Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 604 | 605 | (Page 606) | 607 | 608 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Marehemu Omar Ndege Mgori

  Mwili wa marehemu Omar Ndege Mgori unaondoka leo hii huko nchini India na utapokelewa siku ya Jumapili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere Dar es salaam Saa Saba mchana siku hiyo.

  Mazishi yatafayika siku ya jumatatu Oktoba 13,2014 kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.

  Msiba kwa sasa upo Mbezi beach nyumbani kwa marehemu.

  Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa pindi zitakapo kuwa zikitufikia.

  0 0


  Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili,Lillian Kamazima (kulia) na Mshindi wa Tatu,Jihhan Dimachk mara baada ya kutawazwa rasmi usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.Sitti Mtemvu alianza kwa kunyakua Redds Miss Chang'ombe na baadaye Redds Miss Temeke. Sitti ni binti wa Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu.
  Picha zote na Othman Michuzi.
  Habari kamili na mapicha kibao yatafuata.

  0 0

   Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime akifikishwa mahakamani wakati wa hatua za awali za kesi hiyo.
   ------------------------
  Na Mwene Said wa Globu ya Jamii
   MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imefuta  mwenendo wa kesi ya mauaji iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini dhidi aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime na wenzake 11, wanaohusishwa na kuporomoka kwa jingo la ghorofa 16 katika mtaa wa Indira Gandh na kuua watu 27 badala yake wafunguliwe mashitaka ya kuua bila kukusudia.
   
  Akisoma uamuzi huo,Jaji Salvatory Bongole Ijumaa iliyopita baada ya kukubaliana na hoja zilizowasilishwa mbele yake na mawakili wa upande wa utetezi kuwa na mashiko ya kisheria. Jaji Bongole aliamuru washtakiwa kuendea kushitakiwa kwa makosa ya zamani ya kuua bila kukusudia na siyo makosa ya mauaji.
   
  Alisema washtakiwa wanastahili kuendelea kuwa nje kwa dhamana zao kama livyokuwa kabla upande wa Jamhuri kubadilisha hati ya mashitaka yao Marchi 12, mwaka huu kutoka mauaji ya bila kukusudia na kuwa kesi ya mauaji ya kukusudia.
   
   Jengo lililoporomoka Marchi 29, mwaka 2013 katika mtaa wa Indira Gandhi ulioko katika wilaya ya Ilala, jijijini Dar es salaam na kuua watu 27. 
  Jaji alitupilia hoja za upande wa Jamhuri ulikuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Bernard Kongola kuwa hati ya mashitaka ya mauaji ya kukusudia iliyowasilishwa mahakamani ilikuwa sahihi na inajitosheleza kuwawezesha washitakiwa kupanga utetezi wao. Katika uamuzi wake uliopokelewa kwa shangwe na washitakiwa na ndugu zao waliokuwa wamefurika katika viunga vya  Mahakama Kuu, Jaji Bongole alisema kuwa kitendo cha kubadilisha mashitaka kutoka mauaji ya bila kukusudia hadi mauaji ya kukusudia kulifanywa kwa nia mbaya na upande wa Jamhuri.
   
  Alieleza kuwa upande wa mashitaka ulikuwa na nia ya kuwafanya washtakiwa wabaki rumande na hii ilidhihilishwa tangu awali pale walipofikishwa kwa mara ya kwanza kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia na upande wa mashitaka ukapinga dhamana.
   
  Mara baada ya Mahakama ya Kisutu kuwapa washtakiwa dhamana upande wa Jamhuri ulikata rufaa kupinga dhamana hiyo. Hata hivyo, Jaji Bongole alifafanua kuwa upande wa Jamhuri uliachana na rufaa hiyo mara baada ya mwaka mmoja kupita uliwasilisha Mahakama ya Kisutu maombi ya kubadilisha hati ya mashitaka ya mauaji ya kukusudia.
   
  “Mabadiliko haya hayakufanywa kwa nia njema bali yalilenga kuwanyima haki washtakiwa… Vitendo vya makusudi vya namna hii havikubaliki na vinapaswa kukoma mara moja,” alisisitiza jaji huyo wakati akisoma uamuzi wa kuwabadilishia washtakiwa hao hati ya mashitaka.
   
  Mbali na Fuime, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Razah Ladha (68), Goodluck Mbaga (35), Wilboard Mugyabuso (42), Mohamed Abdulkari (61), Charles Ogare (48), Zonazea Oushoudada (60), Vedasto Richale (59), Michael Hemed (59), Albert Munuo (56), Joseph Ringo (43) na Ibrahim Mohamed.
   
  Katika kesi ya msingi, upande wa Jamhuri unadai kuwa Marchi 29, mwaka 2013 katika mtaa wa Indira Gandhi ulioko katika wilaya ya Ilala, washtakiwa hao waliwaua watu 27. 
  Katika tukio hilo watu 27 walipoteza maisha wakiwemo Yusuph Khari, Kulwa Alfan, Hamada Musa, Kessy Manjapa, Hamis Mkomwa, Boniface Bernard, Suhail Karim, Salman Akbar, Selemani Haji, Selemani Mtego, Sikudhani Mohamed, Ahmed Milambo na Salum Mapunda.
   
  Wengine ni Selemani Mnyamani, John Majewa, Mussa Mnyamani, Devid Herman, William Joakim, Abdulrahaman Mwiha, Emmanuel Christian, Mmanyi Ngadula, Adivai Desiki, Emmanuel Wahai, Augustino Chuma, Gabriel Godwin Kamwela, Philipo Kusimula, Betod Mwananengule na Zahda Abbas


  0 0

  Mahujjaaj wakiendelea na Tawaaf katika Baytul Haraam. Kutufu ni kuiznguka Al Ka'abah mara saba ambayo ni mojawapo katika Manaasik ( Ibada za Hajj)

   Msikiti wa Makkah ulivyofurika msimu wa Hajj wote wakiwa katika ibaadah. picha hii ilipigwa baada ya salal ya Alfajiri kutoka ghorofa ya pili Haram.
   Wazee , watoto, kike kwa kiume wakiendelea na Ibada ya Tawaaf. Haram . Al Ka'abah ni sehemu pekee ambapo mchanganyiko kati ya wanawake na wanaume katiba Ibada umeruhusiwa
  Wanaofanya ibada ya Tawaaf wakiashiria mbele ya Hajarul aswad ( jiwe jeusi) sehemu ambayo huanzia na kumalizia Tawaaf
  Hapa ni karibu na Maqaam Ibraahiym, sehemu ambayo Nabii ibraahiym 'Alayhi Salaam alikuwa akisimama kufanya Ibada. Ni sunnah kusali rakaa mbili baada ya kumaliza Tawaaf nyuma ya Maqaam Ibraahiym

  0 0
 • 10/12/14--03:24: DAR TAMBARARE....


 • 0 0

   Meneja Mkazi wa Miradi wa Shirika lisilo la Kiserikalilimalojishughulisha na masuala ya Changamaoto zitokanazo na ongezeko ya Idadi ya Watu Duniani DSW Bw. Avit Buchwa akizungumza na Afisa Habari kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Jonas Kamaleki wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayoendelea mkoani Tabora
  Vijana wa DSW wakifafanua kuhusu progamu ya Kijana Kwa Kijana inayoendeshwa na Shirika l Meneja Mkazi wa Miradi wa Shirika lisilo la Kiserikalilimalojishughulisha na masuala ya Changamaoto zitokanazo na ongezeko ya Idadi ya Watu Duniani DSW Bw. Avit Buchwa akizungumza na Afisa Habari kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Jonas Kamaleki wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanaVijana wa DSW wakiigiza wakati mdahalo wa vijana kuhusu Stadi za Maisha ikiwa ni moja ya programu katika kuadhimisha Wiki ya Vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani Tabora.yoendelea mkoani Taboraao kwa kushirikisha vikundi vya vijana.
  Vijana wa DSW wakiigiza wakati mdahalo wa vijana kuhusu Stadi za Maisha ikiwa ni moja ya programu katika kuadhimisha Wiki ya Vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani Tabora.
  Baadhi ya Vijana wa DSW wakifuatilia mada wakati wa mdahalo wa vijana kuhusu Stadi za Maisha ikiwa ni moja ya programu katika kuadhimisha Wiki ya Vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani Tabora.Picha na Frank Shija, Tabora

  0 0

   Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi Kombe kwa kiongozi wa timu ya Mshikamano,ambapo timu hiyo imenyukwa goli moja dhidi ya timu ya Amani,mchezo huo wenye lengo la kuimarisha na kudumuisha amani na mshikamano tulionao umefanyika katika Uwanja wa Taifa,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali
  Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda akikabidhi Kombe kwa kiongozi wa timu ya Amani,ambayo imeibuka kinara katika mashindano hayo kwa kuichapa timu ya Mshikamano goli moja.Mchezo huo wenye lengo la kuimarisha na kudumisha amani na mshikamano tulionao umefanyika katika Uwanja wa Taifa,jijini Dar  ukijumuisha viongozi mbalimbali wa dini ya Kikristo na Kiislamu,ambapo pia viongozi wa ngazi mbalimbali wa dini na serikali walihudhuria.
   Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Amani
   Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Mshikamano
   Sehemu ya umati wa watu waliokuwepo kushuhudia mechi ya Amani na Mshikamano,iliyofayika jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa.
   Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda akizungumza jambo mbele ya wachezaji wa timu ya Amani na Mshikamano,zilizoundwa mahsusi katika kuadhimisha siku ya amani duniani,ambapo  viongozi wa dini uliojumuisha Masheikh, Maimamu, Maaskofu, Wachungaji na Mapadre.Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,Shoto kwake ni Mkuu wa  Mkoa wa Jiji la Dar,Mh.Said Meck Sadick na Rais wa TFF,Bwana Jamal Malinzi.

  Katika mchezo huo wa kujenga amani na mshikamano uliopo nchini,Mwamuzi msaidizi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar,Mh. Said Meck Sadick na mwamuzi aliyeshika kipyenga alikuwa ni Kamishna wa Kanda Maalumu, Seleman Kova 
  Mkuu wa Mkoa wa jiji la  Dar, Mh.Said Meck Sadick  ambaye alizungumza machache na kumkaribisha Mgeni Rasmi wa mchezo huo wa Viongozi wa Dini kati ya Amani na Mshikamano,Waziri Mkuu,Mh Mizengo Pinda pichani kulia. 
   Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Mussa ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mchezo huo,akizungumza machache. 
   Rais wa TFF,Bwan, Jamal Malinzi akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar, Mh.Said Meck Sadick  ambaye alizungumza macheche na kumkaribisha Mgeni Rasmi wa mchezo huo wa Viongozi wa Dini kati ya Amani na Mshikamano,Waziri Mkuu,Mh Mizengo Pinda.

  0 0

  "Uzalendo kwanza" Shabiki wa timu ya Taifa Stars akishangilia 
   Mshambliaji wa Timu ya Taifa Stars,Thomas Ulimwengu akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Benin wakati wa Mchezo wao wa Kirafiki unaoendelea hivi sasa ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo,Taifa Stas inaongoza bao 4-0 mpaka sasa.
   Kiungo Mshambuliaji wa Taifa Stars,Amri Kiemba akiipatia timu yake bao la pili katika Mchezo wao wa Kirafiki unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo,Taifa Stas inaongoza bao 4-0 mpaka sasa.
   Raha ya Ushindi,Timu ya Taifa Stars wakishangilia mara baada ya kupata goli la nne dhidi ya timu ya Benin.
   Mchezaji wa timu ya Taifa Stars akielekea golini mwa timu ya Benin
  Ni furaha na miluzi kwa wingi imetawala hivi sasa ndani ya uwanja wa Taifa hivi sasa,mara baada ya timu ya Taifa Stars kuongeza bao la nne dhidi ya timu ya Benin kwenye mchezo wa kirafiki unaoendelea hivi sasa ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar

  0 0

   Wananchi wakitazama ajali iliyotokea maeneo ya Hedaru Wilayani Same mkoani Kilimanjaro jioni ya leo, ambapo ajali hiyo ilihusisha gari ndogo yenye namba za usajili T653 BZR kuingia chini ya uvungu wa basi la abiria lijulikanalo kwa jina la Happy Nation. Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari  abiria wote waliokuwemo ndani ya gari ndogo (ambao idadi yao haikujulikana) walipoteza maisha papo hapo. Aidha bado haikufahamika mapema chanzo cha ajali hiyo ni nini.


  0 0

  Mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars,Juma Luizio akiipachikia bao nne timu yake katika mtangange wa kikataifa wa kirafiki dhidi ya Benin,uliomalizika hivi punde katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imeshinda 4-1 dhidi ya Benin.
   Wachezaji wa Taifa Stars,wakishangilia ushindi wao huku wakiwaacha wapinzani wao wa Benin wakiwa hoi tena wakiwa hawaamini wanachokiona uwanjani hapo.
   Washabiki wa Taifa stars wakiisapoti vilivyo timu yao.
   Ubao wa ulionyesha hivi kabla jamaa hawajapata la kufutia machozi.
   Shangwe tupu ilikuwa uwanjani hapa.
   Dogo muokota mipira akiisikilizia baridi iliyoambatana na kimvua cha kiaina.
   Uzalendo ndio mpango mzima,pamoja na kwamba mvua ilikuwa ikinyesha lakini hakuna alietaka kuondoka uwanjani hapo hasa kutokana na burudani safi iliyoonyeshwa na Taifa Stars leo.Picha na Othman Michuzi.,MMG.

  0 0


  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua kituo cha polisi cha wilaya ya Uyui akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora, Oktoba 11, 2014. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe Fatuma Mwasa na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Mhe. Lucy Mayenga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, ACP Suzan Kaganda (kulia) baada ya kufungua kituo cha polisi cha wilaya ya Uyui akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora, Oktoba 11, 2014.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, ACP Suzan Kaganda (kulia) baada ya kufungua kituo cha polisi cha wilaya ya Uyui akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora, Oktoba 11, 2014. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0

   Meneja Uhusiano wa Umma  wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akiwakabidhi rasmi vijana wa kundi la”WAKALI SISI”la kiwalani jijini Dar es Salaam simu zao aina ya Vodafone Smart Kicka,ambazo ni moja kati ya zawadi walizojishindia  katika fainali za shindano la Dance 100% hivi karibuni na kujishindia kitita cha  Tsh Milioni 5 na simu hizo zimeunganishwa na mtandao wa Vodacom Tanzania  muda wa maongezi kiasi cha  shilingi laki moja.
   Mabingwa wa shindano la Dance 100% 2014” WAKALI SISI”wakimsikiliza  kwa makini Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia) wakati alipokuwa akiwahusia kuhusiana na matumizi mazuri ya simu  baada ya kuwakabidhi rasmi ya simu zao aina ya Vodafone Smart Kicka zilizounganishwa na Vodacom na muda wa maongezi wa kiasi cha  shilingi laki moja ambazo ni moja ya zawadi walizojishindia katika fainali ya shindano hilo na kuibuka washindi wa kwanza na kujizolea kombe pamoja na kitita cha shilingi milioni 5.

   Kiongozi wa kundi la”WAKALI SISI” la Kiwalani jijini Dar es Salaam,Baraka Kambona(kushoto) akipokea mfuko wenye simu aina ya Vodafone Smart Kicka zilizounganishwa na mtandao huo na kuwekewa muda wa maogezi wa shilingi laki moja toka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ikiwa ni kati ya zawadi walizojishindia katika fainali ya shindano la Dance 100% hivi karibuni na kuondoka na kitita cha  Tsh Milioni 5.

    Mabingwa wa Dance 100% 2014”WAKALI SISI”wa Kiwalani jijini Dar es Salaam,wakionesha simu aina ya Vodafone Smart Kicka zikiwa na muda wa maongezi wa shilingi laki moja mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (kulia)kundi hilo liliibuka mshindi wa kwanza  katika fainali ya shindano hilo hivi karibuni ambapo walijinyakulia kitita cha shilingi milioni 5.

  Kundi la”WAKALI SISI”ambalo ni mabingwa wa shindano la Dance 100% 2014 wakionesha makali yao ya kucheza dansi katika makao makuu ya Vodacom walipofika katika hafla fupi yakukabidhiwa  rasmi ya simu zao aina ya Vodafone Smart Kicka zilizounganishwa  na muda wa maongezi wa kiasi cha shilingi laki moja ambazo ni moja ya zawadi walizojishindia katika fainali ya shindano hilo na kuibuka washindi wa kwanza na kujizolea kombe pamoja na kitita cha shilingi milioni5.
  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile, mchana wa leo ametiliana saini makubaliano ya mkataba wa kuanzisha Mradi wa Maji katika Wilaya ya Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro.. 
   Dr. Likwelile alisaini Mkataba huo kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya uchumi ya Afrika. Aliye wakilisha Benki hiyo ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia. 
   Aidha katika kutiliana saini Mkataba huo Dr. Likwelile alimueleza Eng. Yousef I. Al-Bassam kuwa Serikali ya Tanzania inatambua kuwa BADEA imetoa Dola za Kimarekani milioni 12.0 sawa na shilingi Bilioni 20.1 za Kitanzania kwa ajili ya kusaidia mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. 
  Hivyo inatoa shukrani zake za dhati kwa BADEA kwa kusaidia kuchochea maendeleo ya Tanzania. “Msaada huu tulioupata leo utaisaidia Serikali kutatua tatizo la maji katika wilaya ya Same na Mwanga, hii inaonyesha ni jinsi BADEA unaunga mkono na kutekeleza jukumu zima la kushiriki katika masuala ya kijamii na ya kiuchumi kwa nchi yetu ya Tanzania, hivyo tunaomba muendelee kutusaidia”. Alisema Dr. Likwelile. 
   Dr. Likwelile alimueleza Eng. Yousef I. Al-Bassam kuwa, kama anavyofahamu gharama za mapendekezo ya mradi mzima ni Dola za Kimarekani million 110.43 na hii inahitaji uchangiaji kutoka katika mifuko mingine kama mfuko wa maendeleo wa Saudia , Mfuko wa Kimataifa wa OPEC na Serikali kuchangia fedha kusaidia mradi huu. 
  "Kwa hili sina wasiwasi nalo kwani ninafuraha kujua kwamba umeshakubaliana na ninaujasiri kuwa jitihada zako zitafanikiwa. Mradi huu wa maji wq wilaya ya Same na Mwanga unalenga kusaidia kuwepo kwa maji kwenye jamii mbalimbali zilizopo kwenye mradi huo.” Aliongeza Dr.Likwelile. Aliendelea kusema kuwa,mradi huo utakapo kamilika: 
  (i) utaongeza kiwango cha watu wengi kuweza kupata maji safi na salama ya kunywa. 
  (ii) Uchumi wa Same na Mwanga utaimarika pamoja na hali ya afya kwa jamii nayo itakuwa imara hasa kwa maeneo yale yanayoguswa na mradi. 
  (iii) Hali ya maisha ya watu wa Same na Mwanga itainuka. 
  “Mafanikio ya ukamilishaji wa mradi huu ni muhimu sana kwa uchumi wa jamii na maisha bora kwa watu wa wilaya ya Same na Mwanga”. Alisema Likwelile. Dr. Likwelilie alimalizia kwa kusema kuwa“Tanzania na Saudia ni marafiki wa muda mrefu sana, hivyo tutazidi kushirikiana na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa”. 
    Imetolewa na: Ingiahedi Mduma 
  Msemaji - Wizara ya Fedha 
  Washington D.C
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali  Dr. Servacius Likwelile akiwa na ujumbe kutoka Tanzania wakiwa tayari kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. Aliye kushoto kwake ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti  na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia.Fedha hizo zimetoka BADEA.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr.    Servacius Likwelile akitia saini makubaliano ya mradi wa maji katika Wilaya ya Same na Mwanga. Aliye kushoto kwake ni Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti  na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia. Aliyeko kulia ni Bi. Suzan Mkapa, Mkurugenzi wa sheria kutoka Wizara ya Fedha.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr.    Servacius Likwelile  na Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti  na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia, wakibadilishana mikataba hiyo baada ya kutiliana saini.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr.    Servacius Likwelile  na Eng. Yousef I. Al-Bassam ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti  na Mkurugenzi Msimamizi wa mfuko wa maendeleo wa Saudia, wakiionyesha mikataba hiyo kwa waliohudhuria sherehe hiyo  baada ya kutiliana saini.  0 0

  Wachezaji wa Kagera Walio chini ya Miaka 15 wakishangilia baada ya mpira kumalizika kwenye Uwanja wa Kaitaba dhidi ya Geita kwenye Mashindano ya Copa Coca Cola, Mchezo uliochezwa leo Jumapili 12.10.2014. Kagera wameifunga Geita Bao 2-0.

  Na Faustine Ruta, Bukoba
  Kagera wameanza vyema Mashindano ya soka kwa vijana walio chini ya miaka 15, Copa Coca Cola, Leo Jumapili 12.10.2014 Asubuhi baada ya kuichapa Timu ya Geita bao 2-0 kwenye Uwanja wa Nyumbani Kaitaba.
  Bao za Kagera zimefungwa kipindi cha kwanza na cha pili. Bao la kwanza limefungwa kipindi cha kwanza dakika ya 28 na Avith Frolian aliyekuwa amevalia jezi namba 10. Na bao la pili lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 61 na Kepteni wao Patrick Amos baada ya Kagera kupiga kona na Kepteni wake kuruka juu na kufunga kwa kichwa. Kagera watarudiana na Geita kwao jumamosi tarehe 18 wiki ijayo.
  Mchezaji wa Kagera akiendesha...Mashambulizi kwa timu ya Geita leo jumapili Asubuhi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0
 • 10/12/14--20:00: ngoma azipendazo ankal

 • Yemi Alade - Johnny

  0 0
 • 10/12/14--20:30: KUMBUKUMBU
 • Mzee Daniel Madaha Machemba.

  Baba yetu Mpenzi,Ni miaka 27 sasa imepita tangu ulipoenda kwenye makao ya kudumu Baba yetu Mpendwa tarehe 13/10/1987
  Kumbukumbu yako bado ipo utafikiri jana tu kwa sisi uliotuacha nyuma, uwepo wako bado upo.

  Unakumbukwa na wengi tu, katika familia. Kipekee una kumbukwa sna na Mkeo, Mama Machemba.

  Watoto wako: (1) Mary Mbati
  (2) Dr. James Machemba
  (3) Richard Machemba
  Wajukuu zako: (1) Godwin Mbati, (2) Careen Mbati (3) Joanne Machemba (4) Daniel Machemba
  Pia unakumbukwa na dada zako, Thereza na Ndekele, wajomba, wakwe, pamoja na ndugu na Marafiki.

  Sisi tulikupenda sana lakini Mungu alikupenda zaidi, pumzika kwa amani
  Jina la Bwana lihimidiwe.
  Amina.

  0 0

  Makamu Rais wa timu ya Simba,Geofrey Nyange Kaburu akipuliza Vuvuzela jana kwenye kiwanda cha Bia ,mkoani Arusha wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe iliwakutanisha wafanyakazi wa kiwanda hicho.
  Makamu Rais wa timu ya Simba,Geofrey Nyange Kaburu(kushoto) na Mjumbe Kamati Kuu ya timu ya Yanga,Mohamed Binda,wakicheza danadana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe kwenye kiwanda cha Bia mkoani Arusha jana. 
  Mashabiki wa timu ya Simba na Yanga ambao ni wafanyakazi wa kiwanda cha kampuni ya Bia mkoani Arusha wakivuta kamba jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe iliyowakutanisha wafanyakazi wa kiwanda hicho
  Mashabiki wa timu ya Yanga ambao ni wafanyakazi wa kiwanda cha kampuni ya Bia mkoani Arusha wakishangilia baada ya kushinda mashabiki wa Simba katika mchezo wa kuvuta Kamba jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe mkoa wa Arusha iliyowakutanisha wafanyakazi wa kiwanda hicho.
  Wafanyakazi wa kiwanda cha Bia,Arusha ambao ni mashabiki wa timu za Simba na Yanga wakicheza mchezo wa Foosball jana kwenye uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ilifanyika kwenye kiwanda hicho. 

  0 0

  Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano (kushoto) akimkabidhi kombe dereva Francis John Kinaulanga (kulia) baada ya kuibuka dereva bora wa mwaka 2014 wa shindano la scania ”Scania Driver of the year competition 2014” lililofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe jijini Dar es Salaam.
  Mshindi wa shindano la Scania Scania Driver of the year competition 2014” Francis John Kinaulanga (katikati) akiwa na mshindi namba mbili Ramadhani Ahmad Danga (kulia) na Winston Rwegalulila Rwechungura (kushoto) baada ya kutangazwa washindi kwenye Viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe jijini Dar es Salaam.
  Madereva wote wa shindano la scania ”Scania Driver of the year competition 2014” lililofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja.


  0 0

  TIMU ya Taifa ya Safari Pool imeonyesha uwezo wa juu baada ya kuzichapa timu za kombania za Mikoa ya kimichezo ya Ilala na Temeke kwa siku tofauti katika kujiweka sawa na mshindano ya Afrika ya mchezo huo yajulikanayo kwa “Safari All Africa Pool Championship”.

  Timu ya Safari Pool ilianza mchakato wa kujipima ikiwa ni sehemu ya maandalizi natimu ya Kombania ya Mkoa wa kimichezo wa Ilala ambapo waliibuka na ushindi wa 12-9 katika mchezo uliochezwa Ijumaa octoba 10,2014 kwenye Ukumbi wa Mashujaa jijini Dar es Salaam.

  Baada ya kutoka Ilala walikutana na timu ya Kombania ya Mkoa wa Temeke Jumamosi Octoba 11,2014 katika mchezo ulichezwa katika Ukumbi wa Mpo Afrika Tandika jijini Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa 13-3.

  Octoba 12,2014 timu itakutana pia na Kombania ya Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni katika mchezo unaotarajiwa kufanyika katika Ukumi wa Face 2 Face uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa timu ya Taifa, Denis Rungu alisema kikosi chake kiko safi na mchakato wa mechi za kirafiki tatu za mikoa ya kimichezo ya Ilala, Temeke na Kinondoni ni semu ya kupima kikosi chake lakini pia ni sehemu ya mchujo wa kupata wachezaji 8 kutoka kundi la wachezaji 16 walioko timu ya Taifa.

  Alisema Kocha timu inatarajiwa kuingia Kambini leo ambapo ndio sehemu muafaka ya kujiandaa vema na mashindano ya Afrika kwa mwaka 2014 ambapo Tanzania ndio muandaaji.

  Mashindano ya Safari All Africa Pool Champonship yanatarajiwa kufunguliwa rasmi Octoba 16 na kumalizika Octoba 18 ambapo mgeni rasmi anayetarajiwa mkufungua mashindano hayo ni Waziri wa Habari Utamaduni, Vijana na Michezo.

  Nchi zilizothibitisha kushirika mpaka sasa ni mabingwa watetezi Zambia, Afrka Kusini, Kenya, Cameroon, Lesotho, Malawi, Uganda na wenyeji Tanzania.
  Nahodha wa timu ya Taifa ya mchezo wa Safari Pool, Charles Venance akicheza wakti wa mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Kombaia ya Mkoa wa kimichezo wa Temeke uliochezwa katika Klabu ya Mpo Afrika Tandika mwishoni mwa wiki.Timu ya Taifa ilishinda 13-3.
  Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Safari Pool wakiwa na viongozi wa Mkoa wa kimichezo mara baada ya timu ya Taifa kibuka na ushindi wa 13-3 dhidi ya timu ya kombania ya mkoa huo iliyochezwa mwishoni mwa wiki.

older | 1 | .... | 604 | 605 | (Page 606) | 607 | 608 | .... | 3284 | newer