Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 618 | 619 | (Page 620) | 621 | 622 | .... | 3348 | newer

  0 0

   President Xi Jinping of China welcomes President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete to the Great Hall of the People in Beijing this evening during the official formal reception at the climax of the State visit at the invitation of the Chinese leader.

   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and the First Lady Mama Salma Kikwete pose for an official photograph with their host China’s President Xi Jinping and his wife China’s First Lady Peng Liyuan shortly after they arrived for an official formal reception at the Great Hall of the People in Beijing this evening.
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and the First Lady Mama Salma Kikwete pose for an official photograph welcomed by their  host China’s President Xi Jinping and his wife China’s First Lady Peng Liyuan

  President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete and his host Chinese President Xi Jinping inspects a guard of honor mounted China’s People Defense force in Beijing this evening during a formal reception at the Great Hall of the people. President Kikwete is on a State Visit to China at the invitation of President Xi Jinping.
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his host President Xi Jinping waves to the cheering crowd during a formal reception for the President and his delegation held at the Great Hall of the People in Beijing at the climax of his State visit today.
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete introduces former OAU/AU Secretary General Salim Ahmed Salim to China’s President Xi Jinping during the formal reception held at the Great Hall of the People in Beijing this evening.Left is the Minister for Foreign Affairs Mr Bernard Membe and second left is CCM Secretary General Abdulrahman Kinana.

  China yamwaga neema kubwa kwa Tanzania


  Jamhuri ya Watu wa China leo, Ijumaa, Oktoba 24, 2014, imetangaza neema kubwa kwa Tanzania, ikiwa ni pamoja na kutoa dola za Marekani milioni 85 kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuisaidia Tanzania kufanya mageuzi ya viwanda.

  Neema hiyo ya China kwa Tanzania imetangazwa na Rais Xi Jinping wa nchi hiyo katika mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati yake na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye yuko katika ziara rasmi ya siku sita katika China.

  Mazungumzo hayo kwenye Jumba la The Great Hall of the People yamefanyika baada ya Rais Kikwete kukaribishwa rasmi katika Jamhuri ya Watu wa China kwa kupokelewa na Rais Xi Jinping katika eneo la East Plaza ya Jumba hilo.

  Katika mapokezi hayo ya kuvutia na kusisimua, Rais Kikwete amepigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride la ukakamavu la Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa China la People’s Liberation Army.

  Katika mazungumzo hayo, Rais Xi Jinping alitangaza kuwa China itaipatia Tanzania kiasi cha dola milioni 85 ikiwa ni mchanganyiko wa msaada na mkopo usiokuwa na riba, fedha ambazo Tanzania itaamua yenyewe jinsi gani ya kuzitumia.

  “Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania kuboresha maisha ya wananchi wake, napenda kutangaza kuwa Jamhuri ya Watu wa China itatoa kiasi cha RMB milioni 200 ikiwa ni msaada na RMB 200 milioni nyingine zikiwa ni mkopo usiokuwa na riba kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kiasi cha RMB 100 milioni za msaada kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambazo zitatumika kwa kadri Serikali hizo mbili zitakavyoamua,”amesema Rais Jinping.

  Rais huyo wa China pia ametangaza kuwa nchi hiyo itaisaidia Tanzania katika uendelezaji wa maeneo ya uwekezaji ya EPZ, uendelezaji wa miundombinu, itaharakisha ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na itaingia katika shughuli za kutafuta gesi na mafuta katika ukanda wa Bahari ya Hindi katika eneo la Tanzania.

  Rais Jinping pia ametangaza kuwa Serikali ya China imefanya uamuzi wa kuikarabati Reli ya Uhuru ya TAZARA inayounganisha Tanzania na Zambia na yenye urefu wa kilomita 1,860 na kusaidia uendeshaji wa reli hiyo. “Ili kutekeleza uamuzi huu kwa haraka, napendekeza kuundwa kwa kamati ya pamoja ya wataalam kuandaa ramani ya namna ya kuitoa reli hiyo katika matatizo yake ya sasa.”

  TAZARA ndiyo reli ya kwanza duniani kujengwa na Jamhuri ya Watu wa China ambao utaalamu wake sasa unasakwa na nchi nyingine nyingi duniani.

  Rais Jinping pia ametangaza kuwa Serikali yake itatoa nafasi 100 za masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi kutoka Tanzania katika miaka mitano ijayo, itaongeza idadi ya madaktari ambao China inapeleka Tanzania, itahimiza makampuni zaidi ya China kuwekeza katika Uchumi wa Tanzania na kuzishawishi taasisi za kifedha za China kuanzisha shughuli zake katika Tanzania.

  Kiongozi huyo wa China pia ametangaza kuwa nchi yake itajenga chuo kikubwa cha mafunzo ya ufundi katika Tanzania na itaendelea kushirikiana na Tanzania katika eneo la uimarishaji wa ulinzi na usalama.


  Rais Jinping amesema kuwa urafiki na uhusiano kati ya China na Tanzania ni mfano unaong’ara wa uhusiano mzuri na mwema duniani na kuwa China iko tayari kutoa uzoefu wake wa maendeleo kwa Tanzania bila wasiwasi wowote.

  Rais Kikwete amemshukuru sana Rais Jinping na Jamhuri ya Watu wa China kwa misaada yake ambayo baadhi yake haikutarajiwa


  Imetolewa na;

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu – Dar es Salaam.

  24 Oktoba, 2014.

  0 0

  kijana mmoja mkazi wa Pasua mjini Moshi ambaye jina lake halikufahamika mara moja amenusurika kufa baada ya kupokea kipigo kitakatifu kutoka kwa wanachi wenye hasira kali,baada ya kuiba simu katika duka moja la mchele na kumpa mwenzake aliyefanikiwa kukimbia nayo. 

  Tukio hilo limetokea jioni hii katika duka la mchele la Lucki rice mart lilipo double road katikati ya mji wa Mokijana mmoja mkazi wa Pasua ambaye jina lake halijafahamika mara moja amenusurika kufa baada ya kupokea kipigo kutoka kwa wanachi baada ya kuiba simu katika duka la mchele na kumpa mwenzake aliyefanikiwa kukimbia nayo.
  Tukio hilo limetokea jioni hii katika duka la mchele la Lucki rice mart lilipo double road katikati ya mji wa Moshi.

  Kijana huyo ambaye anatajwa kufanya matukio  ya wizi katika maduka mbalimbali ya jirani na duka hilo ambapo walifika wawili nakufabikiwa kuiba simu ambayo mmoja wapo alifanikiwa kukimbia nayo kuelekea eneo la Njoroshi. 

   Kijana huyo ambaye anatajwa kufanya matukio ya wizi katika maduka mbalimbali ya jirani na duka hilo ambapo walifika wawili nakufanikiwa kuiba simu ambayo mmoja wapo alifanikiwa kukimbia nayo kuelekea eneo la Njoro.

  Baada ya kupokea kichapocho alimriwa kufuta sehemu zote zilizochafuka kwa damu iliyokuwa ikimtoka wakati wa kichapo hicho kama anavyoonekana pichani hapo juu. 
  Bahati yake nzuri,askari waliweza kufika mapema eneo la Tukio na kumuokoa kwa kumchukua na kumpeleka kituoni.

  0 0
 • 10/24/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Hafsa Kazinja - Nimuokoe nani

  0 0
 • 10/24/14--21:30: Article 19


 • 0 0

   Mkuu wa matawi wa Benki ya Exim Kanda ya Ziwa, Bw. Justus Mukurasi (wapili kushoto) akibadilishana mkataba na Mwenyekiti wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Stand United, Bw. Amani Vicent (wapili kulia) wakati wa hafla fupi iliyofanyika mkoani Shinyanga jana. Mkataba huo utaiwezesha benki kuidhamini timu hiyo katika ligi kuu ya mpira wa miguu ya Vodacom (VPL) katika msimu wa 2014/2015. Wakishuhudia wa kwanza kushoto ni Meneja Msaidizi Tawi la Shinyanga, Bw. Hatunga Nicodemus na Katibu wa kamati ya Fedha, Bw. Bakari Salum (Wa kwanza kulia).

  Benki ya Exim imesaini makubaliano ya kuifadhili timu ya mpira wa miguu ya Stand United FC ya mkoani Shinyanga. Hii ni timu ya kwanza kupata ufadhili toka Benki ya Exim. Ufadhili huo wa mwaka mmoja utaisaidia timu hiyo kushiriki katika ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu wa 2014/2015.

  “Makubaliano haya yanaikutanisha Benki ya Exim na mchezo mkubwa kuliko yote Tanzania,” alisema mkuu wa matawi ya Benki ya Exim kanda ya ziwa, Bw. Justus Mukurasi jana katika hafla fupi iliyofanyika mkoani Shinyanga. Aliongeza kuwa hakuna mchezo wenye watazamaji, wafuatiliaji na mashabiki wengi zaidi nchini kama mpira wa miguu.

  “Timu ya Stand United inanguvu kubwa ya kuunganisha mashabiki  wa kanda ya ziwa. Hivyo ni jambo stahiki kwa Benki ya Exim kuisaidia timu hii ambayo mashabiki wake ni miongoni mwa wateja wa Benki ya Exim,” alisema Bw. Mukurasi.

  Mukurasi aliongeza kuwa pande hizo mbili zilifanikiwa kuingia katika makubaliano ambayo yataiwezesha benki hiyo kuifadhili timu ya Stand United toka Ligi Kuu Tanzania bara ilipoanza.

  “Kwetu sisi udhamini tuliofanya sio tu wa nembo, nbali ni ufadhili wa muda mrefu utakaozinufaisha pande zote mbili,” alisema Mukurasi.

  ”Tunatumai kuwa kila mmoja wetu ataweza kujifunza kutoka kwa mwenzake ili kupata matokeo mazuri kwa pamoja. Exim itasaidia kukuza na kuundeleza mchezo wa soka na hivyo kuiwezesha benki yetu karibu zaidi na wateja wake,” alisema Bw. Mukurasi.

  Naye, Mwenyekiti wa Stand United FC, Bw. Aman Vicent alisema kuwa timu yake inayofuraha kubwa kuingia katika makubaliano na Benki ya Exim. “Tunadhamiria kuimarisha uhusiano huu ili kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu,” alisema Bw. Vicent.

  “Kwa niaba ya Stand United FC, ningependa kuishukuru Benki ya Exim kwa jitiada zao za kusaidia wachezaji wetu na timu kwa ujumla. Tunafanya kazi kubwa kuhakikisha tunainua vipaji vya wachezaji wetu ili na wao waweze kufika mbali zaidi,” aliongeza Bw. Vicent.
    

  0 0

   Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi la Meja Jenerali mstaafu, Herman Lupogo wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Meja Lupogo alifariki Oktoba 19 katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo. 
   Mke wa marehemu akiweka shada la maua.
   Familia ikiweka shada la maua.
   Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiweka shada la maua.
   Mashada ya maua yakiwekwa.
   Heshima kwa marehemu Meja Jenerali Herman Lupogo.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  IMG_2656
  Pichani juu na chini ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimtambulisha mgeni rasmi Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka kwa baadhi ya wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.IMG_2657
  IMG_2672
  Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akipokea heshima ya wimbo wa taifa kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe za maadhimisho miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
  IMG_2703
  Waziri wa Ardhi , Nyumba na maendeleo ya makazi, Profesa Anna Tibaijuka akikagua gwaride maalum kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake zilizofanyika leo jijini Dar.

  0 0
  0 0


  0 0

  Kaka Michuzi hii nimekutana nayo barabara ya Bagamoyo Road leo hii! Ni utaratibu na tabia mbaya kwa madereva na raia tunaotumia vyombo vya usafiri....ni hatari kwa usalama wetu! Tuwakemee

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Mhe. Dkt injinia Binilith Satano Mahenge (kulia) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mhe. Abdulkarim Hassan Shaha (wapili kulia),Pamoja na  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira wakikaguwa Mazingira katika moja ya kiwanda cha Mifuko ya Plastiki (East African Industy)kilichopo Mbagala jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt injinia Binilith Satano Mahenge (kushoto),akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mhe. James Lembeli (Mb),baada ya kuwasili kiwanda  kinachozalisha mifuko ya plastiki cha Binfijaa kilichopo barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira, Mhe. Dkt injinia Binilith Satano Mahenge (wa nne kulia),Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira  Mhe. James Lembeli Mb (wa tano ulia), pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Ardhi, Maliasili na Mazingira wakikaguwa mifuko Inayozalishwa na kiwanda cha BinFijaa kilichopo barabara ya Pugu jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Eden Garden Education Trust ya Mkoani Kilimanjaro wanaotarajia kufanya mitihani yao ya mwisho siku chache zijazo wakiingia ukumbini kwa ajili ya sherehe ya kuwaaga iliyofanyika shuleni hapo,Mbele ni mkuu wa Utawala shuleni hapo Peter Nayor .
  Wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Eden Garden Education Trust wakiingia kwa madoido uwanjani.
  Baadhi ya wazazi wenye watoto wao katika shule ya sekondari Eden Garden Education Trust wakifuatilia sherehe za kuaga wahitimu wa kidato cha nne.
  Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Eden Garden Education Trust wakifurahia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika sherehe yao ya kuagwa.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Baadhi ya watendaji wa TANAPA,wakimsikiliza Waziri Nyalandu alipotembelea hifadhi ya taifa ya Arusha.toka kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA ,Paschal Shelutete,Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Erastus Rufungulo na Betrita Loibook ,Mhifadhi Mkuu Arusha National Park. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akiteta jambo na Mhifadhi Mkuu Arusha National Park,Betrita Loibook.
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar walipokutana katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha na kumshawishi kutembelea hosptali ya Africa Amini Hearing Center.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Yummies Bakery ni mabingwa wa kuoka mikate mbalimbali, wakitumia kauli mbiu yao ya '' we bake to differ'' yaani tunatofautisha uokaji, kwa kuoka mikate bora kabisa na yenye ladha Nzuri; wapo Sinza Mori wanatizamana na kituo cha mafuta cha Big Bon , pia wana branches zao Masaki Chole Road Kituo cha Tax, Mwenge nyuma ya police post na Mbezi njia ya chini Kituo cha Msikitini, ukifika hapo utapata mikate mizuri ya brown , sweet breads, white breads, milk breads, maandazi , chapati , Pan Cakes, bites za aina zote, cookies, pastries, doughnouts,biscuits,pizza na burgers.

  Yummies Bakery pia ni mabingwa wa kutengeneza keki za aina zote kuanzia birthday, wedding, anniversaries, graduations, corporate events. wanatengeneza keki zenye picha kwa kutumia karatasi maalum za icing sugar zinazoweza kuprint picha za aina mbalimbali zinazolika; leta picha yako, ya mwanao au chagua cartoon yeyote tutaprint na kuweka juu ya keki.

  Wasiliana nao kwa namba 0655 672772 au 0657 913807
  Pia kwa email : yummiesb@gmail.com
  '' Chagua Yummies upate ubora'

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Polland jijini Warsaw akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 24, 2014. Wengine Pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara cha Polland, Bw. Marek Kloczko,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Polland, (Under Secretary Of State Ministry of Foreign Affairs), Bibi Katarzyna Kacperczyk na Bwana Jerzy Pietrewiez ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi ya Polland.
  Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Polland wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipowahutubia jijini Warsaw Oktoba 24, 2014.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua matrekta yanayotengenezwa katika kiwanda cha ROL- BRAT kilichopo Warsaw, Polland akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo Oktoba 24, 2014.


  0 0

  Na Editha Karlo wa Blog ya jamii
  WIZARA ya Elimu na mafunzo ya ufundi imepigilia msumari wa kuendelea kuwazuia wanafunzi wa shule za sekondari na shule za msingi za bweni na kutwa kumiliki simu za mkononi wakiwa shuleni na yeyote atakayekamatwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Jenista Muhaga wakati wa mahafali ya kidato cha nne na darasa la saba wa shule ya sekondari ya Mwilayamvya medium iliyopo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

  Akisoma hotuba kwa niaba ya Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mkaguzi Mkuu wa shule kanda ya Magharibi Hadrian Mlelwa alisema kuwa serekali imeendelea kukazia mkazo wa kukataza suala la wanafunzi kuwa na simu mashuleni.

  ''ninachowaomba waalimu na walezi mashuleni wawe wanawasaidia wanafunzi pale wanapokuwa na matatizo kwa kutumia simu za shule au za ofisi kupiga kwa wazazi wao au walezi kueleza shida zao za si vinginevyo''alisema

  Aliwataka wanafunzi hao kufuatilia masomo ambayo ndiyo yamewapeleka shuleni na wakimaliza masomo yao watakumbana na hayo mambo mtaani.

  Naye Mkuu wa shule hiyo King Saguda alisema kuwa jumla ya wahitimu 219 walimaliza elimu ya msingi na sekondari huku wahitimu wa kidato cha nne 175 wakiwa ni na wahitimu wa darasa la saba wakiwa ni 24.
  Mgeni rasmi katika mahafali ya saba kwa shule ya sekondari Mwilamvya Medium Hadrian Mlelwa kwa niaba ya Naibu Waziri wa Elimu,Mh. Hadrian Mlelwa akisoma hotuba yake.
  Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne ya darasa la saba shule ya sekondari Mwilamvya Medium Kasulu kwa Niaba ya waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Hadrian Mlelwa akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa shule hiyo kwenye chumba cha maabara pembeni ni Mkuu wa shule hiyo King Saguda.
  Mkaguzi Mkuu wa shule kanda ya magharibi akisoma maelezo yalipo kwenye jiwe la mradi wa maji kaika shule ya Mwilamvya Medium baada ya kuuzindua mradi huo shuleni hapo.
  Baadhi ya wahitimu wa darasa la saba katika shule ya Mwilamvya Medium Wilayani Kasulu wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi(ambaye hayupo pichani).
  Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwilamvya wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa hotuba yake.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara maalum.Mhe. Mark Mwandosya akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kenya Mhe William Ruto wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Mhe. Mwandosya alimuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe hizo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara maalum,Mhe. Mark Mwandosya na mkewe Lucy Mwandosya wakisalimiana na Rais wa kwanza wa Zambia Mzee Kenneth Kaunda wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Mhe. Mwandosya alimuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe hizo ambazo zimefanyika Mjini Lusaka jana.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara maalum,Mhe. Mark Mwandosya (wa tatu kulia ) pamoja na Mkewe Lucy Mwandosya wakishiriki kuimba Wimbo wa Taifa wa Zambia wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Wengine kutoka kulia ni Kaimu Rais wa Zambia Mhe Edgar Lungu ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi, na wa pili kulia ni Makamu wa Rais wa Nigeria Monance Namadi Sambo.

  0 0

   Wadau wa Kundi la Kandanda katika Mtandao wa kijamii wa Facebook ambao leo wamekutana pamoja katika kusherehekea maadhimisho ya miaka minne ya Kundi hilo,kwa kusakata mtanange mkali sana katika Uwanja wa TCC Club,Changombe jijini Dar es Saalam.Mtanange huo ulizikutanisha timu mbili zilizoundwa na wadau Dizo Moja na Ismail.TeamDizo iliibuka kidedea kwa kuinyuka TeamIsmail mabao 4-1 bila huruma na kufanikiwa kutwaa kombe la shampeni.
   Muanzilishi wa Kundi la Kandanda ndani ya Mtandao wa kijamii wa Facebook,Patrick Dumulinyi (wa pili kulia) akikabidhi kombe la ubingwa kwa Nahodha wa TeamDizomoja,Husolin Ulomi baada ya kuishinda TeamIsmail mabao 4-1 katika mtanange wa kuadhimisha miaka minne ya kuanzishwa kwa kundi hilo,leo kwenye Uwanja wa TCC Club,Chang'ombe jijini Dar.
   Muanzilishi wa Kundi la Kandanda ndani ya Mtandao wa kijamii wa Facebook,Patrick Dumulinyi. 
   Beki wa TeamIsmail akichambuliwa na Beki wa TeamDizomoja wakati wa mchezo wa kuadhimisha miaka minne ya kundi la Kandanda ndani ya Mtandao wa Facebook,uliochezwa asubuhi ya leo kwenye Uwanja wa TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
   Mshambuliaji wa TeamIsmail,Majaliwa Mkinga (kushoto) akionyesha ufundi wake mbele ya Beki wa TeamDizomoja katika mchezo uliopigwa leo kwenye Uwanja wa TCC,Chang'ombe jijini Dar.hadi mwisho wa Mchezo TeamDizomoja iliibuka kidedea kwa ushindi Mnono wa Mabao 4-1.

  Super Sub wa TeamIsmail,Nassor Binslum akimtoka mchezaji wa TeamDizomoja,Damas.


  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Balozi Ombeni Sefue ameeleza kufurahishwa na miradi ya sekta ya afya inayopendekezwa kuingia katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

  Balozi Sefue aliyasema hayo mara baada ya kutembelea jijini Dar es Salaam juzi, maabara inayokutanisha wataalamu mbalimbali kutoka SErikali na sekta binafsi wanaochambua miradi michache ya afya itakayoingizwa katika mfumo wa utekelezaji wa haraka wa miradi wa BRN.

  “Binafsi nimefurahishwa na maeneo ya kipaumbele mnayoendelea kuyafanyiakazi ili yapendekezwe kuingia katika BRN. Naahidi kuwa mtakapokamilisha mapendekezo yenu haya Serikali haitasita kuyafanyiakazi,” alisema Balozi Sefue.

  Balozi Sefue alisisitiza kuwa sekta ya afya ni muhimu katika maisha ya watanzania hivyo kuingizwa kwa baadhi ya miradi yake ya kipaumbele katika BRN kutasaidia kupatikana huduma bora zaidi.

  BRN ni mfumo mpya wa utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ulioanza kutekelezwa Julai mosi, 2013 ukiwa chini ya Kitengo cha Rais cha Utekelezaji wa Miradi (PDB).

  Akizungumza katika kikao hicho, Mtendaji Mkuu wa PDB, Bw. Omari Issa alifafanua kuwa mtindo wa maabara ni moja ya hatua nane katika mfumo wa utekelezaji wa miradi wa BRN ambapo wataalamu mbalimbali hujifungia kwa wiki sita kuchambua sekta husika na kuibua maeneo ya kufanyiwa kazi.

  “Katika maabara hii ya afya kama ilivyokuwa katika sekta nyingine zilizoshaingia BRN, wataalamu hawa wamekaa na watafanyakazi hii kwa wiki sita bila kulipwa posho,” alisema Bw. Issa na kuwapongeza wataalamu hao kwa kufanyakazi kwa uzalendo.

  Maabara hiyo ambayo mpaka sasa imeshakaa kwa wiki tano tayari imebaini maeneo ambayo yatapendekezwa kupewa kipaumbele katika sekta ya afya. Sekta za awali zilizokwishaingia BRN ni elimu, kilimo, maji, uchukuzi, nishati, ukusanyaji mapato na uboreshaji wa mazingira ya biashara.

  0 0

   Kampuni ya Kariati Matracktor Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omary Kariati, leo imekabidhi matrekta manne kwa wakulima wa wilaya ya Kondoa (matrekta matatu) na Mbarali (trekta moja), katika hafla iliyofanyika leo asubuhi, kwenye Ofisi za Kariati Matrektor, Kinondoni, Dar es Salaam. Zinazofuatia ni picha za hafla hiyo. Picha/Maelezo na Bashir Nkoromo
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kariati Matractor, Omary Kariati akimkabidhi fungua za trekta Mwakilishi wa wkulima wa Kondoa, Karoli Lubuva, katika hafla ya makabidhiano hayo, iliyofanyika leo.
   Kariati akikata uatepe kuzindua makabidhiano ya trekta hizo
   Kariati akiwapa maelezo kuhusu trekta husika kabla ya kuzikabidhi kwa wawakilishi wa wakulima hao leo.
  Kariati akilijaribu moja ya matrekta hayo akiwa na mwakilishi wa wakulima kutoka Kondoa Karoli Lubuva.

older | 1 | .... | 618 | 619 | (Page 620) | 621 | 622 | .... | 3348 | newer