Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

BALOZI SEFUE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA DICOTA MJINI DURHAM, MAREKANI

$
0
0
Balozi Sefue akishangiliwa na kina mama wa DICOTA waliokuwa wamevalia sare kumkaribisha kufungua Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA 2014) Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika Hoteli ya Millenium mjini Durham, North Carolina. 
Balozi Sefue akizungumza na Meya wa Durham, Mhe. Bell
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifungua rasmi Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA 2014) Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika Hoteli ya Millenium mjini Durham, North Carolina. Washiriki kwenye mkutano huo ni pamoja na Watanzania kutoka Majimbo mbalimbali ya Marekani, Wajumbe kutoka Serikalini na Sekta Binafsi na Serikali ya Marekani. Katika hotuba yake ya ufunguzi Balozi Sefue alilipongeza Baraza la DICOTA kwa juhudi na mafanikio mbalimbali na pia alisema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi hizo.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula (mwenye scarf) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo, Mwalimu Christopher Mwakasege na Wajumbe wengine wakimsikiliza Balozi Sefue (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa DICOTA 2014
Balozi Mulamula akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa DICOTA 2014
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


Halima Mdee akamatwa na Polisi walipowatawanya BAWACHA

$
0
0

Jeshi la polisi katika Kanda maalum ya Dar es Salaam limetumia maji ya kuwasha kuwatawanya wafuasi wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) waliokuwa wakijiandaa KUANDAMANA hadi Ikulu.


Aidha, jeshi hilo limemkamata Mwenyekiti wa BAWACHA, Mhe. Halima Mdee aliyekuwa akiyaongoza maandamano hayo.

BAWACHA walipanga kuandamana hadi Ikulu ya Dar es Salaam kwa nia ya kuonana na Rais Jakaya Kikwete ili kumsishi asisaini Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, ambayo ilipitishwa na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba siku ya Alhamisi mkoani Dodoma.

Jeshi la Polisi lilizuia maandamano hayo kupitia taarifa yake iliyoitoa hapo jana.

Mwanalibeneke edwin moshi atembelea redio ya kijamii iliyopo kwenye mji wa Tübingen, Ujerumani

$
0
0
 Redio Wüste Welle ni redio ya kijamii iliyopo kwenye mji wa Tübingen nchini Ujerumani ambacho kimekuwa kikijihusisha na shughuli za kijamii ikiwemo kutoa mafunzo ya vitu mbalimbali vinavyohusiana na taaluma ya uandishi wa habari. Mwanalibeneke Edwin Moshi alikuwa ni mmoja wapo kati ya waliopata hiyo fursa Mbali na shughuli zake za utangazaji wa redio pia ni mmiliki wa mtandao wa kijamii wa EDDY BLOG

mahafali ya tano ya Bodi ya Ununuzi na Ugavi yafana jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Mkurugenzi wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Dk Clemence Tesha (kushoto) akiwaapisha wahitimu wa shahada ya kwanza  ya Bodi ya Ununuzi na Ugavi, kwenye sherehe za mahafali ya tano yaliyofanyika kwenye viwanja vya bodi hiyo, Dar es Salaam
 Wahitimu wa Mahafali ya tano ya Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakionekana wenye furaha muda mfupi baada ya kutunukiwa vyeti, stashahada na shahada za ununuzi na ugavi kwenye sherehe za mahafali ya tano yaliyofanyika kwenye viwanja vya bodi hiyo, Dar es Salaam
 Wahitimu wa Mahafali ya tano ya Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakila kiapo cha utii na uaminifu muda mfupi baada ya kutunukiwa vyeti, stashahada na shahada za ununuzi na ugavi kwenye sherehe za mahafali ya tano yaliyofanyika kwenye viwanja vya bodi hiyo, Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Sr. Dk Hellen Bandiho, akizungumza na wahitimu mbalimbali wa vyeti, stashahada na shahada za ununuzi na ugavi kwenye sherehe za mahafali ya tano yaliyofanyika kwenye viwanja vya bodi hiyo, Dar es Salaam, katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, na Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Dk Clemence Tesha
Wahitimu wa Mahafali ya tano ya Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kwenye sherehe za mahafali ya tano yaliyofanyika kwenye viwanja vya bodi hiyo, Dar es Salaam

DKT SHEIN AWASILI KISIWANI PEMBA LEO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed  Shein na Mkewe Mama Mwanawema Shein  wakisalimina na Viongozi mbali mbali  alipowasili katika uwanja wa Ndege  wa Karume Pemba leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwana Mwema Shein wakisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Vikosi vya Ulinzi Pemba mara baada ya kuteremka Ndege katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo ( Picha na Ramadhan Othman Ikulu )

BALOZI SEIF AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA MAREKANI, AKAGUA UJENZI WA BARABARA WETE, PEMBA

$
0
0
 Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ms Shimoja Dr. Robert Shumake akimtambulisha Makamu wa Rais wa Kampuni ya maendeleo ya ujenzi ya Detroit Nchini Marekani Bw. Andrew G. McLemore kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi walipokutana kwa mazungumzo VIP ya Uwanja wa ndege wa Pemba. Aliyepo kushoto na Balozi Seif ni Afisa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani Mh. Suleiman Saleh.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani ambae pia ni Murugenzi wa Kampuni ya Ms Shimoja Dr. Robert Shumake kwenye uwanja wa ndege wa Pemba.
 Meneja wa Kampuni ya Mecco Bwana Abdullkadir Mohamed Bujeti akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa bara bara ya wete gando inayoejngwa na Kampuni hiyo.
Balozi Seif akisalimiana na Mtoto mlemavu  anayeishi katika Kijiji cha Gando jina halikupatikana mara moja baada ya kukaguwa ujenzi wa Bara bara ya Wete - Gando inayoendelea kujengwa na Kampuni ya Mecco yenye Makao Makuu yake Nairobi Nchini Kenya. 
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

simba mambo yaleyale.... yatoka sare ya 1-1 na Stand United

$
0
0
Golikipa wa timu ya Stend United, John Mwenda akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe wakati wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka  Tanzania uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1. (Picha na Francis Dande) 
Mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe akimtoka beki wa Stand United, Idd Mobby.
Maguri akiipangua ngome ya Stand United.
Idd Mobby akimdhibiti Emmanuel Okwi.

MATOKEO YOTE YA LEO
SIMBA 1- STAND UNITED 1
PILISI MORO 1- KAGERA SUGAR 1
AZAM FC 0 - TANZANIA PRISONS 0
RUVU SHOTING 0 - MBEYA CITY 0
COASTAL UNION 2 - NDADA FC 1

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BALOZI KAMALA AMKABIDHI CHETI CHA UTAMBUZI BWANA SAITOTI

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji  ya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa pili Kutoka kulia) akimkabidhi cheti cha utambuzi Bwana Saitoti kumshukuru kwa kazi nzuri anayofanya ya kutafuta fedha Ubelgiji ya kusaidia kupambana na Umaskini Handeni Tanzania. Bwana Saitoti ametafuta fedha za kusaidia kutekeleza miradi ya maji Handeni. Balozi Kamala amekabidhi cheti hicho leo Ubelgiji- Antiwerpen. Balozi Kamala amesema kila mwaka Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji utakuwa unatoa vyeti mbalimbali vya kutambua kazi nzuri zinazofanywa na Asasi Zisizo za Kiserika za kutafuta fedha ya kusaidia kutekeleza miradi mbalimbali Tanzania.

uzinduzi rasmi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 inayoendeshwa na Kilimanjaro Premium Lager

$
0
0
Viongozi wa timu za Simba na Yanga, Geofrey Nyange Kaburu, kushoto ambaye ni Makamu wa Rais Simba na Mohamed Bhinda, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga (kulia) wakivuta kamba kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 inayoendeshwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager. Uzinduzi huo rasmi kwa wadau wa Simba na Yanga ulifanyika leo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja wa bia hiyo, George Kavishe na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Bi Kushilla Thomas (aliyevaa suruali nyeupe).
Viongozi wa timu za Simba na Yanga, Geofrey Nyange Kaburu, kushoto ambaye ni Makamu wa Rais Simba na Mohamed Bhinda, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga (kulia) wakipeana tano  kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe 2
Mashabiki wa timu za Simba na Yanga wakivuta kamba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 ya Kilimanjaro Premium Lager kwa wadau wa Simba na Yanga uliofanyika katika Viwanja vya Leaders jijini Dar   es Salaam leo chini ya Kilimanjaro Premium Lager .
Mashabiki wa Timu za Simba na Yanga wakicheza muziki wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 kwa wadau wa timu hizo mbili katika hafla iliyofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam leo.
Mashabiki wa Timu za Simba na Yanga wakiingiakwenye viwanja vya Leaders wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 kwa wadau wa timu hizo mbili katika hafla iliyofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam leo.
Viongozi wa timu za Simba na Yanga, Geofrey Nyange Kaburu, kushoto ambaye ni Makamu wa Rais Simba na Mohamed Bhinda, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga (kulia) wakishindana kupiga danadana kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe 2 inayoendeshwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager. Uzinduzi huo ni kwaajili ya wadau wa timu hizo ulifanyika jana viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam leo.

mdau saidi mkwawa atetea utafiti wake, ala nondozzzz...kiulainiiiii....

$
0
0
Mdau  Mhandisi Saidi Mkwawa wa wakala wa ukaguzi Madini Tanzania (TMAA) akiwa anatetea utafiti wake ili apate nondozz ya Master of Engineering Science (Metallurgy) katika Chuo kikuu cha curtin university, campus ya  Western Australia School of Mine hivi karibuni. Utetezi ulipita kwa mafanikio
 Mdau Mhandisi Mkwawa wa wakala wa ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) akitoa neno  la shukrani kwa wafadhili kwa niaba ya wenzake mara baada ya kutunikiwa nondozzzz ya Master of Engineering Science (Metallurgy) KUTOKA CHUO KIKUU CHA CURTIN NCHINI AUSTRALIA.
 Mdau Mhandisi Mkwawa wa wakala wa ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) AKIPOKEA CHETI MAALUM KUTHIBITISHA AMEMALIZA KULA NONDOZZZZ  ya Master of Engineering Science (Metallurgy) KUTOKA CHUO KIKUU CHA CURTIN NCHINI AUSTRALIA KUTOKA KWA MWAKILISHI WA AUSTRALIA AWARDS .

 Mdau Mhandisi Mkwawa wa wakala wa ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) AKIWA NA WAHITIMU WENZAKE MARA BAADA YA kutunikiwa nondozzzz ya Master of Engineering Science (Metallurgy) KUTOKA CHUO KIKUU CHA CURTIN NCHINI AUSTRALIA.
 Mdau Mhandisi Mkwawa wa wakala wa ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA)  AKITAFAKARI SAFARI NDEFU ALIYOPITIA KABLA YA kutunikiwa nondozzzz ya Master of Engineering Science (Metallurgy) KUTOKA CHUO KIKUU CHA CURTIN NCHINI AUSTRALIA.
 Mdau Mhandisi Mkwawa akifurahia nondozzz yake kwa kuruka hewani kama hua

ukumbi mpya wa sherehe jijini Dar es salaam wavutia wengi

$
0
0
 Cardinal Rugambwa Social Centre ni ukumbi mpya wa sherehe ambao umeanza kazi pale pembeni pa Kanisa la Mtakatifu Peter (St. Peter's) jijini Dar es salaam, ambao unaongeza idadi ya kumbi za aina hiyo zenye kila kitu cha kisasa. Na tayari umekuwa kimbilio la wadau wengi wenye sherehe mbalimbali.
Usiku wa kuamkia leo Ankal alikuwepo kwenye ukumbi hio maridadi katika mnuso wa send off uliohudhuriwa na wadau kibao, akiwemo Baba Paroko wa kanisa hilo Fr. Kaombwe (kushoto kwa Ankal) ambaye pamoja na hao wadau wengine ni wadau wakubwa wa Globu ya Jamii.
 Ankal na wadau wakiwa kwenye ukumbi huo maridadi wa Cardinali Rugambwa katika mnuso wa send off uliohudhuriwa na wadau kibao.

JK AKAGUA Chuo cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu UDOM

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa sehemu mbalimbali na  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Shaaban Mlacha (mbele) na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula (kulia) alipofanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Chuo  cha Sayansi ya Afya na Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu cha chuo hicho mjini Dodoma Ijumaa Oktoba 3, 2014. Alikuta ujenzi umeshakamilika na kilichobaki ni uwekaji wa samani na vifaa vya kufanyia kazi ili kitovo hicho kianzi kazi rasmi hivi karibuni. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Ngoma azipendazo ankal

Semina ya Fursa 2014 yafanyika Mjini Singida leo

$
0
0
 Mmoja wa washiriki wa Semina ya Fursa akiuliza swali kwa Meza kuu ya watoa mada kuhusiana na mradi wa ufugaji wa kuku.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF),Bwa.Ally Mkulemba akizungumza faida mbalimbali za kujiunga na shirika hilo la NSSF,alisema kuwa vijana wanapaswa kuamka kwa sasa na kuanza kuzichangamkia fursa zitokanazo na shirika hilo,ikiwemo mikopo,bima ya Aya na mengine kwa maendeleo na ujenzi wa maisha bora
 Msanii wa Bongofleva Baba Levo,ambaye pia ni mmoja wa mabalozi wa shirika hilo la NSSF,akielezea yeye na wasanii wenzake wanavyonufaika na fursa mbalimbali zipatikanazo na shirika,Baba Levo amewataka wasanii mbalimbali ambao bado hawajajiunga na shirika hilo wakiwemo na vijana mbalimbali wafanye hivyo sasa,kwani shiriki hilo linatoa fursa nyingi za kuwawezesha vijana kuwapa wigo mkubwa wa kutimiza ndoto za maisha yao
 Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakimsikiliza Msanii mahiri wa Mashairi pichani,Mrisho Mpoto,alipokuwa akizungumza ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya KBH,ilioko nje kidogo ya mji wa Singida.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.

Tuesday 7 October opening '8 Years Waiting' by Cloud Chatanda at Alliance Française

$
0
0
Dear Friends
 Tuesday 7 October at 19.30 Cloud Chatanda is opening his exhibition ‘8 Years Waiting’ at Alliance Française.
A selection of mixed media drawings from one of Tanzanians most talented illustrators and artists.



MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AUNGANA NA WAUMINI KATIKA SWALA YA EID EL-HAJI JIJINI DAR LEO.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiungana na waumini wa dini ya Kiislamu katika swala ya Sikukuu ya Eid El- Hajim iliyoswaliwa katika Msikiti wa Istiqaama, jijini Dar es Salaam, leo. Wa pili (kulia) ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kushiriki swala ya Sikukuu ya Eid El- Hajim iliyoswaliwa katika Msikiti wa Istiqaama, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal, akiagana na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kushiriki nao katika swala ya Sikukuu ya Eid El- Haji iliyoswaliwa katika Msikiti wa Istiqaama. Picha na OMR

Mahafali ya 36 ya Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) yafana

$
0
0
Baadhi ya wahitimu wa National Board of Accountants and Auditors (NBAA)  wakiwa katika maandamano ya kitaaluma wakati wa maafali ya 36 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam jana ambapo jumla ya wahitimu 855 walipata Degrii ya juu ya uhasibu (CPA) na wahitimu 82 walitunukiwa cheti cha utunzaji wa hesabu (ATEC.)
 Mkurugenzi wa Bodi ya NBAA Bw. Pius Maneno akitoa hotuba fupi kabla yakumkaribisha mgeni rasmi wakati wa maafali ya 36 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam 
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda  Mhe. Janeth Mbene akiongea na wahitimu (hawapo pichani) wakati wa maafali ya 36 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam 
 Baadhi ya wahitimu wa NBAA wakifuatili kwa makini matukio yaliyokua yakiendelea wakati wa maafali ya 36 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam jana ambapo jumla ya wahitimu 855 walipata CPA na wahitimu 82 walipata cheti cha utunzaji wa hesabu.
 Baadhi ya wahitimu wa NBAA wakifuatili kwa makini matukio yaliyokua yakiendelea wakati wa maafali ya 36 yaliyofanyika katika kituo cha NBAA Mbweni jijini Dar es Salaam jana ambapo jumla ya wahitimu 855 walipata CPA na wahitimu 82 walipata cheti cha utunzaji wa hesabu.
Picha na Genofeva Matemu - Maelezo

MADRASA RAHMAN YA SEGEREA JIJINI DAR INAWAPA MKONO WA EID MUBARAK

$
0
0
Madrasa Rahaman na Nurysery School iliyopo Segerea mwisho jiji Dar-Es-Salaam,inawatakia waumini wote Eid Mubarak.Mnakaribishwa sana Madrasa  Rahaman na Nurysery School kituo kinachotoa Elimu yenye maadili mema kwa watoto. Eid Mubarak. usikose kujumuika nasi kwa simu +255(0) 757 608303 au 0712840960

WASHINDI WA MBIO ZA BAISKELI ZA SHIMIWI WATUNUKIWA MEDALI

$
0
0

 Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake kutoka RAS Pwani akijitahidi kukaza mwendo katika mbio za baiskeli za kilomita 32 zilizoanzia kituo cha Melela Mlandizi na kuishia kituo cha Lake Oil katika mashindano ya SHIMIWI  mjini Morogoro leo.
 Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw.Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia)  akimvisha medali ya fedha mshindi wa pili wa mbio za baiskeli kwa wanawake kutoka  RAS Pwani, Agatha Gambi (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro leo. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
 Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanawake kutoka Uchukuzi Johari Moshi akimalizia mbio za baiskeli za kilomita 32 zilizoanzia kituo cha Melela Mlandizi na kuishia kituo cha Lake Oil katika mashindano ya SHIMIWI  mjini Morogoro leo.
 Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw.Daniel Mwalusamba (wa pili kutoka kulia)  akimvisha medali ya shaba mshindi wa tatu wa mbio za baiskeli kwa wanawake kutoka  Uchukuzi, Johari Moshi (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo mjini Morogoro leo. Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.
Mshiriki wa mbio za baiskeli za wanaume za SHIMIWI kutoka Ikulu John Fataki akiwasili kituo cha mwisho cha mbio hizo cha Lake Oil kutoka kituo cha njia panda ya Mkata mjini Morogoro leo.Wengine ni viongozi wa SHIMIWI Taifa wakishuhudia.

BBA: Hotshots Interview with Idris (Tanzania)

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images