Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

KIBONZO CHA NATHANI MPANGALA


AFRICA DIASPORA MARKETPLACE III LAUNCHED AT TANZANIA EMBASSY

$
0
0
The Embassy of Tanzania in Washington, DC hosted the launch of the African Diaspora Marketplace III (ADMIII), on October 27th 2014. ADM is an opportunity for African diaspora members who are involved in businesses in their home country to acquire a grant from the United States Agency for International Development (USAID), which works together with Western Union and Homestrings to provide grants and technical support to these businesses. The Marketplace was initiated in 2009 in recognition that many Africans in the US are involved in projects in their home country but could use some extra help in terms of funding and technical support. ADM III will be open for application submission toward the end of 2014 and will focus mainly on funding African businesses that are looking to increase the use of ICT in their work. More information available at www.diasporamarketplace.org.
Jeffrey L. Jackson, Senior Private Sector Advisor, USAID speaking about the launch of ADM III. 
H.E. Ambassador Liberata Mulamula sharing her remarks to the audience of the ADM III launch. Since ADM I and II had only one Tanzanian participant, she encouraged those in the Tanzanian diaspora to take advantage of this opportunity and apply for the grant funding. As a woman Ambassador, she was heartened to announce that the ADM has a strong partnership with the African Womens Entrepreneurship Program (AWEP), and that there is a special effort to promote women-owned businesses.

Ambassadors and representatives of the African diplomatic corps in Washington DC.

MAADHIMISHO YA MWEZI WA HUDUMA KWA WATEJA WA NBC YAZIDI KUNOGA

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Rukia Mtingwa (kulia) akizungumza na mteja wa benki hiyo, Job Mwakibinga katika tawi la Mlimani City ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yanayoendelea ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja ambapo maofisa wa benki hiyo hutembelea matawi mbalimbali na kuhudumia wateja.
 Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Rukia Mtingwa (katikati) akizungumza na mteja wa benki hiyo, Job Mwakibinga katika tawi la Mlimani City ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja ambapo maofisa wa benki hiyo hutembelea matawi mbalimbali na kuhudumia wateja. Kulia ni Mkuu wa Matawi ya NBC, Gaudence Shawa.
 Mkuu wa Matawi ya Benki ya NBC, Gaudence Shawa (kulia) akizungumza na na mmoja wa mteja wa benki hiyo katika tawi la Mlimani City ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja ambapo maofisa wa benki hiyo hutembelea matawi mbalimbali na kuhudumia wateja.
 Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Rukia Mtingwa (kushoto) akizungumza na mmoja wa wateja wa benki hiyo katika tawi la Mlimani City ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Huduma kwa Wateja wa NBC.
Baadhi ya wateja katika Tawil la NBC Mlimani City wakipewa viburudisho wakati wakisubiri kuhudumiwa. Ili kuadhimisha mwezi wa huduma kwa wateja maofisa wa benki hiyo hutembelea matawi mbalimbali ili kuzungumza na kupata maoni yao kuhusu ubora wa huduma wazipatazo. 

MwanaFA kuangusha bonge la shoo nyumbani Tanga

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn  Mworia(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati alipokuwa akizungumzia kuhusiana na shoo ya”Vodacom life is better”itakayofanywa na msanii wa muziki wa kizazi kipya MwanaFA (kushoto)siku ya ijumaa katika klabu ya La Casachika mjini Tanga.Kulia ni Meneja wa msanii huyo Lusajo Mwaisaka.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya MwanaFA (kushoto)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na maandilizi ya shoo yake ya “Vodacom life is better”atakayoifanya siku ya ijumaa kwenye klabu ya La Casachika mjini Tanga,Anaeshuhudia katika ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia na kulia ni Meneja wa msanii huyo Lusajo Mwaisaka.


Wakazi wa Tanga wametakiwa kukaa mkao wa kula kwani  burudani ya nguvu ya muziki itapigwa moja kwa moja jukwaani siku ya tarehe 31 ya mwezi huu wa Oktoba katika ukumbi wa Lasachika mkoani humo.

Shoo hiyo ya kipekee na ya aina yake italetwa na si mwingine bali ni mkali wa muziki wa bongo flava nchini anayepasua anga ya Afrika ya Mashariki kwa vibao vyake mbalimbali si mwingine ni MwanaFA. Mwanamuziki huyo atafanya shoo laivu mkoani Tanga chini ya udhamini mkubwa wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania akisindikizwa na DJ Zero pamoja na mtangazaji wa Clouds FM B12.

Msanii MwanaFA mwenye mafanikio makubwa ya kimuziki wa kizazi kipya nchini amekuwa ni kivutio kikubwa kwa mashabiki wa ndani na nje ya nchi kila mahali anapoalikwa kufanya shoo na hivyo kujizolea sifa lukuki na hata kuchaguliwa kuwania tuzo mbali mbali za muziki nchini. 

Akizungumzia juu ya shoo hiyo ya kukata na shoka kwa wakazi wa mkoa wa Tanga, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia alisema Vodacom Tanzania wakiwa kama wadau namba moja wakuu wa kuinua tasnia hii ya muziki na michezo kwa ujumla wameamua kudhamini shoo ya “Vodacom Life is better”itayofanywa na MwanaFA  mkoani Tanga ikiwa ni sehemu ya burudani kwa wateja wao, kufurahi kwa pamoja na kuwashukuru kwa kuendelea kutumia huduma za kampuni hiyo.“Hivyo ndivyo Vodacom tunafanya maisha ya wateja wetu kuwa murua”.Alisema Mworia.

“Hakuna kitu ambacho tunajali na kukithamini kama wateja wetu, haijalishi wawe kona gani ya Tanzania, walipo popote tutawafikia. Vodacom imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kwa kipindi chote hicho watanzania wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya tuwe mtandao unaaongoza kwa mawasiliano nchini.” Alisema Mworia.

Kwa kuongezea Mworia amewaomba wakazi na mashabiki wote wa MwanaFA  na muziki wa Hip Hop  kujitokeza kwa wingi katika shoo hiyo iliyopewa jina la”Vodacom life is better show”kwani mbali na burudani kuwepo kutakuwepo na huduma na bidhaa mbali mbali za Vodacom. “Hivi ndivyo amabavyo Vodacom tunafanya maisha ya wateja wetu kuwa murua” alisema Mworia.

Naye MwanaFA alisema kwamba katika kunogesha  shoo yake hiyo ameamua kuambatana na DJ Zero ambaye atakuwa akifanya mambo yote kwenye jukwaa kwani ni mkali na anaijua kazi yake kwa hiyo shoo hiyo si ya kukosa kabisa kwani nimejipanga vya kutosha kuwaburudisha ndugu zangu wa nyumbani kwa hiyo uwepo wako tu pale utakufanya ujisikie vizuri kwani nitatenda haki kwenye shoo hiyo.Nawapenda sana wakazi wa Tanga na nipo tayari kuwaburudisha kama nifanyavyo sehemu zingine ndani nan je ya nchi.Alisema MwanaFA.

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA MWEZI WA WANAWAKE WAJASILIAMALI (MOWE) JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi rasmi wa Maonesho ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, wakati aliwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 28, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi Maonesho ya mwezi wa Wanawake Wajasiliamali (MOWE).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi msaidizi wa Kampuni ya Kazymate, Mariam Mjewa, kuhusu Jarida maalum la ‘Mchakarikaji’  wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Chupa ya kinywaji cha Dodoma Wine wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Oktoba 28, 2014.

Tanzania yaeleza mipango yake ya kuendeleza Jotoardhi

$
0
0
 Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi Kamati ya Watoa Maamuzi ya nchi zilizo katika Bonde la Ufa katika kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wa nchi zilizo katika Bonde la Ufa wakijadiliano jambo wakati wa kikao cha wajumbe hao kujadilia masuala mbalimbali kuhusu utekelezaji wa Jotoardhi kwa nchi wananchama.
 Baadhi wa Wajumbe wa Kamati ya Watoa Maamuzi wan chi zilizo katika Bonde la Ufa wakiendelea na kikao kujadili hatua mbalimbali zilizofikiwa na nchi wananchama katika masuala ya jotoardhi katika nchi zao, kuangalia faida zalke, changamoto na namna ya kuzitatua.
Mmoja wa Wakufunzi wa mafunzo yanayoendelea leo  kabla ya kufunguliwa rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa ya Jotoardhi akitoa mafunzo kwa baadhi ya washiriki wanaohudhuria mafunzo hayo jijini Arusha.

CHID BENZ APANDISHWA KIZIMBANI JIJINI DAR LEO KWA SHITAKA LA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA,AKOSA DHAMANA, KESI YAKE KUTAJWA TENA NOVEMBA 11

$
0
0
 Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini leo Dar es Salaam kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
 Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akiingia Mahakamani leo.
 Chidi Benzi akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi.

MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi Abdallah Makwaro (29), maarufa kama Chid Benz, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Chid Benz amefikishwa  mapema leo saa 3:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusomewa mashitaka yake. Saa 7:50 mchana alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo, hakimu aliamuru msanii huyo kutolewa nje ili akave vizuri nguo baada ya suruali aliyokuwa amevaa mlegezo maarufu kama kata kei kuonyesha nguo yake ya ndani.
“Kwanza mtoeni nje aende akavae nguo hizo zinazodondoka…” aliamuru Hakimu.

Saa 7:54 alirejeshwa ndani ya chumba cha mahakama upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Inspekta Jackson Chidunda, ulimsomea mashitaka yake.

Wakili Kombakono alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.

Wakili huyo wa serikali alidai kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na vifaa vinavyotumika kuvua dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.

Mshtakiwa alikana mashitaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na dhamana dhidi ya mshtakiwa.

Hakimu Lema alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazoamini na siyo walimu na dhamana ya Sh. Milioni moja.

Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na amepelekwa mahabusu hadi Novemba 11, kesi hiyo itakapotajwa.

NAIBU WAZIRI KAIRUKI AFUNGUA MAFUNZO YALIYOANDALIWA NA RITA NA NBS.

$
0
0
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Angellah Kairuki Jana alifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kuwajengea uwezo Maofisa wa Serikali watakaoshiriki Kuandaa Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kuboresha Mfumo wa Usajili na Upatikanaji wa Takwimu zake Nchini.

Mhe. Kairuki amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia maelekezo ya Wakufunzi kwa makini ili waweze kuandaa mpango kazi utakaotekelezeka ili kuleta mabadiliko makubwa katika Hali ya kiwango cha Usajili wa Matukio Muhimu kwa mwanadamu (Vizazi, Vifo, Ndoa na Talaka) hivyo kuchochea maendeleo nchini.

Mafunzo Hayo ya Siku Tano yanafanyika katika Hoteli ya Oceanic Bay, Bagamoyo na yanahusisha Wakurugenzi na Maofisa waandamizi kutoka Idara za Sera na Mipango wa Wizara ambazo ni Wadau wakuu wa Usajili wa wananchi, Maofisa wa RITA, NBS na idara nyingine za Serikali.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Mr. Yacob Zewodi, Bi Celia De Klerk na Bi. Thandi Makale ambao ni Washauri Waelekezi wa Kimataifa.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angellah Kairuki akifungua Mafunzo yaliyoandaliwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya kuwajengea uwezo Maofisa wa Serikali watakaoshiriki Kuandaa Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kuboresha Mfumo wa Usajili na Upatikanaji wa Takwimu zake Nchini.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bw. Phillip Saliboko akitoa maelezo kuhusu Mafunzo yali yofunguliwa.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angellah Kairuki katika picha ya pamoja na Washiriki.
Mafunzo yanaendelea...

KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI YATEMBELEA SUDAN

$
0
0
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji jana imeanza ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Ushirikiano wa Nchi za Bonde la Mto Nile (Nile Basin Initiatives) nchini Sudan.

Lengo la ziara hiyo ni kupata uelewa wa pamoja kuhusu ushirikiano uliopo katika kusimamia na kuendeleza rasilimali za Bonde la Mto Nile kati ya Nchi wanachama, huku Tanzania na Sudan zikiwa ni miongoni mwao.

Katika ziara hiyo Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe ambaye ameambatana na kamati hiyo amesema kwamba, dhumuni kuu la ziara hiyo ni kwenda kuona na kujifunza namna Sudan inavyotumia maji ya Mto Nile kwa ajili ya maendeleo yake kiuchumi katika shughuli za kilimo, ufugaji, utalii na biashara.

“Tanzania inachangia asilimia 28 ya maji ya Mto Nile na ina utajiri mkubwa wa rasilimali hii ya maji, hivyo hatuna budi kujifunza kutoka kwa wenzetu ili nasi tupate ufahamu mzuri na tuweze kupata maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali kupitia rasilimali hii. Na hatua ya kwanza ni kuona wenzetu wa Sudan wanafanya nini mpaka kufikia hatua kubwa waliyopiga leo hii”, alisema Prof. Maghembe.

Ziara hiyo ni mwaliko kutoka nchi ya Sudan na itachukua siku nne, itajumuisha kutembelea Bwawa la Merowe linalotumika kwa ajili ya kuzalisha umeme na shughuli za kilimo cha umwagiliaji, inategemewa kuleta tija kwa maendeleo ya Sekta ya Maji nchini na uchumi kwa ujumla.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na Kiongozi wa Kamati ya Bunge ya Kilimo Sudan, Dk. Habib Makhtom wakisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Kurugenzi ya Maandalizi ya Miradi Sudan, Inj. Mohamed Elsheikh.
Wajumbe ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji, Assa Hamad, Said Nkumba na Abdulsalaam Ameir wakiangalia moja ya mashine zinazotengenezwa katika kiwanda cha GIAD.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Prof. Peter Msolla, Meneja Mkuu wa kiwanda cha GIAD, Inj. Salah Dafaalla na Mjumbe wa Kamati, Abdallah Ali.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji wakisikiliza maelezo kutoka kwa moja ya wahandisi katika kituo cha Gridi ya Taifa ya Umeme Sudan.
Ujumbe kutoka Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa kituo cha Gridi ya Taifa ya Umeme Sudan.

MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZASERIKALI TANZANIA AKUTANA RAIS SHEIN

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania Ludovick Utoh alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania Ludovick Utoh alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi baada ya mazungumzo yao.[Picha na Ikulu.]

President Kikwete in Hanoi,Vietnam today

$
0
0
President Dr Jakaya Mrisho Kikwete lies a wreath at the Mausoleum of the First President Ho Chi Minh in Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014.
President Dr Jakaya Mrisho Kikwete visits the Hung Fen Food Stuff Corporation at Trung Son in Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014.
President Dr Jakaya Mrisho Kikwete in a souvenir photo with workers of the Garment 10 Corporation textile mill he visited at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014.
President Dr Jakaya Mrisho Kikwete shown some historical items as he visits the Garment 10 Corporation textile mill at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014.
President Dr Jakaya Mrisho Kikwete visits the Garment 10 Corporation textile mill at Nguyen Van Linh Street in Sai Dong Ward, Gia Lam District, Hanoi on his last leg of his two-day official visit to Vietnam today October 28, 2014.

Scholarships Oil and Gas

$
0
0
Since 2011 the University of Dar es Salaam (UDSM), specifically the Department of Chemical and Mining Engineering, the Norwegian University of Science and Technology (NTNU) of Norway and the Angolan University of Agostinho Netto are collaborating under the ANTHEI project to train professionals for petroleum engineering and geosciences at Masters level. Already three batches of a total of 28 Tanzanian students have been enrolled under the program. In this program the students spend one year in Norway for class work and another year at the University of Dar es salaam and the industry for project work and thesis. While in Tanzania the students are under the responsibility of the Tanzanian project coordinator at the University of Dar es Salaam with the support of local professors, NTNU Professors and Statoil Professionals. Statoil is a Norwegian oil Company already engaged in petroleum activities in Tanzania. Under the same scheme, another batch of 10 students will be granted scholarship next year (2015) to undertake M.Sc. in Petroleum Engineering and in Petroleum Geosciences. The scholarship covers subsistence allowance (stipend), travel grant to and fro, tuition, insurance and stationeries. The certificate will be issued by NTNU. Read more from the following link http://www.wavuti.com/2014/10/scholarship-for-statoil-master.html#more

TAARIFA YA KUKOSEKANA HUDUMA YA MAJI KWA SIKU MBILI JIJINI DAR

$
0
0
Dawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48  kwa siku za Alhamisi na Iijumaa ya tarehe 30 na 31 Octoba 2014, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ili kuruhusu mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (cross-connection) katika mtambo wa Ruvu Chini eneo la Chambezi, Bagamoyo. 

Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji; 
Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe. 

Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya rufaa Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na Keko.       
Wananchi mnashauriwa kuhifadhi maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.
Au piga simu huduma kwa wateja namba 022- 2194800  / 0658-198889
Dawasco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na ofisi ya uhusiano, 
Dawasco - Makao Makuu.

FORUM TO PROMOTE SUSTAINABLE MOUNTAIN DEVELOPMENT AGENDA IN AFRICA ESTABLISHED

$
0
0
The first Africa Mountains Regional Forum closed Friday at Ngurdoto Mountain Lodge in Arusha, Tanzania, and called upon African states to develop and implement mountain-specific policies and laws and mainstream sustainable mountain development in their national development agenda. The forum that attracted over 100 participants from different African countries formally established the African Mountain Forum as the main coordinating body to promote the sustainable mountain development agenda in Africa. 

 “The mountain places across Africa are under attack because of the belief that the closer you are [to the mountain], the better the status that you have,” said Hon. Lazaro Nyalandu, the Tanzanian Minister for Natural Resources and Tourism and the chief guest. “We have invited Members of Parliament from Arusha and Kilimanjaro regions to discuss the creation of the Mt. Kilimanjaro and Meru Ecosystem Protection Fund. Something has to be done, we are going to protect this ecosystem.”

 The meeting was also attended by Uganda’s Minister of State for Environment, Hon. Flavia Munaaba Nabugere. The mountains forum was organized by the East African Community in partnership with Albertine Rift Conservation Society (ARCOS) and the Africa Mountain Partnership Champions Committee (AMPCC).

 It was made possible with support from the US Agency for International Development-East Africa (USAID/EA) which is supporting the EAC Biodiversity agenda through the PREPARED Programme, as well as the United Nations Environment Programme (UNEP), Austrian Development Cooperation and the Swiss Agency for Development and Cooperation. 

 The Principal Environment and Natural Resources Officer, East African Community, Ms. Wivine Ntamubano, who represented the Hon. Jesca Eriyo, EAC Deputy Secretary General, Productive and Social Sectors, said, “The East African Community’s emphasis is on the protection and conservation of shared trans-boundary, environment, natural resources and ecosystems that call for common approaches and collective measures. ” 

Trans-boundary mountains in the region include the Mt. Elgon, which bestride Kenya and Uganda; the Virunga range shared by Rwanda, Uganda and Democratic Republic of Congo and Mt. Rwenzori at the border of Uganda and DR Congo. Mountains are the water towers of the world, supplying half the world’s population with freshwater for drinking, domestic use, irrigation, industry and hydropower.

 Given the growing scarcity of water resources, experts say integrated and proper management of mountain water resources should become a global priority. The forum concluded with the adoption of the Arusha Outcomes in which the delegates requested the African Union together with the African Ministerial Conference on the Environment (AMCEN), Regional Economic Communities and other partners to adopt an Africa regional mountain agenda together with its governance framework for sustainable mountain development in Africa. The participants also called for inter-sectoral collaboration in the protection and management of African mountains given their critical importance as water towers, centers for economic development and a source of livelihoods for the mountain communities.
Left to Right - Hon. Flavia Munaaba, Ms. Wivine Ntamubano, Dr. Sam Kanyamibwa and Hon. Lazaro Nyalandu at the Africa Mountains Regional Forum

COMESA, EAC, SADC MINISTERS AGREE TO LAUNCH AFRICA’S LARGEST FREE TRADE AREA

$
0
0
The Tripartite Sectoral Committee of Ministers meeting in Bujumbura, Burundi from 24 – 25 October 2014, agreed that the Tripartite Summit of Heads of State and Government to be held in Egypt in mid-December 2014 would launch the Tripartite Free Trade Area taking into account the fact that the majority of the Tripartite Member/Partner States have made ambitious tariff offers and were agreed on Rules of Origin to be applied in the interim whilst further work continues on product specific Rules of Origin.

The Tripartite Free Trade Area encompassing 26 Member/Partner States from the Common Market for Eastern and Southern Africa (COMESA), East African Community (EAC) and the Southern African Development Community (SADC), with a combined population of 625 million people and a Gross Domestic Product (GDP) of USD 1.2 trillion, will account for half of the membership of the African Union and 58% of the continent’s GDP.

The Tripartite FTA popularly known as the Grand Free Trade Area, will be the largest economic bloc on the continent and the launching pad for the establishment of the Continental Free Trade Are (CFTA) in 2017.

The Tripartite Free Trade Area offers significant opportunities for business and investment within the Tripartite and will act as a magnet for attracting foreign direct investment into the Tripartite region. The business community, in particular, will benefit from an improved and harmonized trade regime which reduces the cost of doing business as a result of elimination of overlapping trade regimes due to multiple memberships.

The launching of the Tripartite Free Trade Area is the first phase of implementing a developmental regional integration strategy that places high priority on infrastructure development, industrialization and free movement of business persons. In order for the Tripartite FTA to realize inclusive and equitable growth, the meeting agreed on the need for expeditious formulation and implementation of a regional industrial programme.

The Chairperson of the Ministerial meeting, Honourable Chiratidzo Iris Mabuwa, Deputy Minister of Commerce and Industry of Zimbabwe, hailed the agreement to launch the Grand FTA as a milestone in regional and continental integration.

“Africa has now joined the league of emerging economies and the grand FTA will play a pivotal and catalytic role in the transformation of the continent”, she declared at the close of the meeting. “We have made significant progress in negotiations on trade in goods, and we now need to expedite negotiations on trade-related areas, including trade in services, intellectual property and competition policy to ensure equity, among all citizens of the wider region”, she declared.

ISSUED BY MR. SINDISO NGWENYA, SECRETARY GENERAL OF COMESA AND CHAIRPERSON OF THE COMESA-EAC-SADC TRIPARTITE TASK FORCE

Bujumbura, Burundi, 25 October 2014

CHANGAMKIENI FURSA ZA MWANAMKE NA UCHUMI - MH. DENDEGO

$
0
0
Na Christian Gideon, Angels moment.

Wanawake wajasiriamali mkoani Tanga wametakiwa kujitokeza na kuchangamkia fursa zitakazotolewa na kampeni ya mwanamke na uchumi inayotarajiwa kutolewa mwanzoni mwa mwezi ujao mkoani Tanga ambapo zaidi ya wanawake 300 watanufaika na mafunzo hayo yanayotolewa na kampuni ya Angels Moment ya jijini Dar Es Salaam.

Mkuu wa wilaya ya Tanga Mheshimiwa Halima Dendego amesema fursa zitakazotolewa ni fahari kwa wanawake na wajasiriamali wa mkoa huo kwani elimu inahitajika sana wakati huu wa ushindani wa biashara “ Fursa kama hizi mara nyingi ni nadra kuzipata na Kampeni ya mwanamke na uchumi ni jibu la changamoto mbalimbali kwa wajasiriamali kwani elimu watakayoitoa ni fursa pekee ya kusonga mbele kibiashara na kiuchumi kwa wanawake wa mkoa wa Tanga” alisema.

Mkuu huyo wa wilaya amewaomba Wadau mbalimbali waendelee kujitokeza kuunga mkono juhudi za Kampeni ya mwanamke na uchumi kwani kupitia akina mama huduma zao zitaweza kufahamika na kunufaika kwani ndiyo nafasi pekee ya kukutana na wajasiriamali na kusaidia kuinua uchumi wa akinamama na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mahada Erick amesema kuwa kampeni ya mwanamke na uchumi ni jawabu la changamoto zinazokumba biashara na ujasiriamali kwani elimu na semina zitakazotolewa zitawapa msingi wa kuanza upya kuandaa biashara na ujasiriamali kwa ujumla na pia kutoa hamasa kwa akinamama katika kujiletea maendeleo.

“ Kampeni hii inalenga kutoa hamasa na ari kwa akinamama kusonga mbele kimaendeleo, Hakuna ubishi kuwa akinamama wana juhudi kubwa sana za kutafuta fursa za kujiongezea kipato, ila tatizo ni elimu ya msingi ya kuangalia fursa zinazowazunguka na jinsi ya kuendeleza biashara zao.”

Angels Moment itawakutanisha akinamama waliofanikiwa kibiashara na ambao wanafanya ujasiriamali mbalimbali ili kuelezana mbinu mbalimbali za mafanikio. Pia kutakuwa na wataalamu watakaotoa elimu ya ujasiriamali, uwekezaji, uwekaji akiba na elimu ya afya’ anasisitiza.

Kampeni ya Mwanamke na uchumi Mkoani Tanga itafanyika tarehe tano na sita mwezi ujaokatika Ukumbi wa Naivera ambapo utapambwa na msanii Linah Sanga ambaye ni balozi wa Wanawake.

Wadau walioungamkono kampeni ya mwanamke na uchumi ni MKoani Tanga ni pamoja na SSRA,NSSF,TBS,PSPF,GEPF,AGHAKHAN HOSPITAL,MINJINGUMAZAO,HSC, na NAIVERA COMPLEX .
Mkuu wa wilaya ya Tanga mheshimiwa Halima Dendego akitoa wito kwa taasisi na mashirika mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi za kampeni ya mwanamke na uchumi Zinazotolewa na kampuni ya Angels Moment ili kumkomboa mwanamke mjasiriamali.
Mkurugenzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mahada Erick {kulia} akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kampeni ya mwanamke na uchumi itakayotolewa tarehe 5 na 6 mwezi ujao mkoani Tanga,kushoto ni mkuu wa wilaya ya Tanga mheshimiwa Halima Dendego.

customized wristbands for you

MSANII LULU AITAMBULISHA FILAMU YAKE MPYA IITWAYO MAPENZI YA MUNGU LEO.FILAMU YAINGIA SOKONI LEO

$
0
0

 Msanii wa Sanaa ya Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Alipokuwa akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo amewashirikisha Flora Mtegoha au Mama Kanumba na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Linah Sanga.

 Msanii Wa Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU leo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).,Kulia ni Mmoja kati wa wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ajulikanae kama Flora Mtegoha almaarufu kama Mama Kanumba

Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Evance Stephen akiongea na wanahabari leo katika Ofisi za Proin Promotions Ltd zilizopo Mikocheni mtaa wa Ursino wakati wa Utambulisho wa Filamu mpya ya Lulu Iitwayo MAPENZI YA MUNGU.

Msanii Elizabeth Michael aka Lulu leo ametambulisha Filamu yake Mpya ambayo imeingia sokoni leo iitwayo MAPENZI YA MUNGU, huku akiwa amemshirikisha Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga na Mama Kanumba.

Wakati akiilezea filamu hiyo leo mbele ya wanahabari Lulu amesema Kuwa Ni Filamu inayofundisha na Kutoa somo kwa mtu yoyote yule ambae yupo hapa duniani kwa kuendelea kuonyesha kuwa MUNGU YUPO. Akiongezea kuwa..."Sisi kama binadamu tumekuwa tukifanya mambo mengi sana hapa Duniani na kupelekea kumsahau Mungu na pengine kuendelea kufikiria kuwa yote tuyafanyayo ni kwa uwezo wetu kumbe Sio uwezo wetu na Ni Mapenzi ya Mungu tu ndio yanayofanya sisi kufikia hapa tulipo leo"

Filamu ya MAPENZI YA MUNGU imekuwa gumzo kabla ya kutoka kutokana na watanzania wengi kuwa na shauku ya Kutaka kumuona Lulu tena mara baada ya Kuonekana  katika Filamu Zake Mbili zilizotangulia za FOOLISH AGE na FAMILY CURSE. Sasa Lulu kuonekana tena katika kiwango cha Juu katika Filamu hii Mpya ambayo imeingia Sokoni Leo.

Filamu ya MAPENZI YA MUNGU ni filamu inayosambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.

Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii yafanya ziara katika Miradi mitatu ya NSSF jijini Dar

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Rajabu (aliesimama) akizungumza wakati wa kuwakaribisha Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii,waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.Katika ziara hiyo ya Wabunge chini ya Mwenyekiti wao,Mh. Said Mtanda (katikati) walivutiwa sana na maendeoe ya miradi hiyo na hivyo kulipongeza Shirika la NSSF kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya.Picha zote na Othman Michuzi.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (aliesimama) akifafanya jambo mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam
Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akielekeza jambo wakati akitoa taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (wa pili kulia mbele) akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda alieambatana na ujumbe wake wakati wakitembelea miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii wakiangalia namna maji yanavyotolewa chini kwa ajili ya kuweka nguzo za Daraja la Kigamboni.

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images