Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 594 | 595 | (Page 596) | 597 | 598 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Gregory Teu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (kulia) wakizinduwa madarasa na ofisi ya walimu katika Shule ya Msingi Msenjelele. Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa ambaye pia ni Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara, Gregory Teu pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (wa kwanza kulia) wakishirikiana kuzinduwa vyumba vya madarasa pamoja na ofisi za walimu katika Shule ya Msingi Msenjelele. Majengo hayo yamejengwa kwa msaada na Benki ya Posta Tanzania. Naibu Waziri Wizara ya Viwanda na Biashara, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Gregory Teu (kushoto) akimkabidhi cheti maalum cha shukrani Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (kulia) mara baada ya kukabidhi madarasa na ofisi ya walimu iliyojengwa kwa msaada na benki yake (TPB). Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Msenjelele walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa madarasa yao wakiwa katika picha ya pamoja. Nyuma yao ni sehemu ya jengo la madarasa na ofisi za walimu zilizojengwa na TPB kwa msaada. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (kulia) akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi Msenjelele katika hafla ya uzinduzi wa vyumba vya madarasa pamoja na ofisi Shule ya Msingi Msenjelele.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (wa tatu kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Gregory Teu (wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wageni na wanafunzi walioshiriki hafla hiyo ya kukabidhiwa ofisi na madarasa. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi (wa tatu kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Gregory Teu (wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wageni na wanafunzi walioshiriki hafla hiyo ya kukabidhiwa ofisi na madarasa.

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akifafanua jambo kwa washiriki (hawapo pichani),wa semina ya Fursa iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa hoteli ya KBH,iliyoko nje kidogo ya mji wa Singida,ambapo watu mbalimbali wakiwemo wanavyuo walishiriki.
   Mmoja wa washiriki wa Semina ya Fursa akiuliza swali kwa Meza kuu ya watoa mada kuhusiana na mradi wa ufugaji wa kuku.
   Mwakilishi kutoka Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF),Bwa.Ally Mkulemba akizungumza faida mbalimbali za kujiunga na shirika hilo la NSSF,alisema kuwa vijana wanapaswa kuamka kwa sasa na kuanza kuzichangamkia fursa zitokanazo na shirika hilo,ikiwemo mikopo,bima ya Aya na mengine kwa maendeleo na ujenzi wa maisha bora.
   Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakimsikiliza Msanii mahiri wa Mashairi pichani,Mrisho Mpoto,alipokuwa akizungumza ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya KBH,ilioko nje kidogo ya mji wa Singida.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
   Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya kutoka kundi la Hip hop lijulikanalo kwa jina la WEUSI,Niki wa Pili akizungumza mbele ya mamia ya washiriki wa semina ya fursa iliyofanyika katika hoteli ya KBH nje kidogo ya mjini wa Singida,Niki amewataka vijana mbalimbali kuhakikisha ndoto zao haziishii njiani na badala yake wazifanyiekazi ili kujiletea maendeleo katika maisha yao ya kila siku,pia amewataka kuitumia vyema fursa wanayoipata katika njia mbalimbali.v
   Mmoja wa washiriki wa semina ya Fursa,akiulaza swali na pia kuielezea fursa aliyonayo katika harakati za kutafuta maendeleo.
  Mkurugenzi wa kampuni ya  Automobile Garage,Joseph Msuya akifafanua jambo kuhusiana na namna alivyoaianzisha kampuni yake na kufikia hapo alipo,akitumia teknolojia za kisasa kabisa katika suala zima la ufundi wa magari,utengenezaji Viyoyozi vya magari na mambo mengine mbalimbali.
   Baadhi ya Washiriki wa Semina ya Kamata Fursa,Jitathimini,Jiamini,Jiongeze wakiwa ndani ya ukumbi wa hoteli ya KBH,iliyoko nje kidogo ya mji wa Singida wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikizungumzwa.Semina ya Fursa 2014 inaandaliwa na Waandaaji wa Tamasha la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida. 
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Kipindi kipya cha Televisheni kinachotoa fursa kwa Watanzania waliopo katika foleni za barabarani kutoa maoni na kujadili mustakabali na maendeleo ya Taifa.........Ni muda ambao wengi tunaelekea nyumbani, baada ya kutoka katika pirikapirika na shughuli za kujiongezea kipato. Pamoja na changamoto mbalimbali tunazokutana nazo, lakini kwa sasa tunajikuta katika changamoto nyingine kubwa .... FOLENI ! 
   Hosted by # Khalid Ali Gangana.


  0 0

   Wanachama wa Chama cha Wananchi CUF wakiwa katika msafara wa mapokezi ya Mwenyekiti wa chama hicho,Prof Ibrahim Lipumba
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Prof Ibrahim Lipumba mwenye shati jekundu na kofia nyekundu akiwapungia mkono wanachama wa chama cha CUF mara tu baada ya kufika katika ofisi za CUF Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma
   Polisi wakiwa katika ulinzi wa Prof Ibrahim Lipumba
  Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge wa Chama Cha Wananchi CUF – Shaweji Mketo akiwahutubia  wakazi wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma,kutokufanya makosa  wakati  wauchaguzi wa serikali  za mitaa uliotangazwa  kufanyika Disemba 14 mwaka huu wahakikishe wanakipigia Chama cha Wananchi CUF
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Prof Ibrahim Lipumba akiwahutubia maelfu ya wananchi waTunduru waliojitokeza kumsikiliza katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja baraza  la Iddi Tunduru mjini. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Balozi mpya wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dorah Msechu akisindikizwa kuingia kwenye kasri ya Mfalme wa Sweden ili kuwasilisha hati zake za utambulisho.
    Balozi mpya wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dorah Msechu na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuonana na Mfalme wa Sweden  kasri ya Mfalme wa Sweden akipofika kuwasilisha hati zake za utambulisho.
     Balozi mpya wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dorah Msechu akikaribishwa kuonana na  Mfalme wa Sweden kuwasilisha hati za utambulisho
  Baada ya kuwasilisha hati za utambulisho jioni yake kulifanyika hafla iliyoandaliwa na jumuiya ya Watanzania nchini Sweden kumkaribisha rasmi. Hapo Balozi Dorah Msechu akiamkia kadamnasi ya Watanzania kwenye sherehe hiyo.
  Kwa picha zaidi tembelea libeneke la ubalozi 
  wa Tanzania nchini Sweden... BOFYA HAPA

  0 0
 • 10/03/14--13:30: KINANA AWASILI TANGA MJINI
 •  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka na kivuko cha MV.Pangani kuelekea Wilaya ya Tanga mjini ambapo anatazamiwa kukagua miradi mbali mbali na kushiriki ujenzi wa maendeleo,wengine pichani ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Pangani Ndugu Hamis Mnegero.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Pangani baada ya kuvuka na MV.Pangani
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi waliojitokeza kumuaga wakati akielekea Tanga mjni.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kigombe ,Pangani ambapo  aliwaeleza lazima kuwa makini katika kuchagua viongozi wa kijiji kwani wengi wamekuwa wakiuza ardhi ya wananchi kiholela na kusababisha matatizo makubwa ya ardhi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Tanga mjini Mh.Omari Nundu wakati wa mapokezi katika kata ya Marungu wilaya ya Tanga mjini.

   Wananchi wa kata ya Marungu wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM kwenye kata yao.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Gwen Guthrie - Outside In The Rain

  0 0

  10311052_1940774076061511_5395068416549286320_n
  Pichani ni Zuhura Matata mgonjwa mwenye uhitaji wa upasuaji utakaofanyika nchini India.

  Kipindi cha “Mimi na Tanzania” kinachoongozwa na mrembo aliyewahi kushika taji Miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu, kinatoa shukrani kwa watanzania wote walioguswa na kufanikisha michango ya matibabu ya Zuhura Matata mwenye tatizo la kuvimba mguu ambao unahitaji Oparesheni nchini India.
  Kupitia Akaunti yake ya mtandao wa kijamii Facebook muongozaji wa kipindi hicho Hoyce Temu ameandikia ujumbe wa kuwashukuru watanzania. Soma hapa chini.
  Untitled
  Zuhura Matata ambaye tulimuombea msaada wa kwenda India kupitia kipindi cha Mimi na Tanzania, amefanikiwa kupata pesa zote shilingi milioni 15 sawa na dola elfu kumi. Ataondoka tarehe 21 Oktoba kuelekea India na kuanza Matibabu! Usikose kutazama kipindi cha Mimi na Tanzania, Jumapili, Chanel Ten kuanzia saa tatu na nusu usiku. Mimi Hoyce Temu natangaza rasmi kufunga michango kuanzia sasa kwani pesa tulizoomba tumepata zote! Asanteni Tanzania!
  10639696_1940773056061613_8215664022486093041_n
  Pichani ni Mtangazaji wa Kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu alipomtembelea Zuhura Matata kwa ajili ya mahojiano.

  0 0

   Waumini wa Dini ya Kiislam wa dhehebu la Aswar Sunni kutoka maeneo mbali mbali jijini Dar es Salaam,wakiwa wamejumuika pamoja kwenye viwanja vya Jangwani jijini kwa swala ya Idd el Hajj mapema leo asubuhi.Waislam hawa wanaungana na wenzao waliopo kwenye Idada ya Hija huko Makka.
   Waumini wa Dini ya Kiislam wa dhehebu la Aswar Sunni kutoka maeneo mbali mbali jijini Dar es Salaam wakisoma dua mara baada ya Swala ya Idd el Hajj iliyoswaliwa mapema leo asubuhi kwenye viwanja vya Jangwani,jijini.
   Maalim akitoa Mawaidha katika swala hiyo ya Idd el Hajj katika viwanja vya Jangwani,jijini Dar es Salaam leo.
   Waumini wa Kiislam wakiondoka kwenye viwanja vya Jangwani,jijini Dar es Salaam mara bada ya swala ya Idd el Hajj.

  0 0

  UKOO WA MWEMA NA NKYA UNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MAMA/DADA YAO MPENDWA BI SOPHIA RAJAB NKYA KILICHOTOKEA JANA 3/10/2014 SAA 2.45 USIKU  KATIKA HOSPITALI YA KCMC MOSHI.

  MAZISHI YATAFANYIKA LEO TAREHE 4/10/2014 SAA KUMI ALASIRI KATIKA MAKABURI YA MOSHI MJINI.

  HABARI  ZIWAFIKIE NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI WALIOPO NDANI NA NJE YA NCHI.  0 0

  Dear Family & Friends,
   On the outside chance that you have not yet donated 1 minute of your life to vote for Under The Same Sun (UTSS), PLEASE donate that minute now – SEE BELOW.

  If you have voted but did not ask your family and friends to do the same, PLEASE do it now. If you are part of a business, church or student body, please send this email to them.

  Voting ends October 11th. Thanks to so many voters, UTSS has taken over first place today BUT we must remain in the top 3 to be eligible for the grant.

  Click here to see the voting results so far:


  IF YOU HAVE NOT YET VOTED, KEEP READING:
   UTSS has become eligible for a One Hundred Thousand Euro grant from the Netherlands. Every year, the Dutch Ministry of Foreign Affairs awards the Human Rights Tulip to a human rights defender who promotes and supports human rights in innovative ways.

  UTSS has been shortlisted to 1 of 30 charities from the original 1 of 160. The next phase of shortlisting will bring us to 1 of 3 charities who become eligible for the grant. This next phase of shortlisting will occur through a website voting system.

  Please vote for UTSS.

  FIRST – click here
  THEN – follow these INSTRUCTIONS: 
  -        Click on the pink VOTE icon on the right side of the page to proceed to the voting ballot
   -        Then enter your email address
   -        Then click on the VOTE icon again
   -        Within a few seconds you should receive a confirmation email – MAKE SURE YOU CONFIRM YOUR VOTE.
   -        If the confirmation email does not arrive within a few seconds, check your spam mail
   DONE
   Thanks so much for your vote,

  0 0

  KAMPUNI inayokwenda kwa jina la Wait & Watch Film Company Ltd, ipo mbioni kukamilisha filamu yake ya kwanza itakayojulikana kama ‘Lifti’ inayotengenezwa kwa umakini wa hali ya juu.
  Adam Mchomvu, mmoja  ya wasanii walioshiriki katika filamu ijulikanayo kwa jina la Lifti.
  Filamu hiyo itakuwa ya kwanza tangu kampuni hiyo iliposajiliwa kwa ajili ya kujihusisha na kazi mbalimbali za sanaa, ikiwamo filamu hapa nchini, huku ikiwa na mipango lukuki.
  Akizungumza leo asubuhi, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Athuman Kilo, maarufu kama 'Dr Kilo' alisema kuwa wamejipanga imara kuteka soko la filamu hapa nchini.
  Alisema mashabiki wa filamu watapata burudani kamili pamoja na kujifunza kutoka kwenye filamu hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inaandaliwa kwa utulivu wa hali ya juu.
  “Hii ni kazi ya kwanza ambayo tunaamini itaanza vyema kwasababu vichwa vimetulia na kuangalia namna gani akili zetu zinafanikisha kutoa kazi nzuri.
  “Naomba wadau wote wakae mkao wa kula kuisubiri filamu hii ambayo kwa sasa ipo katika hatua za mwisho kabisa kukamilika na itakuwa moto wa kuotea mbali,” alisema Dr Kilo.
  Baadhi ya watu walioshiriki katika filamu hiyo ni pamoja na Adam Mchomvu, Khamis Said, Sudi Ally ‘Akui’, Sadiki Manyeko, Jazzmin, Tatu Kingwande, Mzee Jengua na wengineo.

  0 0

   Beki namba 5 wa timu ya soka ya Ardhi, Selemani Kungulilo (kushoto) akiwania mpira pamoja na beki  wa timu ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Seif Kibangu (kulia) katika mchezo wa SHIMIWI uliofanyika leo uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.Mambo ya Ndani ilishinda kwa bao 1-0.
   Timu ya soka ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya mechi kati yake na Ardhi katika uwanja wa Jamhuri,Morogoro leo.
   Viungo wa timu ya soka ya Sheria (jezi ya orange) wakimzonga mlinzi wa timu ya soka ya Kilimo, John Tamba katika mchezo wa SHIMIWI uliofanyika uwanja wa Tumbaku mjini Morogoro leo.
   Timu ya soka ya Kilimo kabla ya mpambano dhidi yake na timu ya Sheria katika uwanja wa Tumbaku mjini Morogoro.Kilimo ilifunga mabao 5-4.
  Timu ya soka ya Sheria kabla ya kuanza kwa mpambano dhidi yake na Kilimo uliofanyika uwanja wa Tumbaku mjini Morogoro.
  Mchezaji wa timu ya soka ya Ardhi, Martin Utonga (kulia) akiwania mpira pamoja na beki namba mbili wa timu ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ibrahim Msumai (kushoto) katika mchezo wa SHIMIWI uliofanyika leo uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.Mambo ya Ndani ilishinda kwa bao 1-0.
  Picha zote na Happiness Shayo

  0 0

   Bondia Francis Miyeyusho (kushoto)  akitunishiana misuli na Emilio Norfat ambao watazipiga kesho Jumapili October  5 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga mpambano wa raundi nane.
  --------------------------------------------  
   MABONDIA mbalimbali watazipiga siku ya Jumapili kwa ajili ya mpambano wa ubingwa ambapo bondia kutoka mkoa wa Tanga Tanzania Alen Kamote 'Rasta'' atazipiga na Osgood Kayuni wa Malawi kugombea ubingwa wa Dunia wa UBO kg 61.
  Hiyo ndio siku ya kufurahia kwa wakazi wa Tanga kwani mpambano huo pia uatasindikizwa na mapambano mengine ambapo bondia wa Dar es salaam Thomas Mashali atavaana na bondia kutoka Moshi Alibaba Ramadhani kugombania ubingwa wa Africa wa UBO kg 72 
  Pia siku hiyo kutakuwa na mpambano mwingine  mkali kati ya bondia namba moja kwa ubora katika uzito wake featherweight  Fransic Miyayusho atakaezipiga naEmilio Norfat ambaye nae ni namba mbili katika uzito huo

  Mapambano hayo yaliyoandaliwa jijini Tanga na promota mkongwe nchini Ally Mwazoa ambaye kwa hivi sasa analeta burudani ya masumbwi nchini kupitia Mwanzoa Promotion


  Siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani.

  0 0
 • 10/04/14--04:48: DUUUH.... NOMA!!
 • Dereva wa Daladala akiangalia kama anaweza kulichepusha gari lake kwenda kwenye barabara kuu,mara baada ya kuamriwa na Askari kurudi huko.hii imetokea mapema leo katika eneo la Namanga,jijini Dar.

  0 0
 • 10/04/14--05:31: Mahakama wang'ara Shimiwi
 • Timu ya Mahakama ya Tanzania imeendeleza wimbi la ushindi katika michezo ya Shirikisho ya Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (Shimiwi) inayoendelea mkoani Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri.

  Timu ya Mahakama ambayo inanolewa na kocha wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya Taifa, Abdallah “King Mputa” Kibadeni jana iliibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Ras Tanga na kuingia hatua ya robo fainali.

  Wakati timu ya soka ikiingia katika hatua hiyo muhimu, timu ya mchezo, kamba (wanawake na wanaume) na netiboli nazo zimeingia katika hatua hiyo ya mtoano itakayoanza kesho kwenye uwanja wa huo.

  Kamba wanaume watacheza na Waziri Mkuu wakati wanawake watapambana na Uchukuzi wakati netiboli itaonyeshana kazi na Uchukuzi pia. Katika mchezo wa jana wa soka, mabao ya Mahakama yalifungwa na Kinei Mwanzini, Michael Turuka, Jackson Ndaweka, Christopher David na Mike Cassian.

  Awali, timu hiyo ilishinda dhidi ya Mipango kwa bao 1-0 kabla ya kuisambaratisha Maliasili kwa mabao 2-0 na baadaye kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uchukuzi.

  Kiongozi wa timu hiyo, Twaha Ali alisema kuwa wamefarijika na mwenendo mzuri wa timu zao na matumaini yao kuibuka washindi kwa michezo yote. “Tupo vizuri katika kila mchezo, tunatarajia kufanya vyema na kutwaa ubingwa mwaka huu,” alisema Ali.

  Mratibu wa timu hiyo,Mushumbuzi Samweli alisema kuwa mashindano hayo ni magumu kutokana na maandalizi ya kila timu, hata hivyo watafanikiwa kurejea na ushindi.
  wachezaji wanawake wa mchezo wa kamba wa timu ya Mahakama walishindana na wapinzani wao wa Mipango kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro katika mashindano ya Shimiwi inayoendelea mpaka sasa. Mahakama ilishinda kwa 2-0.
  kocha wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya Taifa, Abdallah “King Mputa” Kibadeni akiiweka sawa timu yake.

  0 0  0 0

   Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kampuni ya No Fake Zone,Lina Sanga ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Oletemba,akiimba jukwaani mbele ya umati wa watu wakati wa tamasha la Fiesta lililofanyika jana katika uwanja wa Namfua,kulia ni mmoja wa wacheza shoo wake akiwajibika jukwaani.
   Kundi mahiri la muziki wa kizazi kipya litambulikalo kwa jina la Makomando wakilishambulia jukwaa la Fiesta hapo jana ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.
   Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta ndani ya Uwanja wa Namfua hapo jana mjini Singida. 
   Ilikuwa ni shangwe tu ndani ya uwanja wa Namfua wakati tamasha la Fiesta likiendelea.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nyumba ya vipaji ya THT,Rachael akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani),wakati wa tamasha la Fiesta likendelea ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
   Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Dully Sykes anaetamba na wimbo wake wa Togola akiwaimbisha mashabiki wake,kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida hapo jana.
   Msanii Mwana-FA na Linah wakiimba kwa pamoja wimbo wao wa Yalaiti jukwaani,huku miluzi na makelele ya mashabiki yakiwa yametawala kila kona ya uwanja wakati wa tamasha la Fiesta likiendelea.
   Wasanii mahiri wa muziki wa Bongofleva,Ney wa Mitego na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa pamoja kupitia wimbo wao unajojulikana kwa jina la Huko kweni Vipi,ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Namfua mjini Singida.PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wote waliohudhuria mkutano kwa kuwapingia mikono yote miwili.
   Wananchi nao hawakuwa nyuma kumpungia kiongozi wao.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwapungia mkono maelfu ya watu waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Tanga mjini ambapo aliwaambia muda wa kuwaambia watanzania maendeleo yapo kwenye mipango umekwisha na kutaka viongozi kutimiza wajibu wao.
   Wananchi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo pamoja na yote alizungumzia uchumi wa Tanga ambapo aliwaambia wananchi hao lazima reli na bandari zifanye kazi ili uchumi wa mkoa wa Tanga ubadilike.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 594 | 595 | (Page 596) | 597 | 598 | .... | 3283 | newer