Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

DSTV Tanzania yazindua kifurushi kipya

$
0
0
3
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia), akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba.(katikati), Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Barbara Kambogi, na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice, Furaha Samalu.

KAMPUNI ya Multichoice Tanzania kupitia huduma ya DSTV imewataka wasanii kupeleka kazi zao ili waweze kutambulika nje na ndani ya nchi. Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Meneja Masoko wa kampuni hiyo Furaha Samalu wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba .

Alisema kifurushi hicho mahususi kwa watanzania chenye chanieli zaidi ya 65 za kitaifa na kimataifa zikiwemo za Maisha Magic Swahili inayoonesha filamu za Kiswahili, chaneli ya telemundo, chaneli ya nickelodeoni na Disney junior zinazoonesha vipindi vya watoto.
Alitaja chaneli nyingine zitakazopatikana kwenye kifurushi hicho ni Afrika magic Epic Movie, Discovery world, CBS Action, CBS reality na CBS drama pamoja na Select sport 1 na 2 kwa vipindi vya michezo.
1
Meneja Masoko wa Multichoice, Furaha Samalu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Octoba 1,2014 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kifurushi kipya cha DSTV Bomba.

“Uzinduzi wa kifurushi hichi ni jambo la furaha na msisimko sana kwetu kuona kuwa sasawatanzania wanaweza kupata kifurushi kinachokidhi mahitaji yao.
“Kila wakati multichoice inafanya jitihada za kudumu namna ya kuwapa wateja wetu uwanja mpana wa burudani kwa uwepo wa filamu , makala, habari, vipindi vya watoto, muziki, vipindi vya dini na michezo,” alisema.

Aliongeza kuwa kifurushi hicho kitagharimu kiasi cha shilingi 17,000 kwa mwezi ambapo watakao jiunga watapata DSTV ikiwemo na gharama ya ufundi kwa shilingi 99,000 kwa kipindi maalum. Alifafanua kuwa kifurushi hicho pia kitawapa fursa watanzania kuangalia Chaneli za Super Sport select1 na 2 ambayo inatonesha ligi kuu ya Uingereza, kombe la klabu bingwa ulaya, ligi kuu ya Hispania, ligi kuu ya Ujerumani pamoja na riadha na ngumi.
2
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akitoa ufafanuzi kuhusiana na kifurushi hicho.
5



Waandishi wa habari wakiwa kwenye uzinduzi huo.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).

WAFANYAKAZI WA UNFPA, TUSHIKAME PAMOJA FOUNDATION NA PROJECKT INSPIRE WAONYESHA UPENDO KWA WAZEE MSIMBAZI CENTRE

$
0
0
IMG_2450
Daktari kijana Brian Mushi wa Projeckt Inspire akionyesha upendo kwa mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho kilichopo Msimbazi Centre mara baada ya kumpima Presha wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.

WAZEE wanaoshi katika makazi ya Msimbazi Centre Jijini Dar es salaam karibu na kanisa la Mtakatifu Maria wa Fatma, Msimbazi walipata faraja kubwa baada ya kutembelewa na makundi matatu ya jamii.

Makundi hayo ni pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) hapa nchini, Tushikamane Pamoja Foundation na madaktari vijana wanaounda kundi la Projeckt Inspire chini ya mradi wa Inspire Healthy. Makundi hayo yalifika katika kituo hicho katika kuadhimisha siku ya wazee duniani.

Wakiwa na lengo kuu la kuwafariji, kukagua afya zao na kuheshimu uwepo wao, makundi hayo pia yaliwapa zawadi za vyandarua, sabuni za kufulia na kuogea, pampers, Thermos Flask, vikombe vya chai, sahani za kulia, vijiko, sukari, njugu mawe, Tshirts, viatu, nguo, vyombo vya kufanyia usafi .
Pia walipiga picha za pamoja za ukumbusho.

Siku ya Wazee Duniani imetengwa kwa ajili ya kuweaenzi na pia kuwakumbuka kwa mambo waliyofanya kuendeleza kizazi cha wanadamu.
IMG_2514
Dr. Brian Mushi wa Projeckt Inspire akimpima presha mmoja wa wazee wanaoishi kwenye kituo hicho.
IMG_2523
Dr. Brian Mushi wa Projeckt Inspire akichukua vipimo vya damu kwa ajili ya kupima sukari kwa mmoja wa wazee wanaolelewa kwenye kituo hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani.

PIGA KURA UBORESHE MAISHA YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

$
0
0
a href="http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2014/10/Untitled.jpg">Untitled
Shirika linalojibidisha na kutetea na kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Under the Same Sun, (UTSS) limeteuliwa kushindania Tuzo ya Haki za Binadamu ijulikanayo kama "Tulip" itolewayo nchini Uholanzi. Iwapo UTSS watashinda tuzo hiyo, ni dhahiri kwamba kutakuwa na mapinduzi makubwa katika uboreshaji wa maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi. 

 Shiriki kwa kupiga kura ili UTSS washinde Tuzo hii na kulinda ndugu zetu wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania kwa kupiga kura hapa chini na kusambambaza tarifa hizi kwa taasisi na watu mbalimbali.
Kwa kupiga kura hiyo bofya hapa

BALOZI LUMBANGA AFUNGUA RASMI MKUTANO WA MAAFISA MIPANGO

$
0
0
 Mgeni Rasmi wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango, Balozi Dkt. Matern Lumbanga akizungumza na washiriki wa Mkutano huo kabla ya kuufungua rasmi.
 Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba wakati wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango unaofanyika jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya viongozi wa wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani). Kutoka Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara, anayemfuatia ni Bw. Paul Sangawe (Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi) na Kulia ni Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu) Bibi Florence Mwanri.

Washiriki wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani).

Mwakilishi wa IFAD amtembelea Waziri Mifugo na Uvuvi ofisini kwake leo

$
0
0
Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Kamani (Mb), Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Kimatifa la IFAD (International Fund for Agricultural Development) Ndugu Francisco Pichon (wa pili kushoto) alipomtembelea Ofisini kwake Dodoma. Mwakilishi wa IFAD alikuwa akielezea maendeleo katika utekelezaji wa mradi wa kuchimba visima virefu vya maji kwa binadamu na mifugo unaofadhiliwa na IFAD katika Wilaya za Bahi, Chamwino, Kiteto na Kondoa. wengine katika picha Ms. Mwatima Juma, Afisa wa IFAD nchini Tanzania (wa kwanza kushoto) na kushoto kwa Mheshimiwa Waziri ni Ndugu. Salim Mwinjaka (Mkurugenzi Msaidizi, Sera na Mipango-Wizara ya Maeneleo ya Mifugo na Uvuvi).

bei ya madafu leo

Safari Lager kudhamini Mashindano ya Mchezo wa Pool Afrika 2014

$
0
0
 Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza udhamini wa Mashindano ya Mchezo wa Pool Afrika (2014 All Africa BlackBall Pool Championsship) yanayotarajiwa kufanyika nchini kuanzia Oktoba 16-18,2014 kwenye Ukumbi wa Burget,Kunduchi Jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo yatashirikisha timu kutoka Zambia,Afrika Kusini,Malawi,Lesotho,Kenya,Uganda na Wenyeji Tanzania,ambapo mshindi wa jumla ataondoka na kitita cha Dola za Marekani elfu 5,huku wa pili akipata dola elfu 2.Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa ambao ndio Waratibu wa Mashindano hayo,Amos Kafwinga.
 Kocha wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa Pool Tanzania,Dennis Lungu akieleza namna timu yake ilivyojipanga vyema kushiriki kwenye mashindano hayo,huku akijitamba kuwa ushindi lazima ubaki Tanzania,kwani anaiamini timu yake.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo na kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa,Amos Kafwinga.
Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa ambao ndio Waratibu wa Mashindano hayo,Amos Kafwinga akitoa shukrani nyingi kwa wadhamini wao ambao ni Safari Lager kwa kuweza kufanikisha mashindano hayo kufanyika hapa nchini.

EFM kukutana na wasikilizaji wake kupitia Tamasha la Muziki Mnene

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Radio 93.7 EFM,Kanky Mwaigomole (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo,wakati akizungumzia kuwepo kwa Tamasha la "Muziki Mnene" lenye dhumuni la Radio hiyo kukutana na kuwashukuru wasikilizaji wake katika maeneo mbali mbali jijini Dar,kwa namna walivyoipikea Radio hilo na kuwa nayo pamoja hadi sasa.Katika Tamasha hilo la Muziki Mnene ambapo safari hii litafanyika Oktoba 4,2014 Ukonga Magereza.Wengine pichani ni Mhariri Mkuu wa Radio hiyo,Samira Kiango (kulia) na Afisa Uhusiani wa Radio hiyo,Lydia Charles Moyo.
 Mhariri Mkuu wa Radio 93.7 EFM,Samira Kiango (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya namna Tamasha hilo litakavyokuwa likifanyika.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Radio 93.7 EFM,Kanky Mwaigomole.
Mmoja wa Watangazaji wa Radio 93.7 EFM kupitia kipindi cha Genge,Pennyl Mungilwa akifanya mambo yake kwenye kipindi chake hicho.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA KONGAMANO LA BIASHARA LA KIMATAIFA KWA NCHI ZA AFRIKA JIJINI DUBAI, FARME ZA KIARABU

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika majadiliano kuhusu utengamano wa Afrika na Fursa za biashara na Uwekezaji Katibu na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Richard Sezibera, wakati wakihojiwa na Mwandishi wa habari wa Kimataifa na Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Eddo Media’, Mark Eddo (kushoto).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania < dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika majadiliano kuhusu utengamano wa Afrika na Fursa za biashara na Uwekezaji, na baadhi ya viongozi, Katibu Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Richard Sezibera (katika) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ghana, Hanna Tetteh, wakati wakihojiwa na Mwandishi wa habari wa Kimataifa na Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Eddo Media’, Mark Eddo (kushoto).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa nne kutoka kulia) akijumuika na baadhi ya viongozi wakati alipohudhuria Mkutano wa GBF, uliofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis jijini Dubai.
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Mchechu (wa tatu kutoka kulia) akijadiliana jambo na Prof. Ahmada Ktahib kutoka Tume ya Utalii Zanzibar wakati walipohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Atlantis nchini Dubai.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Viongozi na wawekezaji baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo. Picha na OMR

TMA KUJENGA VITUO VYA HALI YA HEWA KWENYE MAZIWA YA VICTORIA,TANGANYIKA NA NYASA

$
0
0
Meneja wa Huduma za Utabiri wa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Samwel Mbuya (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kufungua vituo vya kutolea huduma za hali ya Hewa katika maziwa ya Victoria,Tanganyika na Nyasa.Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA),Monica Mutoni.

Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) imedhamiria kufungua Ofisi za Kutolea huduma za hali ya Hewa ili kupunguza ajali katika maziwa hapa nchini. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Meneja wa Huduma za Utabiri wa TMA Bw. Samwel Mbuya wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imeona kuna umuhimu wa kujenga vituo vya kutoa huduma za Hali ya hewa nchini katika maziwa ya Victoria,Tanganyika na Nyasa, vituo hivi vitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali kwa kuwa tutafunga vifaa vya kisasa vya kupima hali ya hewa Alisema Mbuya.

Aidha Mbuya amesema kuwa TMA imeendelea kuboresha huduma za utabiri wa Baharini kwa kuweka maboya maalum katika ukanda wa bahari ya Hindi pamoja na kufungua kituo cha hali ya hewa katika Bandari ya Zanzibar.

Mbuya alibainisha kuwa kwa upande wa usafiri wa anga TMA imeendelea kutoa huduma zenye kukidhi vigezo vyenye hadhi ya Kimataifa ili kuleta usalama kwa watumiaji wa Usafiri huo nchini.

Akizungumzia kuhusu uboreshaji wa mtandao wa vituo,Mbuya alisema kuwa hivi sasa mtandao huo umeongezeka ikiwemo kusimikwa kwa rada mbili za hali ya hewa moja ipo katika eneo la Bangula-Dar es salaam na nyingine iko katika hatua za mwisho huko Kiseke-Mwanza.

Pia Mbuya aliongeza kuwa Mamlaka hiyo imefanikiwa kuongeza wigo wa usambazaji taarifa zake hadi kufikia zaidi ya radio 40 za kijamii lengo likiwa ni kuwafikia wananchi waliopo vijijini.

Dira ya TMA Inalenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2015 Mamlaka hiyo inatoa huduma katika viwango vya Kimataifa.

Wizara ya uchukuzi yasaini mkataba na kutekeleza amradi wa treni za kisasa nchini

$
0
0
Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Kipalo Kisamfu(aliyevaa koti la kaki), na Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Marekani na mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja kutoka nchini Marekani, Robert Shumake wakisaini Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo asubuhi katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi. Wanaoshuhudia na Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe (wan ne kutoka kulia), na wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Shaaban Mwinjaka ( wa tatu kutoka kushoto) pamoja na wawakilishi kutoka kwa Mwanansheria Mkuu wa Serikali, Mwenyekiti wa Bodi ya TRL.
Balozi wa heshima wa Tanzania Nchini Marekani na mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja , Robert Shumake, akiwaelezea waandishi wa habari(hawapo pichani), namna treni ya mwendo kasi itakavyotengezwa baada ya utiaji saini wa Mkataba wa maelewano wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo asubuhi katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) , akisisitiza jambo wakati akiongea na Balozi wa Heshima wa Tanzania Nchini Marekani na na mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja, Robert Shumake, ofisini kwake kabla ya kusaini Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zijulikanazo kama Diesel Multiple Unit(DMU) zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), leo asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (mwenye tai nyekundu), akisisitiza jambo kabla ya utiaji saini Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo asubuhi katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi.
Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Marekani na mfanyabiashara nchini Marekani na mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja, Robert Shumake akimueleza Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi, Wizara ya Uchukuzi, Peter Lupatu namna treni ya mwendo kasi itakavyofanya kazi, kabla ya utiaji saini wa Mkataba wa awali wa mradi wa treni za kisasa zitakazohudumia abiria kutoka stesheni ya Dar es Salaam mpaka Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi. Treni hiyo itabeba abiria 800 mpaka 1000. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

VODACOM YAENDELEZA KAMPENI YAKE YA"WAIT TO SEND" YA WIKI YA USALAMA BARABARANI

MISS UNIVERSE TANZANIA 2011 NELLY KAMWELU ENROLLS AT THE NEW YORK FILM ACADEMY

$
0
0
Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu is in New York and has started her studied in acting at the New York Film Academy . New York Film Academy-School of Film and Acting (NYFA) is a for-profit film school and acting school based in New York City. Nelly’s enrollment is part of her scholarship to the institution that she was awarded when she won the Miss Universe Tanzania title.

Nelly Kamwelu won the Miss Universe Tanzania and Miss Southern Africa International titles in 2011. She represented Tanzania in Miss Universe 2011 in São Paulo, Brazil, Miss International 2011 in China, Miss Earth 2011 in Manila, Philippines, and Miss Tourism Queen International in China. 

Nelly is the only beauty queen who has competed in four Grand Slam Pagents (Miss Universe, Miss International, Miss Earth and Miss Tourism Queen International) in a single year. Nelly has featured in Music Videos of Tanzanian Musicians and also recorded a song Say it to my face before her departure for Miss Universe 2011. The song was released on YouTube while she was participating in the beauty contest in São Paulo, Brazil 2011.

New York Film Academy's programs include film directing, film producing, screenwriting, cinematography, film editing, documentary filmmaking and courses in acting. Since 2010, Miss Universe Tanzania has been sponsored by NYFA and all winners (Hellen Dausen, Nelly Kamwelu and Winfrida Dominic) have attended the Academy.

 Betty Omara, Miss Universe Tanzania 2013 will get her chance to attend the Academy once she hands over her crown this October.

BALOZI KAMALA AKUTANA NA WAZIRI WA UCHUMI NA BIASHARA WA SERIKALI YA BRUSSELS

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimkabidhi kitabu kinachobainisha fursa za uwekezaji Tanzania Waziri wa uchumi na biashara wa serikali ya Brussels Mhe. Didier Gosuin. Balozi Kamala amekutana na waziri Gosuin ofisini kwake Brussels leo.

SEKTA ZA KILIMO,VIWANDA NA BIASHARA ZAKUZA PATO LA TAIFA KWA ASILIMIA 6.9

$
0
0
Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Morrice Oyuke (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukuaji wa Pato la Taifa kwa bei ya Soko leo jijini Dar es salaam. Wengine ni Bw. Fred Matola, Mtakwimu Mkuu Takwimu za Uchumi (kushoto), Bi. Adella Ndesangia (wa pili kutoka kulia) ambaye ni Mtwakimu Mkuu wa Ofisi hiyo na Bi. Jovitha Rugemalila.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO

Sekta za Kilimo,Viwanda, Biashara za jumla na rejareja zimetajwa kuongoza katika kuchangia kukua kwa pato la Taifa kwa asilimia 6.9 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2014.

Akitoa taarifa ya kukua kwa pato la Taifa leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Morrice Oyuke amesema kuwa kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2014 sekta hizo zimetoa mchango mkubwa wa kukuza pato la Taifa.


Lori ya maji taka aina ya IVECO - ZETA inauzwa

$
0
0
Lori ya maji taka aina ya IVECO - ZETA inauzwa. yenye ujazo wa lita 6000 ya maji taka, pia lita 2000 ya maji masafi kwaajili ya Pampu ya kuoshea magari. ina hali nzuri sana haina shida yoyote, kwa maelezo zaidi piga simu namba hizi: 

0767-191275 au 0652-260868. 


NEWS ALERT: MAHAKAMA YAZUIA KUFANYIKA KWA ‘BANG BANG BEAR FEST’ JUMAMOSI HII, LIMEKIUKA SHERIA ZA HAKI MILIKI

$
0
0
Mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam imezuia kufanyika kwa tamasha lililopewa jina ‘Bang Bang Bear Fest’ lililokuwa linatarajiwa kufanyika Jumamosi hii.

Uamuzi wa mahakama hiyo umetokana na malalamiko yaliyotolewa na Bongo5 Media Group ambao wanamiliki wazo halisi la tamasha la aina hiyo liitwalo Dar es Salaam Bear Fest.

Kwa hali hiyo mahakama hiyo imetoa amri ya kusitishwa mara moja kwa ‘Bang Bang Bear Fest’ lililokuwa lifanyike October 4 kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama, Dar es Salaam pamoja na kulipa hasara yoyote iliyotokana na kuingiliwa kwa haki miliki hiyo.

Airtel na UNESCO wazindua radio ya kwanza Uvinza Kigoma

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM chini ya ufadhili wa shirika la UNESCO na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, ambapo wanawezesha jamii ziishizo pembezoni mwa nchini kupata mawasiliano ya radio jamii na kuboresha upatikanaji wa taarifa muhimu. wakishuhudia ni Meneja huduma kwa jamii Airtel Hawa Bayumi, Mwakilishi wa shirika la kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Rose Haji, na Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Nuru Kalufya.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya akiongea wakati wa uzinduzi wa redio Jamii Uvinza FM chini ya mradi wa radio jamii unaofadhiliwa na Airtel kwa Kushirikiana na UNESCO. pichani ni Mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya akiwa na wawakilishi wa radio na UNESCO.
Meneja huduma kwa jamii wa Airtel,Hawa Bayumi akiongea wakati wa uzinduzi wa redio Jamii Uvinza FM chini ya mradi wa radio jamii unaofadhiliwa na Airtel kwa Kushirikiana na UNESCO. pichani ni Mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya akiwa na wawakilishi wa radio na UNESCO.
Mwakilishi wa shirika la kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Rose Haji akiongea wakati wa uzinduzi wa redio Jamii Uvinza FM chini ya mradi wa radio jamii unaofadhiliwa na Airtel kwa Kushirikiana na UNESCO. pichani ni Mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya akiwa na wawakilishi wa radio na UNESCO.

MH. MEMBE AKABIDHI HUNDI YA DOLA LAKI 1 KWA FAMILIA YA BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard K. Membe (Mb) (katikati) akikabidhi hundi yenye thamani ya Dola za Marekani laki moja kwa mtoto wa Brigedia Jen. Mstaafu Hashim Mbita, Bibi Shella Mbita. Bibi Mbita alipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Baba yake ambayo imetolewa na Rais wa Zimbabwe, Mhe. Robert Mugabe kutokana mchango mkubwa alioutoa Brig. Jen. Mbita katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika. Mwingine katika picha ni Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Edzai Chimonyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Tuzo iliyotolewa na Rais Mugabe kwa Brig. Jen. Hashim Mbita wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa SADC uliofanyika Victoria Falls nchini Zimbabwe mwezi Agosti 2014. Waziri Membe alieleza kuwa Rais Mugabe alitoa Tuzo ya Munhumutapa kwa Brig. Jen Hashim Mbita kutokana na mchango wake mkubwa katika harakati za kutafuta uhuru Kusini mwa Afrika. Brig. Jen. Mbita anakuwa mtu wa kwanza sio Mkuu wa Nchi kutunukiwa Tuzo hiyo ambayo kwa kawaida hutukiwa Wakuu wa Nchi pekee. Wengine katika picha ni Balozi wa Zimbawe nchini Tanzania na binti yake Brig. Jen. Mbita, Bibi Shella. 
Bibi Shella akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Zimbabwe kutokana na zawadi ya Dola 100,000.00 kwa Baba yake mzazi
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Shiyo Innocent (tai nyekundu) na Afisa wa Ubalozi wa Zimbabwe nchini Tanzania wakifuatilia kwa makini mkutano wa waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakiwa kazini.

FUNDI KAZINI....

$
0
0
Leo kamera ya Globu ya Jamii,imemnasa fundi huyu makiri wa kupaka rangi kwenye majengo marefu jijini Dar kama aonekanavyo hapo.

Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images