Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 592 | 593 | (Page 594) | 595 | 596 | .... | 3283 | newer

  0 0

  DSC_0177
  Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwalimu Hadijah Nyembo (kulia) akitoa nasaha zake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya (wa pili kulia) kuzungumza na wakazi wa wilaya ya Uvinza kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM mkoani Kigoma. Kutoka kushoto ni Meneja wa huduma za kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambao ndio wadhamini wakuu wa redio Uvinza FM, Bi. Rose Haji Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio Bi. Nuru Kalufya.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
   
  Na Mwandishi wetu, Uvinza - Kigoma
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya amesisitiza uadilifu katika vyombo vya habari jamii kwa kutangaza habari zisizoumiza hisia kwa wananchi wengine na kuepuka migogoro.
  Akizindua kituo cha redio jamii cha Uvinza FM, Luteni Kanali Mstaafu Machibya alisema kuwa vyombo vina wakati mgumu hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015.

  “Changamoto hii inaweza kuepukika kwa kuhakikisha habari zinazotolewa zinalenga kuendeleza utamaduni wa amani, upendo, utulivu na uvumilivu na kuepuka viashiria vinavyoweza kusambaza chuki kwa lengo la kufanikisha chaguzi salama.

  Mkuu wa Mkoa huyo amesisitiza umuhimu wa kuutumia uhuru wa kutoa na kupata habari vizuri kwa kusema kwamba uhuru huo usitumike kutoa habari zinazopendelea upande mmoja na kukandamiza mwingine kwa kuwa hali kama hiyo husababisha machafuko.

  “Kwa mujibu wa Ibara ya 18 (b) ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kila mtu anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi, lakini haki hiyo iende sambamba kwa kuzingatia Sheria za nchi na kuhakikisha habari hizo haziumizi hisia za wananchi wengine,”
  DSC_0206
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya akisoma risala wakati wa uzinduzi wa kituo cha redio jamii Uvinza FM ambapo alilipongeza shirika la UNESCO kwa juhudi kuwaweka karibu wananchi na serikali kupitia mawasiliano ya redio.

  Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya ameitaka redio jamii Uvinza kuonyesha uwezo wao ili waweze kujitangaza na kujijengea imani kwa wanajamii wao kuwa wanaweza. “Ni kwa hali hiyo tu mtaweza kujulikana, kutambulika na kupata udhamini na matangazo ya kutosha.”
  Amewataka wanajamii kukitumia vyema kituo chao cha redio ili kiwe chachu ya kuleta na kukuza maendeleo katika vijiji, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.


  0 0

  Katibu na Mwanasheria mkuu wa kampuni ya ufuaji umeme ya IPTL, Bw. Joseph Makandege akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) nakala ya hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya Tanzania ikizuia benki ya Standard Chartered ya Hong Kong na Tanesco kuendelea kuwabugudhi wamiliki wa IPTL na kuingilia uendeshaji wa mitambo yake. Kushoto ni Meneja Rasilimali watu wa IPTL Bw. Aidan Kaude. 

  ·         Yasema Bw. Sethi kuendelea kusimamia mitambo ya ufuaji umeme ya Tegeta.

  Mahakama Kuu ya Tanzania imeiamuru Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong na Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO) kuacha kuingilia utulivu, umiliki, usimamizi na utawala wa Mitambo ya ufuaji umeme ya Bw. Harbinder Singh Sethi iliyopo Tegeta, na kusubiri uamuzi wa mwisho wa kesi yao ya msingi.

  Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions Limited (PAP) zilifungua kesi kwa kuhoji uhalali wa maamuzi ya Kituo cha Kimataifa cha Kutatua Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) dhidi ya Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCB-HK) na Martha Renju (anaedaiwa kuwa msimamizi wa mali zake), ijulikanayo kama "Decision on Jurisdiction and liability" iliyotolewa katika kesi ya ICSD namba ARB / 10/20.


  0 0
 • 10/02/14--04:34: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamiliusi Membe (Mb.) akizungumza na baadhi ya wanamichezo walioshiriki michezo ya Jumuiya ya Madola Glasgow, Scotland mwezi Agosti, alipo kutana nao na kufanya kikao cha kutathmini matokeo ya timu ya Tanzania katika kituo cha michezo cha Filbert Bayi kilichopo Kibaha Mkuza. Wanamichezo wakimsikiliza kwa makini Waziri Membe (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.   Viongozi mbalimbali wa vyama vya michezo wakimsikiliza                   Waziri Membe (hayupo pichani).                     
  Wakwanza Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mambo ya Nje, Bw.Mkumbwa Ally, na wapili kutoka kushoto ni Afisa Mambo ya Nje Bw. Imani Njalikai wakifuatilia kikao kati ya Waziri Membe na wanamichezo walio shiriki michezo ya jumuiya ya madola Glasgow, Scotland.

  BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

  0 0

  Meneja wa Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya fainali ya mashindano hayo yatakayofanyika jumamosi Don Bosco Oysterbay jijini. Kulia ni Mratibu wa shindano hilo la Dance 100%, Happy Shame.
  Mratibu wa shindano la Dance 100%, Happy Shame ( kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya fainali ya shindano hilo litakalofanyika jumamosi Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Uhusioano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu.

  FAINALI za shindano la kucheza muziki maarufu kama Dance 100% linalofanyika chini ya uratibu wa Kituo cha East Africa Television ltd  na kudhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, zitanayika Jumamosi hii ya Oktoba 4, Viwanja vya Don Bosco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

  Mratibu wa shindano hilo Happy Shame alisema jijini Dr es Salaam jana kuwa, fainali za shindano hilo ambalo safari yake ilianza Julai 19, mwaka huu kuanzia hatua ya kusaka washiriki hadi mchujo litashirikisha makundi matano.

  Alisema kutokana na kila kundi kutaka kuibuka mshindi na kujitwalia kitita cha sh mil 5, kwa muda mrefu yamekuwa yakijifua kuhakikisha wanafanya kweli siku hiyo mbele
  ya jopo la majaji wakiongozwa na Super Nyamwela.

  Shame alisema, shindano la mwaka huu limekuwa na msisimko wa aina yake zaidi kuliko miaka miwili iliyopita baada ya mambo mbalimbali kuboreshwa na zaidi kiasi cha vijana kuona ni fursa kwao sio tu kupata fedha, pia kuendeleza vipaji vyao.

  “Ushindani umekuwa mkubwa sana katika shindano la mwaka huu ikilinganishwa na miaka mingine kutokana na sababu mbalimbali.  Shindano pia limeanza kupata mashabiki, tunashukuru sana sapoti ya wadhamini wetu Vodacom Tanzania,” alisema.

  Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu,alieleza kuwa  mbali ya dau hilo kwa mshindi, kila mshiriki pia atapatiwa simu iliyounganishwa na  mtandao wa Vodacom.

  Nkurlu alisema jana kuwa, kundi litakaloibuka nafasi ya pili katika fainali hiyo, litajipatia zawadi ya sh Milion 1.5 na mshindi wa tatu atapata kiasi cha laki 5.

  Alisema kampuni ya Vodacom inajivunia kudhamini shindano hilo kwa njia hiyo ya udhamini wakitambua umuhimu wa vijana kujiajiri kupitia vipaji vyao na kuongeza kuwa, kwa kipindi chote cha mchakato wa shindano hilo, vijana wamejifunza mengi.

  “Vijana wameonyesha uwezo mkubwa kuanzia hatua ya mchujo hadi sasa kiasi cha kuwapa majaji wakati mgumu. Tunaamini hata baada ya fainali, vijana hawa watajiendeleza zaidi kimuziki,” alisema Nkurlu.

  Makundi hayo matano yaliyoingia hatua ya fainali, vijana wamekuwa wakionesha vipaji na umahiri mkubwa wa kucheza staili mbalimbali za muziki ambayo ni Wazawa Crew, Best Boys Crew, The W.T, Wakali Sisi na The winners Crew.

  Nkurlu aliongeza kuwa, kwa vile vijana hao wamejiweka katika mazingira ya kutumia vipaji vyao kujipatia ajira, Kampuni ya Vodacom-Tanzania inaona fahari kudhamini shindano hilo wakisaidia juhudi za serikali kupambana na tatizo la ajira.

  “Takwimu zinaonesha kuwa kila mwaka vijana zaidi ya 800,000 wanaingia katika soko
  la kusaka ajira ndio maana, Vodacom Tanzania kwa kulitambua hilo, tumekuwa mstari wa mbele kusaidiana na serikali na wadau wengine kuwajengea vijana msingi,” alisema Nkurlu.

  Kuhusu zawadi, Nkurlu alisema kundi litakaloibuka mshindi, litaondoka nash mil 5, huku kila mshiriki katika katika kundi hilo akipatiwa simu aina ya Vodafone ikiwa na muda wa maongezi wa sh. 100,000.

  0 0
 • 10/02/14--06:01: Article 18


 • 0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.Picha zote na Othman Michuzi.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi akitoa hotuba fupi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuja kufungua Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania,Balozi Charles Sanga akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.
  Sehemu ya Wageni kutoka nchi mbali mbali wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia namna mahindi yanavyosagwa na kupatikana ungwa wakati alipotembelea Banda la Maonyesho ya Utalii la Burundi,kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia ngoma ya utamaduni ya Taifa la Burundi alipotembelea Banda la Maonyesho ya Utalii la Burundi,kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Utalii "Swahili International Tourism Expo (SITE)" kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 2,2014.

  AU

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akizungumza na wajumbe wa Baraza Dogo la Wafanyakazi la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kabla ya kulizindua Baraza hilo katika Hoteli ya Livingstone mjini Bagamoyo leo. Katika hotuba yake, Abdulwakil aliwataka viongozi wakuu wa jeshi hilo kushirikiana kikamilifu na watumishi wote ili kuleta mabadiliko chanya ndani ya jeshi hilo. Wapili kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Pius Nyambacha, Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Zimamoto na Uokoaji, Shwaybu Mohamoud. Watatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA), Andrew Mwalisisi na wapili kushoto ni Katibu wa Tughe tawi hilo, Andason Kalewa.
  Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kushoto) akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kulia-meza kuu) kuzungumza na kulizindua Baraza Dogo la Wafanyakazi la Jeshi hilo. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (Tughe) tawi la Zimamoto na Uokoaji, Shwaybu Mohamoud. Watatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA), Andrew Mwalisisi na wapili kushoto ni Katibu wa Tughe tawi hilo, Andason Kalewa. Uzinduzi wa Baraza hilo ulifanyika katika Hoteli ya Livingstone mjini Bagamoyo leo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watano kushoto- waliokaa), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa (watano kulia), Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza Dogo la Wafanyakazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji baada ya kuzinduliwa baraza hilo katika Hoteli ya Livingstone mjini Bagamoyo leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayoratibu Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Omari Issa akiwapa changamoto leo Alhamisi Wakuu wa Mikoa na Wilaya (hawapo pichani) kufanya uamuzi wa haraka katika utekelezaji wa majukumu yao na kutosubiri mpaka wafuatiliwe.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa na viongozi wengine wakifuatilia hotuba ya Mtendaji Mkuu wa PDB, Bw. Omari Issa mjini Dodoma leo Alhamisi aliyekuwa akiwakumbusha watendaji hao waandamizi umuhimu wa kuchukua uamuzi kwa haraka na kutosubiri kufuatiliwa katika mambo ambayo yamo ndani ya uwezo wao.
  Baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Wilaya na watendaji waandamizi waliohudhuria Semina iliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa PDB, Bw. Omari Issa (hayupo pichani) alipokuwa akitoa mada kuhusu uwajibikaji mjini Dodoma leo Alhamisi.
  Mtendaji Mkuu wa PDB, Bw. Omari Issa akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiq walipokutana leo Alhamisi mjini Dodoma wakati wa semina inayoendelea kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya na maofisa waandamizi. (Picha zote kwa Hisani ya Ofisi ya Rais-PDB).

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka (kulia) akizunguma wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Picolo, Kawe jijini Dar es Salaam. Kushoto ni baadhi ya wahariri hao.
  Mkurugenzi wa Utafiti, Tathimini na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi akiwasilisha mada kuhusu Mafao ya Pensheni, wakati wa semina hiyo ya wahariri, Dar es Salaam jana.
  Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, wakisikiliza mada hiyo, iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Utafiti, Tathimini na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi.
  Wahariri wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa katika semina hiyo.


  0 0  0 0

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati meza Kuu) akisikiliza maelezo mafupi toka kwa Mratibu wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani, Kanali Sambulo Ndrovu(hayupo pichani) kabla ya kufunga rasmi Mafunzo hayo leo Oktoba 02, 2014. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(wa pili kulia) ni Mratibu Msaidizi wa Mafunzo hayo Kamishna Msaidizi wa Magereza toka Nchini Zimbabwe, Didmas Chimvura(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi ya ufungaji wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani ambayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo jumla ya Maafisa Magereza 27 toka Nchi za SADC ikiwemo Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Mauritius, Swaziland na Zimbabwe wameshiriki kikamilifu Mafunzo hayo.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akikabidhi cheti kwa Mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya Ulinzi wa Amani, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Nchini Tanzania, Pendo Kazumba. Mafunzo hayo yamefanyika kwa wiki mbili na yameendeshwa na Kituo cha Mafunzo cha SADC kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza Tanzania(kushoto) ni Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC Bregedia Jenerali Christopher Chellah.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja akifanya mahojiano Maalum na Waandishi wa Habari toka Vyombo vya TBC1 na ITV Mkoani Kilimanjaro mara tu baada ya kufunga rasmi Mafunzo ya Ulinzi wa Amani kwa Maafisa Magereza toka Nchi za SADC leo Oktoba 2, 2014 Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa sita kushoto) na Mkuu wa Kituo cha Mafunzo cha SADC, Bregedia Jenerali Christopher Chellah(wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Magereza Wanawake toka Nchi za SADC ambao wameshiriki kikamilifu Mafunzo ya wiki mbili ya Ulinzi wa Amani katika Chuo cha Maafisa Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Magereza toka Nchi za SADC(waliosimama) walioshiriki Mafunzo ya Ulinzi wa Amani ambayo yamefanyika kwa wiki mbili katika Chuo cha Uhamiaji, Moshi Mkoani Kilimanjaro. Mafunzo hayo yamefungwa leo na Kamishna Jenerali wa Magereza ambapo jumla ya Maafisa Magereza 27 toka Nchi za SADC ikiwemo Tanzania, Mauritius, Afrika Kusini, Swaziland, Botswana, Namibian na Zimbabwe wamehitimu Mafunzo hayo Maalum ya Ulinzi wa Amani(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi , Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Mbwana . J. Mbwana (Kulia)akisalimiana na Rais wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) Tchagbele Sadamba wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa AATO unaofanyika Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Dkt. James Diu.
  Rais wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika(AATO) Tchagbele Sadamba (Kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa AATO Bi Margreth Kyarwenda ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Cha Usafiri wa Anga (CATC) , kinachomilikiwa na TCAA wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa AATO unaofanyika Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.
  Baadhi ya wataalamu wa sekta ya Usafiri wa Anga Tanzania wakifuatilia kwa karibu mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vyuo vya Usafiri wa Anga Barani Afrika( AATO) unaofanyika mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili mbinu za kuboresha mafunzo ya usafiri wa anga barani Afrika.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Dominicas Lusasi District Administrative Secretary - Bunda district talk to farmers of being motivated to have the best cotton crop at farmers forum held in Bunda district to give farmers an opportunity to discuss of the milestones and challenges in the sector while exploring expectations for the next season.
  Mr Japhet Kwangula drives his point home on the importance of getting input on time and in the quantity required. This was at farmers forum held in Bunda district to give farmers an opportunity to discuss of the milestones and challenges in the sector while exploring expectations for the next season.
  A cotton farmers talk about the benefits of contract farming during a farmers forum held in Bunda district to give farmers an opportunity to discuss of the milestones and challenges in the sector while exploring expectations for the next season.

  0 0


  0 0

  Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Maji (jezi ya kijani) wakipambana na mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya TAMISEMI (jezi ya orange) katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mkoani Morogoro.TAMISEMI iliibuka mshindi kwa bao 1-0.
  Picha na Happiness Shayo-Morogoro

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubuia Kikao cha Kazi kwa Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri katika ukumbi wa Chimwaga Chuo Kikuu cha Dodoma leo Oktoba 2, 2014. PICHA NA IKULU

  0 0


   Wadau mbalimbali wakiwasili kwenye hotel ya Millennium Durham tayari kwenye DICOTA 2014 utaonza rasmi Ijumaa Oct 3, 2014 kwenye mji wa Durham jimbo la North Carolina mkutano utamalizika siku ya Jumapili Oct 5, 2014 kwenye picha kushoto ni mpiga picha za kiwango na maarufu kutoka DMV Bi Iska Jojo na makamu wa rais DMV Bi, Harriet Shangarai wakielekea vyumbani baada ya kuwasili kwenye hotel ya Millennium muda si mrefu na kukutana na ukodak wa Vijimambo ambao utakuwepo kwenye mkutano huo kuwakilisha.
   Maafisa wa DICOTA wakihakiki usajili wa wadau waliofika mapema leo siku ya Alhamisi Oct 2, 2014 tayari kwa DICOTA 2014 Convetion.
   Wadau wakifuatilia usajili wao kuhakikisha kila kitu kipo sawa wadau wawili kushoto ni Suleiman Zanangwa na Focus wawakilishi wa Tanzania Ports Authority
  Msanii wa vichekesho kutoka kundi la Ze Komedi Masanja mkandamizaji akicheza na simu yake kutupia mawili matatu kwenye mitandao ya kijamii akiwa nae tayari kuwakilisha kwa mara ya kwanza katika historia ya DICOTA ndani ya Durham, North Carolina.

  Wawakilishi toka Global Land Solutions toka Tanzania wakipata picha ya kumbukumbu kama walivyokutwa na kamera ya Vijimambo kwa picha zaidi bofya HAPA

  0 0

  Odyssey - Going Back To My Roots

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikinga maji wakati wa kuzindua mradi wa maji wa kata ya Mkalamo wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha dumu la maji mmoja wa wakazi wa kata ya Mkalamo
   Wananchi wa Kata ya Mkalamo  wakichota maji safi na salama kwenye mradi wa maji ya kisima kilichogharimu zaidi ya shilingi milioni 29 ambacho kimefadhiliwa na hifadhi ya Taifa ya Saadani.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchimba mtaro wa bomba la maji  wa kata ya Mkalamo wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali ya ujenzi wa ofisi yaCCM kata ya Mkwaja.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

older | 1 | .... | 592 | 593 | (Page 594) | 595 | 596 | .... | 3283 | newer