Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

OFISI YA WAZIRI MKUU YAFANYA TATHMINI YA HALI YA CHAKULA NA LISHE MKOANI SIMIYU

$
0
0
Bw. Clement Ngosha wa kijijini Kabita Wilayani Busega, Simiyu, akitumia mbegu za mahindi kueleza hali ya chakula kijijini hapo kwa wataalam wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Oktoba, 2014.
Mtaalam wa Usalama wa chakula kutoka Wizara ya kilimo, chakula na Ushirika, Bi. Tatu Kayumbu akiihoji moja ya kaya kijijini Mwamanyili,Wilayani Busega, Simiyu wakati wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu kijijini hapo, Oktoba, 2014.
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Kabita wilayani Busega, Simiyu wakifuatilia mkutano wa kijiji uliokuwa ukijadili hali ya Chakula na Lishe kijijini hapo wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ilipofika kijijini hapo kufanya tathmini ya masuala hayo Oktoba, 2014.

Na. Ibrahim Hamidu

Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Uratibu wa maafa inafanya Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe Mkoani Simiyu katika Wilaya zake zote ambazo ni; Halmashauri za Wilaya za Bariadi, Itilima, Maswa ,Bariadi Meatu na Busega.

Akiongea mkoani Simiyu kiongozi wa Wataalam wa tathmini ambaye pia ni mratibu wa shughuli za maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Edgar Senga alibainisha kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imefikia maamuzi hayo ya kufanya tathmini mkoani Simiyu baada ya mkoa huo kutuma maombi katika Ofisi hiyo kuwa wana upungufu wa chakula.

“ Ofisi ya mkoa ya Simiyu ilileta maombi kwa ofisi ya Waziri Mkuu kuwa wanaoupungufu wa chakula takribani tani 48,975, kwa kuwa Ofisi yetu ndio yenye dhamana ya kuratibu misaada ya chakula hivyo haikuwanabudi kufanya tathmini ya haraka ili kubaini hali ya chakula ya mkoa huu ili kuweza kuamua namna ya kushughulikia maombi yao ya msaada wa chakula” alisema Senga.


TANZANIA YAJIVUNIA KUFIKIA MALENGO YA MILENIA KATIKA AFYA, ELIMU

$
0
0
DSC_0564
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya Umoja wa Mataifa inayotarajiwa kuanza kuadhimishwa Ijumaa wiki hii (kushoto) ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

Na Mwandishi Wetu
KATIBU MKUU wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule amesema serikali ya Tanzania imefikia kwa kiwango kikubwa baadhi ya malengo ya milenia ya afya na elimu. MOblog Tanzania inaripoti

Akizungumza katika mahojiano maalumu na MOblog Tanzania ofisini kwake jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mkutano na wanahabari juu ya wiki ya Umoja wa Mataifa inayotarajiwa kuanza Ijumaa wiki hii, Haule amesema Tanzania imeyafikia kwa kiwango kikubwa malengo ya milenia katika afya na elimu.

UK Trade & Investment London/South East Trade Mission to Tanzania

$
0
0
14 UK companies cutting across various sectors e.g. Education and Training, Security, Consultancy, Healthcare amongst others are hoping to penetrate new trade opportunities within Tanzania by taking part in UKTI London and South East trade mission to Tanzania between October 22nd-24th 2014

This is the first, independent visit by UKTI London and South East to Tanzania and East Africa.

Tanzania is fast emerging as a thriving commercial entity with a GDP growth rate of over 7% year upon year. The major city of Dar es Salaam where we will be staying is the centre of most government activity as well as being the major commercial centre with its own deep water port with trading links to the landlocked countries of Malawi, Zambia, Democratic Republic of Congo, Burundi, Rwanda and Uganda.


Tanzania not only has some of the best wildlife in the world but also huge natural resources ranging from gemstones to natural gas. As such, it is fast becoming the regional hub for a number of multinational corporations. This will be an exciting opportunity for UK businesses to see what they can bring to the country.


As part of the programme which is being organised by UKTI in Tanzania, the delegates will have a first-hand opportunity to meet and speak with local trade associations and their members e.g. the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) and the Tanzania National Chamber of Commerce and Industry (TNCCI) and the newly set-up British Chamber of Commerce Tanzania (BCCT).

 They will also have a chance to speak directly with business at a Business to Business event scheduled for Thursday, 23rdOctober at the Serena Hotel from 1.00 to 4.00pm. We believe this will create a great opportunity for the visiting companies to meet and discuss business directly with business.     

David Billingsby, UKTI International Trade Adviser, who will lead the London delegation, said:

“Having worked in Tanzania before, I know the excellence of the reception these British companies will receive. I am certain that the mission will be successful and the delegates will be saying Asante           sana!”

The delegation will include the following companies who will then relocate to Kenya for 26th-30th October:

Edward Munyard - Eagle Scientific
Carl Gibbard - Concept Smoke Screen Ltd          
Mike Thompson - tph Machine Tools     
Sudhir Patel - Velmo International         
Christine Meade - GSVO    
Hanaa Chattun - Lacaze     
Adam Hersi - Haad Logistics Ltd  
Chris Stephenson & Dan Olal - McKinney Rogers
Peter Charnaud & William Charnaud - Scott & Sargeant Woodworking Machinery           
Umair Munir - MAP IT Services     
Robert Magembe - InterVAS Limited UK 
William Rhys-Jones - Cobham Tactical Communications & Surveillance    
Joy Okwuadigbo - Highbury College        
Nemish K Mehta - e-tel (uk) ltd 

WORKSHOP ON INTERNET SECURITY LAUNCHED AT COSTECH

$
0
0
On 20th October 2014, The Tanzanian Commission for Science and Technology (COSTECH) in collaboration with The Islamic Educational, Scientific and Cultural Organization (ISESCO), the Commission on Science and Technology for Sustainable Development in the South (COMSATS), the Inter Islamic Network on Information Technology (INIT) and the COMSATS Institute of Information Technology (CIIT), launched the internet security workshop. The five days international workshop themed “Internet Security: Enhancing Information Exchange Safeguards” intends to provide a forum to the young scientists/researchers, practitioners, academicians, system administrators, systems programmers and students from the developing countries to learn about the latest advancements in the field of internet security. The workshop has brought together participants from Uganda, Nigeria, Senegal, Kenya, Pakistan and Tanzania.
Permanent Secretary Ministry of Communication, Science and Technology Professor Patrick Makungu giving his speech at the launching ceremony

During the event, Professor Patrick Makungu, Permanent secretary Ministry of Communication Science and Technology said that as the information technology sector is growing, the threats to cyber security are increasing. “This is an important workshop since it focus on training of the trainers’ he added “Lack of technical know-how, lack of laws and legislations specific to cyber crime, coupled with inefficiency digital literacy among the public at large has made efforts to curb online piracy suffer setbacks.
Dr. Aicha Bammoun from The Islamic Educational, Scientific and Cultural Organization (ISESCO) giving a speech during the event.

Meanwhile, Mr. Muhammad Afiq-ur-Rehman the senior program officer of INIT said that data and applications on networks have to be secured to the optimum level.

“The use of computer has become a major element in government and business activities, tampering with these networks can have serious consequences for agencies firms and individuals,”he said.

Tajamul Hussain, COMSATS program advisor said that the workshop will allow IT professionals to collectively address relevant issues and challenges related to information and internet security. He added that COMSATS is committed to develop and strengthen linkages among the countries of the south for exchange of resources, technology and knowledge.

Dr Aicha Bammoun from ISESCO said that the training is expected to enhance sensitize on the problems of cyber crime, encourage the preparation and adoption of harmonised framework of cyber security and legal and regulatory environment as to reduce threats in cyber security.

On his part, Dr Hassan Mshinda, COSTECH Director General said that there is a great need of IT professional to be equipped skills on cyber security in Tanzania to ensure cyber security.

This is the fourth internet security workshop the first three events of this series were held in Syria (2011), Jordan (2012) and Tunisia (2013) respectively.

Tanzania is reported to have so far lost nearly 10 billion shilling (equivalent to USD $ 6 million) through cyber related fraud crimes, involving mostly card skimming and ATM thefts. But we are not resting. As of now, there are more than 300 cyber crime cases being investigated, some of which are about to be benched in courts of law, according to the records from the Ministry of Home Affairs.
Participants of the internet security workshop in group photo with the Permanent Secretary Ministry of Communication, Science and Technology, Professor Patrick Makungu

TANZANIA WOMEN ASSOCIATION UK (TAWA UK) INVESTMENT MEETING INVITATION.

$
0
0
Mrs Joyce Kallaghe wife of the Tanzania High Commissioner UK ( Mama Balozi UK) and Tanzania Women's Association UK  ( TAWA UK ) Invites all women  who are interested in exploring Investment and Business opportunities in Tanzania, at an Investment Information meeting which is to be held at:

Tanzania High Commission 
Tanzania House
3 Stratford place
London W1C 1AS
Tel: 0207 569 1470

Date: Wednesday 22nd October 2014
Time: 16:00hrs

GUEST OF HONOUR: Mama Tunu Pinda , Wife of the Prime Minister.of Tanzania.
GUEST SPEAKER : Mrs Anna Matinde - Board Director for Tanzania Private Sector Foundation. 
WE URGE ALL TANZANIA WOMEN IN UK TO ATTEND THIS INFORMATIVE AND NEVER TO MISS OPPORTUNITY.

More Infornation Please Contact:
Mariam Kilumanga- +44 7803706243.
Mariam Mungula: +44 7770 910901

ASANTENI NA KARIBUNI WOTE.

Update ya msiba wa MAREHEMU REHEMA RAMADHANI BARAKA, mdogo wake mwenyekiti wa ASET BARAKA MSIILWA

$
0
0

Ifuatayo ni update ya msiba wa mdogo wake Mwenyekiti wa African Stars Entertainment (ASET) Baraka Msiilwa, Marehemu Furaha Ramadhani Baraka, kilichotokea wikiendi iliyopita huko Ubelgiji.


Taarifa ni kwamba mwili wa Marehemu mdogo wetu Furaha unaondoka Brussels kesho  usiku kwenda Zurich. Utalala Zuruch na kusafirishwa Jumatano Asubuhi kwa ndege ya shirika la Swiss Air, na unatarajiwa kuwasili Dar es salaam siku  hiyo hiyo ya Jumatano mnamo saa mbili usiku

Mazishi yamepangwa kufanyika siku ya Alhamisi  milango ya Alasir katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya kuuswaliwa katika Mskiti wa Maamur Upanga. Msiba upo nyumbani kwa marehemu mama yetu Kinondoni Hananasif/ Mkwajuni hapa Dar es salaam. 

Habari hizi ziwafikie ndugu, jamaa, jirani na marafiki popote pale walipo. Tuzidi kumuomba Mola aiweke roho ya mareheme mahala pema peponi

 - AMIN

Lundenga alizungumzia sakata la umri wa Miss Tanzania 2014

$
0
0
 Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya sakata la umri halali wa Mrembo alietwaa taji hilo Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu (kushoto),katika mkutano huo Lundenga alitolea ufafanuzi swala la umri wa Mrembo huyo kulingana na vilelezo alivyopewa na mrembo huyo wakati akijiunga na mashindano hayo 

"Katika mashindano ya yetu,Washiriki wote hujaza fomu maalum zilizoandaliwa na Kamati ya Miss Tanzania,katika fomu alizojaza mrembo wa Miss Tanzania 2014 Sitty Abbas Mtemvu amejaza tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni Mei 31,1991 na hivyo kuwa ni sahihi kushiriki mashindano yetu" Alisema Lundenga mbele ya wanahabari hao.

Lundenga aliendelea kusema kuwa Mashindano ya Miss Tanzania hayaruhusu mshiriki yeyote mwenye mtoto kushiriki, hivyo katika swala la Sitti Mtemvu kuwa ana mtoto, hilo halina ukweli wowote bali ni uvumi tu wa kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mrembo huyo kuonekana akiwa katika picha na mtoto alieomba kupiga nae.
 Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akionyesha nakala ya cheti cha kuzaliwa cha Mrembo Sitti Mtemvu alicholetewa na wazazi wake.
 Nakala halisi ya Cheti hicho inayoonyesha Mrembo huyo amezaliwa Mei 31,1991.
Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akizungumza machache na waandishi wa habari.

WENYE SILAHA ZA NYUKILIA WATUHAKIKISHIE USALAMA -TANZANIA

$
0
0
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Ramadhan Mwinyi akichangia majadiliano kuhusu ajenda ya uthibiti wa silaha za nyukilia hapo siku ya jumanne. Akizungumza msimamo wa Tanzania kuhusu silaha hizo, Balozi Mwinyi amezitaka nchi zinazomiliki silaha hizo kuonyesha utashi wa kisiasa wa kuzipunguza na kuzidhibiti ili zisisambae kiholela lakini pia waihakikishie dunia usalama wake.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wakifuatilia majadiliano kuhusu upunguzaji wa silaha za nyukilia ambapo wazungumzaji wengi pamoja na Tanzania walisisitiza haja na umuhimu wa kuwa na maeneo huru yasiyo na silaha za nyukilia kwa usalama wa dun dunia na wakatoa wito kwa Shirika linalohusika na masuala ya Nguvu za Nyukilia kuhakikisha kwamba kila nchi inakuwa na haki ya kupata elimu na teknolojia inayohusiana na nguvu za nyukilia bila ubaguzi au upendeleo.

CHADEMA NACHINGWEA WAKIKIMBIA CHAMA CHAO NA KUJIUNGA NA CCM, WAZIRI CHIKAWE APOKEA KADI ZAO NA KUWAKARIBISHA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akizionesha kadi za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Kata ya Lionja, Wilayani Nachingwea, Hashimu Halifa (kulia). Waliorudisha kadi hizo na kujiunga na CCM ni Lusia Mohammed, Abdu Ngawina na Mohammed Kindamba. Waziri Chikawe ambaye yupo katika ziara ya kikazi jimboni kwake aliwaomba Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo kuhakikisha chama kinaimarishwa zaidi na kuwakaribisha wanachama wote wanaotoka vyama vingine ili wajiunge na CCM.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata ya Lionja, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe ambaye yupo katika ziara ya kikazi katika Jimbo lake la Nachingwea aliwaomba wajumbe hao kuhakikisha chama kinaimarishwa zaidi na kuwakaribisha wanachama wote wanaotoka vyama vingine ili wajiunge na CCM.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kulia) akizungumza na Mjumbe wa CCM Kata ya Lionja ambaye ni mlemavu wa miguu, Hassan Chingwale baada ya kumaliza kikao chake na Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe yupo katika ziara ya kikazi jimboni mwake, aliwaomba wajumbe hao kuhakikisha chama kinaimarishwa zaidi na kuwakaribisha wanachama wote wanaotoka vyama vingine ili wajiunge na CCM. Picha na zote na Felix Mwagara.

Tumieni namba za simu kudhibiti uendeshaji holela - UDA

$
0
0

Miongoni mwa mabasi ya shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) yanayofanyakazi katika maeneo mbali mbali jijini Dar es Salaam. Na kila basi lina namba za simu ili kurahisisha abiria na watumiaji wa mabasi hayo kutoa maoni juu huduma zitolewazo na mabasi ya shirika hilo.


Abiria na watumiaji wengine wa barabara Dar es Salaam wameombwa kusaidia katika kudhibiti uendeshaji holela na tabia zisizokubalika zinazofanywa na baadhi ya madereva wa mabasi ya abiria na makondakta wa Dar es Salaam kupitia namba za simu zilizochapishwa katika mabasi yote ya Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA).


Taarifa iliyotolewa na uongozi wa UDA jana na kusainiwa na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Bw.  George Maziku, imesema utumiaji wa namba hizo utaisaidia pia kampuni kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja wake. 


 “Tunawakumbusha wateja wetu wapendwa pamoja na watumiaji wengine wa barabara kuripoti uzembe wowote au utovu wa nidhamu utakaofanywa na madereva na makondakta wa UDA ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao ambazo zitasaidia kuboresha huduma zetu kwa jamii kwa ujumla.”


“Mbali na kuboresha utoaji wa huduma zetu, UDA inalenga kuwa mfano wa kuigwa kwa mabasi mengine ya abiria nchini katika uzingatiaji wa sheria, utoaji wa huduma nzuri kwa wateja na kuwa kichocheo cha kupunguza  foleni katikati ya jiji la Dar es Salaam. Hii itakuja pale ambapo wamiliki wa magari binafsi watakapoanza kutumia usafiri wa umma wenye gharama nafuu,” alisema.


Bw. Maziku alisisitiza kuwa uongozi wa UDA utachukulia kwa uzito mkubwa na kuyafanyia kazi maoni yote yakayokuwa yakitolewa kupitia namba hizo zilizotolewa ili kuondokana na dhana potofu iliyopo kuwa wamiliki na waendeshaji wa kampuni za magari ya abiria ni watu ambao hawajaelimika.


Alisema kuwa, mbali na uwepo wa namba hizo za simu, UDA itaendelea na utekelezaji wa utaratibu wake wa kutuma waratibu kupanda mabasi ya kampuni hiyo na kuripoti juu ya utendaji kazi wa madereva na makondakta wa mabasi hayo.


“UDA imelenga kuhakikisha kila mteja anapata huduma bora ambazo zinakidhi matarajio yao na wakati huohuo, zikiwa zinaendana na matakwa elekezi ya usalama barabarani,” aliongeza.


UDA ina zaidi ya mabasi 400 yanayofanya kazi, hii inaifanya kuwa kampuni kubwa zaidi ya magari ya abiria Tanzania. 

Chuo Kikuu Ardhi kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka na taka ngumu

$
0
0
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mpango wa chuo hicho wa kuendelea na jitihada za kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka na tanga ngumu ikiwemo ujengaji wa miundombinu ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji na gesi asili ya kupikia, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa chuo hicho Prof. Gabriel Kassenga.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi ambaye pia ndiye mtaalam wa teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka (waste treatment facilities) Dkt. Shabaan Mgana Akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna Teknolojia hiyo ya kubadili taka ngumu na maji taka inavyotumika na kuwasaidia wananchi walioonesha nia ya kuitumia ikiwamo kupata mboji kwa ajili ya mazao, mimea pamoja na kupata gesi asili ya kupikia, ambapo mpaka sasa kiasi cha nyumba 100 za awali katika mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na nyumba mia moja katika Chuo Kikuu cha Ardhi zimeshaunganishwa katika Mradi huo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Idrissa Mshoro.
Mkemia Mkuu wa Kiwanda cha Mansoor Daya Chemicals Bw. Benedict Mtenga Akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) jinsi wanavyoendelea kunufaika na teknolojia hiyo ya kibiolojia ikiwemo kutumika kusafisha maji taka yanayozalishwa na kiwanda hicho na kuepusha uharibifu wa mazingira,wakati wa ziara iliyofanywa katika kiwanda hicho ili kuona jinsi teknolojia inavyofanya kazi.
Miundombinu ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji zilizojengwa katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Ardhi, mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na katika kiwanda cha Madawa ya Binadamu cha Mansoor Daya Chemicals.

Article 20

CONSCIOUS LEADERSHIP SUMMIT 2014

Zuriel Oduwole Steals The Show at Africas Biggest Movie Awards Night - 2014 Nollywood Movies Awards

$
0
0
It was billed as the Centenary Celebrations edition of the 2014 Nollywood Movies Awards night at the prestigious Intercontinental Hotel in Victoria Island - Lagos last Saturday. The actors, producers, directors, and movie faithful filed past the "Red Carpet" into the events main auditorium. However, the star attraction right from the Red Carpet was a new face to Nigeria's movie making industry.

Zuriel Oduwole, at 12 years old was a fresh, young, bright, and eloquent attraction, from the moment she arrived early for the Red Carpet. A Special guest of the events organizers in recognition of her award winning documentary work in 2013 on the 1963 OAU Formation, and her current documentary in production this year, she dazzled the cameras, wowed the anchors, and the whispers grew among the crowd with the recurring question "Who is that Girl". She was invited by many TV networks to speak to their audience, and inspire the children who would watch the feed.

Award night host 'Denrele' was quick to add that he was a big fan of Zuriel, having heard her on the TITI radio show a couple of days earlier, talking about her current work with children on basic hand hygiene. Half way into the Award show, she was invited on stage to give her version of the event, and introduce the MC of the night in her own words.

Zuriel is currently finishing her third documentary due at the end of 2014, and it focuses on a brighter Africa, starting with Nigeria, as part of her "Rebranding Africa" initiative.
 Zuriel Oduwole. 

KUIMARIKA KWA MFUMO WA KUDHIBITI FEDHA HARAMU

$
0
0


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA FEDHA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                   
KUIMARIKA KWA MFUMO WA KUDHIBITI FEDHA HARAMU

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kudhibiti Fedha Haramu (The Eastern and Southern Africa Anti - Money Laundering Group (ESAAMLG)) ulioanzishwa mwaka 1999,  kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja ya kudhibiti fedha haramu na ufadhili wa ugaidi kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika.  Baada ya kuanzishwa kwa umoja huo, Tanzania ilitunga Sheria za Kudhibiti Fedha Haramu mwaka 2006. 

Umoja wa ESAAMLG umejiwekea utaratibu wa kufanya tathmini ya mifumo yao ya kudhibiti fedha haramu na ufadhili wa ugaidi kwa kuzingatia mazingira ya nchi wanachama na viwango vya kimataifa vilivyowekwa na kikosi kazi cha kimataifa kijulikanacho kama “The Financial Action Task Force “(FATF)”.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilifanyiwa tathmini ya mfumo wake wa kudhibiti fedha haramu na ufadhili wa ugaidi mwaka 2009.  Tathmini hii ilihusu maeneo ya kisheria, sera na kitaasisi.  Aidha, mkutano wa FATF uliofanyika mwezi Juni, 2014 mjini Paris - Ufaransa, ulijadili hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Tanzania na kuridhika kuwa hatua hizo ni kubwa na endelevu  na kuwa ipo dhamira ya hali ya juu ya kisiasa katika kuimarisha mfumo wa kudhibiti fedha haramu na ufadhili wa ugaidi nchini.  

Pamoja na hatua hizi muhimu za kuimarisha mfumo wa kudhibiti fedha haramu na uhalifu kwa ujumla, Kitengo chetu cha Kudhibiti Fedha Haramu kimekua mwanachama wa umoja wa vitengo vya kudhibiti fedha haramu duniani unaojulikana kama “Egmont Group of Financial Intelligence Units”. Kujiunga na umoja huu kutakiwezesha kitengo cha kudhibiti Fedha Haramu  Tanzania kuimarisha ushirikiano na taasisi zinazoshughulikia udhibiti wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi duniani, kurahisisha kupata taarifa za kiintelijensia zinazotakiwa katika utendaji wake wa kazi na kuongeza weledi na tija ya utendaji kazi kupitia mafunzo maalum na ubadilishanaji utaalam baina ya vitengo vya udhibiti wa fedha haramu. 

Kutokana na hatua zote hizi, tunapenda kuujulisha umma kuwa, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeingizwa katika orodha ya nchi zenye mifumo imara ya Kudhibiti Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi na hivyo tutaendelea kuimarisha na kusimamia mfumo wetu kwa manufaa na usalama wa mali za wananchi wetu.


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila fedha haramu wala uhalifu inawezekana!!
Taarifa hii imetolewa na

Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha



11468 Dar Es Salaam

Waziri Kawambwa afanya ziara Mkoani Morogoro

$
0
0
Picha na Habari Na John Nditi, Morogoro

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, amefanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Morogoro iliyaonza  Oktoba 20 na kufikia tamati  22, 2014

Katika ziara hiyo ya kikazi, waziri baada ya kupkea taarifa ya hali ya elimu mkoa, alitembelea Shule ya  Kilakala Sekondari ya wasichana wa vipaji maalumu kwa ajili ya kupata taarifa za elimu na kukagua miundombinu ya shule.

Waziri huyo mwenye dhamana na sekta ya elimu, pia alikitembelea Chuo cha Ualimu Morogoro , ambapo nako alipokea taarifa ya Chuo na kukagua miundombinu ya Chuo hicho.

Ziara ya Waziri huyo imefikisha pia katika wilaya ya Mvomero ,ambapo alitembelea Shule ya Sekondari ya Kata Kipera ambayo ilipewa fedha na serikali za ujenzi wa nyumba ya mwalimu na maabara ambazo zimekamilishwa.

Mbali na Shule ya Kipera, Waziri huyo aliitembelea Shule kongwe la Sekondari Mzumbe , ambapo alipatiwa taarifa na kukagua miundombinu ya shule , pia aliitembelea Shule ya sekondari Mvomero kukagua ujenzi wa maabara na madarasa ya 'A' Level .

Hata hivyo Waziri huyo licha ya kutembelea shule za sekondari, alipata fursa ya kuitembelea shule ya msingi Manyinga 'A' na kupokea taarifa ya shule hiyo , ambapo pia alikiteembelea Chuo cha Ualimu Mhonda  akiwa na lengo la kupata taarifa na kukagua miundombinu ya Chuo hicho.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Kawambwa, katika ziara hiyo ya siku tatu, ilimfikisha pia Wilaya ya Kilosa, ambapo baada ya kupokea taarifa ya elimu ya wilaya , aliitembelea shule ya msingi Mazinyungu ili kukagua miundombinu ya shule hiyo.

Pia shule nyingine za sekondari alizozitembelea wilayani humo ni ya Rudewa na Kilosa Sekondari , ambapo pia alipata fursa ya kukitembelea Chuo cha Ualimu Ilonga kwa lengo la kupata taarifa ya maendeleo ya elimu na  hali ya miundombinu ya chuo.
Waziri Dk. Kawambwa (suti nyeusi) akipata maelezo ya matumizi ya mkaa rafiki unaotengenezwa na pumba za mpunga na vumbi la mbao na kupunguza gharama ya matumizi ya gesi na kuni kwa huduma za chakula shuleni hapo.
Waziri Dk. Kawambwa (suti) akisikiliza maenezo ya Mwalimu wa Somo la Fizikia walipotembelea maabara ya somo hilo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa ( suti nyeusi kulia) akifafanua jambo wakati akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari KilaKala ya Wasichana wa Vipaji Maalumu , Tabitha Tusekelege, wakati Waziri huyo akitoka kuangalia vyumba vya maabara ya Kemia, Fikizikia na Baolojia na majengo mengine yaliyopo Shuleni hapo Oktoba 20, 2014, alipofanya ziara na kuzungumza na wanajumuiya ya Shule hiyo.

DR. KAMANI AKABIDHI NG'OMBE 83 WA MAZIWA KWA WAFUGAJI WADOGO

$
0
0
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Titus Kamani, amekabidhi mikopo ya Ng’ombe wa maziwa themanini na tatu (83) kwa kikundi cha wafugaji cha Somangira walioko Kigamboni wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

Ng’ombe hao ambao wamenunuliwa kwa mkopo uliotolewa na Covenant Bank wana uwezo wa kuzalisha maziwa zaidi ya Lita 20 kwa siku. Akizungumza na wakazi wa eneo hilo Waziri Kamani ametanabaisha  kuwa mikopo ya aina hiyo italeta mapinduzi makubwa katika sekta ya mifugo.

“Kitendo cha kukabidhiwa Ng’ombe kwa kikundi cha wafugaji wadogo wa Somangira kinafanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu hususan katika sekta ya mifugo, Mikopo ya aina hii imekuwa ikitolewa i kwa Ranchi za taifa lakini haikuwahi kutolewa kwa wafugaji wadogo wadogo” alisema Dk. Kamani na kuongeza kuwa,.

“Hatua hii ni ya kupongezwa sana hasa kutokana na Uhitaji mkubwa wa Maziwa uliopo nchini kwa sasa, ambapo kama nchi tunatakiwa kuzalisha lita bilioni 9 za maziwa kwa siku ili kuwatosheleza watu wetu lakini kwa sasa tuna uwezo wa kuzalisha lita bilioni mbili tu, Hivyo ninaomba benki hii kwa kushirikiana na wadau wengine waendelee kutoa mikopo hii kwa vikundi vingine ili kuongeza uzalishaji”. Alisema.

Aidha, Dr Kamani aliwataka wana kikundi hao kuhakikisha wanawatumia ng’ombe hao katika kujipatia kipato na kurudisha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwezesha vikundi vingine kukopa kupitia marejesho hayo.

Awali, akizungumza na wananchi wa Somangira Mkurugenzi wa Covenant Bank, Bibi Sabetha Mwambenja amesema ng’ombe hao 83 wamekatiwa bima hivyo endapo gg’ombe hao watakufa au kupatwa na tatizo lolote kampuni ya bima itachukua jukumu la kumlipia mkopo wake mfugaji aliyeathirika.

“Licha ya kutoa mikopo ya ng’ombe kwa hawa wakulima, Covenant Bank, tumekwenda mbali zaidi kwa kuwawezesha wakulima hawa kupata mafunzo ya ufugaji wa kisasa wa Ng’ombe wa Maziwa kutoka kwa wataalam wa bodi ya maziwa na tayari mabanda yamekaguliwa na kujiridhisha kuwa sasa watakuwa mahali salama’’, Alisema.

Kwa Upande wake Katibu wa Kikundi  hicho Bi. Getrude Mpelembe, aliishukuru Benki hiyo huku akitoa wito kwa Serikali kuboresha miundombinu kwa wafugaji wadogo kwa kuwapatia wataalam wa kutosha na kutafuta soko la maziwa la uhakika.
Mkurugenzi wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, akimpokea Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr, Titus Kamani, wakati akiwasili katika hafla ya kukabidhi Ng’ombe 83 wa Maziwa kwa wafugaji wadogo wa Kikundi cha Somangira walioko Kigamboni Jijini Dar es Salaam, Ng’ombe hao wamenunuliwa kwa Mkopo kutoka Covenant Bank.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Somangira, Kigamboni Jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi Ng’ombe 83 wa maziwa kwa kikundi wafugaji wadogo wa kijiji hicho Ng’ombe hao wamenunuliwa kwa Mkopo kutoka Covenant Bank. Pamoja nae katika Picha ni Mkurugenzi wa Covenant Bank. Sabetha Mwambenja.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani, akikamua Maziwa kutoka kwa moja ya Ng’ombe 83 wa Maziwa, punde baada ya Kuwakabidhi kwa wafugaji wa kikundi cha Somangira – Kigamboni jijini Dar es Salaam, wanaoshuhudia ni Mratibu wa Kikundi hicho Bibi. Getrude Mpelembe(kushoto) Mkurugenzi wa Covenant Bank. Bibi Sabetha Mwambenja (Katikati) na Mwenyekiti wa Wajasiriamali wasio katika Sekta Rasmi, Dauda Salmin.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr. Titus Kamani, akikabidhi moja ya Ng’ombe 83 wa Maziwa, kwa Bibi. Robi Chacha ambaye ni miongoni mwa wanakikundi 83 waliokabidhiwa Ng’ombe hao ambao wamenunuliwa kwa Mkopo na Covenant Bank. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Covenant Bank. Sabetha Mwambenja, (Mwenye miwani katikati) na Mwenyekiti wa Wajasiriamali wasio katika Sekta Rasmi Dauda Salmin.

LEO IMETIMIA MIAKA 10 TOKA FREDDY "SUPREME" NDALA KASHEBA ATUTOKE

$
0
0
Na John Kitime
LEO tunatimiza miaka kumi toka kifo cha mwanamuziki mahiri Freddy Supreme au maarufu kama Ndala Kasheba. Freddy alianza kufundishwa gitaa na baba yake wakati akiwa na umri wa miaka 12. Baba yake alijua kupiga gitaa japo hakufanya kazi ya uanamuziki, alikuwa akipiga gitaa nyumbani baada ya saa za kazi.
Moja ya bendi maarufu ambazo zilimtambulisha sana Fredd ilikuwa Orchestra Fauvette, Freddy alieleza kuwa bendi ya Orchestra Fauvette ilianza tarehe 7 mwezi wa sita mwaka 1964 katika jiji la Lubumbashi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Jina hilo Fauvette kwa kiswahili ni Chiriku, bendi ilikuwa na muimbaji ambaye waliamini alikuwa anaimba kama chiriku na hivyo kuipa bendi hiyo jina hilo.
Vyombo vyao vya muziki walinunua Ujerumani kupitia duka la muziki la Dar es salaam Music House (duka lipo mpaka leo). Vyombo vilikuwa vya aina ya Hofner, jina lililoheshimika sana kwa wanamuziki wakati huo. KUSOMA HABARI KAMILI BOFYA HAPA
Freddy "Supreme" Ndala Kasheba akitumbuiza umati wa washabiki katika bustani ya Mnazi Mmoja mwaka 1980
Freddy "Supreme" Ndala Kasheba akitumbuiza mabalozi wakati walipofanya semina elekezi katika hoteli ya kitalii ya Ngorongoro Februari 2007
Ankal akisikiliza wimbo wa "Yellow Card" wakati Kasheba alipokuwa akimalizia kuurekodi katika studio za Makuti zilizokuwa Shariff Shamba jijini Dar es salaam mwaka 2006. Usikilie hapa chini
Freddy "Supreme" Ndala Kasheba akisalimiana na Balozi Mohamed Maharage wakati wa semina elekezi kwa mabalozi katika hoteli ya kitalii ya Ngorongoro Februari 2007.

Mwanamuziki Tarsis Masela kuzindua albamu yake ya kwanza Novemba 21

$
0
0
MWANAMUZIKI wa muziki wa daansi, Tarsis Masela (mwenye miwani), anatarajia kufanya uzinduzi wa albamu yake ya kwanza iitwayo Acha Hizo utakaofanyika Novemba 21 kwenye Ukumbi wa Ten Lounge (zamani Business Park) ulioko  Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini dar leo Masela, ambaye pia ni mwanamuziki na Rais wa bendi ya Akudo, alisema kuwa albamu hiyo itakuwa na nyimbo saba na zina ujumbe mbalimbali ambao unalenga kuelimisha jamii.

Masela alizitaja nyimbo zilizoko katika albamu hiyo kuwa ni pamoja na Tabia Mbaya ambayo amemshirikisha ‘Mfalme’ wa taarabu, Mzee Yusuph, Chaguo Langu, Nimevumilia (Lady Jay Dee).

Alisema nyimbo nyingine ni Vidole Vitatu, Penzi Langu Limezidi Asali, Mwiko na Tusiachane.
“Hii ni albamu yangu ya kwanza tangu nianze muziki, nimeshirikisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya na taarabu ili kuifanya iwe na ladha tofauti na ubora wa juu,” alisema Masela.

Aliongeza kuwa katika uzinduzi wake atasindikizwa na wasanii mbalimbali ambao kwa sasa wako kwenye mazungumzo ya mwisho ili kulifanya onyesho hilo liwe na ubora wa aina yake.

Naye Meneja wa msanii huyo, Ray Matata,alisema kuwa maandalizi ya onyesho hilo yanaendelea vizuri na wamejipanga kufanya mapinduzi kwenye muziki wa dansi.

Matata alisema kwamba Masela ameonyesha nia na amewataka wadau wa sanaa ya muziki kujiandaa kushuhudia onyesho lenye ubora wa kimataifa.

Serikali kuendelea kuiwezesha Tume Opresheni Tokomeza - Mh. Kairuki

$
0
0
Serikali imeahidi kuendelea kuiwezesha na kuipa ushirikiano Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza ili iendelee kutekeleza na hatimaye kukamilisha majukumu yake kama ilivyokusudiwa.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Angellah Jasmine Kairuki amesema hayo jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Oktoba 22, 2014) wakati akizungumza na Wajumbe wa Tume hiyo waliomtembelea ofisini kwake ili kubadilishana mawazo.

“Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano na kuwawezesha ili mtekeleze majukumu yenu kama ilivyokusudiwa,” amesema Naibu Waziri katika mkutano huo uliohudhuriwa na Mwenyekiti wa Tume Jaji Kiongozi Mstaafu Hamis Amir Msumi na Wajumbe wengine Jaji Mstaafu Stephen Ihema, Jaji Mstaafu Vincent Lyimo na Katibu wa Tume hiyo Wakili Fredrick Manyanda.

Ahadi ya Naibu Waziri Kairuki ilifuatia kauli ya Mwenyekiti wa Tume hiyo kuwa Tume yake imekuwa ikipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wananchi na Serikali tangu ilipoteuliwa tarehe 1 Mei mwaka huu.

“Tunashukuru kwa ushirikiano tunaoupata kutoka Serikalini,” amesema Jaji Msumi na kufafanua kuwa viongozi wa Serikali wa wilaya na mikoa wametoa ushirikiano mzuri kwa Tume yake katika awamu ya kwanza ya kukusanya taarifa na malalamiko.

Jaji Msumi amesema kuwa katika awamu hiyo iliyofanyika katika mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Mbeya wananchi na viongozi wa Serikali katika maeneo hayo walitoa ushirikiano mkubwa.

“Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halamashauri walitupa ushirikiano wa kutosha na wananchi walikuwa na shauku kubwa ya kukutana na Tume,” amesema Jaji Msumi alipokuwa akizungumzia awamu ya kwanza ya ziara ya Tume yake iliyofanyika kuanzia tarehe 17 Septemba, 2014 hadi 6 Oktoba mwaka huu.

Jaji Msumi pia amemweleza Naibu Waziri kuwa Tume yake inatarajia kuanza awamu ya pili ya kutembelea mikoa sita ya Kanda ya Ziwa kuanzia kesho (Alhamisi, Oktoba 23, 2014) hadi tarehe 18 Novemba mwaka huu ili kukusanya taarifa na malalamiko katika kuhusu Operesheni Tokomeza. Mikoa itakayotemebelea na Tume hiyo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu na Mara.

Rais Jakaya Kikwete, kwa mujibu wa Kifungu cha 3 cha Sheria ya Uchunguzi Sura ya 32, aliunda Tume ya Uchunguzi (Commission of Inquiry) kuhusu vitendo vilivyotokana na uendeshaji wa Operesheni Tokomeza tarehe 1 Mei mwaka huu.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki (MB) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Jaji Kiongozi Mstaafu Hamis Amir Msumi (kushoto) na Wajumbe wengine wa Tume hiyo, Majaji Wastaafu Stephen Ihema (kulia) na Vincent Lyimo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo (Oktoba 22, 2014).
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images