Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 23.10.2014


Airtel yatatua changamoto za uhaba wa vitabu vya sayansi Katika shule ya Sekondari Mukulati Mkoani Arusha

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  imeedelea kuungana na serikali katika kusaidia kuboresha maendeleo ya sekta ya elimu  nchini ambapo imetoa vitabu vya ziada na kiada  katika masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari mukulati wilayani Arumeru mkoani Arusha

Licha ya Kada ya sayansi kuwa ndio chimbuko kubwa  la wataalamu wengi katika fani mbalimbali bado  inatajwa kutofanya vizuri kutokana na uhaba wa miundombinu na vifaa stahiki ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya kada hiyo. 

Meneja wa Airtel mkoa wa Kilimanjaro  Paschal Mikomagu  akizungumzia mchango wa kampuni hiyo wakati wa mahafali ya 17 ya shule ya sekondari mukulati amesema Airtel kwa kutambua changamoto mbalimbali ndani ya kada ya sayansi nchini ikiwemo uhaba wa vitabu vya kujifunzia  imeamua kuwa na utaratibu wa kugawa vitabu hivyo.  Leo tumehudhuria mahafali  na kuchangia kutatua moja ya kero zinazokumba sekta ya elimu na tuaamini kwa msaada huu wa vitabu vitaongeza ufaulu wa wanafunzi na kusaidia shule kufanya vizuri kitaaluma

Tutaendelea kutimiza dhamira yetu kwa vitengo ya kusaidia kutatua changamoto mbalimbali mashuleni na kuhakikisha tunaboresha uwiano wa vitabu kwa wanafunzi hadi kitabu kimoja kwa mtoto moja au wawili.

Kwa upande wake Diwani wa  kata ya Olkokola Joseph laizer  leo ni sisi Airtel imetoa msaada huu wa vitabu ambavyo vitasaidia shule hapa , lakini zaidi tunawaomba Airtel waendelee kujitolea kushirikiana nasi  na kutufadhili katika ujenzi wa maabara katika shule hii ili kuweza kufikia malengo tuliyowekewa ya kuhakikisha kila shule ya sekondari inajenga maabara kwa ajili ya mafunzo ya ziada

Akiongea mara baada ya kupokea vitabu hivyo MkeeVitalisi Martine mkuu wa shule  kwa msaada huu umeongeza uwiano wa vitabu shule hapa ambapo kwa sasa kitabu kimoja kitatatumika na wanafunzi wawili,  napenda kuwhakikishia vitabu hivi havitakaa kwenye kabati bali vitatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa ili atimaye watoto waweze kupata ujuzi kupitia vitabu hivi

Nao baadhi ya wanafunzi walito maoni yao kuhusu mchango huu shule ni hapo ambapo Happy Lyimo alisema natoa shukurani za dhati kwa niaba ya wanafunzi wenzangu kwa Airtel kwa kutupatia mchango wa vitabu vingi vya sayansi. Nimatumaini yangu kuwa vitabu hivi vitasaidia kuinua taaluma kwa wanafunzi na  shule kwa ujumla.
Meneja Mauzo wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mkoa wa kilimanjaro Paschal Bikomagu kushoto akimkabidhi baadhi ya vitabu vya sayansi kwa Diwani wa kata ya Olkokola Joseph laizer kwa niaba ya shule ya sekondari Mukulati mkoani arusha wakati wa mahafali ya 17 ya kidato cha nne ya shule hiyo.
Makamu mkuu wa shule ya sekondari Mukulati ya mkoani arusha mwalimu Vitalisi Martine akiwakabidhi baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo vitabu vya sayansi vilivyo tolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakati wa mahafali ya 17 ya kidato cha nne katika shule hiyo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA BALOZI WA BOTSWANA NCHINI,PIA AKUTANA NA BALOZI WA RWANZA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Botswana nchini Tanzania, anayemaliza muda wake, Oliphant Tuelonyana, aliyefika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Botswana nchini Tanzania, anayemaliza muda wake, Oliphant Tuelonyana, aliyefika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Picha na OMR

UTUMISHI YAFANYA KIKAO KAZI KWA VIDEO CONFERENCE NA MIKOA YA SINGIDA,ARUSHA NA DODOMA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akifungua kikao kazi kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference)kilichojumuisha Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Naibu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kulia) akifuatilia mada wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference) kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Afisa Utumishi Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi.Sakina Mwinyimkuu akiwasilisha katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Ki-elektroniki (video conference) kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni viongozi wa Ofisi ya Ris Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada.
Baadhi ya viongozi na watumishi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwa njia ya Kielektroniki (video conference) kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo.
Afisa Utumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bi.Magreth Ngondya (kushoto) akiwasilisha mada katika kikao kazi kilichofanyika kwa njia Ki- elektroniki (video conference) katika kikao kazi kati ya Utumishi na Mikoa ya Singida, Arusha, Dodoma na Tume ya Mipango katika ukumbi wa Utumishi mapema leo. Wengine ni viongozi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada.

AU YAWATUNUKU DKT. SALIM NA BALOZI MBITA TUZO ZA JUU ZA MWANA WA AFRIKA

$
0
0

Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim akipokea Tuzo ya Juu ya Umoja wa Afrika ya Mwana wa Afrika kwa Mwaka 2014 kutoka kwa Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Mhe. Balozi Smail Chergui. Tuzo hiyo  ilitolewa mjini Arusha pembezoni mwa Warsha ya Tano ya Ngazi ya Juu kuhusu Amani na Usalama Bararani Afrika iliyoandaliwa na Umoja wa Afrika inayoendelea mjini humo. Tuzo hiyo pia imetolewa kwa Balozi Mstaafu na Mpigania Uhuru Mahiri Barani Afrika, Balozi Hashim Mbita. Tuzo hizo zimetolewa kwao kutokana na mchango mkubwa walioutoa Barani Afrika na kwa Umoja wa Afrika ambapo Dkt. Salim alikuwa Katibu Mkuu wa saba wa OAU kuanzia mwaka 1989 hadi 2001. Kwa upande wake Balozi Mbita alikuwa Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Ukombozi Barani Afrika chini ya OAU kuanzia mwaka 1974 hadi 1994 ilipomaliza kazi yake baada ya Uhuru wa Afrika Kusini.
Balozi Chergui akimkabidhi Cheti cha Tuzo hiyo Dkt. Salim.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Vodacom yafungua duka jipya jengo la Quality Centre Uchumi

$
0
0
Katika kuhakikisha wakazi wa Temeke na Ilala wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imefungua duka jipya katika jengo la Quality Centre Uchumi  lililopo katika barabara ya Nyerere ambalo ni moja ya kituo kikubwa cha biashara jijini Dar es Salaam likiwa na maduka makubwa,ukumbi wa sinema,sehemu za burudani na maofisi.

Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma  kwa mawakala wa Mpesa na uuzaji wa bidhaa  za Vodacom na litawawezesha wateja wa  barabara ya Nyerere,Keko,Ilala,Chang’ombe na Temeke kupata huduma kwa karibu.

Ofisa Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji  wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh, alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa  ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza  kuboresha maisha morani kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo.

“Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia”Anasema Saleh.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa,aliipongeza Vodacom kwa kufungua duka katika eneo hilo lenye wananchi wengi na kuongeza kuwa anaamini litawaokolea muda waliokuwa wanatumia kufuata huduma za Vodacom mbali na kuwasihi kutumia huduma ya M Pesa kwani ni huduma iliyo bora na yenye usalama zaidi.

Vodacom ina mtandao wa maduka  82 na wakala mbalimbali wakuuza bidhaa zake nchini na  duka lililofunguliwa leo ni la sita kufunguliwa katika wilaya ya Temeke.Hivi karibuni inatarajia kufungua maduka katika maeneo ya Mbagala,Buguruni,Sea Cliff na Bagamoyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa wa kwanza toka kulia pamoja na Meneja wa duka hilo Irene Njovu na Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Hassan Saleh wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka jipya na la kisasa la Vodacom Tanzania,lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere ambalo ni moja ya kituo kikubwa cha biashara jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Majira Rayusa Yassini aliefika katika uzinduzi wa duka jipya na la kisasa la Vodacom lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.Akimiminiwa kinywa cha mvinyo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa(kushoto)ikiwa ni moja ya ishara ya uzinduzi wa duka hilo.Wanaoshuhudia wa pili toka kushoto ni Meneja wa duka hilo Irene Njovu na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa(kushoto)na Mwandishi wa habari wa Gazeti la Majira Rayusa Yassini aliefika katika uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Vodacom lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam wakigonganisha glasi zenye mvinyo ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa duka hilo. Wanaoshuhudia wa pili toka kushoto ni Meneja wa duka hilo Irene Njovu na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Silaa(katika) akiangalia moja ya Simu zinazouzwa katika duka jipya la na la kisasa la Vodacom lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam,mara baada ya kuzindua rasmi duka hilo kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia na kushoto kwa Meya ni Ofisa Mkuu wa Idara ya Uuzaji na Usambazaji wa Vodacom Hassan Saleh na kulia ni Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa kampuni hiyo Upendo Richard.
Baadhi ya waandishi na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa katika uzinduzi wa duka la Vodacom Tanzania, lililopo Quality Centre katika barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.

RAIS WA TOC KUFUNGA KOZI YA MAKOCHA

$
0
0
Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid kesho (Oktoba 24 mwaka huu) atafunga kozi ya makocha ya Leseni C ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Hafla ya ufungaji kozi hiyo iliyoshirikisha makocha 32 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na kuandaliwa na TOC kupitia Olympic Solidarity kwa ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itafanyika saa 5 asubuhi kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kozi hiyo ya wiki mbili iliyoanza Oktoba 12 mwaka huu iliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Ulric Mathiot kutoka Shelisheli.

Makocha walioshiriki kozi hiyo ni Ahmed Suleiman Simba (Alliance), Akida Saidi (Lindi), Ally Bushir Mahmoud (Zanzibar), Aloyce Akwilin (Pwani), Amin Rashid Mdowe (Zanzibar), Augustino Dakto Damian (Katavi), Athuman Bilal (Shinyanga), Bakari Shime (Tanga), Charles Mayaya (Shinyanga) na Choki Abeid (Geita).

Wengine ni Edna Lema (Morogoro), George Melchior (Kagera), Godfrey Kapufi (Katavi), Hamis Mabo (Kigoma), Hawa Bajangero (TWFA), Ibrahim Mulumba (Geita), Jemedari Said (TAFCA), Kenny Mwaisabula (TAFCA), Madenge S. Omari (Mara), Milambo Camil (Tabora) na Mohamed D (Ruvuma).

Pia wapo Mohamed Ismail Laiser (Manyara), Mohamed Muya (Dodoma), Ngawina Ngawina (Mtwara), Nicholas Kiondo (Ilala), Osuri Charles Kosuri (Simiyu), Rachel Palangyo (TWFA), Salvatory Edward (Temeke), Seif Bausi Nassor (Zanzibar), Yusuf Macho (Kigoma), Wilfred Mollel (Iringa) na Zacharia Mgambwa (Rukwa).

Makocha watakaofaulu kozi hiyo watapewa Leseni C za CAF wakati watakaoshindwa watapewa vyeti vya ushiriki tu.  

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

KERO YA UCHAFUZI WA MAZINGIRA KWA BAADHI YA WAKAZI WA JIJI LA MBEYA


mkutano wa masuala ya madini wafanyika mjini Morogoro

$
0
0
Kamishna wa Madini, Mhandisi Paul Masanja (kushoto) akieleza jambo kabla ya ufunguzi wa Kikao cha Kazi cha Idara ya Madini. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Alfred Shayo ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika kikao hicho.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Alfred Shayo (katikati) akifungua rasmi kikao cha Kazi cha Idara ya Madini kilichofanyika hivi karibuni katika hoteli ya Kings Way ya Mkoani Morogoro. Kushoto ni Kamishna wa Madini, Mhandisi Paul Masanja na kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini- Uratibu, Mhandisi John Shija.


Baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao cha kazi cha Idara ya Madini wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa katika kikao hicho.
Kamishna wa Madini, Mhandisi Paul Masanja (kushoto) akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Alfred Shayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha Idara ya Madini kinachofanyika katika hoteli ya King’s Way ya Mkoani Morogoro.
Kamishna wa Madini, Mhandisi Paul Masanja (wanne kutoka kushoto, waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha kazi cha Idara ya Madini kilichofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Kings Way ya Mkoani Morogoro. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Alfred Shayo ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika kikao hicho.

WAZIRI CHIKAWE AMKABIDHI MKUU WA WILAYA NACHINGWEA MABATI 2000 KWA AJILI YA UJENZI WA MAABARA SHULE ZA SEKONDARI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo mabati 2000 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara za Shule 20 za Sekondari wilayani humo. Waziri Chikawe ametoa msaada huo baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa agizo kwa kila mwana jamii nchini kuchangia ujenzi wa maabara katika shule za Kata nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Abdalla Chikawe (wapili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Valery Kwembe wakiyaangalia msaada wa mabati yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo kwa ajili ya kuzisaidia Shule za Sekondari za Kata kwa ajili ya ujenzi wa maabara. Makabidhiano ya mabati hayo 2000 yalifanyika nyumbani kwa Waziri Chikawe mjini Nachingwea leo. Picha zote na Felix Mwagara.

Dkt. Shein akutana na kuzungumza na Balozi wa Marekani,ikulu Zanzibar

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Bradley alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Bradley baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Bradley baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI (PAC) YAJADILI HESABU ZA MWAKA WA FEDHA WA 31 DESEMBA, 2012 BAADA YA RIPOTI YA CAG, KWA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC)

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Zitto Kabwe akiongoza kamati hiyo siku ya tarehe 23 Oktoba, 2014 katika Ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili hesabu za mwaka wa fedha wa 31 Desemba, 2013 kwa Shirika la Bima la Taifa (NIC) baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
Mbunge wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Ismail Rage akichangia mada wakati wa kamati hiyo siku ya tarehe 23 Oktoba, 2014 katika Ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam, kujadili hesabu za mwaka wa fedha wa 31 Desemba, 2013 kwa Shirika la Bima la Taifa (NIC) baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt. Edmund Mndolwa (kushoto) akijibu maswali toka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali kwa lengo la kujadili hesabu za mwaka wa fedha wa 31 Desemba, 2013 kwa Shirika la Bima la Taifa (NIC) baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Justine Mwandu akichangia mada kuhusu kujadili hesabu za mwaka wa fedha wa 31 Desemba, 2013 kwa Shirika la Bima la Taifa (NIC) baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wakichangia mada wakati wa Kamati ya kujadili hesabu za mwaka wa fedha wa 31 Desemba, 2013 kwa Shirika la Bima la Taifa (NIC) baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). kamati iliyofanyika siku ya tarehe 23 Oktoba, 2014 katika ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam,
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia kwa karibu kikao cha Kamati ya Hesabu za Serikali kilichofanyika siku ya tarehe 23 Oktoba, 2014 katika ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili hesabu za mwaka wa fedha wa 31 Desemba, 2013 kwa Shirika la Bima la Taifa (NIC) baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DSM)

MSAADA TUTANI ILI KUOKOA UHAI WA MTOTO HUYU

$
0
0

Mtoto  Zabibu Salum Abdalah
---------------
Na Steven Augustino wa demasho.com, Tunduru.
MZAZI wa mtoto wa miezi sita Zabibu Salum Abdalah ,ambaye kichwa chake kina kuwa kikubwa kila siku tangu azaliwe ameomba msaada wa fedha ili kufanikisha kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.

Mama mzazi wa Mtoto Bi. Zainabu Mustafa Rajab,alisema kuwa Binti yake huyo alizaliwa April 24 mwaka huu katika hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Tunduru,na kwambatatizo hilo la kuanza kukua kwa kichwa chake lilianza kujitokeza mwezi mmoja baadaye.

Alisem abaada ya tukio hilo,walianza kuhangaika kutafutamatibabu katika hospitali mbalimbali ,lakini hadi leo juhudi zao zimegongamwamba ,baada ya kuandikiwa barua ya Rufaa inayowata kakumpeleka kijana wao huyo katika Hospitali ya TaifaMuhimbili.

Alisema kutokana na wanafamilia hao kutokuwa na uwezo kifedha taarifa hiyo imewakatisha tamaa ya kuokoa maisha ya kijana wao huyo hali ambayo imewafanya kuwaangukia Watanzania wenzao,ili kuomba msaada huo utakao jumuisha nauli ya kutoka Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kwenda Jijini Dar es Salaam, pamoja na gharama za matibabu.

Bi Zainabu aliendelea kufafanua kuwa baada ya kuandikiwa barua hiyo ,yeye na mzazi mwenzie , walienda katika ofisi ya MkuuwaWilaya , ilikuomba msaada la kini waliambulia kupewa barua ya utambulisho wa kuwaomba msaada wananchi mjini humo, 
 Lakini hadi sasa hakuna msaada wowote walioupata kupitia mfumo huo wa barua.

Alisema kwa mtu atakaye guswa na tukio hilo anaweza kutuma msaada wake kwa kutumia Simu na mba 0685179479 ya animtandao wa Airtel money.
Akizungumzia tukio hilo ,Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya yaTunduru Dr. Alex Kazula, pamoja na kuthibitisha kuwepo kwa tukio la mgonjwa huyo, alisema kuwa Hospitali yake imechukuwa uamuziwa kumpatia Rufaa hiyo, baada ya maafisa tabibu waliopo Hospitalini hapo kutokuwa na ujuzi wakutibu maradhi hayo.

KUMBUKUMBU

$
0
0
MAREHEMU DAFROSA KWEKA MSENGI 
11-05-1970 - 24-10-1999

Leo umetimiza miaka kumi na tano(15) tangu ulipoitwa mbinguni kwa BABA. Kweli ua zuri limerudi kwenye Bustani ya Eden.

Hatuna cha kusema, tumebaki kushukuru tuu maana imeandikwa tushukuru kwa kila jambo. Tunakumbuka sana Upendo na Ushirikiano uliokuwa nao, Uchapakazi na Uzuri uliokuwa nao. Kweli ulikuwa mfano wa kuigwa, hata kazini kwako wanakukumbuka.

Dafrosa, tupo kama ulivyotuacha ila tumepungukiwa tena na mama yako URSULA ambaye tumemzika hivi karibuni baada ya kuugua kwa muda mrefu sana. Imani yetu ni kuwa ipo siku wote tutakutana tena paradiso. 

 Unakumbukwa sana na mumeo mpendwa DR. IBRAHIM MSENGI, mwanao wa pekee JESCA, nduguzo JANE,FESTO,EUGENIA,ELIZABETH,CECILIA na THADEI,shangazi yako mpendwa SR. DEVOTHA KWEKA CDNK, Wajomba,Mashemeji na Mawifi wa kwa BASI wote,WAKWEKA wote wa NARUMU,kina MSENGI wote wa MKALAMO – SINGIDA,Wafanyakazi wa idara ya fedha za Kigeni – Benki kuu,Majirani wa TEMEKE –MIKOROSHINI na TABATA ,Ndugu,Jamaa na Marafiki wote. 

“RAHA YA MILELE UMPE Eee Bwana…….”

SWEDEN YATOA BIL. 42/- KUSAIDIA MIRADI UN

$
0
0
DSC_0216
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kutiliana saini makubaliano kati ya nchi ya yake na Umoja wa Mataifa ambapo wametoa fedha kusaidia miradi ya Umoja wa Mataifa kwenye ofisi za ubalozi wa Sweden jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.(Picha na Zainul Mzige).

Na Mwandishi wetu
SWEDEN imeyapatia mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini jumla ya shilingi bilioni 42/- ili kusaidia katika miradi yake ya maendeleo inayofanya nchiini Tanzania.
Makubaliano ya fedha hizo yametiwa saini jana kati ya Balozi wa Sweden Lennarth Hjelmaker na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez.

Fedha hizo ambazo ni sawa na dola milioni 24, zitaelekezwa kwenye miradi ya UNDAP inayoendana na sera za Sweden za kuwezesha masuala ya utawala bora, ustawi wa jamii, wanawake na watoto na usawa wa kijinsia.

Kwa mujibu wa Balozi wa Sweden, fedha hizo zitasaidia utekelezaji wa Mkukuta, Mkuza na Matokeo makubwa sasa (BRN) mipango inayofadhiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa .

Alisema ni matumaini yake kuwa fedha hizo zitaboresha hali ya kufanya biashara, kuwekeza kwa lengo la kutoa ajira zaidi,kuwezesha uchaguzi huru, kuimarisha huduma za jamii, kuimarisha mipango, uwajibikaji na kuimarisha mawasiliano ya radio kwa ajili ya upashanaji habari vijijini ili kusaidia maamuzi yenye mtazamo mpana zaidi miongoni mwa watu wa vijijini.
IMG_2231
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Lennarth Hjelmaker (kulia) na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakitiliana saini makubaliano ya msaada wa fedha hizo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ofisi za ubalozi huo.


Introducing Zipompapompa, Tanzania's newest female comedian

$
0
0
Mama wa Mitindo Asia Idarous-Khamsin akimuandalia vazi la khanga mchekeshaji na MC  maarufu nchini Zipompapompa ambaye ni mmoja wa wasanii mashuhuri wataonogesha tamasha kubwa la aina yake la SIKU YA MSANII Jumamosi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. Msikilize Zipompapomba hapo akitoa yake chini...

INTRODUCING "HERI MUZIKI - NCHI YETU"

Wajumbe wa idara ya utumishi ya uwalimu watembelea nyumba za PSPF zilizopo eneo la Lukobe mjini Morogoro

$
0
0
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Neema Muro, (Kushoto), akizungumza na baadhi ya wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, kwenye eneo la mradi wa nyumba za Mfuko huo eneo la Lukobe mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Wajumbe hao walifanya ziara hiyo mara baada yab kuhudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa lengo la kuwaelimisha juu ya faida mwanachama anazoweza kupata anapojiunga na Mfuko huo.
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Neema Muro, (Kushoto), akiwapa maelezo, baadhi ya wajumbe wa tume ya utumishi wa walimu, kuhusu mradi wa nyumba za Mfuko huo, zilizoko eneo la Lukobe mjini Morogoro, mwishoni mwa wiki.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (Mwenye T-Shirt), akiwapa maelezo wajumbe wa idara ya utumishi wa walimu, kuhusu nyumba za Mfuko huo zilizoko eneo la Lukobe mjini Morogoro, mwishoni mwa wiki mara baada ya kuhudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mjini humo.

Article 22

HOFU YA UGONJWA WA EBOLA YATANDA MJINI MOSHI

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.

WAKAZI wa kata ya Shirimatunda katika maanispaa ya Moshi, wameingiwa na hofu ya kupoteza maisha yao,kufuatia taarifa za kuwapo kwa mtu anayedhaniwa kuwa na ugonjwa hatari wa Ebola anayehudumiwa katika zahanati ya kata hiyo.


Kutokana na hofu hiyo,halmashauri ya manispaa ya Moshi imelazimika kuifunga kwa muda usiojulikana zahanati hiyo na kuwahamishia wagonjwa katika hospitali nyingine ikiwamo ya St Joseph katika manispaa hiyo.



Ripota wetu ambaye alikuwa eneo la zahanati hiyo alishuhudia baadhi ya madaktari wakiongozwa na mganga mkuu wa manispaa hiyo,Dk Christopher Mtamakaya pamoja na wataalamu wengine wa afya wakifanya kikao cha dharura kujadili hali hiyo.



Kadhalika,waandishi wa habari waliokuwepo katika zahanati hiyo
walishuhudia baadhi ya wataalamu wa afya wakiwa na mavazi rasmi yanayotumiwa na madaktari wanaohudumiwa wagonjwa wa Ebola.



Pamoja na kikao hicho,Zahanati hiyo imewekwa tangazo katika lango kuu linalosomeka 'Huduma zote za afya zimesitishwa kwa muda, Utawala' hali ambayo imeendelea kuzua maswali mengi kwa wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu katika zahanati hiyo.



Mwenyekiti wa mtaa wa Kigongoni,kata ya Shirimatunda ilipo zahanati hiyo,Juma Sambeke alisema hajashirikishwa katika maamuzi ya kugeuza Zahanati hiyo kama Karantini ya mtu anayedhaniwa kuwa na Ugonjwa wa Ebola.



Alisema kuwapo kwa karantini hiyo kumeanza juzi majira ya saa 10 jioni baada ya kupokea taarifa kutoka afisa mtendaji wa kata hiyo kwamba zahanati hiyo itafungwa kwa muda ili kumhudumia mtu anayedhaniwa kuwa Ebola.



"Manispaa haikuwa sahihi kuitumia zahanati hii kama karantini ya hofu ya Ebola, hapa kuna shule ya chekechea, sekondari, seminari ya Don Bosco na majirani kama unavyowaona....wasipopewa elimu na kama huu ni ugonjwa wa Ebola watu watakufa sana"alisema.



Sambeke alisema maeneo yatakayoathirika zaidi na kufungwa kwa zahanati hiyo ni Shirimgungani,Cherereni ya Moshi vijijini,Karanga,
Soweto,Bonite madukani na mtaa wa Kigongoni ambapo zahanati huudumia zaidi ya watu 5,000 kwa mwezi.



Kwa upande wake diwani wa kata ya Shirimatunda,Felix Mushi alisema huduma za utoaji wa chanjo ya magonjwa ya Rubella na Surua zimehamishiwa katika ofisi ya mtendaji wa kata hiyo huku wagonjwa wengine wakihamishiwa maeneo mengine.



Alisema tarifa za awali alizopata ni kwamba mtu huyo alipokelewa
katika uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA), ambapo
alisafirishwa hadi kwenye zahanati hiyo baada ya kudai kuwa na dalili zinazoashiria ugonjwa wa Ebola.



Aidha taarifa zaidi zinadai kuwa wataalam wamechukua sampuli kutoka kwa mgonjwa huyo kwa ajili ya vipimo, ili kujiridhisha, wakati huduma nyingine za matibabu zikiendelea kutolewa kwa mgonjwa huyo anayedaiwa kusafiri kutoka nchini Senegal.



Mmoja wa wakazi anayeishi jirani na zahanati hiyo, Thadei
Sangawe,alisema ameanza kufanya mawasiliano na ndugu wengine waliopo maeneo mengine mkoani humo ili aweze kuhamisha familia yake kuepuka madhara kama ugonjwa huo utakuwa wa Ebola.



"Tunaomba viongozi wenye dhamana hususani madaktari watoe taarifa kwa wananchi juu ya hii hofu iliyopo,maana kukaa kwao kimya kutasababisha wananchi washindwe kuchukua tahadhari na hivyo kusababisha madhara"alisema.



Hata hivyo akizungumza na waandishi wa habari, mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Shaban Mtarambe, alisema hayuko tayari kuzungumza kwa maelezo kuwa suala hilo ni la kitaalam zaidi linalohitaji waataala wa kada ya afya kulizungumzia.



Naye mganga mkuu wa manispaa ya Moshi,Dk Christopher Mtamakaya alipohojiwa kuhusiana na taarifa za kuwapo kwa mgonjwa huyo hakuwa tayari kuzungumza zaidi na alipotumiwa ujumbe wa simu ya mkononi alijibu kwa kifupi, huo ni Uvumi.



Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa huo,Dk Mtumwa Mwako alipohojiwa kuhusiana na kuwapo kwa mgonjwa huyo naye alisema hafahamu na aliomba kupewa muda kwani alikuwa katika kikao.



Kuhusiana na suala la mgonjwa huyo,katibu tawala wa mkoa huo, Dk Faisal Isa alisema taarifa za kwanza anapata kutoka kwa mwandishi wetu na akaomba muda wa kufuatilia zaidi.

Lango kuu la kuingia zahanati ya Shirimatunda likiwa na tangazo la kusitishwa kwa huduma za afya katika zahanati hiyo kwa hofu ya kuwapo kwa mgonjwa wa Ebola.
Baadhi ya wagonjwa na wauguzi katika zahanati ya Shirimatunda
wakihamia katika ofisi ya mtendaji wa kata ya Shirimatunda kuendelea na huduma za tiba ikiwamo utoaji wa chanjo ya Surua na Rubella
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images