Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

WATOTO WALEMAVU MAHENGE WANUFAIKA NA MSAADA WA BAISKELI

$
0
0
 Mtoto Mwidini Ligubuga kutoka kijiji cha Mbuga akifurahia kiti chake kutoka kwa Kibaran Resources . Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo nchini Bw.  Grant Pierce, na kulia ni Mkurugenzi Mkuu  Bw. Andrew Spinks 


 Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mahenge Bw. Furaha Lilongeri akimbeba Mtoto Magdalena Nwira kutoka kijiji cha Kichanganyi kupokea kiti chake. Mkurugenzi wa Kibaran Resources Grant Pierce anasaidia kukitayarisha hicho kiti.
Watoto Mahenge wakipokea viti kutoka kwa kampuni ya Kibaran Resources 
Kampuni ya Kibaran Resources inayojihusisha na utafiti wa uchimbaji wa madini ya Uno kwenye Kijiji cha Epanko, imetoa msaada wa baiskeli 30 za walemavu kwa watoto wenye ulemavu katika kata ya Mahenge wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro. Baiskeli hizo zimeundwa maalumu kwa watoto wanaoishi vijijini. 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi baiskeli hizo, Bw. Grant Pierce, ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Kibaran Resources Tanzania amesema kuwa msaada huo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya kijamii ambayo kampuni imeazimia kuifanya kulingana na msimamo wa kampuni hiyo wa kuwa karibu na jamiii inayowazunguka. 
“Msaada huu ni sehemu ya azimio tuliloweka la kuwekeza katika jamii zinazotuzunguka. Watu wanaoishi na ulemavu husahaulika katika jamii na hawapati haki zote zinazostahili kwa binadamu. Haki za binadamu ni sawa kwa watu wote bila kujali ulemavu wao. Kukosa uwezo wa kujihudumia mwenyewe, huleta mateso kwa binadamu hasa watoto. Tunafurahi kuwasaidia watoto katika jamii hii kwa kuwapa uwezo wa kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine kwa urahisi na tunaamini itasaidia kuboresha maisha yao ya kila siku.”, Alisema Grant Pierce. 
Naye kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri Furaha Lilongeri akimwakilisha Mkuu wa Wilaya  Mh. Francis Miti  kama mgeni rasmi wakati wa shughuli hiyo ya kukabidhi baiskeli za walemavu kwa watoto alisema kuwa amefurahishwa na moyo wa kampuni  hiyo kwa kujali jamii inayoizunguka haswa kundi hilo la walemavu katika wilaya. 
“Nimefurahishwa sana na kitendo cha Kibaran Resources kujitolea katika kuwasaidia watoto hawa. Kwa niaba ya Wilaya, napenda kuushukuru uongozi pamoja na wafanyakazi wote wa Kibaran Resources kwa moyo wenu wa kujali watu walio katika mazingira magumu, ikiwemo watoto wenye ulemavu. Msaada huu utawawezesha watoto hawa kushirki shughuli mbalimbali katika jamii pamoja na kufikia malengo yao, kama vile kwenda shule kama watoto wengine ili kujipatia elimu ambayo ni msingi wa maisha yao.”, alisema bwana, Furaha Lilongeri.

Wakizungumza kwa niaba ya watoto wao, walezi wa watoto waliopewa baiskeli hizo wametoa shukurani kwa uongozi wa kampuni ya Kibaran Resources kwa kuwasaidia watoto wao kutimiza ndoto zao za kushiriki katika fursa zilizopo kwenye jamii sawa na watoto wengine wasio na ulemavu. 
“Naishukuru sana kampuni ya Kibaran. Msaada huu tumeupokea kwa furaha kubwa kwani watoto wetu sasa watapata uhuru ambao hawakuwa nao awali. Kwa sisi walezi, hii ni ahueni kubwa sana. Ni vigumu mara nyingine kwa watu kuelewa changamoto ya kulea mtoto mwenye ulemavu. Baiskeli kama hizi zinaondoa mzigo mkubwa sana kwetu”. Alisema Anton Nkawamba, mmoja wa walezi waliohudhuria shughuli hiyo. 
Baadhi ya viti viliachwa katika hospitali ya mkoa ili kusaidia watoto wagonjwa wenye ulemavu wakati wanahudhuria hospitali hiyo kwa huduma za matibabu. Viti hivyo hutengenezwa na Shirika la nchini Australia liitwalo Wheelchairs for Kids, shirika ambalo wafanyakazi wake ni wastaafu wanaojitolea.  
Kibaran Resources ni kampuni iliyosajiliwa kwenye soko la hisa la Australia inayojihusisha na biashara ya uchimbaji wa madini aina ya UNO (Graphite) na Nickel nchini Tanzania. Kwa sasa shughuli za Kibaran zimejikita katika eneo la Epanko jirani na Mahenge, Wilayani Ulanga katika mkoa wa Morogoro. Kampuni hiyo imekuwa ikifanya utafiti wake kwa takribani miaka mitatu katika eneo la Mahenge na pia ina mradi katika eneo la Merelani, Kaskazini Mashariki mwa Tanzania. 
Mnamo tarehe 20/08/2014 kampuni ya Kibaran Resources ilitoa msaada wa madawati 148 katika shule ya Epanko iliyokuwa inakabiliwa na upungufu wa madawati na hivyo kutoa fursa kwa wanafunzi 292 kufanya kazi zao za darasani wakiwa wamekaa. Kibaran Resources iko katika utafiti wa kujenga mgodi katika eneo la Epanko. Mgodi huo utatengeneza nafasi za ajira kwa wakazi wa eneo hilo na hivyo kupunguza tatizo la ajira katika mkoa huo.


Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi duniani yafanyika leo jijini Dar es salaam.

$
0
0
 Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akiteta jambo na moja ya mtoto mwenye tatizo la kichwa kikubwa anayepata huduma Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI).

 Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma(Kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub(mwenye T-shirt nyeupe) na Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani leo Jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akimlisha keki Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani leo Jijini Dar es salaam.
 Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akimlisha keki mmoja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa  katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani leo Jijini Dar es salaam

 Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub.

tangazo la msiba: Dkt Kansolele Ntevi afariki dunia

$
0
0
IMG-20141025-WA0035
Familia ya Ntevi inasikitika kutangaza kifo cha Mpendwa wao  Dkt Kansolele Ntevi kilichotokea ghafla tarehe 22/10/2014 jijini Dar es salaam.  Habari ziwafikie ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote popote pale walipo.
 Mazishi yanatarajiwa kufanyika jumatatu Tarehe 27/10 / 2014 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam. 

Kutakuwa na ibada ya kuuaga mwili wa mpendwa wetu marehemu Dr. Kansolele Ntevi nyumbani kwake maeneo ya Kunduchi baada ya chuo cha jeshi njiapanda ya Madini, barabara ya vumbi, nyumba ya tatu. 

 Kwa mawasiliano na familia piga namba 0767004908 au 0717017820
Pole saana Dada Dorothy wa Dorcas Catering
Sisi tulimpenda, Ila Mungu kampenda zaidi.
Jina la Bwana na Lihimidiwe - AMINA

MBWEMBWE ZA TIMU YA STAND UNITED

$
0
0
Stand United wakiingia uwanjani na katapila tayari kucheza na Yanga, mwenye shati la kitenge hapo mlagoni ni Mbunge wa Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini amekuwa bega kwa bega na timu ya Stand United.

Ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Anastazia Mukabwa Ft Rose Muhando - Kiatu

Article 9

MAKAMU WA RAIS AHUTUBIA WASANII KWENYE MADHIMISHO YA SIKU YA MSANII MLIMANI CITY JANA USIKU OCTOBA 25-2014

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tunzo Edward Said Tingatinga msanii aliyejitolea maisha yake kwa Jamii, kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tunzo Josephat Kanuti msanii aliyejitolea maisha yake katika tasnia ya sanaa Nchini,   kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

 Wasanii na wananchi mbalimbali waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo wakifuatilia kwa karibu matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika kwenye ukumbi huo. (Picha na OMR).
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

HEPI BESDEI YA KUZALIWA ANKAL SAMIYA

$
0
0
Ing. Ally Mlunga na Mai waifu wake Swabra Ngomoi, wanayofuraha kusherehekea pamoja na binti yao siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza miaka miwili. Kwa pamoja wanamtakia maisha mema yenye mafanikio.
Besdei gel Samiya akisaidiwa na kaka yake (Salum) kugawanya Keki ya besdei yake ili yeye na waalikwa wengine wapate kuila. Mambo ya kata keeeki tuleeeeeee... kata keeki tuleeeeee...!!!
Besdei gel Samiya akipewa kampani na kaka yake Salum katika siku yake hii ya furaha.

BIASHARA HARAMU YA MKAA INAPOFADHILI UGAIDI

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, New York

Inaweza ikawa ni taarifa za kushangaza kuwa hata mkaa ambao ni nishati inayotumiwa na jamii kubwa sehemu mbalimbali hususani Barani Afrika kwamba mapato yatokanayo na biashara hiyo yanaweza kuwa chanzo ya mapato kwa makundi ya kigaidi.

Taarifa kwamba mapato yatokanayo na mkaa yanatumika ndivyo sivyo, zimejidhihirisha mwishoni mwa wiki ( Ijumaa ) pale Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipopitisha kwa kura Azimio namba 2182 la mwaka 2014 ambalo pamoja na mambo mengine linaweka vikwazo na kupiga marufuku biashara haramu ya mkaa huko Somalia.

Upigaji marufuku hiyo na vikwazo dhidi ya biashara ya mkaa inatokana na kile kilichoelezwa wakati wa mkutano wa Baraza , kwamba kundi la kigaidi la Al- Shabaab limekuwa linanufaika na biashara hiyo kwa kuchukua sehemu ya mapato . Azimio hilo lilipita kwa kura 13 za kuliunga mkono huku wajumbe wawili Jordan na Urusi wakipiga kura ya kutoegemea upande wowote. Baraza linawajumbe 15 ambapo watano kati yao wanakura ya veto.

Vikwazo dhidi ya Biashara haramu ya mkaa kutoka Somalia iliwekwa kwa mara ya kwanza mwaka 2012 kwa azimio 2036. Na kwamba tangu kuwekwa kwa vikwazo hivyo kumekuwapo na ongezeko la biashara hiyo ya mkaa kiasi cha kuifanya Serikali ya Mpito nchin humo kulalamika kwa Baraza la Kuu la Usalama.

Baadhi ya wajumbe waliozungumza baada ya kupitishwa kwa Azimio hilo ambalo pia linaongeza muda wa vikwazo vya silaha, wameeleza kuwa kundi la Al-Shabaab linapata theruthi moja ya mapato yanayotokana na biashara hiyo ambayo inaeelezwa kuwa thamani yake ni dola za kimarekani 250 milioni.

Kupitia Azimio hilo Baraza linatoa wito kwa wadau mbalimbali zikiwamo nchi zinazochangia walinzi wa Amani nchini Somalia, kupitia AMISOM kutoa ushirikiano katika kudhibiti biashara hiyo .

Aidha Azimio linatilia mkazo wa ukaguzi wa meli zinazopita katika mwambao wa pwani ya Somalia na zile zinazopita katika kina kirefu. Na hasa pale inapohisiwa kwamba huenda zikawa zimebeba bidhaa hiyo au silaha na zana nyingine za kivita ambazo zinadhibitiwa kupita Azimio hilo. Na kwamba bidhaa hizo zikikamatwa basi viharibiwe mara moja.

Pamoja na Azimio kutilia mkazo vikwazo dhidi ya biashara hiyo ya mkaa, biashara ya haramu ya silaha na au uingizaji wake. Pia limeongeza muda wa mamlaka kwa Walinzi wa Amani wanaohudumu chini ya Umoja wa Afrika ( AMISOM) hadi mwaka 2015.

WAZIRI CHIKAWE ATANGAZA KUTETEA JIMBO LAKE

$
0
0

PIX 1

Na Felix Mwagara, Nachingwea.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe ametangaza rasmi kuwa atagombea tena katika nafasi ya ubunge kupitia CCM katika uchaguzi Mkuu ujao na kulitetea jimbo lake. Alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa CCM wa Wilaya na Kata ya Mtua, wilayani Nachingwea katika sherehe ya kuwapokea viongozi na wanachama wapya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliojiunga na CCM wilayani humo. 

Waziri Chikawe alisema wananchi wake bado wanamuhitaji kwa hiyo hawezi kuacha kugombea nafasi hiyo kwani wazee na wananchi mbalimbali katika Kata zote alizokuwa akipita kufanya mazungumzo nao wanamuomba agombee tena nafasi hiyo. 

“Wakati nikiingia ubunge mwaka 2005 katika jimbo hili kulikuwa hakuna lami na barabara nyingi za kwenda vijijini zilikuwa hazipitiki na pia maji yalikuwa shida lakini sasa barabara za lami mjini Nachingwea zimejengwa, maji yanapatikana tena yasio na chumvi, barabara vijijini zinapitika kwa kuwa zimechongwa vizuri kwa kuwawezesha wakulima kupitisha mazao yao,” alisema Chikawe huku akishangiliwa na mamia ya wananchi waliofurika katika sherehe hiyo. Picha/Story na Felix Mwagara.

Serikali yapiga marufuku ukataji wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake

$
0
0

unnamed3Naibu waziri wa Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri akiwa na wataalamu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wakikagua msitu wa Siha mkoani Kilimanjaoro alipotembelea juzi . Waziri Nyalandu aliruhusu nguzo nza umeme kupita katika msitu huo ili kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo kupata umeme.
unnamedWaziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akimsalimia mmoja wa wagonjwa waliofuata huduma katika zahanati ya Ngarenanyuki wilayani Arumeru ,juzi  alipoitembelea baada ya Mbunge wa jimbo hilo kumlalamikia kuhusu tozo ya ushuru wa magari na wagionjwa wanaopita katik Hifadhi ya Taifa ta Arusha ili kupata huduma katika hospitali hiyo. Waziri Nyalandu aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba katika zahanati hiyo kupita bure hifadhini. unnamed1Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akimtaarifu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu juu ya adha wanayopata wananchi wa jimbo klake wakati wakiiingia katika Zahanati ya tiba za Asili cha Ngarenanyuki mkoani Arusha juzi , kutokana  na tozo la pesa kupitia hifadhi ya Taifa ya Arusha. Waziri Nyalandu aliamuru wananchi wanaohitaji kupata tiba katika zahanati hiyo kupita bure hifadhini. unnamed2Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiwa na Mbunge wa Siha ambaye ni Naibu waziri wa Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri wakikagua kitalu cha miti katika shamba la mitiulioko wilayani humo juzi. Waziri Nyalandu aliruhusu nguzo nza umeme kupita katika msitu huo ili kuwezesha wananchi wa wilaya hiyo kupata umeme n akuondoa mgogoro uliozuia mradi huo kwa muda mrefu.
……………………………………………………………..
Serikali imepiga marufuku ukataji wa miti nchini hata kama ikiwa mtu amepanda nyumbani kwake anatakiwa kuomba kibali kwajili ya kukata mti huo.

Akizungumza wilayani Siha juzi ,Waziri wa Maliasili na Utalii , Lazaro Nyalandu amesema kwamba Tanzania inawez a kuwa jangwa baada ya miaka 15 kutokana na uvunaji mbaya wa bidhaa za miti unaofanyika nchini .
“Tukiendelea kukata miti kma hivi tutakuwa tunatengeneza janga la kitaifa kwa hiyo kwa sasa naomba niseme rasmi kuwa hakuna mtu anaruhusiwa kukata miti au mti hata kama ameupanda nyumbani kwake, ni lazima aombe kibali kwa maafisa wa misitu. Tunatakiwa kushiriki kwa pamoja katika kutunza mazingira yetu” alisema.

Nyalandu alisema kasi ya ukataji miti nchini imekuwa kuubwa kwa sasa kutokana na kuongezeka kw aidadi ya watu na kuwa kwa mwaka mmoja pekee hekta 350,000 hukatwa huku kikiwa hakuna jitihada za kurejesha iliyoondolewa.

“Kwa kaddri siku zinavyozidi kwenda na watu kuongezeka baada ya miaka kumi misitu itakuwa inavunwa kw azaidi ya hekta 850,000 nchini kwa mwaka, hii ni hatari kubwa, lazima tufanye jitihada zaidi kukomesha tatizo hili”.

Aliwaagiza wakuu wa wilaya za Arusha na kilimanjaro kuunda timu ili kuandaa  hadidu za rejea kwa ajili ya kupatia kikosi kazi ambacho kitaandaas andiko kw ajili ya kuanzisha mfuko huo.

Mtendaji Mkuu wa wakala wa misditu (TFS) Juma Mgoo alisema kwamba misitu ilianza kutunzwa mtokea enzi za wakoloni lakini tatizio kubwa linalotokea kw asasa ni watu wengi kuivamia kutokana na mahitaji ya nishati na uchomaji wa misitu.

Alisema kwamba kwa msitu wa asili kawaida huwa na mita 30 za ujazo wakati kwa upande wa misitu ya kuoandwea huwa wna ujazo wa zaidi ya mira za ujazo 400 hadi 600 kitu ambacho alishauri  umuhimu w akupanda miti zaidi ili iweze kukabiliana na ongezeko la mahitaji na kuokoa misitu iliyopo.

Waziri Nyalandu alitoa maagizo ya kuruhusu nguzio za umeme kupita katika msitu wa wilayani Siha ili kufanywa wananchi waweze kupata nishati ya umeme ili kuokoa matumizi ya kuni kama nishati na kulinda misitu.

“Umemem ni nishati mbadala badala ya kuni na mkaa kwa hiyo napenda kuwaeleza kwamba ni bora miti michache ikatwe ili pupisha nguzi za umeme ili wananchi wakipata nishati hiyo waache kutumia kuni na kuharibu misitu na kutumia umeme kama nishati mbadala” alisema.

WAZIRI MKUU PINDA ATEMBELEA KIWANDA CHA TREKTA POLAND

$
0
0


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda atatuma wataalamu wa sekta ya kilimo ili waje kufuatilia suala la mahitaji ya trekta ili kuziba pengo la mahitaji yake nchini Tanzania.



Alisema lengo la Serikali la kuanzisha sera ya Kilimo Kwanza lilikuwa ni kuwasaidia wakulima kupata ruzuku ya pembejeo, mbegu bora, na dawa za mifugo ili waweze kuongeza ushalishaji.



“Kutokana na mkopo wa Serikali ya India, tulipata matrekta 1,846 ambayo hayakuchukua muda kuisha. Sasa hivi tunatafuta wabia wengine wa kutupatia zana za kisasa za kilimo kwa sababu matunda yake mazuri tumeyaona, tunataka kilimo cha Mtanzania,” alisema.



Jana asubuhi(Ijumaa, Oktoba 24, 2014), Waziri Mkuu alitembelea kampuni ya Farmers inayotengeneza vipuri pamoja na matrekta ya kulimia na kuvuna yenye ukubwa wa Horse Power 80 na 72 ambayo alielezwa kwamba yanavumilia hali ya udongo mgumu wa Afrika.



Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Farmer, Bw. ZDZISLAW ZUKIEWICZ alisema vifaa vinavyotengenezwa na kampuni hiyo vina waranti ya miaka saba na vinaweza kuhimili udongo wa miamba na mawe wa ardhi ya Tanzania.



Kampuni hiyo inatengeneza matrekta, mashine za kuvuna mazao shambani (combined harvester), mashine za kukata nyasi za malisho ya mifugo pamoja na vipuri vyake. Alisema bei ya trekta ni wastani wa Euro 22,000 na wako tayari kuleta vifaa hivyo Tanzania kama watapewa oda.



Waziri Mkuu amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini Poland jana mchana ambapo asubuhi alikutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kufanya vikao na baadhi ya wafanyabiashara wa jiji la Warsaw.






IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAPILI, OKTOBA 26, 2014

SERIKALI KUOMBA MKOPO POLAND - WAZIRI MKUU

$
0
0
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali inaangalia uwezekano wa kupata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland utakaoliongezea Taifa uwezo wa kuhifadhi chakula tofauti na hali ilivyo sasa.

Alisema uzalishaji mwaka huu umetoa ziada ya tani milioni 1.5 za nafaka na tani 800,000 za mpunga ikilinganishwa na ziada ya tani 300,000 iliyokuwepo mwaka jana. “Serikali inakabiliwa na changamoto ya kupata soko la uhakika kwa mazao ya wakulima kwa sababu tulizoea kumtumia Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kama mnununzi mkuu na uwezo wezo wake ni tani 240,000 tu kwa mwaka,” alisema.

Akizungumza baada ya kutembelea kampuni ya MLYNPOL ambayo inanunua mazao kwa wakulima na kusindika nafaka jana mchana (Ijumaa, Oktoba 24, 2014) Waziri Mkuu alisema teknolojia ya ujenzi wa maghala makubwa ya kuhifadhia chakula katika muda mfupi ndiyo suluhisho pekee kwa wakulima wa Tanzania katika kipindi tulichonacho.

“Wenzetu wana teknolojia ya kisasa ya ujenzi wa SILOS (maghala makubwa ya kuhifadhia chakula) pamoja na namna bora ya kuhifadhi chakula, na sisi tuna changamoto ya kuwasadia wakulima kuuza mazao kutokana na uzalishaji mkubwa wa nafaka ambao umetokea mwaka huu,” alisema.

Alisema ni mapema mno kujua kiasi cha fedha ambacho Serikali inatarajia kukopa lakini alithibitisha kwamba atatuma timu ya wataalamu kutoka sekta husika ili wafanye mazungumzo rasmi na Serikali ya Poland na kukamilisha taratibu za upatikanaji wa mkopo huo.

Waziri Mkuu ambaye alisafiri km. 500 kwenda mji wa CHOJNOW kilipo kiwanda cha kutengeneza maghala (SILOS) na kusindika nafaka aliguswa na teknolojia inayotumika kwenye kiwanda hicho cha MLYNPOL ambapo kwa siku moja kina uwezo wa kusindika tani 360,000.

Mji wa CHOJNOW upo kusini Mashariki mwa Poland na pia hauko mbali na mipaka ya nchi za Ujerumani, Czeck na Austria. Kwa gari dogo ni kati ya saa 3 hadi 4 hadi kufika miji mkuu ya nchi hizo ambayo ni Berlin, Prague na Vienna.


Akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, mmiliki wa kiwanda hicho kikubwa nchini Poland, Bw. WITOLD KARCZEWSKI alisema kiwanda hicho kinaposindika ngano kina uwezo wa kutoa unga laini wa mikate (refined flour), unga wa lishe (grain/brown flour), unga wa kutengeneza pasta na tambi na wa mwisho hutolewa kwa ajili ya chakula cha mifugo.

“Nafaka zikifika, zinasafishwa, zinakaushwa, zinapimwa unyevunyevu uliopo na kuanza kusindikwa kulingana na aina ya nafaka inayoletwa. Tunakusanya mazao haya kutoka kwa wakulima kwenye majimbo 16 ya nchi hii,” alisema.

Akifafanua kuhusu matumiai ya umeme kwenye kiwanda hicho, Bw. ALEKSANDR ZINGMAN ambaye pia ni mshauri na mbia wa Bw. KARCZEWSKI, alisema kiwanda hicho kinatumia megawati moja ya umeme kwa saa moja lakini matumizi yanaweza kupungua kuligana na ukubwa ama udogo wa kiwanda.

“Kama Serikali inahitaji kiwanda kidogo zaidi ya hapa, tunaweza kuwajengea na matumizi ya umeme lazima yatapungua,” alisema.

Kampuni ya MLYNPOL ina wafanyakazi 250 ambao kato yao, 200 wanafanya kazi kiwandani kwa shifti tatu za saa nane nane kila moja.

Waziri Mkuu anamalizia ziara yake ya siku tatu nchini Poland jana mchana ambapo asubuhi alikutana na Watanzania waishio Poland na baadaye kufanya vikao na baadhi ya wafanyabiashara wa jiji la Warsaw.

TAA yataka wanafunzi wachangamkie masomo ya anga

$
0
0
Mgeni rasmi, Mwanasheria Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Wakili Msomi, Ramadhan Maleta (katikati mwenye tai) akiangalia kazi za wanafunziza darasani walizozionesha kwake na kwa wazazi wakati wa mahafali ya kidato cha nne ya shule ya sekondari ya Lilian Kibo, Goba Matosa, Dar es Salaam juzi.
Wakili Maleta akiangalia chura anavyopasuliwa wakati wa somo la bailojia wakati akioneshwa na mwanafunzi wa shule ya Lilian Kibo.
Wanafunzi wa shule ya Lilian Kibo wakitumbuiza kwa nyimbo wakati wa mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo juzi.

MKUTANO WA CCM KIBANDAMAITI MJINI UNGUJA LEO

$
0
0
Umati mkubwa wa wananchi waliofurika katika uwanja wa Demokrasia kibandamaiti mjini unguja wakiwa katika mkutano wa hadhara wa CCM uliohutubiwa na Makamo Mwenyekitiwa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali mohamed Shein[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]


China to Boost Bagamoyo Special Economic Zone

$
0
0
A permanent Secretary in the Ministry of Finance Dr.Servicius Likwelile, a representative from the Sultanate of Oman together with an official from China Merchants Holdings International sign a memorandum of Understanding(MoU) between the Government of Tanzania, China Merchants Holdings international and State General Reserve Fund of Oman on a Strategic Partnership for the Development of Bagamoyo Special Economic Zone(SEZ).The Signing ceremony took place at the Shenzen Hilton Hotel in China in the Presence of President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete (photo by Freddy Maro).

MROKI AJIPIGA RISASI NA KUFA ARUSHA

$
0
0

MFANYABIASHARA wa Arusha anayemiliki kampuni ya Tanzania Bush Camp yenye kambi za watalii katika hifadhi za Serengeti mkoani Mara na Manyara iliyopo katika mikoa ya Arusha na Manyara, Timoth Mroki (36) amejiua kwa kujipiga risasi tatu kifuani akiwa katika baa maarufu ya Arusha Raha iliyopo la Shams, jijini hapa.

Kisa cha kujiua kwake kimetajwa ni kusababisha ajali, baada ya kuligonga gari jingine katika eneo la Mbauda wakati akitokea katika makazi yake yaliyopo eneo la Kwa Mrombo, jijini hapa.

Alifikwa na mauti katika tukio lililotokea kati ya saa 1:30 na saa 2:00 usiku, ndani ya baa maarufu ya Arusha Raha.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Mroki alifika katika baa hiyo baada ya kufanikiwa kuwatishia kwa risasi waendesha bodaboda waliokuwa wamemzingira katika eneo la ajali na kisha kuondoka kwa kasi kwa gari lake aina ya Nissan Navara. 

“Alipiga risasi mbili hewani waliokuwa wamemzunguza wakanywea, akatumia mwanya huo kukimbia na moja kwa moja akafika Arusha Raha pengine kwa lengo la kujificha, na hapo akaanza kunywa…

“Ingawa inaonekana alikotoka alikunywa kidogo, alipofika Arusha Raha alikunywa haraka pombe mbili kali aina ya Valuer na wakati anamalizia ya tatu, akajikuta anazingirwa tena na wale waendesha bodaboda,” anasema mtoa habari huyo na kuongeza kuwa, baada ya kufyatua tena risasi mbili nyingine hewani, lakini bila ya dalili ya watu hao kutishika, ndipo akaamua kujimiminia risasi.

Habari zaidi zinasema wakati anazingirwa, naye akijihami kwa risasi wasamaria wema wakiwa harakati za kupiga simu polisi walishitukia polisi wakiingia katika eneo la tukio lakini tayari Mroki alikuwa ameshajitoa uhai baada ya kujimiminia risasi kifuani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatusa Sabas hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, ingawa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi ya wilaya ya Arusha imekiri kuwepo kwa tukio, lakini chanzo chetu kikikataa kutajwa jina gazetini kwa kuwa si wasemaji wa matukio ya jeshi hilo mkoani Arusha.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TETESI ZA KUWEPO MGONJWA ANAYEHISIWA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII 

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TETESI ZA KUWEPO MGONJWA ANAYEHISIWA KUWA NA UGONJWA WA EBOLA  MKOANI KILIMANJARO

 Utangulizi

Mnamo tarehe 22 Oktoba 2014, Wizara ilipokea taarifa kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ya kuwepo kwa mgonjwa aliyehisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola. Mgonjwa huyu mwanaume ana umri wa miaka 37, na mkazi wa Dar es salaam (Kimara ) ambaye alikwenda Kilimanjaro tarehe 20 Oktoba 2014 katika kijiji cha Kirua kwa ajili ya kusalimia ndugu. Mgonjwa huyu alikuwa na dalili za homa kali ( 38.2 0c), maumivu ya Misuli, kuchoka na maumivu ya kichwa pamoja na maumivu ya koo na kupoteza hamu ya kula.
 
Mgonjwa huyu anatibiwa katika Kituo cha Afya Shirimatunda, Kilimanjaro kuanzia tarehe 22.10.2014 ambako yupo hapo hadi sasa. Mgonjwa huyu kikazi ni “Land Surveyor” na hufanya kazi zake nchini na nje ya nchi ikiwemo nchi ya Senegali. Mnamo siku za karibuni alikwenda nchini Senegali kwa kazi za mkataba na kurejea nchini mwanzoni wa Oktoba 2014. Hata hivyo, mgonjwa huyu hakuwa na historia ya kusafiri kwenda nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola yaani Liberia, Guinea au Sierra Leone.
   

Mwandosya amwakilisha Rais Kusimikwa kwa askofu Kigoma

$
0
0
 Askofu wa Kanisa Katoliki  Jimbo la Kigoma, Joseph Mlola akipongezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Asie na Wizara Maalum), Prof Mark Mwandosya alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye ibada ya kusimikwa kwa askofu huyo iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Kigoma, jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Asie na Wizara Maalum), Prof Mark Mwandosya akiwasalimia waumini wa Kanisa Katoliki alipomwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye ibada ya sisimikwa kwa Askofu wa Kanisa Katoliki  Jimbo la Kigoma, Joseph Mlola iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Kigoma, jana. 

CHANZO CHA MAJI IKORONGO MKOMBOZI WA MJI WA MPANDA

$
0
0
 Wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakiangalia chanzo cha chemichemi ya maji cha Ikorongo kilichoko kilometa 13.2 kutoka Mpanda mjini. Chanzo hicho kina uwezo wa kutoa maji ya kutosha mji wote wa Mpanda.
 Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Magdalena Mkeremi (aliyejifunika mtandio) akifafanua jambo kwa timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi Rais, Tume ya Mipango walipotembelea chanzo hicho hivi karibuni
 Mhandisi Happiness Magalula, Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Miundombinu na Huduma (mwenye sweta la blue) akitaka ufafanuzi wa miundombinu ya kuwezesha maji kuwafikia wananchi kutoka katika chanzo hicho. Bomba la inchi kumi limetandazwa kutoka kwenye chanzo hicho mpaka mjini ambako kuna tanki kubwa la maji yanayosambazwa katika mji wa Mpanda na vitongoji vyake.
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images