Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

Mh. Ummy Mwalimu azitaka Halmashauri zote nchini kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa mazingira

$
0
0
Halmashauri zote Nchini zimetakiwa kuendelea kuhamasisha na kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya utunzaji wa mazingira na pia kuimarisha miundombinu ya masoko ambayo ni mibovu na ya kizamani.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara ya kutembelea masoko ya manispaa za Temeke na Ilala za jijini Dar es Salaam.

Amekumbushia pia kila Manispaa kuzingatia agizo la Makamu wa Rais la kufanya usafi kila jumamosi ya mwanzo wa mwezi pia ametoa wito watu kutooneana aibu katika kutupa taka hovyo. Kila mtu awe mlinzi wa mwenzie kuhakikisha anatunza mazingira ianavyotakiwa na pia hatupi taka hovyo, alisema Mheshimiwa Ummy.

Katika ziara hiyo aliongea na wafanyabiashara katika masoko hayo na walimwambia changamoto wanazokutana nazo katika swala zima la kudumisha usafi katika sehemu zao za biashara ni uhaba wa maji na vifaa vya kufanyia usafi.

Ziara hiyo ni muendelezo wa ziara za mbalimbali za Viongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika kuhakikisha utunzaji wa Mazingira unafanikiwa kwa kiasi kikubwa katika jiji la Dar es Salaam na Nchi ya Tanzania kwa ujumla.
Naibu Wazir Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Injinia Mussa Natty.
Naibu Wazir Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akipata maelezo juu ya usafi wa mazingira eneo la soko unavyofanyika. Anayetoa maelezo ni Mwenyekiti wa Soko la Tandale Sultan Ally Kinombo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika ziara kukagua soko la Temeke la Stereo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke Protidas Kagimbo.

EAC PARTNER STATES URGED TO IMPLEMENT SQMT TO FACILITATE REGIONAL TRADE

$
0
0
The Director General of EAC Customs and Trade Directorate, Mr. Peter Kiguta has urged EAC Partner States to play their roles in the implementation of EAC  Standardization, Quality Assurance, Metrology and Testing Act (SQMT) in order to realize the intended benefits of harmonized standards, promote trade and increase competiveness of products in the region.

Speaking during the official opening of the 18th Meeting of East African Standard Committee, which is  underway at the EAC headquarters, Mr. Peter Kiguta disclosed that the EAC Secretariat will soon undertake a mission to Partner States to sensitize the Ministers responsible for SQMT matters on the need to expedite the alignment of national laws and regulations in order to allow the region to have a uniform documentation for the targeted activities.

He said that implementation of EAC Standards should promote trade, increase competiveness of products in the region, ensure health and safety of citizens, protect environment to mention but a few of the expectations.

The Director General commended the East African Standards Committee for excellent efforts in the regional integration process and in particular the establishment of vibrant quality infrastructures in the region in the areas of reduction of standards related NTBs, mutual recognition of quality marks which have facilitated movement of goods, building of reliable laboratories some of which have achieved international recognition as well as enhanced networking with international SQMT organizations.

The 23-24 October 2014 meeting is being held as follow up of the recommendations from 17th Ordinary meeting of East African Standard Committee held in 2013 in Arusha,Tanzania.

The two-day meeting is expected to consider among others; matters arising from the report of the 17th EASC meeting; annual reports of the East African Technical Sub-committees for the period July 2013-September 2014, and progress reports from Development Partners on implementation of EAC Projects on Standardisation.

In addition, the meeting will consider report of meeting of Legal experts on consolidation of national positions on amendment of the SQMT Act; meeting of Technical Management Board (TMB) held in Zanzibar as well as CEOs meeting on Quality Information System and progress report by the Secretariat

bei ya Madafu

JK AKUTANA NA UONGOZI WA MAKAMPUNI YA CHINA YANAYOTAKA KUWEKEZA KATIKA UJENZI WA RELI NCHINI TANZANIA

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia ramani ya Tanzania inayoonyesha mchoro wa reli ya Kati inayotarajiwa kujengwa upya na kwa viwango vya kisasa wakati alipokutana na uongozi wa juu wa makampuni ya China yakiongozwa na China Railway Group Ltd. Makampuni mengine ni SINOSURE, Exim Bank, China Development Bank na China Agriculture Development Bank. Rais Dkt. Kikwete yuko nchini China kwa ziara rasmi ya kikazi (State Visit).
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya China Railway Group Limited Bwana Li Changjin na msafara wake kuhusu mpango wa serikali ya Tanzania wa kujenga reli mpya na ya viwango vya kisasa kutoka Dar Es Salaam hadi Kigoma, Tabora kwenda Mwanza, Kaliua kwenda Mpanda hadi Ziwa Tanganyika. Mazungumzo hayo yalifanyika huko Beijing tarehe 24.10.2014.PICHA NA JOHN LUKUWI.

WIZARA YA MALIASILI YABARIKI KUANZISHWA KWA MFUKO WA KULINDA MLIMA KILIMANJARO NA MLIMA MERU

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza wakati wa kikao kilicho shirikisha Kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira,Wabunge katika majimbo ya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,Wakuu wa wilaya zinazopakana na mlima Kilimanjaro na mlima Meru,TANAPA na Idara ya Misitu,(kulia)ni kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Ibrahim Msengi.
Naibu waziri wa TAMISEMI ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Siha ,akichangia wakati wa kikao cha kuanzishwa kwa mchakato wa uanzishwaji mfumo wa kiikolojia wa mlima Kilimanjaro na Mlima Meru ambao utalinda milima yote miwili.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AFUNGA MAFUNZO ELEKEZI YA WATUMISHI WAPYA

$
0
0
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Barnabas Ndunguru akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (hayupo Pichani) katika ufungaji wa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya wa Wizara.Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Sihaba Nkinga akiongea na baadhi ya Watumishi wapya wa Wizara katika ufungaji wa mafunzo elekezi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo aliwaasa kuwa na maadili katika utendaji wao wa kazi.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Sihaba Nkinga katikati akiongea na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. Leonard Thadeo kulia na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermens Mwansoko kushoto mara baada ya kufunga mafunzo elekezi kwa watumishi wapya wa Wizara.

MOI yajiimarisha katika utoaji huduma muhimu za Tiba na Upasuaji

$
0
0
Na Hassan Silayo-MAELEZO

Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imeendelea kuwa nguzo muhimu nchini katika utoaji wa huduma za tiba na upasuaji.

Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi wakati wa Mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Patrick amesema kuwa MOI imesaidia kuokoa zaidi ya asilimia 95 ya watanzania ambao kwa namna moja au nyingine wangeweza kupoteza maisha yao au kupata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali.

“MOI kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kuokoa maisha ya watanzania kwa zaidi ya asilimia 95 kutokana na kutoa huduma muhimu ya za tiba na upasuaji wa wagonjwa wanaopokelewa na hivyo kupunguza vifo na rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi” alisema Mvungi.

Akizungumzia kuhusu upasuaji wa kitaalam wa mgongo (specialized Spine Surgeries) Mvungi alisema kuwa Taasisi hiyo imeendelea kufanya na zaidi ya asilimia 99 ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wamepona na kurudi katika hali zao za kawaida.

Naye Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi Taasisi hiyo Bw. Almas Jumaa alisema kuwa zaidi ya wagonjwa 1,256 ya wagonjwa wa upasuaji mkubwa wa nyonga walipasuliwa salama na zaidi ya asilimia 95 ya wagonjwa hao wamepona kabisa.

Pia Almas alisema kuwa pia Taasisi imeendelea kutoa matibabu ya magonjwa ya ubongo yaliyokuwa yanahitaji upasuaji yamefanikiwa kufanyika kwa zaidi ya asilimia 80 na wagonjwa waliokuwa na matatizo hayo wamepona na kuondolewa kwenye hatari ya kupoteza uhai.

Taasisi ya MOI imewataka watanzania kuitumia Taasisi hiyo na kuacha kufuata matibabu nje ya nchi kwa gharama kubwa tofauti na kama wangepata huduma hizo hapa nchini kwa gharama nafuu.
Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Patrick Mvungi akieleza kwa vyombo vya habari(hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya Taasisi hiyo ikiwemo kufanikiwa kwa zaidi ya asilimia 95 ya kutoa huduma muhimu za Tiba na Upasuaji kwa wagonjwa wanaopokelewa na hivyo kupunguza vifo na rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi,wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar ea Salaam. Kushoto ni Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Almas Jumaa.
Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Almas Jumaa akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi Taasisi hiyo ilivyoendelea kuwa nguzo Muhimu katika kuokoa maisha ya watanzania ambapo upasuaji wa kitaalam wa mgongo umeendelea kufanyika na kufanikiwa kwa zaidi ya asilimia 99 na kusaidia kuwaondoa wagonjwa wenye tatizo hilo katika hatari ya kupotea uhai.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi. PICHA NA MAELEZO.

ANKO HASHIM LUDENGA AFUNGUKA ZAIDI KUHUSIANA NA SAKATA LA UMRI WA MISS TANZANIA 2014

$
0
0
Mkurugenzi wa Lino Angency International Ltd Hashim Lundenga
Hivi karibuni kulifanyika mashindano ya kumsaka mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2014 (Miss Tanzania 2014) ambapo Sitti Mtemvu alitangazwa kuwa mshindi.
Baada ya kutangazwa huko, kukawa na mambo mengi yaliyosemwa kumhusu. Kuanzia tetesi za kuwa kadanganya umri mpaka elimu. Kuwa kuna rushwa ilitumika mpaka kusemwa ana mtoto.
Mkurugenzi wa Lino Angency International Ltd Hashim Lundenga, anazungumza na mitandai ya Vijimambo na Kwanza Production kuweka bayana
KARIBU



WARSHA YA KUHUSU AMANI NA USALAMA BARANI AFRIKA YAHITIMISHWA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Mnasa Nyerembe akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Magese Mulongo ya kufunga Warsha ya siku tatu kuhusu Amani na Usalama Barani Afrika iliyoandaliwa na Umoja wa Afrika na kufanyika katika Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha.
Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Afrika na nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz kwa pamoja na Balozi wa Ethiopia katika Umoja wa Afrika Mhe. Konjit Sinegiorgis wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Nyerembe (hayupo pichani) alipokuwa akifunga Warsha hiyo ya Amani na Usalama Barani Afrika iliyowakutanisha Mabalozi, Wataalam wa masuala ya Amani na Wasuluhishi.
Sehemu nyingine ya Wajumbe wakimsikiliza Mhe. Nyerembe (hayupo pichani) akiwemo Rais Mstaafu wa Cape Verde, Mhe. Pedro Pires (kulia).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Waziri Mahenge akutana na Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mhe. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (aliyesimama), akizungumza na Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, kuhusu Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira katika Migodi ya Bulyankulu, North Mara, Geita na Buzwagi, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Ummy Mwalimu, akiwa pamoja na Mbunge wa Mafia, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. Abdulkarim Hassan Shaha (wa pili kulia).
Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira,wakifuatilia hotuba inayotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Muheshimiwa Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani).
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndg. Sazi Salula (wa katikati), akiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu Inginia Anjelina Madete (wa kwanza kushoto) wakifuatilia kwa makini hotuba inayotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Muheshimiwa Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (hayupo pichani).

Ukarabati na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda wakamilika

$
0
0
Serikali imekamilisha ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoa wa Katavi na hivyo kuufanya uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za binafsi na biashara.

Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Bw Seneti Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo, unaweza kutumika kutua na kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile ndege kubwa zinaweza kutua kwa dharura.

Aliiambia timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango iliyotembelea uwanja huo mwishoni mwa wiki kuwa uwanja huo umeongeza idadi ya wasafiri mara dufu kutokana na ukarabati na upanuzi uliofanyika.

Meneja wa Uwanja huo alisema idadi ya abiria imeongezeka kutoka abiria 285 mwaka 2009 hadi 2,390 mwaka 2013/14.

Bw. Lyatuu alisema kuwa uwanja huo umekarabatiwa na barabara ya kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa kiwango cha lami kutoka urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30 hadi kufikia urefu wa mita 1,820 na upana wa mita 30.

Alisema maeneo mengine yaliyokarabatiwa ni pamoja na kujenga uzio na mifereji ya kupitishia maji ya mvua. “Kwa sasa kiwanja kipo vizuri na ndege za aina zote zinaweza kutua hapa uwanjani hivyo, tunawakaribishwa wadau wote kuutumia uwanja huu” alisema Bw Lyatuu.

Eng. Caroline Mntambo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Makao Makuu Dar es Salaam alisema kuwa tayari wamealika mashirika ya ndege yanayofanya biashara hapa nchini kuanzisha safari katika uwanja huo. Mashirika hayo ni pamoja na ATC, Precision Air, Fast jet nk.

Eng Mntambo alisema kwa sasa shirika la ndege la Auric Air tayari limeanzisha safari za kwenda Mpanda ambapo linasafirisha abiria kutoka Dar- Mpanda – Mwanza mara tatu kwa wiki.

Alisema ndege zingine zinazotua uwanjani hapo kwa sasa ni pamoja na za UNHCR, ndege za kukodi na ndege za serikali.
Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, Mkoa wa Katavi Seneti Lyatuu akiwaonesha timu ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda. Nyuma yake (mwenye suti nyeusi) ni Mhandisi Caroline Mntambo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndenge Tanzania, Makao Makuu, Dar es Salaam.
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda Bw. Seneti Lyatuu akifafanua jambo wakati timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipotembelea kiwanja hicho.
Timu ya ukaguzi ikitazama barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda.
Barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoani Katavi.
Mhandisi Caroline Mntambo (mwenye suti nyeusi) akifafanua jambo kwa timu ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Uwanja wa ndege wa Mpanda umekarabatiwa na kupanuliwa hivyo , kuwa katika hali nzuri kwa matumizi ya ndege zote za binafsi na biashara. PICHA NA JOYCE MKINGA

new video: Special For You by Julio ft Chege

CHIKAWE AIBOMOA NGOME YA CHADEMA NACHINGWEA,VIGOGO, WANACHAMA WAO WARUDI KWA KISHINDO CCM

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (watano kulia waliosimama) akiwa na wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kukikimbia chao cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Wananchama hao 23 wakiongozwa na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa chama hicho wilayani Nachingwea, Manufreda Malenga (watano kushoto waliosimama) walifanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo. Picha zote na Felix Mwagara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akimkabidhi kadi ya CCM, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani humo, Manufreda Mathias Malenga. Kiongozi huyo pamoja na wanachama wengine 22 wa chama hicho wamekikimbia chao chao na kujiunga na CCM na kufanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akimpongeza Mwenyekiti wa Vijana wa Chadema Kata ya Mtua, Habibu Oswadi (kushoto) baada ya kukabidhi kadi ya chama chake. Kiongozi huyo wa Kata pamoja na wanachama wengine 22 wa chama hicho wamekikimbia chao chao na kujiunga na CCM na kufanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Abdalla Chikawe (wapili kulia kwa mgeni rasmi).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na Viongozi wa CCM Wilaya, Kata pamoja na wananchi waliofurika katika Uwanja uliopo jirani na Ofisi za CCM Kata ya Mtua katika sherehe kubwa ya kuwapokea viongozi wawili na wanachama 21 wa Chadema waliojiunga na CCM wilayani humo. Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi ambapo aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo.
Mwanachama mpya wa CCM ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Nachingwea na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Nachingwea, Manufreda Mathias Malenga akizungumza kwa hisia baada ya kupewa nafasi kueleza furaha yake baada ya kukabidhi kadi ya Chadema na kupewa kadi pamoja na sare za CCM. Malenga aliwashukuru Viongozi na wanachama wa CCM kwa kumkaribisha katika chama hicho na kuahidi kutoa ushirikiano wake ndani ya chama hicho. Kiongozi huyo pamoja na wanachama wengine 22 wa chama hicho wamekikimbia chao chao na kujiunga na CCM na kufanyiwa sherehe kubwa iliyofanyika katika Kata ya Mtua ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati meza kuu) alikuwa mgeni rasmi aliwapokea wanachama hao na kuwapa kadi pamoja na sare za CCM ili kuanza mapambano ya kupambana na upinzani wilayani humo.

MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARI WAMA-NAKAYAMA

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


Wanafunzi Taasisi ya Mufunzo Uanasheria kupata mikopo - Dkt. Migiro

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akikagua Jengo la Mahakama ya Mafunzo katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania leo (Ijumaa, oktoba 24, 2014) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu wake Mhe. Angellah Jasmine Kairuki na kulia ni Mkuu wa Taasisi hiyo Jaji Dkt. Gerald Ndika.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro akikagua Jengo la Mahakama ya Mafunzo katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania leo (Ijumaa, oktoba 24, 2014) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu wake Mhe. Angellah Jasmine Kairuki na kulia ni Mkufunzi wa Taasisi hiyo Bw. Goodluck Chuwa.
Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania Jaji Dkt. Gerald Ndika (kulia) akiongea na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro nje ya Jengo la Mahakama ya Mafunzo katika Taasisi hiyo leo (Ijumaa, oktoba 24, 2014) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu wake Mhe. Angellah Jasmine Kairuki na kulia ni Mkufunzi wa Taasisi hiyo Bw. Goodluck Chuwa. (Picha na Martha Komba, Wizara ya Katiba na Sheria).

Serikali inakamilisha taratibu za kuwasilisha Bungeni Muswada wa Sheria unaolenga kurekebisha Sheria ya Bodi ya Mikopo ili kuwawezesha wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) kupata mikopo kwa ajili ya mafunzo yao.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Asha-Rose Migiro amewaambia wanafunzi wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam leo (Ijumaa, Oktoba 24, 2014) kuwa lengo la Serikali kukamilisha mchakato huo katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia sasa.

POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA BENKI ILI KUBAINI NJAMA ZA WIZI

JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 39

Sky Light Band kupamba Nyama Choma Festival Mwanza Jumamosi Hii.

cheki songombingo la bodaboda mjini hanoi, vietnam

$
0
0
Wingi wa pikipiki na baiskeli katika mji Mkuu wa Vietnam, Hanoi, ni balaa. Yeyote aliyewahi kutembelea mji huo mkongwe anakiri kwamba songombingo la pikipiki na baiskeli si la kawaida, hasa ikiwa unatembea kwa miguu. 
Takwimu rasmi zinasema kulikuwa na pikipiki milioni 4 mwaka 1996 katika Vietnam yote. Leo idadi hiyo ipo mjini Hanoi peke yake, ambapo inaaminika kuna jumla ya pikipiki milioni 39 nchi nzima, ikimaanisha kwamba, ukiondoa wazee sana, na watoto, karibu kila M-Vietnam ana yake. 
Leo Ankal,  aliyeko Hanoi, mji ambao umekuwa na wakaazi tokea miaka 3000 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, kashuhudia hali hiyo katika mtaa mmoja sehemu za Hanoi ya zamani. Mambo ndio kama hivi…
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images