wa Gracie Ju jitsu huko Australia. Tanzania Karate do federation imemtunuku Dan ya sita
Sensei Dudley Mawalla akitunukiwa Dan ya saba na Mwenyekiti wa Tanzania Karate do Federation Sensei Godfrey Kalonga (kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Karate Do Association Sensei Philip Chikoko
Sensei Rumadha Fundi akicheza kata. Yeye ametunukiwa Dan ya Sita

Dkt. Kigwangala aongoza Mbio za Amani 2014, ahimiza amani nchini

$
0
0
Wanasiasa wameaswa kudumisha amani, upendo na mshikamano wa Tanzania, ili kuepuka vurugu zinazoweza kujitokeza ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikisababishwa na makundi ya wanasiasa, kwa kutoa ujumbe kwa wananchi unao chochea kuvurugukika kwa amani ya Tanzania. 

Akizungumza na wanamichezo wa vilabu mbalimbali vya kukimbia (Jogging) kutoka Tanzania bara na Zanzibar, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,  Mbunge wa jimbo la Nzega, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Dk. Hamis Kigwangala amesema wakati bunge maalum la Katiba lilipokuwa likitunga katiba inayopendekezwa, kuliibuka baadhi ya wanasiasa waliokana kushiriki katika bunge hilo na kutofautiana katika baadhi ya mambo kuingizwa katika katiba hiyo, huku wale waliobaki ndani ya bunge maalumu la katiba kwa asilimia takriban 85 wakiheshimu maamuzi ya watanzania na kuhakikisha katiba mpya inapatikana. 

Hivyo amewataka wanasiasa pamoja na kuwa mapendekezo yao hayakuingia ndani ya katiba wasiwe chanzo cha kutokuridhika kwao kulazimisha na watanzania wengine wasiridhike na kwamba Watanzania waachwe siku ya kuipigia kura katiba inayopendezwa itakapo tangazwa, Watanzania waipigie kura ya ndio au hapana na kwamba waamue kwa utashi wao bila uchochezi wa wanasiasa.

 Katika Tamasha hilo lililopewa jina la Mbio za Amani 2014, Dk, Kigwangala pia amehimiza umuhimu wa kufanya michezo kila wakati, kwani michezo ni Afya, Furaha, Amani, Upendo na Ajira, huku akivitunuku vyeti baadhi ya vilabu vya Jogging kwa kushiriki katika tamasha hilo. 

Tamasha hilo limeshirikisha wanamichezo wa vilabu vya Jogging kutoka Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam, ambapo limeandaliwa na Faita Jogging & Sports Club ya jijini Dar es Salaam, huu ukiwa ni mwaka wa tatu kuandaliwa.
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki katika zoezi la viungo mara baada ya kupokea vikundi hivyo vya Jogging kutoka maeneo mbalimbali nchini. 
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akishiriki katika zoezi la viungo mara baada ya kupokea vikundi hivyo vya Jogging kutoka maeneo mbalimbali nchini. 
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr. Khamis Kigwangala akipokea vikundi hivyo vya Jogging kutoka maeneo mbalimbali nchini. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Msingi wa Makosa Katika Mchakato wa Kutafuta na Kupata Viongozi wa Kisiasa Tanzania na Suluhisho Lake - Sehemu ya pili

ngoma azipendazo ankal

BENKI YA MKOMBOZI YATANGAZA MAUZO YA AWALI YA HISA ZAKE,YAWAOMBA WATANZANIA WAJITOKEZE KUZINUNUA

$
0
0
Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Mkombozi,Bwa Masha J. Mshomba akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),Mwishoni mwa wiki jijini Dar, kuhusiana na kuwafahamisha Watanzania kuhusu mauzo ya awali ya hisa za benki  yao ya Mkombozi,ikiwemo pia na kuwaomba Watanzania washiriki katika ununuzi wa hisa za Benki hiyo ya Mkombozi,shoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Mkombozi  Bwan. Edwina Lupembe.

HOSPITALI YA KAIRUKI YAPATA TUZO YA UBORESHAJI VIWANGO VYA HUDUMA YA AFYA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Hospital ya Kairuki, Dk. Asser Mchomvu akiwa amebeba tuzo aliyokabidhiwa na na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati). Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid.
Picha ya pamoja.

Na Mwandishi Wetu 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ameukabidhi uongozi wa Hospitali ya Kairuki (KH) tuzo ya waliofanya vizuri katika vigezo mbalimbali vya uboreshaji viwango vya huduma ya Afya katika mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji Viwango vya huduma ya Afya uliofanyika wiki iliyopita (Octoba 31-2014) katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Hospital ya Kairuki, Dk. Asser Mchomvu alisema sifa ya mafanikio yao mpaka wakapata tuzo hiyo yanatokana na mafunzo  kwa wafanyakazi wa Hospital wapatao 20 yaliyoendeshwa na Wizara ya afya ikishirikiana na Jhpiego,CDC na PEPFAR.

Dk. Mchomvu aliongeza kuwa mafunzo kuendelea kutolewa na wakufunzi wa ndani (inhouse training), kuundwa kwa timu maalum ya ndani kwa ajili kufanya ukaguzi wa kushtukiza ndani na utayari wa KH kushirikia katika zoezi la udhibiti na uzuiaji wa maambukizi.

Aidha, Dk. Mchomvu alieleza kuwa siri nyingine ni ushirikiano mzuri baina ya manegimenti ya KH na timu ya wakaguzi toka wizara ya Afya katika kutekeleza maagizo na mapendekezo na kuyafanyia kazi.

“Kwa upande wetu maeneo yaliyofanya vizuri katika zoezi ili ni pamoja na mashine bora za kuuwa vijidudu (sterilization unit) na eneo zima katika kitengo hicho, eneo la kuifadhi/ kutenganisha na usafirishaji wa taka hatarishi, taka mbichi na taka mchanganyiko pia chumba cha upasuaji kufuata taratibu stahiki za kimataifa katika kuzithibiti maambukizi,” alisema Dk. Mchomvu.

Aliongeza kuwa wakati huohuo KH imezindua kampeni maalum za muda mrefu katika kuchunguza na kutibu magonjwa yasiyoambukiza, mfano saratani ya matiti, saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya tezi dume (prostate). Saratani hizi ndizo zinazoongoza kwa  hapa nchini.
Moja ya mashine za kisasa za kupima saratani ya matiti katika Hospitali ya Kairuki.

“Lakini pia KH imezidi kuboresha huduma katika vitengo vya macho, sikio, pua na  koo kwa kupata mitambo ya kisasa katika nyanja hizo,” alisema Dk. Mchomvu.Aliongeza kwa kusema kuwa KH imezindua wodi mpya ya kisasa hasa kwa ajili ya wanachama  wa mfuko wa Bima ya taifa ya afya. (NHIF) na wodi maalum ya watoto.

Wengine waliotunukiwa tuzo hizo za uboreshaji wa huduma za afya ni Hospitali ya Bugando-Mwanza pamoja na Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC). 

Tuzo hizo zilitolewa na Wizara ya Afya wakishirikiana na Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Marekani (CDC) na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR).

MSAMA AUCTION MART KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI WAKAMATA VIFAA MBALIMBALI VYA KUDURUFU KAZI ZA WASANII

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani), moja kati ya mashine 4 za  kurudufu CD  feki zilizokamatwa katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa wa Polisi, D/SSGT Daniel Gingo. (Picha na Francis Dande)
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), wino unaotumika kunakshia makasha ya CD feki wanazozitengeneza
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), baadhi ya CD feki zilizokamatwa

=========  =======  =======  =======
KAMPUNI ya Udalali ya Msama Auction Mart ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama ikishirikiana na Jeshi la Polisi Kituo cha Urafiki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, imekamata kompyuta za kufyatua kazi feki za wasanii zenye thamani ya mil18.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama, alisema mitambo hiyo imekamatwa kwa ushirikiano mkubwa kati ya pande hizo tatu pamoja na sapoti ya wasamaria wema. Alisema kopyuta, mashine na kazi feki zenye thamani ya mamilioni ya fedha, zimekamatwa eneo la Kimara-Machungwani, jijini Dar es Salaam na mtuhumiwa huyo amefikishwa katika kituo cha Polisi kwa ajili ya mchakato wa kiheria wa kufikishwa mahakamani. 

Msama alisema akiwa mdau wa masuala ya burudani kupitia kampuni yake ya Msama Promotions Ltd ambayo imekuwa ikiratibu matamasha ya Muziki wa Injili, amekuwa akiguswa na kitendo wanjanja wachache kunufaika na jasho la kazi ya wengine.Alisema wizi wa kazi za wasanii mbalimbali umekuwa kikwazo cha mafanikio ya wahusika ambao licha ya kuifanya kazi hiyo kwa muda mrefu, wameshindwa kupiga hatua kiuchumi kutokana na wajanja hao kuingiza kazi feki mtaani ambazo huuzwa kwa bei ya kutupa.

Msama alisema kazi hiyo ngumu ambayo imekuwa ikifanywa na kampuni yake kwa kushirikiana na wadau wengine, anashukuru kwamba kadiri siku zinavyosogea wengi wamezidi kukamatwa kutokana na ushirikiano ambao wamekuwa wakipewa.“Msama Auction Mart tunachukua nafasi hii kulipongeza Jeshi la Polisi hasa Kituo cha Ubungo ambacho wamekuwa msaada mkubwa kwetu katika vita hii ya kupambana na
wezi wa kazi za wasanii,” alisema Msama.

Aliongeza, kwa ushirikiano mkubwa wa Jeshi la Polisi na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, anashukuru kazi hiyo imekuwa ikisonga mbele kwa kazi feki kuzidi kukamatwa katika maeneo mbalimbali ya nchi katika kulinda maslahi ya wasanii.Alisema tangu kuanza kwa kazi hiyo ngumu ya kukabiliana na wizi wa kazi za wasanii, kampuni yake imekamata vifaa mbalimbali vya kukamilisha kazi hiyo na kazi zenye jumla
ya shilingi bil.12.

YAMOTO BAND YAWEKA HISTORIA BUKOBA

$
0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba.
BENDI inayokuja kasi hapa nchini, Yamoto Band" kundi la vijana wenye vipaji vipya usiku wa kuamkia leo imefanya kufuru ndani ya Ukumbi wa Burudani wa "Lina's Night Club" uliopo hapa Mjini Bukoba. Ambao waliimba nyimbo zao matata za 'Najuta' ya Yamoto Band na nyingine zinazounda Album zao na kuhudhuriwa na umati wa Mashabiki ndani ya ukumbi huo na kuwafanya mashabiki muda wote kuvamia jukwaa kwa Makamuzi hayo ya kufa Mtu. Yamoto Band ambao ndio kwa mara ya kwanza kuja Hapa Mjini Bukoba wakiletwa na kampuni ya Shemeji Investment kushiriana na Ibra Cadabra.Taswiara ya Mashabiki Waimbaji wa Kundi zim la Yamoto Band wakilishambulia jukwaa!!

SHERIA NGOWI AFUNIKA KATIKA MAONYESHO YA MAVAZI YA 'MERCEDES BENZ FASHION WEEK AFRICA 2014' NCHINI AFRIKA KUSINI

$
0
0
Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014016
Mbunifu wa kimataifa wa mavazi kutoka Tanzania, Sheria Ngowi amedhihirisha kuwa yeye ni nguli katika ubunifu baada ya kufunika katika onyesho la mavazi la kimataifa lijulikanalo kama Mercedes Benz Fashion Week Africa 2014 lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Ngowi alionyesha mkusanyiko wa mavazi aliyoyaita 'PRIDE' yaani kujivunia, kama moja ya njia za kumuenzi Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere pamoja na viongozi mashuhuri waliopigania uhuru Afrika.

Afrika Kusini ilizizima na kuduwaa kwa muda usiopungua dakika 15 pale ambapo mavazi mbali mbali yaliyobuniwa na Ngowi yalipokuwa yakioneshwa katika ukumbi wa Melrose Arch.

Sheria Ngowi alionyesha mkusanyiko wa mavazi aina ya suti yenye ubunifu na ueledi wa hali ya juu kwa kutumia vitambaa vya kisasa na kale vilivyonakshiwa kwa maua na rangi za kuvutia kama nyekundu, zambarau, machungwa, nyeupe na nyeusi huku mengine yakiwa bila maua lakini yaliyong'aa kwa kutumia rangi imara kama blu, kahawia na kijivu.

Onyesho hilo la Mercedes Benz Fashion Week Africa 2014 lilihudhuriwa na watu mbali mbali wakiwemo viongozi wa umma kutoka Afrika kusini, Balozi wa Tanzania Afrika Kusini, Radhia Msuya, wabunifu wa mavazi kutoka nchi za Afrika kama Taibo Bacar kutoka Mozambique, David Tlale kutoka Afrika Kusini, waandishi wa habari kutoka sehemu mbali mbali za dunia na wadau wa mitindo.

Mercedes Benz Fashion Week Africa 2014 ni onyesho la kimataifa linalofanyika nchini Afrika Kusini mara moja kwa mwaka likikusanya zaidi ya wabunifu wa mavazi 35 kutoka Afrika kwa ajili ya kuonesha ubunifu wa mavazi yao ambapo kwa mwaka huu Sheria Ngowi ni mbunifu pekee aliyechaguliwa katika onyesho hilo kutoka Tanzania.

Sheria Ngowi anasifika kwa ubunifu wa mavazi aina ya suti, kanzu,sare za makampuni, mashirika, shule na hafla mbalimbali kama harusi.Mbunifu huyu alifungua rasmi ofisi zake zilizopo Masaki, mtaa wa Buzwagi mkabala na Ubalozi wa Angola mwaka mmoja na nusu uliopita ambapo alianza kazi kwa kuwatengenezea mavazi watu kutoka nchi mbalimbali duniani.
Mercedes-Benz-Fashion-Week-2014-Sheria-Ngwoi-Bellanaija-October2014015


KINYWAJI CHA SHUDA COCKTAILS CHAZINDULIWA JIJINI DAR

$
0
0
Kampuni ya A&K HOLDINGS LTD mwishoni mwa wiki ilizindua kinywaji cha Shuda Cocktails hafla iliyofanyika Novemba 1, 2014 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, kinywaji hicho kimetengenezwa kwa ufanisi na kuchanganywa katika vipimo maalum ili kupata bidhaa zenye ladha nzuri zinazolenga na kukubalika na matabaka yote ya wanywaji au watuamiaji wa vileo. Ujazo wake ni 700ml. Bidhaa hii inazalishwa nchini Uingereza.

Meneja Masoko ya Kinywaji cha Shuda Cocktails, Bernadetha Daudi akiongea katika uzinduzi wa kinywaji huo mwishoni mwa wiki iliyopita Nobemba 1, 2014 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya A&K HOLDINGS LTD ambao ni wasambazaji wa kinywaji cha Shuda Cocktails akiongea katika uzinduzi wa kinywaji hicho, halfa iliyofanyika  mwishoni mwa wiki iliyopita Novemba 1, 2014 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAFUNZO YA ELIMU YA UJASIRIAMALI KWA WASHIRIKI WA SHINDANO LA MASHUJAA WA KESHO MKOANI MTWARA YAMALIZIKA

$
0
0
Mafunzo ya elimu na ujasiriamali kwa washiriki wa shindano la Mashujaa wa  Kesho yanayoratibiwa na kampuni ya Statoil Tanzania, yenye lengo la kumjenga  kijana kuwa mjasiriamali yamekamilika hivi karibuni.

Akibainisha aina ya mafunzo ya ujasiriamali waliyopata vijana hao, Erick
Mchome Afisa Mahusiano wa Statoil-Tanzania amesema kuwa
Mafunzo waliyopata vijana hao yamelenga kuwawezesha vijana kuandika mpango wa biashara ikiwa ni hatua ya awali katika harakati za ujasiriamali.

Pamoja na hilo vijana pia wamefundishwa kujenga uwezo wa kujieleza kwani sifa moja ya mjasiriamali ni kujiamini na kuweza kusimama mbele ya wateja kunadi biashara yake. ‘’ Tumekuwa na siku nne nzuri za mafunzo na ni imani yetu kuwa vijana hawa hamsini na ziaidi watakuwa chachu ya mafanikio kwa vijana wenzao kwani mafunzo haya yamewatoa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine,’’ alisema Mchome.

Sambamba na hayo vijana hao ambao walifikia idadi ya hamsini na zaidi wamefundishwa namna ya kujijenga kama wajasiriamali ikiwa ni pamoja na namna za kutafuta mtaji, kupanga mapato na matumizi na pia kutenga faida kwa kila biashara watakayofanya. Lengo la mfunzo haya ni kuchochea ari ya ujasiriamali kwa vijana ambao wameshiriki na kuingia awamu ya pili ya shindano la mashujaa wa kesho. 

Kwa upande vijana waliochaguliwa kuingia hii awamu ya pili wao wamesema kuwa elimu waliyoipata imewafungua macho na kupanua mawazo sana. Majadiliano yamewaonyesha wazi kwamba kuna fursa nyingi sana nje ya kuajiriwa.

“Nawashukuru Statoil-Tanzania pamoja na wasimamizi wa mafunzo haya kwani elimu tuliyopata hapa ni msingi mkubwa kwa sisi kuwa wajasiriamali, kufanya biashara zetu ilitukamate fursa za biashara ambazo zipo mbele yetu. Kuna njia nyingi sana za kutafuta maisha ”, Alisema Ally Seleman mshiriki wa shindano la Mashujaa wa Kesho.

Mafunzo ya elimu ya biashara na ujasiriamli yalianza toka tarehe 27 Oktoba
2014 na kuendelea kwa siku nne.Mara baada ya mafunzo hayo kukamilika vijana wamepewa siku 12 za kuaandika mawazo ya biashara na kuyakusanya siku ya jumatano ya tarehe 12 mwezi Novemba ili kuweza kuingia katika awamu ya pili ya mchakato wa kupata washindi wa shindano hili la Mashujaa wa kesho.

Shindano la mashujaa wa kesho lilizinduliwa mnamo mapema mwezi Septemba na linatarajiwa kufika kilele mwanzoni mwa mwezi Desemba ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani elfu tano kutoka kampuni ya Statoil.


Wabunge Bunge la SADC wamchagua Mh. Makinda kuwa Rais mpya wa Bunge hilo

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisoma hotuba yake ya shukrani kwa wajumbe wa Mkutano wa 36 wa Bunge la SADC ambao ni Maspika na Wabunge kutoka Mabunge ya nchi wanachama wa wa SADC baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Bunge hilo kwa miaka miwili ijayo Mjini Victoria Falls, Zimbabwe.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akielekezwa jambo na Katibu Mkuu wa Bunge la SADC Dkt. Esau Chiviya mara baada ya kukalia kiti cha Urais wa Bunge hilo baada ya kuchaguliwa rasmi kuwa rais wa Bunge hilo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda ambaye pia ni rais wa Bunge la SADC akiahirisha rasmi Mkutano wa 36 wa Bunge hilo baada ya Kumalizika jana. Makinda alichaguliwa kuwa Rais wa Bunge hilo na wajumbe wote wa Mkutano huo jana.
Spika wa Bunge la Zimbabwe Mhe. Jacob Mudenda akimpongeza Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Bunge la SADC kwa miaka miwili ijayo. Pembeni kulia ni Spika wa Bunge la Afrika Kusini Mhe. Mhe. Baleka Mbete
Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe akimpongeza Makamu wa Rais wa Bunge la SADC Mhe. Njovya Lema (Malawi) baada ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo sambamba na Rasi wa Bunge hilo Mhe. Anne Makinda (katikati) jana wakati wa Kumalizika kwa Mkutano wa 36 wa Bunge hilo. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.

Na Owen Mwandumbya, Victoria Falls, Zimbabwe
Hatimaye wajumbe wa Mkutano wa 36 wa Bunge la SADC ambalo linaloundwa na mabunge ya  nchi wanachama wa SADC (SADC PF) wamemchagua kwa kishindo Spika wa Bunge la   Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda kuwa Rais wa Bunge hilo kwa kipindi cha miaka miwili ijayo.

Makinda ambaye alikuwa hana mpinzani katika uchaguzi huo, aliungwa mkono na wajumbe wote wa Mkutano huo ambao ni Maspika na Wabunge kutoka mabunge ya Nchi wanachama wa SADC jana tarehe 2 Novemba, 2014 wakati wa kuhitimisha Mkutano wa 36 wa Jukwaa la Mabunge ya SADC uliokuwa ukifanyika katika Hotel ya Elphant Hii iliyopo Mjini Victoria Falls Nchini zimbabwe.

Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Katibu Mkuu wa Bunge la SADC Dkt. Esau Chiviya alisema kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za Bunge hilo, kanuni ya Kanuni ya 42 (2) i  inatamka wazi kuwa endapo kutakuwa na mgombea mmoja pekee, basi  atawahoji wajumbe na endapo watamkubali basi atamtangaza rasmi kuwa amechaguliwa kushika nafasi hiyo.

“ Kwa kuwa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda hana mpinzani na kwa kuwa nimewahoji na wote mmemuunga mkono, basi natangaza kuwa ndiye Rais mpya wa Bunge la SADC kwa miaka miwili ijayo”. Alitangaza Dkt. Chiviya

Awali kwa mujibu wa utaratibu wa uongozi ndani ya chombo hicho, Makinda alitakiwa kugombea nafasi hiyo pamoja na Spika wa Ushelisheli na Msumbiji ambao wote kwa pamoja hawakushiriki uchaguzi huo na kuamua kumuunga mkono Spika Makinda

Akisoma hotuba yake ya shukrani kwa wajumbe wa Mkutano huo, Mhe. Makinda amewashukuru wajumbe wote walioshiriki katika uchaguzi na kumuunga mkono ili aweze kuwaongoza katika kipindi kingine cha miaka miwili.

“ Ninalo deni kubwa kwenu kwa jinsi mlivyoniunga mkono na kama mnavyojua jukumu letu kubwa mbele yetu ni kuwa na Bunge imara la SADC jambo ambalo nawahakikishia kwa pamoja tutafanikiwa

Makinda alisema kama mnavyojua, malengo makuu ya SADC PF ni kuwa na Bunge la kikanda litakalowakilisha mawazo ya pamoja kutoka kila Bunge la Nchi wananchama wa SADC, hili ndilo lengo kuuu la waasisi wa umoja huu walilokusudia wakati wa kuanzisha chombo hiki mwaka 1997 hivyo nasisi lazima tulienzi na kulitekeleza.

Mhe. Makinda amesisitiza kuwa kwa miaka 17 iliyopita ya uhai wa Bunge hili la SADC wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutimiza malengo yake kama ilivyojiwekea katika Katiba yake ambayo ni kukuza na kuimarisha utawala wa kisheria, Kusimamia Masuala ya usawa wa Kijinsia, Utawala bora,pamoja na kukuza demokrasia katika ukanda wa SADC.

Aidha aliwakumbusha wajumbe na wanachama wa Bunge hilo kuwa, anachukua nafasi hiyo huku Bunge hilo likikabiliwa na changamoto lukuki za kiutendaji ambazo nyingine ni za kimuundo, kiuchumi na za kimkakati.

“Bado kuna haja ya kutatua changamoto mbalimbali ndani ya Bunge letu hususani Ukosefu wa namna bora ya kuwasilisha maamumizi ya Bunge hili ndani ya Utaratibu wa Jumuiya ya Wanacham wa nchi za SADC, Uwajibikaji hafifu kuhusu maamuzi ya Bunge hili kwa nchi wanachama, ukosefu wa namna bora ya kushirikiana na Bunge la Afrika, mawasiliano hafifu kati ya Chombo hiki na Mabunge ya Nchi wananchama, Uhaba wa rasilimali watu na fedha za kuendeshea chombo hiki. Alisema Makinda

Mkutano wa huo wa Bunge la SADC umemalizika rasmi jana baada ya pia kuchaguliwa makamu wa Rais wa Bunge hilo ambaye ni mhe. Njovya Lema Mbunge kutoka Malawi.

BENKI YA UWEKEZAJI YA ULAYA (E.I.B), YAIPIGA JEKI BENKI YA CRDB

$
0
0
BENKI ya CRDB imesaini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 43 baina ya benki ya uwekezaji Ulaya (E.I.B) kwa ajili ya kuwakopesha na kuwasaidia wafanyabiashara wanaofanya shughuli za kukuza uchumi.


Akizungumza jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei alisema benki yake kwa kushirikiana na EIB imeamuwa kusaidia jamii nchini hivyo mkataba huo ni mwanzo wa ushirikiano endelevu utakaohamasisha upatikanaji wa ajira.


Alisema kufanyakazi na benki ya EIB kutasaidia kukuza biashara katika maeneo muhimu kama uvuvi, usindikaji wa chakula, usafiri, biashara pamoja na huduma zote za kiuchumi.


“Mimi kama kiongozi wa CRDB Tanzania ninamamlaka ya kusaidia hizi sehemu za soko na kuongeza jitihada za kumaliza umaskini, pia kuongeza shughuli za kiuchumi za wateja wetu ili kufikia lengo la kuongeza mapato katika benki yetu,” alisema Kimei.


 Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alisema mkataba huo pia una lengo la kuisaidia benki ya CRDB katika kuendesha shughuli zake mbalimbali.


Alisema ni jambo la faraja kuona benki kama EIB imekubali kuiamini CRDB na kuipa mkopo wa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara.


“Tunachokiamini kuwa hii benki kutoka Ulaya siyo benki ndogo ni kati ya benki kubwa zilizopo hapa duniani, sasa kama wamekuja hapa kwetu na wakaonyesha nia njema ya kutusaidia endapo watabaini kuwa pesa zao azitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa watavunjika moyo,” alisema.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akiwasili ukumbini wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mkopo wa sh. Bilioni 43 kutoka Benki ya Uwekezaji Ulaya. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi CRDB, Martin Mmari na (katikati) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis (kulia) akisaini mkataba wa mkopo wa sh. bilioni 43 na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya Benki hiyo kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara Wadogo na Wakati. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB, Martin Mmari na Wa pili kulia ni, Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Eric Beaume.
Mwakilishi wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Nikolaos Milianitis (kulia) akibadilishana hati na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya benki hiyo kusaini mkopo wa billion 43 na benki ya CRDB kwa ajili ya kuwakopesha wafanyabiashara Wadogo na Wakati. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NBC BANK APPRECIATES ITS BEST PERFORMERS

$
0
0
NBC Bank Tanzania Managing Director, Pius Tabazarwa (R) awarding one of the banks Accounts Opening Centre best Performer, Shilwa Mwashemele at a function in Dar es Salaam at the weekend. Second left is NBC Head of Service Quality, Jane Dogani and banks Head of Customer Service, Ngwitika Mwakahesya.
NBC Bank Tanzania Managing Director, Pius Tabazarwa (R) presenting a certificate of excellence service recognition in supporting the Corporate Banking department to James Swai who works at the NBC Accounts Opening Centre at an occasion in Dar es Salaam. Looking on right is NBC Head of Customer Service, Ngwitika Mwakahesya and other officials.
NBC Bank Tanzania Managing Director, Pius Tabazarwa (R) presenting a certificate of excellence service recognition in supporting the Corporate Banking department to Anna Kalata who works at the banks Accounts Opening Centre at an occasion in Dar es Salaam at the weekend. Looking on right is NBC Head of Customer Service, Ngwitika Mwakahesya and other officials.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images