Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

WAMA YAKABIDHI MAJENGO YA MADARASA SHULE YA SEKONDARI NYAMISATI MKOA WA PWANI WILAYA YA RUFIJI

$
0
0
 Makamu Mwenyekiti WAMA,Mama Zakia Meghji akikata utepe kabla ya kumkabidhi majengo ya madarasa Naibu Waziri TAMISEMI, Kassim Majaliwa (wa pili kushoto) Mkuu wa wilaya ya Rufiji Nurdin Babu (wa pili kulia) na Kiongozi wa WAMA (kulia)
 Viongozi wakitembelea moja ya sehemu za shule.
 Makamu Mwenyekiti WAMA Zakia Meghji akizungumza.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Chanjo ya ugonjwa wa surua na rubella Manispaa ya Ilala yavuka lengo

$
0
0
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Ilala Dkt. Willy Sangu akionyesha picha ya yenye maelezo ya Chanjo ya kukinga ugonjwa wa Surua na Rubella wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya zoezi la chanjo hiyo linalofanyika nchi nzima.

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Manispaa ya Ilala imevuka lengo la kutoa chanjo ya ugonjwa wa Surua na Rubella kwa watu 468,297 ambapo awali lengo lao lilikuwa kutoa chanjo hiyo kwa watu 445,801 wakati wa wiki ya kutoa chanjo hiyo nchini.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manispaa ya Ilala Dkt. Willy Sangu leo jijini Dar es salaam alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya zoezi la chanjo hiyo linalofanyika nchi nzima.

Dkt. Sangu alisema kuwa zoezi la kutoa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Surua na Rubella linaendelea vizuri katika Manispaa ya Ilala kama ilivyopangwa ambapo linafanyika kwa muda wa wiki moja katika kote nchini. “Ninawaomba watu wote ambao hawajajitokeza kupata chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Surua na Rubella, wafike kwenye vituo vya kutolea chanjo hiyo ili kuokoa maisha ya watoto, akina mama wajawazito, akiba baba na vijana” alisema Dkt. Sangu.

Dkt. Sangu alisema kuwa idadi ya watu walioitikia wito wa kupata chanjo hiyo imekuwa kubwa katika Manispaa ya Ilala suala ambalo linawapa faraja ambapo watu wa rika zote wamejitokeza kupata huduma.

Ili kutoa huduma ya chanjo kwa wakati kulingana na ratiba, Dkt. Sangu amesema kuwa imewalazimu kuongeza vituo 30 ambapo timu ya wahudumu kutoka kwenye vituo mama inatoka ili kuwafuata wananchi waliko.

Awali Manispaa ya Ilala ilitenga vituo 236 vya kutoa chanjo hiyo kwa wananchi ndani ya Manispaa hiyo.

Dkt. Sangu amesema kuwa mafanikio idadi kubwa hiyo ya mwitikio wa watu kupata chanjo katika manispaa ya Ilala yanatokana na sifa ya kuwa katikati ya jiji ambapo watu wengi hupata huduma mbalimbali za kijamii.

Kwa upande wake Afisa Muuguzi Hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo Ilala Queen Lutufyo amesema kuwa mwitikio wa watu kuja kupata chanjo ni mzuri na hawajakosa wateja muda wote wakati wa kutoa huduma hiyo kituoni hapo.

Aidha, katika zoezi la kutoa chanjo hiyo magonjwa ya Surua na Rubella wahudumu pia wanatoa dawa za magonjwa ya matende, mabusha, minyoo na matone ya vitamin ‘A’.

Muda wa kutoa huduma hiyo ya chanjo vituoni ni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni licha ya kwanba wakati mwingine huduma hiyo hutolewa hadi saa 1:00 usiku kulingana na idadi ya wateja waliopo katika kituo wakati huo kuanzia Oktoba 18 hadi 24 mwaka huu.

Zoezi la kutoa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Surua na Rubella nchini linaongozwa na kauli mbiu inayosema “Linda, Okoa, Zuia ulemavu- Kamilisha Chanjo” na kusimamiwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa ufadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Kusaidia Watoto (unicef), Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la Misaada la Marekani (UNSAID) na Muungano wa watoa chanjo duniani (Gavi).

Mh.Samia Suluhu mgeni rasmi uzinduzi wa njia mpya za shirika la ndege la Flydubai jijini Dar leo.

$
0
0

Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo wa njia mpya ya shirika la ndege la Flydubai lenye makao yake makuu Dubai..
Mgeni rasmi,Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano,Mh Samia Suluhu akizungumza mapema leo katika uzinduzi wa njia mbili mpya za ndege ya FlyDubai aina ya Boieng 737-800,uliofanyika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar.
Makamu wa Rais mwandamizi katika shughuli za kibiashara wa shirika la ndege la FlyDubai ,Bwa.Sudhir Sreedharan akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wana habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani) katika hafla fupi ya uzinduzi wa njia mbili mpya za shirika la ndege hiyo kutoka Dubai kuja jijini Dar es salaam na Zanzibara (nchini Tanzania). Bwa.Sudhir amesema kuwa shirika hilo la Flydubai liliingia katika soko la kibiashara kuanzia mnamo mwaka 12009,ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kuongeza njia mpya sita (six new routes ) .
 Wageni waalikwa wakishangilia jambo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tukio hilo .

BALOZI KAMALA AKUTANA VIONGOZI WAANDAMIZI WA BENKI BENKI YA BNP PARIBAS

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Benki ya Kimataifa ya BNP PARIBAS baada ya kumaliza kikao nao leo Brussels. Wa kwanza kulia ni Bwana Guy Vandevelde Makamu wa Rais wa Benki hiyo.

Article 7

SOS VILLAGES IKISHIRIKIANA NA MONTAGE INAWALETEA CHAKULA CHA HISANI

$
0
0
MONTAGE
SOS VILLAGES IKISHIRIKIANA NA MONTAGE INAWALETEA CHAKULA CHA HISANI KATIKA KAMPENI YAO YA ‘NIJALI, MCHANGO WAKO TUMAINI LA MAISHA YANGU’ KWA AJILI YA WATOTO WA SOS VILLAGES ITAKAYOFANYIKA TAREHE 24/10/2014 PALE HOTEL YA SERENA MJINI ZANZIBAR KUANZIA SAA MOJA USIKU.

MGENI RASMI ATAKAWA MHESHIMIWA MAKAMU WA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR MOHAMMED GHARIB BILAL, TICKET ZINAUZWA SHILLING LAKI MBILI ZA KITANZANIA AU SHNG MILION MBILI KWA MEZA YA WATU KUMI, PIGA SIMU NO 0756-860231 AU 0715-003355 UNAWEZA PIA CHANGIA KWA KUPITIA EASY PESA NO 0774 022270 AU TIGO PESA 0652 475847

PUSH MOBILE MEDIA LTD, PARTNERS WITH APALYA TECHNOLOGIES FOR OTT VIDEO STREAMING TECHNOLOGY

$
0
0
Push Mobile Managing Director, Freddie Manento (L) exchange documents contract with Apalya Technologies International Business, Rishabh Gunjal, Apalya to provide best-in-class mobile video solutions across East and Central Africa. 

Dar es Salaam. Tanzania’s leading interactive mobile communications technology provider, Push Mobile has partnered with Apalya Technologies, South Asia’s leading technology platform provider to enhance mobile video and live TV streaming experience in Tanzania and into other markets across the region.

Freddie Manento, Push Mobile Managing Director, speaking at the signing ceremony held at Push Mobile offices said the partnership serves to cement Push’s vision and mission of being the mobile communications market leader in East Africa and the international sphere and a provider of high quality products and services.

 “Our partnership with Apalya Technologies is in line with our strategy to expand our video and Live TV streaming technology to new markets around the region and they are the right technology partners to take us there.” said Manento.

On his part Rishabh Gunjal, Apalya Technologies’ AVP – International Business said “Apalya Technologies is excited to partner with Push Mobile in their drive to provide best-in-class mobile video solutions across East and Central Africa. Apalya’s leadership across the emerging markets of India and South Asia as well as their 8 year track record in working with some of the biggest global telecom brands will be a great leverage in helping Push Mobile serve the growing mobile market in this region.”

He said that the firm partnership promises the best platform in terms of technology and content offering providing an opportunity to mobile network operators to monetize their mobile data network with best possible consumer experience.

Television stations and production houses can use this platform to create new revenue stream in digital media space. Consumers will also have access to best of local and international content at an affordable price across all video streaming supported devices like feature phones, smart phones, tablets and PCs. 

Mahakama ya Tanzania imedhamiria kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza akiwaeleza waandishi wa (hawapo pichani) mikakati iliyoweka iliyowekwa na Mahakama ya Tanzania ili kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote na kwa wakati kwa vitendo, kwa kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa mahakamani, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi. Mary Gwera. Picha na Hassan Silayo-maelezo

Afrika ni salama pamoja na kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola – Rais Kikwete

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilkisha nchi zao nchini China wakati alipokutana nao jijini Beijing China leo asubuhi.Raius Kikwete yupo nchini China kwa ziara ya kiserikali.(picha na Freddy Maro)

Maadhimisho Ya Miaka 70 ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Kuanza Kesho Mjini Arusha

$
0
0
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Saba wa wadau wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, yamekamilika ambapo mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 700 toka nchini na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Arusha, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Eliud Sanga, amesema maadalizi yote ya mkutano huo, wenye kauli mbiu ya "Maadhimisho ya Miaka 70 ya Ukuaji na Huduma Bora, LAPF", yamekamilika ambapo utakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF.

Bwana Sanga amesema Mfuko wa LAPF  ndio mfuko unaoongoza sii tuu kwa kutoa mafao bora, bali pia ndio mfuko unaoongoza kwa kuwa na afya bora kabisa ambapo kwa sasa una rasilimali zenye thamani ya shilingi bilioni 700, LAPF ndio mfuko unaoongoza kukua kwa kasi zaidi ambapo unakuwa kwa asilimia 21 kwa mwaka!.

Ameendelea kutoa sifa za LAPF kuwa ni pamoja na kuwa ndio mfuko unaolipa kwa haraka zaidi, ambapo mstafuu kama anastaafu kesho, LAPF wao wanalipa jana!.

Bwana Sanga hakuishia hapo, amesema LAPF ndio mfuko unaoongoza kwa utunzani wa mahesabu kati ya mifuko yote kwa mujibu wa NBAA, na ndio mfuko unaokuwa kwa kasi zaidi kwa mujibu wa SSRA!.

Mkutano huo, utafunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Hawa Ghasia, na Kufungwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Gaudensia Kabaka.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Eliud Sanga, akizungumza na Waandishi wa habari mjini Arusha, kuhusu Mkutano wa 7 wa Wadau wa LAPF, unaokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF. Kushoto ni Meneja Masoko wa LAPF, James Mlowe, kushoto kabisa ni Meneja Takwimu, Tathmini na Hadhari wa LAPFBw. Aboubakar Ndwata.Kulia ni Meneja wa LAPF Kanda ya Kaskazini, Rajabu Kinande.
Meneja Kanda ya Dar es Salaam wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Amina Kassim akizungumza na Waandishi wa habari mjini Arusha, kuhusu Mkutano wa 7 wa Wadau wa LAPF, unaokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF. Kushoto ni Meneja Masoko wa LAPF, James Mlowe na Kulia ni Meneja wa LAPF Kanda ya Kaskazini. Rajabu Kinande.
Meneja Kanda ya Kaskazini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Rajabu Kinande, akizungumza na Waandishi wa habari mjini Arusha, kuhusu Mkutano wa 7 wa Wadau wa LAPF, unaokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Pensheni wa LAPF. Kushoto ni Meneja LAPF Kanda ya Dar es Salaam, Amina Kassim, na Meneja Masoko wa LAPF, James Mlowe

Tahariri ya Globu ya Jamii: Sakata la Miss Tanzania 2014 Sitti Abbasi Mtemvu lipatiwe muarobani

$
0
0
 Jumamosi   Oktoba 11, 2014 fainali za Miss Tanzania  zilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. Umati mkubwa wa wapenzi wa urembo waliokusanyika hapo ulishuhudia Bi. Sitti Abbas Mtemvu akinyakua taji hilo, akiwashinda warembo wengine 29 na kuwa malikia wa 20 wa urembo nchini.
Sitti, aliyeanza mbio za kuwania taji hilo katika awamu ya vitongoji kwa kujisafishia njia kwa  kuibuka Miss Chang’ombe na baadaye Miss Temeke,  alifuatiwa na  Lillian Kamazima aliyekuwa mshindi wa pili na mshindi wa tatu alikuwa  Jihhan Dimachk.

Kama ilivyo ada, kwenye ushindani pana kushinda na kushindwa. Vile vile penye kushinda ama kushindwa kuna furaha na  kuna manung’uniko, kwa pande husika wa  hayo.  Kwa ushindi wa Sitti yote hayo yalitokea kwa pamoja kama ilivyokuwa katika fainali kadhaa zilkizopita.

Historia inasema kwamba kila palipofanyika mashindano ya Miss Tanzania, kumekuwepo na aina Fulani ya tafrani. Tokea mashindano ya kwanza yaliyofanyika mwaka 1967,  ambapo mrembo Theresa Shayo alishinda, mashindano yakapigwa marufuku kwa kuonekana ni kinyume cha maadili ya Mtanzania.

Mwaka 1994 wadau kadhaa wakajitokeza na kufufua mashindano hayo. Bi Aina Maeda akaibuka kuwa mshindi  wa kwanza, wa pili akiwa Lucy Ngongoseke na watatu akawa  Dotto Abuu.  Zogo likaibuka hapo kuwa  Aina kapendelewa maana hakuwa akiishi nchini, na kwamba aliingia mashindanoni moja kwa moja akitokea Afrika mashariki.

Emily Adolph wa Dodoma alishinda taji hilo mwaka 1995, na zogo lake likawa ameshiriki kinyume na matarajio kwani alikuwa bado ni mwanafunzi.  Mwaka uliofuatia, yaani mwaka 1996, Shose Sinare akateuliwa kuwa Malkia wa Urembo Tanzania. Huyu alikuwa na vigezo vyote, ikiwa ni pamoja na sura na umbo zuri na msomi. Tatizo kwake lilikuwa ni kimo. Wadau wakalalamika kuwa hakustahili kuwakilisha nchi kwa kuwa mfupi.

Mambo hayakuishia hapo. Mwaka 1997 mshindi alikuwa Saida Kessy kutoka Arusha,  ambaye hakulalamikiwa sana, kama ilivyokuwa kwa Miss Tanzania wa miaka ya 1998 (Basila Mwanukuzi), 1999 (Hoyce Temu), 2000 (Jaquiline Ntuyabaliwe),  2001 (Happiness Magese), na mwaka 2002 (Angela Damas).

Zogo liliibuka  Mwaka 2003 wakati mrembo Sylvia Bahame alipovaa taji hilo, malalamiko yakiwa kwamba pamoja na kuwa mzuri kwa sura, lakini maumbile yake manene pamoja na meno yenye mwanya vilizua tafrani. Mrembo Faraja Kotta alifuatia mwaka 2004, ambapo hakukuwa na malalamiko sana.

Mwaka 2005 Miss Tanzania Nancy sumari ndiye pekee ambaye alipokelewa vyema na karibu kila mtu, hasa hasa alipoweza kushika nafasi ya tano kwenye mashindano ya dunia. Rekodi ambayo haijavunjwa na yeyote hadi dakika hii. Nancy anaendelea kuwa mfano wa kuigwa hadi leo hii ambapo hana tone la ‘skendo’ ya aina yoyote maishani mwake – kabla na hata baada ya U-Miss. 
Mshindi wa mwaka 2006 alikuwa Wema Sepetu, ambaye kibinfasi hakuwahi kulalamikiwa sana, akafuatiwa na  Richa Adhia mwaka 2007. Huyu alisumbuka sana kutokana na malalamiko kuwa alikuwa ni Mhindi, jambo ambalo wapinga ubaguzi wa rangi waliweza kupigania na kushinda. Ila zogo lake halikuwa dogo…

Nasreen Karim alivaa taji mwaka 2008, na akamaliza muda wake bila zogo, akifuatiwa na Miriam Gerald mwaka 2009, kabla ya Genevive Emmanuel Mpangala kuvaa taji mwaka 2010, na kubahatika kumaliza muda wake bila makelele.  Mwaka 2011 aliibuka Salha Israel, akafuatiwa na Lisa Jensen mwaka , ambaye alimpasia taji Brigit Alfred mwaka 2013. Wote walikuwa hawana matatizo.

Tatizo limeibuka mwaka huu wa 2014 katika umbo la  mshindi wake Sitti Abbas  Mtemvu, ambaye kwa wiki ya pili sasa kila upenyo wa habari umeelezea wasiwasi kuhusu umri wake, na huko mitandaoni nakala za leseni ya udereva na hata hati ya kusafiria vimesambazwa kudai kuwa ana umri wa miaka 25. Wengine walibandika hata picha za mrembo huyo akiwa amebeba mtoto, waliyedai kuwa ni wake – ambavyo ni kinyume cha kanuni za kamati ya Miss Tanzania.

Jana, Kamati ya Miss Tanzania ikiwa chini ya Mwenyekiti wake Anko Hashim Lundenga, pamoja na Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas  Mtemvu,  na mama yake mzazi, walikutana na wanahabari kufafanua utata huo wa umri na madai ya kuwa mrembo huyo hana au ana mtoto. Vyote walikanusha na kutoa cheti cha kuzaliwa kinachoonesha kuwa kazaliwa Mei 31, 1991.

Mkutano huo na wanahabari haukuweza kumaliza kiu ya wadau na wadadisi, na badala yake ukawa kama umechochea kuni katika sakata zima la umri wa Sitti. Wengi wakidai kwamba mchanganuo wa umri wake pamoja na masuala ya ,miaka ki- elimu vina wasiwasi, hivyo makelele yanaendelea.

Hatuna nia ya kujiweka upande wowote katika hilo. Tahariri hii ina kusudio la kutafuta suluhu katika swala hilo, ili kulinda heshima si ya shindano hilo pekee bali pia jina la Tanzania katika tasnia hiyo na nyinginezo, maana hilo linasambaa hadi kwenye tasnia zote zinazoshirikisha vijana, utamaduni na michezo.

Ushauri wetu ni  kwamba vyombo vyote husika,  chini ya Wizara ya Habari, vijana , utamaduni na michezo, visiache hili liendelee kuwa gumzo mitaani na mitandaoni na kuendelea kuliweka rehani jina la Tanzania Kimataifa. Hatua za makusudi na haraka zichukuliwe ili kieleweke.

Globu ya Jamii inashauri sakata hili lipatiwe muarobaini haraka sana. Iundwe tume huru itayoshirikisha wataalami na wadau wanaohusiana na tasnia hiyo pamoja  vyombo vya  dola na kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Miss Tanzania ni mwakilishi wa wananchi wote wa Tanzania na si wa kundi la watu fulani.  Hivyo muafaka wa jambo hili unahitajika siku tatu zilizopita.

Endapo ukweli utapatikana na kudhihirika kuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Abbasi  Mtemvu hana hatia, basi aombwe radhi kistaarabu nasi sote tujipange nyuma yake na kumsaidia katika maandalizi yake ili akafanye vyema huko kwenye Miss World.

Na endapo atapatikana na hatia, inabidi awajibike yeye mwenyewe kwa kuvua taji hilo. Hapo kamati ya Miss Tanzania nayo itabidi iombe radhi Watanzania kwa kizaazaa hiki. Hili pia liwe kama kengele ya kuamsha, ambapo huko mbeleni yanayojazwa kwenye fumo za washiriki lazima yahakikiwe na wataalamu husika kwa kila jambo.

Wakatabahu

Ankal






WANA WA NGWASUMA WAIBUKA NA ALBAMU MPYA "CHUKI YA NINI" KESHO UKUMBI WA ARCADE

happy diwali wishes from exim bank

Article 22

Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika Mahojiano na Mtangazaji Mahiri wa Kipindi Cha Dira ya Dunia BBC Salim Kikeke jijini London


HYUNDAI presents Heavy Construction Equipment at Oil & Gas Conference.

$
0
0
 
HYUNDAI Sales Manager, Mr. Alen Nkya (left) clarifies a point to the Deputy Minister for Energy and Minerals of Tanzania, Hon. Stephen Masele and other delegates regarding Construction Equipment and Industrial Vehicles used in oil and gas projects during International Oil & Gas Conference held in Dar es Salaam.

CRDB, THE BANK THAT LISTENS, WISHES YOU A HAPPY DIWALI DAY

mark your calender and get set for 1st annual gala dinner in houston

FIRST AFRICAN MOUNTAINS REGIONAL FORUM CALLS FOR MAINSTREAMING OF MOUNTAINS IN THE DEVELOPMENT AGENDA

$
0
0
The first African Mountains Regional Forum has started at Ngurdoto Mountain Lodge in Arusha, Tanzania. The three-day forum to take place from October 22-24 is to provide an opportunity for different sustainable mountain development stakeholders to enhance understanding of common conservation and development issues in the region.

The forum is organized by the Albertine Rift Conservation Society (ARCOS) and the Africa Mountain Partnership Champions Committee (AMPCC) in partnership with the East African Community (EAC), United Nations Environment Programme (UNEP), and other partners. Participants from African government institutions, academia, civil society, media and the private sector are in attendance.

Dr. Sam Kanyamibwa, the executive director of ARCOS, called the meeting “a celebration of the fragile mountain ecosystem.” 

Hon. Magessa Mulogo, the Arusha Regional Commissioner in a statement delivered by the District Commissioner Arumeru District, Mr. Deus Munasa, said Tanzania is well endowed with mid-range mountains including Mt. Kilimanjaro, Africa’s highest mountain, which attracts more than 35,000 climbers a year. 

MH. PINDA AKUTANA NA WAZIRI WA BIASHARA NA UWEKEZAJI WA UINGEREZA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Nchi Biashara na Uwekezaji wa Uingereza, Lord Livingstone mjini London Oktoba 22a, 2014. Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini Dianna Meryrose.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Nchi, Biashara ya Uwekezaji wa Uingereza, Lord Livingstone mjini London, Oktoba 22, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images