Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 622 | 623 | (Page 624) | 625 | 626 | .... | 3353 | newer

  0 0

  The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) today organised a one day Stakeholders meeting on “Code of Political Parties Election Broadcasts” in Dar Es Salaam 
  The Director of the Tanzania Information Services (MAELEZO) Mr Assah Mwambene makes his contribution  during the meeting
  A cross section of participants
   The Director of Broadcasting Mr Habbi N. Gunze addresses the stakeholders meeting.  Third left  is the  Chairperson of the Content Committee of the TCRA Engineer  Margreth Munyagi  franked by other Content Committee officials .(Photos by Courtesy of TCRA)

  0 0
 • 10/28/14--10:44: HAPA VIPI??


 • 0 0

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza (wa pili kushoto), Mbunge wa Ilala na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mussa Azzan Zungu (kulia), Mbunge wa Tumbe Mhe Rashid Ally Abdallah (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini China Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahman Shimbo muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam jijini Hanoi leo Oktoba 28, 2014.
  Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na wenyeji wake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam leo Oktoba 28, 2014
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na wenyeji wake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam leo Oktoba 28, 2014.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza na Balozi wa Tanzania nchini China Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahman Shimbo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam jijini Hanoi leo Oktoba 28, 2014. PICHA NA IKULU

  0 0
 • 10/28/14--11:03: Article 0


 • 0 0

  Rais wa Zamani wa Malawi,Mama Joyce Banda akiwa na Mtangazaji wa BBC,Charles Hilary wakati alipotembelea Shirika hilo la Habari nchini Uingereza jana.
  Rais wa Zamani wa Malawi,Mama Joyce Banda akiwa kwenye picha ya pamoja na Watangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC London,Nchini Uingereza.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.), leo tarehe 28 Oktoba, 2014 amefanya ziara katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu – Ilala, Dar es salaam, kwa lengo la kukagua maendeleo ya utoaji wa mafunzo kwa wananchi. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu hutoa mafunzo ya muda mrefu, muda mfupi na mafunzo nje ya chuo, ambayo yote yamelenga katika kutoa stadi na maarifa mbalimbali yanayowawezesha washiriki kupata ujuzi ili waweze kujiajiri wenyewe au kuajiriwa katika Taasisi mbalimbali kwa lengo la kuzalisha mali na hivyo kujiongezea kipato na kupunguza umaskini. Kwa upande wa mafunzo ya muda mrefu asilimia kubwa ya Wanafunzi wanaojiunga na Chuo hiki ni watu wenye ulemavu, wengi wao wakiwa na ulemavu wa akili.
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi na uongozi wa wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Ilala – Dar es salaam , wakati alipofanya ziara Chuoni hapo leo Oktoba 28, 2014.
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana(Mb.) akiongea na watumishi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu ( hawapo pichani), wakati alipofanya ziara Chuoni hapo, leo Oktoba 28, 2014. Kushoto ni Bwana Stephen Saro, Afisa Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Bibi Pulcheria Ndamugoba.
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana(Mb.) akikagua mazingira ya utoaji wa mafunzo katika madarasa ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, ikiwa ni pamoja na kuhojiana na washiriki wa mafunzo (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba 28, 2014. Kulia ni Bwana Stephen Saro, Afisa Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Bibi Pulcheria Ndamugoba.
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.) akiangalia mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakitolewa kwa washiriki wa darasa la Uashi, katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba 28, 2014.
  Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu, Bibi Pulcheria Ndamugoba akitoa ufafanuzi kuhusu eneo la chuo kwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb.) wakati alipofanya ziara katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu - Ilala, Dar es salaam, leo Oktoba 28, 2014.

  0 0

  Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akizungumza muda mfupi kabla wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hawajapigia kura ya kutaka vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha ambavyo Marekani imeiwekea Cuba viondolowe. nchi 188 zilipiga kura ya ndiyo, mbili zilipiga kura ya hapana na tatu zilipiga kura ya kutofungamana na upande wowote.

  Na Mwandishi Maalum , New York

  Kwa mwaka wa 23 sasa hapo jana ( Jumanne ) Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamepigia kura Azimio linaloitaka Marekani iondoe vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha dhidi ya Cuba.

  Katika upigaji kura huo , nchi 188 ikiwamo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilipiga kura ya ndiyo Azimio hilo ambalo liliwasilishwa mbele ya wajumbe na Waziri wa Mamb ya Nje wa Cuba, Bw. Bruno Rodriquez Parrilla Marekani na Israel zenyewe zilipiga kura ya hapana, huku Micronesia, Marshall Islands na Palau wakipiga kura ya kutoegemea upande wowote ( abstentions).

  Akizungumza kabla ya upigaji kura huo kufanyika, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Ramadhan Mwinyi aliungana na wazungumzaji wengine katika kuitaka Marekani na Cuba kumaliza tofauti zao za kidiplomasia ili waweze kushirikiana na nchi nyingine katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazomkabili mwanadamu.

  Akasema dunia imeshuhudia namna gani mataifa mengi yalivyojitoa muhanga zikiwamo Cuba na Marekani ambapo wamepeleka wataalamu wao wa afya, wanajeshi na vifaa ili kuukabili ugonjwa wa Ebola katika nchi za Liberia, Sierra Leone na Guinea ambazo zimeathirika vibaya kwa ugonjwa huu.

  Akasisitiza kuwa mlipuko huo wa Ebola umethihirisha namna gani mataifa yanavyoweza kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja na kwamba mataifa yanatakiwa kujenga mshikamano imara dhidi ya maadui wa binadamu na siyo kupingana wenyewe kwa wenyewe.

  Balozi Mwinyi akaongeza kuwa Tanzania ambayo ni nchi rafiki kwa Marekani na Cuba, kwa mara nyingine inasikitika kusimama na kuzungumzia kuhusu vikwazo hivyo ambavyo licha ya maazimio mengi kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Bado vikwazo vinaendelea.

  Vile vile Balozi Mwinyi amesema hali ya kuendelea kwa vikwazo hivyo kunasikitisha kutokana na sababu kuu mbili za msingi. Kwanza kuchelewa kulipatia ufumbuzi tatizo hilo kunadhoofisha hadhi ya Umoja wa Mataifa, chombo chenye dhamana ya kuhifadhi Amani na usalama wa kimataifa, kuhuisha haki za binadamu, uchumi na ustawi wa wote.

  Akasema inaposhindikana kutekelezwa kwa maazimio yanayopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ni kushindwa kwa wanachama wote. Sababu ya pili ambayo amesema inasikitisha ni kuona kuwa Nchi ambayo ilikuwa mwazilishi wa Umoja wa Mataifa ( Marekani) inaendelea kupuuza wito ambao umekuwa ukitolewa mara kwa mara, wito unaotolewa wanachama wa Umoja wa Mataifa wa kutaka kusitishwa mara moja na bila masharti yoyote vikwazo dhidi ya Cuba.

  “ Tatizo hili ( vikwazo) linaweza kuwa ni la kati ya nchi hizo mbili. Lakini kuendelea kwake na muda mrefu kunavuka mipaka ya nchi hizi mbili” akasema Balozi Mwinyi

  0 0

  Until the recent past, the recounts of most Tanzanians in the Diaspora had been filled with horrific and disappointing experiences regarding mismanagement of funds and investment attempts back home in Tanzania. Most Diasporas entrusted their projects and investments back home to their immediate relations, which, more often than not, led to devastating consequences. Some Diasporas even fear the thought of returning home with little to show for their stay abroad.

  The question that lingered in most of us was, is there a permanent solution to this problem? 

  The solution is found

  In 2012, Tanzania Diaspora Initiative (TDI) was formed. In many ways, this is a response to the needs and concerns of all Tanzanians in the Diaspora. Whether you need to invest, buy land, start a business, follow up on projects, and even get current updates on the information on all of the above, TDI acts as a hub to cater for all your needs.

  Born out of real passion to cater for the needs of Tanzanians in the Diaspora and provide permanent solutions to the series of diaspora related problems and concerns, Tanzania Diaspora Initiative goes further to provide a platform where information can be easily obtained, shared and help in making important decisions about investments and contributing to the wellbeing of the communities back home.

  TDI understands that diaspora is part of Tanzania that has a potential role to play in fast-tracking the country’s economy through various areas such as dividends, investments, expertise and many other areas. However, if these areas aren't fully exploited for the benefits of our economy, Tanzania loses a lot in that front. 

  What is TDI?

  TDI is a solution to the Professional needs of the Tanzanians in the diaspora. They key issue is to help bridge the gap between the professional needs of the Diaspora and their actual projects back home. This is what Diaspora need to have a peace of mind in ensuring their investments, projects or businesses are running smoothly while they are continuing with their lives abroad. In other words, TDI helps to save money and time for Diasporas while it handles all the issues locally with qualified professionals in their fields. 

  In order for any project or investment to run smoothly, there is a need of professional involvements. TDI shares the pride of having qualified professionals with a lot of experiences in their respective fields capable of catering for the needs of the Diasporas. 

  The aggregate skills within TDI and at the disposal of Tanzanians in the diaspora include project management, property management, Job opportunities. Investment opportunities, inspection of works and provision of professional reports, estate agency, land-use advise, document processing and management including title deeds, planning permission, and many other tailor-made solutions.

  How you benefit from TDI

  As TDI works locally in Tanzania, it ensures a strong link to communicate the latest information to the Diasporas from the core sources in Tanzania. These information can be on investments, some changes in rules and regulations, or any interesting information that could be of use for the people who are looking to invest and contribute back to their local communities. These kinds of information are communicated to all valid registered members with the TDI. You can have that chance by simply registering to the TDI and ensure you do not get left out from the important potential information concerning investments or opportunities back home.

  Join us and be a part of the bigger Community
  --
  The TDI Team

  0 0
 • 10/29/14--02:43: TANZIA
 • Familia ya Mzee Solomon Seth Gwassa wa Forest, Mbeya inasikitika kutangaza kifo cha babu yetu Mzee Seth Asombwile Gwassa(miaka 99) kilichotokea tarehe 27/10/2014 huko kijijini kwake Ilundo-Kiwira, Rungwe-Mbeya. Mipango ya mazishi inafanyika huko huko kijijini kwake, na mazishi yatafanyika tarehe 29/10/2014. Habari ziwafikie watoto wa marehemu popote walipo, wapwa wa marehemu popote walipo, wajukuu wa marehemu waliopo Mbeya, Dar es salaam, Vietnam na China, na vitukuu wote.

  Mwanga wa Milele umwangazie ee Bwana.
  Amen

  0 0  0 0

  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro akipokea kutoka kwa Balozi wa Palestina nchini Dkt. Nasri Abu Jaish ambaye amemtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro akiongea na Balozi wa Palestina nchini Dkt. Nasri Abu Jaish ambaye amemtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki akiongea na Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Segore Kayihura aliyemtembelea Naibu Waziri ofisini kwake jijini Dar es Salaam ili kubadilishana mawazo.

  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki akiongea na Naibu Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) nchini Mhe. Luana Reale aliyemtembelea Naibu Waziri ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo. Picha: Wizara ya Katiba na Sheria

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa la kujadili matumizi ya Nishati itokanayo na joto ardhi katika Nchi za Afrika zinazopitiwa na bonde la ufa. Kongamano hilo limeanza leo Oktoba 29, 2014 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt Bilal, kufungua kongamano hilo.
  Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya waliohudhuria kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia.


  0 0

  Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam,wakioneshwa na Meneja miradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza moja ya progamu zinazopatikana katika Kompyuta zinazowawezesha kupata taarifa ya masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao wakati alipotembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam Theresia Ng’wigulu (kulia) Meneja miradi na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Renatus Rwehikiza(kushoto ) pamoja na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (katikati)wakimsikiliza mmoja wa wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa,Matha Galus akiwaelezea jinsi anavyoweza kupata taarifa za masomo mbalimbali kwa njia ya mtandao, wakati walipotembelewa na maofisa wa Vodacom shuleni hapo kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
  Baadhi ya Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Theresia Ng’wigulu watatu toka kulia pamoja na maofisa wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu wa kwanza kushoto na Renatus Rwehikiza(kulia)wakimsikiliza Mwalimu wa somo la kompyuta wa kidato cha pili Nicolas Wilson wa shule hiyo akiwafafanulia jambo kuhusiana na elimu ya mafunzo ya kompyuta wakati walipotembelewa na maofisa hao kujua maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.
  Wanafunzi wa kidato cha pili wakiwa darasani katika shule ya sekondari ya Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam,wakiwa na nyuso za furaha walipotembelwa na Maofisa toka Vodacom Foundation kwaajili ya kujionea maendeleo ya mradi wa TEHAMA uliofadhiliwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Samsung.Zaidi ya wanafunzi elfu tano wa shule nne za sekondari jijini wanaendelea kunufaika na mradi huo.

  0 0

  Mkutano wa faragha wa Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa umeandaliwa na ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi ikishirikiana na UONGOZI Institute yenye lengo kuu ya viongozi hawa kujadiliana kuhusu mada kuu ya Mifumo ya Ufuatiliaji na Tathmin, pamoja na maswala mbali mbali za kitaifa. Mkutano huu wa siku mbili ulifanyika tarehe 27-28 Oktoba, 2014 mjini Dodoma.

  “Napenda kuishukuru sana Taasisi ya Uongozi, na Mtendaji wake Mkuu, Prof. Joseph Semboja, kwa mchango wao mkubwa katika kuandaa na kuendesha mikutano yetu hii, na juhudi nyingine za kujenga uwezo wa uongozi kwa watendaji waandamizi na wakuu ndani ya Utumishi wa Umma,” alisema Balozi Sefue kwenye ufunguzi wa mkutano huu.

  Mkutano ulikuwa na mada mbali mbali zinazohusu mifumo ya ufuatiliaji na tathmini, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa utekelezaji miradi ya kipaumbele, yaani Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now!) baada ya mwaka mmoja wa kutekeleza mfumo huo, pamoja na uzoefu kutoka Afrika Kusini kutoka kwa Dk. Sean Philips, Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kwenye Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini.

  “Ukweli ni kuwa kila mahali duniani ambapo kumewekwa mifumo madhubuti ya ufuatiliaji na tathmini, iwe Serekalini au sekta binafsi, matokeo chanya na makubwa yamekuwa wazi na ya haraka,” alisema Balozi Sefue.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifungua Mkutano wa faragha wa Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa tarehe 27 Oktoba, 2014.
  Prof. Joseph Semboja, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi (UONGOZI Institute) akiratibu mkutano.
  Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar, Dr. Abdullhamid Yahaya Mzee, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Tanzania, Balozi Ombeni Sefue na Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais – Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB), Bw. Omari Issa wakisikiliza mada.
  Baadhi ya viongozi waliohudhuria Mkutano wa faragha wa Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa mjini Dodoma leo Juma Tatu.
  Dk. Sean Phillips, Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini kwenye Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini, akitoa mada ya uzoefu wa Afrika Kusini katika ufuatiliaji na tathmini.

  0 0

  Kigali is to play host to the 8th Inter-Parliamentary Relations Seminar (Nanyuki Series), scheduled for October 31st to November, 1st 2014. The seminar is organized by EALA in conjunction with the Association of European Parliamentarians with Africa (AWEPA).

  The Seminar themed: “Insecurity and Terrorism as Threats to EAC Integration: How Can EAC Develop a Common Position”  brings together an estimated 250 participants drawn from Partner States National Assemblies, EALA, academicians, high ranking Government officials as well as other regional stakeholders.

  The seminar is to be facilitated by high profile speakers from within and beyond the East African Community region who will make presentations and spur discussions on the status of the EAC economy, status of security in the EAC region and the role of Parliamentarians and other stakeholders in ensuring regional peace and security in the EAC sub-region.

  Partner States agree that peace and security are pre-requisites to socio and economic development within the Community and vital to the achievement of the Objectives of the Community (see Article 5 (3) (f)).

  In this regard, the Partner States agree under Article 125 to foster and maintain an atmosphere that is conducive to peace and security through co-operation and consultations with a view to prevention, better management and resolution of disputes and conflicts between them. The Treaty further emphasises close co-operation in defense affairs. The EAC has also signed the Protocol on Peace and Security and the protocol is currently undergoing ratification in the Partner States.

  The seminar takes place against a background of efforts to contain the heightened insecurity in the region.  In the latest attack last year, Westgate shopping mall in Nairobi was hit by perceived terrorists who killed 70 people, injured hundreds and destroyed property worth millions of shillings. 

  The seminar aims at promoting functional relations between EALA and the National Assemblies as envisaged in Article 49 of the Treaty for the Establishment of the EAC. The issues for discussion will lead to proposals aimed at resolving the challenges that afflict the quality of life of the East African people and opportunities that are in place. It is through this forum that EALA briefs the Members of National Parliaments on the progress made in the integration process of EAC and the role of EALA in that process.

  It is anticipated that Members of the National Assemblies will be provided with an opportunity to appreciate the progress made so far in the EAC integration process and therefore the issues discussed will subsequently find their way to be agendas for National Assemblies.

  0 0


  Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii


  Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemwachia kwa dhamana Msanii  wa Muziki wa Kizazi Kipya (bongo fleva), Rashidi  Makwaro (29), maarufa kama Chid Benz, baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya mahakaman hiyo.

  Chid Benz, alifikishwa mahakamani hapo jana akikabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

  Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema alisema mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wa wawili wanaotoka kwenye taasisi zinazotambulika na wasio walimu pamoja na kusaini hati ya dhamana ya Sh. milioni moja.

  Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Inspekta Jackson Chidunda.

  Wakili Kombakono alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.

  Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.

  Wakili huyo wa serikali alidai kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.

  Mshtakiwa alikana mashitaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

  Hakimu Lema alisema kesi hiyo itatajwa Novemba 11, mwaka huu.

  0 0

  H.E. Dilma Rousseff, President of Brazil
  H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to Her Excellency Dilma Rousseff on the occasion of her re-election as President of the Federative Republic of Brazil.

  The message reads as follows.

  “Her Excellency Dilma Rousseff
    The President of the Federative Republic of Brazil,
    Brasilia,
    BRAZIL.

  I have received with great pleasure the news of your re-election to the highest office of your country. On behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, I wish to convey my sincere and warmest congratulations to You and through you to the Government and the people of the Federative Republic of Brazil for your election to the Presidency of Brazil.

  Your re-election is a sign of the trust and confidence that the people of Brazil have in your leadership qualities. As you continue discharging the noble duties bestowed upon you, I would like to assure Your Excellency of my continued co-operation in further strengthening the bilateral relations that so happily exist between our two countries.

  Please accept, Your Excellency, my personal regards and best wishes for your continued good health and success”.

  ISSUED BY: THE MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES SALAAM

  29TH OCTOBER, 2014

  0 0

  Ajali mbaya imetokea jioni ya leo katika eneo la Tengeru,Jijini Arusha ikihusisha gari dogo aina ya Toyota Hiace (pichani juu) linalofanya safari zake kati ya Usa River na Katikati ya mji wa Arusha na Lori la Mafuta. Chanzo cha Ajali hiyo inaelezwa kwamba ni hiyo daladala lilikuwa likijaribu kulipita gari jingine ndipo likakutana na loli hilo la mafuta na kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya abiria wote waliokuwa kwenye daladaa hilo ambao idadi yake haijafahamika rasmi.taarifa kamili itawajia baadae kidogo.Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya JAMII Kanda ya Kaskazini.


  0 0

  001_resized_5 (1)Juu na chini mwandishi wa makala katika safu ya Waraka kutoka Houston ndani ya gazeti la Raia Mwema, Innocent Mwesiga, Pharm.D na mke wake Carretta Mwesiga, FNP wakifurahia miaka 10 ya ndoa yao hivi karibuni katika visiwa vya Bahamas. (Kutoka blog hii tunawapa hongera sana) 002_resized_6(Picha kwa hisani ya Sunday Shomari).

  0 0
 • 10/29/14--12:53: Death Announcement
 • The late Mbaki Gwassa
  born October 1969- died October 2014

  The family of Mzee Solomon Seth Gwassa of Forest, Mbeya announces death of their beloved family member Mbaki Solomon Gwassa, that had happened on 28/10/2014 on road accident along Tunduma Road, Mbeya.

   The sudden death just happened while the family was on burial preparations for their elder Mzee Seth Asombwile Gwassa who died on 27/10/2014. 

  The family just ask for prayers from whoever has been emotionally touched by the death of this young man. The update for this sad news can be enquired through the following mobile numbers.

  Salathiel Gwassa +255 784 900 131
  Lusekelo Gwassa +8613220114394

  RIP brother Mbaki Amen.

older | 1 | .... | 622 | 623 | (Page 624) | 625 | 626 | .... | 3353 | newer