Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Mapendekezo yawasilishwa kwa uongozi wa Benki ya Dunia

$
0
0
Katika mkutano muhimu uliofanyika jioni hii hapa mjini Washington DC. Kati ya ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile na Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika pamoja na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo ulimpatia nafasi nzuri sana Dr. Likwelile kuweza kueleza mambo muhimu ambayo Benki ya Dunia ingepaswa kuyafahamu.

Katika mawasilisho yake katibu Mkuu huyo aliwaeleza viongozi wa Benki ya Dunia kuwa ,anashukuru kwa ushirikiano mkubwa ambao ameupata kutoka Benki ya Dunia na kusema kuwa hii imeisaidia sana Tanzania katika kupiga hatua kiuchumi. Akiendelea kuzungumza Dr. Likwelile alisema kuwa pamoja na kufanikiwa katika ushirikiano huo kumekuwa na tatizo ambalo lina sababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa Bajeti.

Hili amelieleza kuwa linatokana na masharti ya wafadhili kutaka kwanza mambo yanayohusu IPTL kupatiwa ufumbuzi , kitu ambacho hakikuweko kwenye makubaliano. “ IPTL haina uhusiano na makubaliano ya awali suala hili limeingia katikati hii inaathiri utekelezaji wa kibajeti.”alisema.

Aidha aliendela kueleza kuwa sera ya Benki ya Dunia inadai kuwa kabila la Kimasai limetengwa na hivyo kutaka baadhi ya miradi isiende sehemu nyingine zaidi ya umasaini, hii nayo ni changamoto nyingine”. Katika mazungumzo hayo ilionekana kweli kuwa kwa kuchelewesha kutoa fedha kwa ajili ya miradi kunachangia sana kurudisha nyuma maendeleo.

Kwa mapendekezo haya mawili makubwa kama yatafikishwa kwenye ngazi ya juu na yakafanyiwa kazi basi nchi yetu itapiga hatua kama ilivyojipangia. Wakurugenzi hao waliyapokea mapendekezo hayo kwa mikono miwili na wakaahidi kuyafikisha na kuyafanyia kazi. Hali ya hewa mjini hapa ni ya baridi na manyunyu ya hapa na pale.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile akiwasilisha mapendekezo yake kwa Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo.
Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose ambaye ndiye anachukua nafasi hiyo wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akiwasilisha mapendekezo yake kuhusu hali halisi ya misaada.
Ujumbe kutoka Tanzania ukimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akiwasilisha mapendekezo yake kwa Bw. Denny H. Kalyalya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake wa kundi namba 1 la Afrika na Bw. Peter Larose Mkurugenzi Mtendaji mpya anayeachiwa kiti.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania wakiwaangalia kwa mshangao wakurugenzi hao wawili walipokuwa wakiingia (hawapo kwenye picha).habari/picha na Ingiahedi Mduma,Wizara ya Fedha.

KIPINDI MAALUM CHA UFUNGUZI WA BARABARA YA MWENGE - TEGETA ULIOFANYWA NA RAIS KIKWETE HIVI KARIBUNI

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA. Kumalizika kwa mkutano wa DICOTA 2014

$
0
0

Baraza la waTanzania waishio nchini Marekani (DICOTA) limemaliza mkutano wake wa mwaka Jumapili ya Oktoba 5 jijini Durham jimbo la North Carolina ambao kwa wengi waliohudhuria, wameonyeshwa kuridhishwa nao
Mwenzangu Mubelwa Bandio, anayo taarifa kamili.

Hii ni sehemu ya ripoti za Kwanza Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 11, 2014

BALOZI KAMALA APOKEA ZAWADI TOKA KWA MWENYEKITI WA JIJI LA Turnhout, Ubelgiji

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Jiji la Turnhout la Ubelgiji Mhe. Peter Segers baada kufungua rasmi Maonesho Wasanii wa kuchora wa nchi mbalimbali wakiwemo wa Tanzania wanaojulikana kwa jina la Tinga Tinga. Maonesho hayo yataendelea hadi mwishoni mwa mwezi huu.

Maonyesho Wiki ya Vijana yashika kasi Tabora

$
0
0
Afisa Ushauri wa Vijana wa UNFPA – Tanzania Bi. Farida Juma malezo kuhusu njia sahihi ya matumizi ya Kondomu kwa baadhi ya vijana waliotembelea banda la UNFPA katika viwanja vya Maonyesh ya Wiki ya Vijana yanayofanyika mjini Tabora.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Esther Riwa akigawa jarida la Si Mchezo kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la Wizara hiyo katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana mjini Tabora.
Afisa Utamaduni wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Simon Peter akielezea kuhusu namna ya uandishi wa miswada ya Filamu kwa mmoja wa vijana awaliotembelea banda lao katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana mjini Tabora.

Waziri Membe Aongoza Matembezi ya Hisani Dar es Salaam

$
0
0
Matembezi ya hisani yaliyoanzia Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe Mwenge yakielekea Parokia ya Sinza kupitia barabara ya Shekilango. Matembezi hayo ya kilomita mbili yaliongozwa na Mhe. Membe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.) (wa pili kushoto mstari wa mbele) akishiriki matembezi ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokovu ya Kanisa Katoliki Sinza, Dar es Salaam mapema leo asubuhi..Wa kwanza kushoto ni  Paroko, Father  Cuthbert Maganga Sasagu, na wa tatu kushoto ni  Mwenyekiti wa Parokia hiyo, Bw. Arnold Mwasumbi.
Waziri Membe akizungumza na waamini wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokovu Sinza.
Baadhi ya waamini wa parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokovu Sinza wakimsikiliza Waziri Membe .
Waziri Membe akipokea Zawadi ya picha kutoka kwa Paroko Sasagu
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na viongowa wa parokia ya Sinza.
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na wapuliza Tarumbeta.

ZIARA YA KIKAZI YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS - MAZINGIRA KATIKA KANDA YA ZIWA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Dkt. Binillith S.Mahenge akipewa maelezo na Mratibu wa NEMC kanda ya Ziwa Bi. Anna Masasi kuhusu uharibifu wa Mazingira ya Mwambao wa Ziwa Viktoria katika eneo la Nera, unaosababishwa na shughuli za Kilimo na ufugaji wa samaki katika eneo hilo jijini Mwanza.
Sehemu ya mwambao wa Ziwa Viktoria katika eneo la Nera jijini Mwanza likionesha shughuli za kilimo zinazofanyika katika eneo hilo na kusababisha uharibifu wa mazingira akioneshwa jinsi taka za plastiki zinavyochakatwa kutwnwza bi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa magugu maji kunakosababishwa na mbolea inayotumika katika shughuli za kilimo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Dkt. Binillith S.Mahenge akioneshwa jinsi taka za plastiki zinavyochakatwa kutengeneza bidhaa mbalimbali, kama vile Mifuko ya Plastiki, alipotembelea kiwanda cha Falcon Parkaging Ltd cha jijini Mwanza. Anayetoa maelezo ni Mkurugenzi wa Kiwanda Bwana Ganeshan Vedagiri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Dkt. Binillith S.Mahenge akioneshwa mbao iliyengezwa kutokana na taka za plastiki katika kiwanda cha Falcon Packaging Ltd cha jijini Mwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Dkt. Binillith S.Mahenge akioneshwa mifuko ya plastiki inayotengenezwa na kiwanda cha Falcon Packaging Ltd kutokana na taka za plastiki zinazokusanywa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Mwanza.

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB TAWI LA MOSHI WAFURAHIA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA.

$
0
0
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Moshi wakiwa katika picha ya pamoja ,aliyekaa ni meneja wa tawi hilo Francis Mollel.
Baadhi ya afanyakazi wa kike wa Benki ya CRDB tawi la Moshi wakiweka pozi la picha pembeni ya Keki.
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Moshi akikata keki kwa ajili ya wateja.
Keki maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa Benki ya CRDB tawi la Moshi wakati wa week ya huduma kwa wateja. 
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.

MASTERS DEGREE ANNOUNCEMENT

$
0
0
          This is to inform those who are interested that there will be an information session about a Master's Degree in Public Health Leadership (MPHL) which is planned to be held in Dar es salaam on October  21st and 22nd, 2014. There will be morning and afternoon sessions on October 21stand Afternoon session on October 22nd, 2014.
This MPHL course is under the Canada's "Save The Mothers" program that is designed in such a way that one can continue with his/her profession by taking modular courses that run for 4 modules in two years.

The Save the Mothers program offers this MASTER’S DEGREE IN PUBLIC HEALTH LEADERSHIP at the Uganda Christian University (UCU) Mukono Campus. 
The program is seeking working professionals in the fields of law, education, politics, social sciences, clergy, media, health care, and others. It enhances professional skills and influence that can be used to save mothers' lives. 
This year’s program will start in February 2015 with four modules. Each module is 4 weeks in length, and two modules are completed each year. This allows students to study and continue working in their respective professions. 
Curriculum for this course focus on the basics of public health, social factors and legalities as it relates to mothers’ health. It also gives leadership tools for participants to impact mothers’ health from their sphere of influence and profession. 
Those who are interested to attend the session please confirm your attendance by Thursday October 16, 2014 to Saida Mukhi Msumi through email: saida99tz@yahoo.com  
The Venue for the information session will be communicated after your confirmation. Please specify the time and day that you would like to attend the session; you may also state your academic background or profession.

  
Saida Mukhi Msumi

For MPHL - Save the Mothers Program



SPORAH SHOW'S EXCLUSIVE: DIAMOND PLATNUMZ LIKE NEVER BEFORE

KINANA ANYWA CHAI NYUMBANI KWA BALOZI WA SHINA, MSOSI WA MCHANA KWA MAMA LISHE IRINGA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata mlo nyumbani kwa Balozi Lucas Mtumbuka (kushoto)wa Shina namba moja eneo la Mkimbizi, alipokwenda kumtembelea yeye na wananchama wake wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Jimbo la Iringa Mjini.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akichukua mhogo ambao ni sehemu ya vyakula alivyoandaliwa na balozi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Usajili Vitambulisho vya Taifa wabishahodi Ruvuma

$
0
0
 Na Thomas William 
 Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imekutana na uongozi wa mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuweka mpango kazi madhubuti wa usajili wa watu katika mkoa huo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27, 2014. 
 Akifungua kikao hicho cha kazi Oktoba 11, 2014, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Joseph Mkirikiti amesema viongozi wa wote wa mkoa huo wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo lenye manufaa makubwa kiuchumi, kijamii na ulinzi na usalama wa Taifa letu. 
 Amesema viongozi wote wa wilaya, tarafa, kata na kijiji wanatakiwa kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenye usajili na kusimamia mwenendo mzima wa usajili katika maeneo yao ya utawala. 
 Mkirikiti amewataka viongozi wote kuwa wazalendo kwa kuhakikisha kwamba wasio Watanzania hawapati vitambulisho wanavyopewa Watanzania ikizingatiwa kwamba mkoa huo umepakana na nchi za Malawi na Msumbiji. 
 Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo, Paya Hamphrey amesisitiza viongozi hao kutekeleza jukumu la usajili kwa kuwa lipo kisheria na ni wajibu wa kila kiongozi wa wilaya, tarafa, kata na kijiji kusimamia sheria za nchi. 
 Akitoa taarifa ya utekelezaji ya NIDA, Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi amesema mamlaka inaendelea na usajili wa watu hivi sasa imekwishasajili Zanzibar, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, inaendelea na usajili Tanga na baadaye Ruvuma na Kilimanjaro. Aliwaomba viongozi hao kutoa elimu kwa wananchi wao hasa kuandaa viambatisho muhimu vinavyothibitisha uraia, umri na makazi kama vile, vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya elimu, pasi ya kusafiria, namba ya utambulisho ya mlipakodi, kitambulisho cha mpigakura na cheti cha bima ya afya na kitambulisho cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
 Pia amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili na wananchi katika mikoa mingine ambao haijafikiwa kuvuta subira kwani wote watafikiwa kulingana na ratiba ya mamlaka.
Juu na chini ni  Washiriki wa kikao kazi cha kuweka mkakati wa utambuzi na usajili wa watu wakiendelea na kikao, katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Songea, Ruvuma Oktoba 11,2014.

Msondo Ngoma Band yasherehekea Jubilee ya miaka 50 jijini Dar es salaam

Redds Miss Tanzania 2014 kujulikana usiku huu Mlimani City jijini Dar

$
0
0
 Pichani ni Washiriki waliochaguliwa kuingia kwenye hatua ya tano bora katika shindano la Redds Miss Tanzania 2014 linaloendelea hivi sasa ndani ya ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar.Picha zote na Othman Michuzi.
 Mmoja wa Washiriki waliongia katika nafasi ya tanno bora shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakijibu maswali mbalimbali
 Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya pichani kulia Ommy Dimpoz akitumbuiza jukwaani akiwa sambamba na msanii Vanessa Mdee mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani),waliofika kushuhudia shindano hilo.
Washiriki wa Redds Miss Tanzania 2014 wapatao 15 mara baada ya kuchujwa. 
 Sehemu ya baadahi ya Wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye shindano hilo la kumsaka Kinara wa Redds Miss Tanzania 2014 
Baadhi ya Washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakicheza moja ya onesho lao la ufunguzi wa shindano hilo,ambapo mshindi atatangazwa usiku huu na kujinyakulia kiasi cha shilingi miloni 18 taslim.
 Baadhi ya Washiriki wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014,wakiwa jukwaani na mavazi ya ufukweni. 
 Msaniii wa Muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee a.k.a V-Money akitumbuiza kwenye shindano la kumsaka mshindi wa Redds Miss Tanzania 2014,yanayofanyika usiku huu ndani ya moja ya ukumbi wa Mlimani,jijini Dar. 
 Washiriki wa shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakikatiza jukwaani na mavazi yao ya ubunifu
 Baadhi ya Majaji wakifuatilia kwa makini 
Pichani ni Washiriki wa Redds Miss Tanzania 2014 wapatao 30 wakiwa jukwaani tayari kwa kuanza kuchujwa kupata washiriki 15 bora. 

NGUMI KALI KUPIGWA OCTOBA 25 KATIKA UKUMBI WA FRIENDS CORNER MANZESE


ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Kala Jeremiah Featuring.Nay Wa Mitego and Mo Music -Simu ya Mwisho

salamu kutoka kwa mama bishanga na shosti yake Julie kutoka Liberia

$
0
0
Mwigizaji mkongwe wa Bongo Movie, Bi Christina Innocent  Marolen, almaarufu kama "Mama Bishanga",  na mfanya kazi mwenzake kutoka Liberia wanonekana wakiwa kazini, Adern Court Alzheimer Home Care huko Ohio, Marekani, wakifurahia uamuzi wa madaktari watano wa Tanzania wanokwenda kuongeza nguvu ya kusaidia kuwatibu raia wa Liberia, baada ya kusoma taarifa hizo kwenye magazeti ya Tanzania. 
Julie Blanton ambae alikuja Amerika miaka mingi mara baada ya vita iliotokea Liberia miaka ya themanini na tisini, huwa anenda kwao kila mwaka kusalimia ndugu zake. 
Julie ameshukru sana Rais Kikwete na watanzania kwa ujumla kwa moyo wao wa upendo na kusaidia nchi nyingine tangia miaka sana iliopita katika nyanja mbali mbali, ikiwa ni pamoja na vita vya ukombozi barani Afrika. Kasema GOD BLESS ALL TANZANIANS.
Mama Bishanga (kulia) na shosti yake Julie pia wanawapa mkono wa herI ya kuzaliwa/ happy birth day  mwanae Kenny @ Henrich na Rais Jakaya  Kikwete, Bishop Desmund Tutu wa Afrika Kusini na wote waliozaliwa tarehe saba mwezi huu wa Oktoba. Kasema  Mungu awaongezee upendo na nguvu ya kufanya kazi na kulitumikia taifa.

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MEJA JENERALI MSTAAFU MUHIDDIN MFAUME KIMARIO MJINI MOSHI

$
0
0
 
 Ma-Meja wakiwa wamebeba Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Meja Jenerali mstaafu wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) huku wakisindikizwa Ma-Kanalki wakiwasili katika makaburi ya Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro Jumamosi Oktoba 11, 2o14

  Rais kikwete akiwa na Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya (kushoto kwa Rais) na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Ibrahim Msengi (kulia) na Meja Jenerali  Ezekiel  Kyunga, mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange (kulia kwa Rais) wakati mwili wa marehemu Meja Jenerali Mstaafu Muhiddin Mfaume Kimario ukiwasili katika makaburi ya Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro Jumamosi Oktoba 11, 2o14
 Mwili wa marehemu ukiwasili katika makaburi ya Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro Jumamosi Oktoba 11, 2o14
 Rais Jakaya  Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Meja Jenerali Mstaafu Muhiddin Mfaume Kimario wakati wa mazishi katika makaburi ya Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro Jumamosi Oktoba 11, 2o14
 Rais Kikwete akimfariji mjane wa marehemu alipokwenda kutoa pole baada ya mazishi
  Rais Kikwete akiwafariji familia  wa marehemu alipokwenda kutoa pole baada ya mazishi
 Rais Kikwete akiendelea kuwafariji familia  wa marehemu alipokwenda kutoa pole baada ya mazishi
 Rais Kikwete akiweka sahihi kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Meja Jenerali Mstaafu Muhiddin Mfaume Kimario mjini Moshi Jumamosi Oktoba 11, 2014
 Waombolezaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Meja Jenerali mstaafu wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) Marehemu Muhiddini Kimario katika  makaburi ya manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mazishi Jumamosi Oktoka 11, 2014.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Meja Jenerali mstaafu wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) Marehemu Muhiddini Kimario katika  makaburi ya manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mazishi Jumamosi Oktoka 11, 2014. PICHA NA IKULU

Mwili wa marehemu Dkt William Shija wawasili nchini leo kutoka London, Uingereza

$
0
0
 Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Dkt William Shija aliyefariki dunia tarehe 4 Oktoba 2014 umewasili nchini leo.
 Ndugu, jamaa na marafiki wakimfariji mama Getrude Shija mara alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar Es salaam.
  Ndugu, jamaa na marafiki wakimfariji mama Getrude Shija mara alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar Es salaam.
Msalaba
 Sehemu ya waombolezaji. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

TAARIFA YA MSIBA

$
0
0
Mwenyekiti wa African Stars Entertainment (ASET) Baraka Msiilwa anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake Bi Furaha Ramadhani Baraka (pichani),kilichotolea wikiendi hii mjini Liege,Ubelgiji.

 Mipango inafanywa kuurejesha mwili wa marehemu nyumbani kwa mazishi. 

Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo

-Amina
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images