Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MEJA JENERALI (MSTAAFU) ROLAND MAKUNDA

$
0
0



JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
 
Simu ya Upepo   : “N G O M E”          Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463      Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                       DAR ES SALAAM, 20, October, 2014
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  www.tpdf.mil.tz
                  
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
 
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa ya ratiba ya kuaga mwili wa Meja Jenerali Roland Makunda (Mstaafu) aliyefariki tarehe  16 Octoba 2014 wakati akipata matibabu katika Hospitali Kuu ya Kijeshi Lugalo.
 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dr Hussein Mwinyi  leo tarehe 20 Octoba 2014 mnamo saa nne kamili anatarajia kuongoza Makamanda, wapiganaji na watumishi wa umma katika kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Roland Makunda kwenye viwanja vya Hospitali ya Lugalo.
 
  
 
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783-309963

TAARIFA KUTOKA JENZI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)

$
0
0


JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO


Simu ya Upepo   : “N G O M E”            Makao Makuu ya Jeshi,

Simu ya Mdomo : DSM  22150463       Sanduku la Posta 9203,

Telex                     : 41051                        DAR ESSALAAM, 20 Octoba, 2014

Tele Fax                : 2153426

Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz

                  

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa ni kosa kisheria kumiliki au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika.

          Aidha,  kumeonekana matukio kadhaa ya baadhi ya vikundi, ama mtu mmoja mmoja kumiliki au kuvaa sare za JWTZ.  Inakumbushwa kuwa kwa yeyote atakayeonekana amevaa ama kumiliki sare hizo sheria itachukua mkondo wake. 


  
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.


Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963

Wana Arumeru Mashariki walivyomuenzi mwalimu Nyerere

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari (kushoto) akiangalia wananchi wake wakiendelea na uchimbaji wa mtaro wa kupitisha Mabomba ya Maji ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya Baba wa Taifa,Mwalimu Julius K. Nyerere kwa kuhakikisha Ahadi ya maji kwa wananchi wa Manyata na Nganana kata ya Usa River inatimia.

Mbunge Nassari aliingia kazini kuanzia asubuhi mpaka jioni. Mradi huu umetoa maji umbali wa kilomita 9 toka kwenye chanzo (Uraki). Wananchi wa Arumeru walikuwa wanakunywa maji ya majaruba ya mpunga kwa miaka yote kabla ya mradi huo ulioasisiwa na Mbinge wa Jimbo hilo,Mh. Joshua Nassari

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mhe. Joshua Nassari akishiriki kazi za mikono za kuchimba mtaro wa maji, kutandaza mabomba na kuzindua mradi wa maji aliouanzisha katika vitongoji Vya Manyata na Nganana.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mhe. Joshua Nassari akichota maji katika moja ya bombo mara baada ya kuzindua mradi wa maji aliouanzisha jimboni hapo.
Furaha ya kupata maji ilikuwa ni ya kila mwanakijiji katika eneo hilo.

MECHI YA YANGA, SIMBA YAINGIZA MIL 427/-

$
0
0
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba iliyochezwa  (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 427,271,000.

Washabiki 49,542 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 65,176,932 wakati asilimia 5 ya gharama ya tiketi kwa CRDB ni sh. 21,363,550.

Kwa upande wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ambayo ni sh. 1,000 kwa kila tiketi, timu mwenyeji Yanga imepata sh. 17,339,700, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 7,431,300 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,771,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni Uwanja sh. 43,678,277.67, gharama za mchezo sh. 24,751,024.01, Bodi ya Ligi sh. 23,295,081.42, TFF sh. 17,471,311.07, DRFA sh. 10,191,598.12, timu mwenyeji Yanga sh. 100,460,038.64 na timu ngeni Simba sh. 71,341,186.86.

WAZIRI MKUU AALIKA WAWEKEZAJI KATIKA AFYA, KILIMO, NISHATI

$
0
0
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imefungua milango kwa wawekezaji kwenye sekta zote lakini mkazi unaelekezwa zaidi kwenye sekta ya afya, kilimo hasa usindikaji mazao, nishati na miundombinu.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Oktoba 20, 2014) wakati akishiriki Mjadala wa Marais (Presidential Keynote Panel) kuhusu fursa za uwekezaji barani Afrika uliolenga kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo barani Afrika hasa katika nchi za Tanzania, Uganda, Ghana na Rwanda ambao umeanza leo kwenye hoteli ya Savoy, jijini London, Uingereza.

Waziri Mkuu aliwasili jijini London jana mchana kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi unaohusu uwekezaji barani Afrika (The Global African Investment Summit – TGAIS) kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete na ameshiriki mjadala huo pamoja na Rais John D. Mahama wa Ghana, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda.

“Tunahitaji wawekezaji kwenye sekta nyingi lakini zaidi kwenye sekta ya afya katika vyuo vya tiba na uuguzi ili tupate watumishi wa kutosha, utengenezaji wa madawa na vifaa vya hospitali na ujenzi wa hospitali,” alisema.

Aliyataja maeneo mengine ya kipaumbele kuwa ni kilimo na na hasa usindikaji wa mazao, hasa ikizingatiwa kwamba asilimia kubwa ya Watanzania inategemea kilimo kwa kujikimu. “Watanzania wengi bado wanategemea kilimo kama njia yao kuu ya uzalishaji, tunahitaji pia kupata umeme wa kuendesha viwanda kutokana na gesi, makaa ya mawe pamoja na geo-thermal,” aliongeza.

Akizungumzia kuhusu uwekezaji kwenye miundombinu, Waziri Mkuu alieleza Serikali ilivyojipanga kujenga reli mpya yenye urefu zaidi ya km. 2,000 kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma, reli ya kutoka Tanga kupitia Arusha hadi Mwanza na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo pamoja na uimarishaji wa bandari za Tanga, Mtwara na Dar es Salaam.

Kwa upande wao, Marais wa Ghana, Uganda na Rwanda walielezea fursa zilizopo nchini mwao kwenye maeneo ya madini, miundombinu ya barabara na reli, umeme, na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Mapema, akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo wa siku mbili, Mwenyekiti wa mkutano huo, Rais mstaafu wa Nigeria, Bw. Olesegun Obasanjo alisema bara la Afrika lina nafasi kubwa ya kuendeleza sekta za maenedeleo kupitia uwekezaji maliasili, Kilimo na usindikaji mazao, nishati na utalii.

“Nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara zina fursa nyingi za uwekezaji na siyo hizi nne ambazo zimewakilishwa leo hapa za Tanzania, Uganda, Ghana na Rwanda. Kuna miradi yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 200 ambayo itapata fursa za kunadiwa kwa wawekezaji kupitia mkutano huu,” alisema.

“Nimewaalika Marais kutoka nchi hizi nne ili watupe mwanga wa kile tunacheweza kufanya katika nchi zao... lakini vilevile tutambue katika bara la Afrika kuna vijana wengi ambao ni zaidi ya asilimia 60 ambao hawana kazi. Tutakuwa tumepotoka tusipoliangalia kundi hili. Ni lazima miradi inayotafutiwa wawekezaji ilenge kuleta ajira kwa vijana wetu, wapate kipato (wealth creation) na technology transfer,” alisema.

Mkutano huo unahudhuriwa na wakuu wa makampuni na taasisi za kibiashara zaidi 400.

MICHUANO YA KOMBE LA CHIKAWE YASHIKA KASI NACHINGWEA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akimkabidhi Kapteni wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Ubungo Stars ya Kata ya Namapwia, wilayani Nachingwea, Hassan Abbas zawadi ya mpira wa miguu baada ya timu hiyo kuongoza Ligi katika Kata hiyo. Timu nne zilishiriki mashindano hayo ya Kata na kufanikiwa kutengeneza timu moja ambayo itashiriki katika mashindano ya Tarafa ya Ruponda na baadaye kufika ngazi ya wilaya ambapo mshindi wa wilaya anatarajiwa kupewa zawadi nono ya Sh 500,000 itakayotolewa na Mbunge wa jimbo hilo. Hata hivyo, Chikawe alitoa jezi seti 170 pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akimkabidhi Diwani wa Kata ya Namapwia, wilayani Nachingwea, Sefu Mwenyewe fedha kwa ajili ya mshindi wa pili pamoja na wasimamizi wa ligi hiyo. Katika mashindano hayo ya ligi yaliyomalizika hivi karibuni, Timu ya Ubungo Stars iliibuka kidedea katika kata hiyo na kufanikiwa kupewa zawadi ya mpira wa miguu. Timu nne zilishiriki mashindano hayo kufanikiwa kutengeneza timu moja ambayo itashiriki katika mashindano ya Tarafa ya Ruponda na baadaye kufika ngazi ya wilaya ambapo mshindi wa wilaya anatarajiwa kupewa zawadi nono ya Sh 500,000 itakayotolewa na Mbunge wa jimbo hilo. Hata hivyo, Chikawe alitoa jezi seti 170 pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo.
Kapteni wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Timu ya Ubungo Stars, Kata ya Nawapwia, Hassan Abbas akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) kwa mchango wake mkubwa ambao ameutoa kwa ajili ya kuzisaidia timu 170 za mpira wilayani Nachingwea na pia kuwawezesha kwa muda mrefu kushiriki katika michezo ambapo inawasaidia kutokuingia katika matukio ya uhalifu mitaani. Waziri Chikawe ameanzisha ‘Chikawe CUP’ ambapo kwasasa mashindano hayo yapo katika ngazi ya Kata mbalimbali ambapo mshindi atapatikana baada ya kufikia ngazi ya wilaya. Timu ya Ubungo Stars ndio iliongoza katika mashindano ya Kata ya Namapwia baada ya kuzishinda timu 3 zilizopo katika kata hiyo. Hata hivyo, Chikawe alitoa jezi seti 170 pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Ubungo Stars ya Kata ya Namapwia wilayani Nachingwea baada ya timu hiyo kuwa mshindi wa kwanza baada ya kuzishinda timu tatu zilizopo katika kata hiyo. Waziri Chikawe aliipa zawadi ya mpira timu hiyo na kuwashauri wazidi kusongo mbele ili timu hiyo ifike hatua ya Wilaya ili wapewe zawadi ya Sh500,000 kwa timu itakayonyakua kombe hilo. Hata hivyo, Waziri Chikawe alitoa jezi seti 170 pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo. Picha zote na Felix Mwagara.

Benki ya Exim yaahidi kuunga mkono juhudi za serikali kuboresha hali ya magereza nchini

$
0
0
Wafanyakazi wa Benki ya Exim tawi la Mwanza na wawakilishi wa gereza la Butimba wakiwa katika picha ya pamoja, muda mfupi baada ya Benki hiyo kukabidhi vifaa vya usafi  kwa gereza la Butimba lililopo jijini Mwanza hivi karibuni. Mchango huo ni sehemu ya shughuli za kibenki za kijamii lakini pia ukilenga kusaidia wafungwa kubadili tabia.

Exim Bank imeahidi kuendelea kusaidia juhudi za serikali katika kuboresha hali ya magereza nchini, ikiwa ni sehemu ya shughuli zake za kibenki za kijamii. Benki iyo imekabidhi vifaa vya usafi kwa wanawake wanaotumikia vifungo katika gereza la Butimba jijini Mwanza, hatua inayolenga kuwasaidia na kuwaelimisha wanawake hao kubadili tabia.

Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika gereza la Butimba jijini Mwanza hapo jana, Mkuu wa Matawi wa Benki ya Exim Mwanza, Bw. Justus Mukuras alisema mchango huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa wafungwa walio katika gereza hilo. Alisema mbali na mchango wa vifaa hivyo, benki hiyo iliajiri mwanasaikolojia ambaye alizungumza na wanawake hao na kuwapa faraja pamoja na kuwafundisha mbinu mbalimbali za maisha. Lengo likiwa kuwafanya kuwa mfano bora katika jamii zao pindi watakaporudi uraiani.

 “Hii ni sehemu ya shughuli zetu za kijamii na hatulengi kuishia hapa, hizi ni jitihada endelevu zilizo chini ya kampeni ya benki yetu ya kusaidia wafungwa wa kike nchini. “Pamoja na mambo mengine, kampeni hiyo inalenga kuwafundisha wafungwa mbinu mbalimbali za maisha na kuwafanya wawe watu bora zaidi. Tutaendelea kuwasaidia vifaa vya usafi pamoja na vifaa vingine kwa watoto wanaoishi na mama zao katika magereza,” alisema Bw. Mukuras.

Wafungwa wengi nchini wanakabiliwa na uhaba wa vifaa vya usafi pamoja na vyakula; hii inatokana na idadi kubwa ya wafungwa katika magereza hali inayopelekea mlipuko wa magonjwa.

 “Sisi kama benki tungependa kutekeleza jukumu letu la kusaidia jamii hususani wanawake wanaotumikia vifungo katika magereza pamoja na watoto wanaoishi na mama zao katika magereza hayo kwani baadhi yao wanakabiliwa na upungufu wa virutubisho na afya duni. Ukipata nafasi ya kuingia katika magereza ndipo utakapobaini idadi ya matatizo wanayokumbana nayo,” aliongeza Bw. Mukuras.

Tume ‘Operesheni Tokomeza’ kwenda Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mwanza na Mara keshokutwa 23 Oktoba

$
0
0
Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Ujangili imetangaza ratiba ya pili ya ziara yake katika Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mwanza na Mara ili kukusanya taarifa na kupokea malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Katibu wa Tume hiyo Wakili Fredrick Manyanda (pichani), Tume hiyo itatembelea mikoa hiyo kuanzia keshokutwa Alhamisi, Oktoba 23, mwaka huu hadi tarehe Novemba 18 mwaka huu.
Katika awamu ya kwanza iliyofanyika kuanzia tarehe 17 Septemba, 2014 na kumalizika tarehe 6 Oktoba, 2014 ambapo Tume ilitembelea mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Mbeya na kukutana na wananchi katika wilaya za Wilaya za Kibondo, Kasulu, Uvinza, Mpanda, Sumbawanga, Mbozi na Mbarali.
Katika awamu ya pili, Wakili Manyanda ameeleza katika taarifa yake kuwa, Tume itatembelea Wilaya ya Bukoba Mjini tarehe 23 Oktoba na tarehe 24 mpaka tarehe 27 Oktoba 2014 itakuwa Wilaya ya Muleba kwa Mkoa waKagera. Na kwa Mkoa wa Geita, Tume itatembelea Wilaya ya Chato tarehe 28 na tarehe 29 Oktoba, 2014 na kuanzia tarehe 31 Oktoba, 2014 mpaka tarehe 1 Novemba, 2014 Tume itakuwa katika Wilaya ya Bukombe.

Kwa Mkoa wa Simiyu, Tume itatembelea Wilaya ya Meatu tarehe 5 Novemba, 2014 na Wilaya ya Bariadi tarehe 8 Novemba, 2014. Na kwa Mkoa wa Mara Tume itatembelea Wilaya ya Bunda tarehe 10 na tarehe 11 Novemba, 2014; Wilaya ya Tarime itakuwa tarehe 13 mpaka tarehe 15 Novemba, 2014 na Wilaya ya Serengeti tarehe 17 mpaka tarehe 18 Novemba, 2014.

Aidha, pamoja na mikutano hiyo, Wakili Manyanda amewaomba wananchi kutuma taarifa na malalamiko kwa njia ya barua, simu na barua pepe. Wananchi wanaweza kutuma barua kwa Katibu wa Tume, Tume ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Ujangili, SLP 9050, Dar es Salaam na barua pepe kwenda opereshenitokomeza@agctz.go.tz

Kuhusu ujumbe mfupi wa maandishi, wananchi wanaweza kutuma kwa namba za simu: Tigo: 0714 826826; Vodacom: 0767 826826; Airtel: 0787 826826; na Zantel: 0773 826826. 

The University of Dar es Salaam Computing Centre (UCC) to conduct International Certification Training and Workshops for Project Management for Professionals

UKAGUZI WA BARABARA YA TUNDUMA - SUMBAWANGA

$
0
0
 Kaimu Meneja wa wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Masuka Nkina (wa kwanza kulia mwenye shati jeupe) akitoa maelezo juu ya utendaji kazi wa mizani ya Nkangamo katika barabara ya Tunduma – Laela- Sumbawanga. Utendaji wa mizani hiyo ni kwa kutumia kompyuta ambapo mteja anachapishiwa risiti yake hapo hapo inayoonyesha taarifa zake zote. Kama mzigo utakuwa umezidi pia risiti hiyo itaonyesha faini anayotakiwa kulia.
 Mhandisi Julius Isoka ambaye ni Mhandisi Mshauri wa Barabara ya  Tunduma- Sumbawanga kutoka kampuni ya Nicholous Odweyer akiwaelezea timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao wanatembelea barabara hiyo jinsi ambavyo daraja linasukwa kutoka chini mpaka juu.  Barabara hii inajengwa kwa ufadhili wa Watu wa Marekani chini ya Mradi wa Milleniam Challenge (MCC).
 Daraja la Kashahanzi moja ya daraja kubwa na linalojengwa kwa umahiri mkubwa katika barabara ya Tunduma  –Sumbawanga.  PICHA ZOTE NA JOYCE MKINGA

News alert: Oscar Pistorius ahukumiwa kifungo cha miaka 5 gerezani kwa kumuua bila kukusudia girlfriend wake

$
0
0
Oscar Pistorius akiwasili katika mahakama ya Pretoria nchini Afrika kusini kusikiliza hukumu yake leo.

Mwanariadha huyo asiye na miguu aliyeshangaza ulimwengu katika michuano ya Olympic mwaka 2012, amehukumiwa kifungo cha miaka 5 gerezani na Jaji wa Afrika ya Kusini asubuhi hii, katika hatua inayofikisha tamati mlolomngo wa muda mrefu wa kesi hiyo iliyokuwa ikifuatiliwa kwa karibu ulimwenguni kote

Pistorius alipatikana na hatia ya kuua bila kukusudia mnamo Septemba 12, mwaka huu, kwa kumtoa roho rafiki yake wa kike mwanamitindo  Reeva Steenkamp, siku ya Valentine’s Day mwaka 2013 kwa kumpiga risasi katika bafu nyumbani kwake Pretoria.

SOS VILLAGES IKISHIRIKIANA NA MONTAGE INAWALETEA CHAKULA CHA HISANI KATIKA KAMPENI YAO YA ‘NIJALI

$
0
0

Tamasha la Handeni Kwetu lawapigia magoti wadhamini

$
0
0
 

WADAU wa mambo ya utamaduni yakiwamo mashirika, makampuni na watu mbalimbali wameombwa kujitokeza kuliwezesha tamasha la Handeni Kwetu 2014, lililopangwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Tamasha hilo linafanyika huku mwaka jana likiwezeshwa kwa kiasi kikubwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ushirikiano na wadau mbalimbali walioliwezesha tamasha hilo kwa mara ya kwanza katika Historia ya Mkoa wa Tanga.

Akizungumza mjini hapa, Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa wadhamini wakijitokeza kwa wingi kutaongeza chachu ya maendeleo ya nchi, sanjari na sanaa ya utamaduni inayotakiwa kuungwa mkono na watu wengi.

Alisema kuwa kitendo cha wadhamini kuendelea kuliunga mkono Tamasha hilo kutachangia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa nchi pamoja na kutangaza utamaduni wa Mtanzania.

“Mwaka jana wadau wengi walijitokeza kuliwezesha tamasha la Handeni, wakiwamo NSSF, hivyo tunaomba msimu huu pia tuendelee kushirikiana kuliwezesha Tamasha la Handeni Kwetu litakalofanyika Desemba 13 mwaka huu, Handeni Mjini.

“Hadi wakati huu, walioonyesha nia ya kulisaidia tamasha la Handeni Kwetu 2014 ni pamoja na SmartMind & Partners iliyopo chini ya Anesa Co. Ltd kwa kupitia kitabu chao cha Ni Wakati wako wa Kung’aa, Phed Trans, chini ya Yusuphed Mhandeni, Handeni Kwetu Foundation, Wait & Watch Film Company Ltd, Qs Mhonda J Apex Group of Companies Ltd na Skyblue Security and Risk Mgt Ltd,” alisema Mbwana.
 

Tamasha la Handeni Kwetu ni miongoni mwa matukio makubwa ya kiburudani mkoani Tanga, ambako zaidi ya watu 500 walihudhuria tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu mipango kabambe ya kuhakikisha kuwa linafanyika kwa mafanikio.

Mheshimiwa Dkt Augustine Lyatonga Mrema ahutubia mkutano wa hadhara jimboni kwake vunjo

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro na Mwenyekiti wa chama cha TLP, Dkt. Augustine Lyatonga Mrema akihutubia katika mkutano wa hadhara jimboni kwake  jana kwa ajili ya kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa na pia kuelezea utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.

Katika jimbo hilo la Vunjo kumekuwepo na Mvutano mkubwa wa kuliwania katika uchaguzi mkuu wamakani ambapo kwa vyama vya CCM tayari kijana Innocent Shirima ameshatangaza nia kama alivyofanya  Mh. James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.

Vodacom Inakuletea AppStar 2014


MAHAKAMA YAAGIZA Halima MDEE NA WENZAKE KUHUDHURIA KESI YAO INAPOPANGWA KUSIKILIZWA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kawe,  Mhe Halima Mdee

Habari na Mwene Said 
wa Globu ya Jamii 
 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeagiza Mbunge wa Jimbo la Kawe,  Mhe Halima Mdee (35) na wenzake wawili kufika mahakamani ili iweze kuanza kusikiliza kesi inayowakabili ya kupinga amri halali ya Jeshi la Polisi na kukusanyika isivyo halali kwa lengo la kwenda Ikulu. 
 Amri hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa mshtakiwa wa kwanza Mdee, wa tatu, Renina Leafyagila na wa sita Sophia Fanuel kutoa kushindwa kufika mahakamani. 
 Wakili wa Serikali Mohamed Salum alidia kuwa upande wa Jamhuri uko tayari kuendelea kusikiliza maelezo ya awali na kwamba hauna taarifa za washtakiwa hao. Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai kuwa wadhamini wa washtakiwa wana taarifa za washtakiwa. 
Mdhamini wa Mdee alidai kuwa alikuwa kwenye ziara za kichama kanda ya ziwa na kwamba alipanga kurejea jijini jana lakini ilishindikana baada ya ndege kuahirisha safari jana (juzi). Mdhamini wa mshtakiwa wa tatu, alidai kuwa mshtakiwa huyo amefiwa na baba yake mzazi na kwamba leo (jana) walikuwa wanafanya maziko. 
 Halikadhalika mdhamini wa mshtakiwa wa sita, alidai kuwa mshtakiwa yuko kwenye msafara wa ziara ya chama na Mdee na kwamba walikosa usafiri wa ndege kurejea jijini Dar es Salaam. 
 Upande wa Jamhuri ulidai kuwa sababu ya mshtakiwa wa tatu ni ya msingi kwa sababu kufa hakuna taarifa. 
 “Mheshimiwa hakimu sababu ya mshtakiwa wa kwanza na wa sita hazina msingi na kwamba mahakama isipokemea itakuwa changamoto ya kuruhusu kila mtu kufanya anavyotaka na kuchelewesha usikilizwaji wa kesi… suala la kufika mahakamani washtakiwa kusikiliza kesi yao ni la msingi na kwamba ziara za kichama hazina uhusiano na mahakama hii “alidai Salum.
 Mhe. Hakimu Kaluyenda alisema wadhamini wahakikishe washtakiwa wanazingatia umuhimu wa kuhudhuria mahakamani na kwamba siku mbili kabla ya kesi wanatakiwa kufanya mawasiliano nao ili kuzuia ucheleweshaji wa kusikilizwa kesi yao. 
 Alisema washtakiwa wanatakiwa kuwepo mahakamani kila kesi yao inapopangwa na alipanga kusikiliza maelezo ya awali Novemba 5, mwaka huu. Mbali na Mdee, Leafyagila,Fanuel,wengine walioachiwa huru ni Rose Moshi, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Edward Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari. Oktoba 7, mwaka huu, Mdee na washtakiwa wenzake, walishindwa kutimiza masharti ya dhamana, baada ya nyaraka za wadhamini kushindwa kukamilika kufanyiwa uhakiki na hivyo kulazimika kulala mahabusu siku moja. 
Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa Oktoba 4, mwaka huu, katika Mtaa wa Ufipa, uliopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, isivyo halali, washtakiwa walikiuka amri halali ya Mrakibu wa Polisi (SP), Emmanuel Tillf, iliyowataka kutawanyika. 
 Ilidaiwa kuwa siku na mahali pa tukio la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko isivyo halali kwa lengo la kuandamana kwenda Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Washtakiwa wote walikana mashitaka hayo.

2ND NATIONAL ECONOMIC FORUM 24TH OCTOBER, 2014, DAR ES SALAAM 2.00PM to 6.00PM, KARIMJEE HAL THEME: ENTREPRENEURSHIP IN NATIONAL DEVELOPMENT; PUBLIC PRIVATE PARTNERSHIP PERSPECTIVE.

$
0
0
I greet you on behalf of the Tanzania Professionals Network, a network that was started as a Non-Governmental Organization which brings together Tanzanian Professionals and corporate from various industries within and outside the country to address cross-cutting issues. The top agenda being mobilizing our resources using the Power of Brain to empower economically Professionals and Tanzanians at large by using opportunities which has already been identified.
TPN has decided to organize the second National Economic Forum to discuss the role of entrepreneurship and national development process. The purpose of this event therefore is to bring professionals both within the country and Diaspora together with the government to discuss the way forward as a nation, basing on Tanzanian individuals.
The event will take place on 24th October, 2014 at Karimjee Hall , Dar es Salaam. We are expecting to have a high government official/ leader as a guest of honour. 
It is in this regard that we are asking you to partner with TPN in this great event by participating to its activities to enable more professionals to know the role of entrepreneurship in National development.

Based on the theme “The role of entrepreneurs and National Development” it is an event of critical and constructive discussions that will address issues and also give possible solutions. This day will bring greater professional involvement and commitment , your participation will rekindle the open and committed relationship between Professionals in all spheres of life.

Through this event you will have an opportunity for Business and Professional Networking; With TPN as a forum of different professionals, leaders and businessmen, you have an opportunity to grow and network with others. During this event we will have presentations from successful Entrepreneurs, government officials, Artists and Professionals on the topics shown in the attached program.

Could you please kindly send your attendance confirmation to our Program officer through:
Administrative Officer-Happy Johnson 0717144343
(you can sms you name/Organization to confirm you attendance)

Yours Sincerely,

Phares Magesa, B.Sc, MBA, IENG, MIET
President - TPN
+255 (0784/0767/0713) 618320

RATIBA YA MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA WATAALAM WA HUDUMA ZA HABARI NA MAKTABA ZA AFYA AFRIKA (AHILA) JIJINI DAR

$
0
0
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akifungua mkutano wa 14 wa Chama cha Wanataaluma wa Habari za Afya Afrika (AHILA) .
Rais wa wa Chama cha Wanataaluma wa Habari za Afya Afrika (AHILA), Nasra Gathoni akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Wanataaluma wa Habari za Afya Afrika (AHILA) unaoendelea katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akimkabidhi cheti mwanachama wa Chama cha Wanataaluma wa Habari za Afya Afrika (AHILA), Monica Samwel kutoka Tanzania wakati wa mkutano wa 14 wa chama hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa AHILA, Nasra Gathoni. 
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akimkabidhi cheti Naibu Mwakilishi Mkazi wa WHO, Grace Saguti wakati wa Mkutano Mku wa 14 wa  Chama cha Wanataaluma wa Habari za Afya Afrika (AHILA) uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa AHILA, Nasra Gathoni.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

GERMANY CONTRIBUTES 20 MILLION EUROS TO EAC TO SUPPORT IMMUNISATION PROGRAMME IN COLLABORATION WITH GAVI

$
0
0
The Federal Republic of Germany through her country director of KfW, German Development Bank, Mr. Wolfgang Solzbacher signed a financing agreement of 20 million Euros with the East African Community (EAC) in support of an immunisation programme in the region that will be implemented in collaboration with the GAVI Alliance.

Speaking during the signing ceremony Amb. Dr. Richard Sezibera, Secretary General of the EAC and Member of the GAVI Board, expressed his appreciation to the Federal Republic of Germany for its support in saving lives. This is a very important and critical programme, and I am sure with such commitment, it will grow, added Secretary General.

Ambassador Sezibera reiterated that the partnership and collaboration between the EAC and the Federal Republic Of Germany go back a long way and include among many others the support to construct the new headquarters of EAC.

The EAC Chief disclosed that the collaboration between the Federal Republic of Germany and EAC has evolved, and involved support to various domains but one notable support relates to child and maternal health especially in the area of vaccines.

In his remarks Mr. Wolfgang Solzbacher said that the new commitments underline that Germany continues to be a strong partner for the EAC, contributing to an integration process that puts the people in the centre.

Earlier before the signing of financing agreement, the new Ambassador of the Federal Republic of Germany to the United Republic of Tanzania his Excellency Egon Kochanke, presented his credentials to the Secretary General Amb Dr Richard Sezibera as a representative to the East African Community.

Since as early as 1998, Germany development cooperation, on behalf of the German Federal Ministry for Economic Cooperation (BMZ), contributes to the capacity development of the Secretariat of the EAC through a variety of programmes and projects.

Germany’s funding for Technical and Financial Cooperation with EAC amounts to about a total of 125.9 million Euros. Germany also provides substantial support for the health sector in selected EAC member states.

The GAVI Alliance is a public-private global health partnership committed to saving children’s lives and protecting people’s health by increasing access to immunization in poor countries.
EAC Secretary General Amb. Dr. Richard Sezibera and German Development Bank country director Mr. Wolfgang Solzbacher, signs the financing agreement.
Mr. Wolfgang Solzbacher and Amb. Dr. Richard Sezibera exchange the financial agreement documents after the signing.
The new Ambassador of the Federal Republic of Germany to the United Republic of Tanzania his Excellency Egon Kochanke presents his credentials to the Secretary General Amb Dr Richard Sezibera.
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images