Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live

MSANII WA FILAMU NCHINI,SINGLE MTAMBALIKE AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

$
0
0

 Single Mtambalike 'Richie'. 

MSANII wa maigizo na filamu nchini,Single Mtambalike maarufu kwa jina la Richie, amefiwa na baba yake mzazi Mzee Mtambalike usiku wa kuamkia leo, Msiba upo nyumbani kwao Tabata,jijini Dar es salaam. 

Rais Kikwete aweka jiwe la Msingi Barabara Usagara -Kisesa,pia afunngua Daraja la Mabatini

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya kilometa 16 kutoka Usagara hadi Kisesa mkoani Mwanza leo.Rais Kikwete yupo mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua daraja la Nyashishi lenye urefu wa mita 67 lililopo katika barabara ya Usagara Kisesa wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara kilometa 16 ya Kisesa hadi Usagara inayojengwa kwa kiwango cha lami leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzibdua rasmi daraja la waenda kwa miguu Mabatini Mkoani Mwanza leo.Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli.
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli akimuongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kukagua daraja la waenda kwa miguu huko Mabatini Mkoani Mwanza leo muda mfupi baada ya kulifungua leo.
Muonekano wa Daraja la waenda kwa miguu liliojengwa Mabatini huko Mwanza lililozinduliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo. (picha na Freddy Maro)

SHIWATA kumuenzi Mwalimu Nyerere

$
0
0
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa ibada maalum ya kumkumbuka Baba wa taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere itakayofanyika katika mashamba yao yaliyopo kijiji cha Ngarambe, Mkuramga mkoa wa Pawani.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana kuwa katika ibada hiyo itaongozwa na Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum kwa upande wa Waislam na Padri John Solomon kwa upande wa Wakristo.

Taalib alisema katika ibada hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Silla na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wamealikwa kuhudhuria ambayo itakuwa sambamba na ugawaji wa mashamba kwa wanachama ambao wamekubali kulima katika shamba la SHIWATA lenye ekari 500.

Alisema SHIWATAitaendelea kuenzi fikra za Hayati Mwalimu Nyerere alizowahi kuzifanya na kuziendeleza wakati wa uhai wake ambako wasanii waliitikia mwito kwa kuanzisha kijiji chao cha Mwanzega chenye ukubwawa hekari 300 za makazi ambako mpaka sasa zimejengwa nyumba 66 na nyingine zinajengwa na kukabidhiwa Desemba mwaka huu.

Alisema SHIWATA yenye wanachama zaidi ya 8,000 imekuwa ikihamasisha wanachama wakewajenge nyumba katika kijiji chao ambacho Serikali imekitambua rasmikwa kukizindua kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru Julai mwaka huu.

Ofisa Habari wa SHIWATA

Airtel yahitimisha wiki ya huduma kwa wateja

$
0
0
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imehitimisha wiki hii inayosherehekewa duniani kwa kuwatembelea wateja wake mbali mbali na kuwashukuru kwa kutumia huduma na bidhaa zake.

Airtel imetembelea wateja wake katika maeneo mbalimbali ikiwa pamoja na Tandika, magomeni, Temeke , sinza, Mbagala, illala , kinondoni na katika maeneo yenye watu wengi na kuongea nao kwa nyakati tofauti lengo likiwa ni kupata maoni juu ya huduma na pia kuwaelimisha kuhusu huduma na ofa mbalimbali.

Alikadhalika wakurugenzi wa Airtel walitembelea wateja katika ofisi zao na kutembelea call center kituo cha kuhudumia wateja waaopiga simu na kuongea na wateja wanaopiga namba 100 kwa msaada zaidi.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha wiki hii Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Bi Adriana Lyiamba alisema” tumekuwa na wiki ya mafanikio makubwa kwani tumepata nafasi nzuri ya kuendelea kuonana na kuongea na wateja wetu ana kwa ana na kuwazawadia ikiwa ni kuwashukuru kwa kuwa pamoja nasi na kutumia huduma zetu.

Tunaahaidi kuendelea kutoa huduma bora zilizo za kisasa na za kibunifu huku tukitoa huduma kwa wateja zenye uzoefu tofauti kupitia kituo chetu cha kupokea simu (call center) maduka yetu na sehemu zote ambazo wateja wanapata huduma zetu. Tunapomaliza wiki hii maalumu kwa huduma kwa wateja tunapenda kuwahakikishia watanzania huduma bora kwani tunatambua huduma bora ni mwendelezo wa maisha ya kila siku na si kwa wiki hii tu.

Akiongea wakati alipotembelewa ofisini kwake Bwana Aliasger Hussein Gomberawala alisema” tunafurahi kwa uongozi wa Airtel kuwa nasi leo hapa, tumekuwa wateja wa Airtel kwa muda na tunafurahishwa na huduma zao kwa ujumla, matatizo ya kimtandao katika technologia hii yapo mengine ni ya uelewa wa vifaa vya kisasa na technologia hivyo elimu inatakiwa kutolewa ili wateja waende sambamba na mabadiliko haya.

Tunaomba Airtel waendelee kutuletea huduma za kibunifu na kuendelea kupunguza gharama za mawasiliano kwani tunategemea sana haya mawasiliano katika kuendesha biashara zetu.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (katikati), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Kassim Mtingwa (wa tatu kushoto) na Meneja Uendeshaji Huduma kwa Wateja, Amit Arora wakikata keki kama ishara ya kufunga Wiki ya Huduma kwa Wateja katika hafla iliyofanyika kwenye Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Airtel kilichopo Quality Centre Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kushoto), akitoa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo wakati wa kufunga Wiki ya Huduma kwa Wateja, katika hafla iliyofanyika kwenye Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Airtel kilichopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kushoto), akimkabithi kifurushi cha zawadi mteja wake Bwana Aliasger Hussein wakati Airtel ilipotembelea wateja wake katika wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wakiwa na maongezi na Bwana Aliasger Hussein wakati Airtel ilipomtembelea ofisini kwake katika wiki ya huduma kwa wateja. pichani ni Meneja huduma kwa wateja Jacob Sumary na Afisa huduma kwa wateja bi Neifita Olomi.

MAAFISA ELIMU WILAYA WAFUNDWA KUHUSU BRN

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Utekelezaji cha MIradi ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Grace Hoka akitoa maelezo kuhusu miradi ya elimu kwa Maafisa Elimu Wilaya (hawapo Chuo cha Adem mjini Bagamoyo leo.
Meneja wa Sekta ya Elimu katika Kitengo cha Rais cha Usimamizi wa Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Jenifa Mhando akitoa maelezo kuhusu BRN na miradi ya elimu kwa Maafisa Elimu Wilaya (hawapo pichani) katika kikao chao kilichomalizika kwenye Chuo cha Adem mjini Bagamoyo leo.
Sehemu ya Maafisa Elimu Wilaya wakifuatilia mada kuhusu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika elimu zilizokuwa zikiwasilishwa na watendaji kutoka Ofisi ya Rais-Kitengo cha Usimamizi wa Miradi ya BRN (hawapo pichani).

Tanzania yawakilishwa katika Mkutano wa Wabunge Vijana kutoka Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mjini Geneva,Uswis

$
0
0
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa Makini Mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mkutano wa Wabunge Vijana kutoka Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini Geneva Uswis. Kutoka kulia ni Mhe. Ester Bulaya, Mhe. Godfrey Mgimwa na Mhe. Neema Hamid. Mkutano huo pamoja na Mauala mengine unajadili changamoto wanazokabiliana nazo Wabunge Vijana hususani wanawake katika siasa.
Mkutano huo ukiendelea.
Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika Picha ya Pamoja baada ya Kumalizika kwa siku ya Kwanza ya Mkutano huo. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe ajisalimisha kwenye Baraza la Maadili na kupewa onyo, Nchambi apewa nafasi kufika kikao

$
0
0
Na. Ally Mataula – Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma

Wakati Vikao vya Baraza la Maadili vikiendelea siku yake ya pili kusikiliza mashauri ya ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995, Baraza hilo likiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Balozi Jaji (Mst.) Hamisi Msumi limetoa onyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Mrisho Gambo kwa kukaidi wito wa kufika mbele ya Baraza hilo kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Hassan Mayunga ambaye alilieleza Baraza kuwa wao kama Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wamejiridhisha kuwa wito wa kuitwa mbele ya Baraza hilo ulimfikia Mlalamikiwa zaidi ya wiki tatu kabla ya kuanza vikao vya Baraza na hivyo Mhe. Gambo amelidharau Baraza kwa kitendo chake cha kutofika tarehe 9/10/2014. Hata hivyo, Bw. Mayunga aliliomba Baraza hilo kuahirisha shauri hilo mpaka Jumatatu tarehe 13 Oktoba, 2014.

Naye Mhe. Gambo alipopewa nafasi ya kujitetea kwa kitendo chake cha kukaidi wito wa kufika mbele ya Baraza alisema kuwa wito wa kumtaka yeye kufika mbele ya Baraza haukumfikia kutokana na yeye kuwa nje ya kituo chake cha kazi na badala yake alipata taarifa ya kutakiwa kukamatwa kupitia vyombo vya habari. Mhe Gambo aliendelea kulieleza Baraza kuwa hakuwa na sababu ya yeye kukaidi wito huo na kwamba baada ya kupata taarifa kupitia vyombo vya habari aliwasiliana na Katibu Muhtasi wake ambaye alimuagiza afungue barua zote zilizofika ofisini kwake kwa jina lake na kama kuna barua kutoka Tume ya Maadili amtumie kwa njia ya fax. Mhe. Gambo alisema kuwa baada ya kutumiwa barua hiyo alianza safari ya kuja Dar es Salaam kuitikia wito wa Baraza.

Akitoa hitimisho kuhusu shauri hilo, Mhe. Jaji Msumi alisema kuwa amri ya kukamatwa mlalamikiwa imefutwa. “Mlalamikiwa amepewa onyo la kumtaka kutii amri ya kisheria ya Baraza. Shauri litasikilizwa tarehe 13/10/2014 saa tatu asubuhi” alisema Mhe. Jaji Msumi.

Kuhusu Shauri linalomhusu Mbunge wa Kishapu Mhe. Suleiman Masoud Nchambi Suleiman ambaye analalamikiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kutowasilisha Tamko la Mali na Madeni kwa kipindi cha mwaka 2012 halikusikilizwa kutokana na Mhe. Nchambi kutofika mbele ya Baraza hilo. Mhe. Nchambi ambaye shauri lake liliahirishwa kusikilizwa katika vikao vya Baraza vilivyofanyika mwaka jana 2013 katika Manispaa ya Tabora hakuweza kufika katika vikao vya Baraza vinavyoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee bila taarifa rasmi ya maandishi.

Kwa Mujibu wa Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bibi Mwanarabu Talle ambaye aliliambia Baraza kuwa Mlalamikiwa anaonekana kuwa ni mkaidi hivyo alipendekeza Baraza kutumia fungu la 24 (4) la Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na 13 ya 1995 ambalo linatoa mamlaka kwa Mwenyekiti kutoa hati ya kukamatwa Mlalamikiwa na Afisa wa Polisi na kufikishwa mbele ya Baraza.

Akihitimisha Shauri hilo Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Jaji Msumi alisema kuwa hii ni mara ya pili kwa Mlalamikiwa kuomba usikilizwaji wa lalamiko lake kuahirishwa.

“Baraza lina wasiwasi kuwa huenda Mlalamikiwa ametumia mbinu za kuchelewesha lalamiko hili. Hata hivyo tunaona ni busara tutoe muda mwingine ambao utakuwa ni wa mwisho. Hivyo lalamiko linahairishwa hadi kikao kijacho. Mlalamikiwa afahamishwe kuwa Baraza halitakubali sababu yeyote tena ya kuahirisha lalamiko hili” Alifafanua Mhe. Msumi.

Kwa upande mwingine, Baraza la Maadili limeweza kusikiliza mashauri mengine yanayowahusu viongozi watatu ambao ni Bw. Venance Kenneth Ngunga – Mhasibu Mkuu, Taasisi ya Technoloji Dar Es Salaam (DIT), Mhe. Mohamed Ally Chambuso – Diwani Kata ya Mzimuni na Bibi Florence Sastony Masunga – Diwani Viti Maalum, Kinondoni, wote walikuwa wanalalamikiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kushindwa kuwasilisha Tamko la Mali na Madeni kwa mujibu wa Sheria.

Pia, Mhe. Msumi ametoa hati ya kukamatwa na kufikishwa mbele ya Baraza hilo Bibi Sarah Kinyamfura Barahomoka ambaye ni Mkurugenza Msaidizi – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kukaidi wito wa kufika mbele ya Baraza kujibu tuhuma zinazomkabili. Kwa mujibu wa ratiba, vikao vya Baraza la Maadili vitaendelea tena siku ya Jumatatu tarehe 13 Oktoba, 2014.
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuahirishwa kusikilizwa Shauri lake mbele ya Baraza la Maadili.
Afisa Sheria Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Filotheus Manula akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu yaliyojiri katika Baraza la Maadili katika siku yake ya pili ya kusikiliza mashauri yanayohusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

MH. MWANJELWA AMWAKILISHA VYEMA KATIBU MKUU WA CCM TAIFA, AWASILISHA MABATI 40 ALIYOAHIDI KATA YA NSALAGA MBEYA

$
0
0
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, (CCM),akikabidhi mabati 40, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, ambaye aliahidi Desemba 4, 2013, alipotembelea Jijini Mbeya na kuona jitihada za wanachama wa CCM wa kata hiyo kujenga ofisi nzuri.
Baadhi ya wananchi wakimpongeza na kumshukuru Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, (CCM),baada ya kufikisha salama mabati 40, ambayo Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, aliahidi Desemba 4, 2013, alipotembelea Jijini Mbeya na kuona jitihada za wanachama wa CCM wa kata hiyo kujenga ofisi nzuri.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa, (CCM), akizungumza na wanachama wa CCM na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wake wa kukabidhi mabati 40, ambayo Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana, aliahidi Desemba 4, 2013, alipotembelea Jijini Mbeya na kuona jitihada za wanachama wa CCM wa kata hiyo kujenga ofisi nzuri. Dr. Mwanjelwa, pia yeye alichangia kiasi cha Tsh.200,000/= na kuahidi kutoa mifuko 20 ya saruji.

kwa picha zaidi tembelea libeneke lake kwa 

BUNGE KUPIGIA KURA KATIBA MPYA NI ISHARA YA KUIMARIKA KWA UTAWALA BORA - MUKASA

$
0
0
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Lilian Mukasa akisoma hotuba katika kikao cha Kamati ya Sita ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani

Na. Ally Kondo, New York
Serikali imesema kuwa mchakato wa kuandaa Katiba mpya ambayo imepitishwa na Bunge Maalum la Katiba hivi karibuni ni ishara ya wazi kuwa, Serikali imedhamiria kuongoza nchi kwa mujibu ya matakwa ya wananchi wake na kuzingatia Utawala wa Sheria.
Kauli hiyo ilitolewa na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Lilian Mukasa alipokuwa anahutubia Kamati ya Sita ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani siku ya Ijumaa tarehe 10 Oktoba 2014.
Bibi Mukasa aliwambia wajumbe wa Kamati hiyo hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kuhakikisha kuwa huduma za kisheria ambazo kwa kawaida zina gharama kubwa, zinawafikia wananchi, hata wale wenye kipato cha chini.
Hatua hizo ni pamoja na kuongeza idadi ya wanasheria wa Serikali, majaji, mahakimu, kujenga mahakama mpya na kuzifanyia ukarabati zile za zamani.
Aidha, Serikali imekuwa ikiboresha huduma za kiamahakama mara kwa mara na hivi sasa inakusudia kuanzisha mpangoutakaowawezesha wananchi kupata huduma za kisheria kupitia simu zao.
Hatua nyingine ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya Mawakili wa kujitegemea pamoja na kuanzisha Shule ya Sheria ambayo inatoa mchango mkubwa katika sekta hiyo. Aidha, Serikali imekuwa na uataratibu wa kuzihamasisha Kampuni za uwakili zilizoimarika ili zisaidie kutoa msaada wa kisheria bure kwa watu masikini na makundi maalum,
Bibi Mukasa aliendelea kueleza kuwa Serikali inatambua nafasi ya mifumo ya sheria katika maendeleo ya nchi, uundaji wa Serikali, ulindaji wa kanuni za demokrasia kupitia Katiba, kulinda haki za binadamu na kutoa miongozo katika mgawanyo warasiliamali. Hivyo, katika nchi yenye mfumo wa sheria unaotambulika na utawala wa sheria ulioimarika, maendeleo na demokrasia pia vinaimarika.
Alibainisha kuwa ili haki ipatikane lazima kila mtu katika jamii husika awe na nafasi sawa katika vyombo vya sheria. Vikwazo vyovyote kama vile kutojua kusoma na kuandika, umasikini, urasimu katika vyombo vya sheria, upungufu wa fedha na wataalamu wa sheria, matumizi mabaya ya madaraka kwa wanasiasa pamoja na matajiri vyote vinakwamisha maendeleo.
Vikwazo hivi, pamoja na vingine ni changamoto kubwa katika nchi zinazoendelea. Katika jitihada za kukabiliana nazo, Serikali ya Tanzania imeanzisha Kitengo cha Msaada wa Sheria katika Wizara ya Katiba na Sheria ambacho jukumu lake ni kuhakikisha kuwa kinatoa msaada wa sheria kwa wanaohitaji.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Christian Bella Featuring Ommy Dimpoz - Nani Kama Mama

GODTEC yasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa Vijana

$
0
0
Meneja wa POSO Kanda ya Ziwa Bw. Emmanuel Kisamba (kushoto) akitoamaelezo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Kampuni ya GODTEC katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani humo kuelekea Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Miaka 15 ya Kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PAFRI Bw. Boniphace Alex akitoa maelezo namna ya jiko lilotengenezwa na Kampuni yake linavyofanya kazi, kwa vijana waliotembelea banda la Kampuni ya GODTEC katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani humo kuelekea Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Miaka 15 ya Kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.Katikati ni Afisa Uhusiano wa Bega kwa Bega Microfinance Bibi. Dorcas David Mlapa na Afisa Mtendaji Mkuu wa PAFRI Bw. Boniphace Alex.
Baadhi ya wafanyakazi wa GODTEC na Bega kwa Bega Microfince wakitoa huduma katika banda lao wakati wa Maonyesho katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani humo kuelekea Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Miaka 15 ya Kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere. Picha na Frank Shija, Tabora

Serikali itaendelea kuimarisha Maisha ya Wananchi - Ellen Maduhu

$
0
0
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bibi Ellen Maduhu akisoma hotuba katika Kamati ya Tatu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Na. Ally Kondo, New York


Serikali imetahadharisha kuwa endapo mchakato wa kuandaa Agenda ya Maendeleo baada ya Mwaka 2015 unaoendelea hivi sasa katika Umoja wa Mataifa, hautazingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu, dhamira ya kufikia maendeleo endelevu itakuwa ni ndoto kwa kuwa katika kila idadi ya watu watano duniani, mmoja wao ana ulemavu.


Kauli hiyo ilitolewa na Bibi Ellen Maduhu, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, alipokuwa anahutubia wajumbe wa Kamati ya Tatu ya Umoja huo jijini New York, Marekani siku ya Jumatano tarehe 08 Oktoba 2014.


Bibi Maduhu alieleza kuwa wakati utekelezaji wa Malengo ya Milenia unafikia kikomo mwaka 2015, ni muhimu watu wenye ulemavu wakashirikishwa kikamilifu katika shughuli za maendeleo. Aidha, ni vema nchi zikawa na utaratibu mzuri kuhakikisha kuwa kundi la watu wenye ulemavu linafaidika na hatua za maendeleo zinazopigwa, kwa kuwa hiyo ni haki yao na ni wajibu wakapatiwa.

PSPF YATOA MSAADA WA KOMPYUTA 12 KWA VYUO VIWILI BAGAMOYO

$
0
0
 Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani kushoto Akimkabidhi Msaada wa Kompyuta Mkuu wa Chuo Kikuu teule cha Marian Father Luke Mbefo  ambapo Kompyuta hizo zitatumika katika Kuhifadhi Nyaraka mbalimbali za Maktaba
 
 Mkuu wa Chuo Kikuu teule cha Marian Father Luke Mbefo  kulia akimshukuru Afisa Mahusiano wa PSPF Bi. Coleta Mnyamani kwa msaada huo
 Afisa Mahusiano wa PSPF Bi. Coleta Mnyamani akizungumza neno Baada ya kukabidhi Msaada huo
Kulia ni Meneja wa Pwani wa PSPF Msafiri S. Mugaka akimkabidhi Kompyuta 10 Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Dkt. Ally S. Mcharazo kwa niaba ya chuo hicho
Meneja wa Pwani wa PSPF Msafiri S. Mugaka  akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ukutubi,Uhifadhi wa Kumbukumbu pamoja na wagani waalikwa wakati wa kukabidhi msaada huo wa kompyuta 10 za kisasa

ADHA YA UKEKETAJI TANZANIA KUJADILIWA NA WABUNGE UINGEREZA

$
0
0
Na Freddy Macha

Jumatano ijayo tarehe 15 Oktoba, 2014...kundi la kina mama watatu akiwemo Mtanzania litashiriki jopo la ukeketaji na Wabunge, London, Uingereza.

Mtanzania, Rhobi Samwelly, mama wa watoto wanne, ni mzawa wa Butiama, Mara. Wenzake ni Comfort Momoh, toka Nigeria, anayetibu wanawake waliokeketwa hospitali mbili za Guy’s na St Thomas, London na Ann-Marie Wilson mkurugenzi wa “28 Too Many.” Shirika hili lenye tovuti yenye http://28toomany.org/ ni maktaba kubwa yenye habari, picha, utafiti na uchunguzi wa ukeketaji duniani.
Bango linalotumika kuchangia makutano na hafla mbalimbali za fedha za ujenzi wa nyumba ya hifadhi ya wasichana Mugumu, Mara

Mwaka1997 Comfort Momoh alianzisha msururu wa shughuli za kuwasaidia akina mama waliokeketwa likiwemo shirika la African Well Women’s Clinic. Bi Momoh mwenye shahada ya uzamili (MA) ni mshauri wa shirika la Afya duniani (WHO) kuhusu adha ya ukeketaji.

Mtanzania Rhobi na Ann-Marie walikuwa baadhi ya wazungumzaji kwenye hafla iliyofanywa Alhamisi na Jumamosi iliyopita kuchanga fedha za kujenga nyumba ya hifadhi kwa wasichana wanaokimbia ukeketaji, Mugumu, Mara.

MH. MAHENGE AFANYA ZIARA KATIKA MGODI WA NORTH MARA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mhe. Dkt. Binillith S.Mahenge akipewa maelezo na Mkuu wa Wilaya ya Tarime alipowasili ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya kikazi katika Mgodi wa North Mara ulioko Wilaya ya Tarime.
Meneja wa Mazingira Mgodi wa North Mara Bwana Thomas Morris akitoa Maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mhe. Dkt. Binillith S.Mahenge (hayupo pichani) alipotembelea Mgodi wa North Mara kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika maeneo ya migodi nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mhe. Dkt. Binillith S.Mahenge (wa tatu kutoka kushoto) akipewa maelezo na Meneja Mazingira Bwana Thomas Morris kuhusu mitambo ya kuteketeza taka zenye sumu zinazozalishwa katika mgodi wa North Mara. Wa pili kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Bwana Gary Chapman.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mhe. Dkt. Binillith S.Mahenge akipewa maelezo ni jinsi gani wanavyoweza kusafisha Maji kwa Mitambo ya kisasa katika Mgodi wa North Mara.

Ubalozi Wa Tanzania Japan Waipaisha Kahawa Kilimanjaro Kwenye Treini Ziendazo Kasi Japan

$
0
0
Kahawa ya Tanzania imekuwa kivutio kikubwa kufuatia ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania Japan na Kampuni binafsi ya M.M. (wauzaji wakubwa wa kahawa ya Kilimanjaro Japan) kuandaa “Special Premium kilimanjaro Coffee Brand ” na kuingia makubaliano na Shirika kongwe la treini ziendazo kasi (Bullet Train) la Tokaido JR Shinkansen. Kahawa hiyo imekuwa kiburudisho kikubwa kwa wasafiri wote wanaotumia usafiri huo ambao ni maarufu sana Japan katika miji mbalimbali. Kwa watumiaji wa usafiri huo wanapoingia katika treini hizo unakaribishwa na matangazo maalum kuhusu kahawa hiyo.

Tanagazo la kahawa hii linasomeka kama ifuatavyo :

“ In commemoration of the 50th Anniversary of the JR (Japan Railway) Tokaido Shinkansen, we deliver this grade AA Kilimanjaro Coffee from Tanzania which also celebrates its 50th anivessary of the country founding. Please enjoy the fresh acidity and flavor this cup featuring designs from Tingatinga Art of Tanzania”

Kahawa hii maalumu imetengenezwa mahususi kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 tangu kuzinduliwa wa treini ya kwanza iendayo kasi Japan sambamba na Tanzania kusherehekea miaka 50 ya Muungano.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania Japan
Octoba, 2014

Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki akagua miradi ya maendeleo inayosimamiwa na Mradi wa Kuifadhi Mazingira wa Ziwa Victoria LVEMP II

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Juma Abdulla Saadala jana alishindwa kuzindua Mashine ya kuchakata Alizeti iliyotolewa na Mradi wa kuifadhi Mazingira wa Ziwa Victoria LVEMP II kwa sababu ya kuwa na kasoro ndogo ndogo za kiufundi na utendaji.

Akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Kilulu nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Mhe. Juma alisema ikiwa ni ahadi yake ya kuzindua mashine hiyo lakini ameshindwa kufanya hivyo baada ya kutokeza kasoro za kiufundi na ya kiutendaji.

Ahadi hiyo aliitoa mwezi Aprili mwaka huu alipokwenda kuzindua jengo la mradi huo lakini ameshangazwa na kitendo cha msimamizi wa mradi huo chini ya Halmashauri pamoja na kamati ya Kijiji kushindwa kukamilisha taratibu zote ambazo zingewezesha Mashine hiyo kufanya kazi.

Pamoja na Mashine hiyo ya kuchakata Alizeti lakini pia Kijiji hicho kimepatiwa trekta moja ya kuwasaidia wananchi kuendesha kilimo chao katika harakati za kunusuru mazingira ya Mto Simiwi ambao kutokana na wananchi kuendesha kilimo kando ya Mto huo umekuwa ukipeleka matope mengi Ziwa Victoria wakati wa mvua nyingi.

Trekta na Mashine ya kuchakata na kukamua alizeti itawawezesha Wanachi wa Kijiji cha Kilulu kuondokana na Umasikini lakini pia kunusuru mazingira ya mto Simiwi ambao humwaga maji katika Ziwa Victoria.

Mradi wa LVEMP II umekuwa ukitoa misaada ya kimaendeleo kwa jamii zinazozunguka mto Simiwi ili ziondokane na kilimo kandokando ya mto huo kwani kilimo kando ya mto huo kimekuwa kikichangia athari kubwa za kimazingira katika ziwa Victoria ikiwemo kupeleka matope mengi kwenye Ziwa hilo.

 Dkt. Juma yuko katika Mkoa wa Mwanza kutembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa chini ya Mradi wa kuifadhi Mazingira ya Ziwa Victoria LVEMP II ambao kwa kiasi kikubwa unafadhiliwa na Benki ya Dunia chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Juma Abdulla Saadala akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Kilulu nje kidogo ya Mji wa Bariadi alipowatembelea kukagua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Mradi wa Kuifadhi Mazingira wa Ziwa Victoria LVEMP II.
Trekta iliyotolewa na Mradi wa Kuifadhi Mazingira wa Ziwa Victoria LVEMP II kwa Wananchi wa Kijiji cha Kilulu kama hatua mojawapo ya kuifadhi mazingira ya mto Simiwi. Wanachi hao wanatakiwa kuacha kuendesha kilimo chao kandokando ya mto huo.
Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Juma Abdulla Saaadala akikagua mashine ya kuchakata alizeti iliyotolewa kwa Wananchi wa Kijiji cha Kilulu nje kidogo ya Mji wa Bariadi na Mradi wa Kuifadhi Mazingira wa Ziwa Victoria LVEMP II.

NHIF Yawapongeza Viongozi wa Dini kwa kuhamasisha kaya kujiunga na CHF

$
0
0
Meneja Mwandamizi wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Kanda ya Magharibi – Tabora Bw. Emmanuel Adina (kushoto) akifafanua jambo kwa Afisa Habari wa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Jonas Kamaleki alipofanya mahojiahano naye kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii unavyo nufaisha Vijana wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana inayofanyika Kitaifa Mkoani Tabora.
Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bibi Catherine Kameka akielezea jambo kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa wananchi walitembelea banda lao wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika Kitaifa Mkoani Tabora.
Baadhi ya wananchi wakipata huduma ya upimaji wa Afya inayotolewa bure na Mfuko wa Taifa waBima ya Afya (NHIF) katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayoendelea mjini Tabora. 

KINANA, NAPE WASHIRIKI UVUNAJI CHAI,MUFINDI

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakishiriki kuvuna majani ya chai, katika shamba la Uniliver, eneo la Ngwazi, katika wilaya ya Mufundi mkoani Iringa, leo Oktoba 10, 2014. Kinana yupo katika ziara ya mkoa huo, kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM. (Picha na Bashir Nkoromo).

Rais Kikwete afungua jengo la PPF Mwanza

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la mfuko wa pensheni la PPF mjini Mwanza jana jioni.Wengine katika picha kutoka kushoto,ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana Wiliam Erio, Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Adam Malima, Mwenyekiti wa Bodi ya PPF Bwana Ramadhani Kija, na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo.
Jengo la Kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa PPF lililozinduliwa rasmi na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mjini Mwanza jana jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio wakiangalia madhari nzuri ya jiji la Mwanza wakiwa katika jengo jipya la kitega uchumi la mfuko wa pensheni wa PPF muda mfupi baada ya kulizindua mjini Mwanza jana jioni.
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PPF Bwana Ramadhani Kija(watatu kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio(kulia) wakimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuzindua jengo la kitega uchumi la PPF mjini Mwanza jana jioni.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio akitoa maelezo kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ndani ya mgahawa uliopo katika jengo jipya la kitega uchumi la PPF muda mfupi baada ya kulizindua rasmi mjini Mwanza.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Shirika la PPF baada ya kuwa amezindua Jengo la Kitega Uchumi la Shirika hilo katikati ya Jiji la Mwanza jana, Ijumaa, Oktoba 10, 2014. Rais Kikwete yuko katika ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Mwanza.(picha na Freddy Maro)
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live




Latest Images