Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

NECTA yafanikiwa kudhibiti udanganyifu na wizi wa mitihani ya taifa nchini.

$
0
0
 Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) bw. Daniel Mafie akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Baraza hilo ikiwemo matumizi ya TEHAMA katika usajili wa watahimiwa na uchakataji wa matokeo ya Mitihani ya Taifa. Kulia ni Afisa Habari wa NECTA John Nchimbi.
  Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Bw. Daniel Mafie akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar s salaam kuhusu utaratibu wa kutoa nakala za vyeti kwa watahimiwa waliopoteza vyeti vyao ambapo utaratibu huo unahusisha uchunguzi wa uhalali wa mwombaji.  Kulia ni Afisa Habari wa NECTA John Nchimbi na kushoto ni Msaidizi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Bi Glee Magemba.
.Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) na Vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga  kuonyesha mafanikio ya Baraza hilo nchini.(Picha na Frank Mvungi-MAELEZO).
 
Frank- Mvungi - MAELEZO
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limedhibiti na kuondoa kabisa tatizo la wizi wa Mitihani ya Taifa na udanganyifu wakati wa Mitihani katika ngazi mbalimbali za elimu nchini.

Mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliopo kati ya NECTA na kamati za uendeshaji mitihani katika ngazi za mikoa na wilaya ili kutatua tatizo la wizi wa mitihani ya taifa na udanganyifu wakati wa mitihani uliokuwa ukifanywa kinyume na taratibu za baraza la mitihani.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza hilo Bw. Daniel Mafie wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jjijini Dar es salaam uliolenga kueleza mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa.

Akifafanunua Mafie amesema kuwa katika mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 13 tu ikilinganishwa na watahiniwa 9,736 waliobainika kufanya udanganyifu mwaka 2011.

Aidha Mafie aliongeza kuwa katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 272 ikilinganishwa na watahimiwa 789 mwaka 2012 na 3,303 mwaka 2011.

Akieleza zaidi kuhusu mafanikio yaliyofikiwa Mafie alisema Baraza hilo limeweza kusanifu mifumo ya Kompyuta yenye uwezo wa kupanga shule katika makundi ya ubora wa ufaulu katika matokeo ya mitihani ya Taifa.

Katika kukabiliana na tatizo la watu wanaotumia vyeti vya watu wengine au kughushi vyeti wakati wa kuomba ajira au nafasi za masomo katika shule mbalimbali ambapo kuanzia mwaka 2008/2009 Baraza hilo lilianzisha utaratibu wa kuweka picha za watahimiwa katika vyeti vyao.

Katika utaratibu huo vyeti hivyo viliwekewa alama za kiusalam hali ambayo imesaidia Baraza hilo kuwa na uwezo wa kubaini kwa haraka na kuwachukulia hatua wale wanaoghushi vyeti au kutumia vyeti vya watu wengine.

Baraza la Mitihani la Tanzania ni Taasisi ya Umma iliyochini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyoanzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 21 ya mwaka 1973 na marekebisho yake ya mwaka 1998 na 2002 kwa ajili  ya kuendesha mitihani ya Taifa kwa lengo la kuweka misingi ya sera ya mitihani, kuendesha mitihani na kutunuku stashahada mbalimbali na vyeti kwa watahiniwa wanaofuzu na kufaulu mitihani iliyo chini yake kisheria.


WAZIRI NYALANDU ARUHUSU WANANCHI WANOENDA KWENYE MATIBABU KITUO CHA AFRICA AMINI KUPITA BILA KULIPA HIFADHINI

$
0
0

Waziri Nyalandu akitoa maamuzi ya serikali kuhusiana na hadha hiyo ambapo ameruhusu wananchi wanaoelekea katika kituo hicho kwa ajili ya kupata matibabu wapite bila ya kutozwa chochote.


Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Arusha(ANAPA) Betrita Loibook akizungumza juu ya tozo hiyo.


Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akizungumza juu ya Adha wanayoapata wakazi wa Vijiji vya jirani na hifadhi ya Arusha ya kutakiwa kutoa tozo kwa ajili ya kupita katika barabaara ya hifadhi hiyo wakati wakielekea katika kituo hicho cha Afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.


Mkurugenzi wa Kituo cha Africa Amini Cornellia Walner akitoa maelezo mbele ya Waziri Nyalandu,Mbunge Nassar na Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa(ANAPA) Betrita Loibook.


Waziri Nyalandu akiteta jambo na mmoja wa wafanyakazi katika kituo hicho aliyefahamika kwa jina la Jamilah Mongi.

TAARIFA KWA UMMA- UREJESHAJI FOMU ZA TAMKO LA MALI NA MADENI

$
0
0
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inawataarifu Viongozi wote wa Umma nchini kwamba tarehe ya mwisho ya kurejesha Fomu za kutolea TAMKO LA RASILIMALI NA MADENI ya viongozi kwa Kamishna wa Maadili kwa mwaka huu ni tarehe 31/12/2014. Fomu hizo za kutolea tamko zimeanza kutolewa na zinapatikana katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma makao makuu Dar es Salaam na katika ofisi za Kanda za Mashariki Kibaha, Arusha, Dodoma, Tabora, Mwanza, Mbeya na Mtwara. Pia Fomu hizo zinapatikana katika Tovuti ya taasisi kupitia www.ethicssecretariat.go.tz na katika tovuti ya Serikali ya www.tanzania.go.tz

Viongozi wa Umma wanapaswa kuelewa kuwa ni Ukiukaji wa Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Kiongozi kushindwa kurejesha Fomu za Tamko lake katika muda uliowekwa na Kiongozi atakayeshindwa kurejesha kwa tarehe husika atachukuliwa hatua kama ambavyo kifungu cha 15 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995 kinavyoeleza. 

Viongozi wa umma wanapaswa kukumbuka kuwa sio wajibu wa kisheria kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi kuwa pelekea viongozi fomu za tamko bali ni wajibu wa kiongozi husika kuzitafuta fomu hizo kwa wakati  ili kutekeleza matakwa hayo ya kisheria.


IMETOLEWA NA
KAMISHNA WA MAADILI

JENGO LA NSSF KUBADILI TASWIRA YA MJI WA MOSHI

$
0
0
 Jengo jipya linalojengwa na Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kukamilika kwake kutabadili taswira ya mji wa Moshi kwa kiasi kikubwa.Ni jengo ambalo limejengwa kisasa ambalo kukamilika kwake kutapendezesha mji wa Moshi. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI KATIKA HAFLA YA KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA RUFIJI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Rufiji ambae pia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid wakati wa hafla ya kuchangia miradi ya maendeleo ya Jimbo la Rufiji iliyofanyika jana jioni Oktoba 26,2014 katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es salaam, ambapo jumla ya shilingi milioni 903 zilipatinana na kuweza kuvuka malengo ya zilizokuwa zikihitajika awali shilingi milioni 500.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua hafla ya kuchangia miradi ya maendeleo ya Jimbo la Rufiji iliyofanyika jana jioni Oktoba 26,2014 katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es salaam, ambapo jumla ya shilingi milioni 903 zilipatinana na kuweza kuvuka malengo ya zilizokuwa zikihitajika awali shilingi milioni 500.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid katikati wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi waliochangia miradi ya maendeleo ya Jimbo la Rufiji iliyofanyika jana jioni Oktoba 26,2014 katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es salaam, ambapo jumla ya shilingi milioni 903 zilipatinana na kuweza kuvuka malengo ya zilizokuwa zikihitajika awali shilingi milioni 500. (Picha na OMR)

UFAFANUZI KUHUSU UHABA WA DAWA MUHIMU NA VIFAA TIBA

$
0
0


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMI.

Kuna taarifa katika vyombo vya habarii liyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la SIKIKA ,kwamba serikali haijalipa kiasi cha shilingi bilioni 90 kwa bohari  kuu ya dawa  na kusababishia ukosefu  dawa katika baadhi ya hospitali.

Ni kweli bohari kuu ya dawa imepungukiwa fedha za kununulia dawa , lakini sio kwa kiasi cha kushindwa kutoa huduma kabisa  kama inavyoelezwa.  Kiasi cha pesa kinachotajwa  si kigeni na serikali imekua ikitoa kiasi cha fedha kidogo kidogo ili kuongeza uwezo wa bohari  ya dawa iweze kufanya kazi ya kununua na kusambaza dawa.

Katika kukabiliana  na hali hii hospitali zote kupitia waganga wakuu wa mikoa na wilaya zimeagizwa kupeleka asilimia  50 ya mapato yanayotokana na uchangiaji kwenda bohari kuu ya dawa.

Kuhusu ukosefu wa matibabu katika Taasisi ya Saratani ocean road,  ni kweli kwa sasa baadhi ya mashine hazifanyi kazi na zinazofanya kazi ni chache hivyo kuzidiwa  wakati fulani.Hatahivyo wizara imekwisha agiza vifaa hivyo ambavyo ni ghali sana toka Canada na vinategemewa kufika wakati wowote kuanzia sasa na pia ikumbukwe kuwa matibabu yanatotolewa  bila malipo na gharama zote  ni za serikali.

Wizara kwa sasa imeagizwa katika mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN)ambapo wataalam wanamalizia kazi za utekelezaji wa mpango huo. Ambapo pia umezingatia namna ya kukabiliana  na jinsi ya kuhakikisha


dawa zinapatikana kwa wakati katika vituo vya matibabu  na kuiboresha zaidi bohari ya dawa. Baada ya kuanza utekelezaji huo suala la ukosefu wa dawa  na vifaa tiba utapungua  kwa kiasi kikubwa  sana.

Pamoja na wizara kupeleka bohari tyadawa pesa kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba, hospitali zihakikishe zinapeleka asilimia 50 ya mapato kama zilivyoagizwa na kutokufanya hivyo kiongozi husika atawajibishwa.

Mwisho wizara inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba dawa na vifaa tiba muhimu vinapelekwa katika vituo vyote , pia inaendelea kufanya kazi na taasisi zote zisizo za kiserikali kwa karibu kwa faida ya wananchi wote.

Imetolewa na :-


Dkt. Seif S. rashidi (Mb)
WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII



27/10/2014

Jotoardhi kichocheo cha Uchumi - RC Arusha

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Arusha
Imeelezwa kuwa, nguvu ya nishati mchanganyiko ikiwemo jotoardhi ni kichocheo na kipimo cha maendeleo kwa nchi yoyote kutokana na umuhimu wa nishati hiyo kwa  shughuli mbalimbali  zikiwemo za uchumi na  viwanda.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa  Wilaya ya Arusha John Mongela wakati akifungua mafunzo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo, kuhusu masuala yanayohusu  jotoardhi yaliyoanza leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

Mafunzo hayo yanashirikisha washiriki takriban 150 kutoka nchi mbalimbali za Afrika zilizo katika bonde la ufa na  nchi nyingine duniani.

Aidha, ameongeza kuwa, mafunzo hayo ni muafaka kwa Tanzania kutokana na uzoefu ambao washiriki wataupata kutoka nchi nyingine ambazo zimepiga hatua katika masuala ya jotoardhi kama Kenya na Ethiopia  ambazo zimechangia katika gridi ya Taifa ya nchi zao kiasi cha megawati 500 za nishati ya umeme unaotokana na jotoardhi.

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia nishati jadidifu, Wizara ya Nishati na Edward Ishengoma, ameeleza kuwa, mafunzo hayo na uwepo wa kongamano hilo kwa Tanzania kuna manufaa makubwa.

Ishengoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la tano la Kimataifa la Jotoardhi alitaja manufaa hayo kama kutangaza hazina kubwa ya jotoardhii iliyopo Tanzania, jambo ambalo litasaidia kuvutia wawekezaji na taasisi zinazofanya utafiti wa masuala ya jotoardhi.

Ameongeza kuwa, nishati ya jotoardhi ni nishati isiyokwisha hivyo uwepo na matumizi yake yatasaidia katika ukuaji wa viwanda ikiwemo kuchangia katika sekta za kilimo na manufaa yake ni makubwa  kimaendeleo.

“Jotoardhi ni chazo ambacho hakiishi. Uzalishaji wake hauna mwisho na una manufaa makubwa. Tanzania tunataka kukiendeleza chanzo hiki kama wenzetu Kenya na Ethiopia”amesisitiza Ishangoma.

Aidha, mafunzo hayo ni mwendelezo wa shughuli mbalimbali zitakazofanyika katika kongamano la tano la Kimataifa la Jotoardhi litakalofunguliwa rasmi tarehe 29 Oktoba, 2014, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal.

Washiriki wa kongamano hilo pia watapata fursa ya kutembelea katika maeneo yenye dalili za jotoardhi ikiwemo Ngorongoro na Manyara lakini pia watapata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela akiongea jambo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku mbili kuhusu masuala ya jotoardhi kwa washirki kutoka nchi zilizo katika bonde la Ufa . Mafunzo hayo yanatangulia kabla ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi litakalofunguliwa tarehe 29 Oktoba, 2014 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
Baadhi ya washiriki wanaohudhuria mafunzo kuhusu masuala la jotoardhi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela hayupo pichani wakati akifungua rasmi mafunzo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela (katikati) akiongea jambo na Kamishna Msaidizi anayeshughulia Nishati Jadidifu , Wizara ya Nishati na Madini, Edward Ishengoma (kushoto) mara baada ya kufungua mafunzo kuhusu masuala yanayohusu jotoardhi.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya masuala ya jotoardhi kutoka nchi zilizo katika bonde kla ufa na nyi nyingine duniani, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela (wan ne kulia).

Dkt. Shein akutana na viongozi mbali mbali ikulu Zanzibar leo

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Muhamed Shein akisalimiana na Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Alvaro Rodriguez alipofika Ikulu Mjini Unguja kwa mazungumzo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Muhamed Shein akifuatana na Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Alvaro Rodriguez baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Muhamed Shein akisalimiana na Balozi Mteule wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Rwanda Ali Said Siwa alipofika Ikulu Mjini Unguja kwa madhumuni ya kumuaga Rais leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Muhamed Shein akizungumza na Balozi Mteule wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Rwanda Ali Said Siwa alipofika Ikulu Mjini Unguja kwa madhumuni ya kumuaga Rais leo baada ya kuteuliwa wadhifa huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Muhamed Shein akisalimiana na Balozi Mpya wa Ufaransa Nchini Tanzania Bibi Malika Berak akiyefika Ikulu Mjini Unguja leo kujitambulisha kwa Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Muhamed Shein akifuatana na Balozi Mpya wa Ufaransa Nchini Tanzania Bibi Malika Berak baada ya mazungumzoyao alipofika Ikulu Mjini Unguja leo kujitambulisha.[Picha na Ikulu.]

21ST MEETING OF THE SECTORAL COUNCIL OF MINISTERS RESPONSIBLE FOR EAC AFFAIRS AND PLANNING ONGOING IN KIGALI

$
0
0
East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania, 27 October 2014:  The 21st Meeting of the Sectoral Council of Ministers responsible for EAC Affairs and Planning (SCMEACP) is currently underway at the Lemigo Hotel in Kigali, Rwanda.

The meeting is considering the status of implementation of Previous Decisions of the SCMEACP; progress report on the status of implementation of the EAC Common Market; status of the EAC Institutional Review.

The meeting will also consider a proposal on the Tenure of Service for Professional Staff of the Community; report on Political Affairs; report of the 3rd Secretary General’s Forum; status of implementation of the Video Conferencing Project; progress Report on the Elimination of Non-Tariff Barriers; and lastly progress report on COMESA-EAC-SADC Tripartite Arrangement.

The 21st meeting of the Sectoral Council will be held through the session of Senior officials from 27th to 29th October; the session of Permanent/Principal Secretaries from 29th to 30th October; and the Ministerial session is on 31st October 2014.

At the official opening of the session of Senior Officials this morning, the EAC Deputy Secretary General (Finance and Administration), Mr. Jean Claude Nsengiyumva expressed the Secretariat’s appreciation to the Government and people of Rwanda for the warm and cordial hospitality extended to all delegations upon their arrival in this beautiful city of Kigali.

The Deputy Secretary General reiterated the critical role of the Sectoral Council in coordinating the regional integration process and said that as the integration process deepens and widens, the Senior Officials will be heavily relied on to provide rational strategies on the integration, noting that their pragmatic recommendations and guidance will assist in further advancing the cause of regional integration and development process.
Chair of senior officials session mr. alfred kitolo, ag. integration secretary, ministry of eac, commerce and industry, kenya making remarks
group photo opportunity

MAMA SALMA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA KOREA KASKAZINI,PAMOJA NA MAMA RACHEL RUTO

$
0
0
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Kaskazini Bwana Kim Yong Nam. Mama Salma alikutana na kiongozi huyo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta ulioko Nairobi tarehe 26.10.2014 akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea nchini China.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Naibu Rais wa Kenya Mama Rachel Ruto kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata mjini Nairobi tarehe 26.10.2014. Mama Salma alisimama kwa muda uwanjani hapo akiwa njiani kurejea nchini akitokea Beijing nchini China kwenye safari ya kikazi. PICHA NA JOHN LUKUWI

Kairuki touts Rule of Law for development

$
0
0
The Government has reiterated its support to the international bodies that are aimed at enhancing the rule of law in the world saying without peace in the world there can be no development.

Speaking in Dar es Salaam today (Monday, October 27, 2014), the Deputy Minister for Constitutional and Legal Affairs Hon. Angellah Kairuki observed that peace and rule of law were inseparable from development.

“We highly value the contributions of international courts and tribunals in advancing the rule of law and peace keeping at the international and national levels,” she said while opening one-week training on the Rule of Law for Judicial Affairs Officers in the United Nations Peacekeeping Operations in Dar es Salaam.

The one-week training is jointly organized by the United Nations Department of Peacekeeping Operations (DPKO), the East Africa Law Society, the Germany’s Centre for International Peace Operations (ZIF).  

“Without peace and the rule of law there can be no development,” she revealed noting that rule of law is the very essence and bedrock of any democratic and successful society.

Ms. Kairuki reminded participants to the meeting about difficulties arising from conflicts and urge them to explore ways of addressing them.

“This training is coming at a time when the Great Lakes Region still smells the blood of innocent men and women … as you look at the Central African Republic, I urge you to go further and explore ways in which Peacekeeping Operations can work together with local actors so that loss of lives can be avoided,” she said in a meeting also attended by Germany Ambassador to Tanzania, Mr. Egon Kochanke.

Others who attended were Mr. Cerian Sebrogondi, Head of European Union (EU) Delegation to Tanzania; Mr. James Mwamu, President of the EALS; Mr. Charles Brieffel and Ms. Stefanie Kirschweng from the Criminal Law and Judicial Advisory Service (CLJAS) and Centre for International Peace Operations (ZIF) respectively who jointly organized the training with the EU, the East Africa Law Society (EALS) and the Criminal Law and Judicial Advisory Service of the United Nations Department of Peacekeeping Operations (DPKO).
Group Photo.

BALOZI SEFUE AFUNGUA MKUTANO WA MAKATIBU WAKUU NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA ,MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa Siku mbili wa Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa hapa Nchini.Mkutano huu wa siku Mbili unafanyika katika Hoteli ya St.Gaspar Mjini Dodoma unawashirikisha pia Manaibu makatibu wakuu wa Wizara zote.
Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa Hapa Nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati akifungua Mkutano wa siku Mbili wa watendaji hao katika Hoteli ya St.Gaspar Mjini Dodoma. Na Deusdedit Moshi Globu ya Jamii Kanda ya kati.

TASWIRA YA DARAJA LA MANZESE JIJINI DAR WAKATI WA JIONI

$
0
0
Wakazi wengi wa maeneo mbali mbali ya jiji la Dar wakiwa wamepozi huku wengine wakipiga soga juu ya Daraja la kuvukia watembea kwa miguu Manzese,Eneo hili limekuwa likipendwa sana na watu hao hasa katika nyakati za sikukuu au mapumziko ya mwisho wa wiki kama walivyonaswa na Mwanalibeneke Othman Michuzi.

MTAA KWA MTAA YA MICHUZI TV JIJINI MBEYA LEO

Isomeni Katiba Mpya Inayopendekezwa sura kwa sura na ibara kwa ibara ili muweze kupata uelewa - Dkt. Migiro

$
0
0
Na Magreth Kinabo

WANANCHI   wameshauriwa kuisoma Katiba Mpya Inayopendekezwa  sura kwa sura na ibara kwa ibara ili waweze kupata uelewa wa masuala mbalimbali yaliyomo ndani ya Katiba hiyo na kuacha kusikiliza maneno  ya watu yenye nia ya kupotosha ukweli.

Kauli hiyo ilitolewa jana  na  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha   Rose Migiro wakati  wa sherehe za mahafali ya pili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana  wanaoishi katika mazingira hatarishi  ya WAMA  Nakayama, iliyopo  wilayani Rufiji  mkoani Pwani.

Dkt . Migiro  ambaye  alikuwa mgeni  rasmi katika sherehe hiyo, ambayo ilihudhuriwa na  baadhi ya viongozi , wakiwemo  baadhi ya wake za viongozi   na wageni  wengine mbalimbali.

“Nchi yetu ilikuwa katika mchakato wa uandikaji wa Katiba Inayopendekezwa kazi  ambayo ilikamilika Oktoba 8, mwaka huu. 
 kazi iliyombele  yenu  ni kuisoma Katiba hii sura kwa sura ibara kwa ibara. 

"Tusikubali kusomewa  na tutakapokamilisha kazi ya kuisoma tuipigie kura ya ndiyo,” alisema Dkt. Migiro.

Akizungumza na katika mkutano wa mabalozi wanazoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu wa China uliofanyika kwenye Nyumba ya kufikia Wageni ya Serikali ya Diaoyutai, Beijing, Rais wa Jakaya Kikwete alisema Kura ya Maoni inatarajiwa  kupigwa wakati wowote Aprili mwaka ujao kama mambo yataenda vizuri.

Rais Kikwete alikabidhiwa Katiba hiyo hivi karibuni mjini Dodoma baada ya Bunge Maalum la Katiba kumalizia kaze yake.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAWEKEZAJI NCHINI POLAND

$
0
0
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni ya Katanja-Neoval Oil, Bw. NICODEMO SWIACKI (kushoto) akiwasilisha mada kuhusu kampuni yao ambayo inataka kuwekeza Tanzania kwenye kiwanda cha kusafisha dhahabu na ujenzi wa hoteli ya kimataifa huko Zanzibar. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Mwigulu Nchemba.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akibadilusha mawazo na viongozi wa kampuni ya Katanja-Neoval Oil baada ya kusikiliza mada yao. Wa pili kulia ni Rais wa Kampuni hiyo, Bw. KRZYSZTOF SWIACKI. (Picha na Irene Bwire wa OWM).

KAYMU AIMS TO ACCELERATE SHIFT TO DIGITAL SALES IN TANZANIA

$
0
0
Kaymu.co.tz is Tanzania's #1 online marketplace. The platform allows buyers and sellers to make the best deals on a wide range of products including electronics, fashion and home appliances, and is the world’s fastest growing online marketplace, with a presence in more than 30 countries in Asia, Africa and Eastern Europe. Kaymu was launched in Tanzania in October 2013 and is backed by Millicom and Rocket Internet, the world’s biggest internet company outside the United States and China.

“We very excited to offer our online marketplace solution to the people of Tanzania. We strongly believe now is a great time to start an online business in Tanzania, and day by day we see rapidly increasing numbers of internet users”, says Erfaan Mojgani, Country Manager of Kaymu Tanzania. “Shop-owners and consumers alike can benefit from the platform, and together we can help move the economy forward.”

According to Mckinsey's Global institute analysis in 2012, there are 5.6 million internet users in Tanzania, Tanzania’s iGDP is $403 million, which is 1.3 percent of total GDP. This is in line with the African average of 1.1 percent but below the aspiring countries’ average of 1.9 percent.

THE LEGEND DJ JD

$
0
0
Ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwako kwa upendo na support yako, kama ulifanikiwa kufika siku ya jumamosi na ijumaa ilikuwa bomba sana, and could have never been possible without you, one way or the other. Thank you very much, naomba Mungu aendelee kukupa nguvu na upendo. Naomba nikukumbushe kuwa jumamosi hii tarehe 1/11 ndio siku ya sheree za kutimiza miaka 2 (2nd anniversary) tangu kurejea kwa Legend, this is where I need your support the most, mjulishe kwa ujumbe huu yeyote ambae unahisi kwa namna moja au nyingine ana love na DJ John Dillinga. Have a lovely sunday, One love to you and God bless you. Dj JD

RAIS KIKWETE AWASILI VIETNAM KWA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI

$
0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa Mjini Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Ndugu Nguyen Phu Trong, katika Makao Makuu ya Kamati Kuu ya Chama hicho tawala cha nchi hiyo Jumatatu Oktoba 27, 2014.PICHA NA IKULU.

Airtel yaipeleka Airtel Trace Music Stars Mikoani

$
0
0
 
 Msanii  chipukizi wa kijiwe cha Matofali jijini Morogoro ajulikanaye kwa jina la Jibwa Kali akionyesha umahiri wake wa kuimba wakati Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani humo
 Msanii  chipukizi ajulikanaye kwa jina la Hamisi Ramadhani aka Brashi Waya 2akionyesha umahiri wake wa kuimba wakati Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani humo. Pichani ni mashabiki na vijana wa kijiwe cha Matofali mkoani Morogoro.
Meneja Uhusiano wa Airte Bwana Jackson Mmbando akiongea na wasanii chipukizi wa Kijiwe cha Matofali mkoani Morogoro wakati Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani humo.

·         Wasanii chipukizi kutoka morogoro watembelewa katika vijiwe vyao na kujiunga na mashindano ya Airtel Trace.

Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel imeendelea kuwafikishia wateja wake na wapenzi wa muziki katika mikoa mbalimbali na kuwaunganisha katika mashindano ya kutafuta mwamamuziki chipukizi ya Airtel Trace yaliyozinduliwa rasmi nchini mwanoni mwa mwezi octoba. Airtel imetembelea Mkoa wa Morogoro na kuzindua rasmi huduma ya Airtel Trace music star katika vijiwe mbalimbali mkoani hapo.

Akizungumza na wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya katika vijiwe mbalimbali mjini Morogoro, Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema huduma hiyo inamuwezesha mtu yeyote mwenye kipaji cha kuimba  kujiunga na kushiriki kwa kupitia simu ya mkononi kwa kupiga namba 0901002233 kisha kurekodi wimbo wake na kuutuma.

Mashindano haya yanatoa mwanya wa watanzania wenye ndoto za kuwa wanamuziki nyota kupata fulsa ya kuzifikia ndoto zao. Sambamba na hilo tutakuwa na washindi watakaojishindia zawadi mbalimbali hapa nchini kama vile pesa taslimu na nafasi ya kushinda na kushiriki mashindano ya Afrika yatakayofanyika nchini south Afrika na kushirikisha washindi wengine toka nchi 13 barani afrika ambabo Mshindi wa Afrika atapata nafasi ya nafasi kwenda kurekodi wimbo wake nchini Marekeni na kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa msanii nguli wa muziki Akon huko nchini Marekani
Nao baadhi ya wasanii waliokutwa kwenye vijiwe vyao waliweza kushiriki shindano hilo kwa kurekodi nyimbo zao kupitia Airtel Trace muziki star huku wakiishukuru Airtel kwa kuwaletea huduma ambayo itawakomboa wasanii chipukizi wasio na uwezo.

Ambapo Hamis Ramadhan  aka brash waya 2 alikuwa na haya ya kusema” tunashukuru Airtel kwa kutuletea mshindano haya kitaani kwani tunavipaji lakini tunashindwa kupiga hatua kwakuwa uchumi ni mdogo tunaamini kwa kuppitia Airtel Trace tutatoka , kukubwa ni kusaidia na kupigiana kura ili tufanikiwe, tunaamini Airtel Trace Tanzania Atatokea Morogoro na hivyo natoa wito kwa wanamorogoro wajiunge kwa wingi na kutumia nafasi hii ili kubuka kuwa masuper star.

Kwa upande wake Ramadhani Nguyao alisema “ nimefurahia mpango mkubwa na wakwanza Tanzania utakaowawezesha wasanii chipukizi kupata fulsa ya kuimba na kurecord wasanii wakubwa kama Akon. Mimi nimevutia na ntajiunga na mashindano haya na waomba watanzania wengi  na wasanii wenzangu wa Morogoro na nje ya Morogoro kujiunga na kushiriki katika mashindano haya ya Airtel Trace Music Stars.

Mashindano ya Airtel Trace Music Stars yalizinduliwa rasmi nchini Mwanzoni na October na yatadumu kwa muda wa mienzi sita ambapo fainali ya mashindano haya inategemea kufanya Mwaka kesho Machi 2015 nchini South Afrika.

  
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images